Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1295 | 1296 | (Page 1297) | 1298 | 1299 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Jana Julai 23, 2016 Rais Dokta John Magufuli alichaguliwa kwa asilimia 100 kuwa Mwenyekiti mpya wa Taifa wa chama tawala CCM, na mtangulizi wake, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, kung'atuka rasmi. Ufuatao ni uchambuzi wa kina kuhusu mabadiliko hayo ya uongozi wa juu kabisa wa chama hicho kikongwe, hasa fursa na changamoto kwa Mwenyekiti mpya Magufuli. Karibuni

  0 0


  0 0

  Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Mageni waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama cha albino wilaya ya Mbinga, baada ya kukabidhi msaada wa mafuta yenye thamani ya shilingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Robert Mageni,akiteta jambo na mtoto mwenye ualbino ambaye hakufahamika jina lake mara moja wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ulamavu wa ngozi yaliyotolewa na chama cha albino wilaya ya Mbinga. 
  Sista Judith Mwageni wa shirika la mtakatifu Wiliam jimbo la Mbinga akiwatambulisha watoto wenye ualbino wanaolelewa na kanisa katoriki jimbo la Mbinga wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa ya ngozi yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga.
  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Magenj akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi mafuta maalum kwa watu wenye ualbino yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya Moshi,katikati ni katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya.
  Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya akitoa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ualbino jana wakati wa kukabidhi msaada wa mafuta wenye thamani ya shlingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo.Picha na Muhidin Amri.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

  Katika jitihada zake za kuongeza ufanisi na huduma bora, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limefungua ofisi za kanda katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Egid Mubofu (pichani) amewaambia waandishi wa habari jana jijini hapa kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa au kuuzwa kwa watanzania zinakuwa na ubora na viwango vinavyotakiwa.

  “Ofisi hizi zitafanya kazi kwa karibu na wazalishaji viwandani ili wananchi wapate bidhaa bora,” alisema na kuongeza kuwa watendaji katika ofisi hizo watakuwa wanafanya ukaguzi  viwandani na kushughulika na maombi ya wazalishaji wapya.

  Alisema ofisi ya mkoa wa Arusha itahudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Arusha yenyewe; Ofisi ya Mwanza itahudumia Kanda ya ziwa mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza yenyewe.

  Ofisi ya Mbeya itahudumia mikoa ya nyanda za juu Kusini ya Iringa, Songwe, Ruvuma, Njombe na Mbeya yenyewe.

  Dkt. Mubofu alisema kwa muda mrefu wazalishaji wa bidhaa viwandani walikuwa wakipata huduma makao makuu ya shirika Dar es Salaam na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa huduma.

  Alisema ofisi hizo zitafichua viwanda bubu vinavyo zalisha bila kufuata utaratibu.

  “Ilikuwa ni vigumu kwa shirika kugundua uwepo wa viwanda bubu katika maeneo ya mikoani na wilayani kwa urahisi kutokana na umbali lakini sasa kazi itafanyika bila kikwazo,”alisema.

  Pia shirika limefungua ofisi mipakani katika mipaka ya Mutukula, Kasumulo na Tunduma.  Awali ilisha fungua ofisi Holili, Horohoro, Sirari, Namanga na Rusumo.

  Alisema kwa upande wa bandari wamefungua ofisi katika bandari ya Mwanza na Mombasa na pia wamefungua ofisi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

  “Ufunguzi wa ofisi za mipakani unalengo la kupunguza miaya ya uingizaji holela wa bidhaa hafifu katika soko la Tanzania unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu,” alisisitiza Dkt. Mabofu.

  Akitoa mfano alisema ufunguzi wa ofisi katika bandari ya Mwanza na Mombasa utapunguza uingizaji bidhaa hafifu toka nchi jirani za Kenya na Uganda.

  Alisema shirika limejipanga vyema na kuwataka wananchi kushirikiana na ofisi za mamlaka nchini kufichua viwanda vinavyozalisha na wafanyabiashara wanaokiuka utaratibu.

  0 0
 • 07/24/16--03:21: YALE YALEEEE.......


 • 0 0

  Julai 23,2016 Taasisi ya Brigite Foundation imezindua mradi wa taa za solar katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuimarisha usalama katika kituo hicho ambacho sasa kina jumla ya watoto albino 220,wasiosikia 61 na wasioona 33.

  Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo mbali na uzinduzi huo wa mradi wa umeme mbadala,watoto katika kituo hicho walishiriki michezo mbalimbali pamoja na kula chakula cha pamoja na viongozi wa taasisi ya Brigitte Alfred Foundation na CSI Electrical Limited.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred alisema mradi huo mkubwa wa kisasa wa taa za sola utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa watoto hao katika kituo hicho.
  Brigitte ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2012 alisema baada ya kuguswa na hali iliyopo katika kituo hicho mwaka jana aliomba Kampuni ya Wakandarasi wa Umeme wa ndani -CSI Kusaidia kufunga umeme katika kituo hicho wakakubali na hatimaye leo mradi huo umezinduliwa.

  “Tunaushukuru uongozi wa CSI Electrical Limited kwa namna walivyopokea maombi yetu na hatimaye kuchukua hatua za haraka kwa kutoa msaada huu pia viongozi wa serikali na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ushirikiano wenu uliosaidia kukamilika kwa mradi huu”,alieleza Alfred.

  “Mradi huu umetimiza na kuunga mkono malengo ya Millenia namba 7 inayolenga upatikanaji wa nishati salama “Affordable and clean energy”,tunatarajia mradi huu utahamasisha na kuchochea ari ya wanafunzi katika elimu ya mazingira na matumizi ya nishati mbadala na watawawezesha kusoma na kushiriki kwa vitendo katika kufikia malengo ya kitaifa na ya kidunia kama kizazi na viongozi wa kesho”,aliongeza.
  Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kuunga mkono juhudi za serikali na kusimamia kauli mbiu ya pamoja ya kuhimiza amani,upendo na kutokomeza kabisa matukio maovu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na kuifanya Tanzania endelee kuwa mahala pazuri na salama pa kuishi.

  Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa alisema wamefunga Panel 13 na mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 75.88.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Baadhi ya wanafunzi tuliosoma Shule ya Sekondari Bwawani tukiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuelekea kuitembelea shule yetu hiyo..

  Na Josephat Lukaza - Bwawani
  Hatimaye waliowahi kusoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani wamefanikisha adhma yao ya kuitembelea iliyokuwa shule yao kwaajili ya Kuwatia moyo na amasa vijana wanaoendelea na masomo katika shule hiyo huku wengi wao wakiwa ni vijana wa kidato cha Kwanza hadi cha Nne.

  Waliowahi kuwa wanafunzi hao waliwasili majira ya saa sita mchana na kupokelewa na waliokuwa walimu wao kipindi hiko wakiwa wanasoma shule hapo na kupata nafasi ya kuonyeshwa sehemu mbalimbali za shule hiyo huku waliokuwa wanafunzi katika shule wakipata nafasi pia ya Kuzungumza machache na wanafunzi wanaoendelea na masomo katika shule hiyo na kuweza kuwasaidia vifaa vya michezo kama mipira huku wakipanda miti kwaajili ya kumbukumbu.
   Mwalimu Leornad Chintowa akiwakaribisha baadhi ya wanafunzi waliopata kusoma katika shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi la Magereza nchini mara baada ya kuwasili kwa waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo mapema leo.

  Waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini waliweza kutoa miche 30 ya miti kwaajili ya kupandwa shule hapo huku wanafunzi wakishukuru kwa kupokea mipira kama zawadi kutoka kwa kaka na dada zao waliotangulia shuleni hapo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Dar es Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imetangaza kubadilisha huduma yake ya fedha ya M-Pesa kutoka teknolojia ya awali ya G1 kwenda mpya ya G2, lengo kubwa ikiwa ni kuboresha huduma hii kwa kuiingiza katika teknolojia ya juu ili iweze kupatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanyaji wa mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.

  Matumizi ya teknolojia mpya ya G2 ambayo miundombinu yake imejengwa hapa nchini itarahisisha matengenezo yake pindi yatakapojitokeza matatizo ya kimtandao pia itawezesha kupanuka kwa matumizi ya huduma hii kwenye kuboresha na kuunganisha  huduma mbalimbali na kibiashara.
  Akiongea wakati wa uzinduzi wa matumizi ya teknolojia hii mpya katika hafla iliofanyika leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa huduma za malipo ya mtandao wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit amesema “Tunawaletea huduma ya M-pesa katika teknolojia mpya na bora zaidi,tunajivunia kwa kazi  nzuri iliyofanyika kufanikisha mabadiliko haya ambayo yatawawezesha watanzania kupata huduma bora za kifedha kupitia huduma ya M-Pesa iliyoboreshwa zaidi.Ubunifu na matumizi ya teknolojia hii mpya yataboresha huduma hii sio kwa wateja wa Vodacom pekee bali biashara mbalimbali na huduma zinazofanyika kupitia huduma hii”
  Sitoyo aliongeza kusema kuwa teknolojia hii  italeta mapinduzi makubwa ya matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu na Vodacom itaendelea kujenga mazingira ya kukuza biashara za malipo kwa njia ya mitandao na kuzidi kuiweka Tanzania mbele katika huduma za biashara kwa njia ya mtandao pia kuongeza wigo wa huduma za kimtandao kama vile kuweka akiba,kuchukua na kulipa mikopo,ufanyaji wa mihamala ya malipo kwa mtandao,huduma za bima na huduma nyinginezo nyingi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang alisema “Kupitia teknolojia ya kiwango cha juu ya Huawei,Huduma za M-Pesa zimebadilika kabisa na kuwa za kiwango kikubwa cha ubora na imeboreshwa zaidi kuweza kukidhi matakwa ya huduma mbalimbali za kifedha.Kwa kutumia timu ya wataalamu wetu tumeweza kujenga miundombinu ya kisasa itakayowawezesha watanzania kupata huduma za kifedha kwa viwango vya kimataifa.Tumefurahishwa na ushirikiano tulioupata kutoka timu nzima ya wafanyakazi wa Vodacom hali iliyotuwezesha kumaliza mradi huu wa kubadilisha teknolojia mapema tofauti na jinsi tulivyotegemea” 
  Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ikiwa ni ya kwanza kwa kutuma , kupokea fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo inaaminika kwa watanzania wengi.Tangia ianzishwe katika kipindi cha miaka 8 iliyopita inao watumiaji wapatao milioni 9.Kupitia teknolojia hii mpya ya G2,huduma za M-Pesa zimeboreshwa kuwa nzuri na  ubunifu wa kutumiwa kwa malipo,  huduma mbalimbali na kuwa na uwezo wa kuunganisha biashara .Mabadiliko haya ni ya kihistoria katika huduma za kifedha kwa njia ya simu nchini Tanzania na kampuni inawahaidi watumiaji wategemee ubunifu wa kila aina kwa matumizi ya huduma hii katika teknolojia hii  ambayo kuanza kwake kutumika nchini  ni mafanikio makubwa katika kuboresha huduma  za kifedha kwa watanzania . Vodacom Tanzania inajivunia kufanikisha kuleta teknolojia hii ambayo inategemewa kuleta  mapinduzi makubwa ya huduma za kifedha nchini.
  For English version CLICK HERE

  0 0


  Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.
  Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.
  Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwakubofya hapa. 
  Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia. 
  Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

  Imetolewa na

  Ofisi ya Katibu Mtendaji
  NACTE

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurgenzi, Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akiongea na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati alipokutana nao hivi karibuni Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo.
  Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akisistiza jambo mbele ya baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati wa kikao hicho Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba akieleza jambo mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu masuala ya sanaa nchini wakati wa kikao hicho Wizarani hapo jijini Dar es Salaam.
  (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)

  Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu nchini ikiwa ni sehemu ya kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakabili Mashirikisho hayo.

  Akiongea hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi alisema kwamba, Mashirikisho yanayounda Shirikisho la Filamu nchini hayanabudi kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kubaini changamoto na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Wasanii na Taifa kwa ujumla.

  Alieeleza kuwa, Wasanii wanapaswa kuzingatia maadili wakati wanapofanya kazi zao za sanaa ili waweze kujijengea heshima kwao, kwa jamii ambayo ndio mlaji wa kazi zao za kisanaa na kwa Taifa kwa ujumla.

  “Mnapofanya kazi zenu za sanaa, jitahidini kufuata miiko ya kazi zenu, tumieni vipaji vyenu vizuri kwa kufuata maadili ya Kitanzania, lakini pia jitahidini kuwainua wale wasanii wanaochipukia ama wale wadogo ili waweze kuwa na hamasa ya kuendeleza kazi zao za sanaa”, alisema, Bi. Kihimbi.

  Bi. Kihimbi aligusia suala la fursa ya kazi za sanaa inayodhaminiwa na Taasisi ya British Council Tanzania na kuwataka wasanii kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha kuwa kila msanii au kikundi kinaandika Pendekezo (Proposal) kuhusu fursa hiyo ili kujiwekea nafasi kubwa kwa wasanii wa Tanzania kushinda fursa hiyo na kuweza kupata fedha za kuendesha kazi za sanaa kulingana na wazo lililobuniwa.

  “Kuweni wabunifu katika hii fursa ili mje na wazo zuri ambalo litawawezesha kushinda hii fursa hasa hii ya nAnA (new Arts new Audiences) kwani inamhusu msanii mmoja mmoja au kikundi”, alisema, Bi. Kihimbi.

  Aliongeza kuwa, Serikali itajitahidi kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaonekana kuwa kero kwa wasanii nchini ikiwemo suala la wizi wa kazi za sanaa (Piracy) ambalo kwa sasa tayari Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye ameonyesha mfano kwa kukamata DVDs feki pamoja na mitambo ikiyotumika kudurufu kazi hizo za sanaa nchini.

  Kwa upande wake, Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alisema kwamba Bodi yake inashirikiana vema na wasanii nchini kwa kuzingatia Sheria za nchi pasipo kumuonea msanii yeyote na kuwataka wasanii kote kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

  Aidha, aliwataka viongozi wa Shirikisho hilo la Sanaa kuendelea na utaratibu wa kupeana taarifa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sanaa na kuwahimiza wasanii kupenda kujiendeleza kielimu ili waweze kumudu soko huku akiwasisitiza kuhakikisha kuwa kazi zao wanazotengeneza zinapata kibali cha Bodi kwa kuwekewa madaraja na zinakuwa na stika halali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuepusha uharamia wa kazi zao.

  Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba ameiomba Serikali kuendelea kushirikiana na Wasanii kwa karibu kwa kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo na ikiwemo suala la uharakishaji wa Sera ya Filamu kwani ndiyo kipaumbele chao cha kwanza, elimu ya namna ya kutengeneza filamu bora, usambazaji wa kazi zao pamoja na adui yao mkubwa ambaye ni uharamia wa kazi za sanaa.

  Ameishukuru Serikali kwa kuunda Sekta mpya ya Sanaa na kusema kuwa, Sekta hiyo itakuwa Mkombozi kwao kwani wanajisikia fahari kutambuliwa na kuwa na kitengo chao cha masuala ya kazi zao huku akiaahidi ushirikiano mzuri kwa sekta hiyo.

  0 0


  0 0

   Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya NMB, Edith Mwiyombela (kulia) akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM. Msanii nyota Nick Wa Pili akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.
   Mmoja wa wasilishaji mada kutoka Kampuni ya Bridge Tanzania Limited akiwaelekeza wanasemina namna nzuri ya kutumia baadhi ya vifaa vya 'printer' na matumizi mazuri ya wino wa mashine hizo.

  0 0


  Katika kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.

  Akizungumza na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
  Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

  Alisema pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi, jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

  "Kwa mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na wengine wamemaliza kidato cha nne," alisema Rose.

  Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa.

  1. BODI YA MAPATO (ZRB)
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 14 cha sheria ya Bodi ya Mapato  ya 1996, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Amour Hamil Bakar kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar. Bwana Amour Hamil Bakar anachukua nafasi ya Bwana Abdi Khamis Faki ambae anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
  Utezi huo unaanza tarehe 1 Agost 2016.

  Aidha kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 15(1) (A) cha sheria hiyo kama ilivyorekebishwa na kifungu 11 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2000, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Khadija Shamte Mzee kuwa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar. Bibi Khadija Shamte Mzee anachukua nafasi ya Bwana Hafidh Ussi Haji ambae uteuzi wake umefutwa.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.

  2.TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Tume ya Maadili ya Umma Namba 4 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Said Bakari Jecha na Bibi Sebtuu Mohammed Nassor kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai, 2016.

  3. BODI YA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 11(1)(a) cha Sheria ya Shirika la Magazeti  ya Serikali Namba 11 ya 2008, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Umi Aley kuwa Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.

  4. TUME YA UTANGAZAJI
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Tume ya Utangazaji ya Zanzibar Namba 6 ya 1997, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Dkt. Ali saleh Mwinyikai  kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.

  5. BARAZA LA SANAA NA SENSA YA FILAMU NA UTAMADUNI
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na utamaduni Namba 7 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Maryam Mohamed Hamdan kuwa mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 Julai 2016.

  6. BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Baraza la Mitihani la Zanzibar Namba 6 ya 2012, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Maryam Abdalla Yussuf kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Zanzibar.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.

  7. SHIRIKA LA VIWANGO LA ZANZIBAR (ZBS)
  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 8(2)(a) cha Sheria ya Shirika la Viwango la Zanzibar Namba 1 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua tena Profesa Ali Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango la Zanzibar.
  Uteuzi huo unaanza tarehe 25 julai 2016.

  0 0

  Imekuwa ni kawaida sasa kwa hawa Waendesha bodaboda kuendesha vyombo hivyo bila kuvaa kofia ngumu japo wanazo na wameziegesha tu kwenye usukani wao kama zionekanavyo picha hizi. Hiki ni kijipu upele kinachotakiwa kutumbuliwa kwa msumali wa bati.

  0 0
 • 07/25/16--02:47: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

   Rais wa Zanzibar, Dkt. Ally Mohamed Shein akizungumza katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa waliopigana vita ambayo hufanyika Julai 25 kila mwaka ikiwa kwa mwaka huu yanafanyika mjini Dodoma.
  Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe ya siku ya mashujaa mjini Dodoma leo.
  Sherehe za kumbukumbu ya siku ya mashujaa zinaendelea mjini Dodoma asubuhi hii mjini Dodoma.


   Taswira mbalimbali mjini Dodoma asubuhi hii ikiwa ni siku ya kuwakumbuka mshujaa waliopigana vita hapa nchini, ambapo kumbukumbu hii hufanyika Julai 25 kila mwaka.

  BOFYA HAPA KUONA LIVE

  0 0

  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufika katika ufukwe wa Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani mwishoni wa wiki, Wafanyakazi hao ikiwa ni utamaduni wao wa kila mwaka kutembelea sehemu mbalimbali kwaajili ya kufurahi pamoja, kujenga mahusiano mazuri wakati wa kazi pamoja na kunywa na kula pamoja.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango amesema kuwa  wameamua kupumzika pamoja, kula na kunjwa pamoja mwishoni mwa wiki kwaajili ya kujenga mahusiano mazuri wakati wa kazi ikiwa ni siku mhimu sana kwao ambayo hufanyika kila mwaka.

  Katika Mapumziko hayo ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City walikuwa na michezo mbalimbali ambayo walishiriki kama Mpira wa Mikuu kwa wote, Kuvuta Kamba, kukimbia na ndimu kwenye vijiko, Mpira wa wavu(Voleball) na kukimbia na Magunia.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City  mashindano wa timu mili za wafanyakazi hao zilipoanza kufuana katika mchezo uliochezwa mchangani katika fukwe za Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
  Kazi Kweli kwelii iiiiii........
  Hapa mwendo wa kukimbia huku wengine akiishiwa pozi la kukimbia na kugusa mchanga kwa viwiko vya mikono.

  0 0

   Msimamizi wa Ushauri na Utafiti (PSPTB), Amos Kazinza akitoa mada LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ugavi, Pindani Nyalile akiwa kwenye semina hiyo. Semina hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa watendaji wa MNH ili waweze kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi. Wakurugenzi na wakuu wa idara wa MNH wametakiwa kutoa haki wakati wa kutoa zabuni. Pia, wameshauriwa kutonunua bidhaa zilizopo chini ya kiwango. 
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akifuatilia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Jeremia akiwa katika semina hiyo LEO. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akisikiliza jambo kwenye semina hiyo.
                Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa idara wakiwa kwenye semina                                 hiyo ya siku tatu iliyoanza LEO katika hospitali hiyo.
  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

older | 1 | .... | 1295 | 1296 | (Page 1297) | 1298 | 1299 | .... | 3286 | newer