Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1294 | 1295 | (Page 1296) | 1297 | 1298 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Wawakilishi wa  wana- Chuo cha utumishi tawi la Singida  wakipeleka  mashuka 72 kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Singida leo tarehe 22/7/2016 ikiwa ni msaada wao waliojitolea kwa kuchangishana
    Bw. Ramadhani Marijani, kiongozi wa msafara wa wanaChuo cha utumishi tawi la Singida  akipeleka  mashuka 72 kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Singida leo tarehe 22/7/2016 ikiwa ni msaada wao waliojitolea kwa kuchangishana
   Wawakilishi wa Chuo cha utumishi tawi la Singida  wakiwasilisha mashuka 72 kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Singida leo tarehe 22/7/2016 ikiwa ni msaada wao waliojitolea kwa kuchangishana

  0 0

   Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akiwaonesha waandishi wa habari bunduki aina ya gobore walioikamata kabla ya kutumika kwa ujambazi wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uharifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha mkoani humo leo mchana.
   Kamanda Sirro akionesha simu walizokutwa nazo watu wanaodaiwa vinara wa kupora simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini.

   Na Dotto Mwaibale
  JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa 
  kuliingizia mapato Taifa ya sh.milioni 198 kutokana na zoezi la uhakiki wa silaha lililofanyika mapema mwaka huu.
  Jeshi hilo limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 14,107 kwa kipindi cha kuanzia Machi Mosi hadi Juni 30 mwaka huu, vile vile Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 1,065.
  Hayo yameelezwa leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na zoezi la kuhakiki wa silaha hizo.
  Alisema zoezi la uhakiki wa silaha lilihusisha mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni.
  "Idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa mikoa yote ni 11,602, na silaha zilizohakikiwa ni pistol 5,073, shotgun 4,707 na rifle 2,974," alisema.
  Kamishna Sirro alisema dosari ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo ni kama vile wamiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 70, na wengine kumili silaha za marehemu kinyume na taratibu.
  "Hawa kwa kweli hatukuwaruhusu waendelee kumiliki hizo silaha, hivyo tulibaki nazo na wale walioshindwa kuzilipia silaha zao kwa muda mrefu pia tulibaki nazo," alisema.
  Kamishna Sirro alisema kutokana na sababu hizo jumla ya silaha 66 walibaki nazo (kusalimishwa), ikiwa ni shotgun 36, rifle 10 na pistol 20.
  Katika operesheni maalumu iliyowezesha kukumata watuhumiwa sugu 1,065, Kamishna Sirro alisema watuhumiwa hawo walikatwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.
  "katika hawa tumefakiwa kuwakamata watengenezaji wa pombe haramu ya gongo wakiwa na lita 952 pamoja na mitambo mitatu, vile vile kuna wavutaji wa bangi na puli zao 277.
  "Matukio mengine ni pamoja na kukamatwa kwa kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari," alisema.
  Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu  kwa makosa ya uporaji  wa simu katika maeneo mbali mbali ya kinondoni, mtuhumiwa wa kwanza ni Richard Augustino 18 aliyekamatwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Coco Beach akiwa na Samsung yenye thamani ya sh. 500,000.
  "Wengine ni Abdalah Chande 36 aliyekematwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Magomeni Mapipa akiwa na simu 11 za wizi, na Abdalah Saidi 22 ambaye alikamatwa maeneo ya Mapipa julai 14 mwaka huu akiwa na pikipiki aina ya boxer ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya ukuporaji simu," alisema.   0 0
  0 0


  0 0

  Taarifa iliyotufikia usiku huu, inaeleza kuwa Askari mmoja wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyetambulika kwa jina la Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay Kinondoni Jijini Dar es salaam, ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

  Taarifa zaidi za zitawajia kadrizitakavyokuwa zikitufikia.

  0 0

  KANISA la Assemblies of God Tanzania (TAG) limewapatia pikipiki 400 waangalizi wa majimbo 33 nchini ya Kanisa hilo,ili kuwawezesha kufanikisha utekelezaji wa malengo makuu kumi ya dira ya maendeleo ya kanisa hilo,ili ifikapo mwaka 2018, utekelezaji wa malengo hayo yote yawe yamekamilika.

  Akizungumza kwa niaba ya waangalizi waliopokea usafiri huo wa pikipiki,Mchungaji Kalebi Patrick Maumbuka wa kanisa la TAG, Ikungi Mkoani Singida alisema usafiri huo wa pikipiki utawasaidia sana kutangaza neno la Mungu kwa haraka zaidi, kwani awali walikuwa wakitegemea usafiri wa mabasi ambayo yalichangia kuwakwamisha kufikisha ujumbe wa neno la mungu kwa wakati muafaka.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Bwana John Mtokambali (wa kwanza kutoka kulia) akimkabidhi mmoja wa waangalizi wa kanisa wa Mkoani Singida pikipiki kwa ajili ya kuwawezesha kutangaza neon la Mungu kwenye maeneo yao.

  Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG, Bwana John Mtokambali akihubiri neno la mungu kwa waumini wa kanisa hilo waliohudhuria kwenye hafla za kuwakabidhi vyombo vya usafiri vitakavyowasaidia kuharakisha kulifikisha neno la mungu.
  baadhi ya waumini wa kanisa la TAG wakiwa kwenye hafla ya makabaidhiano ya vyombo vya usafiri vya waangalizi wa makanisa nchini,sherehe hiyo ilifanyika mjini Singida.
  Jengo la Kanisa la TAG lililopo katika kata ya Mandewa, wilaya ya Singida mjini kulikofanyika hafla ya kuwakabidhi waangalizi wa makanisa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kuharakisha usambazaji wa neon la Mungu kwenye maeneo yao.Picha zote na Jumbe Ismailly

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utaliii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Ibrahimu Musa akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.


  0 0


  0 0


  0 0


   Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,akifafanua jambo wakati akisoma hotuba yake ya Mwisho katika kiti hicho.PICHA NA MICHUZI JR -DODOMA.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ratiba na miongozo mbalimbali kwa Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
  Sehemu ya Meza kuu kama ionekanavyo pichani tayari wamekwisha ingia ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Rais Dkt Shein pamoja na Mwenyekiiti mtarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
   Baadhi ya Viongozi wakuu wa Wastaafu wa chama cha CCM na Serikali kwa ujumla wakifuatilia yanayojili ukumbini .
   Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyekiti ambaye leo anaachia kiti hicho na kukabidhi kwa Mwenyekiti mpya Dkt John Pombe Magufuli,katika mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC),mkoani Dodoma.
  Mwanana mahiri wa nyimbo za Taarab kutoka kundi la Tot Plus Khadija Kopa akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
  Baadhi ya wageni waalikwa kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pia wanahudhuria mkutano huu Maalum wa CCM.Ambapo vyama vya siasa vipatavyo 12 vilialikwa na vyote vimefika katika mkutano huo isipokuwa chama cha CHADEMA.
  Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi ambapo leo mkutano Mkuu Maalum wa CCM unafanyika kwa ajili ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka kumi,Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhiwa kijiti hicho kutoka kwa Mwenyekiti ambaye anamaliza muda wake leo, Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete,mkutano huo unafanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Baadhi ya Wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi ambapo leo mkutano Mkuu Maalum wa CCM unafanyika kwa ajili ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka kumi,Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhiwa kijiti hicho kutoka kwa Mwenyekiti ambaye anamaliza muda wake leo, Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete,mkutano huo unafanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 07/23/16--02:30: CAF YAPATA MDHAMINI MPYA.

 • SHIRIKISHO la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.

  Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.

  Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.
  Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.

  Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon. Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.

  Total itakuwa mdhamini mkuu wa:
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika
  Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
  Super Cup ya Afrika
  Kombe la Mashirikisho
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
  Kombe la Futsal Afrika
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
  Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17.

  0 0

  Hapa ni kwenye Mataa ya Kinondoni Manyanya Jijini Dar.
  Hapa ni Kinondoni Morocco, Jijini Dar. Ukiangalia hiyo Mistari utabani kitu.

  0 0


  KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

  Mkwasa amesema Julai 26 atatangaza kikosi hicho kwa ajili ya kuingia kambini ambapo engo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.

  Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili.

  Taifa Stars mpaka sasa ina pointi moja wakati Chad ikijiitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.

  0 0

  Na  Zainab Nyamka,Glou ya Jamii.
  KOZI za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania sasa itaanza Julai 25, 2016 badala ya Julai 24, 2016 kama ilivyotangazwa hapo awali.

  Kozi hiyo itaanza moja kwa moja kwa waamuzi wenye Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) ambao kwa sasa idadi yao ni 18 na waaamuzi waandamizi ambao idadi yao ni 12.

  Itaanza kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa vipimo (physical fitness test) kwa kila mwamuzi chini ya wawezeshaji wa kozi hiyo kutoka FIFA.

  Wawezeshaji hao ni Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe. Waamuzi hao wenye Beji ya FIFA na wale wanaotarajiwa kuveshwa beji hiyo, wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam Julai 24, 2016.

  Baada ya vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016 kabla ya kuanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

  Mara baada ya programu hiyo, kozi itaendelea kwa waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa michezo kwa msimu wa 2016/2017 na kwamba wahusika wote watajigharamia gharama zote.

  Waamuzi hao wa ligi ya ndani wataripoti na kujisajili Kituo cha Dar es Salaam Julai 28, 2016 na na Julai 29, 2016 na Julai 30, watakuwa na kozi ya kitathmini kasi kwa kukimbia kabla ya Agosti 1 na 2, 2016 kuwa na semina darasani na mitihani wakati Agosti 3, 2016 kutakuwa na semina na mitihani kwa makamishna mbalimbali wa michezo ya mpira wa miguu.

  0 0

  Mwanamuziki kutoka Jamhuri wa Demokrasi ya Congo Koffi Olomide amesafirishwa kwenda mjini kinshasa kutoka Nairobi baada ya kukamatwa Ijumaa usiku.

  Olomide alisafirishwa na shirika la ndege la Kenya Airways, kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa tano unusu asubuhi.

  Mwanamuziki huyo alikuwa amekabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kuenea mtandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Ijumaa asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili.

  Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.

  Akiongea katika kituo cha televisheni ya Citizen, muda mfupi kabla ya kukamatwa, Olomide alijitetea na kusema hakukusudia kumshambulia mwanamke huyo.


  Alisema alikuwa ameingilia kisa ambacho aliamini ni mtu aliyetaka kumpokonya mmoja wa wachezaji densi wake pochi yake au kulikuwa na vurugu fulani.

  Olomide alikamatwa muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano katika kituo kimoja cha runinga jijini Nairobi.

  Mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinnet alikuwa ametoa taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua.

  0 0

   Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio zipatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.
  Mwenyekiti Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kumi.
    Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
   Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10,pichani katia anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete 
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.

  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
   Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa chama cha CCM mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho .


  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Kulia) Ndg Twalib A. Mbasha akitoa  hati ya makabidhiano ya Wilaya kwa Mkurugenzi wa sasa wa Halmashauri hiyo Ndg Zabron I. Bugingo.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg Zabron I. Bugingo (Kushoto) akipata Picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hio Ndg Twalib A. Mbasha. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bwana Abubakar Mussa Mjaka.
  Picha ya pamoja ya aliyekuwa Mkurugenzi na Mkurugenzi wa sasa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Pamoja nawakuu wa Idara/Wataalamu wa Halmashauri. Nyuma waliosimama wa katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri mwenye T-shirt. Picha na Bernad Mpangala.(Mchambuzi wa Mifumo Kilwa (W). 

  0 0


  0 0


  Na. Immaculate Makilika- Dodoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma.

  Amesema hayo leo, wakati alipokuwa akihutubia wajumbe wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.

  “Nitahakikisha katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

  Akiongelea maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka zaidi tofauti na miaka iliyopita.

  Aidha Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,

  Rais Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo litazalisha zaidi ya ajira 20,000.

  Vile vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na kuongeza kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa katika kutekeleza shughuli za maendeleo.

  Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000 ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398 kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.

  Rais Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya kupokea uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.

  0 0


older | 1 | .... | 1294 | 1295 | (Page 1296) | 1297 | 1298 | .... | 3286 | newer