Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1261 | 1262 | (Page 1263) | 1264 | 1265 | .... | 3283 | newer

  0 0


  DVD za Siri Za Familia zitapatikana kuanzia tarehe 1 August 2016 baada ya Season  1 kumalizika. Kila DVD itakuwa na Episode 6 na unaangalia kwa zaidi kidogo ya Masaa 2 na Nusu. Kila DVD itakuwa Shs 2500 rejareja na Shs 2000 kwa wanunuzi wa jumla watakaonunua copies kuanzia 100 (Mia moja).
  Unaweza kutuma order yako sasa kwa SMS au Whatsapp kwenye namba +255 768 355 555. Please usipige simu. @sirizafamilia @sirizafamilia

  0 0
  0 0


  Katika mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel.

  Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao.

  Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu.

  Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.

  Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel. 
  Mmimiliki wa 80/20 blog Shamimu akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari.
  Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel

  Baadhi ya bloggers wakipata futari

  Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO.

  0 0

  Na Daudi Manongi-Dodoma
  Waziri wa nchi na Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.

  Waziri makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

  Aidha amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hii kuanzia katika ngazi ya chini.

  Mhe.Mkamba alisema kuwa upandaji wa miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani Nyanja za Afya,ufugaji,misitu,utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.

  Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira.Pia amehaidi Serikali kutenga fedha za kutosha,kutengeneza Sera nzuri,sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.

  Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazohusiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visiki hai.

  Aidha Waziri Makamba amesema kuwa serikali ina mkakati mkubwa wa uboreshaji wa Sera za Mazingira uku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya Tanzania kuwa ya Kijani.


  Warsha hiyo kwa wabunge imeeandaliwa na shirika la Lead foundation uku ikishirikisha ofisi ya Bunge na wadau kutoka World Vision, Ever Green na World Agroforestry Center ambao walitoa mada mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya kuhifadhi Uoto wa Asili,Kilimo cha kijani,namna ambavyo ufufuaji wa Visika hai na Ngitili zinavyoweza kuchangia Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na kuimarisha mshikamano kitaifa wa ustawishaji Miti.

  0 0

  Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi wa CHUO Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho”  alisema.
  Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngorongoro.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   
   The newly appointed Executive Secretary of Lake Victoria Basin Commission (LVBC), Dr. Ali Said Matano took the Oath of Allegiance before the Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. Present at the brief ceremony was the EAC Director for Human Resource and Administration, Mr. Joseph Ochwada and other senior staff of the Community. 
  Dr. Ali Said Matano (Kenyan) solemnly swore to be faithful and bear true allegiance to the East African Community and to preserve, protect and defend the Treaty for the Establishment of the East African Community as by law established. 
  Dr. Ali Said Matano now officially assumes office as the new Executive Secretary of Lake Victoria Basin Commission following the expiry of Dr. Canisius Kanangire’s (Rwandan) tenure on 26th May 2016. 
  Dr. Matano’s appointment was endorsed by the 33rd Extra-Ordinary Meeting of the EAC Council of Ministers that took place on 27th May 2016 in Arusha, Tanzania. This was after his appointment was approved by the Sectoral Council of Ministers for the Lake Victoria Basin. 
  LVBC is a specialized Institution of the East African Community responsible for coordinating the sustainable development agenda of the Lake Victoria Basin, with its Headquarters located in Kisumu, Kenya. 
  Dr. Matano was the LVBC”s Programmes and Projects Development Officer. The post of Executive Secretary rotates amongst the five Partner States.
   Dr. Matano in grey suit/red tie takes Oath of Allegiance closely monitored by the Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko
   Dr. Matano receives the signed copy of the Oath from the Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko
  Group photo opportunity


  0 0  0 0


  0 0


   Mkufunzi Nathaniel Mjema akiwasilisha mada ya  kujitathmini kwa viongozi wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yaliyowashirikisha Makatibu wakuu na wasaidizi wao.
   Waratibu wa Mafunzo hayo wakifuatilia kwa kina uwashilishwaji wa mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum akitoa mchango katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya  Maendeleo endelevu yaliyowashirikisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar.
   Dkt. Jochen Lohmeier kutoka Uongozi Institute akitoa mada kuhusu kuitathmini Jamii katika mafunzo ya Makatibu wakuu na Wasaidizi wao yanayofanyika Ofisi ya CAG Maisara, Mjini Zanzibar. 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo na kujadiliana kutokana na kazi waliyopewa na wakufunzi wao.
  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akiwaonesha Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa Naakala ya tangazo la Serikali lililotangaza pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano wa kujadili mgogoro baina ya wanachi hao na pori la akiba katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
  Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shaban Kissu (aliyesimama) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa huo katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
  Mzee Mathayo wa kijiji cha Ikengwa akiishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa kuanza kushughulikia mgogoro baina ya wananchi wa kijiji hiko na pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma ambapo kamati iliyohusisha wananchi, Pori la akiba Mkungunero na Uongozi wa Wilaya Kondoa iliundwa kumaliza mgogoro huo.


  0 0

  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.

  Mheshimiwa Samia ametoa kauli hiyo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti club iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam

  Alisema wanaume kama wakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumwinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala ya ujasiriamali.

  "Tuwaingize wanaume kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu katika mapambano hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie nafasi hizo tulete mabadiliko," alisema Makamu wa Rais na kuongeza."Penye mkusanyiko wa watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu, wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje."

  Aliipongeza Taasisi hiyo ya Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu inakuwa na ugumu zaidi kuliko wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana na ujanajike wake.

  "Tuna kazi kubwa ya kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka," alidokeza.


  Mheshimiwa Samia alitumia fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na kuondoa ada katika shule za msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi yao, kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo amewashukuru Watanzania kwa kuchangia madawati.Aliwataka wazazi kuwatunza watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema.

  Mtendaji Mkuu wa Binti Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa shirika hilo liliamua kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha watoto kumudu masomo yao na hatimaye kufikia malengo yao."Kwa hiyo ukiwa na fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari, pedi, vyote tunapokea kwa ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao yanaweza yasitimie kutokana na changamoto hizo,"

  Kampeni hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.Katika hafla hiyo iliyopambwa na onesho la mavazi la watoto Makamu wa Rais ambaye alikubali kuwa mlezi wa Binti Foundation aliahidi kusomesha watoto 100 wakati mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa alitoa ahadi pia ya kusomesha watoto 50.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  mara baada ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.

  Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja  na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia  Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akitazama jambo liliokuwa linaendelea (halionekani pichani) pamoja na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Binti Foundation Johari Sadiq .

  Sehemu ya watoto walioshiriki kuonyesha mitindo mbali mbali ya Mavazi pamoja na Wabunifu wao.
   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Lionel Messi ameifikia rekodi ya Gabriel Batistuta (Bat Goal) ya kuwa mfungaji wa wakati wote kwa timu ya taifa ya Argentina baada ya kuifungia timu yake bao na kufikisha mabao 54. Messi aliiongoza Argentina kuichapa Venezuela mbao 4-1 na kufuzu nusu fainali kwa kupambana na wenyeji Marekani.

  Argentina walianza kujipatia ushindi dakika ya 8 tu pale Gonzalo Huguain alipopachika mpira kimiani kufuatia pande safi alilomegewa na Messi. Dakika 20 baadaye yaani dakika ya 28 Gonzalo Huguain akaipatia timu yake bao la pili. Mnamo dakika ya 43 mwamuzi Roberto Orozco akawazawadia Venezuela penati, ambapo mchezaji Seijas alipiga kwa staili ya "Panenka il Cucchiais" lakini kipa wa Argentina Romelo aliishitukia na kutulia pale pale na kuidaka.

  Dakika ya 60 ndipo 'Rapulga' Lionel Messi akaifungia timu yake bao la 3. Venezuela walijipatia goli la kifuta chozi dakika ya 70 kupitia kwa nyota wake Solomoni Rondon, goli ambalo halikudumu hata dakika 1 kwa dakika ya 71 Lamela akaipatia Argentina bao la 4.
  Nako kwenye dimba la Levis Stadium,Santa Clara Califonia, Chile walimpa Mexico mapumziko ya wiki yaani goli 7-0.Alikuwa mchezaji hatari wa Chile Eduardo Vargas aliyeingia kimiani mara 4, dakika ya 15, 51, 56 na 73.Huku Edson Puch akifunga goli 2, dakika ya 44 na 86, naye Alexis Sanchez akifunga goli moja dakika ya 48. Sasa Chile atapambana na Colombia katika hatua ya nusu fainali.

  0 0

  Na Zainab Nyamka

  MWALIMU Hans Van De Pluijm ameonelea kutokana na mkanganyiko uliopo kuhusiana na beki wa kulia Hassan Kessy ameamua kumtumia beki kiraka Mbuyi Twite katika mchezo wa leo dhidi ya Mo bejaia na zaidi katika mazoezi ya mwisho jana usiku alimuweka Twite kucheza nafasi hiyo. 

  KIKOSI:

  1: Deo Dida
  2: Mbuyu Twite
  3: Oscar Joshua
  4: Kelvin Yondani
  5: Vicent Bossou
  6: Thabani Kamusoko
  7: Simon Msuva
  8: Harouna Niyonzima
  9: Donald Ngoma 
  10: Hamic Tambwe
  11: Deus Kaseke

  SUBSTUTE:

  - Ally Bathez
  - Mwinyi Ngwali
  - Pato Ngonyani
  - Antony Matheo
  - Juma Makapu
  - Godfrey Mwashiuya

  0 0

  Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam,Wakiingia katika eneo la Makao Makuu ya Vodacom Tanzania,Mlimani City kujipatia simu Orijino kwenye Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki.
  Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiwa na mfuko ukiwa na simu Orijino baada ya kununua katika Gulio la siku mbili la simu,Lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam jana, kampuni hiyo imeamua kufanya Gulio hilo kutokana na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kuzima simu feki.
  Baadhi ya Mawakala wa Vodacom Tanzania,wakimhudumia Aron Mwaifuge, baada ya simu yake kuzimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA juni 16 mwaka huu, aliyefika kununua simu Orijino katika Gulio la siku mbili la simu lililoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Wakala wa Kampuni Vodacom Tanzania, Rose Mery(kushoto) akiwasikiliza wateja waliofika katika banda lao wakati wa Gulio la siku mbili la kuuza simu Orijino lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Makao makuu ya kampuni hiyo,Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kampuni hiyo iliandaa gulio hilo kutokana na wateja wengi kuzimiwa simu zao feki na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
  Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius Magoma, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Kenya na Tanzania mara baada ya kutembelea kituo cha Uhamiaji Horohoro. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faifa za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa, kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njiaya kupumua. Hali kadhalika unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Wazi Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya YogaDuniani kwenye ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
   Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati).

   Mkao unaosaidia mwili kuwa imara au kama unavyojulikana "Tadasana". Kutoka kushoto ni Wazir Nape, Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda.
   Umbo lapembe tatu au Trikonasana.

   Yoga ikiendelea, kutoka kulia kwenda kushoto, ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kalaghe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Balozi wa India nchiniTanzania Sandeep Arya, na Balozi Mbelwa Kairuki.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Winga wa zamani wa kimataifa wa klabu ya Yanga anayetajwa kuwa winga wa muda wote nchini kwa vigezo vya waliomuona, Mzee wetu Abdurahman Lukongo amefariki Dunia mchana huu katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.

  Msiba upo nyumbani kwake makutano ya mtaa wa Simba na Kariakoo, Kariakoo jijini Dar es salaam

  Inna lillah wainna ila ilaihi raajiuun...

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
  Askari Polisi wakiwa katika mafunzo maalumu ya kupokea simu katika kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.


  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  KOCHA mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm amesema kuwa ana imani na kikosi chake kuwa kitacheza vizuri kwani ameweza kukaa nao kwa siku kadhaa na amewapa mbinu mbalimbali hasa wanapokuwa wapo ugenini na zaidi amewataka kutokufuata mchezo wa wapinzani wao.

  Pluijm amesema hayo kupitia kwenye mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na kusema wameenda nchini Algeria kwa ushindi ila hawatataka kupoteza mchezo huo zaidi ushindi ndio wanachokitaka au kupata sare ambayo itakuwa na manufaa kuliko kupoteza kabisa.

  "Siku chache nilizokaa na wachezaji na wakafanya mazoezi ya pamoja yanatosha kabisa kuweza kuondoka na ushindi kwani Nimewaambia wacheze mchezo wetu na zaidi wasiwafuate mchezo wao,"amesema Pluijm. Ninachoamini kuwa wachezaji wangu watafuata kile nachowaambia na zaidi wapinzani wangu watatumia uwanja wao wa nyumbani kucheza kwa kujiamini na sisi tutacheza kwa tahadhari kubwa sana.

  Yanga wanacheza leo na Mo Bejaia ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa kundi A ambao utapigwa nchini Algeria saa sita na robo usiku wa saa za Afrika Mashariki. Katika mchezo huo watakosa huduma ya Nahodha wao Nadir Haroub 'Canavaro' anayetumikia kadi nyekundu na Juma Abdul ambaye ni majeruhi.

older | 1 | .... | 1261 | 1262 | (Page 1263) | 1264 | 1265 | .... | 3283 | newer