Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1313 | 1314 | (Page 1315) | 1316 | 1317 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Shehere za kuadhimisha Miaka 80 ya Wekundu wa Msimbazi "Simba SC", Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa tano kushoto), akiwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) pamoja na Baadhi ya viongozi wa Timu ya Simba, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukata keki ya Hepi Besdei ya Simba, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wachezaji wa Zamani wa Simba, wakiongozwa na aliewahi kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo, Mzee Hassan Dalali (kati) wakikata keki ya Hepi Besdei ya Simba, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji "MO" akimlisha kipande ya Keki, Mgeni Rasmi katika Shehere za kuadhimisha Miaka 80 ya Wekundu wa Msimbazi "Simba SC", Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
  MO akisalimiana na Mashabiki wa Simba.

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani,wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival litakalo fanyika Jumamosi hii 13 August 2016 katika viwanja vya Rebstock Park,jijini Frankfurt,Ujerumani ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani
  Kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya. 
  usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com wape Hi at www.facebook.com/ngomaafricaband

  0 0


  0 0  0 0

  Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za vijana na watanzania kwaujumla juu ya kutokufikia Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea umasikini wa watanzania wengi, pia alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo. 
  Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa chuo ch Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto zake na jinsi ya kuzikabili. 
  Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani) ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo.
  Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwsihoni wa wiki iliyopita.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano ,Jijini Dar es salaam. 

  0 0


  0 0

   Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 
  Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 
  Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.
  Wanarianda walioshiriki mashindano ya majeshi  kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu.
  (picha na Selemani Semunyu)

  Na Seleamani Semunyu JWTZ.
  MASHINDANO ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa wanawake  katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .

  Mtanzania Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano  Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua ushindi wa Kwanza.  

  Awali akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi  Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha Ushirikiano.

  Aliyasema hayo leo wakati akizindua wa michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi  Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.

  “ Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.

  Waziri Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.

  Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba  aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo (kulia) akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 ambao umefikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 za mwezi Juni 2016.Kushoto ni Kaimu Meneja wa wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Mwezi Julai, 2016 iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam. 

  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.
  OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) imetangaza mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai 2016 na kueleza kuwa umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 iliyokuwepo mwezi Juni mwaka huu.

  Akitangaza taarifa ya mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016.

  Ameeleza kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2016 zikiwemo bidhaa za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9 huku bei zisizo za vyakula zikihusisha ni gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

  Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni pamoja na bidhaa za gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

  Aidha, ameeleza kuwa pamoja kupungua huko, kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kwenye baadhi ya bidhaa umeonesha kuongezeka katika kipindi hicho hasa kwenye kama mchele, mahindi, unga wa mahindi, vyakula kwenye migahawa na mkaa.

  Bw. Kwesigabo amesema kuwa Fahirisi za Bei nazo zimeongezeka hadi kufikia 103.50 mwezi Julai, 2016 kutoka 103.47 za mwezi Juni 2016, ongezeko ambalo limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula zile zisizokuwa za vyakula.

  Amesema ongezeko hilo la Fahirisi linahusisha kundi la bidhaa na huduma za vyakula na vinywaji baridi, Vinywaji vyenye kilevi na bidhaa za Tumbaku, Mavazi ya nguo na viatu, nishati, maji na Makazi pamoja na Samani, vifaa vya nyumbani na ukarabati wa nyumba.

  Kundi lingine linahusisha gharama za Afya, usafirishaji, Mawasiliano, Utamaduni na Burudani, Elimu, hoteli na migahawa pamoja na bidhaa na huduma nyinginezo ambazo jumla ya Fahirisi za Bidhaa hizo kwa mwezi huo zimefikia 103.50.

  “Baadhi ya bidhaa zilizo sababisha kuongezeka kwa Fahirisi ni pamoja na mafuta ya kupikia asilimia 1.1, samaki wabichi asilimia 6.0, matunda asilimia 4.9, maharage makavu kwa asilimia 2.7, ndizi za kupika asilimia 1.9 na mahindi kwa asilimia 1.5” Amesisitiza Kwesigabo.

  Mbali na hilo ameeleza kuwa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2016 umepungua hadi kufikia asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ya mwezi Juni 2016.

  Kwa upande wa uwezo wa shilingi ya 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 62 mwezi Julai 2016 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 65 ya mwezi Juni, 2016.

  Aidha, hali ya Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki imeonesha kuwa nchi ya Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Julai umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.39 kutoka asilimia 5.80 za mwezi Juni, 2016, Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei uliopungua wa asilimia 5.1 kwa mwezi Julai kutoka asilimia 5.9 za mwezi Juni, 2016.

  0 0

  Mshindi wa Miss kanda ya kaskazini Maurine Ayubu akiwa aakiwapungia mkono mashabiki,mara baada ya kutangazwa kuwa mrembo wa taji hilo akifuatiwa na mshindi wa pili Glory Stephen huku wa tatu akiwa ni Eligiver Mwasha warembo wote hawa wanatarajiwa kuingia kambini kushiriki shindano la miss Tanzania
  Wazee wa Ngwasuma wakitumbuiza kwenye onesho hilo.
  Muaandaaji wa shindano hilo Faustine Mwandago akiwa na warembo walioingia walishinda siku hiyo
  Hawa ndio warembo wote 12 walioshirki shindano la kumsaka Miss Kanda ya Kaskazini katika ukumbi wa Triple A arusha.

  0 0

  Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed (kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa First National Bank, Francois Botha (kushoto) kwa niaba ya washindi kumi wa kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es salaam leo. 
  (Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog). Meneja Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachang’a akiwapigia simu washindi wa droo ya kampeni inayoendeshwa na benki hiyo kuhamasisha uwekaji akiba ili kujikwamua kiuchumi ambapo washindi kumi walijipatia shilingi milioni moja kila mtu. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Sheria wa benki hiyo, David Sarakikya (kushoto), Mtaalamu wa Mfumo wa Habari na Mawasiliano wa FNB, Bi. Ilakiza Hezwa na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed (kulia).

   First National Bank Tanzania imetangaza washindi wa droo ya pili ya kampeni yake ya kuhamasisha uwekaji akiba. Kupitia droo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo jumla ya washindi kumi wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja kupitia mpango huo wa kuwahamasisha Watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

   Akiongea jijini Dar es salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa FNB Tanzania, Francois Botha alisema mbali na kuhamasisha uwekaji akiba, kampeni hiyo inalenga kuhimiza wananchi wote nchini ambao hawajafungua akaunti benki kujitokeza na kuweka akiba. Kupitia droo hiyo ya pili, shilingi milioni kumi imetolewa kwa jumla ya washindi kumi ambao ni Gabriel Mrosso wa Mwanza, Agnes Mndasha wa Dar es salaam, Ebenezer Moshi wa Mwanza, Amiri Mziray wa Dar es salaam, Nelis Kashanga wa Mwanza, Festo Msofe wa Dar es salaam, Daniel Kakesyo wa Mwanza, Boniface Likingo wa Dar es salaam, Michael Lusana wa Mwanza, Benedicto Makoye wa Dar es salaam.

   Botha aliwapongeza washindi hao na kuongeza kwamba benki hiyo inaendelea kufanya jitihada kubwa kuboresha huduma na kuongeza kwamba kampeni hii ni sehemu ya jitihada hizo zilizolenga pia kuongeza idadi ya watumiaji huduma za kibenki nchini. Kupitia kampeni hiyo inayofanyika kwa muda wa miezi mitatu, wateja wa FNB waliopo na wateja wapya wanaingizwa kwenye droo moja kwa moja kutokana na kila shilingi elfu hamsini wanayoweka akiba katika benki hiyo. 

  Jumla ya washindi 30 watanufaika kupitia kampeni katika muda wa miezi mitatu. Click here to Reply or Forward 2.02 GB (13%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 21 minutes ago Details Cathbert Kajuna's profile photo Cathbert Kajuna Show details

  0 0


  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Sekondari zitakazofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi jimboni humo zitapatiwa zawadi ya basi dogo aina ya mini-bus.

  Profesa Muhongo aliyasema hayo jimboni humo alipokuwa akitoa zawadi kwa washindi wa ngoma katika mashindano yaliyomalizika hivi karibuni jimboni humo.

  Alisema rafiki zake alio soma nao nchini Ujerumani katika chuo kikuu cha Goettingen University na chuo cha Technical University of Berlin wameahidi kutoa zawadi hiyo kwa masharti makuu mawili ambayo aliyataja kuwa ni ufaulu wa masomo ya Fizikia, Kemia, Hisabati na Baiolojia (PCM & PCB).
  Sharti lingine lililotolewa na wadhamini hao ni kwamba ushindi wa daraja la kwanza yaani Division I ambapo inatakiwa wanafunzi wasipungue 8 na daraja la pili yaani Division II inapasa wasipungue wanafunzi 12.

  Alisisitiza kwamba ushindani wa aina hiyo utaboresha elimu jimboni humo na hivyo kuwasisitiza walimu na wanafunzi jimboni humo kuongeza juhudi ili kushinda zawadi hiyo nono.

  "Ushindani utaboresha elimu jimboni mwetu, tujitume tupate mafanikio," alisema.

  Profesa Muhongo ameendeleza juhudi mbalimbali za kuhakikisha jimbo hilo linakuwa na maendeleo endelevu kwani amefanikisha kupunguza kero ya madawati jimboni humo na vilevile kuboresha sekta ya afya kwa kugawa madawa na gari za wagonjwa katika vituo mbalimbali vya afya jimboni humo.


  0 0

  UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. 

  Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 253.


  Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.


  MifukoyotehiiimewezakukidhivigezomuhimuvyauwekezajiambavyoniUsalama,UkwasinaFaida (Safety, Liquidity and Returns). 
  Wawekezaji wote wananufaika kwakupata faida shindani hivyo kuweza kukuza mitaji yao, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatariza uwekezaji, utalaamu wa meneja wamifuko, unafuu mkubwa wa gharama na uwazini vichocheo vinavyofanya UTT AMIS kuwa kimbilio lao.

  UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.


   Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi.

   Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS. Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa Maelezo hayo.

  Waziri wa Fedha Dr.Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu  UTT AMIS  wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi.


  0 0

  1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu. Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.

  GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....
  2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).

  Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.
  3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali

  4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................

  5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

  6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk..........

  7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali

  8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Mh.Mwigulu Nchemba leo amewasili mkoani Katavi,na kufanya ukaguzi kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.

  Katika ukaguzi huo, Mh. Nchemba amesema kuwa zoezi la uhakiki linafanyika ili kuchunguza mienendo yao na uwepo wao kwenye eneo la Kambi, amesema kuwa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya ndugu zetu ambao wamekuwa wakijihusisha na watu waovu, kufanya vitendo vya kibaguzi na kutoka nje ya kambi zao na kwenda nchi jirani bila kibali.

  Mbali ya kambi ya Katumba, Waziri Mwiguli alitembelea pia kambi ya Mishamo na kuviagiza vyombo vya usalama na kupitia Seririkali za mitaa kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, na kuongeza kuwa Tanzania haina tabia za kibaguzi "moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru" alisema Mh.Mwigulu.

  "Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi, kuishi na kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na vya kibaguzi. Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu" alisema Mh. Mwigulu.

  Waziri Mwigulu alikutana na Askari wa jeshi la polisi na idara zake zote na pia ametembelea gereza la mpanda ikiwa ni ziara ya kupata uhalisia wa changamoto zinazokabili jeshi la polisi, Magereza, Uhamiaji na zimamoto kwa kila mkoa,ambapo tayari kwa majawabu ya kudumu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi waliopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009
  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mh.Mwigulu Nchemba akiongozana na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Katavi, wakati alipotembelea kambi ya wakimbizi ya Katumba ambako kulikuwepo na zoezi la uhakiki wa waliokuwa wakimbizi kutokea nchi jirani ya Burundi na baadae kuamua kuwapa Uraia wa Tanzania mwaka 2009.


  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye ni Mbunge wa Namtumbo Mhandisi Edwin Ngonyani anawatarifu wakazi wa Namtumbo na watanzania kwa ujumla kuwa habari iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto si ya kweli na ina lengo la kumchafua katika utendaji wake wa kazi.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mhandisi Ngonyani amesikitishwa na taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la Mseto la tarehe 4 Agosti 2016 ikiwa kwenye ukurasa wa kwanza yenye kichwa cha habari kilichoandikwa "WAZIRI AMCHAFUA JPM".

  Habari hiyo ikiwa na nukuu "Waziri wa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kudaiwa kupokea fedha za kufanyia kampeni za ubunge kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama".

  Aidha Mhandisi Ngonyani amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari zenye taarifa kamili na kweli ili kuepuka upotoshwaji. Habari hiyo ilikuwa imedai kuwa Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amepokea kiasi cha dolla elfu 65 kwa Bw. James Sinclair ili zimsaidie kupata nafasi ya ubunge.

  Imeongeza kuwa alipewa kiasi cha dolla elfu 25 kutoka kwa Dr. Alphonce Koigi Machari ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trans Century ili apate nafasi hiyo hiyo ya ubunge.

  Mhandisi Ngonyani amelitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hiyo kwa haraka iwezekanavyo.

  0 0

  Operation Afya Njema ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela mjini Iringa leo.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akieleza mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akitafakari jambo.
   Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa akimtangaza Mkurugenzi mya wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  0 0  0 0  0 0

  TBC inakuletea kipindi kipya maalum ambacho kitawakutanisha wadau mbalimbali wakijadiliana na kuongelea umuhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma, kama ilivyoagizwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli.

  Kutana na Marin Hassan Marin katika kipindi hiki, kitakachoanza Jumatano, tarehe 10 August 2016 na kuendelea kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku TBC1, akikukutanisha watu mbalimbali katika kuchambua uamuzi huu muhimu wa kuhamia Makao Makuu Dodoma.

  Kutakuwa na maswali mbalimbali ambayo watazamaji watashiriki kuyajibu, na mshindi atajipatia zawadi kem kem.

older | 1 | .... | 1313 | 1314 | (Page 1315) | 1316 | 1317 | .... | 3270 | newer