Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

NAIBU SPIKA DKT TULIA ACKSON ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA LOLEZA JIJINI MBEYA

$
0
0
MH.NAIBU SPIKA DKT TULIA ACKSON AKIWA NA WANAFUNZI LOLEZA GIRLS HIGH SCHOOL JIJINI MBEYA SHULE AMBAYO ALIHITIMU KIDATO CHA NNE. KATIKA SHULE HIYO NAIBU SPIKA ALITOA SH. MILIONI 5 KUSAIDIA UJENZI WA BWENI, KAZI AMBAYO TAYARI IMEKAMILIKA

AICC YASHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA (NANE NANE) KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kimeshiriki maonesho ya Nane nane yanayofanyika kitaifa viwanja vya Ngongo, Mkoa wa Lindi. 
Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo yakiwa na kauli mbiu “Kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo. Kijana shiriki kikamilifu. Kupitia maonesha ya Nane Nane mwaka huu AICC pamoja na tawi lake la Dar es Salaam, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) inapata fursa ya kukutana na wadau wake na wananchi kwa ujumla kuwaelezea juu ya huduma zitolewazo na Shirika hilo. Huduma hizo ni pamoja na utalii wa mikutano, upangishaji wa nyumba za makazi na nafasi za ofisi kwa upande wa Arusha.
Afisa Masoko na Utafiti Mkuu wa AICC Bi.Linda Nyanda akitoa maelezo kuhusiana na huduma zitolewazo na AICC na JNICC kwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi SACP Tusekile Mwaisabila (kulia).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Bw.Jomaary M. Saturi akisikiliza kwa makini maelezo toka kwa Mkuu wa Masoko na Utafiti wa AICC Bi.Linda Nyanda, alipotembelea banda la AICC kwenye maonesho ya Nane nane yanayoendelea Mkoani Lindi

Muhimbili Kutumia Mitandao ya Simu Kulipia Huduma za Matibabu

$
0
0

Na John Stephen, MNH

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kuanza kutumia mitandao ya simu, kadi maalimu na kadi za benki kwa ajili ya kulipia huduma za matibabu ili kuthibiti changamoto za upotevu wa fedha na wizi katika ukusanyaji wa mapato ya hospitali hiyo.

Mpango wa kutumia njia za kieletroniki umelenga kukusanya mapato zaidi ili kuiwezesha hospitali hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za uendeshaji na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Lengo la hospitali hiyo ni kuongeza mapato na kupunguza matumizi na kutengeneza mazingira ya kujiendesha na kutoa huduma bora kwa wagonjwa mbalimbali nchini. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja, Bwana Aminiel Aligaesha, hospitali hiyo imelenga pia kuimarisha njia za ukusanyaji mapato ili kuboresha huduma za matibabu na kuboresha maslahi kwa wafanyakazi. 

“Hospitali imelenga kuboresha wadi za kulaza wagonjwa wanaohitaji huduma na malazi binafsi, kuhakikisha wagonjwa wanachangia huduma za matibabu na kuboresha mfumo wa kuandaa hati za madai kwa kampuni na mifuko ya Taifa ya bima ya afya. 

“Hospitali imekusudia kutoa motisha na kuwahamasisha madaktari kuwaona wagonjwa kwa wingi wanaolipia huduma ili kuwavutia kutibiwa katika hospitali hii,” imesema taarifa hiyo. 

Taarifa hiyo imeeleza kwamba hospitali hiyo imedhamiria pia kutoa motisha kwa wafanyakazi wengine ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi. 

Katika hatua nyingine, hospitali hiyo imeweka mikakati ya kupunguza gharama za kununua dawa na vifaa tiba kutoka viwandani (Manufacturers)moja kwa moja.

“Kwa mfano, baada ya kupata kibali kutoka TFDA, Hospitali imenunua dawa za figo (immunosuppressant) kutoka  India kwa Sh 226 milioni wakati hapa nchini zingegharimu Sh 500 milioni,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, hospitali hiyo imeagiza nyuzi za kushonea wagonjwa (sutures) kutoka kiwandani (Ethicon)kwa gharama ya Sh 321 milioni wakati zingegharimu Sh 668 milioni endapo zingenunuliwa nchini.

Katika taarifa hiyo imebainisha kuwa hospitali hiyo imeweza kupunguza gharama za uchujaji wa damu (dialysis) kutoka wastani wa Sh 250,000 kwa kila zamu (session) hadi kufikia Sh171,000.


Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Prosper Mbena atembelea wapiga kura wake

$
0
0
Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Prosper Mbena akiwa njiani kuwatembelea wananchi wake wa kijiji cha Baga mwanzoni mwa wiki hii. Mbena anakuwa Mbunge wa kwanza kutembelea kijiji hicho kilicho mbali na hakina barabara na chenye mto mkubwa wa mvuha na mlima mkali wa Umangu. Wananchi wa huko wanateseka sana kwa  kukosa barabara na daraja kwenye mto Mvuha.

TAMKO LA TFF JUU YA SAKATA LA SIMBA SC NA MO

Jokate ajenga uwanja wa netiboli na kikabu kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified"

SAUTI SOL WANENA MAFANIKIO YA MUZIKI WA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA EFM REDIO.

$
0
0
Wasanii wa kikundi cha muziki cha Sauti Sol kutoka nchini Kenya  wamefanya mahojiano na kituo cha redio cha Efm 93.7 fm kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12:00 hadi saa 3:00 Asubuhi. 
 KATIKA mahojiano hayo Sauti sol wamesema kuwa wanamuziki wa Afrika Mashariki wanalipwa vizuri katika show wanazozifanya ikilinganishwa na wasanii wa Nigeria, vilevile Lugha ya Kiswahili imekua Lugha nzuri yenye vionjo hivyo imeweza kuvutia wasanii wengi wa nje ya Tanzania kuitumia katika nyimbo zao. 
 Baada ya kufanya vizuri kwa nyimbo yao ya "Unconditional bae" walioshirikiana na msanii wa Tanzania Ali kiba, wamewataja pia wasanii wengine wa Tanzania ambao wanatarajia kushirikiana nao katika nyimbo zao zijazo ambao ni Vanessa Mdee, Weusi, pamoja na Diamond Platnumz.

Ajira App Tanzania - Watu waliofanikiwa kupata Ajira kupitia Ajira app


TTCL KUIUNGANISHA TANROADS NCHI NZIMA.

$
0
0
 Menejimenti ya TTCL na TANROADS wakiwa katika hafla ya kusaini mkataba wa TTCL kutoa huduma ya intaneti na  kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kupitia Mkongo wa TTCL.  
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura (Kulia),  Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfungale (Katikati) na  Mwanasheria wa TANROADS Dora Komba (Kushoto) wakisaini mkataba wa makubaliano ya TTCL kutoa huduma ya kuunganisha ofisi za TANROADS nchi nzima. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani baada ya TTCL kupata zabuni ya kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kwenye mkongo wa TTCL.

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL zimetiliana saini Mkataba wa huduma za Intaneti ambapo TTCL itaunganisha ofisi za Wakala hiyo nchi nzima kwa kutumia Mkongo wake wa Mawasiliano. 
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na  kuhudhuriwa na Mtendaji Mkuu (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, Afisa Mtendaji Mkuu (TTCL), Dkt Kamugisha Kazaura pamoja na maafisa Waandamizi kutoka TTCL na TANROADS. 
Mradi huo utakaotekelezwa katika Mikoa 25 na Vituo (3) vya mizani utatumia miundombinu ya mawasiliano ya Kampuni ya TTCL iliyounganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB). Mikoa hiyo ni pamoja Makao Makuu ya TANROADS, Mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma, Tanga, Mtwara, Kibaha, Iringa, Musoma na Bukoba. 

Mikoa mingine ni Dar es salaam(Keko na Mabibo), Lindi, Makambako, Mwanza, Songea, Manyara, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Sumbawanga, Simiyu(Bariadi), Arusha, Mpanda, Moshi, Geita na Morogoro
Kampuni ya Simu Tanzania TTCL inatekeleza Mpango Mkubwa wa Mageuzi ya Kibiashara ambao umelenga kuboresha miundombinu ya Mtandao na biashara ili kukidhi mahitaji ya wateja na Nchi katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasilaino. Hadi sasa, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeunganisha makampuni binafsi, Mashirika ya Umma na ofisi za serikali zaidi ya 80 kwenye miundombinu ya mawasiliano ya TTCL yenye ufanisi mkubwa wa kimawasiliano ndani na nje ya nchi.

MBOWE AMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE NYUMBANI KWAKE SALASALA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe leo Jumatano 03/08/2016 amemtembelea Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai nyumbani kwake Salasala jijini Dar es salaam, ambae amerejea hivi karibuni kutoka nchini India ambako alikwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai nyumbani kwake Salasala jijini Dar es salaam, alipokwenda kumjulia hali leo.

NHIF YASHIRIKI MAONESHO YA NANANANE KITAIFA NGONGO MKOANI LINDI KWA UPIMAJI WA AFYA NA UTOAJI ELIMU KWA UMMA

$
0
0
Ofisa matekelezo wa bima ya afya Salvatory Okum akitoa maelezo ya faida na umuhimu wa uchangiaji wa huduma za matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa wananchi waliotembelea banda la mfuko ambapo elimu kwa umma ni moja ya huduma zinazotolewa.
Timu ya wataalamu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya wakiendelea na zoezi la upimaji wa afya kwenye magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi waliofika kwenye banda la mfuko ngongo mjini Lindi.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwapa maelezo ya mpango wa KIKOA unaowawezesha wanavikundi,wajasiriamali kupata huduma za matibabu kuchangia mara moja kwa mwaka (Shs 76,800),kwa wananchi waliotembelea katika banda la mfuko lililopo kwenye viwanja vya Ngongo mjini Lindi.

mashindano ya Mchezo wa Pool Mkoa wa Dar kufanyika Viwanja vya TCC

$
0
0
CHAMA cha chezo wa Pool Mkoa wa Dar es Salaam kimeaandaa mashindano ya Pool katika kusheherekea siku kuu ya nanenane yatakayofanyika katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaamyajulikanayo kama “88” Pool Competitions 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah alisema maandalizi yako vizuri kwani mpaka sasa mikoa 12 imeshathibitisha kushiriki ikiwakilishwa na baadhi ya vilabu vyake.

Alisema Machellah mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Dodoma, Morogoro,Iringa,Mbeya,Pwani,Tanga,Kilimanjar o,Arusha,Manyara,Mkoa wa kimichezo wa Ilala, Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni na Mkoa wa kimichezo wa Temeke ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.

Mashindano yao yanatarajiwa kuanza rasmi Alhamis tarehe 4 Agosti 2016 na kumalizika siku ya siku kuu ya nane nane tarehe 8 Agost 2016. Zawadi katika mashindano hayo, Bingwa upande wa timu ataibuka na Kashi shilingi laki tano na kikombe, msindi wa pili 250,000/-, mshindi wa tatu 150,000/- na mshindi wa nne ni 50,000/-.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Bingwa atazawadiwa Shilingi 200,000/-, wa pili shilingi 100,000/-, mshindi wa tatu 50,000/- na wan ne ni shilingi 25,000/-.

Mwisho aliwaomba wadau na wapenzi wa mchezo wa pool kujitokeza kuja kushuhudia mashindano hayo katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mashindano ya Pool ya nane nane( “88” Pool Competition 2016), Michael Machellah (kushoto) akiwakabidhi Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wa mchezo huo, Hashim Sheweji(kulia) na Bingwa wa Afrika wa mchezo huo 2014, Patric Nyangusi, kikombe cha mshindi wa kwanza wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho katika viwanja vya TCC Chang’ombe Mkoani Dar es Salaan.Picha Prona Momwi.

MTOTO ATOA MSAADA WA MADAWATI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (kushoto) akimshukuru mtoto Aisha Mshantu kwa Msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma.
Mtoto Aisha Mshantu (kulia )akimkabidhi madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme aliyoyatoa katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma.
Mtoto Aisha Mshantu na wazazi wake Mzee Mshantu (wa kwanza kulia) na Bi Rehema (wa pili kulia) wakiwa amekaa katika madawati aliyoyatoa mtoto huyo kama msaada katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme.

NA RAMADHANI JUMA, DODOMA 

KATIKA hali isiyotegemewa msichana mdogo Aisha Mshantu ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka 2016 ameitikia wito wa Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli wa kuwaomba wadau kushiriki katika zoezi la kuchangia madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nchini ili waondokane na adha ya kujifunza wakiwa wameketi chini.

Aisha ametoa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5.2 katika shule ya Msingi ya Mwenge iliyopo katika kijiji cha Mbabala A Kata ya Mbabala Manispaa ya Dodoma, ambapo amesema hiyo ni ndoto yake ya muda mrefu na kwamba anafuraha kuikamilisha ili kuonesha alivyoguswa na tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wa kujifunza.

Mbali na msaada huo wa madawati, msichana huyo ambaye amezaliwa akiwa mlemavu, pia ametoa msaada wa mataulo maalum 84 kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika shule hiyo yenye thamani ya shilingi laki mbili, kama chachu ya kuwazindua wasijiingize katika masuala ya mahusiano kwa kudanganywa na wanaume kwa kuahidiwa mahitaji madogo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo juzi baada ya kupokea misaada hiyo kwa niaba ya Serikali na Manispaa ya Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme alimshukuru mtoto Aisha kwa msaada huo ambapo alisema msichana huyo ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa watoto wenzake huku akitoa wito kwa jamii kujifunza kutokana na tukio hilo.

“Hakuna fedha isiyokuwa na kazi..Aisha ana mahitaji yake na angeweza kuzitumia fedha hizi kwa matumizi mengine ya binafsi lakini yeye ameamua kusaidia wadogo zake wa shule ya Msingi..hili ni jambo la kijasiri sana kwa mschana mdogo kama huyu na ni funzo kubwa kwa jamii nzima” alisema.

Akielezea ndoto aliyokuwa nayo mtoto wake kwa muda mrefu, mama mzazi wa Aisha Bi Rehema alisema mtoto wake huyo alifungua akaunti ya ‘Jumbo Junior’ katika Benki ya CRDB Dodoma na kuanza kujiwekea akiba kidogo kidogo hadi alipofikia azima yake hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Felister Bura ameahidi kukarabati darasa moja katika shule hiyo ambako madawati hayo yatatumika, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Msichana Aisha ambaye kwa sasa ni Balozi wa Elimu wa Umoja wa Mataifa (UN) kupitia programu ya ‘4 Quality Education’.

BENKI YA NMB YAZINDUA MPANGO WA AGRIBIASHARA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA FEDHA KWENYE KILIMO.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na Benki ya NMB kuzindua biashara ya kilimo Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Renatus Mushi na kulia ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed.

BENKI YA NMB imezindua mpango mkakati wenye thamani ya bilioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma zake za fedha kwa miaka mitano kwenye upande wa Kilimo.

Mpango mkakati huu hususan unahusu kupanua huduma za fedha kwenye mazao zaidi ya kilimo – kutoka matano mpaka zaidi ya 12. Mpango huu utatoa fursa ya huduma za fedha sio tu kwa wakulima (kupitia mfumo wa vikundi na kwa mkulima mmoja mmoja), lakini vilevile utaongeza uzalishaji zaidi kupitia mnyororo mzima wa thamani katika kilimo – yaani tangu kwa mtoa pembejeo, mzalishaji (mkulima), mchakataji, msafirishaji, mfanya biashara (muuzaji wa jumla, wa rejareja, na wanje ya nchi).

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki yake inatambua umuhimu na nafasi ya sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi hii, na ndiyo maana imechukuwa juhudi za makusudi kuboresha na kupanua huduma za fedha zinazolenga kuikuza sekta hii.

Alisisitiza “Kwa kuzingatia umuhimu wa kuboresha sekta ya kilimo Tanzania, tunalenga kujenga mazingira na taratibu ambazo mkulima mdogo na washiriki wote kwenye mnyororo huu wa thamani wataweza kuboresha ufanisi: katika upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji kwa njia za kisasa (mbgu bora, mbolea, kutumia zana na nyezo mabalimbali za kilimo, n.k.), pamoja na ufanisi kwenye masoko. Yote haya yanawezekana kupitia kupatikanaji wa uhakika wa huduma za fedha kwemye kilimo.

“NMB tunaona fursa kubwa sana kwenye sekta ya kilimo”, aliongeza. “Tunaamini kwa kuongeza ushiriki wetu kwenye sekta hii, kutakuwa na msukumo chanya kwenye maisha ya wakulima wetu na wote kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hii, na vilevile kutimiza malengo ya NMB”. Alisisitiza. Bi Bussemaker vilevile alisema kwamba NMB Tayari inawafikia wakulima wadogo wasiopungua 600,000 nchi nzima. Kwenye mpango mkatai huu mpya, benki hii sasa vilevile inawalenga wakulima wakubwa, wafanyabiashara wa pembejeo, wachakataji wa mazao ya kilimo, wafanyabiasha / wauzaji wa mazao na wahusika wengine wote kwenye mnyororo mzima wa thamani katika kilimo.
 Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa biashara ya kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker, Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Seif  Ahmed na Mkuu wa Kitengo cha biashara ya Kilimo wa Benki ya NMB, Renatus Mushi  wakionesha bango la Kilimo Mpango Mzima linalojumiisha Pembejeo, Ukulima, Mazao,Uuzaji,Usindikaji na Usambazaji ulio bora, thabiti na wakisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker akionesha namna benki ya NMB ambavyo inajishughulisha na biashara ya mazao kwa wakulima wa mazao hapa nchini ambapo NMB  katika mpango huo mkakati wenye thamani ya mabilioni kwa ajili ya kuboresha huduma zake za fedha kwa miaka mitano.

WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI BIDHAA ZA NDANI.

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Meneja mauzo wa Kampuni Old East International akiwa anamfafanulia mteja juu ya Crown Cartridge,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane.
Afisa Mipango wa Kampuni Old East International Ephrahim Moses Mwano akiwa anaonyesha Aina ya Wino wa Crown ambao wanatengeneza hapa nchini,Katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Katika viwanja vya nanenane Njiro Jijini Arusha.

Na Woinde Shizza,Arusha.
Wito umetolewa kwa Watanzania watumie na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Old East International ndugu Moses Mwano ,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane njiro Jijini Arusha.

Mwao amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha ubora unaotakiwa kwa mtumiaji.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Old East International amesema kuwa kampuni hiyo ni ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika kutengeneza wino wa kuchapia unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.

Kwa upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za kuifanya Nchi kuwa ya Viwanda.

Sambamba na hayo amewaasa Watanzania watengeneze na kuingiza Bidhaa zenye kukidhi ubora na viwango ,huku akimalizia na msemo usemao " kizuri cha jiuza kibaya chajitembeza akimaanisha kuwa ukitengeneza bidhaa nzuri yenye kukidhi viwango na ubora unaohitajika wateja watafurahiwa nayo.


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 02/08/2016

Usajili Rock City Marathon waanza; RC Mongella awa wa kwanza kujisajili

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella jana alikuwa mtu wa kwanza kujisajili kushiriki Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo mkoani humo Bw Mongella aliekuwa ameambatana na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka, pamoja na viongozi wengine wa mchezo huo alitoa pia aliahidi kukimbia mbio za kilomita 21 ili kuonyesha nia ya dhati katika kuinua mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

“Nitamke rasmi kwamba kwa sasa Rock City Marathon ni agenda ya mkoa na hivyo basi nitahakikisha kwamba mbio hizi zinapata washikiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mkoa huu. Haiwezekani mbio za mkoa wa Mwanza zitegemee wadhamini wengi kutoka Dar es Salaam huku Mwanza kukiwa na makampuni na mashirika yenye uwezo wa kuusaidia mkoa wao,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Mongella msukumo wake huo kwenye ushiriki wa mbio hizo unatokana na si tu nia ya kuinua mchezo huo mkoani mwake bali pia malengo ya mbio hizo ya kutangaza utalii wa ndani wa mkoa huo pamoja na kupinga vita ujangili hususani mauaji ya tembo.

Kwa upande wake Bw Mtaka mbali na kuwapongeza wadhamini wa mbio hizo yakiwemo mashirika ya Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust pia alitoa wito kwa makampuni mengine ya hifadhi na kitalii yafikirie kutumia fursa hiyo kutangaza utalii wa ndani.

“Pamoja na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizi pia yaani kampuni ya Capital Plus International naomba nitoe wito kwao kuhakikisha wanaandaa utaratibu wa kuwaandaa washiriki wa mbio hizo miezi mitatu kabla kwa kuhakikisha wanapata mazoezi ya kutosha ili kama taifa tuwe na matokeo mazuri dhidi ya washiri kutoka mataifa ya nje,’’ alisisitiza.

Akizungumzia mbio hizo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema Mbio hizi zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na lengo la kusaidia utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadha nchini kuanzia umri mdogo kabisa sambamba na kutangaza utalii wa ndani kupitia michezo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella (alievaa kofia nyeusi) sambamba na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka ( wa kwanza kulia) wakisaini fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza. Anaeshuhudia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi yam bio hizo Bw Zenno Ngowi (wa tatu kulia)
ais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi (kushoto) fomu za ushiriki wa Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kusaini ili kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo. Anaeshuhudia (katikati) ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella..
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo. Pamoja na mambo mengine Bw Mongella alielezea adhma yake ya kushirikia mbio za kilomita 21 kwenye Rock City Marathon.
Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza ndg John Mongella ( mwenye kofia nyeusi) pamoja na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania ambae pia ni mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa Rock City Marathon, wadhamini na maofisa wa michezo kutoka mkoa wa Mwanza.

MAKUSANYO YA MAPATO KWA MWEZI WA JUNI ZANZIBAR YAMEFIKIA SHILINGI BILIONI 16.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Umma za Fedha Zanzibar Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d. 
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akimueleza Balozi Mikakati inayochukuliwa na Wizara yake katika suala zima la ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
Picha na –OMPR – ZNZ.

Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar { ZRB }, Ndugu Hamil Bakar  alisema kwamba makusanyo ya Mapato kwa mwezi wa Juni mwaka huu yamefikia shilingi Bilioni Kumi na Sita ikikadiriwa kufikia lengo la makusanyo ya shilingi Bilioni Ishirini mwezi Julai mwaka huu.

Hata hivyo alisema yapo baadhi ya makusanyo yanayofikia shilingi Bilioni Mbili ambayo hupatikana kutokana na mapato ya Wizara na Taasisi mbali mbali za Umma.

Kamishna Hamil  alitoa takwimu hizo katika kikao cha pamoja kati ya Watendaji Wakuu wa Taasisi za Fedha wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d walipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif ameitisha Kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa Mikutano yake ya kukutana na watendaji wapya wa Taasisi hizo kwa kutambuana kufuatia mabadiliko ya muundo mpya wa Serikali sambamba na kuangalia fursa za kukabiliana na changamoto zinazozikabili Taasisi hizo.

Akitoa taarifa fupi katika Kikao hicho Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d alieleza kwamba Bodi ya Mapato Zanzibar ilipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni Mia 272 kwa mwaka kati ya hizo shilingi Bilioni 35.2 zinatokana na mapato ya Wizara.

Dr. Khalid alisema Miezi ya Aprili, Mei na Juni Mwaka huu makusanyo ya mapato yalikadiriwa  kufikia shilingi Bilioni 117 ambapo mwezi juni pekee  makusanyo ya mapato yalifikia  shilingi Bilini 49 ikilinganishwa na mapato ya shilingi Bilioni 37 ya nyuma yake.

Waziri Khalid alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ukusanyaji wa mapato kwa sasa unakwenda  vizuri na kutoa fursa njema ya kupatikana kwa wakati mishahara ya wafanyakazi wa Taasisi za Umma pamoja na viinua Mgongo vya watumishi waliostaafu.

Dr. Khalid alifafanua kwamba watumishi wa umma waliostaafu kazi tokea mwaka 2015 kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi  Serikalini tayari wameshapata viinua mgongo vyao.

Alisema watumishi wastaafu wanaoendelea kusubiri haki yao kwa sasa ni wale waliostaafu katika kipindi cha miezi sita ndani ya mwaka huu wa 2016.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } Ndugu Juma Ameir Hafidh alisema utendaji wa Taasisi hiyo uko katika kiwango   kinachokubalika kibiashara kutokana na ushirikiano mzuri na Mabenki mengine hapa Nchini.

Hata hivyo ndugu Juma alisema zipo changamoto zinazoikabili Benki hiyo ikiwa ni pamoja na usumbufu wa kuchelewa kwa kesi zake dhidi ya Wateja wanaochukuwa Mikopo kwa ajili ya uwekezaji wa miradi tofauti nchini.

Alisema Mwekezaji asiye na mtaji mara nyingi husababisha mitihani katika kuanzisha miradi ambayo baadaye hukumbwa na ukosefu wa fedha za kurejesha deni alilokopeshwa.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Watu wa Zanzibar aliiomba Serikali Kuu kupitia Taasisi na vitengo vinavyohusika na masuala ya uwekezaji kuhakikisha kwamba vinaratibu kwa kina viwango vya fedha za mitaji  vinavyomlazimisha Mwekezaji kuanzisha mradi utakaompa uwezo wa kuchukuwa mkopo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
03/08/2016.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA NA STENDI YA MSAMVU MOROGORO.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe  Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. 
Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi  wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.
 Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016.  Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IFAHAMU HATARI YA KUTUMIA “INTERNET WI-FI” ZA BURE

$
0
0
Ili kuwezesha upatikanai rahisi wa huduma za mtandao – Mahoteli, Viwanja vya ndege na maeneo mengine ya mkusanyiko wa watu kumekua na huduma ya Mitandao inatolewa kupitia teknolojia ya “Hotspot – Wi-Fi” ambapo imeendelea kua na umaarufu mkubwa hivi sasa.

Kama ilivyo katika maeneo mengine ya Hili nalo limekua na upande wa pili ambapo kumeibuka wimbi la wahalifu mtandao wanaotumia udhaifu uliyoko kwenye huduma hizi za bure za “Wi-Fi – Hot spot” kudukua  na kuleta madhara kwenye mtandao.

Wahalifu mtandao wamekua wakiweka “Wi-Fi” za bure ambazo si sahihi “Fake” ambapo wanategemea watu wengi watazitumia na baadae kukusanya taarifa zao na kufatilia vinavyosambazwa kwenye mtandao na baadae kupelekea kufanikisha uhalifu mtandao.

Kampuni ya usalama mtandao ya “Avast” hivi karibuni imefanya jaribio la kuangazia uelewa wa watu juu ya huduma hizi za bure za kujipatia mtandao “Free Wi-Fi” ambapo kampuni hiyo iliweka idadi kadhaa ya “Fake Free (Hot spot) Wi-Fi” kwenye mkutano wa Kisiasa nchini Marekani “Republican National Convention”.

---------------------------------------------------
NOTE: "Travellers should be conscious of hackers who will attempt to physically steal laptops, tablets and cell phones from luggage, hotel rooms or coffee shops when they are left unattended"
---------------------------------------------------

Takwimu zlizo kusanywa na Kampuni hiyo zinasema watu zaidi ya 1200, Walitumia huduma hiyo iliyokua imewekwa kwa mtego na asilimia 68.3 walitoa taarifa zao binafsi. Huku ikielezwa mashindano ya Olympik hili pia linategemewa kujitokeza.

Aidha, Takwimu za jaribio hili ziliendelea kueleza – aribio lilifanikiwa kufahamu Asilimia 38.7 walitumia Facebook; asilimia 13.1 walitumia Yahoo Mail, asilimia 17.6 waliperuzi barua pepe zao kupitia  Gmail, na Asilimia 13.8 walitumia programu zyingine za kuwasiliana kama vile  WhatsApp, WeChat pamoa na Skype.

Kiuhalisia kama zoezi hili lingekua limefanywa na wahalifu mtandao, Hakika wangefanikiwa kudukua kila kinachopatikana kwenye mifumo ya washiriki kaika mkutano huo ambapo jaribio hili lilifanywa. Na hii ni hatari zaidi hasa pale unapo tumia kifaa cha ofisi kilichokusanya taarifa muhimu/za siri ambazo hazikutakiwa kuangukia kwenye mikono ya asiye husika.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images