Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 126 | 127 | (Page 128) | 129 | 130 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Pichani kati ni Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's", "tukiwakumbusha akina  mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda sana" alisema Chando.Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo,Bi.Regina Ogwalla.Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora Mzeru.

  Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa  mrembo wa kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.

  Pia anasema kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa jamii kwa namna mbalimbali.

  Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi  kuhusiana na  uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our heart's",.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Winfrida Korosso akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi bora Bi. Khadija Ahmed.
  Wafanyakazi bora wa Tume wakiwa katika picha na Dereva Mwandamizi wa Tume Bw. Goya Zuberi Mchenga (katikati).
  Mfanyakazi bora wa Tume Bi. Khadija Ahmed akizungumza mara baada ya kupatiwa zawadi na Katibu Mtendaji wa Tume.
  Wafanyakazi bora wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume.

  0 0


  Mkutano wa  kumi na nane wa mwaka kwa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za  Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika  Mei 15, 2013   jijini Dar es Salaam  chini ya mwenyekiti wa umoja huo kwa mwaka 2012/2013 Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP Said Mwema.
  Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa  kamati tendaji za SARPCCO ambao  utafunguliwa na IGP Said Mwema  Mei 13, 2013 na kufuatiwa na Mkutano wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo utakaofunguliwa Mei 15, 2013 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi.
  Katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja na ushirikiano baina ya SARPCCO na Umoja wa Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO).
  Vilevile, mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi Machi jijini Dar es Salaam.
  Aidha suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.
  SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na nne ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Congo, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland na Madagascar.
  Imetolewa na:-
  Advera Senso-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0


  The Scot, 71, has won 38 trophies during his reign at Old Trafford and will now become a director and ambassador for the club.His haul includes 13 league titles, two Champions League crowns, five FA Cups and four League Cups.
  "The decision to retire is one that I have thought a great deal about. It is the right time," Ferguson said.Everton's David Moyes and Jose Mourinho, currently at Real Madrid, are the bookmakers' frontrunners to take over.
  BBC Sports editor David Bond says United are confident of announcing a successor to Ferguson before the weekend.
  He believes they are looking for someone who understands the club's history and is committed to youth development while employing an attractive, attacking style of football.

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania, Bibi Tunu Kavishe, (shoto),akizungumza na Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Jijini Dar,kuhusiana na Benki ya Barclays kuaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk,Mchakato ambao umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006,ambapo pia Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo  fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.

  Matembezi hayo ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu  wa benki  ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii.  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
  Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Barnaba Elias akizungumzia wimbo wake alioutunga na Mwanamuziki mwenzake Jean Pierre ajulikanae kwa jina la Kidumu ambao umezinduliwa leo rasmi ukiitwa  ‘Wanawake”,"Wimbo huo umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias anaejulikana kama  ‘Barnaba’ na Jean Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na maudhui ni kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika kuchangia na kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga"alisema Barnaba.
  Pichani ni baadhi ya Wanahabari waliohudhuria mkutano huo jijini Dar leo.


  BARCLAYS TANZANANIA YAZINDUA MATEMBEZI YAJULIKANAYO KAMA

  Step Ahead Walk 2013


  Kila mwaka Benki ya Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo  fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.


  Matembezi haya ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu  wa benki  ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii.  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.


  Akiongea katika vyombo vya habari leo, Bibi Tunu Kavishe, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania amesema, leo hii tunazindua mziki unaoitwa ‘Wanawake” ambao umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias anaejulikana kama  ‘Barnaba’ na Jean Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na maudhui ni kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika kuchangia na kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga. 

  Tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013 katika hoteli ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita tano (5) na kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa kwa shilingi za kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya Barclays kuanzia tarehe 29 Aprili, 2013.


  Mwaka 2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za kitanzania milioni 150 kutokana na  mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii.  Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
  1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
  2. Matibabu ya Fistula 
  3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi.

  Step Ahead Walk 2013 itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili tuweze kufanya badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania hususani masuala ya uzazi na afya ya watoto. 


  0 0

  Leo hii Uhuruone, Costech na Microsoft wametiliana saini MoU kwa ajili ya BoadBand4Wote itakayosaidia kufikisha internet na vitendea kazi kwenye vyuo vikuu. Utiaji saini huu umefanyika katika hoteli ya Westin mjini Capetown sambamba na mkutano wa World Economic Forum for Africa.


  Pichani Mshirika Mtendaji wa UhuruOne Mihayo Wilmore, Mkurugenzi Mtendaji wa COSTECH,Dk. Hassan Mshinda na Mkurugenzi, Legal & Corporate Affairs, Microsoft for Africa initiatives, Lois Onyango Otieno.

  0 0


  40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
  IT CAN'T GET BETTER THAN THIS!
  SAVE OVER £700!
  BEI ZETU NI CHINI SANA KULIKO SEHEMU YOYOTE

  AIR CARGO TO NAIROBI 
  £2.80 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
  ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN KENYA
  UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA TU KENDA HOUSE
  TOM MBOYA STREET NAIROBI
  FLIGHTS EVERY WEEK
  TO COLLECT CARGO FROM LONDON £25 
  TO COLLECT CARGO FROM OUTSIDE LONDON £50
  MINIMUM WEIGHT IS 35K
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0

  Meneja wa Programu ya Fanikiwa Kibiashara (BDG) Bw. Sosthenes Sambua (katikati) akiongea na Mhandisi Peter Chisawillo (kulia) na mkuu wa wilaya ya Nkasi, Bw. Iddi Kimanta (kushoto) wakati wa mafunzo ya kuwezesha kongano mbalimbali hapa nchini kujenga ubunifu na ushindani mjini Morogoro jana. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Scandnavian Institute for Competitiveness and Development (SICD), Pan African Competitiveness Forum (PACF) na BDG, programu iliyo chini ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

  Na Mwandishi wetu, Morogoro

  Mfumo wa kongano bunifu umetajwa kama mkombozi utakaoleta maendeleo endelevu Tanzania kama utazingatiwa na wadau mbalimbali hapa nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Programu ya Fanikiwa Kibiashara (BDG) ambayo inafanya kazi chini ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Sosthenes Sambua wakati wa mafunzo ya kuwezesha kongano mbalimbali hapa nchini kujenga ubunifu na ushindani mjini Morogoro jana.


  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa utalii na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh. Magessa Mulongo na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mh. Godbless Lema wakitoa msaada wa madawa mbali mbali kwa Hospitali ya St Elizabeth mbele ya Dkt Thomas Kway mganga mkuu wa hospitali hiyo mwenye koti jeupe.na wenye shati jekundu ni Mustapher mkurugenzi wa Bushbuck safaris.

  habari/picha na Mahamoud Ahmad wa blog ya jamii Arusha

  Serekali na wadau wa utalii wametoa vifaa na madawa mbali mbali vyenye thamani ya Tsh.18 milion kusaidia wahanga wa bomu mkoani Arusha na kuahidi kuanzaisha mfuko wa wahanga wa bomu uwasaidie hata baada ya kupona kwa majeruhi hao na kukusanya kiasi cha 100 milion kuanzisha mfuko huo.

  Wakikabidhi kwa pamoja vifaa hivyo naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa vifaa hivyo ni mwanzo wa kusaidia majeruhi hao na hospitali hiyo ya St. Elizabeth kwani ni hospitali nteule ya halmashauri ya Jiji la Arusha hivyo kusaidia kunahitajika kwa wakati huu ili waweze kwenda na kasi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

  Nyalandu akawataka wadau mbali mbali wa sekta ya utalii kufika kwenye hospitali hizo za Mt.Meru,na St.Elizabeth kuona ninamna gain wanaweza kusaidia majeruhi hao waweze kupata matibabu yaliosahihi na kuwa wamejitolea Dakatari bingwa kutoka Hospital ya Agakhan dkt.Aidan Njau kuja kusaidiana na madaktari wa hospital hiyo.

  “Tunatarajia kuanzisha Mfuko wa wahanga uitwao Victim Fund utakuwa ukisaidia majeruhi wakati wakiwa hospitali na baada ya hapo tutaendelea kusaidia hadi watakapoweza kuendelea na maisha yao kwa kuanzia mfuko wetu utakuwa na kiasi cha tsh 100 milion”alisema Mustapher mkurugenzi wa Bushbuck Safari ya jijini Arusha

  Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo alisema kuwa serekali imeamua kuwahamisha majeruhi zaidi ya watano kuhamia kwenye hospitali za Lugalo na Muhimbili kwa matibabu zaidi na kuwa pia wamewaleta Madaktari kutoka Kwenye jeshi la wananchi kusaidiana na madaktari kwenye hospitali zetu wakati huu.

  Mulongo alisema kuwa Mazishi ya wahanga wa bomu yatafanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi siku ya Ijumaa na kuwa wanatarajia waziri mkuu Mizengo Pinda ataongoza maelefu ya wakazi wa jiji la Arusha kwenye mazishi hayo kwa niaba ya serekali.

  Mulongo alisema huu si wakati wa kuchanganya suala hili na imani za kidini na kisiasa na kuwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kutulia na kuacha uchunguzi wa tukio hili uendelee bila ya kutoa manene mbadala.

  “Nawasihi sana kutulia na kuwa serekali ipo pamoja nanyi kwenye wakati huu mgumu hivyo tuendelee kuwa pamoja” alisema Mulongo.

  Kwa upande wake mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alisema kuwa anawapa pole majeruhi na wafiwa wawe na moyo wa subra wakati huu wa majonzi na mungu yupo karibu nao huku akiwataka wakazi wa jimbo lake kuwa kitu kimoja kwenye suala hili la wahanga wa mabomu kwa kuondoa tofauti zao za kisiasa.

  Makampuni mbali mbali yamekuwa yakijitolea vifaa mbali mbali kwa majeruhi wa bomu kampuni zilizotoa misambali mbali siku ya leo ni pamoja na kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC),Viola Safaris,shirika la Msalaba Mwekundu,Ngorongoro Consevetion Athourity na Bushbuck Safari na Hidden Velley Safaris Ltd zote za jijini Arusha.

  Vifaa vilivyotolewa na wadau hao ni pamoja na Magodoro,Mablanketi,Madawa ya inana mbali mbali yatakaosaidia wahanga na Hospitali kwa ujumla pia wamekabidhi kwa majeruhi rozali na vitabu vya mafundisho ya imani na vitenge kwa kinamama.

  Akikabidhi vifaa hivyo mkuurugenzi wa Viola safaris kwa Mganga mkuu.Mfawizi wa hospitali hiyo Dkt Mlay alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kwani Hospitali inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo pia chumba cha wagonjwa mahututi(ICU)hivyo akawataka wadau mbali mbali kushiriki kusaidia ujenzi wa wodi hiyo ya wagonjwa mahututi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)Assah Mwambene (kushoto) akimkabidhi zawadi ya jiko la umeme na gesi iliyotolewa na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Afisa Habari Georgina Misama baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.Nyuma yao (kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu Jamali Zuberi na Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Magazeti Raphael Hokororo (kushoto).
  Afisa Habari Mkuu,Mwanakombo Jumaa akimkabidhi Afisa Habari Georgina Misama , kadi ya pongezi kwa kufunga ndoa hivi karibuni, kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtakia kila la heri kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  World Chambers of Commerce have honoured a Tanzanian-designed scheme to use cell phones to identify and help overturn barriers to free trade across East Africa.


  The scheme won second prize in the World Chambers of Commerce competition for the best project amongst a field of other groundbreaking innovations from Britain, China, the Slovak Republic and Turkey.  The short messaging system (SMS) online non-tariff barrier (NTB) reporting and monitoring mechanism was developed by the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) to get the business community not just to grumble about NTBs but to log them, report them and get them referred to those with the power to overturn them.  The scheme has been supported by TradeMark East Africa, TMEA; a multi-donor-funded organization that seeks to streamline EAC trade to cut the cost of doing business and grow prosperity through strong economic integration. The support is part the TMEA Tanzania’s programme to strengthen private sector advocacy for the removal of NTBs through effectively reporting and monitoring of their existence.  This system is the first of its kind in East Africa and is a beacon in the battle against NTBs, regulatory or official hurdles which slow free commerce and add to the cost of transporting goods to the region, which already has the highest transport costs in the world.  It is a great pleasure to see that the in-house innovation can stretch its wings to the international community. The recognition that the NTBs SMS and online reporting and monitoring system has received is evidence that what we do, as a private sector, in creating favorable business environment adds value to the lives of people; not only because the world can see it but most importantly, that we contribute towards improving people’s welfare by making it easier to report and for authorities to monitor and eliminate all barriers hindering trade flow.  The award was announced during the World Chambers Congress held in Doha, Qatar last month. World Chambers Competition is the only global awards programme to recognize the most innovative projects undertaken by chambers of commerce and industry from around the world. The Competition provides a unique opportunity for chambers to showcase originality & ingenuity, and also demonstrate determination to strengthen SMEs, improve services provided to members. The competition takes place every after two years.  TCCIA acts as the private sector focal point on NTBs and gathers evidence so that it can lobby for their elimination. The system is also a source of information for policy makers who are directly responsible for some of those very NTBs.

  0 0

  Taasisi ya Hassan Maajar imetoa masaada wa madawati 250 katika shule za msingi mkoa wa Mwanza.

  Zaidi ya wanafunzi 700 katika shule tano za wilaya tano ya mkoa wa Mwanza zimepokea msaada wa madawati yaliyotolewa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.

  Jumla ya madawati 250 yalitolea na taasisi hiyo ikiwa ni kampeni yako ya kupunguza tatizo sugu la upungufu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, ilifanyika katika Shule ya Msingi ya Nyaminjundu, iliyoko Wilaya ya Misungwi. 

  Bwana Shariff Maajar, pamoja na Bi Zena M Tenga kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Engineer Evaristi Ndikilo.


  “Ni adimu na mara chache kuona Taasisi za kinyumbani za kiTanzania, kufika hapa mkoani kwetu. 

  Kwa hiyo napenda kutoa shukurani za dhati kwa Taasisi ya Hassan Maajar kwa msaada huu mkubwa na wenye thamani utakaochangia kuboresha elimu katika Mkoa wetu wa Mwanza”, alisema Engineer Ndikilo. 

   “Kama mikoa mengine ya nji yetu, ni wilaya na halmashauri za vijiji ambako msiaada kama hii inaitajika kwa wingi na ni kweli kati ya changamoto nyingi zinazowakabili watoto wetu, moja wapo ni hili la upungu wa mazingira bora ya Elimu, kwa hiyo tunawashukuru Hassan Maajar Trust kwa kuzingatia hizi changamoto na kwa kuufikiria mkoa wetu wa Mwanza”, aliongeza.  Huu ni msaada wa tatu chini wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) mkoa wa Mwanza ni mko watatu kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011.

   Hadi sasa Hassan Maajar Trust imekabidhi jumla ya madawati 1,194 kati ya madawati 1,764; Njombe (680), Singida (264), Mwanza (250). Mikoa itayofawatia ni Lindi na Rukwa. Garama za madawati haya ya mkoa wa Mwanza ni jumla ya Tsh 22,500,000.


  “Lengo letu hususan ni kujitahidi kuhakikisha Taasisi yetu inaboresha mazingira ya kusomea watoto katika shule zetu Tanzania”, alisema Zena M Tenga Mkurugenzi Mtendaji. “Tunatarajia na tunalenga kuhakikisha kuwa kampeni yetu ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto wengi iwezekenavyo na pia tutaendelea kuhamasisha jamii, taasisi tofauti na mashirika tofauti kuendelea kutuunga mkono ilituweze kufanikisha malengo yetu”, aliongeza.

  0 0

  Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa,Chaz Baba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza onyesho maalum la kuiingiza sokoni rasmi kwa albam yao mpya Risasi Kidole,litakalo fanyika siku ya Jumamosi Mei 11,2013 kwenye ukumbi wa Businesss Park,Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku wakisindikizwa na ndugu zao FM Academia Wazee wa Ngwasuma.
  Kiongizi wa Bendi ya FM Academia Wazee wa Ngwasuma,Presidaa Nyoshi El-Sadaat akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Bendi yake itakavyofanya mambo yao siku hiyo ya Jumamosi Mei 11,2013  kwenye ukumbi wa Businesss Park,Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Wanenguaji viongozi wa Bendi zote mbili wakionyesha namna walivyojiandaa vyema.

  0 0
 • 05/08/13--12:37: KUMBUKUMBU

 • ILIKUWA NI SEKUNDE, DAKIKA, SAA, WIKI, MWEZI NA SASA NI MWAKA MMOJA UMETIMIA TANGU BIBI YETU KIPENZI AKANASHE SHEDRACK MAKERE UTUTOKE GHAFLA TAREHE 08/05/2012 SAA 10 JIONI BILA YA KUTUAGA KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIKUSUMBUA.
  UNAKUMBUKWA SANA KWA UCHESHI, UPENDO NA KUWAJALI KILA KIUMBE CHA HAPA DUNIANI. HALIDHALIKA UNAKUMBUKWA SANA NA WANAO, WAJUKUU, VITUKUU, KILEMBWE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO. UMETUACHIA HUZUNI NA PENGO KUBWA KATIKA UKOO.
  MWENYEZI MUNGU, MUUMBA WA MBINGU NA NCHI AENDELEE KUKUPA MWANGA NA RAHA YA MILELE HUKO ULIPO KWANI YEYE NDIYE ALIYETOA NA YEYE NDIYE ALIYETWAA. JINA LA BWANA DAIMA LIHIMIDIWE. AMEN

  0 0

  WILLBARD NA MAI WAIFU WAKE HAPPINESS WAKIFUNGUA CHAMPAGNE


  MR & MRS MKOBA

  TABASAMU LA NGUVU KWA KUKIMBIA UKAPERA
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


                           
         CHAMA CHA MAPINDUZI

                                     TAWI LA UNITED KINGDOM.
  Website: www.ccmuk.org, ccmuk.org/blog, Facebook – chama cha mapinduzi uingereza, Twitter CCM UK.

         

  CCM UK INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE  KUPINGA VIKALI KITENDO CHA KIGAIDI KILICHOTOKANA NA ULIPUAJI WA BOMU KANISA KATOLIKI LA OLASITI JIJINI ARUSHA.

  Uongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Uingereza  tunapenda kuungana na Watanzania wote wapenda amani katika kuwapa salamu zetu za pole  Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha , kutokana na tendo shambulizi la kigaidi la kutupwa bomu kanisani hapo lililosababisha Watanzania Wawili kupoteza maisha na zaida ya 60 kujeruhiwa.

  CCM UK siku zote inawausia Watanzania kulinda Amani yetu na kushikamana kwa pamoja wakati wa kufanya hivyo bila ya kujali tofauti zetu za kiitikadi , kabila , rangi wala siasa .

  CCM UK tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Mwenyekiti wetu wa Taifa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuongoza kwa mfano bora pale alipokatiza Ziara ya muhimu nchini Kuwait na kurudi Nyumbani kwa haraka ili awe pamoja na Wananchi wake katika kuomboleza na kukemea vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.

  Aidha CCM UK  inaishukuru Serikali na Vyombo Vya Dola kwa hatua za haraka zilizochukuliwa katika kutafuta wahusika wa tukio hili la kinyama na lisilo na msingi na kuwaomba watanzania kuwa  watulivu wakati huu na kuviachia vyombo vya dola kufanya kazi yake na kuchukua tahadhari juu ya watu waovu wanaotaka kuwavuruga na kuwafarakanisha kwa misingi ya dini.

  CCM UK inatoa salamu za pole na kuwafariji  familia za wale wote waliopoteza Maisha yao na kuwaombea majeruhi wote  walioumia katika tukio hili wapate nafuuya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

                                                                 

  Imetolewa na Idara ya Itikadi, Siasa na Uenezi

  CCM - UNITED KINGDOM


  0 0

  Waendesha mada katika semina ya kuangalia changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki na njia za kuzitatua wakijadili umuhimu wa elimu ya muziki katika soko la muziki, kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Action Music Tanzania, Mandoli Kahindi, Mkurugenzi wa sanaa kutoka Global Music Academy Ujerumani,William Ramsay, Muaandaaji wa muziki wa Uganda, Kazi Kasozi na Mkurugenzi Mtendaji wa Ketebul Music Kenya, Tabu Osusa


  Semina hiyo ambayo inaambatana na maonyesho ya kazi mbalimbali za muziki yameandaliwa na Bayimba Cultural Foundation ya Uganda ambapo wadau mbalimbali wa muziki kutoka nchi mbalimbali wamejumuika kujadili na kubadilishana uzeofu juu ya soko la muziki kwa nchi za Afrika Mashariki. picha za matukio zaidi tembelea DOADOA

  0 0


  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mulongo katika Uwanja wa Ndege wa KIA.
  Askofu wa jimbo kuu la Arusha Baba Askofu Josephat  Lebulu akizungumza jambo na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda juu tukio lililotokea hivi karibuni.
  Paroko Pedy Kasterino wa paroko ya Tokeo la Bwana Bulka Olasite akimpa maelezo Mhe. spika jinsi mlipuko ulivyotokea katika kanisa la Mt. Joseph Olasite Mjini Arusha.
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwafariji katika majeruhi katika Hospitali ya Mount Meru kufuatia Mlipuko uliotokea katika Kanisa la Mt. Joseph Olasite, Mjini Arusha na kusababisha Vifo vya watu 3 kufariki na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa jumapili iliyopita.
  Paroko Pedy Kasterino wa paroko ya Tokeo la Bwana Bulka Olasite akimuongoza Mhe. Spika kuangalia eneo mlipuko huo ulipotokea.


older | 1 | .... | 126 | 127 | (Page 128) | 129 | 130 | .... | 3284 | newer