Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1262 | 1263 | (Page 1264) | 1265 | 1266 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Happy World Sickle Cell Day... Let's join our efforts in awareness and educating the society about SCD. Let's pray for those in hospitals and those who have passed away due to this unbearable condition. Let's pray more for the families and friends for their beloved ones having SCD. 


  Sickle Cell remains a burden in Tanzania, which is 5th in the World with the number of individuals with Sickle Cell Disease. 
  Understanding the disease would help for instance in seeking professional medical help early on and greatly reduce morbidity and mortality caused by the disease.
  SICKLE CELL FACTS
  ❖ Sickle Cell Disease is an inherited disease from BOTH the father AND mother
  ❖ BOTH parents must at least have the Sickle Cell Trait for them to have a child with Sickle Cell Disease
  ❖ It is a lifetime disease that currently has no cure
  ❖ With proper professional medical care, an individual with the disease can live a long and happy life with a career and family

  0 0

  I thought you might enjoy this photograph of Sensei Nantambu Camara Bomani training Goju Ryu Karate on Coconut Beach in Dar es salaam back in 1975 when I was there - Floyd Webb

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akikagua miundombinu ya choo katika moja ya Shule ya Msingi Kongo Kata ya Joshoni Wilayani Nachingwea katika ziara yake aliyoifanya Kukagua Miradi ya Tasaf pamoja na Utengezaji wa Madawati Mkoani Lindi
   Mkuu wa Mkoa wa Lindi akikagua utekelezaji wa agizo la utengenezaji madawati ya shule wilayani Nachingwea
    Mkuu wa Mkoa wa Lindi akitoa maelekezo wakati akikagua utekelezaji wa agizo la utengenezaji madawati ya shule wilayani Nachingwea
   Mkuu wa Mkoa wa Lindi akiandika kwenye ubao kwa lengo la kuona kama ubao uliojengwa unaandikika vizuri Wilayani Nachingwea
  Mratibu wa Tasaf Wilayani Nachingwea James Mbakile Akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Mfuko Huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi ambae anasikiliza kwa Umakini baada ya Kukagua Ujenzi wa Madarasa 2,Vyoo na Madawati 70 Miradi Uliogharimu shilingi Milioni 68.
  Na Abdulaziz Video,Nachingwea,Lindi
  0 0

  Ule mchezo wa Saka saka unaoendeshwa na kituo cha Efm redio 93.7 namba ya bahati, leo siku ya Jumapili ya tarehe 19/06/2016 umewafikia wakazi wa Ilala pale kiwanja cha Aviation - Banana (Mamlaka ya anga), 
  Baada ya dondo la eneo husika na kitu husika kutajwa hewani  wakazi wa Ilala hawakubaki nyuma bali kukesha wakisaka saka kidubwasha husika  kilochofichwa, Huku washindi wakiibuka na shilingi milioni 3, ambapo mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha shilingi MILIONI 2.
   Washiriki wakijaribu kubadilishana mawazo wakati wakisaka saka
  Baadhi wa wakazi wa Ilala wakiwa wana saka saka kidubwasha kilichofichwa na Efm redio katika eneo la aviation pale Banana kitakacho mpatia mkwanja.
   Haikujalisha mwanaume wala mwanamke wote walihusika katika zoezi zima la kusaka saka.
  Moja kati wa washiriki akiondoka uwanjani akiwaacha washiriki wengine wakicheka baada ya kuwavunja mbavu wakati akipotoa kidubwasha chake kikaguliwe.
  Washiriki wa wasaka saka wakiangalia na kushuhudia washindi waliofanikiwa kuibuka washindi.

  0 0

  SIMU.TV: Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia ofisi ndogo ya Vodacom mkoani Geita na kumuua mlinzi pamoja na kuiba mali zenye thamani ya zaidi shilingi 10;https://youtu.be/Lrh7Yy70S_k

  SIMU.TV: Shirika la Reli nchini kituo cha Dodoma limefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 baada ya kufanikiwa kufufua mabehewa 24 ya mizigo;https://youtu.be/OLxHECJCb8E

  SIMU.TV: Taasisi ya Montage kwa kushirikiana na Serena Hotel wanatembelea kituo cha kulelea watoto wenye mazingira magumu cha Dogodogo Center na kuwapata misaada pamoja na kuwalisha chakula; https://youtu.be/5MegntO6pSI
    
  SIMU.TV: Timu ya soka ya Yanga itashuka dimbani leo baadae kuvaana na wenyeji wao  timu ya soka ya Mo Bejaia nchini Algeria; https://youtu.be/VvpuSD1qgiU

  SIMU.TV: Timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana ya Simbion na kutoka sare ikiwa ni mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Shelisheli; https://youtu.be/S62ccjHHaok

  0 0

   Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam,Wakiingia katika eneo la Makao Makuu ya Vodacom Tanzania,Mlimani City kujipatia simu Orijino kwenye Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki.

   Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam,Wakiingia katika eneo la Makao Makuu ya Vodacom Tanzania,Mlimani City kujipatia simu Orijino kwenye Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki.

   Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiwa na mfuko ukiwa na simu  Orijino baada  ya kununua katika Gulio la siku mbili la simu,Lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika  Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam jana, kampuni hiyo imeamua kufanya Gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kuzima simu feki.
   
   Baadhi ya Mawakala wa Vodacom Tanzania,wakimhudumia Aron Mwaifuge, baada ya simu yake kuzimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA juni 16 mwaka huu, aliyefika kununua simu Orijino katika Gulio la siku mbili la  simu lililoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Wakala wa Kampuni Vodacom Tanzania, Rose Mery(kushoto) akiwasikiliza wateja waliofika katika banda lao wakati wa Gulio la siku mbili la kuuza simu Orijino lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na wateja wengi kuzimiwa simu zao feki na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART),  David Mgwasa akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na UDART  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na UDART  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.

  Na Dotto Mwaibale
  MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

  "Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu.
  Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
  Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari akiongea wakati Mkutano wa wadau ulioandaliwa na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Usafiri wa Anga  TCAA-CCC kabla ya kuzindua tovuti yao. Uliofanyikia Makao Makuu ya TCAA Ukonga Banana.wengine  ni Mwenyekiti wa Baraza Shaban Mtambalikena na  Mjumbe wa Baraza Nelly Mwasongwe. 
  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari, (kulia )akiongea  wakati wa Mkutano wa wadau wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Usafiri wa Anga , ulioandaliwa na TCAA-CCC jijini Dar es Salaam, ambapo pia walizunduzua toviti yao. Wengine  ni Mwenyekiti wa Baraza Shaban Mtambalike.  Mjumbe wa Baraza Nelly Mwasongwe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza Debora Mligo.

  0 0
  0 0


  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi nchini kuhakikisha wanawapa watoto wao elimu tangu wakiwa wadogo ili iwajengee misingi bora katika maisha yao.

  Mheshimiwa Samia ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye mashindano ya Qur'an yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.Alisema wazazi wanapaswa kutambua kuwa hakuna zawadi kubwa kwa mtoto kama elimu kwa sababu itamjengea misingi ya kujua afanye nini katika kuendesha maisha yake kwa mafanikio.

  "Vile vile, niwaombe wazazi tuwatengenezee watoto wetu fursa wapate muda wa kupata elimu. Ukimpa utajiri mtoto na kwa kuwa hana elimu anaweza asiutumie vizuri; lakini ukimpa elimu itamfaa katika kuendesha maisha yake," alisema Makamu wa Rais.

  Aidha, aliwataka washindi wote wa kuhifadhi Qur'an wasisite kutafuta elimu zaidi ya dini na ya dunia kama maandiko ya kitabu kitakatifu cha Qur'an yanavyousia ili iweze kuwasaidia ulimwenguni na huko akhera kwenye maisha ya milele.

  Makamu wa Rais alielezea kufarijika kwake kuona kuwa idadi ya washindani inaongezeka kila mwaka bila ya kubagua jinsia zao na washiriki wa mashindano hayo wakiwa na umri mdogo."Hii inaonyesha kwamba vijana wanayo fursa nzuri ya kuhifadhi Qur'an Tukufu tena juzuu nzima wakiwa wadogo endapo sisi kama wazazi tutalifanyia kazi na kuwahimiza vijana wetu," alidokeza.

  Mapema Katibu wa Taasisi ya Aisha Sururu Foundation iliyoandaa mashindano hayo Bi Jokha Lemky alimweleza Makamu wa Rais kuwa kwa mwaka huu mashindano hayo yameshirikisha mikoa 24 ya Tanzania Bara na Visiwani yakiwa na washiriki 653 ambapo 66 ndiyo wameingia fainali.

  Alisema pamoja na mafanikio hayo lakini Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa kompyuta, photocopy, usafiri, scholarship na zawadi kwa washindi jambo ambalo Makamu wa Rais alisema atajitahidi kufanya kazi bega kwa bega na Taasisi hiyo katika kutatua changamoto hizo.

  Katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Makamu wa Rais alikabidhi zawadi kwa washindi waliohifadhi juzuu tatu hadi 30 ambapo aliyehifadhi juzuu 30 alipata shilingi milioni tano.Mashindano hayo yalihudhuriwa na waumini mbalimbali wa dini ya kiislam wakiwemo Balozi wa Algeria nchini na wawakilishi wa mabalozi wa Misri, Sudan na Iran.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (katikati) akiwasili kwenye ukmbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (katikati) akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Aisha Sururu Bi. Aisha Sururu (kushoto) na Katibu wa Taasisi hiyo Bi. Joha Lemky wakati wa mashishindano ya kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

  Sehemu ya Viongozi waliohidhuria mashindano hayo ya kuhifadhi Quran
  Majaji wa Mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu kwenye ukumbi wa Diamond.
  Sheikh Muharami Mziwanda akitoa elimu juu ya umuhimu wa kuijua Quran kwenye mashindano ya Kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimkabidi mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na mshindi wa jumla wa kuhifadhi quran juzuu 30 ,Ashura Amani (16) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kike walioshiriki mashindano ya kuhifadhi quran kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

  0 0

  Maelfu ya waumini wa dini ya Kiislam toka maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam na mikoani wamejitokeza kwenye Mashindano ya kusoma Quraan Tukufu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

   Vijana kwa wazee  wamejitokeza kushuhudia mashindno hayo.
  Wengine wengi walibaki nje ya uwanja baada ya nafasi kujaa ndani.

  0 0

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC), zimeanzisha rasmi ushirikiano katika maeneo ya utalaam, ufundi na mafunzo katika nyanja ya Usafiri wa Anga.

  Hayo yalibainishwa rasmi jana, baada ya uongozi wa TCAA ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu Hamza Johari ulipokutana na ugeni toka China ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu wa CAAC Xu Hao, walipokutana Makao Makuu ya TCAA, Ukonga Banana jijini.

  Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Johari alisema Tanzania na China zina mkataba ikiwa ni makubaliano muda mrefu katika nyanja ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na mafunzo, ila kinachofanyika sasa ni kuanza rasmi kwa utekelezaji wa makubaliano hayo.

  Johari alisema, hatua hii itasaidia hasa ukichukulia Tanzania uwezo ni mdogo katika nyanja za utaalam na teknolojia katika miundombinu.

  “Lengo ni kuwa na miundombinu ya kisasa lakini kwa gharama nafuu na pia wataalam wetu kuanza kupata mafunzo ya mara kwa mara nchini China”.

  Johari aliongeza pia, eneo jingine litakalofaidika katika kuanza rasmi kwa utekelezaji wa makubalino hayo ni eneo la usalama , ambapo sasa wataalam wa usalama wa Anga wa TCAA watapata fursa ya mafunzo nchini china.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto) akiongea wakati wa kikao kilichohusisha wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China(CAAC). Jijini Dar es Salaam leo , Lengo la kikao hicho ni kuanzisha ushirikiano katika maeneo ya utalaam, ufundi na mafunzo katika nyanja ya Usafiri wa Anga. Watatu kutoka kushoto nni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Nchini China (CAAC) Xu Ho.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto )akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China(CAAC), Xu Ho,Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kuanzisha ushirikiana wa wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya China.(CAAC) kiklichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini China Xu Ho,(CAAC) wakati walipofika pamoja na ujumbe wake kwenye kikao cha kuanzisha ushirikiana wa wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya China.(CAAC) kiklichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Hamza Johari (kushoto wa tatu ) na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China(CAAC), Xu Ho (wane kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mamlaka hizo mbili wakati wa kikao cha kuanzisha ushirikiana wa wataalam kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na wataalam kutoka Mamlaka ya China.(CAAC) kiklichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Na Ally Daud-Maelezo

  SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo mifugo na kuzungushia wigo bustani.

  ‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya. 

  Aidha amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12 hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.Dkt. 

  Ulisubisya amesema kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa huduma za malaria nchini.Akizungmzia huduma za afya kwa akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60 mwaka 20015/16. 

  Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana na Malaria.

  Amesema ili Serikali iweze kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya nchini.Mr. Ruyobya amesema utafiti huu ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam.
  Wadau mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Ally Daud-maelezo.

  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema kuwa kitendo cha Klabu ya Stand United kwenda kuwashtaki katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na  kuibuka kwa  kambi mbili zinazotaka kufanya uchaguzi wa viongozi wapya huku wakiwatupia lawama kuwa  kwa kushindwa kutoa muongozo wowote unaohusiana na sakata lao ni kwamba wanajisumbua na zaidi litaletwa tena chini yao.

  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (Pichani), amesema kitendo kilichofanywa na timu hiyo, hakiwezi kuwashangaza kwa kuwa lazima watarejea kwao katika kupata muafaka. "Kiukweli tunachofahamu ni kwamba Stand ni mwanachama wa TFF na wala siyo Fifa kwa sababu TFF ndio wanachama katika shirikisho hilo, hivyo kitendo cha wao kukimbilia huko siyo tatizo kwetu, maana lazima watataka mrejesho kutoka kwetu".

  Amesema, Lakini kwa upande mwingine sisi hatujapata barua au taarifa yoyote kutoka kwa Stand ila haitapita muda lazima Fifa watume taarifa yao kwani mwisho wa siku wao ndio watatakiwa waje kwetu kutafuta muafaka,” amesema Lucas.

  Stand hivi sasa kuna mgogoro mkubwa, ambapo kuna makundi mawili. Kuna viongozi wale waliowekwa madarakani na wanachama na wale ambao waliwekwa na TFF. Kila upande upo kwenye mchakato wa uchaguzi, kundi la wanachama ambalo linajiita wenye kampuni utafanyika Juni 24, mwaka huu, wakati kundi jingine lililowekwa madarakani na TFF ambalo wanachama wanaliita wavamizi, limetangaza kufanya uchaguzi wake Juni 26, hivyo haijulikani kina nani wana mamlaka ya kufanya uchaguzi huo na ni uongozi upi utakuwa halali kikatiba.

  0 0


  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.

  Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO.

  0 0

  Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wenye ualbino, Ikpowose Ero, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana juu ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa watu wenye ualbino Afrika uliofanyika nchini hivi karibuni, Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN, Alvaro Rodrigers na Mkurugenzi mkazi wa Under the same  Sun.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imeaswa kupiga vita dhidi ya  ukatili, unyanyapaa pamoja na  mauaji Watu Wenye Ualbino ili kuweza  kila mtu kuishi kwa amani katika nchi yake.  

  Katika kupiga vita dhidi ukatili na unyanyapaa ya watu wenye Ualbino ni kuweka mkakati wa kuandaa mashitaka kwa ubora zaidi dhidi ya uhalifu wa Ualbino ,kuandaa kanuni za kusimamia waganga wa jadi pamoja na kuimarisha kampeni maalum na endelevu za ufahamu kwa miaka miwili mfululizo ili kupunguza vifo vitavyotokea mara kwa mara.

  Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar  es Salaam uliohusisha  nchi  29  Kanda ya Afrika,Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero, amesema mauaji ya watu wenye Ualbino  yanaendelea kutokea Barani Afrika na kufanya jamii hiyo kukosa haki ya kuishi  kutokana mauaji dhidi yao.
    
  Amesema  kuna matukio mengi dhidi ya watu wenye ualbino  lakini yamekuwa hayaripotiwi kwa sababu ya usiri katika masuala ya ushirikiana,ushiriki wa familia na ushiriki wa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha.

  Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga amesema serikali inatakiwa kuongeza bajeti yake ili watu wenye Ualbino wapate haki sawa katika masuala ya matibabu.

   “Serikali ihakikishe kuwa vifaa vya kuimarisha uwezo wa kuona vinapatikana kwa ajili ya mtu m wenye ualbino  anapokuwa darasani na kutoa vizuia jua nafuu kama tiba muhimu ili kuziua saratani ya ngozi, ambayo inaendelea kuondoa maisha ya watu hao”amesema Nyanduga.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa The Under Sun (TUS), Vick Mtetema amesema kwa pamoja wataendelea kupambana na unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino.

  Amesema polisi wa kimataifa na watu wa Uhamiaji washirikiane kwa pamoja ili kulinda watu wanaopitisha watu wenye Ualbino.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony Mavunde (kushoto), akipokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 6 kutoka kwa Mkurungenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole iliyopo Manispaa ya Dodoma,mwishoni mwa wiki
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde (wa pili kushoto), akifurahi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliypo manispaa ya Dododma mara baada ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 uliotolewa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk. Jasmin Tsekwa (wa pilikulia) na kulia ni Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma wakiwa wamekaa kwenye madawati ambayo waliikabidhi shule ya msingi makole iliyomjini Dodonma jana ,msaada huo unathamani ya zaidi ya sh milioni 6.
  Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma Rehema Hamisi (kulia) akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliyopo mjini Dodoma, baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa wa benki hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali kupunguza tatizo la madawati mashuleni.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipokea Hundi ya mfano ya shilingi milioni kumi kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni UR Group, Salim Omar, zilizotolewa na kampuni yake k ajili ya ujenzi wa Madawati kwa Shule za Msingi.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imewataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, kutumia fursa ya elimu bure kwa kujifunza kwa bidii ili  taifa lijalo liweze kuwa wataalam wa kutosha  kutokana na mazingira bora ya kusomea yamewekwa.

  Hayo ameyasema leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul alipokuwa akipokea mfano wa hundi ya sh. milioni 10 kutoka katika Kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Limited (UR GROUP) kwaajili ya kuwezesha mpango elimu bure katika upande wa madwati.

  Makonda amesema kuwa wanafunzi wasitumie fursa hiyo kama njia ya kubweteka bali waitumie kama mlango wa kutokea  kwa kuja kuwa viongozi  bora kutokana na mazingira waliosoma.
  Amewataka  wanafunzi hao kujifunza kwa bidii ili kujenga taifa la kesho lenye wasomi wengi ambao watakuwa viongozi kijamii na kitaifa.

  Makonda  aliipongeza kampuni ya UR Group kwa msaada walioutoa na kwamba umeongeza tija kwenye utoaji wa wa elimu bora nchini kwa kuunga jitihada za Rais Dk.John Pombe Magufuli.

  “ katika msaada huu naamini i kutoa ni moyo wala sio utajiri na kila mwanafunzi anatakiwa kutambua kuwa tunapata misaada kutoka kwa watu kama nyie ili kuwafanikisha wao kusoma katika mazingira bora ya kusomea’’amesema Makonda.

  Amesema bado mkoa una uhitaji wa madawati mengi kwaajili ya wanafunzi hasa kwa shule za msingi ambapo ndipo msaada umekuwa ukielekezwa zaidi maana ndio msingi wa elimu.

  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Ezekiel Sizya alisema kwakuona umuhimu wa shughuli zinazofanywa na serikali, wamesukumwa kuiunga mkono hasa katika suala zima la kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure katika mazingira mazuri yakiwemo ya kukalia dawati wawapo darasani.

  Sizya amesema huo sio mwisho kwao wa kuiunga serikali mkono bali wataendelea kujitoa kwa kile wanachokipata ili kuhakikisha kuwa nchi inafikia kiwango kizuri kiuchumi na kielimu.

  “Tulichotoa kwaajili ya watoto wetu sio kikubwa lakini tunaamini tutakuwa tumewasaidia wanafunzi zaidi ya mia moja kutokaa chini badala yake watakalia madawati wawapo darasani,watanzania wenzangu wenye mapenzi mema kuendelea kujitoa kwaajili ya nchi yetu hasa suala zima la elimu ili kujenga taifa la wasomi,”amesema.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bw. Jaskaran Chugh ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Polytra International yenye Makao yake nchini Ubelgiji (katikati) na Bw. Mark Lemki wa Kampuni ya Impala ya Switzerland, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

older | 1 | .... | 1262 | 1263 | (Page 1264) | 1265 | 1266 | .... | 3270 | newer