Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1283 | 1284 | (Page 1285) | 1286 | 1287 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(Katikati) akiongea na wadau wa utamaduni kutoka UNESCO pamoja na Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Louise Crayssac katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Halvor Storrusten katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya Utamaduni nchini, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akiwa katika picha na wageni kutoka UNESCO na Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa baada ya kumalizika kikao kilichokuwa kikijadili mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jinini Dar es Salaam.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea Salaam ya Kijeshi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP. Dhahiri Kidavashari alipowasili Julai 8, 2016 katika Uwanja wa Ndege wa Songwe tayari kwa kufunga Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Julai 9, 2016 katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mkoani Mbeya (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja (kulia) akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Jijini Mbeya jana jioni Julai 8, 2016 (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge akiongea na wananchi wa kijiji cha Nangero wilaya ya Namtumbo alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na kusikiliza kero zao
  Sehemu ya wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda wakiwa kwenye mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
  Mbunge wa jimbo la Namtumbo amabye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano,Uchukuzi na Ujenzi Mhandisi Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda wakati mkuu wa mkoa wa Ruvuma alipofanya ziara kwenye vijiji kusikiliza kero za wananchi
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akiongea na wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda wilaya ya Namtumbo leo wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka na hifadhi ya msitu wa Kipiki.
  Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akijibu baadhi ya hoja za wananchi wa vijiji vya Mhangazi na Kitanda kuhusu uwepo wa mgogoro wa mpaka na hifadhi ya msitu ya Kipiki wakati mkuu wa mkoa wa Ruvuma alipofanya ziara kutembelea eneo hili.

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe  amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.


  Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.

  Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati

    “Niwaombeni suala la kilimo mlipe  msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.

  Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

   “ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.

  Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi lakini pia kuchangia pato la Taifa.

  Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao

  Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.

   “Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

  Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya hiyo.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amefanya uzinduzi rasmi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa Seashells Millenium Hotel, Jijini Dar es salaam

  Shirika hilo lililoanzashwa na Mwanafuzi wa fani ya Udaktari, Juliana Busasi limefanikiwa kufikisha huduma zake za afya na elimu ya afya kwa watanzania Zaidi ya 1327, likiwa na Dira ya Kuboresha Afya na Ustawi Nchini na kuweka mikakati imara kwa ajili ya Kuboresha afya Tanzania katika Nyanja kuu tatu ambazo ni Kuongeza Ubora wa Huduma za Afya zinazotolewa Nchini, Kueneza elimu juu ya kupambana na changamoto mbalimbali za Afya, Kuboresha mipango mikakati ya Kujikinga na magonjwa ambukizi na yasiyo ambukizi kupitia program ya mpya iitwayo NURU YA AFYA.

  Dkt. Kigwangalla aliunga mkono jitihada hizo za TAHMEF na kwa kutambua uhumimu wa jambo hilo, alichangisha fedha kwa ajili ya Kutoa msingi mzuri kwa shirika hilo ili kufanikisha Juhudi za Kuboresha Taifa katika Nyanja za Afya.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimpongeza Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi kwa jitihada anazofanya za kusaidia jamii katika nyanja ya Afya na Tiba.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akihutubia katika Uzinduzi huo.
  Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi akizungumza.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na baadi ya washiriri na viongozi wa Shirika hilo.

  0 0

  SIMU TV: Shirika la umoja wa mataifa la kushunghulikia idadi ya watu duniani UNFPA kwa kushirikiana na serikali linatarajia kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani ifikapo July 11 mwaka huu; https://youtu.be/uJBAGpmape8
  SIMU TV: Watanzania wahimizwa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya kimataifa ya mafuta na gesi asilia ili kutambua fursa zilizopo katika sekta hiyo; https://youtu.be/z5xMTO1qvy8
  SIMU TV: Wakazi wa eneo la Tukutuku mkoani Tabora wamuomba mkuu wa mkoa wa Tabora kusitisha zoezi lake la kuwaondoa eneo hilo; https://youtu.be/oEabKNkC128
  SIMU TV:  Inaelezwa kuwa Miili ya watu saba kati ya tisa waliopoteza maisha katika ajali ya boti iliyotekea hivi karibuni katika mto Ruvuma yapatikana; https://youtu.be/LMwr76JtjLA
  SIMU TV: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe aipa ruhusa RITA kufuta bodi za wadhamini takribani 500 zilizobainika kutokuwa hai; https://youtu.be/f7oFLFIVGTM
  SIMU TV:  Hatimaye serikali yakamilisha ujenzi wa kivuko cha Kibunduguru  kilicho katika kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe mkoni Mbeya ; https://youtu.be/JbJRrlHlMlM
  SIMU TV: Serikali ya Tanzania yasema haitaweka saini katika mkataba wa Economic Partnership agreement EPA baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya ili kulinda uchumi wa nchi;https://youtu.be/DxtLp5wDRZQ
  SIMU TV: Waendesha bodaboda wa mkoa wa Mtwara washauriwa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ili kupata bima ya afya kwa bei nafuu; https://youtu.be/aBJIWuFm0q4
  SIMU TV: Serikali ya Zanzibar pamoja na serikali ya China zaingia makubaliano ya ujenzi wa shule ya kisasa katika kukuza elimu visiwani humo; https://youtu.be/8UtnlrlfKbc
  SIMU TV: Inaripotiwa kuwa  mtoto wa mmoja wa miaka minne visiwani Zanzibar afanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi ; https://youtu.be/-k20-1H7Lg4
  SIMU TV: ligi ya mpira wa wavu jijini Dar Es Salaam inatarajia kuendelea leo kwa michezo mitatu itakayofanyika katika uwanja wa taifa: https://youtu.be/ipAwsKXl5lo
  SIMU TV :Fainali ya kukata na shoka ya kombe  la  mataifa ya Ulaya inatarajia kufanyika na kushirikisha nchi mbalimbali kutoka nje ya Ufaransa: https://youtu.be/wAMv6cyYkEE
  SIMU TV:Fahamu mambo mengi kutoka kwa wadau wa michezo  wakikujuza kuhusu mashindano ya shambalai mkoani Tanga: https://youtu.be/i1j_qJHcL00

  0 0

  Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

  Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi  (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

  Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.

  Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa upande wa kipa bora ni Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).

  Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons). Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).

  Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba). Waamuzi bora katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewapongeza wateule wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. "Kama wadhamini tuna matumaini makubwa kuwa  msisimko wa ligi hii utazidi kuongezeka katika msimu ujao na kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka wanaoifuatilia hapa nchini na nje ya nchi."

  Alisema Vodacom itaendelea kudhamini ligi hiyo kubwa ya soka nchini  ili kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji nchini. Pia kuwawezesha wachezaji kujipatia ajira na kuboresha maisha yao kupitia sekta ya michezo bila kusahau kuwapatia burudani wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (wapili kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu,Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Afoisa Matekelezo wa Mfuko huo Gladness Madembwe, Afisa Uhusiano, Zaria Mmanga, Afisa wa Fedha, Edward Kerenge na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (pichani katikati), akimpatia maelezo mwananchi huyu Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.
   Afisa wa Fedha wa WCF, Edward Kerenge, (kulai), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Mfuko huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

  0 0
 • 07/09/16--04:24: MAGIC FM BAMIZA TOP 20 CHART

 • 0 0


   Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Bunge  alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya sabasaba.
   Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akeielekeza jambowakati alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya sabasaba.  
   : Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wakati alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya sabasaba.
  Mke wa Rais wa Awamu ya tatu mama Anna Mkapa akimsikiliza Rais Msataafu ya awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati  alipotembelea banda la EOTF katika maonesho ya kibiashara ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam
  Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kulia akiuliza jambo kwa afisa wa Shirika la maendeleo ya Petroli nchini juu ya utendaji kazi mbalimbali wa shirika hilo.( 

  0 0


  0 0

  KAMPUNI ya Chemi & Cotex inayotengeneza bidhaa za za afya ya Mdomo ya Whitedent imezindua mchezo wa bahati nasibu wa kujishindia moja ya magari 25 aina ya Suzuki Alto K10 jijini Dar es Salaam leo.

  Bahati nasibu hiyo imezunduliwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru wakati wa kusherehe madhimisho ya  miaka 25 ya Whitedent jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa  Kiwanda cha Chemi & Cotex kimeadhimishi miaka yake 25 kuwaajili ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 

  Nae Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan amesema kuwa katika kusherekea miaka 25 ya bidhaa ya Whitedent wametaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio ya kampuni yao.

  Amesema kuwa wananchi watawashirikisha kwa kuchezesha baahati nasibu hiyo ili kujipatia zawadi ya gari ambayo ni Mpya kwa kuotea ndani ya gari kuna maboksi mangapi kwa kujaza fomu ya kushiriki katika shindano hilo.

  Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa Viwanda hapa nchini ni mkubwa tunauwezo wa kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa watanzania kwa bei nafuu na pia kuuza ulimwenguni kote. amesema Swaminathan

  Shindano hili lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam pia limezinduliwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Musoma pia wanategemea kuzindua katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,Morogoro na Kigoma katika kusherekea miaka 25 ya Whitedent hapa nchini.


  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
  Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan akizungumza wakati wa sherehe za kusherekea kutimiza miaka 25 ya kampuni ya Whitent iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru akiweka maboksi ya Whitedent katika gari jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya washiriki wa shindano hilo kubashiri katika mchezo wa bahati nasibu kujua kama kuna boksi ngapi katika kila gari ambalo limewekwa maboksi hayo. 

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi.

  Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).

  Akizungumza na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.

  Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi na viwango vya Kimataifa.

  Wakati huohuo, TFF inatarajia kuimarisha Kurugenzi yake ya masoko ambako sasa ataajiriwa Mkurugenzi wa masoko na habari.

  Lengo has ni kuendana na halihalisi ya uendeshaji mpira duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.

  Lengo ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpirwa a miguu zinatokana na mpira wa miguu na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati muafaka “ Alisema Mwesigwa Selestine”

  Kwa nafasi za kazi katika TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz

  0 0

  Watangazaji wa Kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa na Kituo cha redio cha TimesFm ya jijini Dar, Sandra Temu na Raheem wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm redioni ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
  BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku. 
  Mc Pilipili akitoa kibwagizo mara baada ya kukaribishwa. 

  0 0

   Wadau kutoka Tanzania,Yusuf Dossaji, Akil Kasamali and Mustan wakiipeperusha vyema bendera yetu ya Taifa wakati walipokwenda kuangalia moja ya mechi za Kombe la Mataifa ya Ulaya, huko Nchini Ufaransa.
  Wadau wakiwakilisha ndani ya Dimba hilo.

  0 0

  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa  posho ya chakula kwa watu ambao si askari.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki  anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000  kama posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka  wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.

  Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi  anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.

  Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma zinazomkabili.


  Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha  malipo hayo hewa. 


  0 0  0 0


  0 0

  Kampuni ya ORIFLAME imezindua bidhaa zake mpya kwenye soko la Afrika Mashariki ambapo vipodozi maalum vitakavyokufanya ngozi yako kuonekana yenye kukaa na safi wakati wote kwa ngozi imeingia dukani kwa sasa.


  Bidhaa hiyo maalum ni ya kusaidia ngozi kung’aa ambapo watumiaji wa bidhaa za ngozi wameshahuriwa kutumia bidhaa hiyo kwani imetengenezwa kwa vitu halisi ikiwemo matunda,mimea na majani ya hasili na kufanya ngozi kuwa katika hali ya afya wakati wote wa matumizi.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Mary Riung amebainisha kuwa, bidhaa hizo zitasaidia watu wengi kwani zimetengenezwa kwa ubora.

  “Bidhaa hizi ni nzuri kwani zitakufanya kuweka ngozi yako kuwa nzuri ikiwemo kuondoa makunyanzi, kuondoa madoa na kufanya kuwa na rangi moja usoni. Ni bidhaa bora na itapatikana kwetu pekee katika soko la hapa Tanzania na Afrika Mashariki” alieleza Mary Riung.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra amebainisha kuwa, kampuni hiyo ambayo ilianzishwa tokea 1967 imekuwa ni miongoni mwa makampuni yanayofanya vizuri katika bidhaa zake na watu wengi wametokea kuipenda hivyo kwa bidhaa zao zote wanazotengeneza zimeendelea kuwa na ubora Duniani kote.

  Miongoni mwa bidhaa zao ni pamoja na NovAge ambayo imetengenezwa mahususi kumfanya mtumiaji ambaye ngozi yake imeonekana kuzeeka na endapo ataitumia vipodozi hivyo vitamfanya kumuondolea hali hiyo na kuonekana safi kama kijana kwani inaondoa makunyanzi ndani ya kuanzia wiki 12 huku ikiwa imethibitishwa na wataalamu kwa kuongeza ‘collagen kwa asilimia 200.

  0 0


   Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, Kozi Na. 28 ya Mwaka 2016.
   Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, Kozi Na. 28 ya Mwaka 2016 wakila  kiapo  cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoonekana katika picha wakiwa wakakamavu.
   Mgeni rasmi akimkabidhi cheti cha sifa mmoja wa Askari Wahitimu ambaye amefanya vizuri zaidi katika nyanja ya Nidhamu katika kipindi chote cha Mafunzo hayo.

   Gadi Maalum ya Gwaride la kunyakua iliyoundwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakitoa heshima mbele ya Jukwaa la Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(hayupo pichani).
   Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa karibu Maonesho mbalimbali katika Uwanja wa Gwaride kwenye hafla ya kufunga Mafunzo hayo.
   Wakufunzi kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(KMKGM) wakionesha onesho la kijasiri kama inavyoonekana katika picha.

   Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya.
   Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP - John Casmir Minja(wa pili kulia)akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa pili kushoto) mara baada ya sherehe za kufunga Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza, Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza - Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam kutoka kwa Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo Julai 9, 2016 Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.

older | 1 | .... | 1283 | 1284 | (Page 1285) | 1286 | 1287 | .... | 3278 | newer