Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1312 | 1313 | (Page 1314) | 1315 | 1316 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza na wanahabari wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Godfrey Weston Zambi (Wapili Kulia) wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Wengine pichani ni viongozi waandamizi wa TADB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Wapili Kulia), akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Bw. Adam Kamanda (Kulia).
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Kushoto) akipata maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kulia).


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

  Imeelezwa kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege  cha Dodoma utakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka tisini kuweza kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa ukanda wa kati.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa baada ya  kutembelea  kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco anayetekeleza kazi hiyo inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika kwa muda na kwa viwango vilivyokubalika.

  Amesema mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku arobaini na tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye kiwanja hiki itatumika kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.

  "Tunaamini kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze kutua na kuruka" amesema Prof. Mbarawa.

  Naye Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati na upanuzi inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na viwango na kukamilika kwa wakati

  "Tulipewa kazi hii na tunaahidi kuwa  itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia usafiri wa Anga", amesema Eng. Mdemu.

  Ameongeza kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara  ya kuruka na kutua ndege.

  Mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha  ndege cha Dodoma umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 11.8 na kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege zitakazosafirisha abiria wa mikoa ya kanda ya kati.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho Mkoani Dodoma.


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani,wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival litakalo fanyika jumamosi hii 13 August 2016 katika viwanja vya Rebstock Park,jijini Frankfurt,Ujerumani ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani,kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya.

  usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananachi wakati lipotembelea maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake) wakikagua vipando vya kabeji wakati walipotembelea banda la Magereza kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia picha yake iliyochorwa na kutolewa kwake na Chama cha Wandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania mkoani Mbeya (TAJATI) katika kilele cha sherehe za Maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwaja wa wa John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8, 2016. Watatu kulia kwake ni mkewe Mary na wapili kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria kwenye kilele cha Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Agosti 8, 2016.


  0 0

  UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 253. 

  Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika mfuko husika. 

  Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwa kupata faida shindani hivyo kuweza kukuza mitaji yao, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu mkubwa wa gharama na uwazi ni vichocheo vinavyofanya UTT AMIS kuwa kimbilio lao. 

  UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.
  Waziri wa Fedha Dr.Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu UTT AMIS wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi. 
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa Maelezo hayo. 
  Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi. 


  0 0  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisalimiana na Mkuu wa Wiliya Mjini Bi. Marina Joel Thomas (katikati) aliekuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
  Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” (kulia) Silima Haji Haji akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katika sherehe ya kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa.
  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akizunguza na wafanyakazi wa Wilaya ya Magharibi “B” na walikwa katika sherehe ya kumpongeza na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu iliyofanyika viwanja vya Skuli ya Urafiki Wilaya ya Magharibi “B”.
  Aliekuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.​
  Sehemu ya walikwa katika sherehe ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mjini Ayoub Mohammed Mahmoud na kuwaaga wafanyakazi waliostaafu.


  0 0

  Kuna baadhi ya magazeti na mitandao imekuwa ikiandika kuwa Dkt. Kigwangalla amesoma high school na aliyekuwa 'Tabibu', Ndg. Juma Mwaka, shule ya Kigoma Sekondari na kwamba walikuwa marafiki; hizi ni habari za uongo, za kupika zenye kupotosha ukweli ili kuwaaminisha watu kuwa 'wanajuana' na pengine wana ugomvi 'binafsi'. 

  Nimekuwa nikimpuuza kwa sababu sikuwa na haitotokea nikawa na nia mbaya dhidi ya mtanzania mwenzangu yeyote kwa sababu tu mimi nina dhamana ya uongozi. Sinaga tabia hiyo. 

  Uongo ukirudiwa rudiwa hubadilika na kuwa ukweli. Leo nimeamua, hapa chini, kukanusha ili watanzania pia mumpuuze, tuendelee kuimarisha huduma za tiba asili na tiba mbadala kutoka kwa matabibu wa kweli wanaofuata taratibu na siyo wasanii kama huyu. Uongo ama uzushi dhidi yangu mimi binafsi kamwe hautonirudisha nyuma mimi kama mtumishi wa umma. Lazima ifike mahali tujenge nchi ya watu 'serious' wanaofuata Sheria, Kanuni na Taratibu. Wanaoheshimu Serikali. Kwenye Afya za watanzania hatuwezi kuvumilia usanii, lazima tuwalinde walaji. Hili ni jukumu tulilopewa na Mhe. Rais. Tutasimamia Sheria ipasavyo. Hatutolegeza hata kidogo. 

  1. Sikusoma 'high school' Kigoma Sekondari. Nimesoma O'level (form I - IV) Kigoma Sekondari. High School nilisoma Shinyanga Sekondari. Sikumbuki kusoma katika shule zote hizi mbili na mtu mwenye Jina Hilo. Kama alisoma Kigoma Sekondari labda mbele yangu ama nyuma yangu. Pia kipindi nasoma Kigoma Sekondari, hakukuwa na 'high school'. 

  2. Ndg. Juma Mwaka hajawahi kuwa rafiki wala adui yangu. Sina ugomvi binafsi. Nafanya kazi ya kusimamia Sheria ya tiba asili na tiba mbadala ipasavyo. 

  3. Naithamini tiba asili na tiba mbadala na Ndiyo maana nimeongoza Wizara ya Afya kufanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo hili, ikiwemo kuweka utaratibu mzuri na rahisi zaidi wa kusajili watoa huduma, dawa zao, mazingira wanapotunzia dawa, wasaidizi wao, viwanda vyao, na pia kuweka mikakati ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa za tiba asili na tiba mbadala sambamba na kufanyia utafiti dawa zao na kudhibiti ubora wa dawa zenyewe na dozi wanazowapa wateja. 

  4. Muulizeni Ndg. Juma Mwaka anaposema ana ugomvi 'binafsi' na mimi, anamaanisha nini, ugomvi upi? Juu ya nini? Awape taarifa kamili. Mimi Sina ugomvi naye. Kwanza sikuwahi kumjua kabla ya ziara yangu ya kikazi pale Foreplan, ntakuwaje na ugomvi na mtu nisiyemjua? Si utakuwa ujuha huo? 

  5. Mnaofuatilia suala hili mtakeni Ndg. Juma Mwaka awape majibu ya Msingi ya hoja za wakaguzi kutoka Wizara ya Afya. Mimi nilikuwa msimamizi nikiwapa nguvu wataalam wafanye kazi yao. Wataalamu walikuwepo, nao ana ugomvi nao 'binafsi'? Mwambieni awajibu kama dawa za tiba ya kisasa kukutwa kwenye eneo lake la kazi ilikuwa halali? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya maboksi 200 ya dawa? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya magunia 10 ya dawa za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa usajili? Alikuwa na uhalali wa kuendelea kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wateja wake wafuate dawa pale ili wasikatishe dozi? Tena kinyume na katazo la Baraza la tiba asili na tiba mbadala! Yeye yuko juu ya Serikali? Yuko juu ya Sheria? Ama anadhani anaweza kuidhihaki na kuiogofya Serikali? 

  6. Baada ya ziara yangu ya December 2015, ambapo sikutoa maelekezo ya kumfungia wala kumfutia kibali, niliwaelekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala kuwa wawaite wawaelekeze matabibu wote wafuate Sheria, kanuni na taratibu. Waliitwa. Wakaelekezwa. Waungwana wakatii. Yeye hakutii, wakamfuta. Baada ya kufutiwa usajili, akaendelea kujitangaza na kutoa huduma, yeye ni nani?

  7. Kufanya haya ni kuvunja sheria za nchi. Na makosa haya yana adhabu zake. Sisi kama Serikali tumeagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Serikali ina mkono mrefu, itamkamata. Itamtia nguvuni na atafikishwa mahakamani. Ataenda kujitetea huko kuwa ana 'ugomvi binafsi' na Naibu Waziri Kigwangalla! 

  Mwisho, aende akafuatilie kisa cha mfanyabiashara wa kigiriki aliyesema ameiweka Serikali mfukoni - Mwalimu Nyerere alimfanya nini! 

  Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananachi wakati lipotembelea maonyesho ya wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inafufua sekta ya ushirika na kuwachukulia hatua kali watendaji wote waliohujumu ushirika na kusababisha machungu kwa wanaushirika ili iwe fundisho kwa wengine.

  Pia ameitaka Wizara hiyo kupitia upya sekta ya ushirika kwa kuanza na viongozi walipo ndani ya wizara hadi mikoani kuhakikisha kama wanafanya kazi zao ipasavyo na kuwaondoa watakaobainika kwa uzembe.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumatatu, Agosti 08, 2016) wakati akifunga maadhimisho ya sherehe za nane nane kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

  Hata hivyo Waziri Mkuu amesema mkulima, mfugaji na mvuvi mdogo au mmoja mmoja hawezi kupunguza umaskini bila ya kuwa na chombo cha kuwaunganisha na kuwapa nguvu ya kutetea bei ya mazao yao kama ushirika. Aidha, ushirika imara utawasaidia kutafuta soko, kupata mikopo ya riba nafuu.

  Amesema pamoja na umuhimu wa kuwepo kwa ushirika, tasnia hiyo imewaumiza wakulima wengi na kuwafanya kukata tamaa katika uzalishaji kutokana na usimamizi mbovu, ubadhirifu na ubabe wa baadhi ya viongozi wa ushirika.

  “Wahimizeni na kuwashawishi wakulima, wafugaji na wavuvi kujiunga katika vikundi vya ushirika vya uzalishaji na SACCOS. Aidha, elimu ya ushirika inayotolewa kwenye maonesho ya mwaka huu, iwe changamoto kwenu kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,” amesema.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali haitamvumilia mfugaji anayelisha katika maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji, Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kulinda maeneo hayo.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha alisema sekta ya kilimo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo katika kipindi cha miaka mine mfululizo nchi imeweza kuzalisha chakula cha ziada, ambapo kwa mwaka huu imezalisha kwa asilimia 123.

  “Mafanikio hayo yanachangiwa jitihada za Serikali katika kutoa ruzuku ya pembejeo, taasisi za utafiti ambazo zimekuwa zikitafiti aina bora ya mbegu zikitafuta mbegu bora na wakulima walioamua kuwekeza kwenye kilimo,” alisema.

  Naibu Waziri Ole Nasha alisema katika ukanda wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ni nchi mbili tu za Tanzania na Zambia kati ya nchi 15 za jumuia hiyo hazikabiliwiu na baa la njaa.

  Licha ya mafanikio hayo Naibu Waziri huyo aliwaomba wakulima kuendelea kuzalisha kwa kufuata kanuni bora za kilimo pamoja na kutumia pembejeo bora.

  Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus Mwanakatwe ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuwatetea pamoja na utatuzi wa kero za muda mrefu zilizokuwa zinawakabili wakulima ikiwemo ya tozo.

  Hata hivyo Mwanakatwe ameiomba serikali kuitafutia ufumbuzi changamoto ya upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo. Pia ameomba Serikali iwezeshe Benki ya Kilimo (TADB) kufungua matawi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili wakulima wake waweze kupata mikopo kwa urahisi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMATATU, AGOSTI 08, 2016.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

  Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE kitaifa katika uwanja wa NGONGO Manispaa ya LINDI mkoani LINDI kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI. 

  Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya NGONGO, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

  “Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”

  Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema maadhimisho ya sikukuu ya NANE NANE ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.

  Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla. 

  Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.

  Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.

  Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dakta PHILIP MPANGO amehimiza wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais 
  8-Aug-16

  0 0

   Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Engen Petroleum Tanzania Lt, Paul Muhato akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea kutimia Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo, iliyofanyika katika Mgahawa wa Rodizio, Mikocheni Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Engen Petroleum Tanzania Lt, Paul Muhato akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi Engen Tanzania wakati wa hafla ya kusherehekea kutimia Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo, iliyofanyika katika Mgahawa wa Rodizio, Mikocheni Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Engen Petroleum Tanzania, wakimsikiliza Mkurugeni Mkuu wao, wakati wa hafla ya kusherehekea kutimia Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo, iliyofanyika katika Mgahawa wa Rodizio, Mikocheni Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Engen Petroleum Tanzania, Paul Muhato (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, wakati wa hafla ya kusherehekea kutimia Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo, iliyofanyika katika Mgahawa wa Rodizio, Mikocheni Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, PWANI 

  WAFANYAKAZI wametakiwa kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanachapa kazi kwa bidii bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo. 

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti mpya wa chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na afya (Tughe)Mkoa wa Pwani Catherine Katele,wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho ulioambatana na uchaguzi wa viongozi.

  Mwenyekiti huyo alisema kwamba wafanyakazi wa Mkoa wa Pwani wanapaswa pia kuachana na makundi ambayo hayana maslahi yoyote kwa taifa kwani serikali iliyopo madarakani haipo tayari kumvumilia mtumishi mzembe anayeshindwa kutimiza wajibu wake.

  “Mimi kwanza napenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa kuweza kuniamini na kunichagua kuwa mwenyekiti wao mpya wa Tughe Mkoa wa Pwani, lakini kitu kikubwa nawaomba tuachane na kufanya kazi kwa mazoea hii ni hatari sana na kitu cha msingi ni kila mmoja wetu atekeleze majukumu yake ipasavyo,”alisema Catherine.

  Katele,alisema kwamba katika uongozi wake atahakikishe anaweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwasaidia wafanyakazi kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuwapa moyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Aidha aliongeza kuwa ataweza mpango kazi wake wa kupita katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwapa elimu wafanyakazi kuhusina na uwajibikaji pamoja na utawala bora.

  Alisema,Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Magufuli haitaki kuona mtumishi au mfanyakazi yeyote analeta masihara katika utekelelzaji wa majukumu yao hivyo ni vema kuhakikisha wanajenga misingi imara katika kucha kazi na sio vinginevyo.

  “Ni vema wafanyakazi sasa tubadili tabia zetu na tuendana na kasi ya Rais wetu, nadhani mnatambua serikali ya wamu ya tano haitaki kuona mtumishi ambaye ni mzembe kwa hivyo na sisi tujifunze ii kuepukana na kutumbuliwa,”alisema Mwenyekiti.

  Katele,alisema anatambua kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wafanyakazi na wanachama wa Tughe kiujumla lakini kamwe wasitumie migomo na maandamano yasiyo na tija katika kudai haki zao ila ni vyema watu wakafuata utaratibu ulio sahihi.

  Alisema,mara nyingi watu wanadhani kufanya migomo ndio suluhu ya kupata haki zao jambo ambalo sio sahihi na kwamba madhara ya kufanya hivyo ni makubwa kwani wanaweza kupoteza kazi bila sababu ya msingi.

  Alisema ,kwasasa atatumia nafasi yake kushirikiana na wakuu wa idara ili kuona jinsi ambavyo wanaweza kuchukua hatua sahihi za kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki na maslahi yao kwa wakati.

  Hatahivyo,Katele amewataka wafanyakazi kutii sheria za kazi huku akiwaomba watumishi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili waweze kusaidiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwenyekiti huyo mpya Catherine Katele alichaguliwa na kuwa mshindi baada ya kupata idadi ya kura 38.

  0 0


  Na Mathias Canal, Dodoma

  Maonesho na Mashindano ya mifugo Kitaifa sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde wakati akifunga maonesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Kati Dodoma yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja wa Nzuguni kwa kauli mbiu ya "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).

  Amesema kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli inatekeleza azma ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma ameishauri Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi na ile ya Biashara na masoko kuangalia uwezekano wa kuanzisha rasmi maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ya Kimataifa (International Agriculture Trade Fair) katika uwanja wa Nzuguni ambao ndio uwanja wenye eneo kubwa kwa maonesho ya Kilimo hapa nchini.

  Aidha ametoa wito kwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo kuendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

  "Naomba niwaambie wakulima na wafugaji wetu kuwa maonesho ninayoyafunga hii leo ni muafaka na fursa nzuri kwao hususani vijana kwenda kuanza mara moja kutumia mlichojifunza na kuleta mapinduzi yenye maendeleo chanya yanayotarajiwa kiuchumi, hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuzikumbusha Halmashauri za serikali za mitaa zote kuwahamasisha wakulima, Wafugaji na wadau wengine kutumia teknolojia zilizooneshwa hapa kuongeza ufanisi wao katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi” Alisema Mavunde

  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini maelekezo ya namna ya kuchakata mihogo kutoka kwa mkulima wa zao hilo tangu mwaka 1980 kutoka Kijiji cha  Nzuguni Josiah Malogo Ndoya
  Mhe Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini namna ya kulima mahindi kwa mbinu bora na za kisasa ili kuwa na mavuno yenye tija.
  Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza maelekezo katika banda la Halmashauri ya Wilaya  ya Chemba kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa katika kilimo cha kisasa 

  Mhe Mavunde alipotembelea banda la ushonaji la Jeshi la kujenga Taifa JKT katika Maonesho ya Nane nane kabla ya kuyafunga rasmi 
  006 Mhe Mavunde alipotembelea banda la maonesho ya wanyama aina ya mbuzi, Ng’ombe na Kondoo la kampuni ya Ranchi za taifa (NARCO LTD) .


  0 0  Mwananchi aliyefika katika banda la Huduma ya Afya ya Macho akifanyiwa uchunguzi wa Macho katika maadhimisho ya sherehe za Nane Nane mkoani Lindi leo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mheshimiwa George B. Simbachawene alipotembelea banda la Sightsavers na idara ya afya mkoa akisikiliza kwa makini maelezo ya shughuli zinazofanywa na washirika hawa ili kutokomeza ugonjwa wa vikope mkoani Lindi hadi sasa jumla ya wagonjwa 830 wamekwisha pata usawaziswaji wa vikope mkoa wa Lindi. Katika wilaya ya Ruangwa na Nachingwea, kulia akizungumza Dr. Leonard Ndeki afisa mradi kutoka shirika la Sightsavers Tanzania katikati mwenye T-Sheti ya bluu ni Dr. Mwita Machage Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Lindi

  Timu ya washiriki toka shirika la Sightsavers na watumishi wa Idara ya Macho Mkoa wa Lindi waliokaa wakiendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa macho, Ushauri na Tiba kwa wananchi wa mkoa wa Lindi. Kutoka kushoto Dk. Mwita Machage, Dk. Leonard Ndeki (Sightsavers), Bw. Richard Shaban na aliyesimama mwenye T-Shirt nyeusi ni Zera Ombeni.
  Baadhi ya wanawake na wanaume wa mkoa wa Lindi waliofika kwenye banda la Sightsavers na Idara ya afya mkoa kupata huduma ya macho wakisubiria kupata huduma wakisubiri kuhudumiwa na wataalam wa Macho. 


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga gitaa na kuimba wakati wa uzinduzi wa shindano la Club Raha Leo msimu wa tatu katika ukumbi wa Club 71 Kibo Complex Tegeta Jijini Dar es Salaam Agosti 7,2016.

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM

  Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imedhamiria kurasimisha kazi ya sanaa kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizundua msimu wa tatu wa kipindi cha televisheni cha kusaka vipaji vya wasanii chipukizi cha Club Raha Leo Show na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wadau wa sanaa na wasanii ili kufanikisha azma ya serikali ya kurasimisha sekta hiyo kuwa rasmi kama shughuli ya kiuchumi.

  “Tutashirikiana na nyinyi katika kuiendeleza sekta ya sanaa nchini ili kuwezesha vijana wengi wenye vipaji kuweza kujiajiri na kuajiri wengine kupitia kazi zao za sanaa” alisema Mhe. Nape.

  Mhe. Nape Moses Nnauye amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano mbalimbali ya kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kuweza kufikia malengo ya kuendeleza sekta ya sanaa nchini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba amesema kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litaendelea kushirikiana na wadau wa sanaa nchini kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii mbalimbali ili kuwezesha sanaa kuwa ajira rasmi katika kuinua kipato cha msanii na uchumi wa taifa kwa ujumla.

  Naye Mratibu wa Club Raha Leo Show Bibi. Susan Mungi amesisitiza wasanii kuheshimu kazi zao na kuzifanya kwa ustadi mkubwa kwani ndio nyezo muhimu katika kuendeleza kazi ya sanaa nchini kwa kuifanya kuwa kazi mojawapo ya kiuchumi.

  Club Raha Leo Show ilianzishwa kama Kipindi cha redio kilichorushwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuwa shindano kubwa Tanzania la kusaka, kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wanaochipukia nchini, na huu ni msimu wa tatu wa shindano hilo.

  0 0

  Mkutano wa Kimataifa kuhusu ugonjwa wa Hemophilia limemalizika Orlando, nchini Marekani Julai 24-28, 2016. Lilikutanisha zaidi ya wadau 6,000 kutoka takribani nchi 130 duniani chini ya World Federation of Hemophilia (WFH). Hemophilia ni ugomjwa wa damu wa kurithi ambapo damu inakosa uwezo wakuganda pale mshipa unapodhurika. Huwapata zaidi watoto wa kiume. Malengo makuu yalikuwa kuboresha tiba na maisha ya wagojwa.

  Pamoja na mambo mengine, kongamano ni jukwa la kutambua jitihada zinazofanyika duniani kote hususani utafiti wa kupata tiba na uangalizi bora kwa wagonjwa. Hutengeneza jukwa na mtandao kwa wagonjwa, wazazi /jamaa, madaktari bingwa, wahudumu, watengeneza sera na watafiti wa dawa na kujenga mahusiano na baraza la kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa washiriki toka sehemu mbalimbali duniani.

  Moja ya mafanikio ni ugunduzi wa dawa (factors) zenye uwezo wa kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi (longer half-life drugs) na hivyo maisha bora kwa wagonjwa. Pili ni upatikanaji wa misaada (donations) ya dawa kutoka makampuni yanayotengeneza dawa kwa nchi maskini. Ikumbukwe nchi hizi hazimudu kununua dawa kwa wagonjwa kutokana na bei yake kuwa kubwa. Tanzania imewakilishwa na Raisi wa Chama cha Hemophilia Bw. Richard Minja

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya Ushindi wa pili katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Mbeya, Julius Sang'unda wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin Mtono . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ngao ya ushindi wa tatu katika kundi la Tasisi na Mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Eneo la Ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geofrey Kirenga wakati alipofunga Maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 8, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos makalla na wapili kulia kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. Kulia ni Mwenyekiti wa TASO wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Crispin Mtono

  0 0

  TIMU ya Simba imeweza kutoka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya AFC Leopards kutoka nchini Kenya, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 80 ya tangu kuanzishwa kwa timu ya Simba.

  Simba iliweza kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa ambapo dakika ya 38 Ibrahim Ajib aliipatia Simba bao la kuongoza baada ya kupokea pasi safi toka kwa Jonas Mkude na kuachia shuti la chini chini umbali wa kama mita 25.

  Kipindi cha pili Simba iliwaingiza Muzamir Yassin, Jamal Mnyate na Laudit Mavugo ambao walibadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza mashambulizi na kuwafanya mabeki wa Leopards kuwa 'bize' muda wote kupambana na washambuliaji wa simba jambao ambalo lilishindwa kufua dafu mbele ya washambuliaji hao.

  Dakika ya 55 Ajib tena anaifungia Simba goli la pili baada ya Mavugo kuichambua vyema safu ya ulinzi ya Leopards na kumrahisishia mfungaji.

  Dakika kumi baadae Kichuya alifungia Simba goli la tatu baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Mavugo.

  Ilichukua kama dakika saba hivi baada ya goli la tatu, pale Mavugo alipoifungia timu yake goli la nne baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na Kichuya ambaye aliwafanya mabeki wa Leopards kuwa nae macho muda wote.

  Mashabiki wa Simba waliohudhuria mchezo huo wameonesha imani kubwa kwa kikosi chao hicho kilichosukwa chini ya Omog kwa ushirikiano na Jackson Mayanja.
  Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Laubit Mavugo akishangilia mara baada ya kuipatia timu yake bao la Nne dhindi ya Wageni wao, AFC Leopards ya Nchini Kenya, wakati wa Mtanange wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu wa Msimbazi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Hadi kipenda cha mwisho kilipolizwa na Mwamuzi, Heri Sasi, Simba ilikuwa ishaichakaza AFC Leopards kwa Bao 4 - 0. 
  Nahodha wa Timu ya Simba, Jonas Mkude akiangalia namna ya kumtoka Mchezaji wa Timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya, Bernard Ongoma, wakati wa Mtanange wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu wa Msimbazi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.Simba imeshinda 4-0.
  Mgeni Rasmi katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya Simba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiongozana na viongozi mbali mbali wa Timu ya Simba kuingia uwanjani kuwasalimia Wachezaji pamoja na Washabiki waliofurika kwa wingi uwanjani hapo.
  Msemaji wa Timu ya Simba, Haji Manara akitoka kuwasabahi mashabiki wa Simba waliofurika uwanja wa Taifa leo.
  Wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta wakitoa Burudani uwanjani hapo.


  0 0

   Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (wa pili kushoto), akizungumza na wamiliki wa shule za udereva (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers Buguruni Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla na Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati
   Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati), akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni. 


  Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  0 0


  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho 23 ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Sehemu ya Wakazi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Luteni Joseph Benedict Lyakurwa wa Suma JKT alipotembelea eneo lao na kujionea shughuli mbali mbali za kilimo na ufugaji kwenye kilele cha maadhimisho ya 23 ya sikukuu ya wakulima ya Nanenane mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Daraja la kwanza Halima Kikwega wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane , Ngongo Lindi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi mikono wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya Wakulima Nane nane mkoani Lindi.
  ...............................................................
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane kitaifa katika uwanja wa Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani Lindi kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
  Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Ngongo, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.
  “Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”
  Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.
  Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
  Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.
  Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.
  Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amehimiza wananchi kote nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

older | 1 | .... | 1312 | 1313 | (Page 1314) | 1315 | 1316 | .... | 3272 | newer