Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1268 | 1269 | (Page 1270) | 1271 | 1272 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila (wa tatu kutoka kushoto), pamoja na watendaji wakuu wa  wizara, wakifuatilia kwa makini taarifa ya Maendeleo ya Master Plan ya miji ya Arusha na Mwanza, iiliyokuwa ikitolewa na Wataalam wa Mradi wa kuendeleza miji hiyo  wa Kampuni ya Surbana ya nchini Singapore. Master plan hizo,zinatarajiwa kukamilika ifikapo; Agosti 19, 2016.

  0 0

  Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu  TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.
  Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.
   Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa  BAA Gwamaka Andrew (Kushoto) akimkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia)
  Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakiwa katika uzinduzi wa BAA
   Mgeni Rasmi akipata picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa BBA waliomaliza muda na wale wa sasa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  0 0

  Maandalizi ya mwisho mwisho ya Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yamepamba moto, ambapo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amefanya ziaa ya kukagua maandalizi hayo. Pichani ni Waziri Mwijage akikagua maandalizi kwenye moja ya mabanda. Kulia ni Kaimu Mkuugenzi wa Tantrade, Edwin Rutageruka. Maonyesho hayo yanaanza kesho tatehe 28/6-8/7/2016.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na kauli za baadhi ya viongozi wa Young Africans SC kushawishi mashabiki wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja kwa moja wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Dar es Salaam. 

  TFF ikiwa msimamizi mkuu wa mpira wa miguu Tanzania, inawajibika na mara moja inachukua nafasi hii kuwatahadharisha baadhi ya viongozi wa Young Africans, wanachama na mashabiki wao kutofanya hivyo kwani itakuwa ni kinyume na  kanuni za mashindano na mikataba ya udhamini katika hatua hii. 
  Ikumbukwe kwamba CAF inamiliki asilimia mia moja ya haki za habari na masoko katika ngazi hii ya makundi na jaribio lolote la kukwamisha matangazo ya biashara au utengenezaji na urushaji wa matangazo ya televisheni au ukwamishaji wa shughuli zingine kama hizo kwa CAF au wakala aliyeteuliwa na CAF kutaigharimu klabu mwenyeji si kwa kutozwa faini tu lakini pia uwezekano wa kuondolewa mashindanoni. 

  Pia TFF inatoa tahadhari hiyo ikiwamo ile ya utamaduni wa kukaa uwanjani ili kuepusha aina yoyote ya vurugu kwenye michezo yake hususani hii ya hatua ya makundi. TFF inafahamu kuwa tayari viongozi wa Young Africans walikwisha kusoma nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusu kanuni na masuala ya udhamini kwa timu zinazofuzu hatua ya Nane Bora.
  Wapenzi wa Yanga wanaombwa kufika kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu  timu yao ikiwa ni njia ya kuitia hamasa.Hata hivyo shamrashamra hizo zifanyike kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za Mpira wa Miguu na sheria za nchi. 
  Vitendo vya kuashiria vurugu na kufanya vurugu vikithibitishwa katika taarifa ya Mwamuzi, Janny Sikazwe wa Zambia; Kamishna wa mchezo, Celestin Ntangungira wa Rwanda na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza, hatua zake zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo KUONDOLEWA KWENYE MASHINDANO. Vilevile vitendo vya kutishia amani,kudhuru mwili au kuharibu mali vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kijinai. 
  Katika mchezo huo wa kimataifa Na. 107, Mwamuzi Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. 
  Wakati huohuo, kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kinatarajia kukaa siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2016. Taarifa zaidi itatolewa karibuni.

  …………………………………………………………………….
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

  0 0


  Kituo cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe, kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa mbalimbali vikiwe vile vya usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya Watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam.

  Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho, Said Fella, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke ambayo pia ni majirani zao ambapo pia amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa likifika Hospitalini hapo kuchangia misaada mbalimbali.

  Said Fella ameongeza kuwa, alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.

  “Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema Fella.

  Akipokea msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.

  “Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oximeter cha kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka au la na Mashine ya Nebulizer yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema Nyumbiage.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake takribani 50 alioambatana nao hospitalini hapo, msanii anayeunda kundi la Yamoto, Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya hivyo wakati mwingine watakapopata nafasi.

  Tukio hilo la aina yake kwa kundi hilo ambalo ufanya mara kwa mara katika kutembelea jamii na kusaidia misaada, limeweza kupongezwa na baadhi ya ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wenyewe kwa kueleza kuwa ni tendo la kuigwa na kila mmoja wetu hasa wasanii ambao ni kioo cha jamii.Baadhi ya vijana wanaounda kundi la Mkubwa na Wanawe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati wa tukio hilo lililofanyika leo Juni 26.2016.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akielezea namna vijana wake walivyoguswa na kuamua kujitolea kwa ajili ya watu wenye kuhitaji wakiwemo wa Hospitali hiyo ya Temeke.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akimkabidhi baadhi ya vifaa Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage Baadhi ya wasanii wa kundi la Yamoto Band ambao pia wanatoka Mkubwa na Wanawe wakitoa vionjo kadhaa wakati wa tukio hilo.
  Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akishukuru kwa hatua hiyo ya kurudisha fedhila kwa Jamii.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
  Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
  Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
  Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

  Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.

  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.

  Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
  Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

  Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.

  Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa).  0 0

   Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipinga mpira kuashiria uzinduzi wa rasmi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016. Uzinduzi huo umefanyika Jumapili 26 Juni 2016 kwenye makao makuu ya Airtel Tanzania Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016 jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
   Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars.
  Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars.
  Airtel yazindua msimu wa 6 wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016
  Dar es Salaam, Jumapili 26 Juni 2016  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua msimu wa sita wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars na kuwapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) za kukuza mchezo wa soka.

  “Programu za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale duniani. Ndiyo maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo matunda yake yameonekana dhahiri katika kipindi cha miaka mitano iliyopita”, alisema Nnauye.   

  Alitoa mfano wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambayo wachezaji wake 10 wa kutumainiwa wametokana na Airtel Rising Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars vilevile yanaoneka dhahiri kwenye timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo wachezaji wake wote wanatokana na programu hii ya vijana”, alisema Nnauye. Klabu za daraja la kwanza na ligi kuu Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya Airtel Risings Stars. 


  Waziri amewataka viongozi wa soka kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel Rising Stars ili kuweza kubaini vipaji vingi zaidi kupitia mashindano haya ya vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu za wasichana na wavulana kuanzia ngazi ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa kampuni ya Airtel Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo imesaidia kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo huo marufu hapa nchini.

  Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha kuaminika”, alisema.
  “Kwa kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar, Airtel Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia mchezo wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa Tanzania. Ni njia ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga mkono”, alisema.  

  Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya Airtel Rising Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa soka hapa nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono. Naamini kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.
  Airtel Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke,  Arusha, Lindi na Zanzibar.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la bima la taifa Sam Kamanga akikabidhi hundi ya tshs milioni 95,000,000 kwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Natujwa Mellau kwa ajili ya malipo ya gari la halmashauri lililopata ajali maeneo ya kerege Bagamoyo.
   Kaimu Mkurugenzi wa shirika la bima la Taifa Sam Kamanga akizungumza na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya bagamoyo,Natujwa Mellau ofisini kwake Bagamoyo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumsalimia Rais.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheuin akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada  mazungumzo yao.
  [Picha na Ikulu.] 27/06/2016.

  0 0

   Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina, Dodoma.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (hayumo pichani wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango mwishoni mwa wiki.
  (Stori na Picha na Joyce Mkinga)  Na Joyce Mkinga.
  SEKTA Binafsi katika ngazi zote ni lazima ishirikishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21 uliozinduliwa hivi karibuni.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliyasema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
  Bibi Florence Mwanri amesema sekta binafsi ni wadau muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo hivyo, wanatakiwa kushirikishwa katika mipango yote ya Serikali.

  “Katika mipango yetu katika ngazi zote lazima sekta binafsi ishirikishwe kwa sababu wao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo” alisema Bibi Mwanri.

  Amesema maafisa mipango wanapoibu miradi mbalimbali katika ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa ni lazima sekta binafsi ishirikishwe ili kuwapa fursa nzuri ya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo ambao unalenga katika Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya watu.

  Mkutano huo uliwashirikisha wachumi na maafisa mipango 170 kutoka katika wizara, idara za serikali, sekretarieti na mikoa na wilaya, taasisi za utafiti, na sekta binafsi ulikuwa na kaulimbiu ya Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21.

  Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na utelekezaji wake.
  Mpango huo unatarajia kugharimu Trilioni 107 ambapo Sekta binafsi itachangia  Trilioni 48.

  Akiwasilisha maazimio ya mkutano huo Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kutoka Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete amesema Serikali na sekta binafsi wakutane pamoja na kupanga mikakati ya kutekeleza mpango huo wa maendeleo.

  Vile vile, Dkt Madete alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuingiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia katika mipango ya Serikali ikiwa ni pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
  Mkutano huo uliandaliawa Tume ya Mipango kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

  0 0

  Jiwe la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300.
   (Picha na Francis Dande).
  Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
   Rais John Magufulia (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikli. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.

  0 0

   Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Tanzania, Bw George Shumbusho (aliesimama) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 


  Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

   Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kulia ni Mkuu wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji.
   Mkuu Wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House, Al-Kareem Bhanji aki akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kushoto ni Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga.
   Kikundi cha Sana cha Bagamoyo wakiigiza kama Waathirika wa Dawa za Kulevya.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
  Kituo cha Usaidizi Wa Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Bagamoyo Sober House leo,June 26,2016 kimeadhimisha siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya.

  Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka June 26 lakini kwa Mwaka huu Kituo cha Sober kimeadhimisha siku hiyo Wilayani Bagamoyo.

  Akizungumza katika Maadhimisho hayo,Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga amesema vita vya Mapambano ya Dawa za Kulevya si vya Serikali pekee wala vya mtu mmoja bali ni vita vya kila mtu,ambaye anapaswa kuwajibika katika eneo husika ili kutokomeza kabisa uingizwaji Wa Dawa hizo.

  Pia,Mkuu huyo Wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi Wa Dini ,Wananchi pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa pamoja katika kutoa taarifa za kuwafichua waingizaji Wa Dawa hizo ili Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria.

  Amesema,Serikali imeahidi kupatikana kwa eneo kubwa ili kuendeleza kituo hicho na kuwasaidia vijana ambao ndio waathirika wakubwa Wa janga hilo na kuitaka jamii kuwatambua na kuwabaini waathirika wa Dawa hizo.

  Kwa upande wake,Mkuu Wa Kituo hicho cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji amesema kituo hicho kimesaidia watu zaidi ya 100 mpaka sasa,ambapo ametoa Changamoto za ukosefu wa Majengo kituoni hapo  jambo ambalo limepelekea kwa sasa kulipa kodi kubwa ya pango.

  Pia ameiomba Serikali kupatikana Ardhi ya kutosha ili kuweza kuongeza majengo na kukidhi haja ya kupokea Waathirika 200 ikiwa Wanaume 150 na Wanawake 50.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. wengine ni wanachama wa Simba sport Club.
   Balozi wa Amani wa Simba, Risasi Mwaulanga akizungumza kuhusiana na wanachama na mashabiki wa Simba kwenda kuishangilia timu ya Yanga katika mchezo utakaochezwa katika uwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  BALOZI wa Amani wa Simba, Risasi Mwaulanga amewataka Wanachama wa Simba na wapenzi wa mpira wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwa ajili ya kuishangilia na kuisapoti Timu ya Yanga katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa. Wanachama hao wa Simba kutoka Wilaya ya Temeke wamesema kuwa uzalendo unatakiwa kuwekwa mbele na wao kama wapenda soka basi hakuna budi kuweza kuishangilia Yanga kwani kama wakifanya vizuri nchi itajitangaza.

  Amesema kuwa, kuna wanachama wengi wa Simba ambao watajitokeza kwa wingi kuweza kuisapoti Yanga katika mchezo huo pia wanaamini kuwa kama watafanya vizuri na kuchukua kombe hili basi wataongeza timu katika michuano ya kimataifa. "Tunapocheza kwenye mechi za ligi tunakuwa na ushindani ila wakati mtani wetu anacheza mechi za kimataifa ni lazima tuonyeshe uzalendo na kuishangilia kwa juhudi zetu zote ili iweze kufanya vizuri,".

  Naye Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa anafurahishwa sana na hatua ya wanachama hao kuja kuisapoti timu yao hasa katika kipindi hiki cha michuano ya kimataifa na zaidi mafanikio ya Yanga yataitangaza zaidi nchi.  "Tunawashukuru wanachama wa Simba kwa kujitikeza kuja kuunga mkono timu yetu kwenye michuano ya kimataifa na sisi tunaungana nao pia tunapenda kuwaomba radhi Wanachama wa Simba na uongozi kwa ujumla kwa kitendo cha wanachama wetu miaka ya nyuma kwa kuwashangilia TP Mazembe na kitendo hicho hakitajirudia tena,"amesema Muro.

  Amewaomba wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi na wakivaa jezi zao pamoja na timu zingine kuja kuisapoti Yanga na amemshukuru aliyekuwa Rais Wa Simba Ismail Aden Rage kwa hatua aliyoionesha kwa kuisapoti katika kipindi chote.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Na Estom Sanga-TASAF.
  WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa Menejimenti ya taasisi hiyo kukutana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

  Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za kupambana na Umaskini nchini..

  Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na kuongeza uchumi wao.

  Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umeanza kusisimua hamasa ya walengwa wa Mpango huo kuboresha maisha yao kwa kiwango cha kuanza kuboresha makazi yao kwa kujinunulia mabati na kuezeka nyumba,kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi nahata nguruwe.

  Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga amesisitiza watumishi wa Mfuko huo kuendeleza jitihada za kuwahudumia wananchi na hususani walengwa wa Mpango kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama zinavyoelekeza.

  Zifuatazo ni picha za watumishi wa TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa mikutanowa taasisi hiyo maarufu kama “Mlimani City conference hall” ulioko makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
   Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kilele cha wiki ya Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga, ( hayupo pichani) kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti) akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi (hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mobisol Tanzania Henrik Axelsson (Kushoto) akionyesha vifaa mbalimbali vinavyozalishwa na kampuni hiyo wakati wa ufunguzi wa huduma zake wilayani Bagamoyo hivi karibuni. 

  Imefanikiwa kufikisha huduma wa wateja robo milioni kanda Afrika Mashariki Kampuni kutoka nchini Ujerumani inayotoa huduma ya kusambaza umeme wa jua na kuuza vifaa vyake imeweza kubadilisha maisha ya familia robo milioni maeneo ya vijijini kuwa na maisha ya kisasa kutokana na kufikiwa nishati ya umeme katika nchi za Rwanda,Tanzania na Kenya. 

   Mobisol,kampuni ya Kijerumani inaoongoza kwa kutoa huduma za umeme wa jua imeweza kufunga umeme wa nishati ya jua kwa familia 50,000 ikiwemo sehemu za biashara katika maeneo wanayoishi wananchi wenye vipato vya chini ambao hawajafikiwa umeme wa gridi ya taifa kwenye nchi za Tanzania,Rwanda na Kenya. Kupitia mpango wake maalumu wa kukopesha unaowawezesha wateja kufanya malipo kwa awamu kupitia simu za mkononi yanaochukua kipindi mpaka kufikia hadi miaka mitatu, wananchi wengi wenye vipato vya chini wameweza kujiunga na kuufurahia mpango huu.Mteja anatakiwa kulipia shilingi 999 kwa siku ambapo akikamilisha malipo atapata umeme wa uhakika wenye nguvu zinazoanzia 80W hadi kufikia 200W kulingana na mahitaji yake kwa matumizi ya vifaa vya nyumbani. 

   Meneja Masoko wa Mobisol Tanzania,Allan Rwechungura amesema jijini Dar es Salaam kuwa mbali na wateja kuunganishiwa umeme wa jua kwa mpango unaoleta unafuu mkubwa pia wanaweza kujipatia vifaa bora vya matumizi kama vile mashine za kukata nywele,vifaa vya muziki (Music system),pasi,feni na vifaa vinavyoweza kuwaongezea wateja vipato mfano chaji maalumu ya kuchajisha simu kibiashara.

   “Mobisol ni mkombozi wa kuondoa tatizo la umeme kwa wateja wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kufungiwa umeme wa jua kwa mara moja kwa gharama zinazofikia Dola za Kimarekani 800 ila imewawekea mpango maalumu unaowawezesha kulipia huduma hii kwa awamu.

  Dhamira yetu ni kuona huduma hii inaleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya wananchi na sio kuwasha taa tu ama kuchaji simu”Alisema. Aliongeza kuwa kampuni inatoa ofa ya kufuatilia iwapo wateja wake wanapata huduma ya uhakika kwa kipindi cha miaka mitatu na iwapo kunakuwepo na matatizo yanarekebishwa na wataalamu wake waliobobea katika ufundi wa mitambo inayozalisha umeme wa jua,dhamira kubwa ikiwa ni kubadilisha maisha ya wakazi wa maeneo ambayo hayajafikiwa umeme wa gridi ya taifa hususani maeneo ya vijijini kuwa bora. 

   Rwechungura alisema moja ya malengo ya kampuni pia ni kuwawezesha watoto wanaosoma shule maeneo ya vijini kuweza kujisomea kwa kutumia mwanga wa umeme,kuweza kusikiza redio , kuangalia televisheni na kuperuzi kwenye internet ili wapate taarifa na fursa ya kuelimika “Uwekezaji wetu kwenye sekta hii vilevile umejikita katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kuwaongezea vipato kupitia uzalishaji unaofanyika kwa kutumia nishati ya umeme”. 

   Wakati huohuo Rwechungura ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza kampuni ya Mobisol itashiriki katika Maonyesho ya kimataifa ya Biashara maarufu kama SabaSaba yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.Maonyesho hayo ya biashara yatawawezesha wananchi kujua huduma zinazotolewa na kampuni ya Mobisol nchini ikiwemo kununua bidhaa za kampuni hususani Televisheni bora zenye ukubwa tofauti ambazo zimekuwa zikiwavutia wateja wengi. “Televisheni ni kifaa pekee kinachowawezesha kupatikana taarifa , burudani na kinachounganisha jamii,wakazi wa vijijini kupitia televisheni wanaweza kuunganishwa na dunia nzima,wanahitaji kuishi maisha ya kisasa na sisi tupo kwa ajili ya kubadilisha maisha ao kuwa bora”.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KIKOSI cha Yanga kipo tayari kuwavaa TP Mazembe kesho katika mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho Afrika ambapo unatarajiwa kupigwa katika dimba la uwanja wa Taifa huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kimchezo na kisaikolojia. Hayo yamesemwa leo katika mkutano na waandishi wa habari kuwa Wachezaji wapo tayari kwa ajili ua ushindi.

  Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa, kwa sasa kilichobakia ni kuweza kusubiri muda ufike na kwa maelezo ya kocha mkuu Hans Van De Pluijm amehakikishia wanachama wa Yanga kuwa watapambana hadi hatua ya mwisho." Kocha mkuu amesema kuwa wachezaji wote wapo sawa na watapambana hadi hatua ya mwisho na wamewahakikishia benchi la ufundi kuwa wapo uwanja wa nyumbani na watautumia vizuri,".
  Muro amesema kuwa, msimamizi wa mechi hiyo amewataka viongozi wa Yanga kuhusiana na mechi ya kesho katika 
  uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwa  una uwezo wa kuchukua watu 60,000, lakini kesho utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya mashabiki 40,000 kuingia.

  Hayo ni maagizo ya Kamisa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.

  Sasa Mabingwa hao wa Tanzania Bara watashuka kuja kupigana kuonyesha hawapotez mchezo wa nyumbani hata mmoja hasa baada ya ule wa awali kupoteza nchini Algeria.

  0 0

   Mkurungezi Mtendaji wa benki  ya PBZ, Juma Ameir Hafidh,akizungumza na wafanyakazi na Familia zao wakati futari  iliyoandaliwa na benki  ya PBZ katika Hoteli Hyaat Regency jijini  Dar es Salaam.
   Mwanafamilia wa Benki hiyo, Abdul Juma akisoma dua baada ya kufuru katika futali futari iliyoandaliwa na benki katika Hoteli Hyaat Regency jijini  Dar es Salaam.
    Sehemu ya wafanyakazi na familia zao `pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika wakati wa kuchukua futari iliyoandaliwa na benki  ya PBZ katika Hoteli Hyaat Regency jijini  Dar es Salaam.

  BENKI ya PBZ inatarajia kuanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali ifikapo Septemba mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyowakutanisha wafanyakazi wa PBZ na familia zao, Mkurungezi Mtendaji wa benki hiyo, Juma Ameir Hafidh, alisema kwamba kazi ni ibada hivyo kila mmoja.
  Aliwataka wafanyakazi hao kuheshimu fedha pamoja na kutolewa madaraka ikiwemo kumuogopa Mungu ili wasiwe na tamaa na wakaiba.

  Akizungumzia PBZ Mkurugenzi huyo alisema kwamba, kuanzia Julai mosi mwaka huu wataanza mchakato wa kuhakikisha Septemba wanatoa mikopo ya vitu kwa wajasiriamali ili kuwasaidia kukua kiuchumi.

  PBZ pia imewataka wafanyakazi wake kuongeza juhudi, nidhamu, upendo na ari katika kazi kwani ndiyo siri ya mafanikio.

  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akizungumza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam .
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa ufungwaji wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam .
   Baadhi ya washiriki wa wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha Muhas pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam mwishoni 

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imesisitiza utafiti wa kisayansi kwa maendeleo ya taifa na kuhamasisha ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi katika eneo hilo , ili kujenga taifa lenye vijana watafiti na wataalam wa kutosha.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  John Michael aliemuwakilisha kwenye ufungaji wa  Mkutano wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Alisema utafiti wa kisayansi ni muhimu kwa nchi yeyote ikiwemo  Tanzania katika  kuhakikisha inafikia  malengo yake ya maendeleo  ya utekelezaji wa wa malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGS).

  Aliongeza kuwa utafiti wa kisayansi ni kiungo muhimu katika kuweza kufikia malengo ya SDGS  kwa kuwa ndio unatoa muongozo wa kisayansi na mipango ya namna ya kuyafikia malengo hayo.

  Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Ephata Kaaya alisema ni muhimu taifa kuanza kuchukua hatua sasa na kuhakikisha mfumo wa kitaifa wa huduma za afya na uchumi  kwa ujumla  unaweza kukabiliana na mizigo wa magonjwa , kwa njia ya utafiti.

  Aidha Prof Kaaya aliwapongeza wanafunzi wa shahada ya uzamili na wahitimu wa MUHAS  waliowasilisha mada takribani  ya 70 kati ya 170  katika mkutano huo na tofauti  na mwaka uliopita ambapo asilimia 30 ya mada ziliwasilishwa na wanafunzi.

older | 1 | .... | 1268 | 1269 | (Page 1270) | 1271 | 1272 | .... | 3270 | newer