Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110006 articles
Browse latest View live

Wateja GNLD sasa kulipia bidhaa kwa njia ya M-Pesa

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa(kushoto) pamoja na Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel Mutiso,wakipongezana mara baada ya kukamilisha makubaliano ya kibiashara na kampuni inayohusika na uuzaji wa dawa asilia zenye ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania,ambayo itawawezesha wateja wa kampuni hiyo kulipia Ankara zao kupitia huduma ya M-PESA.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa(kushoto) akionyesha njia muhimu za M-PESA pindi mteja akiwa analipia Ankara zake akiwa amenunua bidhaa na dawa asilia zenye ubora wa kimataifa za GNLD Tanzania,wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma hiyo,wanaoshuhudia katikati Mwakilishi wa GNLD Tanzania, Daniel Mutiso,Rais wa vikundi wa GNLD Tanzania,Bi.Dora Juma.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa akimsikiliza jambo na Mkurugenzi wa Timu ya Dunia wa wa kampuni inayohusika na uuzaji wa dawa asilia zenye ubora wa kimataifa ya GNLD Tanzania,Bi.Grace Rubambey,mara baada ya hafla ya kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma ya M-Pesa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria halfa hiyo ya kuwawezesha wateja wa kampuni ya GNLD kuanza kulipia bidhaa mbalimbali zenye ubora wa kimataifa kupitia huduma ya M-Pesa.
Mmoja wa wateja wa kampuni inayouza bidhaa za asilia pamoja na dawa zenye ubora wa kimataifa (GNLD)akiuliza swali juu ya ulipaji pesa kupitia huduma ya M-PESA,wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kauli Ya Serikali Bungeni Kuhusu Mlipuko Uliotokea Arusha Mei 5, 2013

Wadau wa Muziki kuanza kuwapigia Kura wanamuziki wao

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya zoezi la upigaji kura kwa wamamuziki wanaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zilinazoelndelea kupigwa kupitia mitandao ya simu na intanet,wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Sanaa BASATA, Vivian Nsao Shalua,Mratibu wa Tunzo za Muziki Tanzania wa Kutoka BASATA,Angelo Luhala pamoja na Muwakilishi wa Inovex,Lloyd Zhughu.
Muwakilishi wa Inovex,Lloyd Zhughu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya namna kura zitakavyokuwa zikihesabiwa.

EU yaahidi kusaidia Bajeti ya Tanzania Dola milioni 562

$
0
0
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya Wiki ya Umoja wa Ulaya itakayoadhimishwa nchini na kuhusisha shughuli mbalimbali za kijamii. Wengine katika picha ni Balozi wa Hispani nchini Mh. Luis Cuesta Civis(wa kwanza kushoto) , Balozi wa Ireland nchini Mh. Fionnula Gilsenan na ,Balozi wa Nethrland nchini Mh. Dkt. Ad Koekkoek Emmanuel . 

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO_Dar es salaam

UMOJA wa Nchi za Ulaya (EU) umeahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika miradi ya maendeleo, ambapo kwa mwaka ujao wa fedha wa 2013/2014 itaipatia Tanzania zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 562.

Kauli hiyo imetolewa leo na Balozi wa EU nchini Tanzania Mh. Filiberto Sebregondi jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya Wiki ya Umoja wa Ulaya itakayoadhimishwa nchini na kuhusisha shughuli mbalimbali za kijamii.

MAKAMU WA RAIS DKT. AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MPYA WA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia waumini wa Dini ya Kikristo wakati wa ghafla ya kuwekwa wakfu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel Joseph Makala na kuzinduliwa kwa Dayosisi hiyo mpya ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria iliyofanyika jana katika kanisa la Ebeneza Shinyanga mjini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emannuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu na kuzinduliwa kwa Dayosisi hiyo katika Kanisa la Ebeneza Shinyanga mjini jana Mei 5, 2013. Katikati ni Askofu Mkuu KKKT Tanzania, Dkt Alex Malasusa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji Emmanuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa KKKT Tanzania baada ya kuwekwa Wakfu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria na kuzinduliwa rasmi Dayosisi hiyo katika kanisa la Ebeneza Shinyanga mjini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Viktoria Mchungaji, Emmanuel Joseph Makala, baada ya kuwekwa wakfu. Picha na OMR.

Taswa FC, Taswa Queens kuumana na Bongo Movie Jumamosi

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya netiboli, Taswa Queens Jumamosi zitacheza na timu ya wacheza filamu, Bongo Movie FC na Bongo Movie Queens katika mchezo maalum wa kirafiki.

Mechi hizo zimepangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe kuanzia saa 10.00 jioni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.

Majuto alisema kuwa mchezo wa kwanza ambao utahusisha timu za netiboli umepangwa kuanza saa 10.00 jioni ambapo siku hiyo Taswa Queens itakuwa ikicheza mechi yake ya tatu tokea kuanzishwa kwake siku ya sikukuu ya Pasaka mwaka huu.

Mechi ya kwanza ya Taswa Queens ilikuwa dhidi ya Kiliflora Queens na kushinda kwa mabao 28-8 na mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Kombaini ya walimu wa wilaya ya Kibiti na kushinda kwa 36-2.


Majuto alisema kuwa wachezaji wa Taswa Queens chini ya wachezaji wake, Imani Makongoro na Oliver Albert, kutoka Mwananchi Communications Limited aliyechezea nafasi ya GA, Clezencia Tryphone (Tanzania Daima), Elizabeth Mbassa, Sharifa Mustapha na Johari William wote wa Business Times Limited (BTL). Makocha wao ni Amina Mussa kutoka BTL na Zainabu Mussa.


Kwa upande wa Taswa FC, mechi hiyo ni muhimu sana kwao kutokana na matokeo mabaya ya mechi ya mwisho ya kufungwa mabao 2-0 wilayani Kibiti.

Majuto alisema kuwa wamejiandaa vizuri ili kutoa kipigo kwa Bongo Movie katika siku hiyo ambapo bendi ya Msondo itatumbuiza baada ya mchezo huo ulioandaliwa na Dar Bonanza.

“Mechi zote mbili ni sehemu ya maandalizi yetu ya safari ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga, hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kushinda, makocha wangu, Ali Mkongwe na Ibrahim “Maestro” Masoud wameandaa programu nzuri na bila shaka itatoa matunda mazuri,” alisema Majuto.

MAONESHO YA WIKI YA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII KUANZA MEI 13

$
0
0
Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa. 
 Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde akizungumza  wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA. Kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa. 
Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imeandaa Maonyesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 13 hadi 18 mjini Dodoma.

Akizungumza na Habari Mseto, Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka, alisema, makampuni na mashirika mbalimbali yanatarajia kushiriki wiki, ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kuwa, maonyesho hayo itakuwa ni pamoja na mifuko shiriki kutoa elimu kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, juu ya huduma ambazo zinapatikana na tija yake katika taifa.

Aidha, Irene aliongeza kuwa, SSRA inawataka wanachama wa PSPF kuondoa hofu juu kutokuwepo kwa mafao yao katika mfuko huo, na kwamba mafao yao yako salama na hakuna kitakachopoteza mafao ya wanachama hao.

Alisema kuwa, mfuko wa PSPF utakuwa ukipewa bilioni 50 kila mwaka kwa ajili ya kwa ajili kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida.

Irene pia, aliwataka wanachama wa mifuko mbalimbali kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifuko kutokana na SSRA kutoa miongozo juu ya uendeshaji wa mifuko hiyo.

Alibainisha kuwa, mifuko yote imepewa miongozo katika uendelezaji huduma wanazozitoa ikiwamo ya mafao kwa wafanyakazi wanaostaafu.

Alisema kuwa tatizo lililokuwepo kwa mifuko ya PPF na NSSF, kujitoa kwa wingi kwa wanachama wake, jambo linalochangiwa na waajiri, hali ambayo SSRA inataka kuwafuatilia waajiri wanaowanyima wafanyakazi haki zao.

Congratulatory Message to re-elected Prime Minister of Malaysia

$
0
0

Jakaya Kikwete - Doug Pitt Named Goodwill Ambassador Of Tanzania Hosted by President Kikwete

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Congratulatory Message to His Excellency Najib Tun Razak, upon being re-elected as the Prime Minister of Malaysia on 6th of May, 2013.  
The message reads as follows:

"His Excellency Najib Tun Razak,
Prime Minister,
Kuala Lumpur,
MALAYSIA.

Your Excellency,

It is with immense pleasure that I take this opportunity to convey to you, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf warm greetings and congratulations upon your being re - elected as the Prime Minister of Malaysia.  

We in Tanzania are confident that under your able leadership the Government and people of the Malaysia will continue to score remarkable achievements in the years to come.
I take this opportunity to reaffirm my country’s commitment and desire to continue working with you and your Government in further strengthening the existing ties of friendship and cooperation between our two countries and peoples.

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of Malaysia.

Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA’’

Issued by:
Ministry of Foreign Affairs and International Co- operation,
Dar es Salaam.
6th May, 2013.

CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA VIRGINIA (VIU) CHATOA UNAFUU KWA WANAFUNZI WA KITANZANIA WATAKAOJIUNGA NA CHUO HICHO

$
0
0
 Mhadhili akitoa cheti kwa mmoja ya wahitimu wa chuo hicho kwenye maafali yaliyofanyika Jumapili May 5, 2013 Fairfax Virginia.


Baadhi ya wanafunzi Watanzania wanaosoma chuo hicho Kutoka kushoto ni Alex John Luketa(student recruitment and marketing assistant in Virginia international University ),anaefuata Veronica N Magacha ,Cathereen Virginia Minja, Rehema Waziri ,Winfrida Josephat na Jose Fabian
Bendera ya Tanzania inayowawakilisha wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma chuo hicho cha Virginia International University. ikipitishwa mbele na mwanafunzi wa Kitanzania Winfrida Josephat.
 Wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa chuo.
 Bendera za nchi mbalimbali zinazowawakilisha wanafunzi na nchi wanazotoka zikisimikwa.
 Juu na chini ni picha ya pamoja ya wanafunzi waliomaliza chuo
Hapa chini ni Video ya Alex John Luketa akielezea jinsi ya kujiunga na chuo hicho hasa kwa wanafunzi wa kutoka Tanzania hebu msikilize
Now we are recruiting student for summer II and Fall 2013, Virginia International University Now we are can process admission very fast, just find me in FACEBOOK; Alex john Luketa and skype; alex.john.luketa in my number +15712449300 in this number you can get me in whatsapp,Tango,viber and also in my email alex@viu.edu) for more information visit www.viu.edu.

mambo ya gado leo

Charity Dinner and Dance Gala - Geneva, Switzerland

Shambulio la bomu Arusha, Tanzania kwa mujibu wa VOA

msaada tutani

$
0
0
Naomba unirushie hii kwenye blog yetu ya jamii.
Nipo hapa Barbados kwa shughuli binafsi, na nitakuwepo mpaka 11/May/2013.
Nilitaka fahamu kama kuna Mtanzania anaishi hapa.Ningependa sana kukutana nae.
Jina kapuni please just display my e-mail umba34@gmail.com
                                               Mdau

Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao

$
0
0
Na Anna Nkinda – Kuwait

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye matatizo kama hayo waliopo nchini.

Mama Kikwete alilitoa ombi hilo jana alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuona jinsi wanavyotoa mafunzo kwa watoto hao ambayo yameweza kuwabadilisha akili zao na kuwa sawa na za watu wengine.

Alisema kuwa watoto wenye mtindio wa ubongo hata nchini wapo na wanapata mafunzo katika vituo vichache zilivyopo lakini kama watashirikiana kwa pamoja wataweza kubadilishana ujuzi ambao utawasaidia kutoa mafunzo mazuri zaidi kwa watoto hao.

“Ninawapongeza kwa kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kutoa mafunzo kwa watoto hawa kwani ni jambo jema kuwasaidia watu wenye matatizo.

“Watoto hawa wakipewa mafunzo akili yao itakuwa sawa na watu wengine, wakiwa wakubwa na kufikia umri wa kujitegemea wataweza kufanya kazi mbalimbali za maendeleo ambazo zitawaingizia kipato na kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye”, alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Samira Al-Saad alisema kuwa kama watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo watapelekwa shule mapema zinazotoa mafunzo kwa ajili yao watapona na kuwa na akili sawa na watu wengine.

Dk. Samira alisema kuwa wazazi wengi hawajui kwamba matatizo ya mtindio wa ubongo yanatibika kama mtoto akipewa elimu ya darasani na kufanyishwa mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake mwenyewe bila ya kutegemea msaada wa jamaa zao.

“Kituo hiki kilifunguliwa mwaka 1994 na hadi sasa kina wanafunzi 120 ambao wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo na kinajiendesha kwa kupata msaada kutoa Serikalini, watu na mashirika binafsi ya ndani na nje ya nchi”, alisema Dk. Samira.

Aliendelea kusema kuwa umri wa watoto wa kuanza masomo ni miaka sita hadi 15 na kama mwanafunzi atakuwa amevuka miaka 15 atajifunza zaidi mafunzo ya vitendo ambayo yatamuwezesha kujitegemea hapo baadaye.

Dk. Samira alisema, “Wanafunzi wetu wameweza kupata ajira sehemu mbalimbali hii ni baada ya kupata mafunzo ambayo yamewafanya kuwa na akili sawa na watu wengine ambao hawana matatizo haya, kuna baadhi yao tumewaajiri hapa na hivi sasa wanawafundisha wanafunzi wenzao.

Mama Kikwete pia alitembelea Kituo cha Al-Kharafi ambacho kinatoa huduma ya mazoezi kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubungo na kuona jinsi watoto hao wanavyofanya mazoezi yao.

Kituo hicho kinapokea watoto wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi 12 ambao wanafanya mazoezi kwa kucheza michezo mbalimbali ambayo inawabadilisha akili zao na kuwa katika hali ya kawaida .


Akiwa katika kituo hicho alijionea kazi mbalimbali zinazofanywa na watoto hao ambazo ni uchoraji, ushonaji, upishi pia aliona michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyimbo na maonyesho ya mavazi. Mama Kikwete aliambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Kuwait kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI


CHIEF EBOU SHATRY- ALONGA NA SWAHILI TV SEHEMU YA KWANZA

TANZANIA YAHADHARISHA WACHACHE KUAMUA KWA NIABA YA WENGI

$
0
0

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi.

Na Mwandishi Maalum

Tanzania imesisitiza na kutamka bayana kwamba, majadiliano yoyote yanayohusu maslahi ya wengi ni lazima yajadiliwe kwa uwazi, ukweli na yawe shirikishi ili kuepusha misuguano na migongano isiyokuwa ya lazima.

Kauli hiyo imetolewa siku ya jumatatu na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya mkutano wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, inayosimamia masuala ya Utawala na Bajeti.

Makamu wa Rais azindua kitabu cha Profesa Mwandosya

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt. Mohamed Gharib Bilal,  amezindua kitabu kinachohusu Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania kilichoandikwa na Profesa Mark Mwandosya April 16, 2013 wakati wa mkutano wa mamlaka za Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi bara la Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Profesa Mwandosya kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa wasomi kuweka muda na kuandika vitabu vyenye kuchochea tija. Kati ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe
Mama Lucy Mwandosya akimsaidia mumewe Profesa Mark Mwandosya kuandaa vitabu ili awasainie wageni waalikwa katika hafla hiyo.


Remarks by Prof Mark Mwandosya, Minister of State,President‘s Office(Special Duties), at the Launch of the Book on ‘Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania, at the Meeting ofthe African Forum For Utility Regulators, Arusha, Tanzania, 16 April, 2013.


H.E Dr. Mohamed Ghalib Bilal, Vice President of the United Republic of Tanzania,

Hon. Prof. Jumanne Maghembe (MP), Minister for Water.

Hon. Mulongo, Regional Commissioner for Arusha.

Honorable Members of Parliament

Distinguished Delegates and Guests,

Ladies and Gentlemen,

Your Excellency Vice President,
Let me say how much honour you have done me, agreeing to officiate at the occasion of the launch of the book on “Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania:” the English translation of which would be Regulation of Public Utilities in Tanzania.

Development is about the accumulation of knowledge and experience by mankind and the application of this knowledge to master the environment. The transmission of this knowledge from one generation to another is the essence of continuity of civilization

Traditionally in Africa knowledge was passed from one generation to the next orally.  The lack of written languages meant that this knowledge, passed on orally was distorted over time and could not be the basis of improvement of knowledge. I submit that failure to pass on knowledge through the written form is one of the major causes of Africa’s relative backwardness. The Challenge before us is how we could pass on accumulated experience and knowledge, in written form, a form which would be a basis for critique and further improvement.

It is in the context of the aforesaid that I decided to write this book, a larger portion of which was written from my hospital bed.

I have been lucky to have been associated with the evolution of the policy on regulation of utilities in Tanzania, and the establishment and oversight of the Tanzania Communications Regulatory Authority, the Tanzania Civil Aviation Authority, the Surface and Marine Transport Authority, and the Energy and Water Utilities Regulatory Authority.

The Book is written in Kiswahili. Swahili is the national language of Tanzania and Kenya. It is widely spoken in Eastern and Central Africa. It is spoken by more than 120 Million people worldwide. I had in Mind this audience when I embarked on this venture.

My daughter, a student at Birmingham University,  my alma mater, wanted to know why I had decided to write the book in Kishwahili. I asked her a simple question: In what language do you dream? It took her a week to confirm that the language of her dreams was Swahili. Likewise I think in Kiswahili and translate my thoughts into English if need be. I trust I have a future occasion to translate this work into English,or Arabic,or Bambara.

The book deals with the concept of regulation, important aspects of utility regulation, independence of the regulator, consumer protection, structure of regulatory agencies,technical and economic regulation, relationship between the Government and the Regulator, the regulator and the legislature, cross-cutting issues, achievements and challenges, and the way forward.

I would like to take this opportunity to thank my family, my wife, our children and grand children, for their support and encouragement. Many colleagues have reviewed various drafts of this book. They are too numerous to mention.I thank them. I wish to thank the Tanzania utility regulators, EWURA, TCRA, TCAA and SUMATRA, for the support they have rendered to me during the time I was the Minister responsible for these utilities and their continued support.

By way of conclusion, let me end the same way I began, by thanking you Your Excellency, for the honour you have done me to agree to launch the book on “Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania.

Thank you.




WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA KANISA LA OLASITI NA KUZUNGUMZA NA WAUMINI NA VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.
Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo May 7,2013 kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha, Peddy Castelino (kulia) May 7,2013 wakati alipotembelea kanisa hilo May 6,2013 ambako ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia sehemu lilipodondoshwa bomu hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa Pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu (kushoto ) na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo (katikati), May 7,2013 baada ya kutembelea Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha ambako May 6,2013 ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Watani wetu wa Jadi Wachemsha katika World Rugby Sevens Glasgow

$
0
0

Timu ya taifa ya mchezo wa Rugby nchini Kenya ilichemsha vibaya katika michuano ya Rugby sevens iliyofanyika katika uwanja wa Scotstoun, Glasgow siku ya jumamosi tarehe 4 Mei 2013. Walipoteza 17-14 Afrika ya Kusini katika mchezo wao wa kwanza na kufuatiwa kipigo cha 26-0 kutoka kwa Samoa katika mchezo wa pili. Mchezo wa tatu walishindwa kwa 10- 21 kwa Canada ambayo ilihafifisha matumaini yao ya kufanya kufanya vizuri katika Kombe Kuu la robo fainali katika siku ya pili.

Kutokana na kuchemsha kwao ni dhahiri kocha mkuu Mike Friday aliwapa wakati mgumu wachezaji baada ya matokeo mabaya yaliogubikwa na makosa makubwa ambayo yangeweza kwa urahisi kuepukwa. Kenya walionekana kana kwamba walipakwa grisi mikononi kabla ya mchezo kuanza na kufanya kuwa vigumu kupata mpira na kupoteza ki rahisi.

Ingawaje timu ya Kenya ilicheza vizuri kwa kiasi fulani katika mchezo wa kwanza, mchezo wao wa pili dhidi ya Samoa ulikuwa jicho-kidonda na kufanya mashabiki kuuma meno kutokana idadi ya makosa yaliyofanywa. Mchezo wao wa mwisho na Canada walijitahidi kurekebisha makosa yao ya awali na kutia bidii kukaba zaidi na kupunguza nafasi za kupokonywa mpira ingawaje waliishia kushindwa pia.

Kila wakati Kenya ilipokuwa na mpira, wao kuishia kufanya makosa, hivyo kupewa adhabu na penati. Mpaka sasa timu ya Kenya ina pointi 77 na kuwa na matumaini ya kufikia pointi 100 katika mwisho wa mzunguko. Hiyo ina maana Kenya inatakiwa na kuja na pointi 23 kutoka kwa timu ya Scotland na Uingereza. Kama wanaweza kuchukua pointi nane kwa kushinda Glasgow kisha wao kubakia na pointi 15 kwa kushinda Uingereza.

Afrika nzima inawakilishwa na Kenya pamoja na South Africa.
Canada wakijaribu kuizibiti Kenya kufunga goli.

Viewing all 110006 articles
Browse latest View live




Latest Images