Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1267 | 1268 | (Page 1269) | 1270 | 1271 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
    Baadhi ya Wasomi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
   Sehemu ya walohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.


  0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano  na Uchukuzi, Edwin Ngonyani (kushoto)na Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Profesa  Faustine Kamuzora (kulia)  baada ya mazungumzo kati ya wizara hiyo na Viongozi wa  kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Sunil Colaso ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji  (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel  Bi. Beartice Singano.  
  (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP mzee John Momose Cheyo mara baada ya kumaliza kuzungumza na wageni mbalimbali katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Serikali,Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Tume ya Uchaguzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ikulu jijini Dar es Salaam.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Prof. Iddi S.N. Mkilaha (pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa tarehe 24 Juni, 2014 Nyumbani kwake eneo la Boko, Dar es Salaam.
   Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani 
  kwa Marehemu, Boko, Dar es Salaam.
   Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Prof. Mkilaha katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.

   Mkurugenzi Mkuu
  SUMATRA
  25 Juni, 2016

  0 0

  OFISI YA RAIS -TAMISEMI - inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. 


  Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.


  Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

  Imetolewa na Katibu Mkuu,
  OR-TAMISEMI


  0 0

  http://www.sporah.com/

  0 0


  SIMU.TV: Wakala wa barabara mkoa wa Mtwara TANROADS wamefanya zoezi la kuelimisha watembea kwa miguu sambamba na upandaji wa miti ili kutunza mazingira;https://youtu.be/OH8JWCrBSXI

  SIMU.TV: Katika majiji yote matano nchini, Jiji la Mbeya ndio jiji linaloongoza kwa uchafu huku wananchi wakiitupia lawama serikali kwa kushindwa kufanikisha zoezi hilo;https://youtu.be/JJ5-Bgg3yug

  SIMU.TV: Wakazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wamefanya usafi katika eneo la makaburi Msafa ili kuondoa vichaka ambavyo vilikuwa vinatumika kama maficho ya vibaka na wakabaji; https://youtu.be/rP01xfrfU18

  SIMU.TV: Waumini wa kanisa la Mito ya Baraka kata ya Jangwani jana waliungana na waumini wengine Jijini Dar es salaam katika kufanya usafi ili kuunga mkono agizo la mkuu wa mkoa Paul Makonda; https://youtu.be/xfPE6Zam948

  SIMU.TV: Mkurugenzi na mmiliki wa Gazeti la Dira Alex Msama amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kumuomba radhi waziri wa sheria na katiba Dr Harrison Mwakyembe baada ya kuchapisha habari inayomuhusu waziri huyo;https://youtu.be/Zy_ZjInDbUM

  SIMU.TV: Wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Maswa mkoani Simiyu wameshukuru mradi wa TASAF kwa kuwawezesha kusoma vizuri tofauti na hapo awali;https://youtu.be/Lh68PWda-cA

  SIMU.TV: Joto la mchezo kati ya timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys dhidi ya Shelisheli lazidi kupanda huku mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa hii leo;https://youtu.be/EyJ2DA3Fa7E

  SIMU.TV: Zaidi ya wachezaji 100 wamejitokeza hapo jana kushiriki mchezo wa Golf katika viwanja vya Golf vya Makongo; https://youtu.be/H8-Rq5EguqQ

  SIMU.TV: Shirika la nyumba ya Taifa NHC limeanza kubomoa nyumba zake 9 mkoani Morogoro baada ya kushinda kesi yake ya msingi na wakazi wa eneo hilo;https://youtu.be/3NRvECEzwls  

  SIMU.TV: Katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe amezitaka taasisi na halmashauri zitakazopokea fedha za uwezeshaji vijijini kuzitumia fedha hizo ili kuleta maendeleo; https://youtu.be/aYllL6IHji4

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amezitaka halmashauri zote mkoani humo kusitisha malipo kwa wakandarasi wote wa miradi ya maji; https://youtu.be/Ejg-Dr55EEQ

  SIMU.TV: Watanzania wameaswa kutii maagizo ya viongozi wao hususani agizo la Rais Magufuli la kutaka kufanyika usafi kwa mazingira yetu; https://youtu.be/ERLNQiU9rZ4

  SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu la kudumisha amani ni la kila mmoja wetu na kuwataka watanzania kudumisha amani kwa kuepuka vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani; https://youtu.be/m_qM1ip4oBk

  SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga imerejea nchini baada ya kuweka kambi takribani wiki mbili nchini Uturuki tayari kwa mchezo wao dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumanne;https://youtu.be/lkzIwOg-rGo

  SIMU.TV: Usaili kwa vijana wenye vipaji watakaoweza kushiriki katika shindano la Klabu Raha Leo Show linarushwa na TBC 1 & Taifa linazidi kushika kasi katika katika fukwe za Coco Beach; https://youtu.be/THbN1svgqlU

  0 0

  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeshauriwa kufanya semina elekezi kwa wananchi na viongozi wa kisiasa ili kuelimisha kuhusu dhana ya uwezeshaji. 
  Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji kutoka wilaya ya Liwale Bw. Moses Mkoveke wakati wa mafunzo ya uwezeshaji yaliyofanyika mkoani Lindi hivi karibuni.
   
  “Elimu hii ikiwafikia viongozi wa kisiasa katika ngazi ya mkoa, halmashauri, mabaraza ya kata na hata vijiji itasaidia katika kuwajengea wananchi uelewa wa dhana ya uwezeshaji,” alisema Bw. Mkoveke. 
  Alisema hali hii italeta uelewa wa pamoja na hivyo kufanya sera ya uwezeshaji wananchi kutekelezeka kwa urahisi na ufanisi zaidi. 
  Aliongeza kusema kuwa elimu hiyo pia itasaidia kujenga uelewa kwa wananchi juu ya utaratibu wa upatikanaji na urejeshaji wa Tshs milioni 50 kwa kila kijiji kama ilivyoahidiwa na Rais John Magufuli. 
  Mratibu wa dawati hilo kutoka Wilaya ya Lindi, Bi.Yolenda Makumbuli alisema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa namna ya kuunganisha wananchi katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kuibua fursa za biashara na kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
   
  “Changamoto iliyopo ni kubadili mitazamo ya wananchi ili wawe wabunifu katika maeneo yao ili kujiletea maendeleo kiuchumi,” alisema Bi.Makumbuli. 
  Aliongezea kuwa ili kufikisha elimu ya uwezeshaji kwa wananchi, ushirikiano unahitajika toka kwa wadau wote wa maendeleo. 
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uwezeshaji (NEEC) Bi. Anna Dominick alisema mafunzo yalikwenda vizuri na mwitikio kwa waratibu ulikuwa mkubwa na kuwa matarajio ya baraza hilo ni kwamba watakwenda kutekeleza waliyowafundishwa katika maeneo yao.
   
  “Tunapata faraja kuona utayari waliokuwa nao waratibu wa kufanya kazi,” alisema Bi. Anna.
   
  Alisema changamoto kubwa iliyopo katika mikoa ya kanda ya kusini ya Lindi na Mtwara ni mapato na wingi wa kata katika halmashauri, hali inayoweza kupelekea waratibu kutofanya kazi zao kwa ufanisi na ripoti kutofika kwa wakati. 
  Akizungumzia swala la ahadi ya Tshs Milioni 50 kwa kila kijiji alisema baraza litaendelea kutoa semina kuhusu fedha hizo na utaratibu utakaotumika katika kuwafikia wananchi.
   
  Alisistiza kuwa fedha hizo sio zawadi bali ni mkopo ambao utatolewa katika kijiji kwa awamu ili ziweze kuwafikia wananchi wote katika kufanikisha shughuli za kiuchumi ili kupiga hatua kimaendeleo. 
  Mafunzo kwa waratibu wa madawati ya uwezeshaji yameshafanyika katika kanda ya nyanda za juu kusini katika mikoa sita ya Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, Iringa na Njombe. 
  Wiki iliyopita yamemalizika katika kanda ya kusini mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la kutoa mwongozo wa utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
   Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Anna Dominick akitoa mada wakati wa mafunzo ya siku tano kwa waratibu wa madawati ya uwezeshaji yaliyofanyika katika kanda ya kusini mkoani Lindi na kuhusisha mkoa wa Mtwara na kumalizika mwishoni mwa wiki.
  Waratibu wa Madawati ya Uwezeshaji wakiwa kwenye majadiliano wakati wa mafunzo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyofanyika mkoani Lindi na kushirikisha mkoa wa Mtwara kwa kanda ya kusini.  Mafunzo hayo yaliratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).

  0 0

   Mkurugenzi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), Bw. Said Kambi (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano uliojadili nafasi ya mwanamke katika uongozi hasa bodi za wakurugenzi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  kulia ni washiriki wa mkutano huo uliotayarishwa na Jumuiya ya Madola kwa kushirikiana na serikali na IoDT.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), Bw. Said Kambi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano uliojadili nafasi ya mwanamke katika uongozi hasa bodi za wakurugenzi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Wa pili kulia ni Spika Mstaafu Mama Anne Makinda; Mwezeshaji kutoka Malaysia, Bi. Anne Abraham (kushoto) na Mshauri wa masuala ya Jinsia na Maendeleo ya Uchumi, Sarah Kitakule (wa pili kushoto).
  Spika Mstaafu Mama Anne  Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano uliojadili nafasi ya mwanamke katika uongozi hasa bodi za wakurugenzi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), Bw. Said Kambi; Mwezeshaji kutoka Malaysia, Bi. Anne Abraham na Mshauri wa masuala ya Jinsia na Maendeleo ya Uchumi (wa pili kushoto).

  0 0

  Mhe.January Makamba(MB),Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira ) ameitumia Siku ya Tarehe 25 /6/2016 kushiriki katika mahafali ya 24 ya chuo cha biblia Vuga  (VUGA BIBLE )kilichopo katika halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga.  Vilevile Mhe.January Makamba alipata fursa ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayofanywa na chuo hicho,Pia  aliupongeza uongozi wa chuo kwa kutoa elimu mbali mbali kwa wananchi waishio karibu na chuo na bumbuli kwa ujumla.

   Mhe.January Makamba akiwasili chuoni hapo huku akisalimiana na wenyeji  
   Mh Makamba akijifunza namna ya utengenezaji wa Mizinga ya nyuki kwa kutumia udongowa mfanyanzi,mizinga hiyo inauwezo wa kudumu miaka 80-100.
  Mh Makamba akielekezwa jambo huku akijifunza historia ya chuo hicho kwa njia ya picha.
   Akitazama baadhi ya kazi za mikono za kikundi cha wakina mama wa Upendo,kikundi hicho kimepata mafunzo chuoni hapo.
   Mh Makamba akifuruhia jambo kwa pamoja na Wana kikundi hao. 
  Picha zote na Imani Selemani Nsamila  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

  Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

  “Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.Waziri Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.

  Hatua hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.

  Aidha, watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.

  Akizungumzia utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.Dkt Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.

  Katika kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.Wakala hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.


  Baraza la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.
  k1 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k2Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari  akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairukik3Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
  k4 k6 
    Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k7 
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

  0 0

  Kupitia mchezo wa sakasaka unaochezeshwa na kituo cha redio cha EFM leo tarehe 26/06/2016 imewafikia wakazi wa Temeke ambapo wakazi kumi wa wilaya hiyo waliweza kusaka vitu vilifichwa katika eneo la Temeke Mwisho na kila kitu kina thamani ya pesa. Mshindi wa kwanza amejishindia kiasi cha shilingi milioni 2 viwango vingine vya pesa vilivyotolewa kwa washindi ni kuanzia elfu hamsini,laki moja mpaka laki mbili.
   Mmoja wa washindi akishuhudia kiasi alichoshinda, Kutoka kushoto ni Meneja wa matukio na mawasiliano Neema godlays Mukurasi akiwa na Chogo mmoja wa watangazaji wa kituo cha EFM redio.
   Meneja wa matukio na mawasiliano Neema godlays Mukurasi akimkabidhi mshindi Flora Kafunga pesa taslimu kiasi cha shilling Laki moja.
   Mshindi wa kwanza Bi.Doris Joseph aliejipatia kiasi cha shilingi milioni mbili akiwa katika pozi la picha.
  Baadhi ya watu wakishuhudia jinsi washindi wanavyopatikana katika eneo hilo

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo,kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo,Abdallah Zuberi,kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni
  Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akihojiwa na wanahabari

   Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mgutto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo
  Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union, Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao hicho.
  Picha kwa hisani ya kitengo cha 
  Mawasiliano cha timu ya Coastal Union.  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi  wa Operesheni  za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika  kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo
   Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.(
   Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.(
   Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu  wa Mradi wa Uwekaji  Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni
  Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni

  0 0

  Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu waislaam wanaoendelea kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.

  Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka Congo DRC  TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani 'Kessy' na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo jumanne ya wiki hii.

  Klabu ya Simba kwa maksudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.

  Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji Hassan Ramadhani 'Kessy' pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa vilabu hivi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
  Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.

  Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima wachezaji watatu Yanga ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika wachezaji hao ni Shaban Ramadhani Monja Liseki na Alphonse Modest sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini?
  Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya Hassan Ramadhani 'kessy'
  Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili inategemea uungwana wao tu.

  Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.
  Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo.

  Haji Manara
  Msemaji wa Timu ya Simba
  26-6-2016

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akimsaidia kutoa pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/=Gilibert Lutwaze(katika)kwa njia ya huduma ya  M-Pesa, alizojishindia katika promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Mwingine katika picha ni mshindi wa promosheni hiyo, Pascal Mahoni(kulia)aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 5/= Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

   Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/=kupitia promosheni ya”Kamata Mpunga” inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Pascal Mahoni mkazi wa Mkuranga mkoa wa Pwani(kulia)akipokea kitita chake leo toka kwa Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kushoto) katika ni mshindi mwingine wa Milioni 1/= Mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam,Gilibert Lutwaze.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)na Kaimu Meneja wa duka la kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam,Said Ndomondo(kulia)wakiwashuhudia washindi wa promoshe ya”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na kampuni hiyo,wakihesabu pesa zawa mara baada ya kukabidhiwa leo,wapili kulia ni mshindi wa Milioni 5/=Pascal Mahoni ambaye ni mkazi wa Mkuranga mkoa wa Pwani, Mshindi wa Milioni 1/=Pamela Komba na Gilibert Lutwaze,wote ni wakazi wa jijini.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akimkbidhi kitita cha pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/=Gilibert Lutwaze alizojishindia katika promosheni ya ‘Kamata Mpunga’inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akimkabidhi mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, Gilibert Lutwaze(wapili kushoto)kitita cha shilingi Milioni 1/=alizojishindia kupitia promoshe ya”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na kampuni hiyo,wengine katika picha Mshindi wa Milioni 1/=Pamela Komba(katikati)na mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 5/= Pascal Mahoni.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
  Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.
  Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo vitendo vya uhalifu.

  Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
  Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA na wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.

  Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja,upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais.
  26-Jun-16

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
  Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
  Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim  jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
  Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha  za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 06/26/16--07:17: mchungaji mapumzikoni...
 •     

  0 0

   Mpira umeanza kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo Serengeti Boys wanaonekana kutawala mpira na katika dakika ya 15 Nickson Kibabage anaiandikia Serengeti goli la kwanza akitumia maridadi mguu wake kushoto na kutinga nyavuni.

  Dakika ya 22, Ibrahim Ally anaiandikia Stars goli la pili ikiwa ni shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.Mpira umeonekana kuchezwa upande mmoja na Serengeti kukosa nafasi nyingi za wazi.Mpira ni mapumziko na Serengeti wanatoka wakiwa mbele kwa goli 2.

  Kipindi cha pil kimeanza na timu zote kuwa makini ambapo dakika ya 60, Ally Msengi anaiandikia Serengeti goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Shelisheli kuushika ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru penati.
     
  Mchezo kati ya Serengeti Boys na Sechelles unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0. 
   Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakishangilia mara baada ya kupata goli. 
  Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Rashid Mohamed Chambo akimchomoka mchezaji wa timu ya Sechelles,katika mchezo wao unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza  bao 3-0.
   Wachezaaji wa timu ya Serengeti Boys wakionesha umahiri wao dhidi ya timu ya Sechelles
  Mchezaji wa timu ya  Sechelles akiwa amelelala chini katika nginja ngija ya kusaka magoli dhidi ya timu ya Serengeti Boys ,katika mchezo wao unaofanyika hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza bao 3-0. 

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaam 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa Juni 26, 2016. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya wageni  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaam.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na watoto wadogo kuliko wote walioshiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016.Watoto hao ni Abuzar Kholidi wa Tajikistan (Kulia) na Ahmad Abdullah Al-Azhar wa wa Bangladesh. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1267 | 1268 | (Page 1269) | 1270 | 1271 | .... | 3272 | newer