Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1254 | 1255 | (Page 1256) | 1257 | 1258 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Waendesha bodaboda wakikokota pikipiki zao wakati wa kuvuka katika njia ya mabasi ya mwendokasi eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni ushahidi tosha kwamba utii bila shuruti katika jamii ni jambo linalowezekana kabisa endapo kama sheria zilizopo zitasimiwa na kuonekana zinasimamiwa na hatua kuchukuliwa kwa wakosaji bila simile. Yaani, baada ya mamlaka husika kuanza kuchukua sheria kwa wananchi wabishi na wakorofi na kuwafikisha mahakamani mara moja, watumiaji wengi wa barabara, hasa wenye vyombo vya moto vya magari na pikipiki wameshika adabu zao. Kila wafikapo katika njia za mwendo kasi aidha hawapiti kwenye barabara hizo, ama hushuka kwenye pikipiki zao na kukatisha huku wakiwa wakizikokota. Ufuatiliaji wa Globu ya Jamii umeshuhudia haya yakifanyika bila kuwa na usimamizi ama ulinzi. Tunatarajia hali hii itashamiri katika kila nyanja ya maisha yetu.
   Mdau akikatisha barabara ya mwendo kasi maeneo ya Magomeni Usalama akiwa anakokota pikipiki yake. Sheria ni kwamba ukatisha ukiwa umepanda hiyo pikipiki ni kosa na ni kupelekwa rumande na kesho mahakamani. Hakuna mjadala wala faini....
   Hata waendesha baiskeli nao wamekuwa wapole. Kabla ya sheria kuchukua mkondo wake hapo angepita akiwa ameipanda hiyo baiskeli na kuvuka. Sheria ya njia ya mwendo kasi ya UDART inasema endapo kama utagongwa na basi ni wewe utayekuwa umefanya kosa....
  Huyu mdau alikuwa akikokota pikipiki yake iliyosheheni mzigo mkubwa. Pikipiki ikamshinda maeneo ya Magomeni Kagera. Utii wa sheria bila shuruti oyeeee...!!!

  0 0  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Maliwa akiwapungia waumini wa Kanisa katoliki  jimbo la Geita baada ya kuhudhuria sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo hilo, Flavian Kassala  zilizofanyika mjini Geita Juni 12, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa katoliki katika sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo la Geita, Flavian Kassala  (kushoto kwake) zilizofanyika kwenye kanisa kuu katoliki mjini Geita Juni 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), kuhakikisha kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kinaanza kufanya kazi.

  Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo kufuatia kukamilika kwa Data Centre hiyo miezi kadhaa iliyopita na mahitaji ya wadau wa huduma ya kutunza kumbukumbu za taasisi zao katika kituo hicho kuongezeka.

  “Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji mkuu wa TTCL hakikisheni kituo hiki kilichojengwa kwa gharama kubwa kinaanza kutumika na kuwezesha mashirika na taasisi mbalimbali kutunza kumbukumbu zao na kuiletea Serikali mapato”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amesema huduma ya mtandao katika kituo cha Data Centre imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa zao kwa haraka.

  Akizungumza mara baada ya kukagua maeneo mbalimbali unapopita Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Prof. Mbarawa amemtaka Mkurugenzi wa TTCL kanda ya Kaskazini Bw. Peter Lusama kuhakikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unapitishwa juu ya nyaya katika maeneo yenye changamoto za mafuriko ili kuepuka uharibifu wa mara kwa mara na usumbufu kwa watumiaji.

  Aidha amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa DATA CENTRE kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote, ambapo asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na 25 itatunza taarifa za Serikali.

  Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinamilikiwa na Serikali na ujenzi wake umegharimu takribani dola za kimarekani milioni 93.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa Singida na mahali utakapojengwa uwanja mpya na kusisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini kusimamia kikamilifu ujenzi wa uwanja wa ndege wa sasa ambao upembuzi yakinifu wake umekamilika.

  Amesema tayari Serikali imebainisha viwanja 11 vya ndege nchini kote na kuvifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kuvijenga ili viweze kukidhi mahitaji ya soko.

  Amevitaja viwanja hivyo kuwa ni Lake Manyara, Musoma, Iringa, Tanga, Songea, Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambavyo vitapanuliwa na kujengwa kwa kiwango cha lami.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre), jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi. 


  0 0


  NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

  SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa lego la kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti zilizokuwepo. 

  Mgogoro huo ambao umeonekana kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo. 

  Akizungumzia kuhusina na sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kwamba baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu. 

  “Jamani wananchi wa kijiji cha mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama tulivyokubaliana. 

  Alisema kwamba serikali ya awamu ya tano ambayo inangozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli itahakikisha kwamba inaleta mabadiliko chanya kwa kuzingatia usawa bila ya kuwa na uonevu wowote ule hasa katika masuala ya ardhi ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kubwa katika Wilaya ya bagamoyo na maeneo mengine, na kuahidi kushirikiana nao mambo yote ya kimaendeleo. 
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha mwavi kata ta Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mkutano maalumu na kutatua sakata la mgogoro wa ardhi baina yao pamoja na mwekezaji Mkorea, ambaye amepokonywa hekari 131 na zimerudishwa kwa wananchi wenyewe.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Baadhi ya wawekezaji hao ambao ni wakorea wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo. 


  0 0


  0 0


  0 0

  Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Yanga African sports club,Azam FC,Simba sports Club na Prison,Pamoja na Mchezaji bora,Mfungaji bora wa ligi na kocha bora wa msimu huu ulioisha wa  ligi kuu ya soka ya Tanzania bara,Watakabidhiwa zawadi zao mapema mwezi ujao na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni  mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa ucheleweshaji wa kutoa zawadi hizo baada ya kumalizika  msimu wa ligi hiyo mwezi uliopita umetokana na baadhi ya timu zinazoshiriki kwenye mechi za mashindano ya kimataifa kama vile mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika na kuingia kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

  “Tunaomba radhi kwa  timu husika,wachezaji na wadau wa soka kwa zoezi hili kuchelewa ila tunawahakikishia kuwa  zawadi ziko tayari na zitakabidhiwa  mapema mwezi ujao”.Alisema Nkurlu.

  Pia alishukuru wadau wote waliofanikisha ligi hiyo hadi kufikia mwisho ambapo timu yanga ya jijini Dar es Salaam iliibuka tena bingwa kwa mwaka huu “Licha ya changamoto zinazoendeleza kujitokeza katika ligi  yapo mafanikio makubwa na ligi hii inazidi kuwa na msisimko mkubwa nchini tunawashukuru wadau  wote na tuna imani kuwa itazidi kuwa bora katika siku za usoni”

  Alisema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa udhamini wa ligi hii hata katika msimu ujao kwa mujibu wa mkataba wake na TFF na aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi hii ikiwemo kuwawezesha wachezaji kunufaika zaidi katika ushiriki wake.

  0 0

  Muonekano wa Barabara ya kutoka Mbeya kuelekea Tunduma mpaka Mkoani Rukwa, na hiki ni Kipande Kidogo cha njia panda ya Mlowo Mbozi Mkoani Songwe kama ambavyo kinaonekana katika Taswira hii. 
  Hiki pia ni kipande Kidogo cha Barabara hiyo ya Mbeya Tunduma na hapa pia ni njiani kuelekea Vwawa ni mara baada ya kutoka Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.
  Baadhi ya Wafanyabishara wa kuuza Matunda wakiwa katika Kilinge chao cha eneo la Mpemba Wilayani Momba..
  Wataalamu wa kuendesha Gari Ng'ombe wakiwa Sambamba na Gari lao kando kando ya Barabara hiyo..
  PICHA NA MR.PENGO MMG NYANDA ZA JUU KUSINI.

  0 0

  Assalaam alaykum wanajamii.

  Leo hii tarehe 13/06/2016 sisi NGURUMO ZA SIMBA WHATSAP GROUP tumetimiza mwaka mmoja toka kuanzishwa rasmi tarehe 13/06/2015.

  NGURUMO ZA SIMBA ni kundi la mashabiki,wapenzi na wanachama wa Simba ambao wameamua kuungana na kutengeneza kundi moja kubwa kwa kazi ya kujitolea kwa ajili ya Simba SC.

  Kundi letu ambalo leo hii linatimiza mwaka mmoja toka kuundwa kwake,lipo mstari wa mbele kuhakikisha kwamba sisi washabiki,wapenzi na wanachama tunazidi kutoa elimu kwa wale wote ambao hawana uanachama wa Simba SC kufahamu faida za kuwa mwanachama ambazo ni pamoja na kuongeza mapato kupitia malipo ya ada ya mwaka ya Simba SC.

  Tayari mpaka sasa wapenzi na mashabiki wengi walioungana nasi wamepata uanachama wa Simba SC.

  Tupo mstari wa mbele kuhakikisha tunawasaidia wapenzi,washabiki na wanachama kuwa na Umoja ambao ni muendelezo wa falsafa ya SIMBA NGUVU MOJA.

  NGURUMO ZA SIMBA pia imejikita kuhakikisha wana Simba sisi wenyewe kushirikiana katika furaha ama huzuni.

  Tunaendelea kuwaambia wana Simba wote duniani kuwa na subira kipindi hiki kigumu na tuendelee kuwa na ushirikiano mwema na viongozi wetu waliopo madarakani na tuwape ushahuri wa msingi ambao utakuja kutuletea mafanikio msimu unaokuja wa mwaka 2016/2017.

  Simba nguvu moja.

  HAPPY BIRTHDAY NGURUMO ZA SIMBA.

  Imetolewa na:

  DAWATI LA NGURUMO ZA SIMBA.

  0 0

  UONGOZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umekanusha tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Juni 10, mwaka huu katika kijiji cha Nyakabale Mkoani Geita.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

  "Mbunge huyo alisikika katika mkutano wa hadhara kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) huwalazimisha wanawake wanaoingia mgodini bila kibali kufanya mapenzi na Mbwa watumikao kulinda eneo la Ngodi"

  Tenga amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa uzito mkubwa dhidi ya Mbunge huyo kwani taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kuchafua na kutuharibia sifa mbele ya serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na jamii kwa ujumla.

  Amesema kuwa Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) amekuwa akitoa kauli mbalimbali kuwa ni za kichochezi na zinapelekea uvunjifu wa amani kwa wakazi wa Mkoani Geita.

  Pia ameviomba vyombo husika vilivyopewaa maagizo kuchunguza tuhuma hizo vifanye kazi yake kwa kuzingatia haki na sheria ili ukweliujulikane na sheria ichukue mkondo wake amesema Tenga.
  Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kukanusha kwa taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya ki jamii kuhusiana na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM). Kulia ni Mwanasheria wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), David Nzaligo.
  Mwanasheria wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), David Nzaligo akitoa ufafanuzi wa kisheria wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Mhandisi wa Miradi (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa  Barabara zinazoendelea kujengwa ili  kupunguza msongamano  wa magari katika jiji La Dar es salaam, Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.

  Frank Mvungi-Maelezo.
  SERIKALI yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar es salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Akifafanua Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa  kwa wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.

  “Ujenzi wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.

  Kwa upande wa Barabara ya kinyerezi  Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo unaendelea.

  Miradi  ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016  itasaidia kupunguza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa  katika jiji la Dar es salaam.

  Awamu ya Tatu  ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba - Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B - Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.

  Wakala wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika jiji hilo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Jamal Simba Mnyate(mwenye jenzi nyeupe) amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba sc Msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara ingawa ameweka wazi kuwa kuchelewa huko ni kwasababu kuna mambo walishindwa kufikia muafaka.


  "Siku chache zilizopita nilikuja Dar kusaini, lakini tulishindwa kukubaliana na nikarudi Nyumbani Morogoro, nimekuja Dar jana nimesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuelewana. Kwahiyo kila kitu tayari na nimerudi zangu Morogoro, ila kila kitu fresh kabisa na Simba",amesema Mnyate

  Usajili wa mchezaji huyo umeonekana kuwavutia mashabiki wengi wakati tetesi zikitawala kwamba atatua Msimbazi, wengi wao wamesifia na kusema anaweza kusaidia kwenye kikosi cha Simba

  Simba pia imemsajili mlinzi wa Mwadui, Emmanuel Simwanza, ingawa kamati ya Usajili ya klabu hiyo inasema mambo yao ni kimya kimya.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba, akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, yanayofanyika mjini Mbeya Juni 13, 2016.Mafunzo hayo ni muendelezo wa kampeni ya WCF kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani, ILO, kuwapatia mafunzo Madaktari kote nchini, ili kujenga uwezowa kufanya tathmini ya madhara aliyoyapata mfanyakazimahala pa kazi kabla ya kupatiwa fidia. WCF itaanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi Kuanzia Julai 1, 2016.
  Baadhi ya madaktari waliohudhuria mafunzo hayo
   (PICHA ZOTE NA EMMANULE MADAFA).

  0 0

  BODI ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes msimu wa 2016/2017. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu mara baada ya kukamilisha mchakato wa usajili unaoanza Juni 15, 2016.

  Makundi hayo yenye timu nane (8) kwa kila moja, yamegawanywa kwa alama ’A’, ‘B’ na ‘C’
  Kundi A lina timu za:
  1        Abajalo - Dar es Salaam
  2        African Sports - Tanga
  3        Ashanti United  - Dar es Salaam
  4        Kiluvya United - Pwani
  5        Friends Rangers - Dar es Salaam                 
  6        Lipuli - Iringa               
  7        Mshikamano FC -Dar es Salaam         
  8        Polisi Dar - Dar es Salaam  

  Kundi B

  1        JKT Mlale - Ruvuma
  2        Coastal Union - Tanga
  3        Kimondo FC -Mbeya
  4        Kinondoni Municipal Council  - Dar es Salaam
  5        Kurugenzi  -Iringa
  6        Mbeya Warriors- Mbeya
  7        Njombe Mji  - Njombe
  8        Polisi Morogoro   -Morogoro

  Kundi C
  1        Alliance Schools-   Mwanza
  2        Mgambo Shooting  - Tanga
  3        Mvuvumwa FC - Kigoma
  4        Panone FC - Kilimanjaro
  5        Polisi Dodoma   - Dodoma
  6        Polisi Mara -Mara
  7        Rhino Rangers  -Tabora
  8         Singida United -Singida

  0 0

   Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo  cha  mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, John Mabula(Mwenye jenzi ya njano)

  Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Rais Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi japokuwa ametangulia mbele za haki.

  Rais Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu ambazo alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting; kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.

  Rais Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo. Bwana ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  SERIKALI imetoa tamko la kuhairisha mashindano ya umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari Tanzania (Umitashumta na Umisseta) ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari hadi hapo yatakapotangazwa tena.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amesema mashindano hayo yameahirishwa ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari kwani wadau muhimu wa mashindano hayo wote wanahitajika katika kumaliza tatizo hilo.

  Amesema kuwa mpaka jana zilikuwa zimebaki siku 17 tu ambazo Rais John Magufuli alikuwa amezitoa kwa ajili ya kumaliza tatizo la upungufu wa madawati nchini hivyo amewataka wadau wote wa mashindano hayo kuvuta subira hadi hapo zoezi hilo litakapomalizika ndipo waendelee na mashindano hayo.

  Amesema mashindano hayo yanashirikisha viongozi wote katika ngazi ya halmashauri, mikoa na wizara ambapo viongozi hao ndio wanaoshiriki katika kusimamia na kufanya ufutiliaji wa zoezi la utengenezaji wa madawati kama alivyoagiza Rais Magufuli.

  “Kwa vile muda uliobaki kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais la utengenezaji wa madawati ni finyu kwa maana siku 17 tu, serikali imeona ni busara sana kuahirisha michezo hiyo ili nguvu zote zielekezwe kwenye utengenezwaji wa madawati na michezo hiyo itafanyika tarehe nyingine itakayopangwa na kutangazwa,” amesema Simbachawene.

  Ameongeza kuwa, “Nitoe wito kwa walimu wetu waendelee kuwahimiza wachezaji wote walioteuliwa kuendelea na mazoezi katika shule zao wanazosoma, hii itakuwa ni sehemu ya kujitayarisha kwa ajili ya mashindano hayo muhimu mara yatakapopangwa.”

  Michezo ya Umisseta ilipangwa kufanyika kitaifa Jijini Mwanza ambapo ilitakiwa ianze June 13 hadi 22 mwaka huu huku ile ya Umitashumta ilipangwa kuanza June 25 hadi Julai 5 mwaka huu ikiwashirikisha jumla ya washiriki 6,200.

  0 0

   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

  WATU wasiofahamika wanatuhumiwa kuchoma nyumba moja moto kwa kutumia petroli wilayani nyamagana.

  KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio la kuchoma nyuma lilitokea  Juni 13  mwaka huu  majira ya saa 2 katika  shamaliwa ,wilaya ya nyamagana katika makazi  ya samson kaijunga (60).

  Msangi amesema wakati Samson akiwa amelala usiku na familia yake alistuka na kugundua nyumba yake ikiwa inawaka moto ulioanzia sebuleni na kuteketeza baadhi ya mali ambazo ni seti moja ya sofa, kabati, na mbao zilizoezekea paa la juu ya nyumba pamoja na jipsamu na vitu vingine vidogovidogo lakini moto huo haukuleta madhara kwa binadamu.

   Kamanda Msangi amesema wakati familia hiyo ikiwa imelala  watu wasiofahamika walimwaga  petroli ndani ya nyumba sebuleni kupitia dirishani kisha wakawasha moto ulioanzia kuwaka sebuleni na kuanza kusambaa kwenye vyumba,  ndipo wenyenyumba walipogundua na kupiga yowe za kutaka msaada ambapo watu walifika na kusaidia kuuzima moto huo.

  Amesema chanzo cha tukio hilo bado halijajulikana, lakini linahusishwa na wivu wa kimapenzi kati ya mke mdogo anayeishi kwenye nyumba ambapo tukio hilo la moto limetokea na wake wenzake wawili ambao hawana maelewano mazuri, mpaka hivi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

  Moto huo bado hazijafahamika , jeshi la polisi bado linanendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana natukio hilo. juhudi za kuwasaka na kuwatia nguvuni wahalifu wa tukio hilo bado zinaendelea.

  Msangi amewataka wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza wote kwa pamoja kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwatia nguvuni wahalifu hao ambao ni hatari na wanania ovu dhidi ya binadamu wenzao.

  0 0

  Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
  Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.
  Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.


  0 0

  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na viongozi wa Chama na Serikali alipowasili Chaani Masingini kukagua kituo cha Afya cha kijiji hicho kufuatia mwaliko wa Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul- latif.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Kaskazi ‘A’ Hassan Ali Kombo na Daktari dhamana wa Wilaya hiyo Rahma Abdalla Maisra wakati akikitembelea kituo cha Afya cha Chaani Masingini.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatana na viongozi wa Jimbo la Chaani wakiangalia tanuri la kuchomea taka za kituo cha Afya cha Chaani Masingini alipotembelea kituo hicho.


older | 1 | .... | 1254 | 1255 | (Page 1256) | 1257 | 1258 | .... | 3278 | newer