Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

CAG ASSAD AONGOZA KIKAO CHA 70 CHA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa,  Prof. Mussa Assad akizungumza wakati wa hafla ya  kuiaga  Ofisi ya  Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu  za Serikali ya Uingereza ambaye amemaliza ujumbe wake wa miaka sita katika   Bodi.  Mwenyekiti alitumia  fursa hiyo kumshukuru Sir Amyas Morse kwa ushirikiano na weledi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi.
 Ujumbe wa  Ofisi ya Mkaguzi  na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG) muda mfupi kabla ya kuanza rasmi kwa kikao cha 70 cha  Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.  Kutoka kushoto Bw. Isaya Jeremiah, Naibu Mkurugeni Ukaguzi wa Nje,   Bw. Jerome Francis, Naibu Mkurugenzi Ukaguzi wa Nje,  Bw. Salhina Mkumba, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Nje,  na  wa mwisho ni  Bw.  Athuman S. Mbuttuka, Naibu Mkaguzi Mkuu anayesimamia ukaguzi wa Hazina na Umoja wa Mataifa.
 Wajumbe wa  Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto , Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa n Hesabu za Serikali ya India,  Bw. Shashi Kant Sharma,   Mkaguzi  na  Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza, Sir Amyas Morse,  na  Mkaguzi  na  Mdhibiti  Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania, Prof. Mussa Juma Assad,  wakitia saini zao katika  ripoti 11 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa sabini (70), uliofanyika  siku ya  jumanne  hapa  Makao Makuu ya Umoja huo, New York, Marekani. Ripoti hizo ni  matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo. 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa na Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mkaguzi  na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza Sir Amyas Morse ambaye  amemaliza muda wake wa uhudumu wa  miaka sita katika Bodi hiyo. Hafla hiyo ilihusisha pia kukaribishwa  kwa    Bw. Kay Scheller Rais wa Ofisi Kuu ya Ukaguzi ya Ujerumani  anayechukua nafasi ya Uingereza.  Mabadilishano hayo yalikuwa ni  sehemu ya Kikao  cha 70 cha  Bodi ya  Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa ambayo ipo chini ya  Uenyekiti wa Prof Mussa Assad,  Mkaguzi  na Mdhibiti  Mkuu wa  Hesabu za Serikali  kutoka Tanzania.  Kutoka  kushoto ni: Bw. Kay Scheller ( Ujerumani), Sir Amyas Morse ( Uingereza), Katibu Mkuu Ban Ki Moon ( UN), Prof Mussa J. Assad( Tanzania) na Bw.  Shashi Kant Sharma ( India).

Na Mwandishi Maalum, New York.
Bodi ya  Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa,   ambayo   Mwenyekiti wake ni   Mkaguzi na Mdhibiti  n  Mkuu  wa  Hesabu za Serikali, ( CAG) Profesa Mussa J. Assad jana  ( Jumanne)  imerejea  na kuidhinisha  ripoti  kumi na moja za  Mashirika, Mifuko  na shughuli  mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

Katika kikao hicho cha   70 kilichofanyika  hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  pamoja na kuidhinisha ripoti za  Mashirika  na  Mifuko  iliyochini  chini ya Umoja wa Mataifa,  pia Bodi ilipokea  taarifa mbalimbali za kiutendaji zinazohusiana na   majukumu ya  Bodi hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ni    Mkaguzi na  Mdhibiti  Mkuu wa Hesabu wa Serikali ya India,  Bw. Shashi Kant Sharma,    Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza, Sir Amyas Morse, na Mkaguzi na  Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Mussa J. Assad.

Pamoja na  kupitia na kuridhia ripoti hizo kumi na Moja, na  kupokea  taarifa za kiutendaji, shughuli nyingine iliyofanywa na  Bodi ya  Ukaguzi ilikuwa ni pamoja na  kuiaga Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza  baada ya  kumaliza  kipindi chake cha miaka sita ya uhudumu katika Bodi hiyo. 
Hafla ya  kuagwa kwa   Ofisi  ya Ukaguzi ya Uingereza ilihudhuriwa  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Bw. Ban Ki Moon pamoja na wadau mbalimbali ambao ni wateja wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.

 Nafasi ya  Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza  imechukuliwa na Ofisi  ya Ukaguzi ya Ujerumani ambayo  imekaribishwa  rasmi kuwa mjumbe wa Bodi  hiyo.
Akizungumza katika hafla  hiyo ya kuiaga  ofisi ya Ukaguzi ya  Uingereza na  kuikaribisha Ofisi ya Ukaguzi  ya Ujerumani,  Mwenyekiti wa Bodi,  Prof.  Mussa Assad amemshukuru Sir. Amyas Morse  kwa mchango wake yeye binafsi na Ofisi yake kwa uwajibikaji mkubwa na weledi wa hali  ya  juu ambao umefanikisha utekelezaji  wa mamlaka na  majukumu ambayo Bodi hiyo imekabidhiwa na Umoja wa Mataifa.

Akiikaribisha   Ofisi ya   Mkaguzi  na Mdhibiti Mkuu wa Ujerumani,  Prof. Assad  ameelezea matumaini yake  ya kufanya kazi kwa karibu na ushirikiano wa hali  ya juu na  mjumbe huyo ili  kwa pamoja waweze kutekeleza majukumu na mamlaka  waliyokabidhiwa na  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Bodi ya Ukaguzi  ya Umoja wa Mataifa, ilianzishwa   mwaka 1946  na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukagua hesabu za Mashirika,  Mifuko na Taasisi nyingine zilizo chini ya Umoja wa Mataifa,   ili  pamoja na mambo mengine kuhakikisha kwamba Taasisi hizo zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na taratibu za  Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na matumizi yenye tija na adilifu ya   bajeti  kulingana na  mamlaka ya   Mashirika na Taasisi hizo.
Bodi ya Ukaguzi inatekeleza majukumu yake  kama chombo huru na taarifa zote za ukaguzi huwasilishwa kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na wateja  ambao  wanakaguliwa  na  Bodi hiyo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI AZINDUA MIRADI YA TANAPA CHAMWINO, DODOMA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizindua mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lingstone Lusinde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia) Hati ya Makabidhiano ya mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema,  Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Watano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Witness Shoo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania - TANAPA  ambaye pia Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Shirika hilo, Witness Shoo akitoa taarifa ya juu ya miradi miwili iliyofadhiliwa na Shirika hilo katika vijiji vya Ilangali na Manda. Alisema shirika hilo limechangia Tsh. Milioni 148.3 kupitia mradi wa Ujirani Mwema. 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

UCHAFU MBEYA BADO TISHIO.

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA KICHWA TRENI KUGONGANA NA BASI LA UDA JANA USIKU.

$
0
0
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)


Mtu mmoja afariki dunia baada ya basi la UDA kukigonga kichwa cha treni cha Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) katika makutano ya reli na barabara ya Kamata saa 3:20 usiku jana Julai 26, 2016. Marehemu ametambuliwa kwa jina la Omari Abdallah Nyumba mkazi wa Mbagala.

Aidha majeruhi 43 wa ajali hiyo walipelekwa hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo watatu kati yao ni mahututi.

Taarifa za awali za Kikosi cha Polisi Reli zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva Majuto Hamis wa basi hilo la UDA aina ya Hecher lenye namba za usajili T969 CVP kukaidi amri ya kusimama iliotolewa na Mfanyakazi wa TRL. Dereva huyo ni mmoja wa majeruhi ambaye amevunjika miguu na yuko chini ya ulinzi wa Polisi wa Reli akiwa wodini baada ya majeruhi wote kupatiwa huduma.

Kichwa cha treni kilichogongwa ni cha kazi za sogeza Namba 7317 kilikuwa kikitokea kituo kikuu cha treni cha Dar es Salaam. 

Kikosi cha Polisi TRL wameahidi kutoa taarifa zaidi baadae hii leo kuhusu maendeleo ya majeruhi wa ajali hiyo.

Tokea uanze mwaka huu kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto hasa madereva wa pikipiki za bodaboda kutokuwa makini katika kuzitii sheria hizo zinazosimamia makutano ya reli na barabara. 

Tokea kuanza kwa mwaka huu wa 2016 ajali nyingi zimeripotiwa hapa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyoni mkoani Singida zikihusisha vyombo hivyo.

Wito unatolewa na Uongozi wa TRL kwa watumiaji wa vyombo vya moto boda boda , magari mkubwa na mabasi na wananchi kwa jumla kuzingatia sheria ili kuepuka madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na pia upotevu wa rasilimali muhimu ambazo kama zikitumiwa vizuri zitaboresha maisha ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Julai 27, 2016.
DAR ES SALAAM.
.
Muonekano wa Basii hilo baada ya Kugonga treni.


TBS yatoa onyo kwa wanaotengeneza vilainishi feki.

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa onyo kali kwa watu wanaozalisha mafuta ya vilainishi vya mitambo na magari visivyo kidhi viwango vya kitaifa na kimataifa, kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Egid Mubofu (Pichani)amewaambia waandishi wa habari jana jijini hapa kuwa shirika hilo halitakuwa na mjadala kwa wale watakaobainika na kuwaonya waache mara moja.

“Hivi karibuni shirika lilifanya msako mkali wa mafuta ya vilainishi vya mitambo na magari visivyo na viwango na kufanikiwa kuyabaini katika wilaya za Temeke na Ilala,” alisema Dkt. Mubofu.

Alisema katika msako huo walikikamata kiwanda bubu wilayani Temeke na kukifungia na kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Katika msako huo lita 12,296 za vilainishi vya injini zilikamatwa, lita 811 za vilainishi vya mifumo ya breki na kilainishi aina ya ATF lita 1,241; jumla vikiwa na thamani ya Tshs milioni 46.

Pia aliwataka wazalishaji na waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuwapatia bidhaa bora watanzania.

Dkt. Mubofu aliwataka wananchi kususia bidhaa isiyo na alama ya ubora ya TBS kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

“Bidhaa za vilainishi na bidhaa nyingine zote zinapoingizwa nchini lazima zikaguliwe kwa kufuata viwango vinavyotakiwa,” alisema.

Alisistiza kuwa mtu yoyote anayezalisha au anayetaka kuzalisha ni lazima afuate taratibu za nchi.

Alisema shirika litaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na vyombo vingine nchini kama Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) miongoni mwa vingine katika kudhibiti bidhaa zisizo na viwango.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Shirika linategemea sana ushirikiano wa wananchi katika kupata taarifa na kuwataka wanaoishi mipakani kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona bidhaa zinapita bila kufuata taratibu ili kubaini bidhaa hafifu.

VIJANA WAMETAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI VYA UJASILIAMALI NAKUACHA KUTUMIA MUDA WAO KUCHEZA BAO.

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibunguchana,kata ya mkamba ikiwa ni sehemu ya utaratibu ambao ameuweka wa kwenda kushukuru,na kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo leo katiaka kijiji cha kibunguchana  mkoani Pwani.
 Mbunge  wa Mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi fedha taslimu shilingi laki tatu kwa  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Kibunguchana,  Ahamad Mbonde  kwa ajili ya kuazisha msingi wa ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo ambapo pia alifanya harambee ndogo iliyowashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo akiwa Mwenyekiti wa halmashauri, Juma abed ambaye alichangia mifuko kumi yacementi na diwani wa kata hiyo Hassan Dunda alichangia pia mifuko kumi ya  cementi leo mkoani Pwani.
Wananchi wa kijiji cha Lupondo,kata ya mkamba wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Abdallah ulega katika mkutano wake wakuwashuruku wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo huku akihaidi kutoawaangusha nakwamba atakuwa karibu na watu wake. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Mwandishi wetu.
MBUNGE  wa Jimbo la Mkuranga  Abdallah Ulega amewataka vijana wa Wilaya hiyo kujiunga katika vikundi vya vikoba  vinavyoazishwa kwenye maeneo yao  na kwamba wastarajie kuwa ahadi ya rais ya kutoa sh. Milioni50 kila kijijihaitaenda kwa mtu mmoja mmoja bali kwa kukaa katika makundi.

Amesema kuwa kama wananchi wanataka fedha hizo ziwafikie lazima wakae kwenye vikundi na si vinginevyo ,huku akisisitiza akina baba nao kuacha kutumia muda wao mwingi kucheza bao badala yake wajiunge katika vikundi.

Ulega ametoa wito huo  jimbo humo wakati akizungumza na wanachama wa kikundi cha Vikoba cha Tuamke kilichopo katika kijiji cha Lupondo kata ya mkamba.

Alisema kuwa hakuna namna kwani maendeleo yanakuja Kwa kukaa katika vikundi mbalimbali na hata fedha za rais zitaelekezwa katika vikundi hivyo,hivyo kazima watanzania wachangamkie fursa hiyo.

"Binafsi Leo nawachangia sh.laki tatu kwani mmeonesha dhamira ya dhati kupitia risala yenu ambayo mmesoma mbele yangu nami nahaidi nitakuwa pamoja nami kamwe si tawaacha."alisema Ulega.

Aidha alisema kuwa yeye kama mbunge kuna mipango mingi ambayo anayo Kwa ajili ya watu wake ikiwa pamoja na kuleta watu wenye makampuni ya Pikipiki ili kuja katika wilaya hiyo na kukopesha vijana Pikipiki hizo na baadae kulipa kidogokidogo Kwa muda wa miezi 11.

Alisema kuwa lazima vijana,akina baba na akina mama Kwa pamoja wakubali kutengeneza vikundi vya vikoba kwani fursa nyingi zinapitia katika vikoba na si Kwa mtu mmoja mmoja.

Aidha Ulega akiwa katika ziara ya kijiji cha Lupondo alipata fursa ya kufungua jengo la Tuamke Vikoba ambapo pia alitembelea Zahanati ya Kijiji hicho nakuhaidi kutatua tatizo la miundombinu ya Maji.

Alisema kuwa anatambua kuwa Zahanati hiyo inachangamoto kubwa ya Maji hivyo atahakaikisha anasimamia ujenzi wa kisima pamoja na kuona Zahanati hiyo inapata umeme wa Tanesco Kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma.

"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu wote kuleta umeme hapa na kama ule wa tanesco utachelewa basi nitahakikisha naleta solar hapa."alisema Ulega.

Pia mbunge huyo alisema kuwa wananchi watambue kuwa yupo Kwa ajili yao na kwamba watakuwa pamoja katika kipindi chonde cha uongozi wake ikiwa pamoja na kuhakikisha anasukuma huduma jwa wananchi wake.

Naye Diwani wa Kata Dundani ,Hassan Dunda aliwaeleza wananchi hao kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi  huku akisisitiza kuwa watu kukaa katika makundi Kwa ajili kupata mikopo.

Ulega mbali na kufanya ziara katika kijiji cha Kupondo pia alitembelea vijiji vingine mbalimbali ndani ya Kata ya Mkamba ,ambapo pia anaendelea na ziara hizo za kutoa shukrani na kukagua miradi ya maendeleo.

Uzinduzi wa Rock City Marathon; Serikali yawaasa wadau wa riadha nchini.

$
0
0
Rock City Marathon ilizinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam huku wito ukitolewa kwa wadau wa mchezo wa riadha kote nchini kuhakikisha wanafanya jitihada za makusudi kuukomboa mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mbio hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Bw Nape Nnauye,  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo wa Wizara hiyo Bw Alex Nkenyenge alisema kuna haja ya kuwepo kwa jitihada za makusudi miongoni mwa wadau wa mchezo huo ili kurejesha makali ya taifa katika riadha yaliyoonyeshwa miaka ya 1970 na 1980.

Kupitia mkurugenzi huyo Waziri Nape alitoa wito kwa wadau wa mchezo huo kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhakikisha changamoto zinazokwamisha mchezo huo zinatatuliwa ili kuwezesha uwepo wa maandalizi ya kutosha kwa wanamchezo huo.“Ndio maana nawapongeza waandaaji wa mbio hizi kwa kuwa wanashikiri moja kwa moja kukamilisha adhma yetu hii muhimu…kama serikali pia tunaahidi kuendelea kushirikiana nao,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki alisema mbio hizo zinatarajiwa  kufanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zikihusisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo baadhi ya nchi za Afrika, Ulaya na Marekani. Alisema mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.

“Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, mbio za kilomita 3 kwa ajili ya walemavu, mbio za kilomita 3 tena kwa ajili ya wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na mbio za kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19,’’ alitaja.

Alitaja  baadhi ya makampuni yaliyojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited na kampuni ya Real PR Solution.

“ Pia mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuwa zitaambatana na uwepo wa majiko ya wachoma nyama ili kutoa fursa kwa washiriki kufurahia aina hiyo ya kitoweo pamoja na vyakula tofauti vyenye asili ya mkoa huo…ifahamike lengo la mbio hizi kukuza utalii wa ndani ,’’

Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.Akizungumza kwenye hafla hiyo mdhamini mkuu wa mbio hizo  Bw Pratik Patel ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust (AWT) alisema wameamua kuwa sehemu ya mbio hizo kwa kuwa zinaendana na mkakati wao kukuza utalii kwa kulinda maliasili.

“Tunafurahia kuwa sehemu yam bio hizi kwa kuwa lengo lake linaenda sambamba na agenda yetu ya kulinda maliasili na zaidi linaenda sambamba na kampeni yetu ya kupinga vita ujangili inayofahamika kama ‘Okoa Wanyama Wetu; Kataa Ujangili’. Alisema.

 Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya  Habari, Sanaa na Michezo  Bw Alex Nkenyenge (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Rock City Marathon wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki (wa kwanza kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambao ndio wadhamini wakuu wa mbiohizo Bw Pratik Patel (wa pili kulia), Bi Ombeni Savara katibu Mkuu Msaidizi chama cha Riadha Tanzania (wa kwanza kulia) na Joseph Kahama mwenyekiti wa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Joseph Kahama akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
 Mwanaridha mkongwe nchini Bw Juma Ikangaa akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambae ndio wadhamini wakuu wa mbio
 Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya  Habari, Sanaa na Michezo  Bw Alex Nkenyenge akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rock City Marathon.

Leaders to convene in Dar on enabling African businesses

$
0
0
Although recent growth rates in Africa are celebrated in policy and development circles, significant challenges remain with regard to realising the potential of the private sector in Africa. Enabling businesses to enhance the competitiveness of the continent, create employment opportunities and enhance Africa’s economic growth and sustainable development will be the focus of the African Leadership Forum this year. 

The Forum, which will take place on the 28th-29th July, is the third in a series of annual high-level meetings convened by H.E. Benjamin W. Mkapa, former President of Tanzania, with the support of UONGOZI Institute.

According to a statement released by UONGOZI Institute, the African Leadership Forum 2015, with the theme of ‘Enabling African Businesses to Transform the Continent’, will bring together more than 100 key influential leaders and thinkers across the continent, including former Heads of State and leaders from business, government, civil society and academia.

Former Presidents H.E. Joaquim Chissano and H.E. Armando Guebuza of Mozambique, H.E. Thabo Mbeki of South Africa, H.E. Hifikepunye Pohamba of Namibia and H.E. Bakili Muluzi of Malawi are also set to attend the Forum.

“The forum builds on the success of the inaugural dialogue in 2014 on Meeting the challenges of Africa’s transformation and the dialogue in 2015 on Moving towards an integrated Africa”, said the statement, “this year’s event will provide a platform to deliberate on the obstacles preventing African business from flourishing, and what needs to be done about them.”

The African Leadership Forum 2016 will begin with a public plenary on the 28th of July where Mr. Sipho Nkosi, former President of the Chamber of Mines of South Africa will deliver the Keynote Address.

At the end of this one-day event, it is expected that an official statement from participants will be produced, with recommendations on the way forward.


Tanzania yazidi kupaa matumizi ya simu za mikononi

$
0
0
 Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mikononi, ripoti  mpya ya utafiti  iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam imebainisha.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo  ijulikanayo;  ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa  kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)   unahofahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya mawasiliano, Tanzania  imeungana na mataifa ya Nigeria na Ethiopia ambayo  kwa utatu wao yanachukua zaidi ya theluthi moja  ya soko la aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya  watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga  na huduma ya simu za mikononi  huku kukiwa na idadi kubwa ya watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa Mawasiliano ya simu za mikononi  Duniani  ujulikanao kama GSMA umebaini.
Ripoti hiyo pia iliangazia mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
“Zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’ alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji  inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara, serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni 150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
Uwekezaji kwenye mtandao (Network) na simu za kisasa (Smartphones) kunachochea uhamiaji zaidi kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)  unaoendelea jijini Dar es Salaam ukifahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa mawasiliano ya simu za mikononi.

 Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Bw Mats Granryad, akizungumza kwenye mkutano huo.

 Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo. 

NAY WA MITEGO AFUNGIWA, ATOZWA FAINI YA TSH. MILIONI 1.

$
0
0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego).
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote. 

Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.

Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.

Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.

3.Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake. 

Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki 
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza 
KATIBU MTENDAJI, BASATA.

NHC ARUSHA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA MRADI WA SAFARI CITY

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Arusha

Shirika la nyumba la Taifa limeanza ujenzi wa nyumba za mfano kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja na wananchi katika kata ya Olmort jijini hapa mradi utakaojulikana kama Safari city huku likikaribisha wananchi kuja kuwekeza kwenye mradi huo.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa shirika hilo mkoani hapa James Kisarika alisema kuwa mji huo unajengwa kwa awamu na utakuwa na vitu vyote jamii inavyohitaji ikiwemo maji, umeme na mtambo wa kuchakata maji taka.

Alisema kuwa kila kiwanja kitakuwa na huduma za bomba la maji,utengenezaji wa barabara,uandaji wa hati miliki pamoja na michoro huku katika awamu ya kwanza shirika likitoa haki za uendelezaji wa viwanja vyenye ukubwa wa mita za mraba 200-600 na yatapatikana kwa shilingi 35,000 tu kwa mita moja ya mraba.

“Mji huu ni miongoni mwa miji ya kisasa hapa nchini na utaweza kusaidia watu wa kada mbali mbali kupata kumiliki nyumba na kujenga sisi tutakuwa wasimamizi wa mradi huu”alisema kisarika

Alisema kuwa ili kuwa mmoja wa wawekezaji katika mradi huo unapaswa kufuata utaratibu kwa kuchukuwa fomu ambayo ni bure na inatolewa na shirika hilo popote hapa nchini au tembelea tovuti yao www.thesafaricity.com na utalipia asilimia 25% ya thamani ya kiwanja unachotarajia kununua.

Aidha shirika la nyumba la taifa kupitia mradi huo linatoa fursa kwa makundi mbali mbali ya wawekezaji wenye mahitaji ya uendelezaji wa nyumba za makazi kwa vipato tofauti(chini,kati,na juu) majengo ya ofisi na biashara,maduka makubwa(Shoping mall)pamoja na madogo,maeneo ya biashara,maendeleo ya viwanda vidogo vidogo,burudani na utalii,Hospital.uwanda wa elimu,sanjari na huduma zote za kijamii.

Baada ya maelezo hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi wa nyumba za mfano za mradi huo ikiwemo nyumba za makazi nafuu ambazo zitakuwa za mfano kwa nyumba za makazi ambazo wawekezaji hao watatakiwa kujenga kwa mfano huo.

Kutakuwepo na eneo la msitu pamoja na mashine maalumu ya kuchakata maji taka ambayo baada ya kuyachakata maji hayo yatatumika tena kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mradi huo.

USAJILI MWINGINE WA GHALI BARANI ULAYA, NI GONZALO HIGUAIN ATUA JUVENTUS KWA DAU LA PAUNDI 77.3 MIL

$
0
0
Na Dac Popos
Suala la kutumia fedha nyingi za uhamisho kwa wachezaji wa kandanda hasa barani Ulaya linazidi kushika kasi ambapo klabu ya Juventus (vibibi kizee wa Turin) walipo msajili mshambulizi mahiri wa timu ya As Napoli raia wa Argentina Gonzalo Higuain, kwa kitita cha Pound milioni 77.3.

Higuain ambaye alijiunga na Napoli toka Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 34-5 mwaka 2013, anakuwa mchezaji wa tatu duniani kuhamishwa kwa kiasi kikubwa cha pesa nyuma ya Gareth Bale anaye ongoza kwa uhamisho uliofikia Pound milioni 85 toka Tottenham kwenda Real Madrid na Christian Ronaldo toka Manchester United kwenda pia Real Madrid kwa Pound milioni 80.

Hata hivyo imebainika kwamba malipo hayo hayatolipwa yote kwa mkupuo bali yatalipwa kwa awamu mbili.

Higuain ambaye alianza kujulikana kisoka alipokuwa akiichezea timu ya River Plate ya nchini kwao Argentina ameshinda kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa ligi ya Italia Serie A almaarufu kama CAPOCANNONIERE akiwa amefunga magoli 36 na kuisaidia Napoli kushika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Juventus. Hii ni mara ya pili katika karne hii kwa mchezaji mmoja kufikisha idadi ya mabao zaidi ya 30 kwenye serie A, mchezaji wa kwanza alikuwa ni Luca Toni.

aliyefunga magoli 31 akiwa na timu ya Fiorentina msimu wa 2005-06.



Wakati hayo yakijiri Italia, huko Marekani kocha wa timu ya Liverpool (Majogoo wa jiji) Jurgen Klopp amemrudisha Uingereza beki wake kisiki Mamadou Sakho toka kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huko Marekani.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu za kurudishwa huko kwa beki huyo, ingawa taarifa nyingine zikidai kuwa amerudishwa ili akapate matibabu ya mguu ambao huwa unamsumbua, na taarifa nyingine zinadai karudishwa kutokana na nidhamu mbovu aliyoonesha.Vitendo vya nidhamu mbovu vinavyodaiwa kuonyeshwa juu yake kwanza ni tukio la yeye Sakho kuchelewa kufika uwanja wa ndege wakati wakielekea USA, na jingine ni kuuingilia mahojiano ya kocha na waandishi wa habari.
Sakho mwenye umri wa miaka 26 ambaye hivi karibuni alishinda kesi ya kuhusika kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni baada ya kutumikia adhabu ya kufungiwa kwa siku 30 na kusababisha akose kushiriki michuano ya Euro 2016, alijiunga na Majogoo hao kwa dau la Pound Milioni 18 akitokea Paris St-Germain mwaka 2013 na amecheza michezo 55 na klabu hiyo.

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA RUVUMA NA KUKAGUA MAJENGO YA SHULE.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raid TAMISEMI George Simbachawene akikagua jengo la darasa la while ya msingi Luegu wilaya ya Namtumbo baada ya kupata maafa mwaka uliopita.Waziri ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kutoa fedha  shilingi milioni 10 kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo vya kudumu vya wanafunzi ndani ya mwezi mmoja.
Wananchi wa kijiji cha Lundusi Peramiho wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais  TAMISEMI George Simbachawene(hayupo pichani) wakati wa ziara yake  Mkoani Ruvuma leo.

WAKINA MAMA WA WILAYA YA KOROGWE WAFURAHIA MAFUNZO YA UJASILIAMALI YALIOFADHILIWA NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION.

$
0
0
 Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation Sandra Oswald(wapili kushoto) akipatiwa maelekezo na Mariam Jecha (wapili kulia)ambaye ni  bibi  masoko wa kikundi cha 2 Seeds  kilichopo kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga , juu ya utengenezaji na upakiaji wa viazi na mihogo vinavyozalishwa na kikundi hicho  baada ya kupata mafunzo  ya ujasiliamali toka taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds  ya nchini Marekani  yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo inafadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation,wengine kwenye picha ni wajumbe wakikundi hicho.
 Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation,Sandra Oswald (kulia) akishirikiana na wanakikundi cha 2Seeds, wa  kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga  kumenye viazi  kwa ajili ya kutengenza Clips  wakati alipotembelea kikundi hicho kukagua maendeleo ya miradi  mbalimbali ya ujasiliamali ,ufugaji, Kilimo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani  na kufanya kazi zake nchini ambapo  makazi yake makuu  yapo Wilayani Korogwe.
 Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe iliyotengenezwa kitalaam, tayari kwa kupelekwa sokoni, kwa mauzo. Kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi Vinne  vilivyopata elimu ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo  kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania Foundation  kwa  ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani  na kufanya kazi zake nchini.
 Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab (Kulia)akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mashine ya jua inayotumika kukaushia  embe,na mbogamboga   iliyotengenezwa kitalaam,  wakati alipotembelea kikundi hicho kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali,Iliyofadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation  kwa  ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani. 

JAJI MKUU ATEMBELEA JENGO LA MAHAKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI LEO.

$
0
0
  Hili ni jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam.
 Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi akimuelezea jambo alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.
  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alipotembelea  jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.  

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA APOKEA SALAAM MAALUM KUTOKA SUDAN YA KUSINI

$
0
0
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za serikali ya Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo.

Ujumbe huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.

Waziri huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama kwa sasa imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar.

Akipokea ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi za maendeleo kwa amani na utulivu. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI zinazohasimiana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo. 

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan Kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake walioleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake ambao walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ZA TANZANIA NA KOREA, ZATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja,MoFP

SERIKALI za Tanzania na Korea Kusini, zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (Aide Memoire) kwa ajili ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa Maji, Nishati, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA na Viwanda itakayogharimu Dola za Marekani Milioni 300, sawa na TSh.Bilioni 650, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020.

Fedha hizo ni sawa na ongezeko la Dola Milioni 100 ikilinganishwa na kiasi cha Dola Milioni 200 ambazo nchi hiyo ya Korea iliipatia Tanzania kama mkopo wenye masharti nafuu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita (2014 hadi 2016).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, ametia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, huku upande wa Korea Kusini ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Korea Bw. Weon-Kyoung Jo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo wa matayarisho ya kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza miradi hiyo ili iende sambamba na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 uliozinduliwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkakati Mbadala wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA Successor Strategy).

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ya maendeleo iliyochaguliwa kutekelezwa katika sekta zilizotajwa zitachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi.

Bi. Amina Shaaban alisema kwamba Hati hiyo ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea Kusini, yamejikita zaidi katika uboreshaji wa mifumo ya Tehama, kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuboresha miundombinu inayosaidia ukuaji wa viwanda hususan ya nishati ya umeme katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21.

“Ushirikiano wa Tanzania na Korea Kusini umeanza tangu mwaka 2000, kwa kuhusisha taasisi zake mbili ambazo ni Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) ambalo limeipatia Tanzania kiasi cha zaidi ya dola za Marekani 30.9 na Benki ya Exim-Korea ambayo imetoa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 455 sawa na zaidi ya Tsh 900 bilioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka 10 iliyopita” alisema Bi. Amina Shaaban 
Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Wizara ya Fedha ya Korea Weon-Kyoung Jo (kushoto) akizungumza wakati wa mjadala wa Ushirikiano katika misaada ya maendeleo ya kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, yenye thamani ya dola Milioni 300, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo baada ya kusainiwa. Hati hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakipeana mikono baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thmani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300, katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

ASKARI WA TUKIO LA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 15

$
0
0
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU ) Iringa namba G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi. 



Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dkt. Paul Kihwelo, alisema kuwa mshitakiwa amekutwa na hatia hiyo ya kuua bila kukusudia katika shitaka la pili lililosomwa Mahakamani hapo hii leo, baada ya shitaka la kwanza kusomwa na kukutwa hana hatia.


Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Februari 12, 2015, na kufikia hukumu hiyo ya kumtia hatiani hii leo. Tukio hilo lilitokea 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya wanandugu katika foleni ya ukaguzi wa polisi kuingia Mahakamani husikiliza Hukumu ya Askari Polisi.
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi (kulia) akifurahia jambo na ndugu yake mzee Marko Mfugale mahakamani hapo leo.
Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw Deo Nsokolo akizungumza na wanahabari baada ya hukumu ya kesi hiyo.
Picha na Francis Godwin, Iringa.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MWENYEKITI PAMOJA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (TSC) IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Oliva Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Winfrida Gaspa Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (kulia) mara baada ya kuwaapisha ) katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na Mameneja na Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma zenye Matawi yake Tanzania Bara

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mameneja na Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma zenye Matawi yake Tanzania Bara hapo Jengo la Ofisi ya Shughuli za Uratibu wa SMZ Magogoni Jijibni Dar es salaam. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Mjini Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Ofisi hiyo Bibi Shumbana Ramadhan Taufiq na Meneja wa Shirika la Meli la Zanzibar Nd. Salum Ahmad Vuai. Picha na - OMPR – ZNZ.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images