Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MWANZA:MWANAUME MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPINGWA NA KUNDI LA WATU.

$
0
0

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
 MWANAMUME MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPINGWA NA
KUNDI LA WATU WALIOAMUA KIJICHUKULIA SHERIA MKONONI
WILAYANI ILEMELA.

 WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA
KUKAMATWA NA POMBE AINA YA GONGO WILAYANI SENGEREMA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
MNAMO TAREHE 22.06.2016 MAJIRA YA SAA 2:00 USIKU KATIKA ENEO LA KABANGAJA KATA YA BUHONGWA WILAYA YA ILEMELE JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMUME AMBAYE JINA LAKE HALIKUFAHAMIKA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA 40 HADI 45 ANAYEDHANIWA KUWA NA TATIZO LA AKILI ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WENYE HASIRA KALI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUMPIGA NA MAWE PAMOJA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.

AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA NA TATIZO LA AKILI AMBALO LILIMPELEKEA KUWA NA TABIA YA KUBAKA WANAWAKE PAMOJA NA WATOTO WA MAENEO TAJWA HAPO JUU, NA KATIKA SIKU HIYO AMBAYO ALIUAWA MAREHEMU ALIONEKANA MAENEO YA
SHAMBANI AKIMNYEMELEA MWANAMKE MMOJA AMBAYE ALIKUWA AKICHIMBA VIAZI NA PINDI MWANAMKE HUYO ALIPOMWONA ALIPIGA YOWE AKITAKA ASAIDIWE, NDIPO WANANCHI WALIFIKA NA KUMPIGA MTU HUYO HADI KUMUUA. 

MWILI WA MAREHE UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA UTAMBUZI, HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI PAMOJA
NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUJIRIDHISHA KUHUSIANA NA KIFO CHA MTU HUYO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUACHA TABIA ZA MARA KWA MARA ZA KUJICHUKILIA SHERIA MKONONI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI, HIVYO ANAWAOMBA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU WATOE TAARIFA POLISI ILI AWEZE KUCHUKULIWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA PILI MNAMO TAREHE 22.06.2016 MAJIRA YA SAA 9:00 ALAHASIRI NA KUENDELEA KATIKA ENEO LA NYEHUNGE WILAYANI SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WALIFANYA DORIA
PAMOJA NA MISAKO NA KUFANIKIWA KUWAKATA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI. 

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NI 1. ESTER JEREMIAH MIAKA 36 MKAZI WA MAGULUKENDA AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO LITA 9, NA 2. SEVERINE SEBASTIANI MIAKA 20 NA YEYE PIA MKAZI WA MAGULUKENDA AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO LITA
20, KITENDO AMBACHO NI KINYEME NA SHERIA. INADAIWA KUWA WATUHUMIWA WAKIWA NI PAMOJA YA WAKAZI WA KIJIJI TAJWA HAPO
JUU HUFANYA BIASHARA YA KUWAUZIA BAADHI YA WANANCHI POMBE HIYO HARAMU AINA YA GONGO, NDIPO JESHI LA POLISI LILIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NA KUWEZA KUFANYA MSAKO KISHA KUFANIKIWA KUWATIA NGUVUNI WATUHUMIWA WOTE
WAWILI.
           
AIDHA WATUHUMIWA WOTE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUTENDA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE
AINA YA GONGO UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZE KUWAKAMTA WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA POMBE AINA YA GONGO.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Ubia wa TTCL na Bharti Airtel Wafikia Kikomo

$
0
0

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto waliokaa) akitiliana saini na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu) kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mauziano. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali walioshuhudia tukio hilo.

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ambapo sasa inakuwa ikiimiliki TTCL kwa asilimia 100. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mauziano hayo. Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali wa TTCL na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano walioshuhudia tukio hilo. 


Msama amwangukia Dkt Mwakyembe,amwomba radhi.

$
0
0

 
Bw . Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari huku akiwa ameshika gazeti la Dira,wakati alipomuomba Radhi Mh. Dk. Harisson Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba kutokana na Gazeti la Dira analomiliki kumuandika vibaya.

MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari. 

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo. Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe. 

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo. “Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama. 

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi. Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata. 

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama. Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe. 

Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 440 KWAAJILI YA KUSAIDIA KAYA MASIKINI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM 

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini hati ya makubaliano na Benki ya Dunia itayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya fedha katika mradi wa Tasaf kiasi cha Shilingi Bilioni 440.

Hati hiyo ilisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Dar es Salaam, leo, Juni 23, 2016.

Akiongea wakati wa kusaini hati hiyo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika mradi wa Tasaf II kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato chao kupitia ajira za muda zitakazowawezesha kupeleka watoto shule na kuwapatia huduma za afya.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya kazi kubwa iliyowezesha miradi kumi kupitishwa ambayo ina thamani ya Shilingi Trilioni 1.9.

"Miongoni mwa miradi iliyopata ufadhili ni pamoja na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara uliopata shilingi Bilioni 168, mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA), uliopata Shilingi Bilioni 440" Aliongeza Dkt. Likwelile.

Aidha, alisema kuwa Serikali inaendelea na majadiliano na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, ambapo kiasi cha dola Milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Dkt. Likwelile ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake mkubwa na kusema kuwa Serikali itahakikisha kuwa inazisimamia taasisi zinazotekeleza miradi hiyo ili ziweze kutumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird, amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi.

Aliongeza kuwa sekta binafsi ndizo zinatoa ajira kwa wingi na kusaidia kuchangia katika kuongeza mapato ya Serikali. Ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kiuchumi na kijamii kwa faida ya wananchi wake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kushoto), wakisaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird wakibadilishana Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II, Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wakifuatilia maelezo ya Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Katibu Mkuu wa AALCO, Prof. Gastorn

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga )(Mb) kulia akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (Asian – African Legal Consultative Organization (AALCO), Prof. Kennedy Gastorn. Prof. Gastorn alichaguliwa kushika nafasi hiyo wakati wa Mkutano wa 55 uliofanyika mjini New Delhi, India mwezi Mei 2016. Prof. Gastorn alikuja kumuona Mhe. Waziri kwa lengo la kujitambulisha, kushukuru kwa kuungwa mkono na kubadilishana taarifa kuhusu Jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (Asian – African Legal Consultative Organization (AALCO), Prof. Kennedy Gastorn akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo. Alibainisha kwamba nafasi hiyo ni heshima kubwa kwake na nchi kwa ujumla kwa kuwa jukwaa hilo ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya sheria za Kimataifa nchini na Barani Afrika. Aliiomba Serikali ya Tanzania kuendelea kumuunga mkono kwenye utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzisihi nchi za Afrika zijiunge na AALCO. 
Mhe. Waziri akiendelea na mazungumzo yake ambapo alitoa pongezi kwa Prof. Gastorn na kumtakia kila la kheri kwenye utekelezaji wa majukumu yake mapya na kumuahidi ushirikiano wa Serikali ya Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Baraka Luvanda (tai nyekundu) na Afisa wa Kitengo hicho, Bw. Abdallah Mtibora. 

WANANCHI WAIPONGEZA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

$
0
0
Wananchi wameipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa manufaa ya Taifa.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti waliofika katika Uwanja wa Makao Makuu ya Ofisi za Wizara ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Mmoja wa wananchi waliotoa pongezi hizo, Abdulhamid Jumaa alisema wizara imejitahidi kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika.

“Kwakweli mnajitahidi sana, sasa hivi tatizo la kukatika katika kwa umeme limemalizika, nawapongeza ila msibweteke tukajikuta tumerudi nyuma.”

Mwaka huu Wiki ya utumishi wa Umma imeadhimishwa kwa viongozi wa Wizara kusikiliza kero na maoni ya wananchi ambapo wananchi mbalimbali walipata fursa ya kueleza kero zinazowakabili na kuzungumza na Wataalamu mbalimbali.
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini - Idara ya Madini, Mhandisi Chacha Marwa (kushoto) na Mhandisi Chiku Juma wakimsikiliza Hussein Jafari (kulia) akitoa maoni yake kuhusu uboreshwaji wa uchimbaji mdogo wa madini nchini.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Ebahart Diliwa akinakili hoja na ushauri uliokuwa ukitolewa na mwananchi George Mgaya (kulia) ambaye alifika wizarani hapo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mtaalamu kutoka Idara ya Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Phines Sijaona (kushoto) akimfafanulia jambo Alli Hamisi ambaye alifika wizarani hapo kwa lengo la kuwasilisha hoja na ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya nishati na madini.
Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa (kulia) akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Azam Tv, Estabella Malisa (kushoto) kuhusu muitikio wa wananchi wa kutoa hoja na ushauri kuhusu shughuli za wizara katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Ofisi ya Wizara.

Rais Kagame kufungua Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)

$
0
0

Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 01 Julai 2016 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mhe. Dkt, John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Akiwa nchini Mheshimiwa Rais Kagame atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadaye kwa pamoja viongozi hao watashuhudia uwekaji saini wa Makubaliano ya Pamoja (MoUs) baina ya Tanzania na Rwanda katika sekta mbalimbali za ushirikiano. 
Aidha, Mheshimiwa Kagame atashiriki dhifa rasmi ya kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Magufuli .
Mchana wa tarehe 1 Julai, 2016 Mheshimiwa Rais Kagame akiambatana na mwenyeji wake atahudhuria maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kama Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuyafungu.

Ziara hiyo ya Mheshimiwa Kagame inafuatia ziara yenye mafanikio aliyofanya Mhe. Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli nchini Rwanda mwezi Aprili 2016. Ziara hiyo ni ishara nyingine ya kuimarika kwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 23 Juni 2016.

SPIKA AFUTURISHA WABUNGE JIONI YA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia Jambo na Mbunge wa Ilala Azzan Zungu wakati wa futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  kwa ajili ya wabunge leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akishiriki futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya wabunge, kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.
 Wabunge wakishiriki futari kwenye viwanja vya Bunge jioni ya leo Mjini Dodoma.
 Wabunge wakichukua futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge katika viwanja vya Bunge, Mjini Dodoma
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoka kuchukua futari iliyoandaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai jioni ya leo katika viwanja vya Bunge.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

DC WANGING'OMBE:NITANG'OOKA NA WATENDAJI WATAKAONIKWAMISHA KWENYE MADAWATI

$
0
0
Habari na Picha Na Gabriel Kilamlya 
WANGING'OMBE-Njombe
Serikali Wilayani Waging'ombe imesema haiko tayari kuona Shule Inakosa Madawati Hadi Ifikapo Juni 29 Mwaka Huu,  Siku Moja Kabla ya Tarehe Iliyotangazwa na Serikali Kukamilika Kwa Madawati Kwa Nchi Nzima.

Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya Ya Wanging'ombe Dkt.  Asumpta Mshama Leo Wakati Akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo.
Hatua Hiyo Ameitoa Wakati Baadhi ya Maafisa Watendaji wa Kata Wakitoa Taarifa Kuwa Wanaupungufu wa Madawati Kitu Ambacho Amesema Hawezi Kuwavumilia Ilihali Agizo Hilo Ni la Muda Mrefu Sasa.
Amesema Kabla Yeye Hajawajibishwa Juni 30 Mwaka Huu Basi Ataanza na Maafisa Watendaji Hao Ambao Wataonekana Kushindwa Kukabiliana na Suala Hilo na Kwamba Hawezi Kuwajibishwa Pekee Yake.
Kwa Upande Wake Afisa Elimu Msingi Katika Halmashauri Hiyo Mwalimu Haruna Mlilapi Amesema Kwa Wastani Halmashauri Hiyo Haina Upungufu wa Madawati Kwani Kuna Zidio la Madawati Licha ya Shule Chache Kuonekana Kupungukiwa Baadhi ya Madawati Ambayo Ifikapo Juni 29 Mwaka Huu Yatakuwa Yamekamilika.
Katika Kata ya Mdandu Mmoja wa Wenyeviti wa Vitongoji Damian Kihombo Toka Ngelele Kijiji Cha Mdandu Pamoja na Fundi Aliyekuwa Akitengeneza Madawati ya Shule Bwana Zacharia Mng'ong'o Wametajwa Kuuza Madawati Hayo na Kutafuna Fedha Jambo Ambalo Afisa Mtendaji wa Kata Hiyo Bwana Timoth Fute Amelazimika Kuwasweka Lumande.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alisema kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya Watakaoshindwa kuchonga madawati na kuonesha upungufu wa madawati katika shule za Wilaya na mikoa yao Hawatamfaa katika Serikali Yake Jambo Lililowafanya Wakuu wa Wilaya Kuumiza Vichwa Kabla ya Kutumbuliwa.
 Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Dkt. Asumpta Mshama Asema Atawatanguliza Maofisa Watendaji watakaoshindwa kukamilisha utengenezaji madawati ndipo yeye afuate
 Mkuu wa Wilaya Ya Wanging'ombe Dkt.  Asumpta Mshama  Akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo.
 Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo
 Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo
Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo

OMBAOMBA DAR ES SALAAM WATAKIWA KURUDI MIKOA YAO HUSIKA

Wakala wa Majengo nchini (TBA) yakusanya shilingi Bilioni 2.6

$
0
0
Na Ally Daud-Maelezo
Wakala wa Majengo nchini (TBA) wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 43 kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo wapangaji wa nyumba  hizo kushindwa kumalizia madeni wanayodaiwa
Akizungumza hayo katika kilele cha kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha kutoka kwa wateja wao waliowapangisha majengo na bado wanaendelea kukusanya mpaka watakapomaliza.
“Kutokana na mkakati wa kukusanya mapato na kutoa huduma bora kwa wateja wetu tumefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.6 katika kipindi cha miezi mitatu tuliyowapa wateja wetu  kuweza kukamilisha malipo hayo” alisema Bw. Mwakilinga
Mbali na hayo Bw. Mwakilinga amesema kuwa wameamua kutumia siku hiyo kufanya usafi kwenye makazi ya watumishi wa umma na wakazi wengine ili kuweka mazingira bora kwenye miradi yao na jamii nzima kwa ujumla.
“Siku ya leo tumeamua kuitumia kufanya usafi kwenye maeneo ambayo tumeweka miradi yetu kwa watumishi wa umma pamoja na mazingira mengine ili kuepuka na magonjwa yasababishwayo na uchafu” alisisitiza Bw. Mwakilinga.
Aidha Bw. Mwakilinga amesema wanampango wa kupanua wigo wa huduma yao kwa kuwapangisha watumishi  wa umma ambao wanastaafu waendelee kukaa kwenye nyumba hizo ili wasipate shida mara baada ya kustaafu. 
Mbali na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo amesisistiza kuwa  wataendelea na utaratibu wao wa kukusanya kodi  na kuchukua nyumba zao kwa  wale ambao wamekaidi amri yao ya kutolipia kodi nyumba hizo ili wapewe wengine ambao wana huitaji .
Wiki ya utumishi wa Umma imeadhimshwa  kwa kila taasisi ya kiserikali kusikiliza na kutatua kero zinazowapata wateja wanaoutumia huduma za taasisi husika ili kuipeleka nchi katika utendaji bora na mafanikio kwa ujumla.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Bw. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akiwaongoza wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya usafi jijini Dar es salaam katika kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) wakishiriki katika kufanya usafi jijini Dar es salaam ili kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma. Picha na Ally Daud-Maelezo

Bunge lapitisha muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2016

$
0
0
Na: Lilian Lundo 

– MAELEZO, Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ili kuwezesha utekelezaji wa  bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017. 
Muswada huo umepitishwa na Bunge pamoja na marekebisho yake ambayo yametolewa na kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti na wabunge.

Marekebisho yaliyofanyika katika muswada huo ni pamoja na kutoongeza ushuru wa kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10 kwenda 15 ambapo kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti ilishauri Serikali isiendelee na pendekezo hilo kutokana na hatua hiyo kuwa na athari  kwa viwanda vinavyotumia sukari viwandani kama malighafi ya kuzalisha bidhaa nyingine kama juisi na soda.
“Serikali imekubali pendekezo lililotolewa na kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti ya kutoongeza ushuru wa kuingiza sukari ya viwandani kutoka asilimia 10 kwenda asimilia 15, hivyo kuendelea kutoza asilimia 10 iliyokuwepo kwa mwaka huu wa fedha,” alifafanua Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (pichani).
Marekebisho mengine yaliyofanyika ni pamoja na kuondoa adhabu ya kifungo cha miezi Sita kwa wale ambao hawatodai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma na kubaki na adhabu ya kulipa faini kulingana na thamani ya bidhaa.
Aidha Mhe. Mpango amesema kuwa muswada huo umezingatia kwa kiwango kikubwa mapendekezo ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wamiliki wa viwanda, wafanyabiashara na taasisi za Serikali.

KAMPUNI YA TOMONI FARMS LIMITED YAFUNGUA DUKA NA MGAHAWA WA KISASA WA MAZAO YA KILIMO DAR ES SALAAM

$
0
0
MatataG_4336Nje ya duka hilo la kisasa linavyoonekana lililopo katika jengo la Green House, eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam. 
DSC_8003Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa tukio hilo mapema leo Juni 23.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Willybroad Alphonce.
DSC_8013Muonekano wa nje unavyoonekana katika duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani.
DSC_8045
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bw. Franklin Bagalla akifafanua jambo ndani ya duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani
DSC_8047
Baadhi ya bidhaa zinavyoonekana ndani ya duka hilo.

Introducing "CONGRATULATION" song By Kenn DYZOS


MCHEZO YOUNG AFRICANS, TP MAZEMBE KUFANYIKA JUMANNE JUNI 28, 2016 KAMA ULIVYOPANGWA

$
0
0
 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limekataa ombi la Young Africans ya Dar es Salaam juu ya kubadili siku na muda wa mchezo dhidi ya T.P. Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
Katika taarifa ya CAF iliyofika TFF imesema mchezo huo utafanyika Jumanne Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kama ulivyopangwa awali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Young Africans kwa upande wao waliomba mchezo huo ufanyike Juni 29, 2016 saa 1.30 usiku.
Kadhalika, kikao cha maandalizi katika mchezo huo kiliochofanyika leo Juni 23, 2016 kimeagiza uongozi wa Young Africans kuwaelimisha mashabiki wao kukaa katika eneo la mazoea tofauti na mipango yao ya kutaka kukaa eneo lote la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia. 
Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.


Rais Dkt. Magufuli alipozungumza katika Jubilei ya Miaka 50 ya Benki Kuu Tanzania

DIRA YA DUNIA ALHAMISI 23.06.2016

RC MAKALLA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU WA GEPF JIJINI MBEYA LEO, AZINDUA MPANGO MPYA WA BODABODA

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (katikati) akiwa tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Joyce Shaidi na Kulia kwake ni Mkurugeni Mkuu wa Mfuko huo, Daud Msangi. wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Osward Urassa (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Ahmed Kilima.  Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni "Hifadhi ya Jamii kwa Kila Kaya".
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Daud Msangi, akitoa hotuba yake ya ufunguzi iliyoambatana na taarifa fupi ya Mfuko huo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF),  Joyce Shaidi wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango mpya wa Bodaboda (Bodaboda Scheme), leo Juni 23, 2016 katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akimpongeza mmoja wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Mbeya ambayo ni wanachama wa Mfuko wa GEPF kwa kuwa wanachama wapya katika Mpango huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KARATE CLUB OF JUNDOKAN SO HONBU SYSTEM TANZANIA" YAPATA USAJILI NCHINI

$
0
0
Na Zainab Ally Khamis
Dar es salaam School of Journalism (DSJ)
Habari za uhakika zimetufikia kuwa chama cha Karate club of Jundokan So Honbu System Tanzania kimepata usajili, ikiashiria kwamba Tanzania itasonga mbele na kushika nafasi za kimataifa baada ya usajili huo
 Mkufunzi mkuu au Chief instructor wa chama hicho anayetambuliwa kimataifa na baraza la dunia la karate lenye makao yake Okinawa Japan Sensei Rumadha Fundi, mwenye uzoefu wa vyama vitatu vya Goju Ryu tofauti,  alithibitisha hayo.
Sensei Rumadha amesema hayo yamewezekana  baada ya yeye kupata msaada  mkubwa chini ya watu walio karibu sana nae ambao pia imekuwa ni nguvu kubwa inayo mpa moyo wa kuwa na mfumo huo asilia toka visiwa vya Okinawa, Japan.Jundokan So Honbu, ni mfumo unaofundisha mtindo wa Okinawa Goju Ryu katika utamaduni na utaratibu uliyowekwa na Master Chojun Miyagi na kusambazwa na mwanafunzi wake ambaye ni mwanzilishi wa JUNDOKAN, Master Eiichi Miyazato 1957, huko wilaya ya Asato,mji wa Nana, katika kisiwa cha Okinawa, Japan.Maana ya Jundokan " Sehemu ya mafundisho ya mwanzilishi"JUN +DO+ KAN, "jun" imechuliwa toka jina la mwanzilishi wa Goju Ryu, Chojun  na "Do" ikimaanisha mwenendo, " Kan" ikimaanisha shule au mafunzo.Hivyo ndivyo hasa lengo kuu la mfumo huu asilia usio badilishwa au kugeuzwa jinsi unavyofundishwa tokea ulipo undwa na Master Miyagi.Mipango ipo njiani kuwa na tawi lenye lengo na nia kufuata sheria na kanuni za mfumo asilia tu, bila kubadilisha mbinu na "Kata" kama jinsi inavyo bainika na mbinu za " Sports Karate" hasa uchezaji wa "kata" kiujumla.Hivi karibuni, huko visiwani Okinawa katika makao makuu ya tawi hilo, jumuiya ya sanaa ya mapambano " Okinawan BUDOKAN & Karate Federation", imeitambua "Jundokan So Honbu" kama moja ya mitindo asili"Original" kutoka Okinawa inayozingatia maadili na mafunzo yaliyo achwa na mua sisi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.
Pindi mnamo miezi ijayo, tutatoa taarifa ya ufunguzi rasmi wa shule ya karate na uteuzi wa wanafunzi wakuu wasaidizi ambao Sensei Rumadha atajitoa muhanga kuwasaidia kimbinu na ubora wa umahili wa mtindo huu na kuhakikisha mnamo muda wa miaka michache wanapata fursa ya kuwa walimu ( sensei) na kusambaza JUNDOKAN SO HONBU Tanzania yote.
"Msingi tunao mzuri na imara kwa wengi wataojumuika nami kuendeleza hii sanaa hapa nyumbani Tanzania", alisema Sensei Rumadha mwenye uzoefu wa mafunzo hayo ya karate zaidi ya miaka 37 chini ya " ma-sensei" wakuu toka pande zote za  dunia, hasa toka Okinawa, Japan" alisema.
 Picha ya juu:Sensei Rumadha Fundi, wakiwa na Sensei Pedro Cardeira toka Lisbon, Ureno wakifanya zoezi la mbinu ya kuvunja mkono, 
Sensei Rumadha Fundi amesimama mbele ya kumbukumbu ya mnara wa Master Kanryo Higaonna( Mwalimu wa master Miyagi),


Nembo ya chama chake cha Jundokan So Honbu Tanzania 
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images