Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BIA YA ASILI YA NZAGAMBA YAZINDUA PROMOSHENI YA AINA YAKE KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa waandishi wa habari Bia hiyo ya Asili inayopatika maeneo ya Kanda ya Ziwa, wakati uzinduzi wa Promosheni yake itakayowawezesha wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki. Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 19, 2016 kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo.
 Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo akionyesha moja ya maboksi yatakayotumika kwa washiriki wa Promosheni ya Bia hiyo ya asili ya Nzagamba itakayowawezesha wanywaji wake wa Kanda ya Ziwa kujishindia Ng'ombe kila wiki, wakati wa uzinduzi wa Promosheni hiyo, uliofanyika kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo.
Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa mfano namna ya kushiriki Promosheni hiyo ya Nzagamba. Wengine pichani ni Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo (aliebeba boksi), pamoja na Ma Meneja Usambazaji wa Bia ya Asili ya Nzagamba, James Makalla (kulia) na Peter Mwambenja.

WANANCHI WA KIJIJI CHA KISEGESE WILAYANI MKURANGA WAMEIOMBA SERIKALI IWAJENGEE BARABARA.

$
0
0
  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ametembelea shule ya msingi Kisegese,ambapo pia aliweza kuchangia sh.milioni moja katika uazishaji wake leo katika ziara ya kuwashukuru wananchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika 2015,leo Julai 18, 2016 katika Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani.
 Wananchi wa Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega.
 Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akiwasili Kijiji cha Kisegese wilaya Mkuranga mkoani Pwani.

MJUE NDULI IDDI AMINI DADA - MTOTO WA SANGOMA ALIYETIKISA DUNIA

$
0
0
Imeandikwa na Geofrey Chambua 
1. Mzaliwa wa Mwaka 1925 huko Kokobo Magharibi ya Jimbo la Mto Nile, Idd Amin Dada ni Rais wa tatu wa Uganda na yumkini Rais Pekee ambaye hakuna kumbukumbu zozote za shule aliyosoma kwani baada ya baba yake kuitelekeza familia yao, alilelewa na mama yake aliyekua 'mpigaramli' ama sangoma na ambaye hakuhangaika kumpeleka shule kwani muda mwingi alikua kwenye 'kamati ya ufundi'. Hii pia inatokana na ukweli kwamba hakuna popote alipowahi kuandika wala kuruhusu mtu yoyote kuandika juu ya historia ya maisha yake 

2. Nduli Amin alioa jumla ya Wake 6 na kupata watoto 40!!  mmoja ya wakeze alikutwa amechinjwa kinyama baada ya kubainika amechepuka na kuzaa nje ya ndoa. Fashisti Iddi Amini alikua analala na wake wawili kwenye kitanda kimoja kwa zamu (picha zipo)

3. Licha ya 'kutoenda shule' Amini alijiunga na Jeshi la Kikoloni la Mfalme (KAR) kama mpishi na kupanda hadi cheo cha juu kabisa cha Luteni ambacho ni Waafrika wawili tu walikifikia akiwemo yeye ni Milton Obote Rais wa Kwanza wa Uganda. Ikumbukwe hili lilikua jeshi la wazungu na Amin alipanda cheo kutokana na kupendwa sana na wazungu kwa kuwa alikua na vipaji vingi sana na hasa Ndondi  

4. Alijichagua na kujiapisha kuwa Rais wa Uganda baada ya Mapinduzi ya Kijeshi yaliyomuondoa Milton Obote mwaka 1971 na kuongoza kwa miaka nane hadi 1979 

5. Aliua zaidi ya Waganda LAKI TATU kwa kipindi cha miaka nane aliyodumu madarakani kabla ya kusambaratishwa na majeshi ya Tanzania mwaka 1979. Yasemekana Nduli Amin alikua akitafuna nyama za watu aliowaua kwa mkono wake mwenyewe huku vichwa vingine akiviweka kwenye jokofu. Japo inasemekana ni kwa imani za kishirikina  na kwa kuwa huyu bwana alikuwa mchawi na mganga kutoka kwa mama yake......Japo inasemekana ni kwa imani za kishirikina  na maagizo toka 'kamati yake ya ufundi'

6. Aliwahi Kuwatimua Raia wote wenye asili ya India na Pakistani mnamo mwaka 1972 akitaarifukwamba alitumiwa ujumbe na Mungu' akiwa ndotoni na kutaifisha mali zao zote. Yasemekana jumla yao wanaweza kufika kati ya 40000 hadi 80000

7. Alijipa vyeo kibao ikiwemo cha Field Marshal, AL HAJ, Doctor nk na ili kutimiza ndoto yake ya kuwa na vyeo vyote duniani na hasa cha Mfalme kamili, yasemekana alituma barua ya posa kwa Malikia Elizabeth II ili akamilisha vyeo vyote duniani kikiwamo cha UFALME-KING....

8. Aliwahi kuwa Bingwa wa Ndondi za uzito wa Juu nchini Uganda na alishika rekodi hiyo kwa miaka tisa kati ya 1951 hadi 1960
9. Licha ya historia ya maisha ya ukatili na udhalimu wa kutisha, Iddi Amini hajawahi kukamatwa wala kufikishwa kwenye mahakama yoyote hadi umauti wake katika Hospitali ya King Faisal Jedah mnamo mwaka 2003 nchini Saudi Arabia alikokua akiishi uhamishoni baada ya kuugua kwa muda mrefu 

10 Ingawa WAGANDA walisheherekea wakati Iddi Amini anaingia Madarakani, hao hao walisherehekea baada ya Amin kusambaratishwa na majeshi ya Tanzania kutokana na kumchoka kwa jinsi alivyotawala nchi kama nyumbani kwake na kupendwa kuabudiwa kama 'mungu mtu'

11. Funzo kuu aliloacha Iddi Amini mwishoni mwa uhai wake ni pale alipoacha wosia mzito kwamba mikono yake iwe inaonekana nje ya jeneza akimaanisha kwamba alikuja duniani hana kitu na anaondoka akiwa hana kitu na yote aliyoyafanya yamekuwa ubaitli na kujilisha upepo ....nukuu ambayo imedukuliwa na watu  kadha mashuhuri duniani.
.........Duniani hatukuja na kitu na hatutaondoka na kitu.........
Iddi Amini Dada

MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI(WHO), HAPA NCHINI AMALIZA MUDA WAKE, AMUAGA WAZIRI WA AFYA.

$
0
0
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini
Waziri Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora Dkt.Chatora amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya maji, mazingira pamoja na elimu.

Vile vile alishauri Serikali kuongeza nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na kuathiri jamii

amemshukuru kwa ushirikiano wake katika sekta ya afya tangu awepo nchini na ameahidi kuendelea kutekeleza yale yote aliyoishauri wizara
(Picha na Wizara ya Afya)

WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI ZA KANDA YA ZIWA ,WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO.

$
0
0
  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Seni Konda akifurahia zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.

DC MTATURU AKUTANA NA WAZEE WA WILAYA YA IKUNGI AWAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII

$
0
0

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh.Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na zaidi ya wazee 137 kutoka vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida. Katika mazungumzo ya mkuu huyo wa Wilaya na wazee hao yalijikita zaidi katika kujadili namna ya kukabiliana na umasikini kupitia nguvu Kazi ya Taifa (Vijana) katika kilimo na ufugaji wa kisasa. 
 
Dc Mtaturu amewasilisha dhamira ya serikali ya Hapa Kazi Tu chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Joseph Pombe Magufulu kwa wazee wa Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa ujumla ni kupambana na mafisadi, Rushwa na wahujumu uchumi ili kuboresha huduma za Jamii ikiwemo Afya hususani katika kuboresha huduma za Afya kwa wazee wote nchini sawia na Wanawake wajawazito na watoto. 
 
Katika kuhakikisha kunakuwa na chachu ya maendeleo kwaMapinduzikubwa Wilayani humo Mtaturu alisema kuwa serikali imekusudia kuboresha kilimo na ufugaji ili viwe vya tija na kibiashara na kupelekea kupunguza umasikini wa wananchi mwaka hadi mwaka. Mtaturu anakuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza kukutana na kundi la wazee Siku chache baada ya kuapishwa jambo ambalo halijawahi kutokea kwa kiongozi mwingine yeyote Wilayani humo tangu Mkoa wa Singida ulipoanzishwa. 
Kwa upande wao wazee hao wameonyesha wazi mapenzi yao ya dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya na kuahidi ushirikiano uliotukuka katika utendaji wake. 
 
Wakati huo huo wazee hao wamemshukuru Mh Rais Magufuli kwa uteuzi alioufanya kumpeleka Mkuu huyo wa Wilaya kuongoza wananchi hao ambao wameonyesha kukatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani humo ambao wameshindwa kutatua changamoto za wananchi. Awali Dc Mtaturu alikuwa na kikao cha mapema na watumishi wa Halmashauri na wakuu wa idara ili kukumbushana majukumu ya kila mmoja utendaji wake na kuwasihi kufanya Kazi kwa bidii zaidi kwa kushirikiana na wananchi.
 
Mtaturu amewakumbusha watumishi hao wajibu wao wa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kupata thamani halisi ya fedha (Value for Money) kushughulika na kero za wananchi ikiwemo kutafsiri ilani ya Uchaguzi kwa vitendo ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewapa muda wa mwezi mmoja watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanaoishi Singida Mjini takribani kilomita 41 kutoka Wilayani hapo wawe wamehamia Wilayani Ikungi kwani amebaini ni watumishi wanne pekee ndio wanaoishi Wilayani hapa jambo ambalo linapunguza ufanisi wa Kazi. 
 
Katika sekta ya michezo Mtaturu alisema kuwa ili kuibua vipaji na Mkoa wa Singida kwa muda mrefu umekuwa na Sifa ya kutoa wanariadha hivyo ili kuenzi heshima hiyo anataraji kuanzisha Ikungi Marathon ili kuwapa fursa Vijana wenye vipaji kuibuka na kufika mbali zaidi katika medani za riadha.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji J. Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee waliowawakilisha wazee wengine wilayani humo.

Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao.
Mtaturu akisikiliza kwa makini moja ya ushauri uliopatiwa na wazee baada ya kikao kumalizika

RC SHINYANGA AWAFUTA MACHOZI WANAFUNZI WALIOUNGULIWA BWENI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack akishirikiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese kugawa vyandarua kwa wanafunzi walioathiriwa na kuunguliwa kwa bweni katika Shule ya sekondari Shinyanga wilayani Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack akiwafariji wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shinyanga baada ya kuunguliwa bweni lao hivi karibuni alipokwenda kugawa misaada ya vifaa mbalimbali. Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu, Stephen Magoiga.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga, Mwalimu Marxon Paul akitoa taarifa fupi ofisini kwake kuhusu ajali ya moto iliyotokea shuleni kwake hivi karibuni na kusababisha kuungua kwa moja ya mabweni.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani, Shinyanga Nyabaganga Taraba akizungumza wakati wa kikao kifupi na viongozi mbalimbali ofisini kwa mkuu wa shule ya sekondari shinyanga kabla ya zoezi la kutoa misaada.

SOUTH AFRICAN RALLY DRIVER DIED IN TANZANIA AND NOT KENYA

$
0
0
 Tanzania Tourist Board (TTB) wishes to refute claim made by Cara Anna, an Associate Press for Miami Herald, a US based media house who on July 18th , 2016 wrote an article claiming that Mr. Guguleth Zulu, a renowned South African rally driver, died while trying to summit ‘Kenya’s Mt Kilimanjaro’.

We would like to correct this misleading information issued by Miami Herald, that Mt. Kilimanjaro is in TANZANIA and not in KENYA.
TTB has contacted Miami Herald and has demanded that they issue a correct statement via the same media channel they used to issue the misleading information about the location of Mt. Kilimanjaro, so as to put it clear to the International community that MT. KILIMANJARO IS IN TANZANIA.

Issued by:
MANAGING DIRECTOR
TANZANIA TOURIST BOARD
July 19 th , 2016

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI DKT. RIZIKI SHEMDOE AKAGUA UPOKEAJI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA MIUNDOMBINU YA SHULE YA SEKONDARI MDABULO WILAYA YA MUFINDI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe (katikati wa nne) akikagua upokeaji wa wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari mdabulo katika iliyoko Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Shule hiyo ambayo iko umbali wa km 45 kutoka mji wa Mafinga upande wa mashariki mwaka huu imeanza kufundisha programu za masomo ya kidato cha tano na sita katika mchepuo wa Sanaa HGK,HKL na HGL.
Baadhi ya wanafuzi wa shule ya sekondari mdabulo iliyoko wilayani Mafinga mkoa wa Iringa wakipata huduma ya maji safi katika eneo la shule hiyo ambayo ni ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana kwa “O – Level” na wasichana pekee kwa “A – Level”.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe (kushoto) akikagua uwepo wa madawati katika madarasa ya shule hiyo ambayo kwa mara ya kwanza imeanza kufundisha programu za masomo ya kidato cha tano na sita katika mchepuo wa Sanaa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe (katikati) akikagua mazingira na miundombinu ya shule hiyo akiwa ameambatana na viongozi wa shule hiyo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA: BARA LA AFRIKA BADO LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hasa vijijini kwa sababu nchi zake bado hazijamudu kuunganisha huduma hiyo katika maeneo hayo.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa masuala ya maji watafute njia sahihi itakayowezesha kutatua tatizo hilo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoko.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2016) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW) ambao unaokwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.

“Tunategemea baada ya kumazika kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya kumaliza tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili kufikisha maji kwa wananchi,” alisema.

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania alisema, suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali usiozidi mita 400.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya masuala ya maji Barani Afrika alisema maji ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi, hivyo wataalamu wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika katika maeneo yote.

Mkutano huo wa siku tano unahudhuriwa Mawaziri wa Maji kutoka nchi 45 za Afrika na unaongozwa na Waziri wa Maji na Mazingira wa Senegal Amadou Mansour Faye ambaye ni Rais wa AMCOW.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, JULAI 19, 2016.
  

WAZIRI MKUU MAJALIWA: MALIASILI NA UTALII JIPANGENI VIZURI

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii
kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa.“Eneo la misitu limekuwa na matatizo makubwa, watendaji wengi si waaminifu na sura ya wizara si nzuri miti mingi inakatwa na fedha haiingii Serikalini. Huu ni mgogoro mpya,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi wa wizara hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2018) jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.Alisema lengo la mkutano huo ni kukutana na watumishi kusikiliza changamoto zao, kukumbushana wajibu, pamoja na kutoa maagizo ili  yatekelezwe kwa utaratibu unaokubalika kisheria.

Alisema mtumishi ambaye atabainika kuwa haitendei haki nafasi yake kwa
kutokutimiza majukumu ipasavyo hana sababu ya kuwepo kwa sababu serikali inapoteza fedha nyingi kuwalipa watu wasio na tija. Waziri Mkuu alisema sababu inayoikosesha Serikali mapato ni uwepo wa watumishi wasio waadilifu kwenye ofisi za Serikali ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii hivyo kuna umuhimu wa kuzisafisha.

Alisema kuna uvunaji mkubwa wa misitu kuliko upandaji huku asilimia 50 ya mapato yatokanayo na uvunaji huo yanapotea na kuisababishia Serikali hasara ambapo alihoji sababu ya wizara kushindwa kusimamia jambo hilo. Katika hatua nyingine; Waziri Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa mazao ya misitu kwenye barababara mbalimbali baada ya kukosa tija kutokana na upotevu wa misitu unaotokea kila siku.

Alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini  kuanzia Dar es Salaam ambapo alisema ina vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa. “Vizuizi vya katikati ya safari havina umuhimu na badala yake kuwe na vizuizi mwanzo na mwisho ili rasilimali zingine zitumike kuongeza nguvu na umakini wa ukaguzi kwenye vituo vichache vitakavyosalia,”.

“Kwa mfano ukitokea Ikwiriri kuja Dar, kuna vituo vya ukaguzi wa maliasili
visivyopungua sita, kuna Ikwiriri, Kibiti,  Jaribu Mpakani,Mkuranga, Vikindu  kote huku wanakagua lakini linapofika kituo cha mwisho cha Mbagala linakutwa na makosa kwenye mzigo kwanini’’?

“Yule mkaguzi wa kwanza alifanya kazi gani? Kuna tatizo la uadilifu na
ninyi ni mashahidi, sasa naagiza ongezeni nguvu kwenye vituo vikuu vya
ukaguzi yaani mwanzo na mwisho,” alisema. Aidha alisema ni muhimu kukawa na mabadiliko kwenye mfumo wa mauzo ya misitu kutoka wa sasa (kuuza kwa eneo) na kuhamia kwenye mfumo wa mnada ambao utaongeza mapato ya Taifa na utaweka uwazi.

Pia aliwataka watumie mashine za malipo za kielektroniki (EFD),wanapofanya mauzo ya mazao ya misitu ili
kuepusha matumizi ya daftari na risiti bandia ambazo hazitambuliwi na
wizara.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

JUMANNE, JULAI 19, 2016

WANAFUNZI 382 NDIO WANA SIFA YA KUSOMA STASHAHADA YA UALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATI WANAFUNZI 7,805-WAZIRI NDALICHAKO

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi habari juu ya hatua ya serikali waliochukua kwa wanafunzi waliondolewa katika chuo kikuu cha Dodoma leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Katibu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, Kulia ni Kamishina wa Elimu wa Wizara hiyo, Eustella Balamsesa.
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BAADA ya Serikali kufanya uchambuzi wa sifa za Wanafunzi wanaostahili kusoma program maalum ya Ualimu wa sekondari kwa masomo ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),ni wanafunzi 382 ndio wamekidhi kusoma program hiyo kati ya wanafunzi 7,805 waliondolewa katika mgomo wa walimu wa chuo hicho.

Akizungumza na waandishi habari Ofisini kwake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa wamefanya uchambuzi huo ili kutoa haki kwa watu wenye sifa ya kusoma program maalum kwa walimu wa sekondari .

Amesema kuwa vigezo vya wanafunzi hao kusoma ilikuwa ni ufaulu wa masomo ya sayansi kwa daraja C-A ambapo ni wanafunzi 382 ndio wameonekana na sifa hizo kati ya wanafunzi 6595 waliodahiliwa stashahada maalumu ya walimu wa sekondari .

Amesema wanafunzi 52 walipata daraja la nne katika matokeo ya kidato cha sita ambapo ni kinyume cha matakwa stashahada maalumu ya walimu wa sekondari .Amesema kuwa wanafunzi 1,210 walidahiliwa kimakosa kutokana kundi hilo ni walimu wa shule ya msingi ambao hawako katika program maalumu ya walimu wa sayansi.

Profesa Ndalichako amesema kuwa wanafunzi 4,586 wa mwaka wa kwanza program maalum ya stashahada ya walimu wa sekondari wamekidhi vigezo vya ufaulu lakini sio kwa masomo ya sayansi watahamishiwa katika vyuo vya serikali vya ualimu ambavyo ni ,Morogoro ,Butimba, Mpwapwa ,Songea, pamoja na Tukuyu kuendelea na masomo yao huku wanafunzi wa 1,337 wa mwaka pili wanahamishiwa katika vyuo vya ualimu wa shule ya msingi ambavyo ni Korogwe na Kasulu na watajighramia na huku wanafunzi 290 hawana sifa kabisa ya kusoma na wizara kuwataka waombe mafunzo ya sifa zinazolingana.

Amesema wanafunzi 29 watahamishiwa kusoma mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi katika chuo cha Kasulu kwa gharama zao huku 1181 wametakiwa kuomba mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi katika chuo chochote kwa gharama zao. 

BAADA YA COPA AMERICA NA EURO 2016 SASA TWAELEKEA RIO 2016 OLIMPIKI.

$
0
0
Mara nyingi tumezoea kuangalia michezo fulani ikifanyika mahali fulani, mfano mwezi huu na mwezi uliopita tulishuhudia mashindano ya kabumbu ya Amerika ya kusini na yale ya Ulaya pia mashindano ya dunia ya riadha.
Lakini hivi sasa macho na masikio ya wapenda michezo duniani kote yataelekezwa jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil ambako michezo ya OLIMPIKI itafanyika.

Michezo ya Olimpiki ni mashindano ya mkusanyiko wa michezo mbali mbali yanayofanyika pamoja (jiji moja) kila baada ya miaka minne.Baadhi ya michezo hiyo ni Mpera wa miguu,Mpira wa kikapu,Mpira wa magongo,Riadha, Ndondi,Judo,Kuogelea,Sarakasi nk.Michezo ya mwaka huu itajumuisha Nchi zipatazo 206,Michezo takribani 42 itashindaniwa katika viwanja 37 kwa matukio 306.Michezo hii inatazamiwa kuanza Agust 5-21/2016.

Pia michezo hii huwa na kitu tofauti sana na michezo mingine,kitu hicho ni MWENGE wa Olimpiki,Mwenge huu huwashwa na kuzungushwa katika baadhi ya nchi kwenye mabara yote matano ya dunia ili kusisitiza umoja ma ushirikiano.Ukiangilia nembo ya Olimpiki utaona ina viduara vitano vilivyoungana,ikiwa na maana ya mabara matano ya dunia.

Usikose kujumuika nasi kesho ambapo tutakuletea utamu mwingine kuelekea michezo hii,kidokezo ni kuwa Nani mwanzilishi wa michezo hii,ilianzishwa lini na wapi?

MADIWANI WA KYERWA NA BIHARAMULO MKOANI KAGERA WAPEWA SOMO LA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0

Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Magdalena Katunzi akiwasilisha mada ya uzimamizina Udhibiti wa fedha katika Mamlaka za serikali za mitaa. Mada hiyo ilitolewa kwa madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Kyerwa na Biharamuo Mkoani Kagera leo.
Lengo kuu la mada hiyo kwa Madiwani ahao ambao halmashauri zao zimechaguiwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma ni pamoja na kumuwezesha Diwani kupata taarifa na uweewa juu ya taratibu za usimamizi na udhibitiwa fedha katika Mamlaka za Serikali za mitaa.

Aidha Katunzi alianisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mapato vya Mamlaka za serikali za Mitaa, ikiwa ni mapato ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu na Mikopo. Madiwani walifundishwa mbinu za kuongeza mapato ya Hamashauri ambapo walifundishwa namna ya kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, kuboresha viwango vya tozo, kuboresha mbinu za ukusanyaji mapato, kusimamia matumizi ya fedha za serikali ya mitaa na udhibiti wa fedha za Halmashauri. Source:Father Kidevu Blog,Kagera

Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.
Wakuu wa Wiaya za Kyerwa na Biharamulo mkoani Kagera, Kanali Mstaafu, Shaabn Lissu (kushoto) wa Kyerwa na Saada Malunde wa Biharamulo wakiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Ng'ahala (kulia) wakifuatilia mada hiyo.

Serikali na British Council Tanzania zashirikiana kuwapiga msasa Mashirikisho ya Sanaa kuhusu Fursa ya Sanaa ya Afrika Mashariki.

$
0
0
Serikali na British Council Tanzania yawapiga msasa Mashirikisho ya Sanaa namna ya kuandika Mapendekezo ya Mradi wa Fursa ya Sanaa ya Afrika Mashariki. 

SERIKALI kwa kushirikiana na British Council Tanzania imekutana na baadhi ya Viongozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirikisho mbalimbali ya Sanaa nchini na kuwapatia elimu juu ya namna ya kuandika Mapendekezo (Proposals) za Mradi wa kuwania fursa ya sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania.

Elimu hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Bi. Leah Kihimbi lengo likiwa kuwahamasisha wasanii kote nchini kuchangamkia fursa hiyo inayodhaminiwa na Taasisi hiyo yenye Makao yake Makuu nchini Uingereza.

Awali akieleza kuhusu fursa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge amesema kwamba fursa ya sanaa kwa Wasanii zinahusisha sehemu tatu ikiwemo fursa ijulikanao kama nAnA (new Arts new Audiences) ambayo ndiyo imefunguliwa kwa sasa na baadaye fursa nyingine mbili za Creative Hustle pamoja na Mobility East Africa zitafuata.

Ameeleza kuwa kuhusu vigezo vya kujiunga na fursa hiyo ni pamoja Wasanii kuwa na umri kuanzia miaka 18-35, kuwa na Ushirikiano (Partnership) katika ya nchi tano zinazohusisha fursa hiyo, kuwa na Kampuni binafsi au ya Shirikisho, fursa inahusisha fedha ya uandikaji wa Pendekezo (Proposal) zitakazotolewa ni kuanzia paundi 2,000 hadi paundi 20,000 pamoja na kuwa na akaunti namba katika benki fulani.

Amefafanua kuwa, fedha zitakazotolewa na British Council Tanzania sio za mkopo bali ni kwa ajili ya wasanii wote ambao watafanikiwa kuwania fursa hiyo ambapo kwa sasa amesema kwamba wanaanza na fursa ya nAnA, hivyo amewahimiza wasanii nchini kupitia mmoja mmoja pamoja na Mashirikisho yao kuanza kuandika mapendekezo ya kuomba fursa hiyo kwa kujaza fomu ambayo inapatikana katika tovuti ya www.britishcouncil.or.tz

Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge (kulia) akiwaelekeza baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania pamoja na Wadau wa masuala ya Sanaa kuhusu Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na Taasisi hiyo, 19 Julai, 2016 jjijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leha Kihimbi (kulia) akiwasisitizia baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania pamoja na Wadau wa masuala ya Sanaa kuhusu umuhimu wa Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na Taasisi hiyo, 19 Julai, 2016 jjijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge (wa pili kushoto waliokaa mbele) akiwaelekeza baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania pamoja na Wadau wa masuala ya Sanaa kuhusu Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na Taasisi hiyo, 19 Julai, 2016 jjijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ashiriki maadhimisho miaka 59 ya Aga Khan kuongoza Ismailia

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba (Mb.), akizungumza katika maadhimisho ya Miaka 59 ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Shia Ismailia, Mtukufu Aga Khan tangu aliposhika nafasi hiyo.Katika hotuba yake Dkt. Kolimba alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mtukufu Aga khan kwa mafanikio katika kipindi cha uongozi wake na kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo iliyochini ya Taasisi yake. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Ismailia hapa nchini, Bw. Amin Kurji. 
Mhe. Dkt. Kolimba na Bw. Kurji wakiwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mtukufu Aga Khan wakati wa hafla hiyo. 
Dkt. Susan Kolimba akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam aliyebuni mchoro waa Chuo Kikuu cha Aga Khan kitakachojengwa Jijini Arusha. 
Picha na Reginald Philip 
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo nao wakimsikiliza Dkt. Kolimba, wa pili kutoka kulia ni Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshinda. 
Wageni waalikwa . 

GESI YA MAJUMBANI KUAGIZWA KWA PAMOJA.

$
0
0

Na Rhoda James

Imeelezwa kuwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu Serikali itaanza Uagizaji wa Pamoja wa Gesi inayotumika Majumbani (LPG).

Hayo yalielezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo mwazoni mwa wiki wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa mwaka 2016 kuhusu masula ya Gesi ya Mitungi inayotumika majumbani kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Dkt. Pallangyo alisema kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kupata uzoefu kutoka kwa nchi zilizoendelea na pia kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazokabili sekta hiyo ikiwemo usambazaji, usalama na ujazaji wa mitungi hiyo.

Aliongeza kuwa, Uagizaji wa gesi hiyo ya mitungi (LPG) utafanywa kwa Pamoja lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kodi ya serikali inakusanywa ipasavyo kutoka kwenye Sekta hiyo na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawamiliki soko hilo.

“Bei ya gesi ya mitungi inayotumika majumbani ni ghali, upatikaniji wake ni mgumu na pia haipatikani kwa mitungi midogo zaidi ambayo kila mwananchi wa kawaida anaweza kumudu,” alisema Pallangyo

Aliongeza kuwa, nishati hiyo inaleta ushindani ukilinganishwa na mafuta ya taa, na kutolewa mfano kuwa mafuta ya taa yanapatikana kwa urahisi na kwa viwango tofauti ambavyo mwananchi wa kawaida anaweza kununua kulingana na uwezo wake tofauti na ambavyo gesi inapatika na kwenye maduka makubwa na kwa bei ya juu. Na kuongeza kuwa ni vema gesi hiyo ya mitungi (LPG) ikapatikana kwa viwango vya kununulika na kwa bei nafuu.

“Ni vema wafanyabiashara wakubwa wa gesi hii ya mitungi (LPG) wakashirikiana na wafanyabiashara wadogo ili kukabili changamoto zilizopo kwenye sekta hii. Pia waangalie wapi kuna fursa hasa upande wa Afrika,” alisema Pallangyo.

Aidha, Dkt. Pallangyo alisema kuwa gesi hiyo ni muhimu kutokana na fursa nyingi na usalama wake, kutokana na utafiti wa Shirika la Afya Dunia (WHO) uliofanywa kuwa ikiwa nusu ya watu duniani wataitumia gesi hii ya mitungi (LPG) wataokoa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 900 kwa karne ijayo.Pia, aliongeza kuwa utumiaji wa gesi hiyo ya mitungi imekua kwa kiasi kikubwa na kusema kuwa mwaka 2010 hadi 2011 tani 2,225 zilitumika ikilinganishwa na 2014 hadi 2015 tani 5,762 zilizotumika ongezeko ambalo ni kubwa.

Mkutano huo ulishirikisha washiriki kutoka nchi 33 mbalimbali wakiwemo waoneshaji (Exhibitors) kutoka sehemu mbalimbali duniani na ulifadhiliwa na kampuni za Oryx gesi na Hexagon Ragasco.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo wa pili kutoka kulia akiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Michael Mjinja wa nne kutoka kulia pamoja na wadau wa gesi ya mitungi inayotumika majumbani (LPG) kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa Afrika 2016 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo anayeelezea jambo, akiwa pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Michael Mjinja wakiwa katika maonesho ya gesi hiyo ya mitungi inayotumika majumbani (LPG) 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiwa katika banda akipata maelezo kutoka kwa wadau wa LPG. Wengine katika picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

TAFF yaipongeza Serikali kwa juhudi za kupambana na Uharamia wa kazi za sanaa nchini

$
0
0
CHAMA cha Wasambazaji wa  Filamu Tanzania  na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) vimepongeza hatua iliyochukuliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia waziri wake,Nape Nnauye katika kuhakikisha wanatokomeza waharamia na uuzaji wa kazi za wasanii bila kufuata utaratibu za kisheria zilizowekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu,alisema kuwa hatua ya serikali imekuja katika muda muafaka kufuatia kilio cha muda mrefu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara na wasambaji wa filamu na muziki kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingiza na kuuza bidhaa hizo bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kulipa kodi.

Amesema kuwa wafanyabiashara hao pia wamekuwa wakidurufu filamu za ndani ya nchi na kuziingiza sokoni bila ya wasanii kunifaika na kazi zao ikiwemo kazi hizo kutolipiwa kodi hivyo kupelekea kuziuza kwa bei ya chini ukilinganisha na filamu hapa nchini jambo ambalo linasababisha soko la filamu za ndani kudidimia.

Aidha Mwanyilu ameongeza kuwa  baada ya kilio cha muda mrefu hatimaye wameona jitihada za serikali kupitia kwa wizara inayohusika na masuala ya sanaa kuanza kuchukua hatua za makusudi kufanya oparesheni ya nguvu ya kukamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini katika maeneo ya kariakoo.

Kwa niaba ya chama cha wasambazaji wa filamu na shirikisho la filamu Tanzania na vyama vyote vya shirikisho wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa wizara ya habari kupitia waziri wake,Nape Nnauye kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),Bodi ya filamu,Cosota na Baraza la Sanaa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kazi za wasanii nchini zinauzwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na unaotambulika.
 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifamba,akizungumza na waandishi wa habari,Dar es Salaam,leo kuhusu kuipongeza serikali kupitia wizara husika katika kuanzisha oparesheni ya kuwakamata walanguzi wa kazi za wasanii nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu nchini,Moses Mwanyilu,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo wa kwanza kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifamba.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza mwenyekiti wa chama cha wasambaji wa filamu nchini,Moses Mwanyilu (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu wizi wa ulanguzi wa kazi za wasanii nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB YAIPIGA JEKI TANZANIA DOLA MILIONI 200

$
0
0
Na Benny Mwaipaja-WFM 

BENKI ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, imeahidi kuchangia Dola Milioni 200, sawa na Shilingi 433.6b, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2016/2017. 

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es salaam 

Makamu huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia Dola Milioni 150. "Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa serikali ya Tanzania imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa" Alieleza Dkt. Kacou 

Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahili ya maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo. "Tuna malengo matano ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula, kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla" aliongeza Dkt. Kacou 

Amepongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi. Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS). 

Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga. 

"Vilevile tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini" Aliongeza Dkt. Mpango 

Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. "Mpango huo utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda vitapata malighafi ya kutosha" alisisitiza Dkt. Mpango 

Amerejea msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada inayoambatana na masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta maendeleo. 

"Hatutakubali misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe" alieleza Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii. 

Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. 
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha shilingi 433.6bn.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero, alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto), akimsikiliza kwa makini  Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI INAPOTEZA SH.BILIONI 18 KUTOKANA NA KUKOSA RADA.

$
0
0
SERIKALI inapoteza shilingi bilioni 18 kutokana na kukosa rada za kuongezea ndege na kufanya nchi ya Kenya ipate mapato hayo kwa kuwa rada.

Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA), amesema kuwa kutokana na Serikali kukosa mapato wameagiza rada mbili ambazo zitagharimu dola za Kimarekani Milioni 24.

Ngonyani amesema kuwa rada hizo mbili zitafungwa nusu ya anga la Tanzania ambazo zitafanya serikali ya Tanzania kupata fedha kutokana na ndege zitazotumia mawasiliano ya Rada kulipia ambapo kwa sasa hatuna uwezo huo.

Amesema kuwa katika mkutano huo shirika la ndege Presion ndio mwanachama wa IATA huku Shirika la Ndege za Serikali (ATCL) likikosa sifa kuwa mwanachama kutokana ndege zake kushindwa kukidhia vigezo vilivyowekwa.

Ngonyani amesema kuwa kutokana na mkakati wa serikali kwa sasa wanatarajia kununua ndege mbili za kisasa na baadae kuongeza ndege zingine katika kutoa huduma ya wananchi na kwenda hadi nje ya Afrika.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari amesema kuwa wanaendelea katika kuboresha huduma za anga.
Imeandaliwa na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza katika mkutano wa kwanza wa wamiliki wa ndege wa Afrika mashariki na na Afrika kwa ujumla (IATA) jijini Dar es Salaam. Pia katika mkutano huo wanaanalia changamoto mbalimbi katika sekta ya usafiri wa Anga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wa wadau na wamiliki wa ndege wakiwa katika 
Mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) ulioanyika leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images