Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1296 | 1297 | (Page 1298) | 1299 | 1300 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mbunge was jimbo la Mkuranga ambaye pia ni katibu wa wabunge wanaotokana na chama cha Mapinduzi CCM Abdallah Ulega akiwa sambamba na katibu wa CCM mkoa wa pwani Joyce Masunga wakijadiliana jambo kabla ya kumpokea mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt.Jakaya Kikwete
  Baadhi ya Wanachama cha CCM wakinogesha sherehe za kumpokea na Kumkaribisha Dkt Jakaya kikwete ambaye amekabidhi kijiti cha Uenyekiti wa chama hicho kwa Mwenyekiti mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli,kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
  Maandalizi yaliyoambatana na chereko chereko za hapa na pale za kumpokea na Kumkaribisha Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho,Dkt Jakaya kikwete zikiendelea ukumini humo 
  Wanachana na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani wakimsubili kumpokea na kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti mstaafu na Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete katika ukumbi wa Kasuba,Msoga-Bagamoyo.PICHA NA EMANUEL MASSAKA-GLOBU YA JAMII-BAGAMOYO.

  0 0

  Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, liitwalo Asvoko, limeiomba serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashataka mwanamuziki Koffi Olomide. 

  Hii ni baada ya kuonekana katika video iliyosambaa mitandaoni akimpiga teke mmoja wanamuziki wake wa kike kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi ijumaa wiki iliopita.

  Wakati huo huo shirika la Zambia la kilimo na biashara limefutilia mbali tamasha ambalo Koffi alipanga kulifanya nchini humo lililokuwa linatarajiwa kufanyika kuanzia Jumatano hadi Jumatatu Ijayo. Raisi wa taasisi hiyo Ben Shoko amesema kitendo hicho alichokifanya mwanamuziki huyo wa kimataifa katika muziki wa dansi sio cha kiungwana kabisa.

  Ijumaa iliyopita katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata JKIA Nairobi Koffi alinaswa katika video akimpiga teke dansa wake huyo kwa kilichodaiwa alikorofishana na mwanamuziki wa kundi hilo aitwaye Cindy Le Couer ambaye amekuwa na mahusiano naye wa kimapenzi toka 2012.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

  WAAMUZI wa mchezo wa  soka mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha wanachezesha kwa kuzingatia sheria 17 za mchezo huo na kutoa maamuzi yaliyo sahihi ili wasiwe ni moja ya chanzo cha susababisha migogoro n akuvunjika kwa baadhi ya michezo wanayokuwa wakichezesha.

  Kauli hiyo imetolewa na na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoani Pwani (COREFA) Hassan Hassanoo wakati alipokuwa  akifungua mafunzo kwa waamuzi wa mchezo wa soka wa mkoa huo ambayo yaliyofanyika kwenye  uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha  Tumbi.

  Hassano alisema kwamba mwamuzi  wa mchezo wa mpira ni sawa na  hakimu ambaye anapaswa kutoa maamuzi yake kuzingatia sheria kanuni pamoja na taratibu zote ambazo zimewekwa katika kuongoza mchezo wa soka ii kuweza kutimiza malengo ya kuweza kuuendeleza zaidi kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

  “Mimi kikubwa ninachowaomba waamuzi katika Mkoa wa Pwani tuwe makini sana katika kutimiza majukumu yenu, kwani wakati mwingine michezo imekuwa ikivunjika na wengine kutoa malalamikoi, kwa hiyo katika hili hakikisheni mnasimamia sheria zote 17 za mchezo huu wa soka katika Mkoa wetu wa Pwani na sio vinginevyo,”alisema Hassanoo.

  Aidha aliongeza kuwa suala la kuwa mwamuzi wa mchezo wa soko ni wito na  si suala la  biashara kama baadhi yao wanavyofanya kama sehemu ya kujiongezea kipato kwani mwamuzi anapaswa kuhakikisha mchezo unakwisha salama na hata kama unavunjika sababu iwe ambayo ni nje ya uwezo lakini siyo kusababishwa na mwamuzi.

  “Kwa hiyo waamuzi mnapaswa kujifunza kila mara kwa sababu sheria za soka hubadilika kila mara ambapo kwa sasa zimekuwa zikibadilika kama fasheni kwa lengo la kuongeza ladha ya mchezo wa soka hivyo lazima muendane na mabadiliko ya sheria hizo ili kupunguza lawama ambazo zimekuwa zikitolewa ,” alisema Hassanoo.

  Aliwataka waamuzi  wasibweteke na madaraja waliyopo bali waongeze bidii ili wafike madaraja ya juu na kuweza kuchezesha ligi kuu kama walivyo baadhi yao na waweze kufikia kuchezesha michezo inayoandaliwa na Mashirikisho ya Soka Afrika CAF na Dunia FIFA na mkoa utaendelea kutoa mafunzo mbalimbali.

  Kwa upande wake mmoja ya waamuzi ambaye alisoma risala ya waamuzi hao Kasule ambogo alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolipwa posho zao kwa wakati ambapo zamani walikuwa wakilipwa hata kabla ya mchezo.

  Ambogo alisema kuwa pia changamoto nyingine ni kukosa mafunzo hayo ya kujikumbusha sheria za soka kwa muda mrefu hivyo kusababisha waamuzi kushindwa kupanda  madaraja kwa wakati na kuksa hata sifa za kuweza kuchezesha katika ligi kuu ya Tanzania bara.

  KOZI hiyo ambayo ilifanyika kwa siku mbili kwa kuwashirikisha waamuzi  wapatao 60 kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Pwani.

  0 0

   Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.
   Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.  Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubei Ali Maulid na wapili kulia ni Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson.
   Wananchi wa Dodoma waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikilza Rais John Magufuli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini julai 25, 2016.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Mashabiki wakionesha namna mbalimbali za Ushangiliaji hapa kwa mtindo wa Yesu Msalabani mpaka dakika 90 zinamalizika katika mashindano ya Ndondo Cup yatakayofikia mwisho Julai 30 mwaka huu.

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  UHONDO wa Ndondo twende ukaujue Julai 30, hapa Temeke Market hapa Kauzu Fc wote watoto wa Temeke wakitunishiana misuli wakitaka kumjua nani mbabe wa wilaya hiyo. 

  Wakijivunia kulibakisha kombe ndani ya Temeke kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo.

   Ukiutaja uwanja wa Bandari watu wanaweza wakajiuliza ni upi huo ila almaarufu ni WEMBLEY walitumia jina la Uwanja uliopo nchini Uingereza. Katika uwanja huo unaobeba mashabiki zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja ukipewa sifa ya amani na utulivu kwa mashabiki.  

  Hii ni fainali ya aina yake pale timu kutoka Temeke zikitambiana na kila mmoja na kujizatiti katika kulibakisha kombe hilo kwake, Kauzu Fc inakuwa ni fainali yao ya 2 mfululizo wakikumbuka machungu ya kunyang'anywa tonge na Faru Jeuri msimu uliopita.  Temeke Market ni mara ya kwanza kushiriki na kufanikiwa kuingia hatua ya fainali na kuweka rekodi kwa timu yao. Nani kuondoka nalo? Hilo litajulikana Wembley July 30.
  Ukiachilia mbali ukubwa wa mashindano hayo kwa sasa, viongozi mbalimbali wameweza kujitokeza kwa wingi ambapo Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ameonesha kuvutiwa na mashindano hayo na kuwapa majukumu waandaji kuweza kuanzisha mengine kwa ajili ya shule za  sekondari. Katika fainali ya pili, Makonda aliweza kutoa ahadi ya 200,000 kwa golikipa wa timu itakayoingia fainali atazawadiwa huku aliyekuwa mbunge wa Tabora na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage dau lake lilishindwa kukamilika ila ameweza kuwakabidhi waandaaji kiasi cha shilingi 100,000 kwa ajili ya kupatiwa mchezaji atakayefunga goli la kwanza kwenye mchezo wa fainali.
  Hivi kwani timu kubwa haziwezi kuja kuangalia vipaji huku mtaani ?? Swali hilo liliulizwa na Ismail Aden Rage(Pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Misosi FC na Kauzu FC.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  SERIKALI imesema sekta ya kilimo inaendelea kuwa sekta muhimu katika uchumi wa Tanzania kwa asilimia 25% ya pato la taifa na kuajiri asilimia 75% ya watanzania  wakiwemo wanawake na vijana.

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Richard Kasuga wakati wa uzinduzi wa mchezo wa redio uitwao KUMEKUCHA unaotarajia kuonyesha mchango wa wanawake na vijana katika kutokomeza tatizo la uhaba wa chakula nchini.
  Kasuga  amesema kuwa igizo hilo la mchezo wa redio, litaakisi umuhimu wa ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kukuza sekta ya kilimo na kutoa ujumbe kwa vijana kuona umuhimu wa kilimo hasa kilimo cha biashara.

  “Sheria na tamaduni zilizopo zinakwaza juhudi za mwanamke kupata fursa za kiuchumi kwa sababu hawana haki ya kumiliki ardhi au vifaa vya kilimo, vyanzo endelevu vya maji, ukosefu wa mikopo ambayo wanahitaji ili kufanikisha juhudi zao”alisema Kasuga.

  Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la msaada la Marekani (USAID) Randy Chester alisema kuwa mchezo wa KUMEKUCHA umeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media for Development International (MFDI) na kufadhiliwa na USAID kwa lengo la kupunguza uhaba wa vyakula vyenye virutubisho hapa Tanzania.

  Mchezo wa KUMEKUCHA ni mchezo wa redio wa kila wiki ambao unaangazia maisha, vikwazo na fursa za wakulima Tanzania na utaanza kurushwa hewani kuanzia Julai 25, 2016 kupitia Redio Free Afrika, Redio Abood FM, Redio Ebony FM na Redio Bomba FM.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Ngao katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016 .
  Shughuli za maadhimisho hayo ya siku ya Mashujaa zilipokuwa zikiendelea ndani ya uwanja huo wa Mashujaa.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.
  Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
  Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.PICHA NA IKULU

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi  waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.

  *Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

  Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.

  “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.

  Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

  “Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.

  Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

  Wakati huo huo, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.

  Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake.

  “Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.

  Mara kwanza kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.

  Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,    
  DODOMA.

  JUMATATU, JULAI 25, 2016.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Godfrey Simbeye (katikati) akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, kuhusu mafunzo yatakayo tolewa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia tovuti ya taasisi hiyo. Meneja mradi wa TPSF Celestine Mkama (kushoto) wa mwisho kulia Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi.
  Meneja Mradi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Celestine Mkama (kushoto) ) akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Dar es salaam, kuhusu mafunzo yatakayotolewa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia tovuti ya taasisi hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye na Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi.
  Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, namna wajasirimali wadogo na wakati watakavyo weza kunufaika na mafunzo yatakayotolewa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia tovuti ya Taasisi hiyo . kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye. 

  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) itaendesha mafunzo maalum kwa wajasiriamali nchi nzima kuhusu namna ya kunufaika na tovuti mpya ya habari kwa wajasiriamali. 

   Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema taasisi hiyo imeanzisha vipindi vya redio katika vituo mbalimbali vya redio za kitaifa na vituo vidogo vya redio za jamii katika mikoa ya Dodoma, Geita, Kigoma na Mbeya. Vipindi hivyo vya redio vitaenda sambamba na warsha za mafunzo zitakazowahusisha wajasiriamali na wadau mbalimbali katika mikoa hiyo.

   “Kampeni hii imelenga kuongeza uelewa wa wajasiriamali juu ya tovuti hiyo ambayo ina mifumo ya mafunzo kwa wajasiriamali, namna ya kuanzisha na kukuza biashara, upatikanaji wa mitaji, mbinu sahihi za kuendesha biashara, namna ya kutafuta na kuuza bidhaa katika masoko, vilevile kampeni itatoa jukwaa la majadiliano kuhusu mada mbalimbali zinazowahusu wajasiriamali wadogo nchini.” alisema Simbeye.

   Mafunzo yatatolewa nchi nzima na wataalamu waliobobea katika biashara na ujasiriamali kwa kipindi cha miezi nane ili kuwajengea uwezo wajasiriamali waweze kunufaika ipasavyo na tovuti hiyo iliyozinduliwa mapema mwaka huu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage mapema mwaka huu. Tovuti hiyo inayopatikana kupitia www.entrepreneurs.or.tz, www.wajasiriamalitz.or.tz au kwa kupiga namba *148*99*06# ni kituo maalum chenye taarifa zote sahihi zinazomtosheleza mjasiriamali kuendesha biashara kwa mafanikio. 

   “Huduma hii imetolewa ili kuwasaidia wajasiriamali ili waweze kupata nyenzo muhimu za kuendesha biashara, vyanzo vya fedha, kuingia kwenye masoko ya hapa nchini na kimataifa, na taarifa nyingi za kuweza kumsaidia mtu anayetaka kuanzisha biashara na kuwawezesha wale ambao tayari wanafanya biashara kujiongezea ujuzi na uzoefu,” alisema Simbeye.

   Meneja Mradi wa Tovuti hiyo, Celestine Mkama alisema “Tumeona umuhimu wa kuendesha kampeni ya kuongeza uelewa wa tangu wakati tunatengeneza mfumo huu wa habari. Tunatarajia kupitia kampeni hii kuweza kuwafikia wajasiriamali moja kwa moja kupitia vipindi vya redio na warsha na kuweza kutatua matatizo yao kwa kuwapatia ujuzi”. 


  Hivi sasa kuna wajasiriamali zaidi ya milioni tatu nchini na tunajua kwamba ujuzi hafifu ni kikwazo kikubwa katika ukuaji wa biashara ndogo ndogo ambazo ni muhimu sana katika ukuaji uchumi,” alisema Mkama. “Tunataka kuhamasisha matumizi ya tovuti hii na kutoa mafunzo wakati huo huo. Tunaamini jambo hili litawajengea uwezo na kuwapa wajasiriamali ujuzi muhimu wa kuendesha biashara endelevu.”

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mashujaa waliojitoa kwa uzalendo kupigania Tanzania hawana budi kukumbukwa kutokana na kujitoa kwao ili Tanzania isitawaliwe na wakoloni.

  Makonda ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa katika Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, amesema kuwa mashujaa hao walifanya ukombozi kwa uzalendo bila kuangalia dini zao na makabila yao.

  Makonda amesema kuwa kila mtu lazima ajiulize juu mashujaa katika kufanya kazi katika kungalia kutenda haki pamoja na uzalendo kwa masilahi ya taifa.

  Amesema kuwa amani iliyopo nchini imetokana na watu kuwa wazalendo katika kupigania nchi yao na hawakuangalia kupoteza maisha au familia zao.

  Aidha amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi bila kuangalia vyama wanavyotoka au kabila kutokana na umoja uliojengwa na mashujaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka Ngao kwenye Mnara uliopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwakumbuka Mashujaa waliopigana vita hapa nchini. Siku ya Mashujaa hufanyika Julai 25 kila mwaka.
   Askali wakitoa heshima wakati wa sherehe za kumbukumbu ya mashujaa ambayo imefanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wakati wa sherehe za kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita hapa nchini.

  0 0

  Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
  Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva - Switzarland,  Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kwa lengo kuwajengea uwezo watalaam kuhusu ujazaji wa taarifa  kuhusu sababu ya kifo cha mgonjwa pindi wanapojaza cheti cha kifo (Death Certificate).Washiriki  wa Mafunzo hayo ya Siku mbili watakua na jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi wanazotoka kuhusu mfumo huo.
   Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua  sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo. 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Msanii nyota nchini wa filamu, Jacob ‘JB’ Steven ni miongoni mwa waigizaji mbalimbali walioshiriki katika igizo la Kumekucha ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na uhaba wa soko la ajira.

  Igizo hilo ambali pia ni mchezo wa redio (radio plays) limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid) ya ushauri wa Taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Taasisi ya TAHA, ACDI VOCA – NAFAKA, Land O Lakes, Rudi, Mwanzo Bora, The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action Forum) na taasisi ya AMSHA.

  Katika filamu hiyo, JB anatumia jina la Mzee Kidevu ambaye kazi yake kubwa ni kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, JB alisema kuwa amefurahi sana kushiriki katika filamu hiyo ambayo inafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho lao la kutatua matatizo yao. “Nimepanda kushiriki katika filamu na mchezo huu wa redio, umenipa mwanga mkubwa na kupanua wigo wa kazi yangu ya kuigiza, kabla ya kuingia kwenye kuigiza, nilikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa na kusaga na kuuza unga wa chakula, hii ilikuwa fursa kwangu na nimeipenda, nawashukuru wahusika wote waliofanikisha filamu hii,” alisema JB.

  Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester alisema kuwa wamefurahi kujihusisha na masuala mbalimbali yaa maendeleo hapa nchini na kuamua kusaidia mradi huo ambao unahusika zaidi maeneo ya vijini. “USAID imejihusisha katika miradi mingi ya maendeleo nchini, kama unajua, zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo, waahitaji kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa ya maendeleo, mchezo wa Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” alisema Chester. 
  Muigizaji nyota wa filamu nchini, Jacob Steven (JB) akiizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na igizo jipya lilijulikanalo kwa jina la Kumekucha ambalo imeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Katika igizo hilo, JB ametumia jina la Mzee Kidevu. Muandishi wa ‘script’ ya igizo la Kumekucha, Priscilla Mlay (kulia) akizungumza wakati wa utambulisho wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo hilo la Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” 


  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.

  Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.

  "Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.

  "Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa"Amesema Rais Magufuli.

  Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

  Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dodoma  25 Julai, 2016

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), John Kyaruzi (kulia), akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tano ya kilimo ufugaji wa kibiashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya mfuko huo, Dr Rosebud Kurwijila na Mkurugenzi wa Hamashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), Dk. Rosebud Kurwijila (kushoto), akifungua semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi.
    Baadhi ya wafugaji wakifanya wakijadiliana wakati wa  semina ya wafugaji inayolenga kuwainua kiuchumi wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe iliyoandaliwa na  Mfuko wa SAGCOT CTF.

  Na Mwandishi wetu Njombe.
  WAFUGAJI wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo kibiashara ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua kipato chao imeelezwa mkoani humo jana.

  Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF kwa kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua kipato  kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara.  

  Alisema hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa SAGCOT CTF  na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni mkoani Tanga 2015 mafunzo yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya kuwafanya wafugaji wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.  

  “Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa kujua nini mfugaji anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji kutajirika kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo utasaidia wafugaji kufuga kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata  ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.

  “Wafugaji wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini wanachokikosa ni elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF  hautatoa mkopo wa pesa pekee kwa wakulima bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema. 


  Katibu Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani itasaidia wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia wakipewa mbinu ya kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa kibiashara na kwa matumizi yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja,  jamii na pia kujenga afya zao kutokana na kutumia maziwa bora. 

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha kwa wingi.

  Nao baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika wengine waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza kuwa ufugaji wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya zao.

  Mfuko wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka 2002 chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko ulitafuta wabia muhimu kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni mshirika wake katika kutoa utaalamu elekezi. (technical assistance).

  0 0


  Mwanafunzi Sara Sulle wa kidato cha nne shule ya Sekondari Malama Mkoani Mbeya amelazwa katika hospitali teule ya Ifisi Mbalizi kwa siku tano baada ya kupigwa na walimu wanne kwa kosa la kukutwa katika mtandao wa Facebook.
   Baadhi ya Majeraha aliyoyapata maeneo ya miguu.
   Majeraha aliyoyapata mkononi.

  0 0

  Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es Salaam,(ZTO) ACP Awadhi Haji, akitoa elimu kwa madereva wa bodaboda waliopo Kituo cha Daladala cha Tegeta mapema leo hii,akiwataka wafuate sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu pamoja na abiria wao, kwani wasipovaa Kofia ngumu watachukuliwa hatua Kali zakisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani,vilevile akiwataka kutojihusisha  na vitendo vya kiarifu wakiwa na pikipiki zao, pia akiwataka madereva hao wawe wasafi pindi watoapo huduma kwa wananchi.
  Baadhi ya waendesha pikipiki maarufu kama waendesha bodaboda wakinyoosha mikono kumuuliza swali Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum ya Dar es Salaam,(ZTO) ACP Awadhi Haji leo katika kituo cha daladala cha Tegeta jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe (Pichani)kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2016.


  Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

  Dkt. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dodoma


  25 Julai, 2016.


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 
  Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki.
  Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya wanariadha hao.

  Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
  SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza  kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.

  Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.

  Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.

  Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.

  Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.

  Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1296 | 1297 | (Page 1298) | 1299 | 1300 | .... | 3285 | newer