Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1288 | 1289 | (Page 1290) | 1291 | 1292 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dk.Hamis Mwinyimvua (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa.

  Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.


  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

  Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu. Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.

  Dkt. Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

  “Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza ushiriki katika uwekezaji unaochochewa na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari ambao utaweza kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.

  Aidha alisema kuwa kutokana ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu, Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema kuwa katika kongamano hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na halmashauri za Miji na Majiji.

  Akizungumzia kuhusu manufaa ya kongamano hilo, Beng’i alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa wataongeza ujuzi na uzoefu katika kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta za mafuta, gesi, kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.


  0 0


  Mmoja wa washindi wa Tusker milionea Albert Tarimo (kulia) akijadiliana jambo na fundi wa matofali Emmanuel Mboya (kushoto) ambayo aliyonunua kwa kutumia Milioni moja aliyoipata kutoka promosheni Tusker .
  Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile(kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi walioshinda katika droo ya nane ya promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, kushoto kwake ni afisa kutoka Bodi ya michezo ya kubahatishanchini Mrisho Millao akihakiki taarifa za mshindi.

  Ikiwa imebaki wiki moja tu kukamilisha wiki kumi za promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini, mwishoni mwa wiki ilichezeshwa droo ya nane ya promosheni hiyo huku washindi wengine kumi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakitangazwa kujishindia vitita vya shilingi Milioni moja kila mmoja. 

  Hii inafanya idadi ya washindi kufikia 90 tangu promosheni hiyo ianze wiki tisa zilizopita. Droo hiyo iliyofanyika katika studio za ITV na kushuhudiwa na wakaguzi wa wahesabu na Maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini kuhakikisha droo imechezeshwa kwa kufata taratibu na masharti elekezi yaliyowekwa.

  Washindi wa droo ya 8 ya Tusker Fanya Kweli Uwini ni :- God Muingi na Yohana Shirima kutoka Morogoro, Boniface Masanja na Selestin Simon kutoka Mwanza, Evarist Simwita kutoka Kilimanjaro, Obwor Nyambade kutoka Arusha, Rose Moses, Juliana Petro, Innocent Kiwango na Ally Mkemi kutoka Dar es Salaam.

  “Tayari tumeshatoa 90,000,000 kwa watanzania na watumiaji wa bia ya Tusker, ni Milioni kumi tu ndo imebaki kwaajili yako wewe mteja wetu ili kukamilisha Milioni 100 tulizokusudia kutoa kwa wateja wetu. Ni furaha kubwa kwetu kuona wateja wengi wakiendelea kuwa na shauku ya kushiriki lakini wasife moyokwani bado tutaendelea kuwapa zawadi kibao zikiwemo bia za bure. Je ni kina nani watatukamilishia kumi ya mwisho?” alieleza kwa msisitizo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile

  Pia aliongeza kuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti bado ina vitu viruri zaidi vinakuja kwa wateja wake kwani kuelekea ukingoni mwa mwa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini ni maandalizi ya kitu kinginekizuri zaidi. “Kila wakati tunawaza mambo mazuri kwa wateja wetu siku zote make mkao wa kula.” Aliongeza Jasper.Alisisitiza kuwa watanzania kuendelea kushiriki katika wiki hii ya mwisho mara nyingi kadiri wawezavyo ili waweze kuwa na nafasi za kushinda zaidi.

  Promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwili ipo katika mfumo wa kuwazawadia wateja na watumiaji wa bia ya Tusker yenye lengo la kubadilisha maisha ya wateja wa Tusker katika njia tofauti. Wiki chache zilizopita Albert Tarimo alishinda Tsh 1,00,000 ambayo aliitumia kununulia tofalikwaajili ya kujengea nyumba yake katika kiwanja alichokua nacho muda mrefu lakini hakuweza kukiendeleza. Albert ambaye ni meneja wa baa amekiri kuwa maisha yake yamebadilika kupitia promosheni hiyo.

  “Niliposhinda Milioni moja, moja kwa moja niliwaza kufanya kitu ambacho kitakua kinamanufaa kwangu na familia yangu. Tayari nilikua na kijisehemu changu nikaona chamsingi ninunue matofali ili nianze ujenzi taratibu. Mwanzo sikujua wapi naweza pata pesa za kununulia vifaa vya ujenzi wala hata namna ya kuanza msingi wa nyumba, lakini leo Tusker imeniwezesha nimenunua tofali 1000 ntakazotumia kuanza ujenzi hivi karibuni.

  ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki nane zilizopita mikoa yote nchini. Wiki moja tu imesalia kukamilisha washindi 100 wa promosheni hiyo.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifuyngua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.

  Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo.
  Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.

  Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.


  0 0
 • 07/18/16--02:49: EFM YAZINDUA TELECONFERENCE
 •  Watangazaji wa kipindi cha  Joto la Asubuhi Gerald Hando na Adela Tillya
   Pichani juu ni baadhi ya wasanii waliohojiwa live

  Ikiwa ni sehemu ya kuboresha matangazo yake, na kuwasiliana moja kwa moja na wasikilizaji kupitia vipindi vyake, 93.7 Efm Radio, leo (18/07/2016) imeanza kufanyamahojiano ya simu muunganiko zaidi ya tatu kwa kufanya mahojiano na wadau mbalimbali moja kwa moja (live).

  Hatua hii imeanza kupitia kipindi chake cha Joto la Asubuhi ikianza na wasanii wa Muziki nchini Nick wa Pili na Nay Wa mitego live kwa pamoja ambapo wameweza kufanyiwa mahojiano hayo.

  0 0


  Meneja wa Bayport Financial Services, Tawi la Lindi, Lovin Mapunda, mwenye fulana juu ya jukwaa, akitoa msaada wa Sh Milioni mbili katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua, ambapo harambee hiyo iliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele, akifuatilia jambo wakati Meneja wa Bayport Financial Services, taasisi inayojihusisha na mikopo, tawi la Lindi, Lovin Mapunda, hayupo pichani wakati anatoa jumla ya sh Milioni mbili kwa ajili ya mchango wa taasisi yake kwa shule ya Sekondari Lindi, iliyopata balaa la kuungua kwa baadhi ya majengo yake. Picha na Mpiga Picha Wetu, Lindi.

  0 0  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akopokea moja baadhi ya vikombe 11 ambavyo timu ya uchukuzi imeshinda katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mapema mwezi mei mkoani Dodoma, anayemkabidhi ni Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Alex Temba.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akipokea cheti cha ushiriki wa mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mpema mwezi mei mkoani Dodoma, anayemkabidhi ni Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Alex Temba
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Bw. Alex Temba mara baada ya kupokea vikombe 11 ambavyo timu ya uchukuzi imeshinda katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mpema mwezi mei mkoani Dodoma, kati ya hivyo vikombe 5 vilitolewa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli vikiwa ni ushindi wa kwanza katika netball Kamba,Baiskeli na Bao.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho aliyeshika Kikombe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Uchukuzi Sports Club mara ya kupokea vikombe na vyeti vya ushindi wa timu hiyo katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mapema mwezi mei mkoani Dodoma.

  0 0


  MSAJILI wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ametolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu msimamo wa Serikali kwa Benki ya Twigabancorp.

  Taarifa hiyo ilieleweka vibaya kuhusu msimamo wa Serikali kwa benki hii ya Twiga Bancorp. Naomba nieleze kwamba kwa hivi sasa Serikali inasubiri mapendekezo ya kitaalamu yatakayowezesha kutatua changamoto za kimtaji za Twiga Bancorp. 

  Ninaposema changamoto za kimtaji sijasema kwamba benki hiyi ipo kwenye hali mbaya ya kushindwa kujiendesha, ila inahitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisheria na vilevile kuimarisha na kusambaza huduma mbalimbali katika maeneo ya nchi. Hatua hizo zinafuatia agizo la Mheshimiwa Rais kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipangokufuatilia utendaji wa benki ya Twiga Bancorp na kuhakikisha kasoro zilizopo zinatatuliwa.

  “Kuna njia mbalilimbali za kuiwezesha benki kupata mtaji ikiwemo nje ya utaratibu wa Serikali, ndiyo maanaWizara na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikishirikiana na Manejiment ya Twiga Bancorp zinaandaa mapendekezo yatakayoiwezesha Benki hii kupata mtaji ili kuiwezeshakutimiza malengo yake ya kiukuaji na kujiendesha kwa faida.”

  Hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa na Wizara ya Fedhana Mipango na ofisi ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Benki ya Twiga Bancorp. Kwa mfano, mnamo mwaka 2015, Muundo wa Shirika ulibadilishwa ambao pamoja na mambo mengine ulipelekea kuteuliwa kwa Menejimenti mpya, kwa kupitia Menejimenti hiyo mpya  umetengenezwa Mpango Mkakati wa miaka mitano ambao umeanza kutumika Januari 2016, serikali pia ilifanya mabadiliko katika bodi ya wakurugenzi kwa kuteuaBodi mpya ya Wakurugenzi. 

  Kwa ujumla kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji baada ya hatua hizo kuchukuliwa. Kwa mfano benki imeweza kupata Hati Safi ya Mahesabu (Unqualified Opinion) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heasabu za Serikali kwa mara ya kwanza kwenye hesabu zake za mwaka 2015 jambo ambalo halikuwezekana toka Mwaka 2011. 

  “Hizi taarifa zinazosambaa kuwa benki inafungwa sio za kweli. Kwenye benki kuna pesa za wananchi, kuna mikopo iliyotolewa kwa watu mbalimbali, kuna rasilimali za benki ikiwemo rasilimmali watu. Yote hayo yana Utaratibu wake wa kuyasimamia.. Hata ukisikiliza hotuba ya Rais hakusema funga benki ya Twiga Bancorp aliagiza hatua zichukuliwe na kwamba Katibu Mkuu asimamie.” 

  Hivyo tuna wahakikishia kuwa fedha za wananchi zilizo katika benki ya Twiga Bancorp zipo salama na kwamba uongozi uliopo hivi sasa unaendelea kushughulikia changamoto za kiutendaji zilizokuwepo na kama yalivyokuwa maagizo ya Rais hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa. Pia benki hii inaendelea kutoa huduma zake kwa wateja kama kawaida.”

  Mwisho, Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa benki hiiili kuhakikisha tatizo lililopo sasa la mtaji linatatuliwa na kuhakikisha inajiendesha kwa faida. 
   Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu Benki ya Twiga Bancorp. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Cosmas Kimario na Mkurugenzi  Rasilimali Watu na Utawala, Amina Lumuli.
   Maofisa wa Benki hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16(kushoto) akimshuhudia mchezaji wa yanga Abdul Juma,akiwaonesha waandishi wa habariri tuzo yake aliyoshinda ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu.Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  WADAU wa michezo wawataka Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kuboresha zaidi tuzo za Ligi kuu ya Vodacom na kuacha kutumia njia za ujanja katika kuwapata wachezaji wanaostahili kuwania tuzo hizo na kuwapa nafasi wananchi kutumia nafasi yao kuchagua mchezaji aliyeisaidia na kutoa mchango mkubwa kwa timu yake.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti,  Wadau hao wamesema kuwa ukiangalia tuzo hizo hawakuziweka wazi na ni jinsi gani wanapigiwa kura. Tunachojua ni kuwa  waliwataja wanaowania tuzo hizo ila jinsi ya kumpata mshindi ndiyo hatujui wanatumia vigezo kumpata mshindi.

  "Tunajua wanapiga hatua kwenye utoaji wa tuzo hizo ila changamoto kubwa bado ipo hasa katika upatikanaji wa wachezaji wanaowania na jinsi gani wanawapata mpaka kuwatangaza na baada ya kuwataja wanatumia njia ipi kuweza kumpata mshindi na kwanini wasilete kwa wadau na tuamue sio wao tena kukaa na kuamua,"wamesema.

  Tuzo za Vodacom zilifanyika jana usiku huku Timu ya Yanga wakichukua tuzo tano ikiwemo ya Mchezaji bora wa Ligi Juma Abdul, Mchezaji bora wa Kigeni Thaban Kamosoku, Mfungaji bora Amisi Tambwe, Mchezaji Bora mwenye Nidhamu Thaban Kamosoku na Kocha Bora Hans Van De Pluijm.

  Mohamed Husein 'Tshabalala' amechukua tuzo ya mchezaji chipukizi akiwabwaga Shiza Kichuya na Farid Mussa, Ibrahim Ajib akichukua tuzo ya goli bora la msimu pamoja na Mtibwa timu yenye nidhamu. Na kwa upande wa mwamuzi bora iliangukia kwa Ngole Mwangole kutoka Mbeya.

  0 0

  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

  MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA


  TAARIFA KWA UMMA


  MAELEKEZO JUU YA MIRADI YA UBUNIFU WA KUTENGENEZA NDEGE


  1.         UTANGULIZI


  1.1.    Taarifa hii kwa umma imetolewa kwa mujibu wa madaraka ya kisheria aliyonayo Mkurugenzi Mkuu kupitia sheria ya Usafiri wa Anga nchini, sheria namba 80 (iliyofanyiwa maboresho mwaka 2006) pamoja na kanuni zake mbalimbali zilizopo zikiwa na lengo la kuhakikisha hususan usalama katika usafiri wa anga pamoja na kulinda maslahi ya wananchi na mali zao kwa ujumla kutokana na shughuli za usafiri wa anga.


   1.2.    Taarifa hii kwa umma imetolewa ili kuufahamisha umma kwa ujumla juu ya tahadhari za ki-usalama za kuzingatiwa pindi unapofanya shughuli za uendeshaji wa usafiri wa anga nchini Tanzania. Taarifa hii kwa umma imetolewa kufuatia Mamlaka kubaini kwamba hivi karibuni kumeibuka wimbi la watu binafsi pamoja na taasisi zinazodai kuwa na uwezo wa kutengeneza ndege(Helikopta) na wapo katika hatua ya kuzifanyia majaribio ya kuzirusha angani pasipo kuzingatia  kanuni za usafiri wa anga na taratibu zake za ki- usalama zilizopo.


  1.3.    Taasisi ama mtu yeyote anayetarajia kutengeneza ndege au vifaa vyake   anakumbushwa kuhakikisha anafanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za usafiri wa anga ikiwemo pamoja na kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kabla ya kuanza mradi wake.


  1.4.    Lengo ni kuhakikisha usalama kwa wananchi na mali zao, kuzingatia viwango vya ubunifu husika, aina na ubora wa  malighafi   zinazotumika kufanya ubunifu, vipuri vya ubunifu husika,  jinsi ya uundwaji wa  chombo husika unavyofanyika  hasa kuangalia kama vifaa vinavyotumika kutengenezea ndege ni vile vinavyokubaliwa na kanuni za Mamlaka ya usafiri wa anga nchini  pamoja na zile za kimataifa .


  2.    KUTAMBULIWA KWA NDEGE  


  2.1.    Kanuni namba 5 ya usafiri wa anga (inayohusu ubora wa ndege) kanuni ya mwaka 2011 imeweka  bayana kwamba:

  2.1.1     Mamlaka italitambua ombi ama wazo la kutaka kutengeneza ndege, vifaa vya ndege  endapo Mamlaka itajiridhisha kwamba,


  (a)  Kazi itakayofanywa ni ile inayoendana na miundo inayokubaliwa katika utengenezaji wa ndege;

  (b)  Uwepo wa utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na uwepo wa usimamizi wa mhandisi mwenye cheti cha kutengeneza  aina ya ndege husika atakayehakikisha anasimamia hatua zote za ubunifu na ufundi wa ndege husika ; na

  (c)  Taratibu za maandalizi yake zinakubaliwa katika kutengeneza ndege husika.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha na meza kuu baada ya kushuhudia maafisa waandamizi wa polisi waliopandishwa veyo wakila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo, wakiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kamishna wa maadili ya Utumishi wa Umma  Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha na meza kuu na  maafisa waandamizi wa polisi waliopandishwa vyeo baada ya kula kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo, 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha na meza kuu na  maafisa waandamizi wa polisi waliopandishwa vyeo baada ya kula kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo, 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha na meza kuu na  maafisa waandamizi wa polisi waliopandishwa vyeo baada ya kula kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo, 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha na meza kuu na  wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama maafisa waandamizi wa polisi  baada ya maofisa waliopandishwa vyeo kula kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo, 


  0 0

  KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imedhamini safari ya siku sita kwa raia 36 wa Afrika Kusini wakiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo, kupanda Mlima Kilimanjaro yenye lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya Taulo za watoto wa kike.

  Kampuni ya Vodacom inadhamini safari hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa Vodacom kufanya hivyo.
   
  Akizungumza wakati wa kuanza changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kundi hilo la watu 36,Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Henry Tsamburakis alisema Vodacom imetoa mawasiliano wakati wote wa safari ya kupanda mlima ili wasipate tatizo la kushindwa kuwasiliana na ndugu zao pamoja na kutuma picha za matukio wawapo mlimani.

  "Vodacom Tanzania tunajivunia kuweza kuwadhamini watalii na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom kutoka Afrika ya kusini kwa mwaka wa pili mfululizo kwa kudhamini Mfuko wa Mandela ambapo kila mwaka watalii hawa huja nchini mwetu mwezi wa saba kupanda mlima wa Kilimanjaro wakiwa na lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike" alisema Tsamburakis. 

  "Kwa upande wetu Vodacom Tanzania tumeamua kuwapatia udhamini wa mawasiliano ili wasipate matatizo ya mawasiliano wakiwa katika harakati za kupanda mlima Kilimanjaro waweze kutuma picha au kuwasiliana na ndugu zao kwa urahisi zaidi kupitia 4G yetu,"aliongeza Tsamburakis. 

  Alisema Vodacom imetoa vifaa maalumu (Routers) sita zikiwa zimeunganishiwa katika mtandao wa kasi huku zikiwa zimewekewa bando ya GB 10 watakazoweza kutumia kwa muda wote watakapokuwa mlimani.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Gerry Elsdon ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kuwezesha mawasiliano hatua itakayochangia safari yao ya kuelekea katika kelele cha Uhuru katika mlima Kilimanjaro kuwa rahisi zaidi. 

  "Niishukuru kampuni ya Vodacom kwa niaba ya wenzangu, imewezesha mawasiliano yetu kuwa rahisi sasa,kwa sababu tuliamini kuwa tutakua nje ya mawasiliano kwa zaidi ya siku sita kumbe sasa tutaendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa" alisema Elsdon.

  Kwa upande wake mratibu wa safari hiyo ambayo hujulikana kama Treck4mandela,Richard Mabaso alisema lengo la safari hiyo ni kuendelea kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Taulo za kike kwa watoto wa kike wasio na uwezo ili kukitumia pindi wawapo katika siku za hedhi.

  ""Tunatambua changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa wale walioko mashuleni pindi wanapoingia katika siku zao,kupitia Mfuko wa Mandela tumeendelea kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia angalau kupata Taulo ili waweze kuendelea na masomo bila ya kuwa na kikwazo." alisema Mabaso.

  Alisema mbali na zoezi hilo kulenga kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa kike pia limekua likitumika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela.
   Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akizungumza na wageni raia wa Afrika Kusini wanaopanada Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha za kununua taulo za watoto wa kike wawapo katika siku zao za Hedhi.
   Baadhi ya wapagazi katika Mlima Kilimanjaro wakishusha mabegi ya wageni hao kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. 
   Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akimsaidia mmoja wa wageni hao kubadili lugha ya kiswahili katika simu yake kwenda ya Kiingereza. 


  0 0
 • 07/18/16--05:47: Article 8
 • MINISTRY OF WORKS, TRANSPORT AND COMMUNICATION

  TANZANIA CIVIL AVIATION AUTHORITY


  PUBLIC NOTICE


  AIRCRAFT MANUFACTURING PROJECTS IN TANZANIA


  1.         BACKGROUND


  1.1.    This Public Notice is issued pursuant to powers granted to the Director General by the Civil Aviation Act CAP 80[R.E 2006] and the various applicable Civil Aviation Regulations issued under it to ensure specifically safe and secure operations of aircraft and safeguard the interest of the public and their properties from any Civil Aviation undertakings.


  1.2.    This notice is issued to inform the public in general of safety measures to be observed when undertaking civil aviation operations inTanzania. The Notice is issued following the Authority’s awareness that there have been individuals/organisations who claim to have the capacity to manufacture aircraft (Helicopter) and are in the process of testing the aircraft contrary to Civil Aviation Regulations and Safety Implementing Standards.


  1.3.    Organisations and any person intending to manufacture aeronautical products are reminded to ensure compliance to applicable Civil Aviation Regulations and obtain prior approval from the Director General of the Tanzania Civil Aviation Authority before the commencement of such undertakings.


  1.4.    The objective is to ensure that in the interest of safety to people and public property, standards relating to design, materials, construction equipment, performance and maintenance of aircraft or aircraft components are acceptable by the authority and comply with both national and international regulations.


  2.    ACCEPTANCE OF AIRCRAFT


  2.1.    Regulation 5 of the Civil Aviation (Airworthiness) Regulation, 2011 specifies that:

  2.1.1     Authority shall only accept application for production of aircraft or aircraft component if the Authority is satisfied that-


  (a)  the work to be undertaken conforms to specified design as approved by the State of Design;

  (b)  there is in place a suitable arrangement with the holder of a type certificate which ensures satisfactory co-ordination between production and design; and

  (c)  thereis acceptable arrangements for oversight by the State of Design.  3.      DESIGN AND CONSTRUCTION OF AIRCRAFT

  3.1The International Standard as specified in ICAO Annex 8 (Airworthiness of Aircraft) specifies that “Details of design and construction shall be such as to give reasonable assurance that all helicopter parts will function effectively and reliably in the anticipated operating conditions. They shall be based upon practices that experience has proven to be satisfactory or that are substantiated by special tests or by other appropriate investigations or both.


  3.2 Currently Tanzania is not a State of Design, manufacture or production of aeronautical products to be able to effectively oversee the design, manufacturing or production organisations.However, the Authority can make arrangements through cooperation with foreign Civil Aviation Authorities [eg. European Aviation Safety Agency (EASA) and US Federal Aviation Authority (FAA) to ensure that before a product is placed in the public, all the design processes, materials and applicable tests have been conducted to assure the product can endure all the stresses it will be subjected in the air without failure. All components including its engines, propeller, rotors must meet robust tests for endurance in the air.  4.      CONCLUSION


  4.1 In order to safeguard the safety of the public, organisations and individuals are required to ensure compliance to the Civil Aviation Act and its applicable Regulations. Henceforth no one should engage into the design, construction or manufacture of aeronautical products without consultation with the authority for formal processes and procedures to ensure all the applicable tests of materials and manufacture have been appropriately complied with in accordance with global standards for aeronautical products.


  4.2  The Authority supports and encourages such innovations but should be conducted in systematic and systemic manner for the safety of all. In line with that Authority Inspectors will visit premises where such projects have been identified for more consultation and guidance.


  4.3 By virtue of this notice, we urge all individuals and organizations to suspend all undertakings relating to aircraft manufacturing projects and consult the authority for further guidance.

    

  Issued by

  Hamza S. Johari

  DIRECTOR GENERAL

   TANZANIA CIVIL AVIATION AUTHORITY


  JULY 2016

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika ukumbi wa KCC mjini Kigali Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.Picha na OMR.

  KIGALI, RWANDA.

  Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Afrika (AU) kwamba itaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama wa AU katika kujadili changamoto za kiusalama zinazolikabili Bara la Afrika kwa njia ya mazungumzo na upatanishi kama inavyoelekeza Katiba ya umoja huo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akichangia mada kuhusu Hali ya amani na usalama katika Bara la Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika hapa Kigali, Rwanda.Mheshimiwa Samia alisema Tanzania inasikitishwa na inalaani vikali matukio ya uvunjifu wa amani yanayoendelea kujitokeza katika baadhi ya nchi za Kiafrika kiasi cha kutishia usalama wa raia.

  Alielezea mauaji ya Hafsa Mossi, aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na waziri wa zamani wa Burundi na mapigano ya hivi karibuni Sudan ya Kusini ambapo mamia ya raia wasiokuwa na hatia waliuwawa na wengine maelfu wameachwa bila makazi kwamba ni muendelezo wa uvunjifu wa amani katika nchi hizo.

  Aliwataka wadau husika katika nchi za Burundi na Sudan ya Kusini kushiriki kikamilifu katika mazungumzo yanayoendelea kwa kuwa hiyo ndiyo njia muafaka ya kuleta amani, usalama na utulivu wa kudumu  katika nchi zao.Aidha, Makamu wa Rais ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo aliiomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuisadia Sudan ya Kusini katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika mgogoro ulioikumba nchi hiyo.

  Akichangia kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Makamu wa Rais alisema Tanzania kwa ujumla inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kuwa na viti viwili katika baraza hilo na kura ya turufu bila ya masharti yoyote.Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo viongozi walisisitiza suala la kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama na kusema hiyo ndiyo nguzo muhimu katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Bara la Afrika.

  Katika mkutano huo kulikuwa na uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya Afrika ambayo ilitolewa kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Deby wa Chad na nchi mwenyeji wa mkutano, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Mkutano huo ambao ulizungumzia pia gharama za kuendesha umoja huo na masuala ya haki za wanawake ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi zaidi ya 35, Marais wastaafu, wake wa Marais pamoja na viongozi wa serikali.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais 

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
  Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
  Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  0 0


  MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwavulia uvivu wale wote wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.

  Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kueleza maswala kadhaa yausuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina lake.

  “Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inaanza na cheo changu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda na si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda.

  Anasema kuwa juu ya agizo batili lililosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa wasiokuwa na kazi watakwenda jela,sio tamko la account yake bali yeye ameagiza Wenyeviti wa serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.

  Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe hatoacha  kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga.Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huu kuwa makini na kufuata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akizungumza ndani ya kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) knew Kituo cha Mimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) Julai 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki katika Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Kampuni inayoongoza Afrika katika suluhisho za malipo ya mitandaoni na ya kupitia mitandao ya simu, 3G Direct Pay leo imezindua suluhisho jipya la program ya simu (mobile app) ambayo itawawezesha kufanya biashara za malipo ya kadi na simu kupitia simu zao mahala popote na kwa wakati wowote. 

  Programu hiyo inayoitwa mSWIPE+ inawezesha wafanyabiashara kuhakiki malipo kupitia simu zao na pia kuweza kusoma kadi za malipo yanayopitia katika mashine za mauzo (POS) kupitia mfumo unaoitwa Quickpay. Programu hii ya mSwipe+ inaweza kutumika kwa aina zote za kadi za malipo ya kabla na baada (credit na debit cards) na pia malipo ya kutumia simu za mkononi. 

  Mkurugenzi Mkuu wa 3G Direct Pay, Eran Feinstein, amesema kuwa program hiyo imeundwa kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara na wateja wao, kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahala popote na pia kuboresha maendeleo ya malipo ya kadi na biashara za mitandanaoni. 

  “Simu ya mkononi ni muhimu sana katika maisha ya watu wengi. Na program hii inawezesha malipo kufanyika kupitia huu mtandao. Na hii ni katika mipango yetu ya kuhakikisha kuwa mtu yeyote ana uhuru wa kununua, kuuza, kulipa na kulipwa kupitia mtandaoni kwa haraka, usalama na urahisi. Programu ya mSwipe+ ni njia rahisi, ya haraka na yenye usalama inayompa mteja uhuru wa kutumia kadi ya aina yoyote ya malipo, malipo ya kupitia simu, na kuweza kulipa mara moja,” alioongeza Feinstein. 

  Programu ya mSWIPE+ kwa sasa inatumika tu kwenye simu za teknolojia ya android na inaweza kutumika tu kwa wale wafanyabiashara watakaojisajili na mtandao wa 3G Direct Pay na programu hiyo inapatikana katika simu kwenye ‘Google play store’. Kwa simu zinazotumia teknolojia ya IOS bado ujenzi wa programu yao unaendelea. 
  Programu ya mSwipe+ ina kila teknolojia ya ulinzi na usalama wa kimtandao wa kuhakikisha malipo yoyote yanayofanyika ni salama kwa watumiaji.

  0 0

   Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.
   Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akionesha Tsheti amazo zitavaliwa siku ya 24 ambazo zitauzwa kwaajili ya kuchangi pamoja na kuongeza nguvu za kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao hawana nguo nzuri pamoja na wasio na viatu vya shule na mabegi ya shule. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Tasisi ya Blessing.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Mkakati wa  Rais Dk. John Pombe Magufuli  wa elimu bure unatekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu ,huku Taasisi ya Blessing  imekuja na mkakati wa kusaidia wanafunzi wasio na vifaa pamoja sare za shule.

  Taasisi hiyo inatarajia kufanya uchangishaji kwa ajili ya kupata vifaa pamoja na sare za shule kwa wanafunzi ili waweze kusoma bila changamoto vitu hivyo.Uchangiaji huo unatarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu katika ukumbi wa Nkurumah katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

  Meneja wa Taasisi hiyo, Blessing  Mlanga amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanachangamoto ya vifaa na sare hivyo ikiwa watanzania tunaweza kuchangia sehemu hiyo na kuwa tumeunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli.Zawadi amesema kuwa yeye ni kijana wa kitanzania anayesoma Malaysia ameona kuna sehemu ambayo anaweza kuboresha katika upande wa vifaa pamoja na sare.

  Amesema kuwa mradi huo wa sare na vifaa utaanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Arusha na baada hapo wataendelea na mikoa mingine.

  0 0  0 0

    
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kuwaondoa watumishi wote wasiokuwa askari polisi na ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu na ufujaji wa fedha za umma ili kulinda heshima, nidhamu na uadilifu ndani ya jeshi hilo.

  Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18 Julai, 2016 muda mfupi baada ya Naibu Makamishna wa Polisi 25 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi 35 kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Pamoja na kutoa agizo la kutaka wasio askari polisi kuondolewa katika utumishi wa jeshi la polisi, Rais Magufuli pia ameagiza jeshi hilo lichukue hatua dhidi ya wote wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa fedha wakiwemo wanaodaiwa kuiba mabilioni ya shilingi zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa sare za askari mwaka jana 2015.

  "Mnajua kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika.

  "Kama mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi? hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni askari polisi? Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na tuwapangie kazi nyingine uraiani" Amesema Rais Magufuli.

  Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayofanya iliyoliwezesha kujenga imani kubwa kwa watanzania na ametaka viongozi wa Jeshi hilo wawaongoze askari walio chini yao vizuri, wawatie moyo na waache vitendo vya kuwakatisha tamaa kwa kuwaadhibu ama kuwatisha pale wanapochukua hatua stahiki dhidi watu wanaovunja sheria.

  "Sasa mimi niwaombe nyinyi, wale wadogo mnaowaongoza mkawape mamlaka ya kutimiza wajibu wao, hata kama ameshika gari la IGP liache lishikwe IGP atakwenda kujieleza mwenyewe, hata akishika gari la RPC afanye hivyohivyo, hata akishika gari la Waziri au gari la Rais mwacheni atekeleze wajibu wake, sheria ni msumeno, tunawanyima nguvu hawa wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu unamwambia liachie, ukifanya hivyo aliyeshikwa anatoka pale akiwa anatamba kwelikweli na yule askari unamvunja nguvu ya kufanya kazi" Amesisitiza Rais Magufuli. 

  Rais Magufuli pia amelitaka jeshi hilo kuungana na vyombo vingine vya serikali katika kutekeleza shughuli zake zikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bandarini, katika sekta ya utalii na maeneo mengine, kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuondoa watumishi hewa.

  Tukio hili la Naibu Makamishna wa Polisi na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Makatibu Wakuu na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

   Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi DCP na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisaini hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Frasser Rweyemamu Kashai akisaini hati hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.


older | 1 | .... | 1288 | 1289 | (Page 1290) | 1291 | 1292 | .... | 3285 | newer