Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1281 | 1282 | (Page 1283) | 1284 | 1285 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Jana imekabidhi hundi ya kitita cha Shilingi Milioni 6/- kwa ajili ya kudhamini ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi, Kenya kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.
  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu, alisema wao wakiwa wadau wakubwa wa michezo nchini wameona ni fursa njema kusaidia katika ziara hiyo.
  Ziara hiyo ya mafunzo imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya (SJAK), ambapo wahariri 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini watashiriki.
  “Vodacom Tanzania tunaunga mkono juhudi za TASWA katika kuwajengea uwezo wahariri wa habari za michezo na tunaamini watajifunza mengi kutoka kwa wenzao na watakuja kuyatumia mafunzo hayo katika vyombo vyao vya habari na kuwasaidia pia waandishi chipukizi wa habari za michezo,” alisema Materu.
  Alisema kampuni yake imetoa Shilingi Milioni 6/- kufanikisha ziara hiyo na pia itatoa fulana maalum ambazo zitavaliwa na wahariri hao wakiwa huko.
  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, aliishukuru Vodacom Tanzania kwa udhamini wao na kuomba kampuni nyingine zisaidie kuwaunga mkono.
  “Vodacom Tanzania wameonesha ni ndugu zetu wa damu, licha ya maombi yetu ya muda mfupi kwao, lakini wametuchangia kiasi cha kutosha. Bajeti yetu bado kubwa sana kwa ziara hii, milango ipo wazi kwa wengine watusaidie,” alisema Mkoko, ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Kwa mujibu wa Mkoko katika ziara hiyo, wahariri wa habari za michezo wa Tanzania watapata fursa ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari vya Kenya na kubadilishana mawazo na wenzao wa Kenya kuhusiana na utendaji kazi wao.
  Pia alisema kutakuwa na kongamano lililoandaliwa na SJAK jijini Nairobi na litahusisha watoa mada kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) chenye makao makuu yake Lausanne, Uswisi, ambalo pamoja na mambo mengine litajadili umuhimu wa waandishi wa habari katika kupromoti michezo.
  “TASWA inaamini hii ni ziara muhimu kwa wahariri wa habari za michezo nchini na itasaidia kuboresha utendaji kazi wao,” alisema Mkoko na kuongeza kuwa pia wahariri hao watashiriki michezo na wenzao wa Kenya.

   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/-pamoja na T-shirt 60 kwa Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(katikati) jana kwa niaba ya chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu.
   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu(kulia)akiongea na waandishi wa wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/-pamoja na T-shirt 60  kwa Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(katikati)jana kwa niaba ya chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akishuhudia Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu(kulia)akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(katikati) moja ya t-shirt kati ya 60 zilizokabidhiwa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/- jana kwa chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.
  Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(kushoto)akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/- pamoja na t-shirt 60 toka kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu(kulia)jana kwa niaba ya chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu,Katikati ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu.

  0 0

  Seleman Kitenge katika picha kabla ya kupewa tuzo.
  Seleman Kitenge akipokea tuzo kwa furaha na tabasamu kubwa.
  Seleman Kitenge akipiga picha ya pamoja na baadhi ya washindi mbalimbali.
  Vijana na wanafunzi wa Mozambique-Tanzania Centre for Foreign Relations walikuwepo kwa wingi kumpokea shujaa Seleman Kitenge.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  JUMLA ya watoto 13,266 wenye umri chini ya miaka 10 wamenufaika mkoani hapa na huduma za afya zitolewazo na taasisi ya Kikorea ijulikanayo kama UHIC (United Help for International Children).

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo kanda ya Tanzania, Lee Kwiwoon alitoa taarifa hiyo hapa mwishoni mwa juma lililopita katika mkutano uliojumuisha madaktari, manesi na wahudumu wa afya kutoka wilaya tatu za mkoa huu, ambazo zimelengwa katika mradi wa taasisi hiyo.

  Mkurugenzi huyo alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutoa huduma kwa watoto wenye matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowapata wenye umri chini ya miaka 10.

  Aliwaeleza wanasemina hao kwamba watoto wengi walio katika umri chini ya miaka 10 hukumbwa na magonjwa mengi, hasa malaria, upungufu wa damu na utapiamlo. Magonjwa mengine ni pamoja na kifua, kuzaliwa njiti na kuharisha. 
   
  Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo 

  Lee aliwaambia maofisa na manesi pamoja na wahudumu wa afya kwamba jukumu kubwa la taasisi yake ni kuzuia magonjwa yanayowanyemelea zaidi watoto wadogo pamoja na kuhakikisha watoto hao wanakua katika afya bora.

  Alifahamisha kwamba taasisi hiyo ya UHIC imeanzisha mradi ujulikanao Keepers' ambao unawafundisha na kuwapatia mafunzo vijana wanaotoa huduma ya kuokoa maisha ya watoto kutoka janga la njaa, maradhi na kuwasaidia waishi katika mazingira mazuri ya kiafya.

  "Afya na uzuiaji wa magonjwa yawapatayo watoto wengi mkoani Tanga ni suala linalozungumzika na hivyo kuwafanya wadau kuamua kujitolea kuanzisha taasisi zitakazosaidia kuondoa adha hiyo kwa watoto wetu", alisema Lee.

  Mkurugenzi huyo alibanisha kuwa taasisi ya UHIC ni ya kimataifa iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma endelevu za afya kwa watoto waishio maeneo ya vijijini (pembezoni) mkoani hapa. 

  Alisema wamechagua wilaya tatu ambazo ni Pangani, Muheza na Tanga kuwa za mfano katika kuanza na mradi huo ambapo jumla ya vijiji 27 vitahusika. Alisema taasisi yake ina jukumu la kugawa dawa na kwamba wahudumu 24 tayari wamekwishapatiwa mafunzo ya kuhudumia watoto hao katika vijiji husika.
  Lee Kwiwoon akuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo vijana(Keepers) katika vijana waliofundishwa kuhudumia watoto katika masuala ya Afya na Lishe.

  Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Maggid alisema mkoa umepoteza maisha ya watoto wapatao 653 kutokana na magonjwa mbalimbali, yakiwemo malaria, kikohozi, upungufu wa damu na kuharisha.

  Pamoja na kupongeza msaada huo wa Korea akisema kuwa umefika wakati ukihitajika sana, lakini akataka wataalamu wanaopelekwa kwenye vijiji hivyo wapewe ushirikiano unaofaa.

  Mapema, akifungua semina hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa waTanga, Mayassa Hashim alisikitishwa na vifo hivyo ambapo alisema vingeweza kuzuilika kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wazazi . 

  Hata hivyo, Mayassa ambaye pia ni OfisaElimu wa Mkoa, alieleza matumaini kwamba ujio wa taasisi hiyo pamoja na madawa na wataalamu wao itasaidia kuondoa vifo visivyotarajiwa vya watoto wadogo.

  0 0  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh Gerson Lwenge akipata maelezo mafupi ya huduma ya DAWASCO kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea banda la Shirika hilo leo. Maonyesho hayo yaliyofunguliwa mapema wiki hii na Rais wa Rwanda Mh Paul Kagame na yanatarajia kufika kilele mwisho wa wiki hii ambapo kampuni zaidi ya 600 kutoka ndani na nje ya Nchi ya nchi zimeshiriki. (Picha na Robert Okanda)
  Waziri Lwenge akipata maelezo ya upimaji wa ubora wa maji kutoka kwa Afisa Ubora wa Maji wa DAWASCO, Sinza Mongela alipotembea Banda la shuirika hilo leo. 
  Waziri Lwenge akidodosa jambo baada ya kupata maelezo ya upimaji wa ubora wa maji kutoka kwa Afisa Ubora wa Maji wa DAWASCO, Sinza Mongela alipotembea Banda la shuirika hilo leo. 

  0 0
 • 07/07/16--10:59: TASWIRA YA LEO
 • Kamera yetu imeinasa Taswira hii ya Mdau aliebeba kuni, akieleka Baharini eneo la Ufukwe wa Ocean Road jijini Dar es salaam. Hatukuweza kumuuliza anapeleka wapi.

  0 0

  MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani) amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde 

  Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo, akahukumiwa kutengana na kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja, wakati shitaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

  Katika shitaka hilo, Jerry alidaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kutowapa nafasi watani wao wa jadi (Simba) kuingia kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

  Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

  “Kamati ilisikiliza kwa makini taarifa zake alipokuwa anazungumza na vituo vya Redio na kugundua alikuwa sahihi, hivyo hapa hana hatia,”kimesema chanzo.

  Hata hivyo, Jerry Muro amehukumiwa wakati mwenyewe hakuwepo kwenye kikao na inadaiwa hakutoa taarifa ya maandishi juu ya kutohudhuria kwake.

  Badala yake, imeelezwa Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika mapema leo kabla ya kikao kwa ajili ya kutoa taarifa ya mdomo kwamba Muro amekwenda kwao Kilimanjaro kusafisha makaburi ya wazee wake. 

  Lakini Kamati ikaamua kuendelea na kikao kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuchukua hatua ilizochukua. Hata hivyo, Muro ana haki ya kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya TFF.

  0 0

   Maafisa wa Mfuko wa PPF, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda hilo kuhusu Mfumo wa ‘Wote Scheme’ katika maonesho ya 40 ya Biashara ya KImataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mafoto Blog

   Maafisa wa Mfuko wa PPF, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda hilo kuhusu Mfumo wa ‘Wote Scheme’ katika maonesho ya 40 ya Biashara ya KImataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

   Afisa Michango wa Mfuko wa PPF, Glory Maboya, akizungumza na mteja aliyefika katika Banda hilo kujua michango yake katika Maonesho ya Sabasaba.

   Baadhi ya Wananchi wakipata huduma kutoka kwa Maafisa wa PPF katika Banda la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba.

  0 0
  0 0  0 0


  0 0


  MWALIMU HOUSE-NAFASI ZA UPANGAJI.
  Kampuni ya Walimu ya (Teachers’ Development Company Limited) inayo furaha kuutangazia umma nafasi za upangaji katika jengo la MWALIMU HOUSE lililopo Kiwanja Namba 48 Kitalu ‘Y’, ILALA BOMA jijini Dar es Salaam. Jengo linapakana na Barabara ya Uhuru na Kawawa mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Soko la Karume na Ilala maarufu kama Ilala Boma. 

  Nafasi zilizopo katika jengo zinaweza kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za kiofisi, maduka, bank, zahanati, mgahawa, chuo nk.

  Nafasi za upangaji zinapatikana kuanzia ghorofa ya kwanza hadi ya nane kwa ukubwa wa kuanzia square mita 42 hadi 218. Gharama ya Upangaji ni Tshs. 24,000 (Bila VAT) kwa square mita moja ikijumuisha kodi ya pango (rent) na baadhi ya huduma zinazotolewa katika jengo (service charge). 

  Huduma zifuatazo zinatolewa katika jengo letu la Mwalimu House;- 

  (i) Genereta (Stand by Generator) (Mpangaji atachangia fedha kidogo ya mafuta ya Generator)
  (ii) Tenki kubwa la kuhifadhi Maji
  (iii) Lifti ya kubeba watu 10 kuanzia ghorofa ya chini (Basement) hadi ya nane.
  (iv) Eneo kubwa la Parking (Inalipiwa)
  (v) Usafi na Ulinzi (Masaa 24)
  Gharama nyinginezo zitakazolipiwa na mpangaji ni kama ifuatavyo-;

   Tozo ya kuandaa nyaraka mbalimbali (Documentation fee)-Tshs. 236,000/-Italipiwa mara moja katika kipindi chote cha upangaji.

   Tozo ya bima ya pango (security Deposity)-ni kodi ya mwezi mmoja- Italipiwa mara moja katika kipindi chote cha upangaji -Itarudishwa endapo mpangaji atahama bila kufanya uharibifu katika eneo la upangaji.
  Kwa maelezo zaidi au kuona maeneo yanayopangishwa, Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia:-
  Simu ya Mkononi: 0769 084939, 0713 495603, 0765 187365
  Simu ya Mezani: 0222203063
  Email: tdevcoltd@gmail.com;khadijagogo@gmail.com.

  0 0
  0 0
  Mr ALAF (kulia) akitoa zawadi kwa washindi kwa wa mchezo wa ALAF Wheel of fortune katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliotembelea banda la ALAF katika Maonesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Wananchi wakifuatilia maelezo kutoka kwa mhudumu wa ALAF juu ya ubora wa mabati ya ALAF katika maonesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0

  WAFANYAKAZI wa ngazi ya zahanati wanaoongoza kubaki katika vituo vya vya kazi kuliko wa ngazi zingine zote

  Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro wakati akizungumza wadau wa afya wa kutoka mkoa Mbalimbali hapa nchini katika warsha kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam leo.

  amesema kuwa Taasisi ya Mkapa imetoa matokeo ya Tathmini za rasilimali watu ambazo zimefanywa katika sekta ya afya katika Halmashauri 17 za Wilaya zilizopo mikoa 7 ya Tanzania Bara.  

  Dk. Ellen  amesema kuwa  Sababu zinachangia kubaki kwenye vitu vyao kazi ni pamoja na Kupewa motisha ya posho ya kujikimu na nyumba ya kuishi karibu na vituo vyao, Kupewa ardhi kwa gharama nafuu ikiwa na viongozi wa halmashauri wanawasaidia watumishi wa Afya kujiwekea malengo ya utendaji kazi wao.

  Hata hivyo Dk. Ellen ameomba Mfumo wa OPRAS ufanyiwe meboresho ili uendane na baadhi ya kada katika sekta ya Afya. 

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro akizungumza na wadau wa afya wa kutoka mkoa Mbalimbali hapa nchini katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
   Mwakilishi wa shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani( UNFPA) hapa nchini, Dk. Natalia Kanem akizungumza na wadau wa afya katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wadau wa afya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0
 • 07/08/16--05:52: BEI YA MADAFU YA LEO


 • 0 0


  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe amekitaka Kitengo cha Dharura cha Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa ubunifu ili kukabiliana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi mara kwa mara.

  Profesa Mdoe aliyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa malalamiko ya wananchi juu ya ucheleweshaji wa huduma unaofanywa na kituo cha dharura cha TANESCO yamepelekea wananchi kuwa na taswira hasi juu ya shirika hilo. “Ninawataka kuwa wabunifu katika utendaji kazi wenu, kwa kutoa huduma kwa haraka kwa kuwa nyinyi ndio mliobeba taswira ya shirika,”alisema Profesa Mdoe.

  Wakati huo huo akizungumzia sekta ya madini nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa Serikali imejipanga katika kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Alisema kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP), Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini wanaokidhi vigezo. Alitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kuwa na leseni za uchimbaji madini, kuonesha kuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji madini pamoja na ulipaji wa kodi serikalini.

  Alisisitiza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia vifaa na mafunzo ili kukuza uzalishaji wa madini nchini na hivyo sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi .

  Mtaalam kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Nyaso Makwaya (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kushoto) mara alipotembelea banda la TGDC.
  Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Philip Mathayo (kushoto) akitoa maelezo juu ya sera ya madini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) Zena Kongoi (kulia) akielezea mikakati ya shirika hilo katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto)
  Meneja Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage (kulia) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (katikati) matumizi ya majiko sanifu katika kupikia mara alipotembelea banda la REA. Kushoto kabisa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Asteria Muhozya.
  Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Ally Mluge (kulia) akielezea muundo wa shirika hilo kwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la TPDC. 

  0 0

  Ili kupambana na changamoto za ajira Nchini kama kijana hususani mwanafunzi wa elimu ya juu, unaitaji mbinu mbadala za kujikwamua kimaisha. #CampusVybez ya #TimeFm @timesfmtz @sandytemu @djj_one @ inakukutanisha wewe kijana na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi ajira na vijana Antony Mavunde, kuzungumzia mbinu za kujikwamua kwenye ajira @anthonymavunde Jumamosi hii Protea Hotel, saa mbili kamili asubuhi.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) wakati wa ziara yake nchini pamoja na ujumbe alioambatana nao walipokutana na Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) alipokuwa akimfafanulia jambo kuhusu masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. IGP Kachama na ujumbe wake yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimuaga Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama mara baada ya mazungumzo yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. IGP Kachama yupo nchini kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

  Serikali  kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18, na kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni Sao Hill (Mufindi), Buhindi (Sengerema), Meru/Usa (Arumeru), West Kilimanjaro (Hai), Shume (Lushoto), North Kilimanjaro (Rombo), Kiwira (Rungwe) na Kawetire (Mbeya Vijijini).

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) na kufafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.

  Amesema wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususan wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  IJUMAA, JULAI 8, 2016.

older | 1 | .... | 1281 | 1282 | (Page 1283) | 1284 | 1285 | .... | 3286 | newer