Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

SH. BILIONI 876.3 KUTATUA MSONGAMANO MAGARI DSM

0
0
MHE. GERSON LWENGE


NA IMMACULATE MAKILIKA-MAELEZO
SERIKALI imesema   inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336   katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.

Hayo  yalisemwa leo Bungeni na  Naibu Waziri wa Ujenzi   Gerson  Lwenge,  wakati    akijibu swali  Mbunge  wa Jimbo la  Temeke  Abasi Zuberi Mtemvu  lililouliza kuwa  Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?

Alisema   kuwa  inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni  kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh.  bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).

Nyingine ni  Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh.  bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh.  bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa  msaada wa fedha kwa  ajili ya ujenzi.

Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya  Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).

Waziri  huyo  alisema  ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.

Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu  (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive  kuunganisha na Ocean Road.

Article 17

Prof. Mwandosya azindua kitabu cha Marekebisho na Udhibiti wa Sekta ya Umeme Afrika

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiekuwa na Wizara Maalum,Profesa Mark Mwandosya (katikati) akizindua kitabu kinachokuhusu Marekebisho na Udhibiti wa Sekta ya Umeme barani Afrika kilichoandikwa na ndugu Joseph Kapika na Profesa Anton Eberhard wa Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini. Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano wa Mamlaka za Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Afrika uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni.
Waandishi wa kitabu hicho wakiweka saini zao mara baada ya kuzinduliwa rasmi.

Balozi wa Norway Nchini Bi. Ingunn Klepsvik atembelea Chuo cha Ufundi Arusha

0
0
 Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea maelezo mafupi kuhusu Maabara ya Upimaji Udogo
 Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea zawadi ya bangili
 Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Masika(kulia) akitoa maelezo mafupi kuhusu chuo cha Ufundi Arusha kwa balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik mara tu alipowasili Chuoni hapo.
 Mkuu wa Idara ya Mitambo Chuo cha Ufundi Arusha, Eng. Jafari mwanza akitoa maelezo mafupi kuhusu aina mbalimbali za mitambo ya kufua umeme inayotengezwa chuo hapo kwa Balozi wa Norway Chin Bi. Ingunn Klepsvik.
Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea maelezo mafupi kuhusu karakana ya useremala

Wasanii wa kizazi kipya wang'arisha tamasha la Airtel yatosha Mbagala

0
0
  Wasanii wa kundi la Wanaume Halisi wenye makazi yao Jijini Dar es salaam Temeke wakiongozwa na Juma Nature wakipanda jukwaani kwa ajili  kutoa burudani mfululizo wakati wa mrindomo wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
 Msanii wa kikundi cha tip top connection Madii akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vy zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii
 Wasanii wa kundi la Wanaume Halisi wenye makazi yao Jijini Dar es salaam Temeke wakitoa Burudani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
 Msanii mahiri wa Hi Hop nchini maarufu kama FID Q akikamua katika jukwaa maalum la kuitambulisha huduma kabambe ya Airtel Yatosha katika viwanja vya Zakhem jiini Dar es Salaam na kufanikisha kuwaunganisha watanzania na wakazi wa jijini Dar es salaam kwenye huduma ya Airtel Yatosha.

 Kikundi cha wakali dansi cha temeke kikitoa burdani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
Mwanadada msanii chipukizi wa temeke akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vya zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.

CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU

0
0
Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;

1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.

2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.

Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:

Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

MH. PINDA AWAFARIJI WALIOJERUHIWA KWENYE TUKIO LA BOMU JIJINI ARUSHA

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya majeruhi wa bomu la kutupwa kwa mkono lililolipuka katika kanisa Katoliki la Olasiti Arusha wakati alipowatembelea kwenye hospitali ya mkoa wa wa Arusha, Mount Meru, May 8,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wazee wa Feva mmemuona huyu jamaa??

0
0
 Kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa mtu huyu ambaye ni omba omba akiwa amekaa katikati ya barabara ya Bagamoyo karibu kabisa na eneo la Victoria jijini Dar es Salaam, akiomba kwa watu wanaopita na magari katika barabara hiyo. Jambo hili si salama sana kwa mtu huyu kwani lolote linaweza tokea japo hatuombei itokee,hivyo ombi kwa wazee wa feva (wanausalama barabarani) kusaidia kumuondoa huyu mtu mahala hapa haraka iwezekanavyo.


bei ya madafu leo

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI KUFANYIKA MKOANI RUKWA

0
0

Na: Eliphace Marwa – Maelezo

CHAMA cha wauguzi Tanzania kinatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya waaguzi duniani mei 12 ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Rukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Rais wa chama hicho bwana Paulo Magesa alisema maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 12 mei ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Kuziba pengo kufikia Malengo ya Milenia namba 6,5,4”.

Bwana Magesa alisema malengo hayo ya millennia yanalenga kuzuia vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua , kuzuia vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

“Pamoja na changamoto nyingi tunazokutana nazo wauguzi bado tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuhakikisha huduma bora zinawafikia walengwa na hii imeleta mafanikio makubwa kwani vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto vimepungua sana”, alisema bwana Magesa.

Wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini chini ya mpango huu umelenga kuhamasisha akina mama kutumia njia salama za uzazi wa mpango na kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za mama na mtoto.

Aidha, kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho kuanzia tarehe 10 hadi 12 mei yakionesha shughuli mbalimbali za kitaaluma wanazozifanya wauguzi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kiafya kama huduma ya mama na mtoto, huduma za kupima VVU na ushauri nasaha na huduma nyingine nyingi.

Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) ni chama kinachowawakilisha wauguzi na wakunga wote Tanzania bara na Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.

Wateja wa benki waanza kuelimishwa kunufaika na huduma ya M-pesa benki popote

0
0
Mteja wa wa Benki ya Amana Suleiman Mahmud akielezea namna anavyoifahamu huduma ya kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti ya Benki hiyo kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi la kuelimisha wateja kuhusu huduma ya M-pesa benki popote iliyofanyika katika Tawi la Kariakoo jijini Dar es salaam. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanznaia Salum Mwalim (wa kwanza kulia), Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma (wa Kwanza kushoto) na kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo.
Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akielezea kwa waandishi wa habari huduma ya M-pesa benki popote inayowaunganisha wateja wa Benki ya Amana na nyengine mbalimbali nchini kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi la kuwaelemisha wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo. Vodacom imeanza kampeni ya kuelimisha wateja wake na wa benki mbalimbali zilizoaunganishwa na mfumo wa M-pesa benki popote.
Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifafanua jambo kwa mteja wa Benki ya Amana Tawi la Kariakoo Suleiman Mahmud kuhusu huduma ya M-pesa Benki popote inayowapa uwezo wateja wa Amana kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kwa njia ya M-pesa. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma na Kaimu Meneja Tawi la Kariakoo Khamis Gumbo. Vodacom imeanza kamapni ya kuwaelimisha wateja namna ya kunufaika na huduma ya M-pesa benki popote inayopatikana kwenye benki mbalimbali za biashara hapa nchini.

MATUKIO YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI BUNGENI DODOMA LEO

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa Pili kutoka kushoto Mbarak Abdulwakil akielekea kwenye lango la kuingia kwenye Ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachotarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma watatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mwamini Malemi akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw. John Minja.
Sehemu ya watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pichani wakisikiliza kwa makini hotuba ya bajeti ya wizara yao wakati hotuba hiyo ikisomwa bungeni leo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa kwanza kutoka kulia.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw. John Minja wa kwanza kutoka kushoto akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, watatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa kwanza kulia wakiwa pamoja na watendaji wakuu wengine wa wizara hiyo, wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Wabunge wakati wa kikao cha Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayotarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi na Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya bajeti ya wizara yao ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayoendelea kusomwa katika Kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma leo, Bajeti ya Wizara hiyo inatarajiwa kukamilika leo.
Baadhi ya Wakurugenzi wasaidizi , Makaimu Kamanda na Maafisa wa Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiandaa majibu kwa ajili ya kujibu hoja za Wabunge katika kikao cha Mawasilisho ya hotuba ya Bajeti ya wizara hiyo kinachotarajiwa kukamilika leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Bajeti wa Idara ya Uhamiaji wakiandaa majibu kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali zinazotolewa na Waheshimiwa Wabunge katika kikao cha Bunge la Bajeti kinachojadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoanza kusikilizwa jana mjini Dodoma.

MAALIMU SEIF ATAKA WATANZANIA WASIGAWANYIKE KWA TUKIO LA BOMU ARUSHA

0
0
Mahmoud Ahmad,Arusha

Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar(SMZ),Seif Sharif Hamad ametamka ya kwamba tukio la shambulio la bomu lililorushwa katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi na kuua watu watano huku 60 wakijeruhiwa lisitumike kama kigezo cha kuwagawa watanzania kwa misingi yao waliyojiwekea.

Makamu huyo wa kwanza alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea eneo la tukio hilo sanjari na kupata fursa ya kutoa mkono wa pole kwa majeruhi mbalimbali waliolazwa katika hospitali ya mkoa ya Mt Meru.

Alisema kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ila lisitumike kama njia ya kuwagawa watu kwa misingi yao ya dini na kabila.

Alisema kuwa kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa kwa namna yoyote.

“Kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa”alisema Hamad

Hatahivyo,alitoa wito kwa watu wenye taarifa mbalimbali kushirikiana na vyombo vya ulinzi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa watuhumiwa.

Aliwataka wafuasi wa dini mbalimbali sanjari na wanasiasa nchini kutotumia mwanya wa tukio hilo kuleta mgawanyiko ndani ya jamii.

Katika hatuia nyingine meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo alisema kuwa tukio hilo litaathiri sekta ya utalii kwa ujumla na uchumi wa mkoa wa Arusha sanjari na wa taifa kw aujumla.

Lyimo,alitoa kauli hiyo wakati uongozi wa jiji la Arusha wakiwemo madiwani wa vyama tofauti mara walipotembelea hospitali ya St Elizabeth kukabidhi misaada ya mablanketi pamoja na fedha ambazo hakuwa tayari kutaja ni kiasi gani.

MHE. UMMY MWALIMU AZINDUA MRADI WA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI NA KIJAMII UNAOFADHILIWA NA EUROPEAN UNION

0
0
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Mhe.Ummy (katikati ) akielezea namna Wizara inavyowasaidia wanawake kujiinua Kiuchumi na Kijamii,wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi na Kijamii,Mradi unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la CONCERN Tanzania katika Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kasulu,Kigoma na Masasi. Mradi huo Unafadhiliwa na European Union, Umezinduliwa leo jijini Dra es Salaam Kushoto kwake ni .Balozi wa EU nchini Mhe.Filberto Cerian Sebregondi.
Sehemu ya Wageni waliohudhuria Uzinduzi huo.
Balozi wa EU nchini Mhe. Filberto Cerian Sebregondi (katikati) akiteta jambo na Mhe.Ummy Mwalimu Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii(kushoto) na MKurugenzi wa Shirika la CONCERN _Tanzania Bw. James Davey.

taarifa toka shirikisho la tanzania (TFF) leo


msaada tutani: natakiwa nirudi bongo kwa interview ya visa, je nitawini???

0
0

Kwanza shikamoo mzee wa libeneke na wadau wote walionizidi umri.
Mie ni mdau mkubwa wa blog hii inayosomwa kwa wingi duniani leo nineona nami niombee msaada wa mawazo km wasomaji wengine wanaotoa matatizo yao na kupata msaada wa mawazo.
Mie ni kijana mwenye umri wa miaka 30 naishi norway kwa sasa ila ki ukweli kwa miaka 7niliyoishi hapa sijafanikiwa kupata makaratasi kifupo niko illegal nilijiripua km vijana wengi tufanyavyo na majibu ni negative. Sasa bahati ya Mungu nimecheza bahati nasibu ya green card ni nimefanikiwa kuwa mmoja wa waliochaguliwa, natakiwa kujaza form na kufanya interview ambayo itafanyika Dar, Mungu akipenda, mimi kwa kweli mpango wangu nilikuwa sirudi bongo mpaka kieleweke huko as nimeshapoteza muda mwingi, je wadau najua kuna waliowin green card, how sure it is to get a visa?.
Naweza kweli kupata visa au naweza rudi nikaganda? Mnanishauri nirudi?
Naomba msiwe wakali sana maisha magumu ndo yamenifikisha hapa.
Asante ankal, email kapuni please.
Davis

JK AOMBEA AMANI NA MAASKOFU, ATEMBELEA WAFIWA NA MAJERUHI WA BOMU ARUSHA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wanajiunga na maaskofu wa makanisa mbalimbali katika kuombea amani Tanzania alipokwenda nyumbani kwa Askofu Mkuu wa Katoliki Jimbo la Arusha Archbishop Josephat Lebulu (mwenye kanzu nyeupe) kabla ya kwenda kuhani misiba ya watu watatu waliofariki katika mlipuko wa bomu jijini humo Jumapili iliyopita. Pia alitembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Mtakatifu Elizabeth na ya Mount Meru ambako aliwapa pole majeruhi 31 kati ya 64 waliolazwa hadi sasa. 
Habari kamili na picha zaidi baadaye

CHUO CHA DIPLOAMSIA KUIMARISHA IDARA YA LUGHA ZA KIGENI CHUONI HAPO

0
0
Mshindi wa lugha ya kifaransa Eric Ngilangwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ushindi wake huo unaompa fursa ya kwenda nchini ufaransa kujifunza zaidi lugha hiyo, eric amepata fursa hiyo mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la uandishi wa insha kwa lugha ya kifaransa ,shindano liloandaliwa na ubalozi wa ufaransa nchini. kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia,Bw. Ismail Shah.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dr. Bernard Achiula akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) kuhusiana na juhudi mbalimbali ambazo chuo cha Diplomasia zinachukua katika kufundisha lugha za kigeni,katika hafla fupi ya kumpongeza mwanafunzi Eric kwa kufanya vizuri katika shindano ya uandishi wa insha ya kifaransa na kuibuka mshindi.Kulia kwake ni Mjumbe wa Bodi ya Chuo,Bw. Abdulrahman Abdallah.
Mshindi wa lugha ya kifaransa kutoka chuo cha Diplomasia bw Eric Ngilangwa(wa tano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi, eric pia anachukua shahada ya post graduate katika chuo cha diplomasia.chuo cha diplomasia licha ya kutoa wataala wa utatuzi wa migogoro pia kinatoa kozi mbalimbali za lugha za kigen kama kifaransa, kireno, kiarabu,kihispania na hivi karibuni kichina kinaingia chuoni hapo.

MKUU WA MKOA WA MBEYA APOKEA TUZO ZA SAFARI LAGER KWA SHANGWE

0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akimkabidhi rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulia) Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya Safari Lager ambapo jana walikuwa Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akizungumza na wananchi wa Mji wa Mbeya wakati upokeaji Tuzo za Bia ya Safari Lager mkoani kwake jana ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilikuwa Mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. 

MIKOA YATAKIWA KUCHEZESHA COPA COCA-COLA WILAYANI

0
0

Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.

Hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.

Vifaa na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania.

Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images