Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1305 | 1306 | (Page 1307) | 1308 | 1309 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akizindua kisima cha maji kwenye soko maarufu la Kwamrombo kwaajli ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jaffo akizungumza kwenye mkutano wahadhara kwenye soko maarufu la Kwamrombo kabla ya kuzindua kisima cha maji kwaajili ya matumizi ya wafanyabiashara wa soko hilo kilichochimbwa na taasisi ya kidini ya Ansaar MuslimYouth Centre tawi la Arusha.
  Wananchi wakifurahia hotuba ya Naibu Waziri Jaffo ambaye alitumia mkutano huo kumwagiza Meneja wa Tanesco kuwaunganishia umeme mapema inavyowezekana.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro (kushoto) akimweleza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo eneo la Olmoti kilipo kisima cha maji kinachowahudumia wananchi wa Kata ya Olmoti na Olasiti pia maji hayo yatatumika kwenye mahakama ya kimataifa ya MICT,kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Ruth Koya,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo (katikati).
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleiman Jaffo akipata maelezo kando ya Tenki la kuhifadhia maji lenye ukubwa wa ujazo wa lita 60,000 lililopo Kata ya Olmoti jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia(katikati)akifafanua jambo.

  0 0

  Mshindi wa Promosheni ya Bia ya Asili ya Nzagamba inayowawezesha wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki kwa mkoa wa Mwanza, Juma John (kushoto) mkazi wa Kisesa Mkoani humo akipokea zawadi yake ya Ng'ombe Dume la Nzagamba kutoka kwa Mkuu Kiwanda cha Nzagamba Jijini Mwanza,  Herbat Kilembo (kulia) mara baada ya kuibuka Mshindi kwa wiki ya kwanza ya Promoseni hiyo. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo (mwenye Miwani) pamoja na Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo.
  Mshindi wa Promosheni ya Bia ya Asili ya Nzagamba inayowawezesha wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki kwa mkoa wa Mwanza, Juma John akikabidhiwa zawadi yake ya Ng'ombe mbele ya halaiki wa wakazi wa jiji la Mwanza.
  Watumiaji wa kinywaji cha Nzagamba mkoani Mwanza kwenye eneo la Igoma wakifuatilia shindano la kumtafuta mshindi wa Dume la Ng'ombe "Nzagamba" linaloendeshwa na kinywaji cha Nzagamba kwenye mikoa ya kanda ya ziwa.


  0 0

  Na  Bashir   Yakub.

  Mtu akimuumiza mwingine na  aliyeumizwa  akapata  jeraha  linalosababisha  alazwe  hospitali  au  asilazwe   lakini  aendelee  kuishi  na  jeraha  lake  hilo, Swali litakuwa  je  mtu  huyo  akifa  baada  ya  miezi  sita,  saba ,  kumi  au  zaidi   tokea  siku  alipoumizwa   kifo  chake  kitakuwa  kimesababishwa na yule  aliyemuumiza ?.

  1.NINI  MAANA  YA  KUSABABISHA  KIFO.

  Kusababisha  kifo   kunaweza  kuelezwa   katika  namna  nne  tofauti.  Na  hii  ni kwa  mujibu  wa  Sura  ya 16, kifungu cha  203, Kanuni  za  adhabu.

  ( I ) Mtu  amemtia  jeraha  mtu  mwingine.  Na  kutokana  na  jeraha  hilo  mtu  huyo  anakufa.  Haijalishi  amekufa  akiwa  anapata  matibabu  au  laah.  Na  haijalishi  kama  matibabu  hayo  yalikosewa  au  laah. La  msingi  ni  kuwa  matibabu  hayo  yalifanywa  kwa nia   njema na  hiyo  yatosha  kusema fulani  aliyesababisha  jeraha ndiye  huyohuyo  aliyesababisha kifo.

  ( ii ) Pengine  ni  pale ambapo  mtu  anamlazimisha  mtu  mwingine  kwa  kumtishia  akimtaka  atende  tendo   ambalo   linasababisha  kifo  cha  mtu  mwingine.  Mtu  huyo  aliyetishia  atahesabika  kusababisha  kifo.

  (iii) Zaidi,  kutotekeleza  wajibu  ambako  kunapelekea  kifo  nako  ni kusababisha  kifo.  Kwa  mfano   daktari  aliyetakiwa  kumpokea  mgonjwa  na  kumtibia akishindwa  kufanya  hivyo  na  mgonjwa  akafa  basi  atakuwa  amesababisha  kifo.

  ( iv) Pia  ikiwa  mtu  ana jeraha   au  ugonjwa  ambao  kwa  vyovyote  vile  ungemsababishia  kifo  lakini  akatokea  mtu  mwingine  akatenda  tendo  ambalo  linasababisha  mgonjwa  afe  haraka  basi    mtu  huyo  aliyetenda  anahesabika  kusababisha  kifo.


  0 0
 • 08/01/16--14:04: KUMBUKUMBU
 • Marehemu Mpendwa Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba 1954-2012) 

  Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Miaka nne (4) tangu ulipotutoka ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.

  Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa. 

  Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu.

  Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, wajukuu zako, pamoja na marafiki zako wote.

  Ibada Maalum ya Maombi itafanyika tarehe 07/08/2016 Saa 2.00 asubuhi kwenye kanisa katoliki la Mt Maurus Kurasini, Dar es Salaam.

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.

  0 0

  Na Zephania Mandia, Mwanza

  Wananchi wanaoishi katika Kata ya Nyasaka a,b,na c, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa kivukio yaani daraja katika Mto Nyakurunduma ambao unatiririsha maji katika Ziwa Victoria jijini Mwanza.

  Wananchi hao Wamesema tatizo hilo limekua kero kubwa ya miaka mingi kwani mvua zikinyesha mto huo hufurika kiasi cha kusababisha wananchi kushindwa kuvuka mto huo mara kwa mara na wakati mwingine kwa Wanafunzi kupitwa na masomo, imeelezwa kuwa hivi karibuni wanafunzi watatu na madereva wawili wa pikipiki walisombwa na maji wakati wakivuka katika mto huo na kupoteza maisha.

  aidha wananchi hao wamesema walipofikisha taarifa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, aliwahakikishia tatizo hilo lingefanyiwa kazi baada ya mvua kupungua lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika badala yake wananchi hao wamelazimika kujenga daraja la miti ili wapate sehemu ya kuvukia kwani muda wowote mvua zinaweza kuanza tena. 
   Muonekano wa Daraja hilo lililojengwa na Mwananchi wa Kata ya Nyasaka a,b,na c, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
   Watoto wakivuka.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum akizungumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Naibu Katibu wa Rais Nd,Marium Haji Mrisho na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji. Picha na Ikulu,Zanzibar.

  0 0

  SHIRIKISHO la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) limezionya klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuhusiana na mikataba ya wachezaji ambao miakataba yao ambao haikupelekwa kwao kwa ajili ya kuomba kupatiwa leseni za kucheza. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017 KUWA ila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF.

  Na kanuni ya 68(8) inavitaka kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila mkataba wa mchezaji na ni matarajio yao kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji au mchezaji  i na timu na wanategemea kupata ushirikiano.  Kadhalika, kwa mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linakumbusha kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili.

  Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji mtakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 67(8) inataka kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba wa mchezaji, mbali na hilo mchezaji wa kigeni atahitajika kulipia dola 2000 ili kuweza kupatiwa leseni ya kuchezea nchini.

   Pia katika hili tunategemea kila timu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  TIMU ya Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Mtibwa Sugar Agosti 08 ikiwa ni maandalizi ya kuendelea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Mo bejaia unaotarajiwa kupigwa Agosti 13 Jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesema kuwa mechi hiyo itatumika kwa ajili ya kukiangalia kikosi kabla ya kuelekea mchezo wao wa kimataifa wa kombe la Shirikisho ambapo wana nafasi ndogo sana ya kufuzu ila bado hawajakata tama kwani kama wakifanikiwa kushinda michezo ilioyobaki pia inakuwa ni moja ya nafasi nzuri watakayokuwa nayo katika kundi A.

  Deusdedit amesema kuwa, kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi katika viwanja vya Gymkhana na wachezaji wote wako vizuri isipokuwa Geofrey Mwashiuya ambaye bado ana P.O.P ila wengine wameanza mazoezi ua pamoja.

  Mbali na hilo pia katika siku hiyo hiyo, Uongozi wa Yanga umetangaza kuitisha mkutano mkuu wa wanachama watakaojadili masuala ya ndani ya klabu yao pamoja na maendeleo kwa ujumla kuelekea ligi kuu na nini cha kufanya ambapo unatarajiwa kuanza majira ya saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee na baadae watajumuika pamoja Uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huo wa kirafiki.

  0 0


  Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza. EGNO KAMILIUS KOMBA alizaliwa tarehe 20 Oktoba, 1947 katika Kijiji cha Mtungu - Kindimba Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

   Mwaka 1956 alijiunga na Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Kindimba na kuhitimu elimu hiyo mwaka1959. 

  Alijiunga na Shule ya Kati (Middle School) ya Litembo mwaka 1960 na kuhitimu mwaka 1963. Alijiunga na Shule ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1964 na kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 1967. Mwaka 1968 alijiunga na Shule ya Sekondari Karimjee iliyopo Mkoani Tanga na kuhitimu mwaka 1968.

  Marehemu aliajiriwa na Jeshi la Magereza tarehe 02 Agosti, 1972 na kupelekwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya Uaskari katika Chuo cha Usalama – Moshi. Marehemu alihitimu mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 1973 na kupangiwa kufanya kazi Gereza Malya, Mkoa wa Shinyanga.

  Mwaka 1975 akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Magereza, Kamishna mstaafu wa Magereza, Marehemu EGNO KAMILIUS KOMBA alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya masomo ya Shahada ya Kwanza katika Uchumi na kuhitimu mwaka 1978.

  Marehemu akiwa Jeshini alitunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
  Afisa Magereza Daraja la III (PO III)​– ​30/04/1973 – 31/09/1973

  Afisa Magereza Daraja la I (PO I)​​- ​01/09/1973 - 31/06/1976
  Afisa Magereza Mkuu (PPO)​-​01/07/1976 - 30/11/1978
  Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP)​- ​01/12/1978 - 31/09/1980
  Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP)​ - ​01/10/1980 -31/12/1996
  Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) ​- ​01/07/1984 -19/09/1989
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP)-20/09/1989-30/6/1996
  Kamishna wa Magereza (CP) ​- ​01/07/1996 - 30/06/2007 (Alipostaafu kwa umri Mkubwa).

  Marehemu alifanya kazi katika vituo vifuatavyo vya Magereza:-
  Gereza Malya – Shinyanga ​- Tarehe 01/05/1973 - 12/05/1974
  Makao Makuu ya Magereza ​- Tarehe 13/05/1974 – 30/06/2007

  Katika utumishi wake Jeshini Marehemu pia alitunukiwa nishani mbalimbali kama ifuatavyo:-
  •Nishani ya Mstari wa Nyuma ya Vita vya Kagera,
  •Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania na,
  •Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
  Katika utendaji wake wa kazi, Marehemu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujifunza, kutawala na kuyamudu majukumu yake ya kazi ipasavyo. Viongozi na watumishi wa Jeshi la Magereza tunamlilia mno kwa Utumishi wake uliotukuka na hazina kubwa ya utendaji aliyoondoka nayo kwani hata baada ya kustaafu katika Jeshi la Magereza bado alikuwa akitoa ushauri katika mambo mbalimbali ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

  Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo hadi umauti ulipomkuta mchana ya tarehe 31 Julai, 2016 nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho Agosti 3, 2016 Shambani kwake Mvuti, Jijini Dar es Salaam.

  MWENYEZI MUNGU AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA, AMEN.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.

  “Ofisa Elimu njoo kagua haya madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS….

  Alisema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.

  Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.

  Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti na kuuagiza uongozi wa wilaya ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa kuyakagua kabla ya yeye kukabidhiwa.

  Katika hatua nyingine aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  “Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao,” alisema.

  Awali mbunge wa jimbo la Mvomero, Saddiq Murad alisema miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili wilaya hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba hivyo amemuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.

  Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.

  0 0

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungua kozi ya ukocha wa magolikipa ambapo  Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limeipa nafasi Tanzania kuwapa mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping Coach Course) ikiandika historia kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa makocha wa nafasi hiyo baada ya Botswana.

  Makocha wa makipa wapatao  25 kutoka  timu za taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanahudhuria kozi hiyo inayoongozwa na Alejandro Heredia ambaye ni Mkufunzi kutoka FIFA. Makocha hao ni Peter Manyika (Taifa Stars ya Tanzania), Saleh Ahmed (Zanzibar Heroes); Muharami Mohammed (Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys); Mohammed Silima (Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar) na Elyutery Mhoery (Timu ya Taifa ya Wanawake - Twiga Stars) na msaidizi wake ambaye pia anachezea JKT Queens, Fatuma Omary.

  Wengine ni makocha maarufu wa makipa wakiwamo Juma Pondamali (Young Africans); John Bosco (Majimaji ya Songea); Salimu Tupa (Tanga); Bakari Ali Hamadi (Wete Pemba – Zanzibar); Hafidh Muhidin Mcha (Mkoani Pemba – Zanzibar); Mussa Wanena (Kagera Sugar); Juma Bomba (African Lyon), Adam Abdallah Moshi (Simba SC), Idd Mwinchumu (Azam FC) na Hussein Tade (Seeb Club-Oman/Toto African). Pia wamo Khalid Adams (Mwadui FC); Josia Steven (Mbeya City); Herry Boymanda (Tanzania Prisons); Emmanuel Mwansile (Polisi Morogoro); Ben Kalama (Stand United); Abdallah Said (JKT Ruvu); Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar); Augustin Malindi (Mkoa wa Kigoma); Raphael Mpangala (Ndanda FC); Salimu Tupa (Tanga) na nAbdul Mgude (Coastal Union ya Tanga).

  Heredia aliweza kutoa nasaha kwa makocha hao wakati akiwanoa na kusema kuwa “Kinachohitajika sasa ni juhudi tu. Kozi hii haijafanyika pengine hapa barani Afrika zaidi ya Botswana. Mjue kuwa mna bahati na mbinu hizi mzitumie kuweza kujenga magolikipa wziri wataoleta tija baadae.”

  Akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia aliishukuru FIFA na CAF kwa namna inavyoshirikiana na TFF katika kuwapa kozio nyingi za makocha wa timu kwa wachezaji wa mbele, makocha wa makipa na waamuzi wa madaraja tofauti. “Hakuna kipindi TFF imepata kozi za makocha nyingi za makocha kama kipindi hiki cha uongozi wa Jamal Malinzi,” anasema Karia na kuongeza: “Tumetoka kwenye kozi ya makocha wa Daraja A sasa tuko kwenu. Lengo ni Tanzania kuwe na makipa wazuri. Ninyi mtaleta makipa wazuri. Na hii ni kwa manufaa ya sasa na baadaye kwa upende wetu, timu zetu na taifa kwa ujumla.”

  Karia aliwatia hamasa makocha hao wanaoshiriki kozi hiyo kuwa, mara baada ya kozi hiyo ipo siku watakwenda kuwa wakufunzi nje ya mipaka ya nchi kadhalika makocha ambao wanaweza kupata kazi mahala popote duniani hasa ukizingatia walimu wa daraja lao wako Tanzania na Botswana tu.
   Kadhalika, Makamu huyo wa Rais wa TFF alielezea kuwa mpira wa miguu una changamoto nyingi na nyingine husababishwa na watalaamu hao kubweteka kwa mafanikio. “Hili ni tatizo. Tubadilike kifikra na kivitendo. Msilaze damu, kuweni active (mahiri).”

  0 0

   Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
   Afisa utumishi wa Wilaya ya Ikungi Evodius Buberwa akifafanua na kutofautisha majukumu ya watendaji wote ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault (watatu kulia) na ugeni wake wakisikiliza maelezo kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (kushoto). Kulia ni Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Habel Mhanga.
  Baadhi ya Maafisa kutoka nchini Ufaransa ambao waliongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kutembelea Bandari ya Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa waandishi wa habari kutoka nchini Ufaransa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho (wapili kulia) na baadhi ya Maafisa wa Serikali waliofanikisha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam.

  0 0

  Timu ya Madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mi9fupa na upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tayari iko mkoani Mtwara na leo hii wameanza kazi ya kuwafanyia upasuaji wa bure kabisa watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi chini ya udhamini wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika nchi nzima, Dk Othman Kiloloma ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa MOI, zoezi hilo kwa mkoa wa Mtwara peke yake litachukua siku nne ambapo litakuwa likifanyika katika Hospitali ya Ligula, ambapo pamoja na mambo mengine, madaktari wanaofanya kazi katika hospitali hiyo watapewa mafunzo ya jinsi ya kufanya upasuaji wa namna hiyo ili kupunguza tatizo la vifo kwa watoto hao ambao madaktari wa kuweza kuwatiobu wako tisa tu nchi nzima na kati yao nane wapo Dar es Salaam na mmoja tu yuko Bugando, Mwanza.

  Kwa upande wake Afisa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba amelieleza lengo la Taasisi yake kuwa ni kuokoa angalau asilimia 10 tu ya watoto wanaosadikika kupoteza maisha kila mwaka kutokana na changamoto ya kuzaliwa na kichwa kikubwa ama mgpongo wazi, ambapo wengi wao hukosa tiba kutokana na imani za kishirikina, na wakati mwingine sababu za kiuchumi.

  Inasemekana takriban watoto 4000 huzaliwa kila mwaka nchini wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, lakini wanaorudi mahospitalini kwa ajili ya matibabu huwa hawazidi 500, hali inayosababisha wadau wa afya kuamini kwamba aidha watoto waliobaki hupoteza maisha, ama kupata mtinfdio wa ubongo.
   Mkuu wa msafara wa madaktari Dk Kiloloma(kushoto), kutoka MOI, akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara, kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara Dk Sichalwe
   Uongozi wa kambi ya Upasuaji kutoka GSM Foundation na MOI ukijieleza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendegu
  Picha ya pamoja kati ya timu ya Kambi tiba ya Upasuaji, Katibu Tawala na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

  0 0  Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai, wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48.

  BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.

  Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema.wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.

  “Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.  Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.

  “Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja. Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.

  Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu. “Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema

  “Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
  mikopo ndani ya saa 48,” alisema.

  Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake  na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya shughuli zake.

  0 0

  Mkandarasi Jianx-Geo Engineering Group Corporation kutoka China anayejenga sehemu ya barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi kwa kiwango cha lami amepewa wiki mbili kurejesha vifaa vya ujenzi katika eneo la kazi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambao umeonekana kusuasua kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda Mkoani Rukwa.

  Waziri Prof. Mbarawa amesema barabara hiyo imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi KM 75 na Kanazi-Kizi-Kibaoni KM 76.6 ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na viwango kulingana na mkataba.

  “Hakikisheni baada ya wiki mbili vifaa vinakuwepo katika eneo la kazi na mnatekeleza wajibu wenu kukamilisha barabara hii kwa wakati tuliokubaliana ili ianze kutumiwa na wananchi”, amesema Prof. Mbarawa.

  Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa wananchi wanamatarajio makubwa na barabara hiyo kwa muda mrefu hivyo Mkandarasi ahakikishe kazi ya ujenzi katika kipande kilichobaki kwa kiwango cha lami inamalizika ifikapo mwezi Julai mwakani ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo mkoani hapo.

  Aidha, amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha mzani wa kupima uzito wa magari katika kijiji cha Kanondo KM 5 kutoka Sumbawanga mjini ifikapo mwezi Agosti mwaka huu kwa lengo la kudhibiti uzito wa magari yanayofanya shughuli za kusafirisha mizigo na abiria katika barabara hiyo.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Eng. Masuka Mkina amemuhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara zote utazingatia viwango na utakamilika kwa wakati.

  "Nikuhakikishie kuwa tutasimamia na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika mradi wa ujenzi huu ili wananchi wanufaike na kuongeza uchumi wa mkoa ",amesema Eng. Mhina.

  Ujenzi wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda kwa kiwango cha lami unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya kiasi cha Shilingi bilioni 150.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala- Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
  Mkandarasi anayejenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6 akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina.
  Mbunge wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy (mwenye kofia) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua miundombinu ya Bandari ya Kipili, Mkoa wa Rukwa.


  0 0


  Mkuu wa Kitengocha uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) akigawa baadhi ya vifaa vya uhamasishaji kwa wadau waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya sherehe za Wakulima katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana. Maadhimisho ya sikukuu hiyo, yatafanyika Agost 8, 2016.
  Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia) na Bw. Mathayo Mihayo (Kushoto) wakitoa maelezo mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi katika maonesho ya Nane nane.
  Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) katika maonesho ya Nane nane mjini Lindi jana.


  Mkulima akipokea vipeperushi na maelezo toka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. David Mathayo katika maonesho ya wakulima Nane nane mkoani Lindi jana.
  Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Agnes Lubuva akitoa malezo na vipeperushi kwa wageni waliotembelea banda la SSRA katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi wakati wa maonesho ya Wakulima jana.

  0 0

   Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) siku ya jana jioni kwa ziara yake ya siku moja tu jijini Dar es salaam ya kuitambulisha albamu yake mpya aliyoipa jina la “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania. 
   Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ziara yake ya siku moja jijini Dar es salaam ya kuitambulisha album yake mpya inayokwenda kwa jina la “God over everything”. Pamoja nae ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi ambapo kupitia programu yao ya Mziiki wanajishughulisha na uendelezaji wa kazi za wasanii mbalimbali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
  Toka kushoto ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi, Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking, Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye pamoja na Meneja wa Msanii huyo nchini Tanzania Tom Raymond kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza shughuli ya utambulisho wa album ya msanii huyo kwa waandsihi wa habari katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya ukumbi wa Paparazzi jijini Dar es salaam. Msanii huyo alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja kuitambulisha albamu yake ya “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.
  Albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inayoitwa“God over Everthing” (GOE) kutoka kwa nyota wa mtindo wa reggae/dancehall wa kinigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking hatimaye imekemilika.
  Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere (JNIA) jana jioni, msanii huyo wa miondoko ya reggae pamoja na timu yake iliyopokelewa na Spice Africa, kampuni ambayo inayofanya kazi na Patoranking katika kutangaza mziki wake na usambazaji wa albamu mpya ya msanii huyo kwa nchini Tanzania.
  Akizungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika katika ukumbi wa Paparazi-Slipway jioni hiyo hiyo, msanii huyo alitambulisha baadhi ya vibao/nyimbo zake ambazo ziko katika albamu hiyo, baadhi ambazo tayri zinafanya vizuri katia anga za kimataifa kama “Girlie O”, “My woman”, “Make Am”, “Another Level”, “Alubarika” na wimbo wake mpya wa hivi karibuni “No Kissing Baby”aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana. Albamu hiyo imebeba nyimbo zilizotengenezwa katika label yake ya VP records yenye idadi ya zaidi ya nyimbo 16.

  “Albamu hii ni ya kipekee; ina nyimbo kwaajili ya kila mtu, kwa watu wenye umri wowote na kila kona ya Afrika. Nilitaka kulipa fadhila/Heshima kwa asili yangu na pia kukumbatia mfumo mpya wa muziki wa kiafrika ambao unashika kasi Ulimwenguni kwa sasa. Nina furaha sana kuitambulisha albamu yangu kwa mara ya kwanza duniani kwa mashabiki wangu waTanzania”….alisema Patoranking.

  Msanii huyo pia alitumia muda huo kufafanua kwanini alichagua Dar es salaam kama Jiji la kwanza kuitambulisha albamu yake mpya, “watanzania ni watu wazuri sana, nimeona wasanii wengi kutoka Nigeria na mataifa mengine wakija kufanya shoo hapa jinsi wanavyopokelewa vizuri na upendo mkubwa”. Aliwataja baadhi ya wasanii  wa Kitanzania ambao nyota huyu anapanga kufanya nao kazi akiwemo: Navy Kenzo na Vanessa Mdee a.k.a  V-Money ambao kwa maelezo yake ni kama wanafamilia.
  Aliwashukuru mashabiki wake na vyombo vya habari vya Tanzania kwa kuunga mkono mziki wake  kabla  hajabainisha kuwa atatembelea Nairobi, Kampala na Accra-Ghana kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kurudi nyumbani.
  Patoranking pia aliendelea kutaja siri ya kuwa ameanzisha lebo ya kurekodi /studio aliyoiita “his baby”, ambayo msanii wa kwanza ametokea kutoka hapa hapa Tanzania, “Jina lake ni Walid, mnaweza msimfahamu kwa sasa, lakini mtamfahamu, huyu amekusudiwa kufanya mambo makubwa” alisema Patoranking
  Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Spice Africa Joan Nkuzi amesema, ni heshima kubwa sana kwa Msani  nyota wa Nigeria kutambulisha albamu yake kwa mara ya kwanza hapa Tanzania na ndio maana hawakusitasita kuunga mkono juhudi zake. Jukumu kubwa lab Spice Africa kupitia application yake ya Mziiki ni kupeleka muziki wa Kiafrika duniani kote kama wakusanyaji na wasambazaji walioko katika masoko zaidi ya 12 ndani ya Afrika, walitoa uhakika sio tu kufanya kazi na wasanii wenye vipaji, bali pia wasanii ambao ni wanyenyekevu na ambao wanajua malengo yao – ambapo mmoja wao ni Patoranking.

  0 0


  SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imesema imeanza mchakato wa kushirikisha wananchi kuchangia maoni yao juu ya kubadilisha kwa sheria ya ndoa ya sasa inayoonekana kuwa kandamizi kwa wanawake; https://youtu.be/3rIwDf-689o

  SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa, ametoa siku 14 kwa mkandarasi anayejenga barabara wilayani Sumbawanga kurudisha vifaa na kuendelea na kazi; https://youtu.be/cR41cwg4Lbo

  SIMU.TV: Wakazi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa agizo la kuanza kufanya kazi kwa soko lao; https://youtu.be/thcK5duLqRI

  SIMU.TV: Waziri wa Maliasili na utalii Prof Jumanne Maghembe, amezindua bodi ya wakurugenzi ya bodi ya utalii nchini na kuitaka bodi hiyo kuongeza idadi ya watalii;https://youtu.be/EnYfivzMBOs 

  SIMU.TV: Shirika la umoja wa mataifa lam maendeleo na bisahara UNCTAD, limeuingiza mkoa wa Njombe katika mafunzo ya kufuga ng’ombe kitaalamu;https://youtu.be/qT9T_lYcSnE

  SIMU.TV: Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imetoa agizo kwa watu wote waliovamia maeneo ya wazi waondoke mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.https://youtu.be/4rXX6j9lS-Q

  SIMU.TV: Waziri wa katiba na sheria Dr. Haryson Mwakyembe amesema serikali imefanya jitihada kubwa za kuhakikisha inalinda uhuru na haki za mwanamke.https://youtu.be/3oX9dpXzccw

  SIMU.TV: Serikali imepiga marufuku tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyogaiwa kufugia kuku au kuvitumia kupandia miti. https://youtu.be/-5bNXAx2Pc4

  SIMU.TV: Jumla ya hati laki tatu zinatanatarajiwa kutolewa kwa wakazi wa Dar es Salaam baada ya zoezi la urasimishaji wa makazi holela kukamilika. https://youtu.be/OX0c-GC84Yw

  SIMU.TV: Jumla ya watu 93 kati ya watu 1453 waliojitokeza kuchangia damu katika mkoa wa Tanga wamebainika kuwa na homa ya ini. https://youtu.be/xPQIb_-d7PY

  SIMU.TV: Wachinjaji wa ng’ombe na mbuzi katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi kutokana na kupandishiwa ushuru.https://youtu.be/M_V8l5eUsXg

  SIMU.TV: Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imesogeza mbele kesi inayomkabili  mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lisu ya kutoa maneno ya uchochezi.https://youtu.be/1cpA8TL8YJY

  SIMU.TV: Serikali imepiga marufuku kilimo cha mkataba kilichokuwa kikimnyonya mkulima kutokana na mnunuzi kujipangia bei ya mazao. https://youtu.be/uihwW2qN_NU

  SIMU.TV: Serikali imeishauri mifuko ya hifadhi za jamii hapa nchini kutumia huduma za utuzaji wa dhamana za uwekezaji ili kuwezesha fedha za wateja wao kuwa salama zaidi.https://youtu.be/ukt9omDKAhs

  SIMU.TV: Baadhi ya taasisi za fedha zimeanza kuitikia wito wa serikali wa kushusha riba za mikopo ili kuwapa fursa watanzania wengi kupata mikopo.https://youtu.be/yQZXb5osMUE

  SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu TFF limesema halitatoa leseni kwa mchezaji ambaye timu yake haikuwasilisha mkataba wake kwa TFF. https://youtu.be/d8gFwFIfYwU

  SIMU.TV: Mwanachama wa klabu ya Simba Mohamed Dewj ameikabidhi klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni mia kwa ajili ya usajili wa wachezaji. https://youtu.be/JUJ3oCO9Zv4

  SIMU.TV: Takribani wasanii 10 wa filamu na muziki nchini wanatarajia kunufaika kwa kujiingizia kipato kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kuanzishwa kwa b nary itakayosimamia urushwaji wa matangazo kwa mitandao yote ya kijamii.https://youtu.be/99gmONc9-vE

  SIMU.TV: Wanafunzi wa kike wametakiwa kutojiweka kando bali washiriki katika michezo ili kuweza kuonesha vipaji vyao na kuviendeleza. https://youtu.be/hLY42CzFuw4

  SIMU.TV: Manchester city imekamilisha usajili wa kiungo chipukizi Leroy kwa kiasi cha pound milioni 35 akitokea Schalke 04. https://youtu.be/Ap9iBI5jMhY

older | 1 | .... | 1305 | 1306 | (Page 1307) | 1308 | 1309 | .... | 3353 | newer