Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1280 | 1281 | (Page 1282) | 1283 | 1284 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya TANTRADE Sabasaba yanayoendelea katika viwanja hivyo vilivyopo barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam ambapo ameelezea uendelezaji na uuzaji wa nyumba katika maeneo mbalimbali unaoendelea katika miradi yao iliyopo nchi nzima.
  Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akifafanua jambo kuhusu mipango ya shirika hilo wakati akizungumza na wanahabari katika banda la maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya TANTRADE barabara ya Kirwa.
  Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akifurahia jambo na baadhi ya wateja waliotembelea katika banda hilo.
  Clara Lumbanga Ofisa Maeneleo ya Biashara NHC akimuangalia mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo wakati alipokuwa akisaini kitabu cha wageni.
  Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika la NHC wanaoshiriki katika maonyesho ya TANTRADE yanayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba jijini Dar es salaam katika barabara ya Kirwa.

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mufti wa Tanzania, Alhaj Sheikh Abubakary Zubeir (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum pamoja na Naibu Mufti, Sheikh Hamid Jongo katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum akitoa hotuba ya Eid El Fitr, kwa waumini wa Dini ya Kiislam walioshiriki ibada hiyo, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salam za Eid El Fitr, kwa waumini wa Dini ya Kiislam walioshiriki ibada hiyo, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kulia) akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, wakifatilia kwa makini hotuba ya Eid El Fitr, iliyokuwa ikitolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
   
  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Alhaj Mussa Assad akijumuika na waumini wenzake katika Swala ya Eid el Fitr, iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein baada ya kulihutubia Taifa kwenye Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016 katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016.
   akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016. (Picha na OMR)

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuikana Viongozi mbali mbali na Waislamu wengine katika swala ya Sunna ya Eid el Fitri ambayo huswaliwa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja
   Waumini wa Dini ya kiislamu wakiwa katika swala ya Sunna ya Eid el Fitri iliyoswaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan
   Waumini wa Dini ya kiislamu wakisikiliza mawaidha baada ya swala ya Sunna ya Eid el Fitri iliyoswaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Mashekhe waliofika Ikulu Mjini Unguja kupeana mkono wa Sikukuu na kutakiana kheri ikiwa ni kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi bahasha Mzee Suleiman Khamis wa Darajabovu (kulia) alipokuwa akitoa sikukuu kwa wananchi mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja katika  kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Kwa Picha zaidi na Ikulu BOFYA HAPA

  0 0

  Familia ya William H. Shelukindo inapenda kuwataarifu kuwa mazishi huko Arusha ya Mpendwa wao Beatrice Matumbo Shelukindo Mbunge wa zamani wa Kilindi sasa yatafanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 7/7/2016 na sio leo Jumatano tarehe 6/7/2016 kama ilivyotangazwa awali.

  Mazishi yatafanyika kesho saa tisa alasiri pale pale eneo la Oloirien jijini Arusha.

  Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa.
  Jina la Bwana Lihimidiwe.
  AMEN


  0 0

   Hata mbuyu ulianza kama uyoga. Na Bw. Adam wa Adam Auto Garage ya mjini Tunduma mkoani Songwe  amedhihirisha hilo kwa kuunda helikopta inayotumia injini ya gari ambayo anasema anatarajia kuirusha siku Mwenge wa Uhuru utapofika mjini hapo. Picha za ubunifu huu zimesambaa kwenye mitandao ya jamii ila cha ajabu hakuna mamlaka iliyoshituka.
   Bw. Adam akipongezwa kwa ubunifu wake ambao mamlaka husika zinaombwa kwenda na kuangalia namna ya kutumia kipaji hiki cha aina yake kwa maendeleo ya Taifa
   Wananchi wakiishanga helikopta ya Adam Auto Garage mjini Tunduma
   Bw. Adam na timu yake

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria  Baraza la Iddi alilolihutubia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Julai
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na mtoto Asma Maulid baada ya kuhubia Baraza la Iddi kwenye  ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Picha na PMO

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikhe Aboubakar Zubeir wakati alipowasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid El fitri lililofanyika katika viwanja hivyo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika baraza hilo la Eid Elfitri.


  0 0

  Timu nzima ya Kampuni ya Michuzi Media Group (MMG) inawatakiwa Wadau wake wote popote pale mlipo, sikukuu njema ya Idd el Fitr na tuisherehekee kwa amani na mapenzi tele kama ilivyolekezwa katika vitabu vitukufu vya Dini.

  IDD MUBARAK
  MMG TEAM

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye Kaunda suti akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited Bw.  Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya .(Picha E.madafa, D.Nyembe)
  Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited Bw. Derick ambaye kampuni yake ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.

  Ramani ya mradi.

  Na Mwandishi wetu, Mbeya

  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer. Mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika

  Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.

  Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjali na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi. Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali kuu. 
  Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati Hata hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini hayo adhimu ya duniani ya niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo karibu na maeneo ya gereza hilo la Songwe. 
  Kwa mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta sanjali na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.
  0 0

  Shirika la ndege la RwandAir likishirikiana na Jumuiya ya Wanyarwanda waishio nchini Tanzania wanakukarubisha kwenye usiku wa Tamaduni za Rwanda, utakaofanyika Julai 9, 2016 katika Ukumbi wa Mw. Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kutakuwepo na ngoma ya asili kutoka Rwanda na wenyeji hapa Tanzania.

  Njoo ujionee na ujifunze mengi zaidi baina ya nchini hizi mbili.

  0 0

  TAKRIBAN kilometa 10 kutoka Kijiji cha Dakawa kuna kitongoji cha Magogo kilichoko msituni kabisa ambako pia kuna mashamba ya mpunga.


  Msitu huu ambao bado ungali na miti mingi ya asili ambayo imenusurika kucharangwa na wachoma mkaa na wanaotafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ndiko akinamama wapatao 30 wameamua kutundika mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki katika shamba lenye ukubwa wa ekari nne.

  Licha ya kujikwatua vilivyo, lakini wanapoingia katika msitu huu akinamama hawa hawana mchezo kabisa, baadhi yao wanavaa mavazi maalum ya kujikinga na nyuki na kuanza kukagua mizinga yao kama tayari nyuki wamekwishaingia.
  Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi (aliyechuchumaa kushoto) akisaidiana na mwanakikundi cha Dakawa Green Voices, Neema Obeid, kuweka vizuri mzinga.  “Kujipamba ni jambo la kawaida, lakini tunapokuja huku tuko kikazi zaidi,” anasema Neema Obeid huku akipenya kwenye vichaka kuiendea mizinga ambayo iko juu ya miti mikubwa.

  Akina mama hao wa kikundi cha Dakawa Green Voices Women Group wameamua kuingia kwenye ujasiriamali wa ufugaji wa nyuki kwa malengo makubwa mawili – kupata fedha kutokana na mazao ya nyuki pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabinchi.

  “Misitu inateketea, watu wanaendelea kuchoma mkaa na wengine wanafyeka miti ili wapate mashamba, lakini kwa kuanzisha ufugaji huu wa nyuki, kamwe hatutakubali kuona yeyote akikata hata fimbo, achilia mbali miti mikubwa,” anasema Bi. Mariam Bigambo, mshiriki kiongozi wa mradi huo.
  Mwanahabari Judica Losai (wa pili kushoto) akimuuliza maswali Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi, wakati wakiwa kwenye eneo la ufugaji wa nyuki. 


  Mariam Bigambo ni miongoni mwa akinamama 10 waliopatiwa mafunzo nchini Hispania mapema mwaka huu na wanatekeleza kwa vitendo mradi wa Green Voices, ambao unafadhiliwa na taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Women for Africa Foundation inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. Hapa nchini, mradi huo unasimamiwa na asasi ya Environment Media Agenda (EMA) chini ya uratibu wa Bi. Secelela Balisidya.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Huu ni Muendelezo wa Matukio Madogo Madogo yanayo endelea Kujitokeza katika eneo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya ambapo ndipo Sehemu pekee kati ya Sehemu zote kwa Jiji zima kuwekwa Taa za kuongozea Magari na watembea kwa Miguu kwa Mkoa mzima wa Mbeya kiukweli hapa ndipo ambapo pamepewe kipaumbele hicho cha kuwekewa Taa za kuongozea Magari na Watembea kwa Miguu, Lakini cha kushangaza zaidi licha ya eneo hilo kupewe kipaombelele kumekuwa na Vijipu Upele vingi ambavyo vinajitokeza mara kwa mara katika eneo hilo ikiwemo hili la Taa moja Kupigwa Ngwala na Gari na kutelekezwa kama uionavyo hapo katika Taswira ikiwa na Mmoja wa watembea kwa Miguu akisubiri Taa hiyo iweze kumuongoza lakini hali ya kuwa Taa hiyo ikiwa hoi Bin Taabani kutokana na kupokea Ngwala na Gari ambayo hatukuweza Kuifahamu.
  Kichwa cha Taa hiyo Mpya iliyo wekwa hivi karibuni kuajili ya kuongozea Wananchi watumiao Barabara hiyo ikiwa katika Uso wa simanzi Kando kando ya Eneo hilo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya..
  Mmoja kati ya watumiaji wa Barabara hiyo akisubiri Msaada wa Mbinu nyengine ya kumuwezesha kuvuka Barabara kutokana na kumsubiri Muongozaji wake alie Pigwa Ngwala bila mafanikio.
  PICHA NA MR.PENGO MMG.

  0 0

  Ulikuwa mtanange wa kukata na shoka wa nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 inayotimua vumbi kule nchini Ufaransa kati ya Wales iliyokuwa ikiongozwa na Gareth Bale na Ureno ikiongozwa na Christian Ronaldo.

  Mtanange huo ulio kanyagwa katika dimba la Parc de Olimpique jijini Lyon, ulichezeshwa vizuri na mwamuzi Jonas Eriksson wa Sweden na mpaka mapumziko timu hizo hazikuweza kufungana ingawa kila timu ilitengeza nafasi kadhaa za kuweza kujipatia mabao laikn umaliziaji ukawa mbovu.
  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi na walikuwa Ureno wlianza kuhanikiza ushindi,si mwingine bali ni Christian Ronaldo kunako dakika ya 50 yaani dakika 5 tu baada ya kuanza kipindi hicho anafunga bao zuri kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona fupi toka kwa Guerreiro.

  Na dakika 3 baadaye Ronaldo anapiga shuti kali langoni mwa Wales akiwa umbali wa mita 25 na mpira huo unawapita walinzi wa Wales ambapo Luis Nani wa Ureno anaserereka na kuuunganisha wavuni akiianikia timu yake bao la pili.

  Kuona jahazi linazama kocha wa Wales Chris Coleman anamtoa Joe Ladley na kumwingiza Sam Vokes huku akibadili mfumo toka 3-5-1-1 na kucheza 4-3-1-2,lakini hiyo haikusaidia kubadili matokeo mbele ya Ureno waliokuwa wakicheza mfumo wa 4-1-3-2.
  Sasa Ureno anamsubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya wenyeji Ufaransa na Ujerumani kucheza naye fainali siku ya jumapili Julai 10 2016 katika dimba la Stade de France,Paris.

  0 0


  Ustaadh Ibrahim akianza kwa dua kwenye sherehe ya Eid ilizoandaliwa ma Jumuiya ya Kiislam DMV (TAMCO) na kuakaribisha Watanzania wote wakiwemo marafiki zao kwenye sherehe zilizofanyika siku ya Jumatano July 6, 2016 Slver Spring, Maryland nchini Marekani. Picha na Vijimambo na Kwanza Production

  Ustaadh Hajji Khamis kutoka New York akitoa mawaidha ya Eid  kwenye sherehe ya Eid ilizoandaliwa ma Jumuiya ya Kiislam DMV (TAMCO) na kuakaribisha Watanzania wote wakiwemo marafiki zao kwenye sherehe zilizofanyika siku ya Jumatano July 6, 2016 Slver Spring, Maryland nchini Marekani.

  Miss Tanzania USA Aeesha Kamara akijumuika na Watanzania wenzake  kwenye sherehe ya Eid ilizoandaliwa ma Jumuiya ya Kiislam DMV (TAMCO) na kuakaribisha Watanzania wote wakiwemo marafiki zao kwenye sherehe zilizofanyika siku ya Jumatano July 6, 2016 Slver Spring, Maryland nchini Marekani.

  Watanzania na marafiki zao kutoka majimbo mengine wakijumuika pamoja  kwenye sherehe za Eid ilizoandaliwa ma Jumuiya ya Kiislam DMV (TAMCO) na kuakaribisha Watanzania wote wakiwemo marafiki zao kwenye sherehe zilizofanyika siku ya Jumatano July 6, 2016 Slver Spring, Maryland nchini Marekani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Shindano la Airtel Trace Music Stars la Afrika lililofanyika nchini Nigeria linategemea kuonyeshwa live leo kupitia kituo cha television cha Trace chanel 325 saa tatu kamili usiku, katika shindano hilo tutashuhuhia washiriki kutoka nchi 10 barani Afrika wakichuana vikali kila mmoja akionyesha kipaji chake cha kuimba ikiwemo mshiriki kutoka Tanzania Bi Melisa John.

  ili kupata burdani na kushuhudia ni jinsi gani washiriki hawa walivyoonyesha vipaji leo saa 3 kamili usiku fungua kituo cha TRACE Urban namba 325 kinachopatikana kupitia kingamuzi cha DSTV.

  marudio ya kipindi hiki ni siku yatakuwa siku ya ijumaa saa 8 mchana katika kitu hicho hicho cha TRACE.
  mwanamuziki nguli kutoka nchini marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Keri Hilson (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliongia tatu bora ambao wametoka nchi ya Zambia, Tanzania na Madagascar

  0 0

   Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume akimpatia Maelezo juu ya Mradi wa Nyumba wa Kijichi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Prof. Samwel Wangwe alipotembelea Banda la NSSF kwenye Maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akifurahi baada ya kupewa Maelezo ya Mradi wa Viwanja Vya Kiluvya na Meneja kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF.

  Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru akifurahia maelekezo aliyokuwa akipewa na Meneje Kiongozi wa Masoko na Uhusiano Eunice Chiume alipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara.

  Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru akipewa maelezo katika idara ya wakala wa bima wa NSSF na Afisa Bima Isack Peter alipotembelea banda la NSSF, akishuhudia katikati ni Meneja kiongozi Masoko na Uhusiano Eunice Chiume.
  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Prof. Samwel Wangwe Jinsi ya kutoa mrejesho wa Huduma za NSSF alipotembelea banda la NSSF.

  0 0

   Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 kwenye viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere  Barabara ya Kilwa  Dar es Salaam leo.
   Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya kuendeleza jotoardhi Tanzania(TGDC) wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja.
   Kaimu Meneja Uhusiano Tanesco, Leila Muhaji (kushoto), akiwa na  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja walipotembelea banda la TGDC.
   Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (kushoto), akimsikiliza mteja aliyetembelea banda hilo.
   Mteja akisikilizwa.

  0 0  Bw. Deogratius John Ndejembi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

  Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

  Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam  07 Julai, 2016

older | 1 | .... | 1280 | 1281 | (Page 1282) | 1283 | 1284 | .... | 3284 | newer