Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1297 | 1298 | (Page 1299) | 1300 | 1301 | .... | 3283 | newer

  0 0


  0 0

  Na mwandishi wetu.
  MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepokea tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi ubora wa kimataifa, jijini Rome Italy Julai 25, 2016.

  Kutolewa kwa tuzo hiyo  kunafuatia mashindano yaliyohusisha zaidi ya makampuni 300 duniani  ambayo yamesajiliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) na kupitia mchakato wa kupigiwa kura na hatimaye kupata washindi.

  Meneja wa udhibiti wa viwangoTCAA, Magesa Sarota akielezea kuhusu tuzo hiyo alisema pamoja na mambo mengine  mashindano hayo yanaangalia  kampuni husika ni kwa namna gani inahakikisha inaendelea kutoa huduma zenye viwango katika masuala ya Uongozi pamoja na kuwa na mifumo inayohakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi viwango.

  Tuzo hiyo ya TCAA ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari kwa niaba ya Mamlaka. Kupokelewa kwa tuzo hiyo ni heshima kwa Mamlaka na ni motisha ya kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya wa kimataifa.
   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) baada ya kukabidhiwa  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa na Raisi wa kampuni ya Otherways, Charbel Tabet inayoendesha mashindano hayo, jijini Rome Italy.
   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari  akionyesha  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa baada ya kukabidhiwa, jijini Rome Italy.
  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akiwa amepozi na  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa  jijini Rome Italy.

  0 0
 • 07/26/16--01:50: BEI YA MADAFU LEO HII.


 • 0 0


  0 0

   Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa bodaboda waliopo kituo cha daladala cha Tegeta  mapema leo, akiwataka wafuate sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu pamoja na abiria wao,kwani wasipovaa Kofia ngumu watachukuliwa hatua Kali zankisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani. Vilevile amewataka kutojihusisha na vitendo vya kihalifu wakiwa na pikipiki zao na akawataka madereva hao wawe wasafi pindi watoapo huduma kwa wananchi.
    Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akiendelea kutoa elimu kwa madereva wa bodaboda waliopo kituo cha daladala cha Tegeta  mapema leo
   Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akiendelea kutoa elimu kwa madereva wa bodaboda waliopo kituo cha daladala cha Tegeta  mapema leo

  0 0

  KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van De Pluijm amejizatiti kuweza kutoka na ushindi kwenye mechi ya nne ya kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Medema ya nchini Ghana ambapo mechi hiyo itaonyeshwa kupitia chaneli ya Supersport 9 majira ya saa 11:50 jioni


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Luhaka (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan Bruce kwa pamoja wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360 jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipatiwa maelezo na Meneja Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Huawei, Ian Ellis (kulia) alipotembelea Banda maalum la Teknolojia ya Mawasiliano la Huawei Tanzania, baada ya uzinduzi wa Tamasha la Teknolojia, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwl. J.K. Nyerer, Jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Luhaka.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifungua mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya  wajumbe wa  mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, wakifatilia mada jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan Bruce akizungumza na wanahabari juu ya Teknolojia yao ya kisasa waliyoizindua rasmi nchini.
  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wananchi wa mjini na vijijini kutumia simu ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali za kimtandao zinazotumika hapa nchini.

  Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa kimataifa wa chama cha kampuni za simu duniani GSMA mobile 360, Prof . Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano ya simu inawafikia wananchi wote ili kuwezesha kunufaika na huduma za simu za kisasa.

  ‘Ili wananchi waweze kupata maendeleo kwa haraka  na kunufaika na fursa za kimtandao katika masuala ya elimu, biashara, kilimo, afya na ustawi wa jamii kwa ujumla kunahitajika uwepo wa simu za kisasa zinazoweza kuruhusu mifumo ya kimawasiliano’, Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameitaja mifumo hiyo kuwa ni Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao,  Kilimo Mtandao, Serikali Mtandao, Hali ya Hewa Mtandao ambavyo kwa pamoja  vitamhudumia mwananchi kwa ubora na wakati.
  Amesisitiza kuwa serikali inashirikiana kwa karibu na kampuni  za mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma za simu zinakuwa za uhakika na salama.

  Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba mfuko wa Mawasiliano Vijijini unaendelea kunufaisha watanzania na mkakati wa kuhakikisha umeme unafika vijijini unaimarika sambamba na uwepo wa simu za kisasa za bei nafuu.

  Takribani laini za simu milioni 39.9 nchini zinatumika katika huduma mbalimbali na hivyo huchangia uchumi wa nchi.

  Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kukuza sekta ya mawasiliano hapa nchini ambapo hadi sasa tayari kilomita 18,000/- za mkongo wa taifa wa taifa wa mawasiliano zimejengwa hapa nchini.

   “Serikali itaendelea kudhibiti vifaa vya mawasiliano visivyo na ubora ili visiingie nchini na hivyo kuhakikisha watumiaji wa mitandao ya simu wanakuwa salama na wanaitumia mitandao hiyo kwa wakati wote’. Amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Mkutano huo wa siku mbili ambao pia umehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Thomas Luhaka ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Changamoto mbalimbali na kuja na suluhisho na namna bora ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano duniani.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipofanya ziara ya kuitembelea hospitali ya Teule kuangalia changamoto zinazoikabili kulia ni Mganga Mfawizi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.
  Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kulia kuzungumza na watumishi wa Hospitali Teule ya Muheza.
  Mganga Mfawizi wa Hospitali Teule ya Muheza Malahiyo Rajabu kulia akitoa ufafunuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza wakati mkuu huyo wa wilaya alipofanya ziara kwenye hospitali hiyo.

  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars" Charles Boniface Mkwasa(Pichani) ameteua kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya kambi maalum ya Taifa Stars kujiandaa na pambano la kukamilisha ratiba ya mbio za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria.

  Vijana wamepewa nafasi kubwa katika kikosi cha Mkwasa huku kiungo wa Mtibwa Sugar Ibrahim Jeba  pamoja na Joseph Mahundi wa Mbeya City na Jamal Mnyate aliyehamia Simba pia wameitwa kwa mara ya kwanza. Mbali na hao pia amemuita kwa mara nyingine tena Saimon Msuva na Oscar Joshua.

  Timu hiyo itaingia kambini Agosti 1 hadi 5 ikiwa ni kambi ha awali kwa ajilo ya kuwaweka sawa kisaikolojia huku kati ya Agosti 23-25 wataingia kambi ya mwisho kabla ya kuondoka kwa ajili ya kwenda kuwavaa katika mchezo wa marudiano Septemba 02.

  Kikosi Kamili:
  Walinda Milango: Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benno Kakolanya.

  Walinzi: Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mohamed Hussein, Juma Abdul, Erasto Nyoni.

  Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Simon Msuva.

  Washambuliaji: Joseph Makundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib, John Bocco, Jeremiah Juma.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akitoa hotuba yake katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Sauti za Vijana Tanzania wa Kizazi cha Sasa na Kijacho (Next GenerationYouth Voices Tanzania), Ikiwa ni Utafiti uliofanywa ili kuangalia changamoto zinazowakabili Vijana, Mitazamo na matarajio ya idadi ya Vijana Tanzania, uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es salaam Julai 26, 2016.
  Balozi wa Uingereza nchini (anaemaliza muda wake), Balozi Dianna Melrose akitoa ujumbe wake kwa Vijana walioshiriki hafla hiyo ya Uzinduzi wa Sauti za Vijana Tanzania wa Kizazi cha Sasa na Kijacho (Next GenerationYouth Voices Tanzania), Ikiwa ni Utafiti uliofanywa ili kuangalia changamoto zinazowakabili Vijana, Mitazamo na matarajio ya idadi ya Vijana Tanzania, uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es salaam Julai 26, 2016.
  Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye hafla hiyo.
  Kijana wa Kitanzania anayejishughulisha na maswala ya Uchoraji, Ahmed Mohamed akizungumza machache kwenye hafla hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Julai, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, ambapo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania  hususani kutoa mikopo iliyowezesha ujenzi mkubwa wa barabara.


  Pamoja na kuishukuru AfDB Rais Magufuli ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mpango mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme utakaofanikisha ujenzi wa viwanda, ujenzi wa barabara zinazounganisha ndani na nje ya Tanzania na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na rushwa.


  Kwa upande wake Makamu wa Rais wa AfDB Dkt. Frannie Leautier amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozianza katika kujenga uchumi wa Tanzania, kukabiliana na rushwa na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na ameahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu itakayofanikisha mipango na miradi mbalimbali ya Tanzania.


  "Tanzania ni nchi ambayo inapata fedha kuliko nchi zote za Afrika katika mpango wa AfDB kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Afrika,  hizi ni fedha ambazo zinatolewa kwa mkopo nafuu zaidi kuliko mikopo mingine" Amesema Dkt. Frannie Leautier.


  Dkt. Frannier Leautier amebainisha kuwa AfDB inatarajia kuwa Tanzania itanufaika kupitia vipaumbele vitano vya benki hiyo ambavyo ni kusaidia uzalishaji wa nishati, utangamano wa bara la Afrika, maendeleo ya viwanda, usalama wa chakula na kuboresha hali ya maisha.


  Aidha, Makamu wa Rais huyo wa AfDB amesema kuanzia mwakani benki hiyo imepitisha miradi mikubwa mitatu kwa ajili ya Tanzania ambayo ujenzi wa nyumba ya makazi, utoaji wa mikopo vijijini kwa ajili ya kuendeleza kilimo na maeneo ya uchumi kupitia benki ya CRDB na kukiendeleza Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela kilichopo Arusha ambapo benki hiyo itatoa Dola za Marekani Milioni 4.


  Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mwakilishi Mkazi wa AfDB Dkt. Tonia  Kandiero, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dodoma


  26 Julai, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Kushoto ni ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimewangalia  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier akisaini kitabu alichotunga kabla ya kumkabidhi Rais alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea kitabu kutoka kwa   Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier  na ujumbe wake aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wa tatu kulia ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero, kulia ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje Bw. Johannes Jovin akifuatiwa na Mkrugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy. Kushoto ni Mshauri wa Rais Masuala ya Profesa Longinus Rutasitara akifuatiwa na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Katikati ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero

  0 0

  Bombardier Commercial Aircraft announced today that the Government of Tanzania has signed a firm purchase agreement for two Q400 turboprop airliners. The aircraft will be delivered with a 76-seat, dual-lavatory configuration and will be used for commercial airline operations in the region.

  Based on the list price of the Q400 airliner, the firm order is valued at approximately US $62 million.

  “Our Q400 aircraft will provide affordable, convenient and comfortable air transport solutions,” said Dr. Leonard Chamuriho, Permanent Secretary, Ministry of Transport, Works and Communication, Tanzania. “We are committed to providing state-of-the-art service to our passengers and are keen to expand further as our business grows to include new destinations in Tanzania and the African region.

  “Tanzania is a large country with some challenging airfields, and the Q400 turboprop’s capability to operate at these airports, its jet-like speed, long-range cruise capability and outstanding turboprop economics were key factors that guided us in selecting the aircraft for our operations,” added
  Dr. Chamuriho. “The level of in-continent support that Bombardier offers is also very important for us.”

  “This transaction not only solidifies the relationship between the Government of Tanzania, and Bombardier, but also reaffirms Africa as one of the most prolific Q400 aircraft markets. The Q400 aircraft is a showcase for the continent, where it has proved itself to be extremely efficient as well as cost-effective,” said Jean-Paul Boutibou, Vice President, Sales - Middle East and Africa, Bombardier Commercial Aircraft.

  READ MORE HERE

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
  Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji(Pichani) ametoa wito kwa Serikali na Mashirika binafsi kuisaidia Kampuni ya Dar Festival ili Iweze kufanya tamasha la kutangaza utamaduni wa nchi ya Tanzania.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Diwani huyo ambaye pia ni Mlezi wa Kampuni hiyo alipokuwa akilitangaza rasmi tamasha hilo mbele ya waandishi wa habari.

  Khimji amesema kuwa ni jambo jema kuona vijana wanazungumzia suala la utamaduni kwani hali hii inaonyesha dhahiri kuwa wameamua kuirudisha nchi kwenye mstari wa kujali utamaduni wetu.

  “Mataifa yote makubwa yanajali tamaduni zao hivyo ni vema na sisi kama watanzania kuamua kwa dhati kuhakikisha tunarudisha utamaduni wetu, jambo hili sio dogo linahitaji fedha nyingi kwahiyo, tunaomba msaada kutoka kwa Serikali na Mashirika binafsi ili kufanikisha tamasha hili”, alisema Khimji.

  Diwani huyo ameongeza kuwa vijana hao wamejitahidi hadi hapo walipofika lakini kama wakikosa misaada kutoka kwa wadhamini mbalimbali basi tamasha hilo halitoweza kufanikiwa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Faridi Faradji amesema kuwa wameamua kuisaidia Serikali kwa kuangalia njia mbadala ya kukusanya mapato kwa kutangaza utamaduni wa Tanzania kupitia tamasha hilo.

  “Kwa namna moja au nyingine,tuna kila sababu ya kuisaidia nchi yetu kukusanya mapato ili iweze kuendelea kwasababu baadhi ya nchi zingine zimeweza kuendelea kupitia matamasha kama haya”, alisema Faradji.

  Naye Katibu wa Kampuni hiyo, Amini Kingazi amesema kuwa tamasha hilo ni la asili kwahiyo wameamua kulifanyia katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa sababu ni eneo lenye vitu vingi vinavyoonyesha utamaduni wa kitanzania.

  Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kila mwaka, Kwa mara ya kwanza litafanyika mwezi Septemba mwaka huu likijumuisha vitu vyenye asili ya kitanzania kama vyakula vya kitanzania, mashindano ya michezo ya kiasili pamoja na wanamuziki wa kitanzania.

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga (katikati) akiambatana na ujumbe wake wakati wakielekea kwenye Uwanja wa Chipukizi, kulikofanyika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora, iliyofanyika leo Julai 26, 2016. Kata hizo ni Ndevelya, Ifucha, Isevya na Mtendeni.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akimkabidhi mlezi wa Timu Kata ya Ifucha, Moses Singo,wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora, iliyofanyika leo Julai 26, 2016.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akimkabidhi vifaa vya Michezo Mwenyekiti wa Bawacha kata ya Ndevelwa, Mariam Ramadha, kwa ajili ya Vijana wa Kata yake.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora (CHADEMA), Hawa Subira Mwaifunga akionyesha uwezo wake wa kusakata kabumbu mbele ya vijana wa Kata nne za Manispaa ya Tabora mara baada ya kuwakabidhi vifaa mbali mbali vya Michezo.

  0 0

  Mwanamuziki wa Kimataifa wa Miondoko ya Dansi kutoka Nchini Congo, Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama "Koffi Olomide" amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya kuonekana na hatia ya kumdhalilisha kwa kumpiga dansa wake wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya hivi karibini.

  Mwanamuziki huyo alikamatwa mapema leo akiwa nyumbani kwake katika mji wa Kinshasa na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na kukutwa na hatia hiyo.

  Hukumu hiyo imetolewa baada ya ushahidi huo kuonekana akimpiga dansa wake na atatakiwa kuitumikia adhabu hiyo kwani hajapewa nafasi ya kulipa faini ya aina yoyote ile.

  hatua ya kumkamata Mwanamuziki huyo ilifikiwa baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya baadhi ya wadau wa maswala ya kijamii wakiongozwa na Zakarie Bababaswe aliyefungua kesi kwa niaba ya Serikali ikiwa ni madai ya udhalilishaji kwa dansa wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kongo, kuamua kukamatwa kwake na kusema anataka haki itendeke.

  CHINI NI VIDEO INAYOONYESHA TUKIO HILO.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara ,  viongozi wa dini na wanachi wa Dodoma kuhusu mikakati ya serikali ya kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.

  Baadhi ya wazee, wafanyabiashara, viongozi wa dini na wananchi wa Dodoma wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mikakati ya serikali ya kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma baada ya kuzungumza na wazee, viongozi wa dini, wafanyabiashara na wananchi wa Dodoma  kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1297 | 1298 | (Page 1299) | 1300 | 1301 | .... | 3283 | newer