Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1299 | 1300 | (Page 1301) | 1302 | 1303 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Na Jonas Kamaleki.

  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu,Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu itahamia Dodoma juma lijalo kufuatia agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi ,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akiongea na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizoko chini ya ofisi hiyo.

  “Mchakato wa kuhamia Dodoma umekwisha kilichobaki kwa sasa ni utekelezaji, mimi na manaibu mawaziri wangu tunahamia juma lijalo ili tukamkaribishe Mhe. Waziri Mkuu anayehamia Septemba mwaka huu,” alisema Mhagama.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.

  Mhagama amesema kuwa kila kiongozi anayehamia Dodoma inabidi awakute walio chini yake tayari wamekwishahamia ili kumpokea, hivyo akawataka na watendaji ambao wako chini yake watangulie kwa ajili ya kumpokea yeye na viongozi wenzake.

  Aidha, Waziri huyo amesema kwa sasa hakuna mjadala wa kuhamia Dodoma lilobaki ni utekelezaji  tu wa kuhamia Makao Makuu.

  Mhagama amesema kama kuna Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imetenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi, shughuli hiyo ikafanyike Dodoma ambako Serikali inahamia. Kwa kusema hivyo kadhalika na ofisi au Wizara nyingine za serikali ambazo zimetenga fedha ya ujenzi wakajenge Dodoma.
  Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu, Issa Nchasi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri Jenista Mhagama na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma (Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi-Utawala, Samwel Mwashambwa)

  Suala la kuhamia Dodoma sio geni bali limekewepo kwa kipindi kirefu ila utekelzaji wake ndio ulikuwa bado; pia katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 suala hili lipo, alisema Mhagama na kuongeza kuwa kipindi cha nyuma Wizara saba (7) ziliwahi kuhamia Dodoma na kwa sasa Wizara inayoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iko Dodoma.

  Waziri Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanza ujenzi wa jengo lake mjini Dodoma na kusisitiza kuwa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo kwa kujenga ofisi zao Dodoma.

  “Kwa kuwa sisi ni waratibu wa wizara zote inabidi tuunde kikosi kazi kitakachofanya kazi ya uratibu wa kuhama kikiwa Dodoma ili kuwawezesha na watumishi wenzetu kutekeleza agizo la Mhe. Rais la serikali nzima kuhamia huko,”alisema Mhagama.
  Baadhi ya Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenista Mhagama wakati wa kikao kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma.

  Mhagama amesema kuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) wameshafanya kazi nzuri ya upimaji eneo la serikali ambalo litatumika kwa ajili ya ofisi.

  “Tumefika mwisho wa mchakato sasa ni utekelezaji na tunataka watumishi walielewe vizuri suala hili na wawe tayari kulipokea,”alisisitiza Mhagama.

  Kuhamia Dodoma katika kipindi hiki kunatokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alillolitoa tarehe 27 Julai, 2016 mjini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambo ulimchagua kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho tawala.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini. Picha na Geofrey Adroph
   Mdau wa muziki wa dansi, Asha Baraka akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo alijawahi kufanyika hapa nchini.
  Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.

  Baadhi ya waandishi wakiwa kazini

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  UKITAKA kujua aina mbalimbali za vibweka vya kamati za ufundi katika michezo hasa ya soka, pamoja na aina mbalimbali za ushangiliaji basi fatilia mashindano ya Ndondo ambako ndio Mahala pake. Vibweka, vituko na kila aina ya ushangiliaji utauona hapo, Wapo wanaojipaka damu (za kuku), masizi ya mkaa, kujichora mwili mzima na hata wale wanaovaa tofauti na wengine. 

  Raha ya Ndondo ni uipeleke kwenye viwanja ambavyo mashabiki wataweza kuonesha aina zao za ushangiliaji na hutataka kuamini dakika 90 zinamalizika mtu hajashuhudia hata dakika moja kwani muda wote anakuwa anafanya vibweka vinavyowaacha hoi mashabiki waliokuja kushangalia mchezo huo wa soka la mtaani maarufu kama Ndondo.

  Katika uwanja wa Bandari 'Wembley' unawapa nafasi mashabiki kufanya vituko vya kila aina na kufanya mchezo huo kugeuna ni sehemu ya burudani kwa washabiki wengine wa vibweka. 

  Burudani ni kokote, kawaida ya viwanja hivi maeneo ya kukaa watu ni sehemu chache sana ila ukitaka kujua mchezo wa mpira utaona wakitumia kila aina ya njia ili kuweza kuuona. Juu ya miti, juu ya magari kote kunawezekana.
  Hii ndiyo raha ya NDONDO.
  Mtaalam wa Ufundi wa Timu ya Temeka Market akiwasili uwanjani huku akiwa na ulinzi wa nguvu.
  Mtaalam wa Ufundi wa timu ya Kauzu FC
   Mtaalam akiwa tayari kwa kazi ya kuitafutia ushindi timu yake kutokea nje ya uwanja.
  Jukwaa kuu. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki (pichani kulia) akiwasili leo jijini Dar Es Salaam akiwa na Mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR.MMG.
  Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wa siku mbili.Pichani kati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .
  Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
  Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.

  Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jioni ya leo jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.
  Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam jioni ya leo kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 wa siku mbili,utakoanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .

  0 0


  0 0

   Mtendaji wa kijiji cha Tungi kata ya Mkamba Idd Kambangwa mbaye pia ametumbuliwa jipu kutokana na utendaji wake mbovu akikabidhi risala  kwa Mbunge Abdallah Ulega mara baada ya kufanya ziara ya kushukuru kijijini hapo leo.
   Wananchi wa kijiji cha Tungi, kata ya Mkamba wilayani Mkuranga wakimsikiliza kwa makini Mbunge wao Abdallah Ulega wakati akitoa salamu zake za kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanyika mwakajana ambapo pia katika mkutano huo Ulega alichangia sh. Milion moja kwa ajili yakuaza ujenzi wa shule msingi kijijini hapo.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0
 • 07/28/16--03:43: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

   Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA.
   Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
  Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi. Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee. 

  0 0

   Meneja Mawasiliano ya Umma wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Jin Liguo akizungumza na baadhi ya Wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu nchini ambao walipata nafasi ya kwenda nchini China kujifunza maswala ya Teknolojia na Mawasiliano, ikiwa ni sehemu ya kusaidia vijana wa Kitanzania wenye vipaji katika mambo ICT, wakati Wanafunzi hao walipotembelea Banda la Huawei lililopo nje Ukumbi wa Mwl. J.K. Nyerere kunakofanyika Tamasha la Nne la Makampuni ya Simu Duniani (GSMA Mobile 360), jijini Dar es Salaam.
  Meneja Msaidizi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Amani Frank akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu nchini ambao walipata nafasi ya kwenda nchini China kujifunza maswala ya Teknolojia na Mawasiliano, ikiwa ni sehemu ya kusaidia vijana wa Kitanzania wenye vipaji katika mambo ICT, wakati Wanafunzi hao walipotembelea Banda la Huawei lililopo nje Ukumbi wa Mwl. J.K. Nyerere kunakofanyika Tamasha la Nne la Makampuni ya Simu Duniani (GSMA Mobile 360), jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa wanafunzi hao kutoka Chuo Kikuu cha Tanzania, Faith Asenga akizungumza jambo wakati aktoa shukrani wa uongozi wa Kampuni ya Huawei Tanzania, waliofanikisha safari yao hiyo ya kimafunzo nchini China.
  Wanafunzi hao wakiwa ndani ya moja ya Mabanda ya Teknolojia ya Kampuni ya Huawei Tanzania.

  0 0  0 0

   Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah (kushoto), Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (katikati) wakimsikiliza mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa hafla ya kupokea simu 130 zilizotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto)akimkabidhi baadhi ya simu kati ya 130,Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo zilizotolewa na mfuko wa kampuni hiyo wa kusaidia jamii kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”anayeshuhudia katikati ni mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah(kulia) Mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje(katikati)wakiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani)baadhi ya simu kati ya 130 walizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto)zitakazotumika  kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”.
   Mkuu wa kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto)akifungua moja ya simu kati ya 130 zilizotolewa msaada na mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo, kwa ajili ya utafiti wa utumiaji wa dawa za ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell”.wakati wa hafla ya kuzikabidhi simu hizo iliyofanyika jijini Dar e Salaam,Katikati ni mtafiti wa magonjwa ya binadamu wa muhimbili University, Dkt.Mariam Ngaeje na Balozi wa Ugonjwa wa Selimundo”Sickle cell” wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Khadija Abdallah.

  0 0

  Michuano ya kimataifa ya kirafiki (ICC) inaendelea katika nchi za China, Marekani na Australia, na alfajiri ya leo ilipigwa michezo mitatu iliyofanyika nchini Marekani.

  Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika dimba la Sports Moles, Columbus kikosi cha Paris St-Germain chini ya kocha mpya Unai Emery kilitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa vijana wa Real Madrid chini ya kocha Zinedine Zidane cha mabao 3-1.

  PSG waliandika bao la kwanza dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Ikone baada ya kuwapiga chenga walinzi kadhaa wa Madrid na kufunga bao. Madrid walijaribu kusawazisha bao hilo lakini walijikuta wakipachikwa bao la pili kunako dakika ya 24,bao ambalo lilipachikwa na mchezaji Meunier kwa shuti kali la umbali wa mita 25.

  Madrid walionekana kuchanganyikiwa zaidi na kuwapa nafasi PSGkuweza kutawala mchezo na kufanikiwa kufunga goli la 3 kupitia tena kwa mchezaji Meunier kunako dakika ya 39 ya mchezo baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Madrid ambao aliupiga yeye mwenyewe mfungaji wa bao hilo.

  Madrid walijipatia bao la kufutia machozi katika dakika ya 43 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Marcelo. Penati hiyo ilitolewa na mwamuzi baada ya mchezaji Aurier wa PSG kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika mabao yalikuwa hayo 3-1, na zaidi ya hayo kipindi cha pili nacho kiliisha bila ya bao lolote kupatikana.
  Kwenye dimba la Soldier Field Stadium jijini Chicago, mpambano mkali wa kukata na shoka ulipigwa kati ya Ac Milan ya Italia na Bayern Munich ya Ujerumani.Katika mpambano huo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3.

  Walikuwa ni Ac Milan waliohanikiza bao la kwanza kupitia kwa mchezaji M'baye Niang akimalizia kwa ustadi kampa kampa tena ya wachezaji wenzakedhidi ya ya wachezaji wa Bayern. Frank Ribery akitumia uzoefu wake aliisawazishia Bayern Munich bao na muda mfupi baadaye David Alaba akaifungia Bayern bao la pili.Hadi mapumziko Bayern 2, Ac Milan 1.

  Kipindi cha pili Milan waliingia na nguvu mpya na kuweza kusawazisha goli lililofungwa na Andrea Bertolacci.Kabla Bayern hawajakaa vizuri wakapachikwa goli la 3 lililofungwa na Kuck. Watu wakiamini Bayern wamelala,wakafanya shambulizi hatari lililopelekea mchezaji wao kufanyiwa madhambi ndani ya sanduku la hatari na mwamuzi akaamuru mkwaju wa penati upigwe, ambapo bila ajizi Ribery akaukwamisha mpira wavuni na kufanya ubao wa matangazo usomeke 3-3.

  Katika kupigiana mikwaju ya penati Ac Milan wakapata penati zote 5 ambapo Bayern Munich wakaambulia penati 3,na Ac Milan kuibuka washindi wa mchezo huo.

  Goli la dakika ya 4 tu ya mchezo lililofungwa na mlinzi wa Chelsea Gary Cahill kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na Fabregas lilitosha kudumu mpaka mwisho wa mchezo na kuipa ushindi timu hiyo dhidi ya Liverpool.

  Mtanange huo ulipigwa katika dimba la Rose Bowl,Pasadena huko Calfornia ulitawaliwa zaidi na Liverpool kiasi cha asilimia 65 kwa 35 za Chelsea. Kocha Antonio Conte wa Chelsea alitumia muda mrefu kuwahamisa wachezaji wake wajilinde zaidi (kupaki basi) na kuwapa Liverpool muda mrefu wa kulishambulia lango la Chelsea na kufanikiwa kufunga goli lililofungwa na Roberto Filmino lakini kwa mshangao wa wengi mwamuzi wa pambano hilo alilikataa kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea.


  Katikati ya kipindi cha pili mwamuzi alilazimika kumpa kadi nyekundu ya moja kwa moja kiungo wa Chelsea Fabregas kwa kumchezea rafu mbaya mchezaji mpya wa Liverpool mlinzi Klavan, ambaye aliendelea na mchezo baada ya kupatiwa matibabu. Mpaka mwisho wa mchezo Chelsea waliibuka na ushindiwa goli 1-0.

  0 0

   Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo mchana.
   Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.
   Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.

  Dotto Mwaibale.
  UGONJWA wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo watu wapatao  milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati kwa njia ya kujidunga.

  Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.

  Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.

  Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.

  Alisema lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia, wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.

  Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.

  Alisema hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa mipango hiyo.

  "Mkakati unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo mwaka 2030" alisema Dk.  Aikaeli
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Sehemu ya Shehena ya Vilainishi aina ya KY Jerry iliyokamatwa Mkoani Shinyanga leo. Shehena ya Vilainishi aina ya KY Jerry imekamatwa Mkoani Shinyanga leo, hivi karibuni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto kusitisha ugawaji wa Vilainishi miongoni mwa makundi maalumu yaliyo katika hatari ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu, na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) amepokea Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wiki ijayo wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.

  Mhagama amekutana wna wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi katika kukamilisha Mpango Mkakati huo ili kukamilisha utekelezaji huo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama na Naibu Waziri anayeshughulikia ( Watu Wenye Ulemavu )Abdallah Possi pamoja na wakuu wa Idara wakifuatilia uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wa Ofisi hiyo, leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai, 2016.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali akiwasilisha Issa Nchasi akiwaitisha wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Mpango wa Ofisi hiyo kuhamia Dodoma wiki ijayo.

  Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai, 2016.
  Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa kuhamia Dodoma katika JIjini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.

  0 0

  Efm redio katika mwendelezo wa kuwafikia wasikilizaji na wadau wake katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam Ijumaa hii ya tarehe 29/7/2016 inakuletea vipindi vyake vyote live pale Mbagala – Zakhiem kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 12:00 Jioni, ikianza na kipindi cha JOTO LA ASUBUHI. Vipindi hivi vitaambatana na burudani kutoka kwa wasani wa muziki wa singeli wakiwemo Majid Migoma, M-cizo, Dogo niga, Sholo Mwamba na yule mkali wa bongo fleva Juma Kassim maarufu kama Juma Nature pia atakuwepo. Lengo la Nje Ndani ya Efm redio ni kuwaelimisha, kuwapa burudani, kuwahabarisha lakini pia kuwaleta karibu wasikilizaji wake wa kituo cha redio cha E fm.

  0 0

  Rais wa Simba Sport Club  Evans Aveva akizungumza na Vyombo vya Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Simba Week Akiwa Sambamba Katibu Mkuu wa Simba Patrik Kahemela (Kulia) na Afisa Masoko na Mawasiliano Kutoka Eaggroup Richard Ryaganda( kushoto) .

  Simba inasherehekea wiki maalum iliyo Batizwa Jina la Simba Week ambayoImezinduliwa Leo na Rais wa Simba Sport Club Ndugu Evans Aveva na  hufikia kilele chake Tarehe 8 Mwezi Agosti. Mwaka huu siku hii ya Simba week itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya klabu Hiyo. 

  Sherehe za Wiki ya Simba zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza Mabadiliko chanya ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha mwaka mzima.  

  Katika Kipindi Hiki Simba  Sport Club imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwaajili ya kufurahi, kuwatambulisha Rasmi wachezaji,Jezi za timu na kujiandaa kwa Msimu Mpya, siku hii imekuwa Maarufu kama Simba Day. Tangu  Ianzishwe imekua ikiboreka Siku hadi siku, mwaka huu Imeona ni Muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia Mchango wa timu Hiyo kwa Jamii inayoizunguka. 

   Simba iliamua kuanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba Sports Club kufanya kazi za Jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana, kutembelea  Wadau wa Maendeleo na pia Shughuli Nyingine Zenye Tija kwa Timu..Siku ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza Mechi naInter Clube ya Angola kwenye Mechi hii Wachezaji Wapya wataonekana Rasmi baada ya Maandalizi. 

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amekabidhi hundi ya Tsh. 85 Milioni kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza ili litengeneze jumla ya madawati 1,703 yatakayotumika katika Shule za Msingi za Majimatitu na Mbande zilizopo Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam.

  Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 28 Julai, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi iliyopo Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam ambapo Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi madawati katika Shule ya Msingi Chamazi yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania na Jumuiya ya Mabohora Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kutoa mchango huo na pia amewapongeza wadau wengine ambao wameitikia wito wa Rais Magufuli wa kuchangia madawati kwa lengo la kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa chini.

  Waziri Mkuu Majaliwa amesema baada ya kuanza kutekeleza ahadi ya kuondoa ada kwa shule za msingi na sekondari, idadi ya wanafunzi waliojiandikisha kuanza darasa la kwanza katika shule mbali mbali imeongezeka hali iliyosababisha upungufu wa madawati lakini tatizo hilo limetatuliwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini.

  Aidha, amelitaka na Jeshi la Magereza kutengeneza madawati hayo mapema iwezekanavyo ili yakamilike haraka na kuanza kutumika katika Shule za Msingi Majimatitu na Mbande kwani shule hizo zinakabiliwa na idadi kubwa ya Wanafunzi hapa Jijini Dar es Salaam.

  Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Ramadhani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, Wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya msingi Chamazi.
  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi mfano wa hundi Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, SACP. John Masunga (kushoto) leo Julai 28, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi. Waziri Mkuu amelekeza Fedha hizo zitumike kutengeneza madawati ya shule za msingi Majimatitu na Mbande zilizopo Wilayani Temeke.
  Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa ameketi kwenye madawati yaliyotolewa kwa Msaada wa Ubalozi wa Kuwait Nchini Tanzania kama inavyoonekana katika picha.(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imeendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wake  yanayolenga kuboresha utendaji  na utoaji wa huduma zinazokidhi matarajio ya wateja  na kuachana na mtindo wa kutoa huduma  hizo kwa mazoea.

  Mafunzo hayo yanayofahamika kama ‘Culture Change’, yanaendeshwa kwa awamu ambayo yalianza na wajumbe wa bodi, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na sasa yanatolewa kwa maafisa waandamizi wa  na kisha  kwa watumishi wengine wote wa TCAA lengo ikiwa ni kuboresha huduma za Mamlaka kwa wateja.

  Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuboresha huduma kwa wateja wa Mamlaka ni miongoni mwa vipaumbele vya Mamlaka hiyo kwa sasa, ili kuwezesha ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania na kuchangia kikamilifu katika ukuzaji wa uchumi.

  Amesema ni muhimu kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuboresha watumishi ambao ni raslimali muhimu sana katika mafanikio ya taasisi  au kampuni yoyote ile. “Utafiti unaonyesha mafanikio ya taasisi kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na mtazamo chanya wa watumishi kuhusu mahala wanapofanyia kazi ambapo uzoefu na elimu vinachangia kwa kiasi tu mafanikio hayo” ameongeza Hamza.

  Pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yanalenga kuchagiza watumishi wa Mamlaka kutoa huduma zenye viwango vya juu, kuimarisha ushirikiano miongoni mwao, kuwa na mtazamo chanya kuhusu kazi zao, kuachana na utamaduni wa kulalamika badala yake kutafuta suluhu kwa pamoja kutatua  changamoto za mahala pa kazi .
  Meneja Raslimali Watu, Viola Masako (mwenye kipaza sauti) akiwakaribisha watumishi (hawapo pichani) katika mafunzo ya ‘culture change’. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TCAA, Hamza Johari na Mkurugenzi Huduma za Mamlaka, Mbottolwe Kabeta
  Maafisa waandamizi wa TCAA wakifuatilia mafunzo yanayoleanga kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wateja, katika ukumbi wa mikuano wa Mamlaka, Banana- Ukonga

older | 1 | .... | 1299 | 1300 | (Page 1301) | 1302 | 1303 | .... | 3348 | newer