Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1287 | 1288 | (Page 1289) | 1290 | 1291 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) wamezindua rasmi zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia tatizo la UKIMWI na Virusi vya UKIMWI nchini. Kampeni ya kuchangisha fedha kusaidia waathirika wa UKIMWI na Virusi vya UKIMWI  kupitia upandaji Mlima Kilimanjaro hufanyika kila mwaka na mwaka huu ukiwa ni mwaka wake wa  15,Mgodi wa Dhahabu wa Geita umeratibu wapandaji 100 katika zoezi hilo.

   Akizungumza kwenye hafla ya kuwatakia heri wapandaji  wanaoanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa muda wa siku saba,Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ujumbe maalumu kuhusu vita ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI akisema panahitajika ushirikiano wa karibu baina ya Serikali na sekta binafsi ili kupunguza tatizo hilo

  Rais Kikwete amesema kuwa kupambana na UKIMWI pamoja na Virusi vya UKIMWI si jambo dogo hivyo panahitajika ushirikiano kwa Serikali na wadau wote.
  Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia hafla ya kuwaaga wapanda Mlima 100 kwenye Kampeni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM),Kampeni inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS).Pembeni yake kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Terry Mulpeter pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadique.

  ‘‘Serikali imeendelea kufanya jitihada nyingi kupunguza tatizo hili kwa kushirikiana na sekta binafsi kupunguza tatizo hili.Tumekuwa tukishirikiana na wadau kama Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM)  kwa miaka 15 mfululizo kupunguza maambukizi mapya,vifo vitokanavyo na UKIMWI pamoja na unyanyapaa kwa waathirika wa Virusi vya UKIMWI.Tumefanikiwa  kutoka tarakimu mbili kwenda kwenye tarakimu moja’’ amesema Rais Kikwete.


  Rais Kikwete ameongeza kuwa hatua ya Tanzania kufikia asilimia 5.1 ni ya kupongezwa na kwamba jamii isiridhike na hali hiyo badala yake inapaswa kuendelea kuwa makini kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo kuanzia mtu binafsi ngazi ya familia na jamii yote kwa ujumla.
  Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge 2016, Mrisho Mpoto akitumbuiza wimbo wake wa Sauti nenda mbele ya Mgeni rasmi Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi kabla ya kuanza rasmi zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku saba kuchangisha fedha za kusaidia waathirika wa UKIMWI na VVU nchini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter amesema kuwa mwaka huu Kampeni ya Kili Challenge inahusisha wapandaji mlima 100 ambao kati yao,50 watapanda mpaka kilele cha Mlima  Kilimanjaro na 50 wataendesha baiskeli kuzunguka mlima kwa  umbali wa kilomita 380 kwa muda wa siku saba au wastani wa kilomita 60 kila siku.

  Rais Kikwete ameongeza kuwa hatua ya Tanzania kufikia asilimia 5.1 ni ya kupongezwa na kwamba jamii isiridhike na hali hiyo badala yake inapaswa kuendelea kuwa makini kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo kuanzia mtu binafsi ngazi ya familia na jamii yote kwa ujumla.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter amesema kuwa mwaka huu Kampeni ya Kili Challenge inahusisha wapandaji mlima 100 ambao kati yao,50 watapanda mpaka kilele cha Mlima  Kilimanjaro na 50 wataendesha baiskeli kuzunguka mlima kwa  umbali wa kilomita 380 kwa muda wa siku saba au wastani wa kilomita 60 kila siku.

  Bw Terry Mulpeter ameongeza  kuwa jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kuchangisha fedha kupitia Kampeni ya  Kili Challenge ni za kuungwa mkono kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya waathirika wa UKIMWI na Virusi vya UKIMWI.

  Mwaka huu wapandaji Mlima Kilimanjaro kupitia Kampeni ya Kili Challenge  wanatoka katika mataifa ya Tanzania, Afrika ya Kusini,Marekani,Uingereza na Australia .Mpaka sasa Kampeni ya Kili Challenge imechangisha jumla ya Bilioni 12 za Kitanzania fedha ambazo zimetolewa  kwa Taasisi  zaidi ya 30 za Serikali na  zisizo za Kiserikali.
  Baadhi ya wapanda mlima kwa kutumia baiskeli kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita wakijiandaa kupanda Mlima Kilimanjaro


  0 0

  Na Lucas Mboje - Jeshi la Magereza,

  PAROLE ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo Gerezani cha miaka minne na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo vifuatavyo:-

  i).    Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum. Masharti hayo ni  kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake, kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu pamoja na kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii;
  ii).    Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani na;
  iii).    Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.
   
  Parole ni moja kati ya adhabu mbadala na imeonesha mafanikio makubwa katika nchi nyingi duniani.  Utaratibu huu ni wa kipekee kwa kuwa unawagusa wafungwa wa vifungo virefu ambao ndio wengi waliopo magerezani. Aidha, ni utaratibu unaoshirikisha jamii katika urekebishaji kwa kuzingatia usalama wa jamii na dhana kwamba uhalifu ni zao katika jamii.

  Madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu wa Parole  nchini hayatofautiani na madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu huu kwenye nchi nyingine Duniani zikiwepo nchi za Afrika kama vile: Afrika kusini, Zambia na Namibia.  Mfumo wa Parole ulioainishwa hapa nchini unatokana na uzoefu wa Parole unaotumika nchini Canada.  Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa Parole hapa Nchini ni:-
  i.    Kuhusisha jamii katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa badala ya kutegemea serikali peke yake kwani chanzo cha uhalifu ni mazingira yanayotokana na jamii yenyewe.

  ii.    Kuwepo na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wafungwa wenye vifungo virefu magerezani ambao kutokana na urefu wa vifungo vyao hawawezi kufaidika na programu zilizopo za urekebishaji kwa sababu ama watatoka magerezani wakiwa wazee wasiojiweza, watakutana na mabadiliko makubwa kijamii, kiuchumi na kisera wasiyoweza kuyamudu haraka/ipasavyo kwenda na wakati au watafia gerezani.

  Wafungwa wa aina hii hukata tamaa kwani hawaoni sababu ya kuwa na nidhamu wawapo gerezani, hivyo kusababisha usalama magerezani kuwa mashakani.  Parole ilikusudiwa kuwarejeshea matumaini ya kurejea katika jamii na kuishi maisha ya kawaida na kupunguza tishio la kiusalama magerezani na katika jamii kwa ujumla.

  Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi liliwasilisha mapendekezo ya kutungwa Sheria ya Bodi za Parole nchini. Mapendekezo hayo yalijenga hoja ambayo hatimaye iliwasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Novemba, 1994 na kupitishwa rasmi kuwa Sheria ya Bodi za Parole Na. 25/1994. 

  Sambamba na kutungwa kwa Sheria hiyo, kanuni za Bodi za Parole ziliandaliwa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali tarehe 29 Agosti, 1997 (GN. 563/1997) hivyo kuwezesha Sheria hiyo kuanza kutumika rasmi. Hata hivyo Sheria iliyopitishwa haikuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Jeshi la Magereza ambayo yaliwalenga wafungwa wote kunufaika na Parole bila kujali aina na uzito wa makosa. Aidha, Sheria husika haikuanza kutumika mara moja kutokana na sababu zifuatazo:-

  i.    Bodi ya Taifa ya Parole na Bodi za Parole za Mikoa zilizokuwa zimeundwa kwa mara ya kwanza zilivunjwa na kuundwa upya na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kulalamikiwa kuwa uteuzi wa Wajumbe wake haukuzingatia uwiano wa jinsia na dini.

  ii.    Kutokamilika kwa maandalizi ya nyaraka mbalimbali muhimu katika utekelezaji wa mpango wa Parole ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa semina kwa wajumbe wa Bodi za Parole za Mikoa yote nchini ili kufanikisha uanzishwaji na utekelezaji wa Sheria hiyo.

  Baada ya matukio hayo, kikao cha kwanza cha Bodi ya Taifa ya Parole kilifanyika tarehe 19 Agosti, 1999 ambacho kiliwajadili wafungwa watano (5) na kupitisha watatu(3) walioonekana kutimiza  masharti ya kuachiliwa kwa Parole nchi nzima. Idadi hiyo ni ndogo hasa ikizingatiwa kwamba wakati huo magereza yote nchini yalikadiriwa kuwa na wafungwa 27,000. Kutokana na Wafungwa  hao watano waliojadiliwa, ilidhihirisha kuwa Sheria yenyewe ilikuwa   haitekelezeki kama ilivyokusudiwa katika mapendekezo yaliyowasilishwa na Jeshi la Magereza hapo awali.
  Matokeo haya yalisababisha Bodi ya Taifa ya Parole kuishauri  Serikali  kupanua wigo wa sheria hii ili wafungwa wengi zaidi waweze kunufaika. Mapendekezo haya yalilenga kifungu cha nne     cha sheria     ya Bodi za Parole vifungu vidogo (a),(b) na (c) ambavyo vinataja kuwa wafungwa wanaotumikia vifungo vya maisha, waliofungwa kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha,     madawa ya kulevya, kujamiiana na adhabu ya kifo iliyobadilishwa  kuwa kifungo kwamba     hawawezi kupata msamaha wa Parole. Ilipendekezwa kwamba  kifungu hicho kirekebishwe ili     wafungwa wote wa makosa hayo nao wafikiriwe kunufaika na  utaratibu wa Parole bila kujali makosa waliyotenda.
  Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Parole, Sheria Na. 25/1994 ilifanyiwa marekebisho kwa Sheria Na. 5/2002 ambayo ilijihusisha na eneo dogo tu kwamba badala ya mfungwa anayestahili Parole kuwa amehukumiwa kifungo cha miaka nane (8) na kuendelea, ilirekebishwa na kuwa awe amehukumiwa kifungo cha miaka minne (4) na kuendelea.

  Chini ya marekebisho hayo Wakili wa Serikali Mfawidhi wa kanda aliongezezwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Parole ya Mkoa. Hata hivyo suala la aina ya makosa na urefu wa kifungo katika kufikiriwa kunufaika kwa mpango wa Parole lilibaki kama lilivyokuwa hapo awali. Baada ya marekebisho hayo ya Sheria ya Bodi za Parole, Bodi  za Parole za Taifa na Bodi za Mikoa zilizinduliwa upya mwaka 2003, na Bodi ya Taifa ya Parole ilifanya kikao chake cha kwanza mwezi Agosti, 2003  ambacho kilikuwa cha pili tangu Sheria hii ilipoanza kutumika rasmi nchini mwaka 1999.

  Kwa mujibu wa Sheria na Sera za kitaifa kuhusu uboreshaji wa Magereza zinazotolewa kufuatia kuridhiwa kwa maazimio mbalimbali ya Kimataifa katika kuboresha hali za wafungwa magerezani, imeonekana kuwa vifungo siyo njia pekee ya kumrekebisha mhalifu. Adhabu mbadala zimeonekana ni bora zaidi kuliko kifungo kwa vile jamii huhusishwa katika suala zima la kumrekebisha mhalifu. 

  Adhabu mbadala zinazotumika hapa nchini ni pamoja na kulipishwa faini, Kuachiliwa kwa masharti, Probation, Kuachiliwa kwa matazamio, Kifungo cha Nje (EML), Parole, Huduma kwa Jamii n.k. Aidha, katika adhabu mbadala   zilizoainishwa, Utaratibu wa Parole umeonekana unafaa zaidi kwa kuwa ndugu, uongozi wa mtaa/kijiji na mwathirika wa uhalifu hushirikishwa kutoa maoni kabla ya mfungwa husika kunufaika na mpango huu. Aidha, ni adhabu mbadala pekee inayohusika na wafungwa wanaotumikia vifungo virefu magerezani.
   Itaendelea ............wiki ijayo......!.

  MWANDISHI WA MAKALA HII NI AFISA NGAZI YA JUU WA JESHI LA MAGEREZA, 

  0 0
 • 07/17/16--01:00: ZIFF AWARDS POWERFUL FILMS
 • Under the beautiful Zanzibar skies, ZIFF 2016 awarded some of the best films from across the globe.  ZIFF 2016 has seen over a week of film screenings and special events enjoyed by over 60 visiting filmmakers alongside hundreds of invited guests and thousands of Zanzibaris and visitors.

  The Old Fort was the backdrop for the exciting Awards Night event that also saw the announcement of the theme and dates for ZIFF 2017, ZIFF’s 20th anniversary edition – FINDING JOY, July 8th – 16th 2017.

  East African films dominated the awards, with Rwanda’s A Place for Myself winning three awards; The Sembene Ousmane Award, The Signis Prize, and the Golden Dhow for Best Short Film.

  Kenya’s Watatu also was recognized with 3 awards, including the coveted Golden Dhow for Best Feature Film, the Signis Prize and sharing the European African Film Festival Award alongside the Kenyan film Zawadi that also won two awards.

  Directed by Nick Reding and, the film, Watatu, made by Kenya’s leading arts for social change organization – SAFE Kenya – examines the rise of radicalization amongst young Muslims in Mombasa. Part drama, part documentary, and written in part by the citizens of Mombasa.


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  Simu.tv: Wakazi wa kata ya Mkungwe katika Halmashauri ya Kigoma, wameipongeza serikali kwa kuwatekelezea mradi wa maji safi uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 500;https://youtu.be/_v9xX7NaK_M

  Simu.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema mpango wa malipo kwa stakabadhi ghalani, umesababisha migogoro na wakulima kwa watendaji kushindwa kusimamia vizuri; https://youtu.be/d6-3kDBB-So

  Simu.tv: Afisa mwandamizi wa ustawi wa jamii katika taasisi ya mifupa hospitali ya Muhimbili MOI  Mary Michael amesema jamii inapaswa kujitokeza kusaidia tatizo la vichwa vikubwa kwa watoto; https://youtu.be/hlg2EIp4izE

  Simu.tv: Wavunaji wadogo wa miti katika shamba la miti la Taifa Sao Hill wameiomba serikali kuwapatia vibali wavunaji wadogo kuweza kuifanya kazi hiyo; https://youtu.be/U-aFPDGwkl4

  Simu.tv: Mazungumzo maalumu na mbunifu katika masuala ya mavazi nchini Sheria Ngowi; https://youtu.be/EX4UoZo-Ycg

  Simu.tv: Mabingwa wa soka wa Tanzania ambao ni wawakilishi pekee katika mashindano ya Kimataifa Yanga, wamelazimishwa sare  na timu ya Medeama kwa kufungana mabao 1-1; https://youtu.be/XQLgxJ6h5vA  

  Simu.tv: Naibu waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Anastazia Wambura ametembelea kambi ya riadha iliyoko Mbulu na kuwataka wanariadha hao kujiepusha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli; https://youtu.be/6TIaNFbUzBA

  Simu.tv: Kukosekana kwa viwanja pamoja na kutothaminiwa kwa wanamichezo hapa nchini imeelezwa kusababisha michezo kudorora hapa nchini.https://youtu.be/ZutYr8YseK4  

  Simu.tv: Rais Dr John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na kuwapandisha vyeo maafisa wa jeshi la polisi. https://youtu.be/hgjuAPSYo6c

  Simu.tv: Wananchi wa kata ya Magugu wilayani Babati wametakiwa kutunza vivutio vya asili vilivyopo katika kata hiyo ili kuendeleza sekta ya utalii hapa nchini.https://youtu.be/uSGUe6t1BmI

  Simu.tv: Mbunge wa Mbarali Mkoni mbeya ametoa power tiller 104 kwa vijiji 102 vya wilya ya Mbarali ili kuongeza uzalishaji katika kilimo. https://youtu.be/jMfpqc3BUAc

  Simu.tv: Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, kazi, vijana ajira na walemavu Jenista Mhagama ametoa muda wa miezi miwili kwa kampuni ya GS one kukamilisha ujenzi wa barabara kutoka Peramiho hadi kijiji cha Morogoro. https://youtu.be/E0GFJHK-Lnw

  Simu.tv: Mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF umefanya mabadiliko ya muundo wa utendaji wake ili kuwezesha kufikia malengo ya afya bora kwa wote.https://youtu.be/E_Rz2zNzNRI

  0 0


  KIGALI, Rwanda

  Kikao cha 29 cha Baraza la Mawaziri wa Nchi 54 zinazounda Umoja wa Afrika kimekamilika Jijini Rwanda leo huku mawaziri hao wa mambo ya nje wakisisitiza amani na usalama na utekelezaji wa haraka wa maamuzi yenye lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi na kunyanyua maisha ya wananchi barani Afrika.

  Akifugua kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Dkt. Nkosozana Dlamini Zuma amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha Afrika iko salama na ina amani baina yake na wananchi wake,  ili kufikia malengo ya kijikwamua kiuchumi barani Afrika. Aliwaasa Mawaziri hao kusimamia kikamilifu na kuharakisha utekelezaji wa maazimio mbalimbali yanayowekwa na chombo hicho muhimu kwa Afrika ili kuharakisha maendeleo ya Afrika.

  Alielezea umuhimu wa kuharakisha utatuzi wa migogoro sugu barani Afrika ambayo sio tu inahatarisha usalama wa raia wa maeneo hayo, lakini pia husababisha raia hao kupoteza makazi yao ya kudumu na kukimbilia nchi nyingine, tatizo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya bara la Afrika.

  Alikemea mgogoro unaoendelea Sudani Kusini na kukumbusha Mawaziri hao ahadi ya Umoja wa Afrika iliyowekwa na nchi wanachama wakati wakiadhimisha miaka 50 ya umoja huo ya kunyamazisha bunduki ifikapo mwaka 2020.

  “Waheshimiwa Mawaziri, unawajibu wa kuweka dhamira ya dhati ili ku timiza ahadi hiyo kwa Waafrika na kwa vizazi vijavyo barani mwetu“ alisema. gt5“

  Dkt. Zuma akiwa na mwenyeji wa Kikao hicho cha mawaziri, Mhe. Louise Mushekiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda kwa pamoja walihimiza suala la ulinzi na usalama barani Afrika lina umuhimu wa kipekee na ndio maana kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 27 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika nchini Rwanda imejijkia kwenye haki za binadamu hususan haki za wanawake.

  “Tutumie kauli mbiu hii kama chachu ya kukataa kabisa migogoro barani kwetu, na pale inapoanza tuwahi kuitafutia ufumbuzi kabla haijaeuka kuwa vita“ alisema Kamishna Zuma kwa kumalizia.

  Akitoa maoni yake kuhusu msisitizo wa amani na usalama kwenye kikao hicho cha siku mbili, Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki  alielezea kuwa Serikali ya Tanzania inafuatilia kwa karibu amri ya kusitisha mapigano iliyotolewa na viongozi wakuu wawili wa Sudani ya Kusini, yaani Rais Salva Kiir na makamu wake. Alisema ni hatua muhimu ya kuhakikisha usalama wa raia na kuleta amani ya kudumu nchini humo.

  Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika kilitanguliwa na Kikao cha Mabalozi wanaowakilisha nchi zao kwenye makao makuu ya UA nchini Ethiopia. Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kuanza tarehe 17-18 Julai, ambapo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais atamwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Maufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la korosho uko pale pale na unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu wa mwaka huu hivyo ameitaka Bodi ya Korosho kusimamia uamuzi huo.

  “Watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnatakiwa kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanafuatwa. Malengo yetu ni kumpunguzia mkulima mzigo wa tozo nyingi alizokuwa anakatwa,” alisema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 16, 2016) wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mtwara pamoja na taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao la korosho zilizowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.

  Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.
   “Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.

  Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.

  “Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha.

  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Francis Gatare alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ,Francis Gatare mara alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na SerIkali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli Katika Mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda,Francis Gatare kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda mara baada ya Kuwasili nchini humo kwa ajili ya Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika Mkutano huo. (Picha na OMR).

  0 0

  Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Tabora, Hawa Mwaifunga (wa tatu kulia) akizumuka pamoja na Wakina Mama wa Mkoa huo, wakati hafla ya Uzinduzi wa mradi wa mafuta ya Alizeti kwa kikundi cha Wakinamama kiitwacho Wema Group, uliofanyika katika kata ya Malolo Mkoani humo.
  Sehemu ya Wanachama wa Kikundi hicho cha Wema Group, wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora, Hawa Mwaifunga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
  wa viti maalum mkoa wa Tabora, Hawa Mwaifunga akijadiliana jambo na Mmoja wa Wajumbe wa Chama hicho.


  0 0

  Kikao cha NEPAD kikiendelea
  Dkt. Ibrahim Mayaki, Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Maendeleo Afrika
  KIGALI, Rwanda: Afrika inahitaji juhudi za pamoja ili kukuza sekta ya viwanda ambayo itasaidia kwa kiasi kubwa kunyanyua uchumi wa bara la Afrika na hatimaye kupunguza umaskini na kuleta maisha bora.

  Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa NEPAD, chombo cha utendaji cha Umoja wa Afrika, Dkt. Ibrahim Mayaki wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Umoja wa Afrika zilizopo kwenye mpango huo wa maendeleo barani Afrika.

  Kwenye upande wa ajira na viwanda kwa mfano, Dkt. Miyaki alisema kuwa bara la Afrika kwa sasa ndilo lenye vijana wengi kuzidi mabara mengine duniani hivyo kuna nguvu kazi kubwa ambayo isipotafutiwa mpango mahsusi wa ajira kutazidisha umasikini barani humo. Viwanda vya Afrika vikiongezeka, ajira kwa vijana zitapatikana, uzalishaji utaongezeka na biashara ndani ya Afrika itashamiri.

  “Changamoto kubwa barani Afrika ni biashara, ambapo nchi haziuziani bidhaa zake, miundombinu hafifu na umasikini uliokihiri” alisema na kuongeza kuwa wakati muafaka umefika kwa Afrika kuweka mikakati endelevu ya pamoja baina ya nchi za Kiafrika ili kuhakikisha changamoto hizi zinatafutiwa ufumbuzi.

  Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa Mpango wa Maendeleo Afrika (NEPAD) uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Afrika Jijini Kigali Rwanda, wajumbe walielezwa kuwa biashara ina nafasi kubwa ya kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda barani Afrika iwapo misingi imara ya kuendeleza biashara na viwanda itazingatiwa.

  Akizungumzia hali halisi nchini Tanzania, Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye alimwakilisha Mhe. Rais Magufuli kwenye mkutano huo, alisema “NEPAD pia wametambua kwamba biashara ya ndani barani Afrika inaendelea kuwa na jukumu kubwa katika ukuaji wa uchumi na viwanda vya nchi zetu za Kiafrika”.

  Hivi karibuni Waziri Mahia alitangaza Bungeni kuwa Wizara yake sasa inaweka mikakati madhubuti kwa ajili ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye muelekeo wa uchumi wa viwanda (Economic Diplomacy of Industrialization) ambao utazingatia dhamira ya Serikali ya Tanzania kunyanyua sekta ya viwanda.

  “Nimewaelekeza wasaidizi wangu wamualike maalamu wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa ili aje kutuelezea umuhimu wa agenda hii ya biashara na uchumi wa viwanda nchini kwetu” alisema Waziri Mahiga.

  Alimalizia kuwa “ili utekelezaji wa mkakati wa Diplomasia ya Uchumi wa Viwanda ufanikiwe, ni muhimu Serikali nzima na nchi kwa ujumla kuwa thabiti kwenye kutekeleza sera za viwanda na za uchumi na kuzingatia misingi ya kufanya biashara iliyoelezwa hapa na wataalamu”.

  Akielezea umuhimu wa Afrika kukuza viwanda kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Dkt. Carlos Lopez alisema kuwa japokuwa Afrika imechelewa kufanya mapiduzi ya viwanda ikilinganishwa na yale ya Ulaya miaka 200 iliyopita, bado Afrika ina nafasi kubwa ya kunyanyua uchumi wake kupitia viwanda na biashara ya ndani baina ya nchi zake.

  Kilele cha Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kufunguliwa tarehe 17-18 Julai ambapo Wakuu hao wanatarajiwa kupitisha ajenda kadhaa ikiwemo uchaguzi wa Kamishna na Kauli Mbiu ya mwaka huu ambayo ni Haki za Binadamu, Haki za Wanawake.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  17 Julai 2016.

  0 0

  Asalaam Aleikhum,
   Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma zote.

  Ni wiki mbili kamili zitakazotimia leo majira ya saa nane usiku. Muda huo bila shaka nitakuwa katika  anga la dunia nikisafiri kuelekea New Delhi nchini  India kupitia Muscat Oman kwa ajili ya matibabu yangu ya macho.

  Usiku wa siku kama ya leo (yaani Jumapili ya tarehe 3-7-2016) niliamka usiku kwa ajili ya daku, Ndipo nilipogundua jicho langu la kushoto halioni kabisa na  jicho langu la kulia lina uoni wake ulikuwa mdogo.Ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu.

  Najua madaktari mbali mbali wa hapa nchini walifanya kila jitihada za kunusuru macho yangu ila bado ufumbuzi wa tiba yangu bado haujapatikana. Ndio maana naenda kujaribu India.na Insha Allah Mungu atanivua mtihani huu.

  Kiukweli hawa madaktari niwashukuru sana kwa jitihada zao.Rafiki yangu na kaka yangu Dkt. Mohammed wa wizara ya afya, Dkt. Mahunda wa Ocean Road, Dkt. Dalla, Dkt. Chibuga na Dkt. Hassan wa CCBRT na pia Dkt. Datoo wa clinic ya pale Shoppers Plaza Miikocheni. Vile vile Madaktari wa Kituruki pale katika hospitali yao ya International eye clinic maeneo ya Moroco pamoja na wauguzi wao.Mungu atawalipa Insha Allah.
  Kipekee niwashukuru ndugu na rafiki zangu wa KT shop. Hapo mimi ndio maskani yangu jioni.Hawa ni zaidi ya binadaam. Kisasa tungesema show nzima ya safari wanasimamia wao.Wamefanya jitihada zote na kiukweli bila wao sijui ingekuwaje.Kwa wiki zote mbili wamekimbizana na mimi ugonjwa wangu bila kuchoka.

  Pia niishukuru ofisi yangu klabu ya Simba kwa zaidi ya wema walionifanyia.Niwashukuru viongozi wote, Friends of Simba.wanachama na wapenzi wote wa Unyamani kwa kila jambo na dua zao walizonifanyia..Kiukweli sijutii kupenda na kufanya kazi Simba.

  Niishukuru pia serikali ya nchi hii. Nimepokea salaam kutoka kwa Waziri wangu wa michezo.Mhe Nape. Salaam toka kwa waziri na naibu waziri wa afya.Mh Ummy  na Dkt. Kigwangallah. Nimepokea pia salam toka kwa rafiki zangu manaibu waziri Mh Mavunde na Dkt. Possi.

  Lakini kipekee kwa waziri wangu wa mambo ya ndani ya nchi. mtani wangu Mh Mwigulu Nchemba ambae yeye mwenyew alikuja kuniona na kwa niaba ya serikali ameahidi kunisaidia kwa kila hali niweze kupona.
  Na kwa hapa nisiache kumshukru mwambata wetu wa afya katika  ubalozi wetu nchini India.Dkt.  Goroka kwa kusaidia kupatikana kwa hospitali India.Pia nimshukuru Profesa Mohamed Janabi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali Taifa Muhimbili kwa ushauri wake wa kitaalam (nafurahi kusikia jana amethibitiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo nyeti, homgera sana Prof! Unastahili kabisa) .sambamba na daktari wetu wa Simba.
  Sitatenda haki kama sitawashukuru viongozi wakuu wa TFF Rais Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa kwa kila jambo walilonifanyia. Kipekee niwashukuru viongozi wa dini. mashekh na maustaadh kwa dua zao kwangu.sambamba na wachungaji ambao walikuja hadi kwangu kuniombea..Asanteni sana  watu wa Mungu.
  Nisisahau kuwashukuru watani zangu Yanga kwa mchango wao kwangu... Hususan mropokaji 😃😃 wao Jerry Muro.

  Nita-mmiss sana kwa fujo na kebehi zake. Ninamuomba awaandikie TFF kuomba radhi na kisha  yeye naye  ajirekibishe kidogo bana....Nna imani TFF  nao wanaweza kupitia kamati zao wanaweza kuangalia namna sahihi ya kulimaliza hili kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini. Muhimu Jerry apime tu kauli zake. Mpira si kashfa wala kebehi za kuudhi..na si uadui hata kidogo.

  Mwisho niwashukuru ndugu zangu wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) chini ya mwenyekiti wetu Mohamed Bhinda. Hawa ni Alfa na Omega kwangu Kuanzia niliokuwa nao vjana wa Al-Ahly hadi KFDF. Pamoja nao watu wangu wa nguvu.whatsapp groups zote ambazo zimeniombea sana na kunifariji katiika kipindi hiki kigumu.sambamba na kuja kunijulia hali.

  Nikiwasahau wanahabari nitakuwa wa ajabu..Wamefanya kazi kubwa ya kuwahabarisha na kuwapa maendeleo yangu kila siku kupitia vyombo vyao.

  Asanteni sana wote! My family. ndugu zangu. jamaa na marafiki wote.nimejua kwa sasa Haji nna watu na nnamuomba mungu niendelee hivihivi na tabia zangu njema nizilojaaliwa na Manani.Msiache kuniombea kwa kila hatua.kuanzia safari yangu.matibabu na kuiombea familia yangu inayobaki hapa nyumbani.

  Nawapenda sana. Mungu awabariki sana.

  Haji S.Manara

  Safarini India

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Profesa Mohamed Janabi (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( The Jakaya  Kikwete Cardiac Institute ) iliyoko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
  Profesa Janabi, ambaye pia ni daktari Mkuu Binafsi wa Rais Mstafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa akikaimu nafasi hiyo toka kuanza rasmi kwa taasisi hiyo Septemba 2015 na inayoendelea kujizolea sifa kwa huduma zake za moyo  ambazo awali zilipatikana nje ya nchi. Tasisi hiyo hivi sasa inajitegemea.


  Taasisi ya Jakaya Kikwete inatoa matibabu pamoja na  mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya Upasuaji wa Moyo , Usingizi na Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili( MUHAS) na taasisi za moyo  mbalimbali duniani. 


  Hivi majuzi Chuo cha Magonjwa ya Moyo cha Marekani (American College of Cardiology) kimemteua Profesa Janabi kuwa mwanachama (Fellow of American College Cardiology) wa taasisi hiyo yenye wanachama mabingwa 52,000 dunia nzima, akiwa mtu wa kwanza nchini kutunukiwa FCC.
  Taasisi hiyo ina matawi (Chapters) dunia nzima isipokuwa Afrika. Afrika Kusini wana mpango wa kufungua Chapter ambapo ili kuianzisha tawi wanahitajika wanachama sio chini ya 20.
  Kwa mujibu wa Profesa Janabi, hapa Afrika Mashariki juhudi hizo zimeanza ila kwa sasa Kenya ina Fellows wanane na Tanzania ni mmoja pekee ambaye ni  yeye Profesa Janabi. Wanahitaji fellows wengine 11 kutimiza idadi ya kuwa na tawi.
  "Kuna faida nyingi sana kuwa kwenye taasisi hiyo katika kupata elimu ya magonjwa ya moyo, uwezeshaji rasilimali watu (capacity building) na kadhalika.
  "Sisi tuna bahati kwani Makamu wa Rais wa ACC Profesa Mike Valentine kutoka Central Virginia Marekani aliwahi kuwa mwalimu wangu. Yeye alikuja hivi majuzi kwenye kongamanoi letu (2nd East Africa Cardiology Conference) na pia alianzisha mchakato wa wa kuanzisha chapter ya Afrika mashariki iwe hapa Tanzania kutokana na mafanikio yanayoendelea JKCI" Profesa Janabi, ambaye sasa ni  Prof. Mohamed Janabi MD., MTH., PhD., FACC,  ameiambia Globu ya Jamii.
  Profesa Janabi  ni mmoja kati ya viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za serikali ambao  waliteuliwa kushika nyadhifa July 16,  2016 na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  Wengine walioteuliwa ni  Mhe. Augustino Lyatonga Mrema ambaye  ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Prof. William R. Mahalu aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Prof. Angelo Mtitu Mapunda ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

   Wengine walioteuliwa ni Sengiro Mulebya (Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama), Oliva Joseph Mhaiki (Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Gaspar Rutaindurwa (Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Charles Rukiko Majinge (Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili) na Dkt. Julius David Mwaiselage ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  0 0

  Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia bidhaa yake ya Dodoma Wine mwishoni mwa wiki imezindua mvinyo mpya uitwao' Dodoma Rose Wine '. Dodoma Rose ni mvinyo wenye rangi ya pink na rahisi kunywa huku ukiwa na harafu ya kuvutia ya ‘candy floss na ‘raspberry. Mvinyo huu ni unakuwa bora pale unapotumika ukiwa kwenye nyuzi 10 na ukitumia chakula chenye mwanga kidogo. Dodoma Rose inapatikana Tanzania nzima katika ujazo wa 750 ml kwa bei ya rejareja ya Tshs 10,000:00. 

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine, Bi Warda Kimaro, alisema, "Dodoma Wine imekuja na kauli mbiu ya Onjeni ladha tofauti! Ladha tofauti si tu ya kile cha kipekee kutoka Dodoma Wine lakini pia ni wito kwa ajili ya walaji kujaribu bidhaa tofauti za Dodoma Wine na kuchangua ipi ambayo ni bora kwao. Dodoma Wine kwa sasa inapatikana katika vinywaji nne tofauti vya kipekee na vya kufurahisha; Dodoma Dry Red Wine, Dodoma Dry White Wine, Dodoma Natural Sweet Wine & leo tumezindua Dodoma Rose Wine. Dodoma Wine si tu mvinyo ambao unakidhi viwango vya Kimataifa pekee, lakini ni mvinyo wa Tanzania kuwa inatambua urithi wake ".

  Bi Warda alielezea zaidi kuwa, mbali na Dodoma kuwa mji mkuu wa nchi yetu; lakini pia ndio nyumbani kwa mivinyo ya Tanzania kwa kuzalisha mvinyo wa pili mkubwa katika Afrika kusini mwa Sahara, kwa hivyo kanda hii inastahili kuwa na mvinyo wenye jina lake na ndio sababu ikaitwa Dodoma Wine kuonyesha mizizi yake na kutambua urithi wetu. Dodoma Wine ilizinduliwa 2010 Na inatengezwa kutoka kwa zabibu bora kabisa zinazolimwa na wakulima wetu wa Tanzania na hivyo kufanya kuwa kinywaji laini na tamu.

  Akiongea zaidi jinsi kampuni ya TDL inavyounga mkono wakulima wa zabibu, Mkurungenzi Mtendaji wa TDL Devis Deogratius alisema, ‘Wakulima wa zabibu walikuwa na hali ngumu hapo zamani lakini kupitia miradi tumeweza kuwainua wakulima sio tu kuwapa soko la uhakika pekee, lakini pia kwa kuwapa ujuzi wa kulima zabibu kupitia mtaalamu wetu wa kutengeneza kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz, ambaye leo tuko naye hapa’.


  Mtengenezaji wa kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz alipata nafasi ya kuwatembeza wangeni waalikwa na kuwapa uzoefu wa kuonja mvinyo mbali mbali ya Dodoma Wine.

  Devis alimalizia kwa kuwaomba wateja kuijaribu mvinyo wa Dodoma Wine, na sana sana wakati kampeni ambazo zitakuwa zikifanyika kwenye baadhi ya bar na supermarket jijini Dar es Salaam ili kuweza kutambua ni mvinyo ngani unaowafaa. Aliongezea kuwa uzinduzi huu wa Dodoma Rose Wine ni uthibitisho wa Mafanikio yanayotokana na mvinyo wa Tanzania pamoja na wakulima wa zabibu.

  Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mtaalam wa kutengeza mvinyo wa Dodoma Rose Erick Schlunz akiwaelezea wageni waalikwa sifa na ladha ya mvinyo huo mpya uliozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Cheers: Wageni waalikwa wakigonganisha glasi kufurahia uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO wakipongezana baada ya kufanya uzinduzi.


  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampuni ya NAS-DAR AIRCO, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiikaribisha kampuni hiyo katika mkoa wake kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria wa usafiri wa anga.

  Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO, Salim Ajib akizungumza kuhusu kampuni ya NAS-DAR AIRCO ambayo itakuwa ikifanya kazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

  Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya NAS-DAR AIRCO, David Handerson akielezea jinsi ambavyo kampuni yao imejipanga kutoa huduma bora nchini.

  0 0


  Teknolojia ya masomo ya VETA ya Airtel VSOMO mkoani Mbeya wavutia wengi.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wametambulisha mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa njia ya simu za mkononi mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki hii huku mfumo huo ujulikanao kama Airtel VSOMO yaani VETA SOMO ukiwa tayari umeandikisha vijana zaidi ya elfu kumi tayari kuchagua kusoma kozi mbalimbali za VETA tangu kuzinduliwa kwake mwaka huu mei.

  Akiongea wakati wa hafla fupi ya kutambulisha wa mfumo wa Airtel VSOMO katika Ukumbi wa VETA Mbeya Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Kipawa Eng, Lucius Luteganya alisema “Airtel na VETA tumeshafanya utambulisho kwa mikoa mingine minne ikiwemo Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Arusha na leo tuko Mbeya. mpaka sasa zaidi ya vijana 150 mkoani Mbeya wameshajiunga na mtandao wa VSOMO ili kuanza kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu umekubalika hapa hata kabla hatujafika kuutambulisha”

  “ninatoa wito kwenu vijana kujitoa na kuchangamkia FURSA hii inayoletwa kwenu na VETA kupitia mtandao wa Airtel ili muweze kujiajiri kupitia FURSA ya Airtel VSOMO. alisema Eng Luteganya

  Kwa Upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Bw, Charles Mwakalila kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Bw Amos Makalla alipongeza Mradi wa Airtel VSOMO na kubainisha kuwa mfumo huo ni Muarobaini wa suluhisho la kusaidia vijana wengi kupata elimu ya ufundi stadi hasa kipindi hiki tunapoekea kwenye Uchumi wa Viwanda kama ulivyo mkakati ya serika ya Jamuhuri wa Muungano Tanzania

  “hii ni program nzuri sana tukiwa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda kama ulivyo mpango mkakati wa serikali, naamini tutahitaji watendaji wengi sana kwaajili ya viwada hivyo wenye ujuzi kutoka VETA. Nakumbuka hivi karibuni Naibu Waziri wa elimu teknojia na Mafunzo ya Ufundi Eng, Stella Manyanya alitoa tamko kwa mkuu wa VETA Mbeya, akisisitiza VETA ihakikishe inasajili wanafunzi mara mbili ya waliopo, hivyo kupitia mradi huu wa Airtel VSOMO wa masomo ya VETA kwa njia ya simu utasaidia sana VETA Mbeya kusajili hata mara nne ya idadi iliyopo”

  “naweza kusema Airtel VSOMO ni muarobaini wakupunguza changamoto ya ukosefu wa wataalam na watendaji wenye ujuzi tunapoelekea kwenye uchumi wa Viwanda” alisisitiza Bw, Mwakalila

  Nae mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Straton Mushi alisema “Mradi wa Airtel VSOMO uko chini ya Airtel FURSA ili kuwasaidia vijana kujisomea kozi za ufundi stadi kama vile ufundi wa pikipiki, ufundi simu, maswala urembo, ufundi wa kuchomelea na aluminium na kujipatia ajira papo kwa hapo, Airtel tutahakikisha huduma hii inawafikia wengi kupitia mtandao wetu ulionea hapa nchini”

  Airtel VSOMO nimfumo wa utoaji wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu za mkononi uliobuniwa kwa ushirikiano kati Airtel na Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hivyo kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa.

  Meneja wa Mradi VSOMO toka VETA kipawa Bw, Gosbert Kakiziba (wapili toka kulia) akimuonyesha Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya bw Charles Mwakalila (wakwanza kulia) teknolojia ya masomo ya VETA kwa njia ya simu za Airtel wa VSOMO unavyofanya kazi wakati wa haflya ya kutambulisha kwa vijana huduma hii mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Stratom Mushi na Mkuu wa chuo VETA Kipawa ambae ni Msimamizi wa Mradi huo wa VSOMO Eng, Lucius Luteganya.

  Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya bw, Charles Mwakalila (wakwanza kulia) akibonyeza kitufe cha simu ili kuzindua teknolojia ya masomo ya VETA kwa njia ya simu za Airtel wa VSOMO wakati wa haflya ya uzinduzi iliyofanyika mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. aliyemshikia simu ni Meneja wa Mradi huo wa VSOMO toka VETA kipawa Bw, Gosbert Kakiziba (wapili toka kulia) na wengine wakishuhudia ni Mkuu wa chuo VETA Kipawa ambae ni Msimamizi wa Mradi huo wa VSOMO Eng, Lucius Luteganya na Mkuu wa Mauzo wa Airtel Mbeya Bw, Stratom Mushi.
  Picha ya pamoja ya uzinduzi wa Airtel VSOMO ni Afisa elimu wa Mkoa Mbeyabw Charles Mwakalila (katikati) akiwa na waalimu wa VETA pamoja na baadhi ya vijana walijitokeza wakati wa haflya ya kutambulisha kwa vijana huduma hiyo mkoani Mbeya katika chuo cha VETA mwishoni mwa wiki. hii itawewawezesjha vijana kusoma kozi za VETA kwa njia ya mtandao wa Airtel. 

  0 0

  Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa Barmedas Tv ya Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

  Kifo chake kimesababisha majonzi makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waandishi wa habari Jijini Mwanza ambao baadhi yao walipitia mikono ya Sokoro aliefahamika kwa jina maarufu la Mwalimu kutokana na ujuzi wake katika kufundisha nyimbo za Injili na ubobeaji wake katika taaluma ya habari.

  Enzi za uhai wake alikuwa Mwalimu wa kwanza wa Kwaya ya AICT Makongoro waliowahi kutamba na wimbo wa Kekundu huku pia akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza katika kituo cha luninga cha Barmedas Tv Cable ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa njia ya cable tu kabla ya hivi karibuni kupatikana katika ving'amuzi mbalimbali.

  Mwalimu Charles Sokoro alizaliwa mwaka 1965 na mauti yamemfika mwaka huu 2016 akiwa na miaka 51. Ratiba ya Mazishi ni kama ifuatavyo;

  1.Siku ya Jumatatu (18/7/2016 ) saa 10:00 jioni, Mwili wa Marehemu kuwasili kutoka hospitalini Bugando kuelekea Kanisa La AICT Makongoro


  2.Siku ya Jumanne (19/7/2016) Kanisa La AICT Makongororo
  ~Saa 6:00 mchana IBADA ya Kumuaga Mareemu
  ~Saa 7:30 mchana Safari ya kuelekea Malaloni (Makaburini Kitangiri)
  ~Saa 8:30 Chakula na baadaye kuhitimisho.
  Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.

  Ni juzi tu Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba mwingine wa kaka yetu sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha midomo wazi tunahisi km ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.

  Nani asiye mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli alikuwa mcheshi asiye na makuu.

  Aliipenda taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.

  Hakuonyesha umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani asiyejua uwezo wake.kwenye kupiga kinanda?.

  Nani asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?

  Kipindi chake cha ngoma asilia pale Barmedas kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.

  Tutakukumbuka daima tulikuoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo haupo nasi. Huu ni wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu kwa mikono yetu miwili.
  AMINA!
  NAEDWIN SOKO;

  MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).

  0 0

  Gari la Mwendo wa haraka lenye namba za usajili T 968 DGV limegongwa na gari aina ya Cresta lenye namba za usajili T 295 BVC leo katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salam. 
  Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni Dereva wa gari dogo aina ya Cresta kutokuangalia vizuri wakati anavuka barabara ya mabasi yaendayo haraka katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam.

   Gari aina ya Cresta lenye namba za usajili T 295 BVC linavyoonekana katika picha baada ya kugonga gari la mwendo haraka katika eneo la kisutu jijini Dar es Salaam leo.

older | 1 | .... | 1287 | 1288 | (Page 1289) | 1290 | 1291 | .... | 3282 | newer