Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mrishom Mpoto, (kushoto), akimuhudumia mwanachama huyu aliyefika banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 5, 2016 ambako kunafanyika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Mfuko huo umezidi kujizolea wanachama wapya na hivyo kuongeza idadi ya wachangiaji. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Joseph Lyimo, (kushoto), Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akimkabidhi kadi ya uanachama mwanachama Gilbert Nsumba, kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 5, 2016
Afisa Operesheni Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kitengo cha ulipaji mafao, Murwa Clara Kihore, (kulia), akiwapa maeelzo wanachama hawa wa PSPF Maafisa wa polisi, kuhusu masuala yahu uchangiaji na michango kwenye Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye banda la Mfuko huo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jingo la Wizara ya Fedha na Mipango Julai 5, 2016
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Catherine Salema, akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Mtashobya E Mukebezi, kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 5, 2016
Lupakisye Mwaipungu, (kushoto), Afisa Kumbukumbu wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, aimkabidh kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS, Paulo Elisa Kiombo kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 5, 2016.