Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1282 | 1283 | (Page 1284) | 1285 | 1286 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Dkt Leonard Maboko
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).


  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.


  Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).


  Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.

    
  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  08 Julai, 2016.

  0 0


  Dk. Charles Kimei akifurahia huduma za Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Habiba Kisaka akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB juu ya huduma wanazotoa.
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.


  0 0

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India  linalotarajiwa kufanyika julai 10 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Daud Riganda amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kwa ajili ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

  Amesema Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara hivyo ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha sekta za kilimo, viwanda, miundombinu, elimu, afya, nishati na maji.

  Riganda amesema kati ya mwaka 1990 na Juni 2016 TIC imeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.12.

  Alisema miradi hiyo inayoongoza katika kusajiliwa ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53 ni miradi ya kutoka sekta hiyo.

  Pia alisema kongamano hilo limeandaliwa na TIC  kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi nchini(TPSF), Jukwaa la Biashara la India(IBF) na Shrikisho la Biashara na Viwanda la India(FICCI).

  Alisema makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi ya tano za juu kiuwekezaji hapa nchini kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji.

  Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo ili kujijengea uwezo na kuweza kufikia malengo ya sekta ya uwekezaji kupitia viwanda.
  Meneja mahusiano Kituo cha Uwekezaji (TIC) Daud Riganda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India linalotarajiwa kufanyika julai 10 mwaka huu, ambalo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Nje Zacharia Kingu.
  Waandi wa habari wakimsikiliza Meneja mahusiano Kituo cha Uwekezaji (TIC) Daud Riganda, leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Katika kile kinachoonekana kuchoshwa na vitendo vya polisi kuwaua watu weusi huko nchini Marekani, Raia wa nchi hiyo wamefanya maandamano makubwa kupinga kadhia hiyo wanayofanyiwa watu weusi wasio na hatia. Katika maandamano hayo, baadhi ya waandamaji wakiwa na walenga shabaha (sniper) waliwaua polisi watano.

  Tukio hilo limetokea jijini Dalas, jimboni Texas ambapo polisi hao watano waliuawa na wengine sita kujeruhiwa. Mapambano kati ya polisi na raia hao bado yanaendelea na taarifa zinasema kuwa kuna mshukiwa mmoja wa walenga shabaha amejibanza katika eneo la kuegesha magari ndani ya jengo moja na amewasiliana na maafisa wa polisi akiwaeleza kuwa wasipoangalia atawaumiza na kuwaua wote kwani ametega mabomu kuzunguka eneo hilo.

  Mkuu wa polisi wa Dallas, David Brown, amesema wanawashikilia watuhumiwa ingawa si wote. Vyombo vya habari vya jimbo hilo vinasema kumetokea mlipuko mkubwa eneo hilo, lakini habari hizo hazijathibitishwa. Mkuu huyo wa polisi anasema wanamuhoji mwanamke mmoja ambaye alikuwa eneo ambalo mshukiwa ambaye bado anarushiana risasi na polisi amejibanza.
  Maandamano haya yamekuja baada ya kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile wa jimbo la Minnesota na Alton Sterling wa eneo la Baton Rouge jimboni Louisiana.

  Raisi wa Marekani, Barack Obama, akirejea takwimu zinazoonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Wamarekani weusi kupigwa risasi na maafisa wa polisi kuliko Wamarekani wazungu, amesema kuwa ubaguzi huo unafaa kumalizwa.

  ''Visa kama hivi vinapotokea kuna sehemu kubwa ya raia wanaohisi kwamba hawatendewi haki kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, kwa sababu hawatizamwi kwa njia sawa, na hili linauma''alisema.

  0 0

  ILI watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu waweze kutimiza ndoto zao za kimaisha , Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda ameiasa jamii kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto hao sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo hao.


  Ametoa rai hiyo juzi mara baada ya kujumuika pamoja katika chakula cha pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ya yakiwemo madaftari, kalamu, sabuni,vyakula na fedha kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho.

  Alisema watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wanapaswa kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine wanaoishi na wazazi wao hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuona umuhimu wa kutoa chochote alichonacho ili kuwawezesha watoto hao kuipata elimu hiyo kwa ukamilifu. 

   

  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akigawa chakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam katika kusherekea sikukuu ya Iddi. 

  “Tunashukuru kwa sasa Rais John Magufuli ametoa unafuu wa elimu bure kwa watoto katika ngazi ya msingi na Sekondari kwa hiyo kilichopo hapo ni mahitaji madogo madogo ili kumfanya mtoto aweze kufika shuleni na kuudhuria masomo, kama jamii hili ni jambo linalowezekana kabisa tukalitatua kama kila mmoja wetu atakuwa na nia” alisema Mwenda 

  Aidha katika hatua nyingine Mwenda ameahidi kutoa huduma ya mahitaji ya shule kwa watoto wanaosoma darasa la sita hadi sekondari waliopo katika kituo hicho ili kukipunguzia mzigo kituo hicho katika suala linalohusiana na masomo Mbali na hilo pia ameahidi kununua vitanda kwa ajili ya watoto hao na kuvifanyia ukarabati vitanda vilivyoharibika baada ya kuombwa na uongozi wa kituo hicho kutatua tatizo hilo lililodumu kwa muda mrefu kituoni hapo.
   
  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akijumuika pamoja katika chakula cha pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam .   Kwa upande wake Mlezi wa kituo hicho Zainabu Maunga alisema dhumuni la kuanzishwa kwa kituo hicho chenye jumla ya watoto 50, lilikuwa kutoa msaada wa malezi kwa watoto hao waliopatikana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya vifo vya wazazi wao.

  Alisema kituo hicho kinalea watoto hao wakiwemo wavulana 26 na wasichana 24 kwa kutegemea misaada ya watu mbalimbali wanaofika kituoni hapo huku akitaja changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika malezi ya watoto hao. 

  Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa eneo la kituo, mavazi kwa watoto, chakula pamoja na huduma za afya pale inapotokea mtoto kaugua hatua inayomfanya kupaza sauti yake kwa jamii kila siku akiomba imsaidie kutatua changamoto hiyo.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja. 
  Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezindua mashindano ya magari ya hapa nchini  ya 2016 na kuwataka watazania kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mchezo huo ambapo amewataka kuacha kujiweka nyuma na kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila siku. Hayo ameyasema wakati akizindua mashindano hayo ya magari yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho wilaya ya Bagamoyo ikihusisha magari 25.

  Nape amesema kuwa wanachotaka kuona ni kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano hayo na zaidi wanataka kuona wanazidi kuwavutia wageni kwenye mashindano hayo ili kuongeza utalii wandani na kuongeza pato kwa serikali pale watakapoamua kutembelea mbuga za wanyama. 

  “Nawataka watanzania kuzidi kufanya vizuri kwenye mashindano na zaidi wawavutie wageni kwani watakapokuja kwa wingi wataongeza pato la taifa pale watakapotembelea hifadhi za taifa,”amesema. 

  Naye  Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa mwaka jana waliweza kuondoa kauli ya kichwa cha mwendawazimu na walilitekeleza kama walivyomuahidi Raisi mstaafu wa awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi na mwaka huu watazidi kufanya vizuri na watabakisha ushindi nyumbani. Mashindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati  ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni  17.

  Magari hayo  17  ya Tanzania ambapo  Dar es Salaam  magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza na yatakuwa kwa muda wa siku mbili.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mtakwimu, Opiyo Mamu.

  Na Ally Daud-Maelezo.
  Mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi.

  “Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa asilimia 3.2, unga wa muhogo kwa asilimia 2.4, samaki wabichi kwa asilimia 3.8, maziwa mgando kwa asilimia 4.3, maharage mabichi yaliyomenywa kwa asilimia 6.1, kitunguu swaumu kwa asilimia 12.5, njegere kwa asilimia 6.2, viazi mviringo kwa asilimia 2.5, mihogo mibichi kwa asilimia 6.7, magimbi kwa asilimia 4.5, na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7,” amesema Kwesigabo.

  Amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa asilimia 13.8, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.4 na mafuta ya petroli kwa asilimia 4.3.

  Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita.

  Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi asilimia 8.3 mwezi Juni, 2016 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.

  Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi Juni, 2016 kutoka mwezi Disemba, 2015.

  0 0

  Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakisalimiana na Viongozi wa skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiahidi kufufua zao la zabibu Mkoani humo na kuondoa tatizo la njaa kwa kufufua skimu zote za umwagiliaji zinazolegalega na kukosa uongozi imara wakati akizungumza na viongozi wa skimu ya umwagiliaji wa Zao la zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua miundombinu ya maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.


  0 0


  Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akimkaribisha Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete alipotembelea banda hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
  Hapa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
  Rais mstaafu Jakaya Kikwete (katikati), akitoka katika banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 yanayoendelea katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo . Kulia ni Meneja wa banda hilo, Josephiner Kulwa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. Maonesho hayo yatafikia tamati kesho kutwa.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii).

  0 0

  The continent awaits one of the biggest collaborations this year as two of Africa’s fastest rising music stars get paired on the new season of Coke Studio Africa! Get ready to discover fresh sounds from Bongo’s Pop Princess VeeMoney and Nigeria’s reggae/dancehall artiste Patoranking. As if that doesn’t promise to be a killer collabo already — the duo will be produced by South African house music producer DJ Maphorisa of the “Soweto Baby” hit fame.

  It is still VeeMoney season, as she continues to rise. On the last season of Coke Studio Africa, she was paired with Nigerian singer 2Baba. After their song 'All I Need to Know' surpassed a million views on YouTube, it went on to top music charts allover Africa. 2Baba would later add her as one of the main performers on his new Disruption Africa Tour – 2016 edition.

  Vee’s collabo with Patoranking is expected to be killer! How wouldn’t it coming from Patoranking? Remember Girlie ‘O’ featuring Tiwa Savage? Could Bongo's own produce Patoranking's next biggest collaboration? Let's wait and see.

  Vanessa Mdee is East Africa’s most stylish trendsetter. She is credited for releasing a string of successful singles including Nobody But Me featuring South African rapper K.O, Never Ever and Niroge. Her songs enjoy massive airplay across Africa. She is currently Tanzania’s top female artiste and one of the most loved and followed African celebrities.

  In a breakout streak, Patoranking has enjoyed a string of successful singles including My Woman, My Everything featuring Wande Coal, Daniella Whine and Girlie O Remix featuring Tiwa Savage. His travel and tour has seen him perform in several countries recently. They include Tanzania, Mauritius, America and UK. 

  0 0

  Na Daudi Manongi

  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sikukuu za Eid al Fitr na Sabasaba zilisababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara na kuathiri wa baadhi ya shughuli za maendeleo.

  Hatua hii ilitokana na wamiliki wengi wa ‘deport’ za mafuta kufunga kwa ajili ya kushiriki sikukuu hizo.
  Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano (EWURA) Bw.Titus Kaguo wakati wa mahojiano na Idara ya Habari(MAELEZO) wakati akitoa ufafanuzi juu ya uhaba wa tatizo hilo katika Mkoa wa Mtwara lililoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

  Alisema kuwa hivi sasa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo imerejea kwani vituo vingi vimeanza kuuza nishati hiyo baada ya sikukuu hizo kumalizika.

  Bw.Kaguo alisema kuwa kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu binafsi na wahusika hao kushiriki sikukuu hiyo ilisababisha kusimama kwa shuguli hiyo, hatua ilivifanya baadhi ya vituo kukosa nishati ya mafuta na kushindwa kufanya kazi katika kipindi hiki cha sikukuu.

  Aidha amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa nishati ya Petroli na Dizeli ipo kwa wingi kwani kwa siku ya jumanne dizeli lita milioni (5) tano ziliuzwa ukilinganisha na matumizi ya nchini ya siku ambayo ni lita milioni 4.8 na kwa Petroli lita zilizouzwa ni milioni 3.6 ukilinganisha na matumizi ya nchi nzima ya petroli ya lita milioni 2.8. kwa siku.

  Aliongeza kuwa toka jumanne vituo kama Lake Oil,Tsn na Central belt vimeendelea kutoa huduma kama kawaida kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara.

  Mji wa Mtwara siku ya Jumatano ulikumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na hivyo kufanya wakazi wa mji huo kununua nishati hiyo kwa bei ya ulanguzi toka lita shilingi 1950 hadi kufikia shilingi 2500 kwa lita jambo liloathiri shughuli za maendeleo ya wananchi.

  0 0

   Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe.  Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
  Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
  wanatarajia kufuta bodi za wadhamini 180 kutokana na ukiukaji
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wakati wa uchguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi  ambavyo  havionekani kazi zake  na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Mwakyembe  amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA),  kusitisha usajili wa vikundi hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi  ambavyo viko hai na vina vigezo kwa mujibu wa sheria.

  Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo ni hatarishi kwa taifa.

  Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.
  Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa zao.

  Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.

  Amesema kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.

  0 0

  Nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari akiwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. 
  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimpokea kwa shangwe nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimkabidhi taji la maua nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. 
  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) pamoja na Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko.

  0 0


  0 0  Na Sensei Rumadha Fundi


   Kutafakari "Meditation" au katika lugha ya Sanskrit "Dhyana"  ama mtiririko wa mawazo  ni moja ya sehemu kuu Yoga inasisitiza kuidumisha katika sanaa hii ya upanuzi wa mawazo.
  Falsafa  ya Yoga inaamini kwamba ubongo wa mwanaadamu unatoa msisimko wa mawimbi ambayo huwasumbua sana binaadamu kuweza kutumia uwezo wao wa fikra katika asilimia 100 na hatimae mwanadamu hutumia tu asilimia 1, ya fikra zake na zote asilimia 99 hupotea kutokana na upungufu wa utulivu wa mawazo ya mwanaadamu (Concentration/ Focus).
  Hivi karibuni tu, uvumbuzi mpya wa sayansi ya Yoga amegundua kwamba ubongo wa mwanaadam umejengwa katika mchanganyiko wa mabillion ya "Nervr Cells, hatimae kutoa mkondo mdogo wa umeme ( tiny electric current) ijulikanayo kama "Brain waves" ambayo  hubadilika kila sekunde kufatana na mabadiliko ya nguvu za ufahamu wako katika ubongo. Mashine yenye uwezo wa kuweza soma mawimbi hayo ya ubongo hujulikana kama "EEG", au "Electroencephalogram" Chombo hiki kinapo fungwa kichwani mwa binaadamu hutowa mawimbi na kuyasajiri kupitia mashine ya computer screen na kutoa mawimbi yenye kina tofauti kutokana na nguvu za ubongo wa mtu., yaitwayo:
  Beta Wave:
   Mawimbi  ya mizunguko 13 kwa dakika ya ubongo : 
  kutokuwa na utulivu wa fikra'Stress/ Restless"
  Alpha Wave:
   Mawimbi ya mizunguko 8 kwa dakika:  
  msukumo imara kidogo wa nguvu "Steady and rythmic Amplitude".
  Theta Wave:
   Mawimbi ya  4 kwa dakika: 
  Mawazo yenye nguvu za ubongo,
   ubunifu na usanifu wa kisayansi ubongo umetulia.
   Delta Wave:
   Wimbi la 1 kwa dakika. Hapa nikupitia tu njia ya kutafakari ndio mtu huweza kufikia hatua hii ya wimbi moja kwa dakika. Ubongo wenye nguvu zisizo kawaida " Intuitive mind/ subtler mind". Moja ya ngazi hii ina uwezo wa kuwa utabiri wa matokea ya mbele kutokana na upeo  wa fikra.
  Lengo kuu la "Meditation" ni kuwa na uthibiti wa mawimbi ya ubongo kuweza kupunguza kasi yake toke a mawimbi 13 kwa sekunde hadi  wimbi  1 kwadakika na ubongo huo ndio upo katika watu wenye upeo wa fikra zilizotulia kama maji ndani ya mtungi. Maji ya mtungi au kisima yakitulia ina kuwa kama vile kioo, ukiangalia ujiona mwenyewe. Kama maji yakitibuliwa hutoawa mawimbi mengi na kusababisha mvurugano nakutoweza kuona  kimvuli chako mwenyewe au  "Reflection."
  Kupitia sauti itwayo "Matra", ubongo hutumia mbinu hiyo kama chombo cha kukufikisha pale unakotaka kwenda. Pia Yoga ina masomo ya ngazi nyingi 
  Moja ya vitu sanaa Yoga inasaidia kuweza kumudu (Control) ya hisia zako mwilini  yaani "Emotion", "propensities"  kusaidia" Secretions  of Hormones" kumudu hasira   kupitia mazoezi  yenye  utafiti wa kuiga mikao ya wanyama  kadhaa na ndege ambayo inaaminika wanatumia kwa  kujitibu  wenyewe. bila kutumia dawa. Mikao yote ya Yoga (Yoga Postures) inasaidia matatizo kama vile:
  Shindikizo la damu( High blood Pressure), uzito wa mwili (Obesity), kisukari (Diabetes) na matatizo kadhaa ya magonjwa ya wanawake. Hivyo basi, Yoga ina faida nyingi mno ambazo watu wengi hawazifahamu.
  Yoga inaamini kwamba, kuna sehemu 7 za nguvu  ndani ya mwili wa mwanaadamu kupitia uti wa mgongo  au "Kun'da'alini " katika lugha ya Sansrit ( Coiled Serpentine). Sehemu hizo ni :
  1.Muladhara Chakra: ipo katika mkia wa  ya uti wa mgongo
  2.Sva'dhis;tha' na Chakra:ipo sehemu ya kizazi (Groin area)
  3.Man'ipu'ra Chakra: ipo kitovuni.
  4.Ana'hata Chakra katika ya kifua.
  5.Vishuddha Chakra: ipo koromeo (Thyroid Gland) 6. A'jna Chakra: ipo katikati ya macho (Pituitary).
  7. Sahasra'ra Chakra: Ipo katika utosi.

  Mwafunzi anapozidi kuendelea kwa kina katika sanaa ya Yoga, ndipo anapo pita hizo sehemu ya nguvu 7 katika uti wa mgongo na hatimaye kufikia hatua ya kuwa na udhibiti wa hizo hisia zake mwenyewe au  "Propensities".

  Sayansi ya Yoga nipana sana yenye kina kirefu na filosofia yenye karne. Mazoezi ya Yoga husaidia viungo vya ndani ya mwili (Internal Organs) kama vile moyo,figo, maini, kwa kuvikanda ( massage) zaidi ya mwili wanje. Tofauti ya mazoezi ya gym na Yoga ki kwamba: Ukifanya mazoezi  gym (vigorous exercise) unatumia sana nguvu........

  0 0

  Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

  Lengo kuu la Kongamano hili ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

  Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha wafanyabiashara kutoka katika sekta zifuatazo: Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

  Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara. Makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi tano za juu kiuwekezaji hapa nchini (kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji). Kulingana na takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, Kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2.122.

   Miradi inayoongoza katika kusajiliwa na TIC katika kipindi hicho ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53% ni miradi ya kutoka sekta hii. 

  Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unakaribishwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia maofisa wafuatao: Ajelandro Sindano (ajelandro.sindano@tic.co.tz/ +255767660777) au Mr. Nestory Kissima (nestory.kissima@tic.co.tz/ +255654075953). Mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Julai 2016 saa 6:00 mchana.

  Mnakaribishwa sana kushiriki 

  0 0

  ANNOUNCEMENT
  NYTC is in the process of forming a Board of Trustees. If you, or someone you know, is interested and will be a good candidate, please do not hesitate to apply by sending your or their application and a short cover letter describing why you think you or they would be a good candidate to nytc.adhoc@gmail.com by SUNDAY July 18th
  Applications will be reviewed by the independent committee and the appointees will be announced on Saturday July 23rd 2016

  The desired candidates should have characteristics below; must be willing to be interviewed if requested; and must be able to provide references upon request. 
  ✔Have a Solid track record of high integrity and strong character. 
  ✔Have a generosity of spirit and willingness to help others grow and be successful 
  ✔A Recognized, seasoned leader
  ✔Be well-connected. 
  ✔Plays well with others.
  ✔Be willing to challenge things that don’t make sense
  ✔Be reliable and trustworthy. 
  ✔Good communicator
  ✔An active member of NYTC (Paid all their Yearly dues)
  ✔Be a law abiding Person
  --------------------------------------------------------
  Tangazo
  NYTC  iko katika mchakato wa kutengeneza Bodi ya Wadhamini. Kama wewe, au ujua mtu,  mwenye nia na atakuwa mgombea mzuri, tafadhali usisite kutuma  ombi lako au maombi yao na  barua fupi  kueleze kwa nini unafikiri  utakuwa mgombea mzuri kwa nytc.adhoc@gmail.com kabla ya Jumapili Julai 18 2016.

  Maombi yatapitiwa na kamati huru ya uteuzi na watakao teuliwa watatangazwa siku ya Jumamosi Julai 23, 2016
  Wagombea wanaohitajika wanapaswa kuwa na sifa zilizoorodheshwa hapo chini; lazima  wawe tayari kwa Usaili  pindi wakitakiwa kufanya hivyo; na lazima wawe  na uwezo wa kutaja watu wa kuthibitisha sifa zao  (references) pindi watapotakiwa
  ✔Awe na rekodi nzuri ya uadilifu mkubwa na tabia njema.
  ✔Awe na ukarimu wa roho na nia ya kuwasaidia wengine kuendelea na kuwa na mafanikio
  ✔Ana tambuliwa kama kiongozi aliebobea kimaadili
  ✔Awe na mshikamano na watu wote
  ✔Anashirikiana vizuri na wenzake.
  ✔Atoe changamoto katika mambo ambayo hayako makini/hayaeleweki
  ✔Awe mtu wa kutegemewa/ wakuaminika 
  ✔ muongeaji mzuri
  ✔ Awe mwanachama hai, amelipa Ada kamili ya uanachama
  ✔Awe mtiifu wa sheria (asiyemvunjifu wa sheria za nchi)

  Asanteni,
  Rashid Toure(Chairman)
  Charles Kilenga (Committee Member)
  Jessica Chemponda (Secretary)
  Natalia Bakilana (Committee Member)
  Asya Mwilima(Committee Member)
  NYTC Ad-Hoc Selection Committee. 

  0 0
 • 07/09/16--01:43: MILIMA YA RORYA MKOANI MARA
 • Na BMG
  Ni muonekano wa milima ambayo inapatikana katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Mita chache Kutoka Mto Mara ukiwa unatoka au unaelekea wilayani Tarime, ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma-Tarime.


  Maajabu ya milima ambayo iko pande zote mbili za barabara si kwamba yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba na kufanya abiria kuhisi uumbaji wa Mungu uliotukuka katika hii dunia.

  Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katikakati ya milima hii huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala la mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mtelemko huwa ni mtelemko kweli kwani ikiwa wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje japo ukweli ni kwamba ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika milima hiyo.

  Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu zisiiathiri milima hii (mfano katika picha) maana ni tegemeo kwa wanamara na sote twajua umuhimu wa milima kama hii ambayo ina uwepo mkubwa wa mistu ya asili.

  Tazama HAPA Picha Zaidi

  0 0

  Na Geofrey Tengeneza

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuitangaza Tanzania kama eneo bora la Utalii Duniani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo tovuti maalumu ya utalii (Online Tourism Portal) na Nyenzo maalumu ya kutangaza utalii wa tanzania kupitia simu za mkononi ( Tanzania Tourism App).

  Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Bodi ya Utalii Tanzania lililopo ndani ya jingo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

  “ Kwa hakika mnafanya kazi nzuri sana katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, endeleeni na juhudi hizo” alisema Naibu Waziri mara baada ya kupata maelezo mafupi kuhusu mbinu zinazotumiwa na TTB katika kuitangaza Tanzania kama eneo Bora la Utalii Duniani.
  Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani moja ya majarida ya utalii ya TTB yaliyopo katika Banda la TTB.
  Geofrey Meena, Meneja Masoko wa TTB akimwelezea Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Makani amna ambavyo TTB inavyotumia mbinu mbalimbali katika kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Bw. Philip Chitaunga(wa pili kulia ) akitoa maelezo kuhusu namna tuvuti maalumu ya Utalii (Online Tourism Portal) inavyofanya kazi na inavyoweza kutumiwa na wadau wa utalii kwa Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani huku afisa wa TTB Bw. Francis Malugu akisaidia kuonyesha kurasa za tovuti hiyo .
  Naibu Waziri Eng. Ramo Makani akisisitiza jambo kuhusu tovuti maalumu ya Utalii baada ya kupata maelezo kuhusu tovuti hiyo kutoka kwa maafisa wa TTB.

older | 1 | .... | 1282 | 1283 | (Page 1284) | 1285 | 1286 | .... | 3278 | newer