Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

BUNGE LIMEPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA ELIMU.

0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya akitoa ufafanuzi leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu wanapata elimu sawa na wale wasio na ulemavu kwa kuweka miundo mbinu rafiki katika shule na vyuo vyote nchini.
 Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Amina Mollel  akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwawezesha wanafunzi wenye Ulemavu sawa na wale wasio na ulemavu hasa kwa kuangalia miundombinu iliyopo ili iwe rafiki kwa kundi hilo na kuleta usawa katika kupata elimu.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo Bungeni  Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali  wa mwaka 2016.
 Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mbunge Viti Maalum Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi – MAELEZO - Dodoma)


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma. 
Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu anayempatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi  miaka mitatu.

“Muswada unapendekeza kuwa kifungu hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu kipya cha 60A ili kuweka masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa au kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, kinapendekeza adhabu yake iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.

Vile vile mtu atakayebainika kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuolewa au kuoa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitano gerezani au vyote kwa pamoja.

Mhe. Masaju aliendelea kwa kufafanua kuwa, sheria hiyo imependekeza kuwa pale ambapo kosa hilo litafanywa na mtoto basi adhabu yake itakuwa kwa mujibu wa masharti ya sheria ya mtoto. Hii ni kwa sababu sheria ya mtoto inakataza mtoto anayetiwa hatiani kufungwa gerezani.

Aidha marekebisho hayo katika sheria ya Elimu yanalenga kumjengea mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari mazingira mazuri ya kumaliza ipasavyo elimu yake kwa ngazi hiyo.Hivyo basi kila Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu atawasilisha kwa Kamishna wa Elimu taarifa ya robo mwaka kuhusu matukio ya ndoa na mimba kwa wanafunzi katika shule yake na hatua zilizochukuliwa.

Sheria ya Elimu inamruhusu mwanafunzi aliyepewa ujauzito kuendelea na masomo mara tu anapojifungua. Sheria hiyo inasubiri kuwekwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili ianze kutumika.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO MAALUM WA SADC

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (Pichani)ameondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria mkutano maalum wa wakuu wa nchi na Serikali (extra-ordinary summit) wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa niaba ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa atahudhuria kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika) kitakachofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC na utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao unafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).

Januari 20, mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagiza Serikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa nchini humo ifikapo Februari Mosi, mwaka huu. Pia, SADC Double Troika iliitaka nchi hiyo iandae mchakato wa kueleza njia za utekelezaji wa mageuzi kama yalivyopendekezwa kwenye ripoti ya tume hiyo ifikapo Agosti, mwaka huu.

Mkutano huo ulikuwa umepokea taarifa ya Tume ya Usuluhishi ya SADC kwenye mgogoro wa Lesotho iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Dk. Cyril Ramaphosa ambayo iliainisha mambo kadhaa yakiwemo ya kikatiba na kiusalama ndani ya nchi hiyo.

SADC Double Troika ni kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation).

SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.

Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ)

Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk. Aziz Mlima na maofisa wengine waandamizi.

DIAMOND TRUST BANK (DTB) HOST IFTAR EVENT TO THE CUSTOMERS IN TANGA

0
0
Diamond Trust Bank Tanzania (DTB) held an Iftar event to its customers in Tanga on Saturday 25th June 2016. The event took place at Nyumbani Hotel and was well attended by over 200 invited guests and customers.

The event was graced by the presence of Tanga Regional Administrative officer Eng. Zena Said, Retired Tanga Mayor, Hon. Kassim Kisauji and Chief Sheikh of Tanga, Juma Ali Luwuchu.
Chief Guest, Former Mayor of Tanga, Hon. Kassim Kisauji speaks to invited guests during an Iftar event hosted by Diamond Trust Bank Tanzania at Nyumbani Hotel in Tanga over the weekend and was attended by over 200 guests and customers.
A cross section of customers in the buffet line during an Iftar event hosted by Diamond Trust Bank Tanzania DTB) held at the Nyumbani Hotel in Tanga over the weekend and was attended by over 200 guests and customers.
Customers seated and dining during an Iftar event hosted by Diamond Trust Bank Tanzania DTB) held at the Nyumbani Hotel in Tanga over the weekend and was attended by over 200 guests and customers.

WAZIRI NAPE NNAUYE AFUNGUA RASMI STUDIO ZA RADIO YA JAMII KATIKA CHUO KIKUU HURIA, KINONDONI JIJINI DAR LEO

0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.  Kulia ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda. Studio hiyo ni moja kati ya Studio nyingi za Radio za Jamii zilizopo maeneo mbali mbali hapa nchini, zinazodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA). 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza katika kipindi cha moja kwa moja cha Redio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), mara baada ya kuifungua rasmi Studio hiyo, Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda akizungumza wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.

TAASISI YA NITETEE YAIOMBA SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI VIZURI

0
0

Serikali imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa ruzuku kwa taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi ya kufuatilia na kubaini matatizo yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee.

Licha ya serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo, jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale wanaohitaji msaada wa kupata elimu .

Kufatia serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza na kubainisha changamoto zinazowakumba.Yapo malengo yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania.“Lakini wapo Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.

Taasisi ya nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba familia zinazoishi katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.

Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.

Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula katika viwanja vya Bunge, Dodoma

Mkazi wa kigoma ajinyonga kwa kinachosadikiwa kuwa wivu wa mapenzi

0
0
Na Abel Daud wa Globu ya Jamii, Kigoma
Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Norbert Gidion (30) mkaazi wa Masanga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  amekutwa  amefariki  dunia akiwa amejinyonga kwenye mti wa mwembe kwa kile kinachosadikika kuwa ni  wivu wa mapenzi
Kamanda wa polisi mkoani kigoma Afande Ferdinand Mtui, amethibitisha tukio hilo na kusemw kwamba upelelezi wa awali unaonesha kuwa  chanzo cha kifo cha Marehemu Norbert Gidion  ni  kutokuwepo na maelewano dhidi ya marehemu  na mke wake, Bi.Happyfania Caristus. 
"Natoa  wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa mazingira kama hayo husababisha kutokea vifo visivyotarajiwa kwa jamii:, alisema Kamanda Mtui.
Wakielezea tukio hilo wapangaji wenzie marehemu wamesema kuwa kwa kipindi kirefu marehemu alikuwa safari hadi umauti unamkuta na kwamba  hata alivyorudi safari alikuwa halali nyumbani kwa mke wake.
Mzazi wa marehemu Bw. Gidioni Hungu amesema  kuwa mazingira ya kifo hicho imekuwa sintofahamu kwani alikuwa hana maelewano mazuri na mkewe.



MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUMATANO JUNI 28, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA.

0
0
 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila. 
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 

 Na Devotha Kihwelo. 
 MCHEZAJI bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji cha Coca - Cola . Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca - Cola imetambua umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo. “Kwetu sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na Coca - Cola”, alisema. Kiganja alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao na hiyo italeta heshima nchini. Kwa upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa. Alisema Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili kufikia malengo kama aliyofikia Mussa. “Sisi kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo inayoendelea,”alisema. Mussa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti 11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.

NSSF YAOTA ELIMU KUHUSU MAFAO KWA WAFANYAKAZI WA TAZARA

0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa Elimu ya Pensheni kwa wâfânyakazi wa  TÂZARA.

Lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha wânâchama kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa pensheni ya Uzeeni.
Akizungumza na wafanyakazi hao Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa NSSF, Christina Kamuzora alisema kuwa kanuni hiyo imekwishaanza kutumika na kuwahakikishia kwamba malipo yao ya pensheni yatatolewa kwa uharaka zaidi kwa kuwa huduma zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA (hawapo pichani), wakati wa utoaji wa elimu kwa wafanyakazi hao.
 Wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora (hayupo pichani)

introducing "SU" by Yamoto Band featuring Ruby

GGM YATOA VIFAA TIBA KWA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.

0
0
WAFANYAKAZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) wametoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,  Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi amesema kuwa Msaada uliotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kitengo cha watoto ni wadhamani ya shilingi milioni 23.

Pia amesema kuwa msaada huo ni kwaajili ya kusaidia jitihada Serikali katika kuboresha huduma za Afya hasa katika kitendo cha watoto katika hospitali hiyo.
Nae Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mary Charles aliwashukuru wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kutoa msaada katika Hospitali hiyo.
"Lengo la ni kuwa sehemu ya Jamii ambapo uwepo wa Mgodi unaleta manufaa kwa jamii inayozunguka." Alisema Mvungi.

Vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa GGM katika Hospitali ya Muhimbili leo ni Bp Machine 10, Infrsion Pump 2 Themometers 6110, Standing Weighing Scale 6, Nebulises 3 na Pulse Oxymeter 10.

 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi (Wapili kulia) akikabidhi msaada wa Vifaa vya matibabu kwa watoto kwa Chama cha madaktari wa watoto Tanzania ukipokelewa na Mkuu Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 Bara baada Mkuu Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa yaMuhimbili, Aminiel Aligaesha kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa watoto naye akakabidhi Msaada huo uliotolewa na Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM) kwa Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.

 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.

Wizara ya Michezo yakutana na kampuni ya B.C.E.G yazungumzia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa.

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kushoto) akizungumza na Meneja kampuni ya B.C.E.G Bw. Xiong (Kulia) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016.
 Meneja kampuni ya B.C.E.G Bw. Xiong (Kulia) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kushoto) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kulia) akizungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Selcom (Kushoto) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016. 
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

LOVING MEMORY OF OUR DEREST DAD.

0
0
R.I.P DAD IN LOVING MEMORY OF OUR DEREST DAD

GODFREY MWAMKAI KIHIYO.
FROM 27.11.1947 TO 30.06.2015.
It was very painfull whem you left us on 30th June, 2015 it is realy hard to face that fact daily. Athough our lives’ journeys have bid us be apart you will always be in our hearts because in there you are still living. You are dealy remembered by your wife,family friends and neghbours and your children Lilian, Anna, Emmanuel, Gerald and Joseph and grand children Noela,Doreen, Mitshell, Careen, Lisa, Charity, Hans, Alvin, Ian,Lewis and Jordan, inlaws Ladis, Paschal, Dina, Hiltrudes and Sylvia.

"I am the resurrection and the life. He who believes in me will live, even though he dies, and whoever lives and believes in me will never die." (John 11:25-26).

BEI YA MADAFU LEO.

KAMANDA SIRRO AWATAKA WASHABIKI WA MPIRA WA MIGUU WALIO NJE YA UWANJA WA TAIFA KURUDI MAJUMBANI, KWANI UWANJA UMESHAJAA

0
0
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya Mashabiki wa Yanga waliokuwa wamekusanyika nje ya Geti Kuu la Uwanja wa Taifa, kuwataka kutawanyika kurudi makwao kutoka na Uwingi wa washabiki waliokuwepo uwanjani hivi sasa, Kufuatia Mtanange baina ya Yanga na TP Mazembe ya Nchini Congo ikiwa ni muendelezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Kamanda Sirro amewataka Washabiki hao pamoja na wale wanaoendelea kuja Uwanja wa Taifa, kuahirisha safari hiyo kwani Uwanja umeshajaa, hivyo warudi tu majumbani kwani mchezo huo utaonyeshwa pia kupitia Vituo vya Televisheni.
 Kamanda Sirro akimtaka mmoja wa Washabiki hao kuacha fujo.
 Washabiki wa Yanga wakiwa nje ya Geti kuu la Uwanja wa Taifa.
Askari Polisi wakiwatawanya washabiki hao.
 Mshike mshike nje ya Uwanja wa Taifa kwa wale waliokaidi amri ya Jeshi la Polisi.

WAKULIMA WADOGOWADOGO NA WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA KILIMO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

0
0
Dar es salaam, Wanawake wakulima wadogowadogo wakiongozwa na waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na shirika la Oxfam, wamekutana pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na baadhi ya wanafunzi kutoka elimu ya juu, Tanzania kujadili Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17 na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akifungua Mkutano huo wa siku tatu, Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka Kibona alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya majadiliano juu ya Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali ilivyo sasa ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia kuibua changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau suala la mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa katika kilimo.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema mabadiliko ya Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko ya tabia nchi mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba changamoto kubwa zaidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji chumvi kuingia nchi kavu na kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua kwa kina cha maji katika mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao.

Alisema kuwa mambo yote hayo yamekuwa yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana na changamoto hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi ya mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto, matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.

Nao wakulima hao kwa nyakati tofautitofauti walizungumzia suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa changamoto nyingi wanazozipata kwa kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na elimu na huduma mbalimbali zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo basi kupitia mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji wa bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya kilimo nchini.

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Picha na Fredy Njeje .

LISSU AJISALIMISHA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

0
0
Mwene Said wa Blogu ya Jamii Dar es Salaam. 

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amepandishwa kizimbani baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kujibu tuhuma za kuchapisha chapisho la uchochezi lenye kichwa cha habari' Machafuko yaja Zanzibar'. 

Lissu alifika mahakamani hapo jana saa tano asubuhi, kwa ajili ya kuitikia wito wa kumtaka kwenda kujibu tuhuma za uchochezi zinazomkabili baada ya washitakiwa wenzake wawili akiwemo Mhariri wa Mawio ambalo lilifungiwa kwa muda usiojulikana, Simon Mkina kusomewa mashitaka. 

Mbunge huyo na washitakiwa wenzake Mkina na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.Upande wa jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi kwa kushirikiana na Salim Msemo, ulidai mahakamani hapo kuna washitakiwa Lissu, Mkina na Mehboob na mshitakiwa Jabir Idrisa bado hawajampata na wamepata taarifa anaumwa. 

Kadushi aliomba kumsomea mashitaka Lissu, ambapo alimsomea mashitaka matatu ya kula njama kuchapisha chapisho la uchochezi, kuchapisha taarifa yya uchochezi na kosa la tano ambalo ni mbadala wa kosa la pili la kutishia.Wakili huyo alidai Lissu na wenzake kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu, Dar es Salaam, walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’. 

Pia Lissu na wenzake walidaiwa Januari 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa nia ya kuleta chuki na uchochezi kati ya wananchi na mamlaka halali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye uchochezi.Aidha, Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu. 

Lissu alikana mashitaka hayo, ambapo Hakimu Simba alisema Juni 14, mwaka huu, shauri lilipokuja kwa mara ya kwanza upande wa utetezi ulileta pingamizi juu ya uhalali wa mashitaka wakiomba yafutwe.Kesi hiyo itatajwa Julai 14, mwaka huu. 

HIVI NDIVYO VIKOSI VYA YANGA NA TP MAZEMBE VINAVYOINGIA DIMBANI JIONI HII HAPA TAIFA

Waziri Nape akutana na Wanachama wa Shirikisho la kazi za Sanaa za Ufundi Tanzania.

0
0
Na Benedict Liwenga-WHUSM.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ameahidi kuzitataua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) ikiwemo upatikanaji wa Hati Miliki ya Kiwanja kwa ajili ya kazi zao, Ushuru unaotozwa kupitia Idara ya Maliasili nchini pamoja na Sheria ya Tozo katika Viwanja vya Ndege.

Mhe, Nnuaye ametoa ahadi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wanachama wa Shirikisho hilo ambapo amesema kuwa, suala la upatikanaji wa Hati Miliki ya eneo kwa ajili ya kazi za Wachongaji hao alishaanza kuifanyia kazi kwa kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na amewahakikishia kwamba Hati ya eneo hilo itapatikana ili Wachongaji hao waweze kuwa na eneo lao maalum la kazi zao.

‘’Suala la upatikanaji wa Hati Miliki katika eneo lenu ambalo limekuwa likileta minong’ono niachieni mimi kwani najua katika hili kuna baadhi ya watu wenye fedha wanataka kuwakandamiza watu wasio na uwezo kwa kudai kuwa eneo ni la kwao, hapo awali nilishafanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na nawahahakikishieni kuwa haki itatendeka, kwani hakuna mtu mwenye mfuko mkubwa wa kuweza kuiingiza Serikali nzima katika suala hili’’, alisema, Mhe. Nnauye.

Kuhusu suala la Ushuru unaotozwa na Maliasili nchini, Mhe. Nnauye amesema kuwa yuko tayari kukaa na watu wa Maliasili na kuona namna gani ushuru huo unavyotozwa hususani kwa Wachonagji hao pasipo kuonewa mtu ambapo pia ameshauri kuwa baadhi ya kodi ambazo zinazoweza kuua biashara za watu wenye vipato vya chini ni vema zikaondolewa ili zisiendelee kuwaumiza.

Aidha, Mhe, Nnauye ameahidi kutembelea maeneo ya Viwanja vya ndege ili kuweza kujua baadhi ya bidhaa za kazi za Uchongaji ambazo zimekuwa zikikamatwa na Watendaji viwanjani hapo zimekuwa zikiishia wapi ili kuondoa malalamiko yanayoelekezwa katika viwanja hivyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea maelezo kuhusu sanamu iliyochongwa toka kwa Mwandamizi na Msemaji wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Nyunga Joseph Nyunga wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa tatu kushoto) akiangalia kazi za sanaa ya uchongaji ndani ya moja ya mabadanda ya Wachongaji hao wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) wakati alipowasili katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.

PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

Wafanyabiashara wahimizwa kuchukua mashine za EFD.

0
0

Na: Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kugawa Mashine za Kutunza Hesabu za Kodi za Kielektroniki (EFD) bila malipo kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kachwamba alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Neema William Mgaya juu ya mpango wa serikali kugawa mashine hizo Nchi nzima.

“Nia ya Serikali ni kusambaza mashine za EFD Nchi nzima lakini tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo jumla ya mashine 5,703 zinaendelea kugawiwa kwa wafanyabiashara wa kati na wale wadogo ambao mauzo ghafi yao ni kati ya shilingi milioni 14 mpaka milioni 20 kwa mwaka,” alifanunua Mhe. Ashatu.

Aliendelea kwa kusema kuwa, japo mashine hizo zimekuwa zikitolewa bure lakini wafanyabiashara hawafiki katika ofisi za TRA kuzichukua. Hivyo amewataka kundi hilo la wafanyabiashara kufika katika ofisi za TRA wanazolipia kodi katika Mikoa ya Ilala, Kinondoni au Temeke kuchukua mashine hizo, kwani ni wajibu wa kila mfanyabiashara kutumia mashine hizo katika mauzo ya kila siku.

Aidha Mhe. Ashatu amesema kuwa utaratibu wa matumizi ya mashine hizo ulianzishwa kwa lengo la kurahisisha na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za biashara za walipa kodi. Aliongeza kuwa mfumo huo ulianzishwa ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya utunzaji kumbukumbu za mauzo na utoaji wa risiti za mauzo zinazoandikwa kwa mkono.

Vile vile mfumo huo umerahisisha usimamizi na ukadiriaji wa kodi kwa kuwa kumbukumbu zote za mauzo na manunuzi huhifadhiwa na kutunzwa kirahisi kwenye mashine za EFD na taarifa za mauzo ya mlipa kodi hutumwa kwenye seva ya TRA kwa njia ya mtandao kupitia mashine hizo.

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AWAAPISHA NAIBU KATIBU WAKUU LEO.

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein   akimuapisha Dk.Islam Seif Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd,Hassan Abdulla Mitawi  kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Hassan Abdulla Mitawi  baada ya kumuapisha    kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
[Picha na Ikulu.]{28/06/2016.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images