Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MAENDELEO YA TIB WILLIUM LYAKURWA.

0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Maendeleo ya TIB, Willium Lyakurwa.


VIFUNGO GEREZANI BILA FAINI, NA SI VITOCHI VYA TRAFIKI, NDIO DAWA YA KUPUNGUZA AJALI BARABARANI

0
0
 Mabasi yakifukuzana mlima wa Kitonga kuelekea Iringa. Wananchi wengi waliohojiwa na Globu ya Jamii wamependekeza kuwepo na adhabu ya kifungo gerezani moja kwa moja bila kuwepo na faini ya aina yoyote kwa dereva wa mabasi ya abiria na magari mengine kwa kosa lolote lenye kuhatarisha maisha ya watu. Wananchi hao wametolea mfano njia za mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam ambapo wananchi hivi sasa wanaziheshimu njia za mabasi hayo baada ya watu kadhaa kupewa adhabu ya vifungo gerezani bila faini.
Alama barabarani hapo zinamaanisha HAKUNA KUPITA KABISA lakini dereva wa basi anapuyanga tu, tena kwenye kona kona za mlima Kitonga.

MFALME WA AFRO POP TWENTY PERCENT ARUDI KWENYE GEMU KWA KISHINDO NA SAUTI YAKE YA GHARAMA

0
0
Na Sultani Kipingo
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki,  huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.
Twenty Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo  za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.
"Nimerudi kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Studio jijini Dar es salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama  kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, " anaogeza.
Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.
Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses.
"Namkubali sana Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo", anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na  wasanii nyota kibao wakiwemo  Lady Jay Dee,  Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.
 Twenty Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane" uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni "Tamaa Mbaya"  na "Ya nini Malumbano" na "Maisha ya Bongo"  
Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. "Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa  na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent)   akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi zake huku  akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.

TRA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA ZA MAGENDO.

0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) itaendelea kudhibiti na kupambana na  wanaofanyabiashara za magendo katika vituo mbalimbali ambavyo vinaendelea na vitendo vya magendo.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema TRA imefuka lengo la Makusanyo ya kodi kwa mwaka 2015/2016. 

Amesema TRA itazidi kupambana na kuziba mianya yote ya  upotevu wa mapato hususani katika msisitizo wa matumizi wa Mashine za Kieletroniki za kodi za EFDs pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara na kufuatilia madeni.

Pia amesema kuwa TRA itaendelea kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine za Kieletroniki za kodi za (EFDs) kwa kuwakamata na kuwatoza faini au kuwafikisha mahakamani na kuwachukulia hatua za kisheria ili kuhakikisha inafikia na kuvuka malengo.

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeshagawa mashine za Kieletroniki za EFDs 1120 kwa wafanyabiashara wanaostahili kupata mashine hizo bure na ambao hawajachukua machine za kieletroniki za kodi za EFDs ili kuwezesha TRA kukusanya mapato ya Serikali.


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuvuka lengo la makusanyo ya Kosi kwa mwaka 2015/2016.Kulia ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya.
Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya akifafanua juu ya Operesheni ambayo itatumika katika makusanyo ya ndani ambapo watapita nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa na fremu kwa fremu katika kugawa Mashine za Kieletroniki za EFDs kwaajili ya Kukusanya kodi kwa kila Mfanyabiashara Kushoto ni  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata.
Kushoto ni Kamishna wa mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elijah Mwandumbya na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakiwa katika mkutano wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WALEMAVU WALIA NA UPUNGUFU WA WALIMU.

0
0
Mtoto Clara Damian mwanafunzi wa darasa la saba asiyeona akiwa darasani  akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi  patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu na vitabu.

Na Woinde Shizza,Arusha.

Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Patandi iliyopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wamelalamikia tatizo la upungufu wa walimu,vitabu na vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu hali inayokwamisha maendeleo ya kitaaluma hivyo wameiomba serikali na taasisi binafsi kutatua changamoto hiyo.


Mwanafunzi asiyeona anayesoma darasa la saba Clara Damian ni alisema kuwa kumekua na uhaba wa vitabu kwa watoto wasioona na mashine za kuandikia maandishi yenye nundu ambazo ni chache na kwa sasa ni mashine tatu pekee zinafanya kazi ukilinganisha na idadi kubwa ya wanafunzi.


Alisema kuwa miundombinu ya majengo ya madarasa pia yamekua si rafiki kwa watoto wenye ulemavu hivyo anashauri miundombinu ya majengo na shule iendane na mahitaji wa watoto hao.

Mibaku Limba Mwanafunzi asiyesikia (kiziwi) alisema kuwa walimu walioko kwa sasa wanaofundishwa kwa lugha za alama ni wachache ukilinganisha na idadi ya masomo hali ambayo inachangia kuwarudisha nyuma.

Mratibu wa Kitengo Cha Walemavu Mwalimu Anna Shayo Katika Shule hiyo Mwalimu Shayo alikiri kuwepo kwa upungufu wa walimu na vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kuiomba jamii,taasisi na serikali kushiriki katika kuboresha maendeleo ya watoto hao ambao wakijengewa misingi bora ya elimu wanaweza kuwa na mchango kwa jamii badala ya kuwa tegemezi.

Mwalimu Marko Alois Mamuya anayefundisha watoto viziwi ameiomba serikali itoe motisha kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu ili kuongeza ari na hamasa itakayosaidia kupata idadi kubwa ya walimu.



“Tunawaomba wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu majumbani bali wawalete mashuleni huku waweze kupata elimu ,lishe na mazoezi badala ya kuwafungia nyumbani kwani wanazidi kuwa tatizo licha nya uwezo,vipaji na ubunifu walioanao ambao unaweza kuwasaidia wao na jamii yao” alisema Mwalimu Marko.

BASATA LAPIGA MARUFUKU DISCO TOTO, KUMBI ZISIZO NA VIBALI.

0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limepiga marufuku kumbi zote za burudani zisizo na vibali kufanya maonesho ya aina yoyote.

Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani wenye vibali kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Katika hili BASATA linawaelekeza wamiliki na mameneja wa Kumbi zote nchini kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu.

Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi za Eid El Fitr wamiliki na mameneja hawa wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kumezwa na faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali ambayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa ambayo yangeweza kuepukwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

BASATA mamlaka inayotoa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

 BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa sherehe njema ya Eid El Fitr yenye furaha tele. Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza.
KATIBU MTENDAJI

KUPATANA .COM YAZINDUA HUDUMA YA PREMIUM

0
0
 Meneja Mwakilishi wa Kupatana.Com, Makusaro  Tesha akizungumza na waandishi wa habari juu huduma mpya ya Premium waliyoizindua katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu JK. Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mauzo Mabango ya Huduma za Premium, Gift Joshua huduma mpya ya Premium waliyoizindua katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu JK. Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

TANZANIA ni nchi inayokuwa katika teknolojia ya mawasiliano katika kurahisha kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja v ya Mwalimu Julius Kambarage nyerere,  Meneja Mwakilishi wa Kupatana.Com, Makusaro Tesha amesema na kongezea kuwa wananchi wanaweza kutangaza biashara katika kutumia mtandao. Amesema Kupatana.com imeanzisha huduma ambayo Premium ambayo kwa wale watu wanaotaka kutangaza biashara kwa haraka na kuweza kupata wateja mara moja.
Makusaro amesema Kupatana .com ni mtandao wenye soko kubwa nchini kwa kuendesha huduma za kimtandao kwa wananchi kuendesha biashara mbalimbali ya yenye watu milioni 24.7 wanaotembelea.
Amesema kuwa mauzo yanayofanywa katika mtandao huo kwa siku ni zaidi ya vitu 80,000  hali hiyo inaonyesha watanzania wanakwenda na teknolojia.

MASHEIKH WAASA WAISLAMU KUJIKITA KATIKA FUNGAMANO LA AMANI.

0
0
Mkurugenzi wa Benki ya Azania Godfrey Dimoso akizungumza katika hafla ya futari waliyowaandalia Masheikh na wadau mbalimbalu wa kampuni hiyo na kuwataka kufuata nasaha zilozotolewa na masheikh hao.
Baadhi ya wadau wakifuturu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHEIKH  Mahamoud Abdallah  Waziri amewataka waislamu kuweza kujikita kwenye fungamano la Amani ambalo huwakutanisha watu kwa pamoja na kuwasihi kudumisha utamaduni huo  ili kuendeleza amani ambayo ni tunu ya Taifa letu. Amesema hayo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Azania ambapo  mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Sheikh Waziri amewasa  jamii kujikita zaidi  kwenye fungamano la Amani 
na kuwataka watanzania kudumisha utamaduni wa kujumuika pamoja, kufurahika au kubadilisha mawazo ili kuendeleza amani ambayo ndiyo tunu ya Taifa letu.
Ameweza kuupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kufanya tukio hilo adhimu la kuwakutanisha wadau mbali mbali, hasa katika kumi la mwisho la Mwezi mtukufu  la  Ramadhani ambalo ni kumi la Fiedaus lenye maana ya kuomba pepo kwa Mwenyezi Mungu.
Naye Sheikh Muhammed Idd 'Abu Idd', amesema Saumu ni mchango ambao una malengo kwa anayefunga kuendelea na kuwa mtu mwema hata baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani."Moja ya malengo au hekima ya Saumu ni kumfanya mtu aishi vema na jamii yake na kwamba Mwezi huo umeletwa ili kuwabdili watu kutoka kwenye uasi kwenda kwenye  wema," amesema. Ameongeza na kusema kuwa lengo lingine la saumu ni kutengeneza afya kwa wafungaji  jambo ambalo hata matabibu wamekuwa wakilisisitiza.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya Azania, amewapongeza wateja na wadau wao kwa kukubali wito wao na kuhudhiria tukio hilo ambalo anaamini wamepata vitu vya ziada kutoka kwa Masheikh waliotoa nasaha. Amesisitiza kuwa benki hiyo ambayo ni wazawa kwa asilimia 100 itaendelea kuwahudumia watanzania katika mahitaji yao wanayohitaji.

KAMANDA MPINGA AZUNGUMZIA AJALI YA MKOANI SINGIDA

MWANADADA AWAGONGA MAJAMBAZI WALIOMPORA FEDHA KWA GARI, WATIMKA NA KUACHA BUNDUKI AINA YA SMG

MWENYEKITI MPYA WA BODI YA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF), SPIKA MSTAAFU, ANNE MAKINJDA AANZA KAZI RASMI, ATEMBELEA SSRA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI IRENE ISAKA

0
0
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe, Anne Makinda akiwa na  Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, alipotembelea Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kufanya mazungumzo ya kikazi na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mhe. Spika Mstaafu Anne Makinda akiwana katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka (kushoto), mara baada ya mazungumzo ya kikazi leo, katika Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.

VOA SWAHILI Mitaani: Watanzania na maonyesho ya Saba Saba

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 04/07/2016

TAARIFA YA KAIMU MKURUGENZI MKUU, MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA, ENG. JAMES KILABA KUHUSU UKOMO WA MATUMIZI YA SIMU BANDIA NA UANZISHWAJI WA RAJISI KUU YA NAMBA TAMBULISHI ZA SIMU ZA MKONONI

Dar es Salaam City forge ties with Republic of Korea's Yong-In City

0
0
 Dar es Salaam City Mayor, Hon. Isaya Mwita (right) receiving a gift from his counterpart, Hon.  Shin Hyensoo from the Republic of Korea's  Yong-In City in Dar es Salaam.  Mr. Hyensoo led 11 people delegation in a bid to strengthen relation between the two cities in areas of education, culture and economy.
Dar es Salaam City Mayor, Hon. Isaya Mwita (right) greets members of 11 people delegation from the Republic of Korea's Yong-In City in Dar es Salaam.  The delegation was led by the city’s Mayor, Mr.  Shin Hyensoo.  The visit seeks to strengthen relation between the two cities in areas of education, culture and economy.

WAKAZI WA MKURANGA WANUFAIKA KWA KUSIKILIZA EFM REDIO

0
0
Mchezo wa saka saka unaoendeshwa na kituo cha efm redio 93.7 baada ya kufanya shindano hili katika mkoa wa Dar es salaam katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni sasa imeenda mkoa wa Pwani na siku ya jumapili ya tarehe 03/07/2016 iliwafikia wakazi wa Mkuranga katika viwanja vya shule ya sekondari ya Mwinyi.
 Baadhi ya wakazi wa Mkuranga wakiwa wana saka saka katika eneo husika, kidubwasha kilichofichwa.
 Meneja  utafiti na ubunifu wa EFM akihakiki kidubwasha cha mmoja ya washiriki wa saka saka.
 Mshindi wa milioni 2, Bi Zalina Abusheikh  akiwa anahojiwa na mtangazaji Chogo kushoto.
Washiriki wakiwa wanasubiri kukaguliwa kuwa kile walicho kisakasaka nichenyewe.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Nyabaganga Taraba akabidhiwa ofisi

0
0
  
 Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilayani humo leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi. Katika hafla hiyo, Taraba aliwataka watendaji wa wilaya hiyo kujituma kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano pamoja na kuwa waadilifu katika kuwatumika wananchi.
Aidha, alimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo aliyestaafu, Hawa Ngh’umbi kwa utendaji wake huku akiahidi kuendelea kuchota hekima zake.

Mkuu wa Wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo wakati akiagwa baada ya kustaafu.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Wengine kuanzia kushoto waliokaa ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kangese, Mkuu wa wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Wilson Nyamunda.

 Mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake, Hawa Ngh’umbi (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mkuu mrithi wake, Nyabaganga Taraba wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Mkuu mpya wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba akisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi tayari kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo. Picha na Robert Hokororo  WA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU

GOOD NEWS TO ALL NGO’s IN TANZANIA

0
0

Heri Africa Tours & Safaris Ltd with main office at Kisongo, Arusha – Tanzania, invites all NGO’s dealing with international Volunteer’s who are interested to visit one of our National Parks or climb Mt. Kilimanjaro. We offer 15% commission per booking out of cost with a contract of 2 years effectively working with us.  Interested NGO’s please contact us through email address: info@heriafricatours.com  or 
call / whatsapp +255 757 574729 (24hrs –Available). Many Thanks!

PBZ Yakabidhi Msaada kwa Watoto Wa Vituo Vya Mayatima Zanzibar Kusherehekea Sikuku ya Eid Fitr

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumza na wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar, ili kusherehekea Sikukuu baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) akikabidhi msaada wa vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar kusherehekea vizuri sikuku ya Eid Fitry baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuungana na Watoto wenzao kusherehekea sikuku hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumzac wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar.kushoto baaddhi ya watoto wa kijiji hicho.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images