Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1277 | 1278 | (Page 1279) | 1280 | 1281 | .... | 3282 | newer

  0 0

   Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango- Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano , Mwanaidi Shemweta. NIC ilishiriki maonyesho ya 40 katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere maarufu kama sabasaba kama ilivyo desturi ili kutoa elimu kwa umma kuhusiana na maswala ya Bima. Pamoja na kutoa Elimu NIC imepata fursa ya kuelezea bidhaa mpya zilizokwishaanzishwa pamoja na zile mpya zinazotarajia kuanzishwa hususani Bima za KILIMO.  Wananchi wanakaribishwa kuja kupata elimu hizo.
   Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Bw. Elisante Maleko Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja baada ya kutembelea na kupata maelezo yahusuyo maswala ya Bima ndani ya banda la NIC. Wakuu hawa wameona umuhimu wa Bima zitolewazo na NIC na wamesisitiza swala la Elimu liwe endelevu ili jamii ya kitanzania ipate uelewa na hatimaye kukatia bima hizo kwa manufaa ya familia zao.
  Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango-Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akisaini kitabu cha wageni ndani ya banda la NIC baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalamu wa maswala ya Bima NIC.

  0 0
 • 07/04/16--03:05: MAAJABU YA KONOKONO.
 • Na Geofrey Chambua.
  1. Konokono ni mdudu asiye na mfupa hata mmoja mwilini mwake na kazi kubwa ya jumba lake ni kumsaidia mwendo na kuulinda mwili wake na mawaa.

  2. Konokono wanamiliki JINSI MBILI zote mbili ya kike na ya kiume na wao wanapotaka kupandana HUVIZIANA USIKU (nadhani nimeeleweka).

  3. Nchini Japan wataaalamu wamegundua kuwa uteute anaotoa mdudu huyu ni tiba nzuri kwa ngozi ya binadamu, na sasa tiba hiyo imeanza kupendwa barani Ulaya ikitumika sana kwenye saluni kwa ajili ya kusinga (massage). matokeo ya tiba hiyo inayogharimu kiasi cha dola 50 takribani kilo moja ya madafu (Sh 100,000.) huonekana papohapo na kwamba wadudu hao hutoa kamasi zenye protin muhimu kwa ngozi ya binadamu. Konokono hutambaa uso mzima na ukiongeza hela hadi mgongo wote UNATAMBALIWA na hii inaakisi hadi misuli mingine ya mwili na kukufanya ujisikie murua na mwanana kabisa.

  4. Wakati huku Tanzania, konokono akionekana mdudu anaetia kinyaa kwa baadhi ya watu,nchini za China na Japan wanyama hawa wamekuwa wakitumika kama kitoweo na wengi wao hufugwa na binadamu. (Nimewala sana Abuja kule wanatembezwa kwenye mabeseni wakipikwa huwezi kuwatambua mara moja kama ni konokono na ni watamu saaaana na supu yake ni kama supu ya pweza kwa umaarufu huku kwetu......nadhani nimeeleweka)
  5. Watafiti Wafaransa wamebaini kwamba unga wa konkono ni tiba muhimu sana kwa vidonda vya tumbo na mg 10 tu huweza kupunguza zaidi ya 42% ya vidonda vya tumbo na pia hutibu magonjwa sugu ya kurithi ikiwemo pumu na hata kutengenezea manukato.

  6. Nchini Papua New Guinea, Konokono kwa miongo kadhaa wametumika kama sarafu ya nchi hiyo wakati wa UJIMA lakini.

  0 0


  Wakuu wa Wilaya wa Wilaya za Mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Mstaafu Salimu Kijuu mara baada ya kula kiapo.Picha na Editha Karlo wa blog ya jamii-Kagera.
  Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Luteni kanali Denis Mwila akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera (hayupo pichani).
  Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Mkoa wa Kagera akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu,(hayupo pichani).
  Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Saada Malunde akila kiapo cha utii na utumishi na kuilinda nchi mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kagera.

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akimkabidhi vitendea kazi mkuu mpya wa Wilaya ya Bukoba mjini Deodatus Kinawilo.

  Baadhi ya wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Kagera Kabla ya kula viapo wakimpokea mgeni rasmi(ambaye hayupo pichani) wakati akiingia ukumbini.

  0 0

  Na Sultani Kipingo

  Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki, huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.

  Twenty Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.

  "Nimerudi kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, " anaogeza.

  Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.

  Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses.

  "Namkubali sana Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo", anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota kibao wakiwemo Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.

  Twenty Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane" uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni "Tamaa Mbaya" na "Ya nini Malumbano" na "Maisha ya Bongo"

  Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. "Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.

  Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
  Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
  Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi zake huku akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
  Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann  Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.(Picha na Sultani Kipingo)

  0 0
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa. 

  Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

  Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya. 

  Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara. 

  Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba. 

  Imetolewa na 
  Atley J. Kuni 
  Afisa habari na Mahusiano 
  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 
  MWANZA. 
  04, Julai, 2016. 

  0 0

   Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi akikabidhi kitabu kwa Mwenyekiti wa BAKWATA Singida, Sheikh Hamis Mohamed Kituke (kulia) wakati wa  hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wateja wake  mkoani Singida hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud.
   Mkuu wa Huduma za Kibenki zinazofuata kanuni na misngi ya kiislamu (Islamic Banking)  wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliyohudhuria hafla ya futari waliyoiandaa mjini Dodoma hivi karibuni.
   Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, James Kinyanyi (katikati), Mkuu wa Huduma Rejereja za Kibenki wa benki hiyo, Musa Jallow (kushoto), wakizungumza na mmoja wa wateja wa NBC, Yasser Yusuf (kulia),  katika futari waliyoiandaa kwa wateja wa Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakuu wapya wa wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi kwa kujituma katika kuwatumikia wananchi na atakayeshindwa atamshauri Rais amtafutie wilaya nyingine.

  Makonda ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha wakuu wa Wilaya Wanne kati ya watano  katika jiji la Dar es Salaam, amesema Mkoa wake ni wenye idadi kubwa ya watu kuliko mikoa mingine hivyo kila mtu lazima afanye kazi ya kutatua changamoto zilizo mbele yake na bila kufanya hivyo nafasi ya ukuu wa mkoa itakuwa imemshinda.

  Amesema kuwa wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni kupiga marufuku uvutaji wa shisha katika mkoa wa Dar es Salaam, Uvutaji Sigara hadharani na wataofanya hivyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.

  Makonda amesema kuwa operesheni ya kuondoa ombaomba bodo inaendelea na wakuu wilaya wametakiwa kusimamia operesheni hiyo kutokana na mazingira mazuri ya elimu yaliyowekwa kwa watoto hao kusoma ili waweze kuachana na utegemezi huo.

  Makonda amesema kuwa watu wanaowasaidia wanaomba wanafanya makosa kwa kufanya watu hao washindwe kuondoka katika jiji la Dar es Salaam.

  Aidha amesema kuwa tatizo la madawati bado lakini kuna upungufu wa vyumba vya madawati ambayo ni muhimu katika kuweza kuainisha katika kipindi hiki.

  Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo ni, Hashim Mgandilwa  wa  Kigamboni, Felix Lyaviva wa Temeke, Sophia  Mjema wa Ilala na Ally Hapi wa Kinondoni.

  Mkuu wa Wilaya wa Ubungo Humphrey Polepole hajaapa kutokana na udhuru ya msiba wa baba yake mazazi ambaye ataapa baada ya kumaliza udhuru hiyo.

  Wakuu wa Wilaya baada ya kuapishwa walikuwa na  maoni tofauti, kwa upande Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa amesema kuwa kazi yake ni kuitangaza Kigamboni kuwa ni Wilaya katika njia ya mbalimbali ya mawasiliano lakini sifa kwake kuanzisha Wilaya hiyo.

  Naye Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema ametangaza kiama kwa ombaomba katika jiji na kutaka maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi yao na kama watashindwa atawashughulikia.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa amefanya kazi siku 74 kabla hajateuliwa na Rais ameweza kumaliza tatizo la madawati kwa Wilaya ya Kinondoni na kuahidi kuendelea na kasi yake.


   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla ya  kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

  Na Mwandishi wetu.
   MKOA wa Mwanza  kwa kipindi chaa mwezi Juni  mwaka huu umekuwa shwari ikilinganishwa na ya mwezi mei mwaka huu. katika matukio ya uhalifu.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi  amesema kuwa pamoja na kuwa usalama kulikuwepo na baadhi ya matukio makubwa ya jinai kama mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji,kubaka na wizi wa mifugo.

  Amesema licha ya kuwepo kwa hata hivyo matukio  ya uhalifu yaliweza kushughulikiwa na jeshi la polisi wakishirikiana na wadau wa ulinzi na usalama vizuri, kwani baadhi ya watuhumiwa wa uhalifu walikamatwa na kufikishwa mahakamani, ambapo baadhi ya kesi zimemalizika na nyingine zinaendelea katika hatua tofauti mahakamani.

  Taarifa hiyo ilisema kuwa watuhumiwa walioguswa na ushahidi na kukimbia baada ya kutenda matukio ya uhalifu wanaendelea kutafutwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wananchi wenye nia njema ya kukabiliana na uhalifu katika mkoa wetu wa mwanza.

  Katika matukio  katika kipindi cha mwezi juni, 2016 jumla ya makosa 3753 yaliripotiwa, wakati kwa mwezi mei, 2016 makosa 3798 yaliripotiwa, hivyo  kunaupungufu wa makosa 45, sawa na asilimia 1.2%.

  Makosa yaliyotikisa makosa makubwa kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 yalikuwa ni 232 ikilinganishwa na ya mwezi mei, 2016 ambapo makosa makubwa 197 yaliyoripotiwa, hivyo kunaongezeko la makosa 35 ambayo ni sawa na asilimia 15.8%, aidha katika kipindi cha mwezi juni,2016 makosa madogo yaliyoripotiwa ni 3521 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016.

  Makosa ya Kawaida madogo 3601 yaliripotiwa, hivyo kunaupungufu wa makosa 80, sawa na asilimia 2.2%. hata hivyo upungufu huo unatokana na jitihada za jeshi la polisi kubuni na kutumia mbinu mpya za kupambana na uhalifu ambao umekua kutokanana kukua kwa teknologia pamoja na mbinu za kihalifu.

  Makosa yanayotokana na jitihada za jeshi la polisi wakishirikiana nawadau wa ulinzi pamoja na wananchi kupitia misako na doria, makosayapatayo 108 yaliripotiwa katika kipindi cha mwezi juni, 2016 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo makosa 77 yaliripotiwa, hivyokufanya kuwa na ongezeko la makosa 31 sawa na asilimia 29%.

  makosa makubwa na madogo ya usalama barabaranikwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa yote yaliyoripotiwa mkoani mwanza katika kipindi cha mwezi juni, 2016 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji ni 11,100 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapoyaliripotiwa jumla ya makosa 10,490, hivyo kunaongezeko la makosa 1,390 sawa na asilimia 12.5% matukio ya ajali za barabarani yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwezi juni ni 12, ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 13 hivyo kunaupungufu wa tukio 01 sawa na asilimia 08%. matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwezi juni,2016 ni 10.

  Amesema ikilinganishwa na mwezi mei 2016 ambapo pia yalikuwa 10.watu waliokufa kwenye ajali kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 ni 15 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 walikuwa 11, hivyo kuna ongezeko la vifo vya watu  wane  sawa na asilimia 27%.

  Katika kipindi hicho watu waliojeruhiwa kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 ni 21 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo walijeruhiwa watu 06 hivyo kunaongezeko la watu 15 sawa na asilimia 71.4% .

  Katika  kipindi cha mwezi juni, 2016 jumla ya makosa 11,088 yalikamatwa na kutozwa faini na kiasi cha tsh.329, 790,000 ikilinganishwa na mwezi mei 2016 ambapo jumla ya makosa 10,389 ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo ya shs. 311,670,000, hivyo kunaongezeko la makosa 699 na ongezeko la maduhuri ya sh. 20,970,000 sawa na asilimia 6.3% jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani baadhi yao wanaendelea kuficha wahalifu na uahlifu katika maeneo yao na kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa asilimia 100.

  0 0

    Balozi wa Korea, Song, Geum-young akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru baada ya balozi huyo kumtembelea mkurugenzi huyo LEO. Mazungumzo hayo yalihusu maendeleo ya hispitali hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru akitoa historia fupi ya MNH LEO kwa Balozi Korea, Song, Geum-young.
   Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare, Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Dk Julieth Magandi na Mkurugenzi wa Uuguzi, Sister Agnes Mtawa wakifuatilia mazungumzo LEO katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH.
  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusherekea miaka kumi ya letshego Tanzania limited jijini Dar es Salaam leo.

  Baadhi ya wadau wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini wakati wa kusherekea miaka 10 ya kampuni yao.

  Kampuni ya letshego Tanzania limited ikijulikana kama Faidika imesheherekea miaka 10 ya utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini na kuzindua upya safari ya mabadiliko na msukumo wa ujumuishaji kwenye sekta ya kifedha kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tanzania 

  Akizungumza kwenye hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini amesema wataendelea kutoa ufumbuzi wa kifedha utakaoboresha maisha na kuhakikisha ufumbuzi huo unaleta maana kwa watanzania .

  Aidha Dlamini amesema watashirikiana na Serikali kuwajengea ujuzi wananchi na kuhamasisha mahusiano ya kimkakati kwa lengo la kumwinua mtanzania mwenye kipato cha chini pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiria mali kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

  ‘Ili kufanikisha lengo la ujumuishaji wa kifedha faidika imeanzisha ufumbuzi wenye lengo la kuboresha maisha kupitia upatikanaji wa mikopo ya kilimo ,elimu, afya na nyumba kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati na wajasiriamali wadogo’, alisema Dlamini.

  ‘ Uzinduzi huu unakazia ahadi mpya ya Faidika isemayo Tuboreshe maisha’.ameongeza Dlamini. 

  Faidika imefanikiwa kuwafikia zaidi ya watanzania 45,000 nchi nzima ambapo wmenufaika katika maswala ya kifedha kutoka na huduma hizo kutolewa kwa urahisi, stahiki na kwa unafuu zaidi.

  Letshego ni taasisi inayotoa huduma za kifedha ambayo imejitolea kuendeleza ujuzi na vipaji na ina zaidi ya vituo vya uwakilishi 268 kupitia mitandao yake inayohudumia zaidi ya wakopaji laki tatu na wawekaji laki moja.

  0 0

   Mkuu wa Vodacom Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Domician Mkama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa Tecno Camon C9 ambayo itapatika kwenye maduka yote ya Vodaco yalipo Nchi nzimaa kwa bei ya shilingi laki (395,000) za kitanzania leo jijini Dar es Salaam.
   Meneja Mauzo wa TECNO Mobile Tanzania, Fred Kadinala akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kua TECNO inawajali watumiaji wa simu zake hivyo kuamua kuwapa zawadi kubwa na kuwaruhusu waagize simu kwa bei ndogo ili wapate simu hiyo mapema Zaidi. jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Tecno Camon C9,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Watoto wa Mtani Mjini Sumbawanga Wakithili, Kuwa wengi na wanao ongezeka kwa kasi katika Mji wa Sumbawanga, Globu ya Jamii kupitia Ripota wetu kuzunguka katika Mji huo wa Sumbawanga Mjini na kujionea hali halisi jinsi ambavyo watoto Watokao Vijiji vya Jirani na Mji huo wa Sumbawanga wanao kuja Mjini kwa lengo la kujishughulisha na Shughuli ndogo ndogo kwani Asilimia kubwa ya Watoto hao ni walio Ondoka Nyumbani kwao kutokana na Kukimbia Familia zao, Kutafuta maisha Mjini na Wengine miongoni mwao ni wale walio poteza Wazazi wao lakini Asilimia kubwa ya Watoto hao wana Wazazi wao na wamewaacha Vijijini kwao na Wengine walio telekezwa na Familia zao.
  Baadhi ya Watoto hao wakiwa katika jitiada za kuokota MakopoMtaani  kuajili ya kwenda kuuza .
  Baadhi ya Watoto hao wakiwa Nje ya Eneo la Duka wakiendelea na mambo yao.
  Watoto hao wakiendelea kuzunguka Mitaani katika shughuli zao za kila siku.
  PICHA NA MR.PENGO MMG.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mwingiliano wa kazi kati ya Mameya na wakuu Wilaya husababisha kushindwa kuelewana.

  Makonda ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya tano za jijini Dar es salaam, amesema kuwa Mkuu wa Wilaya anaweza kuingia katika Baraza la Madiwani au Katibu Tawala wa Wilaya na wakati mwingine kuweza kuzungumza jambo katika baraza la madiwani.

  Amesema kuwa meya licha kufanya kazi hiyo anatakiwa kuwa na kazi nyingine  ya kumuingizia kipato ambapo ni tofauti na Mkuu wa Wilaya ambaye anamuwakilisha Rais.

  0 0

  His Excellence Egon Kochanke Ambassador of the Federal Republic of Germany learning about Mobisol's high quality solar appliances and HD solar Tv at Saba Saba Trade Fair. 

    Saba Saba visitor learning about Mobisol's HD solar TV and solar home systems at the Mobisol booth in Nkurumah Hall at Saba Saba Trade Fair --- Germany-based solar-service company Mobisol provides a range of solar home systems with an affordable payment plan and is currently showcasing its largest solar HD TV available at the ongoing Dar es Salaam International Trade Fair (Sabasaba). 

  Mobisol Tanzania Marketing Manager Allan Rwechungura said that the largest solar HD TV recently launched in other markets in East African countries has been optimized for the use with Mobisol’s 200W Solar Home Systems. “Our largest solar HD TV is of high quality and comes with a two year warranty.

   Our customers can pay for the solar TV using mobile money in convenient installments, as they acquire the high quality TV together with their Mobisol solar system. The TV was recently awarded by the The Global Lighting and Energy Access Partnership as one of the best off grid appliances and is featured in their 2016 guide for outstanding solar and off-grid appliances. 

  We encourage people to visit us at Sabasaba in Nkurumah Hall to see our products; apart from the TV buyers can also acquire other solar-powered appliances such as haircutters, music systems and radios, irons and business solutions such as multiple phone chargers. 

  Mobisol is also focusing on conserving the environment – while, at the same time, the electricity we provide offers an opportunity for people to utilize it for various income generating activities which improve their economic wellbeing”. 

  To date, Mobisol has installed over 50,000 solar home systems across East Africa. Their systems come in varying sizes from 80 to 200 Wp to match the various energy needs of different households and its solar home systems provide enough electricity to power entire households or businesses with bright LED lights, and run radios, charge mobile phones and power a variety of household and consumer appliances. 

  The larger systems can also power small businesses enabling entrepreneurial customers to create additional income. Mobisol has shops in most parts of Tanzania that are popular known as MobiShop. In 2015, Mobisol won the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC)’s Momentum for Change Award and also a TV was recently awarded by LEAP as one of the best off grid appliances and is featured in their 2016 guide for outstanding solar and off-grid appliances. 

  "The Global Lighting and Energy Access Partnership (Global LEAP) is the Clean Energy Ministerial’s energy access initiative, and is led by the U.S. Department of Energy. Global LEAP was launched as a commitment to the Sustainable Energy for All campaign, and its programs and initiatives support the growth of sustainable commercial clean energy access markets throughout the developing world.

  0 0

  Taarifa iliyotukikia chumba chetu cha habari muda huu, inaeleza kuwa ajali mbali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria, imetokea katika eneo la Manyoni Mkoani Singida na kupelekea vifo vya abiria 24 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

  Akizungumza kwa njia ya kuelezea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nane mchana wa leo, ambayo inayahusisha mabasi ya Kampuni moja ya CITY BOYS ambalo moja lilikuwa likitoka Dar kwenda Kahama huku lingine likitoka Kahama kuelekea Dar. Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.  0 0

  Na Mwene Said,Globu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa onyo kwa  Wabunge Halima Mdee (Kawe)  na Mwita Waitara (Ukonga) kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili dhidi ya  kumjeruhi Katibu Tawala wa jiji, Theresia Mbando.

  kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na leo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa maelezo ya awali dhidi ya washtakiwa.

  Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Esterlia Wilson alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa maelezo ya awali lakini washtakiwa Mdee na Waitara hawapo mahakamani.

  Utetezi ulidai kuwa Mdee ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa amesafiri kwenda nchini Canada na Waitara ni mgonjwa.

  Hakimu alisema sababu zilizotolewa na upande wa utetezi hazina mashiko kisheria kwa kuwa wameshindwa kuwasilisha vielelezo vya kuithibitishia mahakama kwanini washtakiwa wameshindwa kufika kusikiliza kesi yao.

  “Kama kweli mshtakiwa Waitara ni mgonjwa upande wa utetezi mlipaswa kuwasikilisha vyeti mahakamani na kuhusu mshtakiwa Mdee aliyesafiri kwa safari zake binafsi kwenda Canada, siyo sahihi tunapaswa tuheshimu hizi taratibu ili kila kitu kifanyike kwa haki ya pande zote” alisema Hakimu Shahidi.


  Mbali na Mdee na Waitara, wengine ni, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea , Diwani wa Kata ya Tabata Kimanga, Manase Njema , Diwani wa Kata ya Kimara, Ephrein Kinyafu na mfanyabiashara Rafii Juma.


  Wengine waliounganishwa katika kesi hiyo ni, Diwani wa Kata ya Segerea Edwin Mwakatobe (31) na Mkazi wa Tabata Edwin Mwaipaja (40).

  Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa  Februari 27, mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam walimjeruhi Theresa Mbando  na kumsababishia maumivu mwilini mwake.

  Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo kwa nyakati tofauti na  upande wa Jamhuri  ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, uliomba tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

  Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali  Julai 27, mwaka huu, dhamana ya washtakiwa inaendelea.

  0 0

   
   Baadhi ya wananchi wakisaidia kuokoa watu waliopata ajali katika ajali  iliyohusisha mabasi mawili ya abiria, ambayo imetokea katika eneo la Manyoni Mkoani Singida na kupelekea vifo vya abiria papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika eneo la Kijiji cha Maweni kilichopo Tarafa ya Kintinku wilayani Manyoni Mkoani Singida leo.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
   
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam.
   

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiangalia ofisi mpya ya TANAPA iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
  Kuangalia ofisi.

  Jengo la Ofisi za TANAPA zilizopo Dar es Salaam.


  0 0

  Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.

  Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.

  "Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
  "Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi," alisema Chande.

  Nae mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.

  Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande.

  "Tangu walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia," alisema Bi. Kuruthum.Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.

  Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
  Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.


  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa zawadi za vitu mbalimbali kwa vituo 6 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eidd el Fitr. Zawadi hizo zimetokana na fedha zilizopatikana katika Tamash la Pasaka. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (kulia), akimkabidhi mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Irshaadi, Juma Kaseja, sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Eidd el Fitr, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya watoto waliohudhulia hafla hiyo.
  Msama akitoa zawadi za Sikukuu ya Eid el Fitr.

  Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,mapema leo jijini Dar katika vituo sita.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1277 | 1278 | (Page 1279) | 1280 | 1281 | .... | 3282 | newer