Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live

INTRODUCING "MAMA" by PETER MSECHU & BANANA ZORRO


KWAYA YA KINYAKYUSA

B​ARCLAYS CUSTOMERS TO OPEN A BANK ACCOUNT IN 20 MINUTES.

0
0
CUSTOMERS at Barclays Bank Tanzania (BBT), will now have priveledge to open a bank account within 20 minutes.

Speaking during the launching of a program namely 'Barclays Operating Customers' (BOC) in the City of Dar es Salaam at the weekend, BBT Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joel Bendera said that the bank becomes the first bank in Tanzania to start the system that can help customers to open an account for a maximum period of 20 minutes.

The Barclays marketing chief said the operation for this program will be started in two branches. “We will start the operation in two branches Sleep Way and Ohio branches and we hope to expand the operation” he said.

He moreover said this program will help customers to save their time to open an account and not only saving the time to open an account but also even the requirements are very simple which are work identity, settlements identification and sources of income of the customer.

On his part, Barclays Head of Customers Network Retail Banking, Emmanuel Katuma said they have research and testing much the operating system and approve that it can work effectively and accurately.

“We are sure that this program will be successfully and the first in the country because we have spend our time and resources to come up with” said Katuma.

He however said that this program will help the bank to get many customers especially the new account openers, where as one customer may require only 20 minutes maximum to open a new account.

“Before starting this operating we were having the capacity of opening ten to twenty account in one branch but now we will have ability to open one account in every twenty minutes you can see how many accounts can be opened per day in one branch” he added.

Barclays bank has 17 branches in the country and expecting to open new branches soon. The branches are available in 10 regions in the country. 


Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) and banks Head of Operations, Msungu Mwilingo (second right), displaying placard to official launch the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar and banks Head of IT, Dakshit Pandya. 
Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Ag. Head of Marketing and Corporate Affairs, Joe Bendera, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joe Bendera (centre), addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Head of Customers Network, Emmanuel Katuba, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI

UCHAMBUZI WA GEOFFREY CHAMBUA: Nauona Moshi Mweupe Kwa Bi Hillary Clinton

0
0
 Unaweza Kusema Demokrasia Inazidi Kubakwa Duniani Baada ya Raisi wa Sasa wa Marekani Kujitanabaisha Waziwazi Kwamba Anampigia Chapuo Mgombea wa Uraisi kwa Tiketi ya ‘Democrats’ Bi Hillary Clinton na Kujinasibu Kwamba Ndiye Atakayeibuka Kidedea. 
Ukweli ni Kwamba ima faima, bado Clinton ana nafasi kubwa ya kurudi Kwenye Kasri Jeupe la Marekani kama Raisi wa Taifa Hilo Kubwa Kabisa Duniani na SI kama 'The Then American First Lady…….'
Kwa NINI?
1. Ndiye anayeungwa mkono na Waliberali asilimia 67 kwa kuwa siasa zake ni za mrengo wa kati ilihali 33% wameonesha waziwazi kuwa na siasa za Uhafidhina
2. Kete ya Obama kwa Hillary inazidi kung’aa baada ya Trump kuingia mkenge kutokana na uwiano wa madoa baina ya wawili hao, licha ya Hillary kuwa na kimeo cha Bengazi Trump anaonekana kuwa na ‘vimeo vingi Zaidi na hili ndio kete kubwa sana kwa Obama ikiwa ni pamoja na madai yake ya kutokubaliana na uislamu na walatino walio wengi na kusema ‘akiwa Raisi atajenga ukuta dhidi yao’ What We Fear from Donald Trump, We Have Already Seen from Hillary Clinton
3. Mashirika karibu yote ya Kijasusi ikiwemo FBI na CIA wamekataa katu kumpa ushirikiano Trump
4. Mabwanyenye wote wa Kimarekani wakiwemo akina Rockfellers na Cox wanaonekana kumuunga mkono Hillary. Hapa pia ukumbuke  Bernie Sanders ameonesha msimamo wake kumuunga mkono Hillary JAPO ATAENDELEA NA KAMPENI ZAKE
5. Kitendo cha TRUMP kumdhalilisha Hillary kwamba akiwa hedhi atashindwa kubeba majukumu kinaonekana kuwa shubiri ya ushindi kwa TRUMP kwa sababu imekua ni chukizo la uharibifu kwa wanawake walio wengi kwenye sanduku la kura (Donald Trump 'period knickers' are a hit with American women), japo kwa sasa anaonekana kujirudi akisema Hillary ameolewa na mwanaume mkware kwa wanawake akirejeza kashfa za ngono zilizomkabili mumewe enzi za kiti chake (Hillary's Married to 'the Worst Abuser of Women in the History of Politics')
6. Taifa la Marekani limejitengenezea mazingira ya kuwa Taifa la Historia duniani, kwa hapa hakuna shaka kwamba lingependa kuandika historia nyingine ...
Hapa Ikumbukwe kwamba 36% ya wapiga kura wanawawake wanaiunga mkono Democrats ukilinganisha na 20% ya wanaume kwa mujibu ya "TWAWEZA" ya huko. 
Kadhalika asilimia iliyobaki ya vijana wameshajipambanua mahaba yao kwa Bi Clinton……………. "Historic Moment for Women" soma pia Makala ya ‘Could women hand Hillary Clinton the U.S. presidency?


UPENDO WOMEN'S GROUP YA UBELGIJI YAFANYA HARAMBEE YA KUISADIA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TANZANIA

0
0
Mgeni rasmi Dr.Guido Nicolai akifungua hotuba maalumu kuhusu Harambee ya kuchangia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.Kikundi cha Upendo Womens Group kilichopo nchini Ubelgiji jana tarehe 11.06.2016 walifanya Arambee hiyo kuwasaidia kina mama wanaojifungua katika mazingira magumu nchini Tanzania.
Mweka hazina wa kikundi cha Upendo women's Group Begum Chunny akitoa maelewo mafupi jinsi alivyoenda Tanzania kukagua maendeleo yao yanayopatkana katika kuchangia hospital ya Mwananyamala,kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Mrs Theresia Greca. 
Kina mama wa Upendo wakiingia ukumbini kwa shangwe huku wakiimba nyimbo ya kuisifia Tanzania
Burudani ya muziki wa Jazz ilitumbuizwa na kikundi cha  JAIL CITY VETERAN,watu waliburudika sana na muziki huo.
Mmoja wa wawakilishi wa Lions Club Wetteren Rozenstreek ya Ubelgiji akikabidhi hundi  kwa wana  Upendo Women's Group 
Mwakilishi wa Inne wheel wetteren akimkabidhi hundi mwenyekiti wa Upendo Women's Group Mrs Theresia Greca katika kuchangia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



KUMI WENGINE WAWA MAMILIONEA KATIKA DROO YA TATU YA PROMOSHENI YA TUSKER

0
0



 Ni wiki nne zimepita sasa na tayari washindi 20 wameshakabidhiwa vitita vyao kupitia promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti ijulikanayo kama Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini na kumi wengine kumi wametajwa leo katika droo ya tatu ya promosheni hiyo inayofanyika kila wiki. Wiki mbili zilizopita tulishuhudia washindi kumi kila wiki kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni hiyo inayoendelea. Katika droo ya tatu iliyochezeshwa leo, ambako washindi wengine kumi walitangazwa.

Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha na wakaguzi wa nje, walitangazwa washindi kumi ambao ni Julius Lucas, Damas Mathei, Dustan Mhina, Hussein Shaban kutoka Dar es Salaam, Teddy Tarimo kutoka Kilimanjaro, Mwahu Hamis - Arusha, Mary Steve na Marietha Thomas - Morogoro, Domino Juma Shinyanga pamoja na Edison Maxini kutoka Mwanza.

Mbali na washindi wa pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure papo hapo tangu promosheni ilipoanza. Mpaka sasa tayari takribani bia za bure zaidi ya 3000 zimeshagawiwa kwa watumiaji wa bia ya Tusker na zawadi nyingine kibao kama vile tshirt na kofia.

Akizungumza wakati wa droo hiyo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Maston alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ bado inaendelea na tayari washindi wa droo ya kwanza na ya pili wameshakabidhiwa vitita vyao. “Kwa kweli promosheni inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tanzania ambako sasa watumuaji wa Tusker wanaendelea kujitokeza kwa wingi kabisa kushiriki promosheni hii.

Hali hii inaendelea kutupa moyo na kuona kuwa wateja wetu wapo pamoja nasi kutupa sapoti. Leo tumeshuhudia wenyewe washindi kutoka karibu kanda zote nchi nzima Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro and Dar es Salaam. Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa promosheni bado inaendelea na bado tuna mamilioni kwa ajili yao, tunaamini kuwa ndani ya wiki saba zilizobakia tutapata washindi wengine wapya watakaoshiriki.”

Naye mmoja wa washindi Mary Steve kutoka Morogoro aliishukuru sana Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani ilikua kama miujiza kwake kupata kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hiki. “Nipata taarifa kuhusu promosheni hii kupitia maonesho ya barabarani nami kama mtumiaji mzuri wa Tusker nikaona nijaribu.

Sikutegemea kama naweza kuwa kati ya wale wenye bahati, nilikua na shida sana na pesa kwa ajili ya kuongeza mtaji katika biashara yangu sasa naona Tusker imeniokoa na kutatua tatizo langu, nimepata pesa ya kufanyia biashara zangu nawashukuru sana. Ntaendelea kushiriki mara nyingi maana huwezi jua nikawa mshindi tena kwa mara nyingine.” Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wake kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla.

Washindi wote waliotangazwa leo watakabidhiwa vitata vyao katika hafla fupi zitakazofanyika sehemu mbalimbali wiki ijayo.


Afisa Mwandamizi wa ukaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania ,Emmanuel Ndaki akihakiki taarifa za mmoja wa washindi waliotangazwa katika droo ya tatu,kushoto kwake ni meneja wa bia ya tusker Jasper Maston.Meneja wa bia ya tusker Jasper Maston akitoa maelezo kuhusu promosheni ya millioni mia moja na tusker fanya kweli uwini katika droo ya tatu iliyofanyika jijini dar es salaam mwishoni mwa wiki.
droo ikichezeshwa kupata washindi kumi wa tusker fanya kweli uwini. 

MFALME WA PORI .....

0
0


Mwenye nguvu mpishe...

1. Simba ndiye paka mkubwa kuliko wanyama wote wa jamii ya paka na simba wa afrika wamekuwa maarufu kwa jinsi ya umoja, upendo na mshikamano wao na huishi kwa pamoja kwenye kundi la misifa na kundi moja la simba wanakadiriwa kuwa kati ya simba 10-40 wakiongozwa na mfalme wao.
2. Simba dume ndiye mlinzi wa kambi iluhali majike ndio wasakanyaji wa chakula (wawindaji) licha ya hayo, simba dume ndio wa kwanza kula na kwa wastani madume yanakula sana kuliko majike
3. Simba ni mmoja wa wanyama walio katika orodha ya hatari ya kutoweka kabisa duniani kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhifadhi IUCN

4. Simba wa kwanza walipatikana Afrika (sio Kenya), asia na Ulaya lakini yasemakana kwa sasa simba walio katika mazingira Afrika wanapatikana Afrika tu (sio Kenya) kweingineko wanaishia kuwaangalia simba kwenye mizingo yao wanyama (ZOO).
5. Ngurumo za simba zinafika/sikika umbali wa kilomita nane na daima atembeapo visigino vyake havigusi ardhi.

6. Simba wana uwezo wa kukimbia umbali wa maili  50 kwa saa na kuruka futi hadi 36.
7. Simba hulala masaa 20 kwa siku na hasa anapokua ameshiba. Simba huishi kwa wastani wa miaka 10-14 mwituni, huku katika hifadhi huweza hata kufika zaidi ya miaka 20.
8. Simba mkubwa hula mara moja tu kwa wiki wastani wa kilo 20-35 za nyama kwa mlo mmoja kutegemeana.
9. Ingawa simba hujulikana kama mfalme wa pori, simba wengi huishi kwenye nyasi tu na hupenda sana nyasi kavu na ndefu (ellephant grassland), hata rangi ya simba huakisi rangi ya nyasi kama mbinu ya mawindo ila ikumbukwe tu kwamba ubabe wa simba una wapinzani pia kama Tembo (ingawa meno ya mbwa hayaumani)
10. Simba dume anafikia urefu wa mwili pamoja na kichwa wa sentimita 170 hadi 250; kimo cha mbegani ni 120 cm. Dume mkubwa anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 225. Jike ni mdogo wake akiwa na urefu wa 140 hadi 175 cm, kimo cha mbegani cha 100 cm na uzito wa 150 kg. Simba dume anatofautishwa kirahisi kutokana na manyoya marefu ya shingoni ilhali jike hana.

Ila yote hapo juu hayahusiani kabisa na 
Klabu ya Simba SC ya Tanzania tafadhali...

Compiled by Geofrey Chambua 


WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUPIGA VITA MATUKIO YA MAUAJI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania, viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kupiga vita matukio maovu ya mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema anatarajia hali ya amani, usalama na utulivu inaendelea kuwepo nchini, hivyo wananchi hawana budi kushirikiana na kushikamana na Serikali katika kuhakikisha matendo maovu hayatokei katika maeneo yao.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati  alipowasili mkoani Geita kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya kuwekwa wakfu Padre Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Mfano tukio la Mwanza watu wanavaa kanzu na wanaingia msikitini na kukuta wenzao wanafanya ibada kisha wakawachinja, hii haiwezekani kwa binadamu wa kawaida hivyo tushirikiane katika kupiga vita matendo haya,” alisisitiza.

Hivi karibuni jumla ya watu 15 waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika mikoa ya Mwanza,Tanga, Dar es Salaam  na Mara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga amesema vitendo vya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga vimepungua baada ya kuanzisha kampeni maalumu ya kukemea mauaji hayo.

Alisema katika kampeni hiyo wameamua kuwatumia walimu, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wauguzi ambao wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina na badala yake wajikite katika masuala ya maendeleo.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI MBALIMBALI WILAYA YA MBINGA VIJIJINI, RUVUMA

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauriya ya mji wa Mbinga, Oscar Yapesa (kushoto) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga vijijini, Venance Mwamenge mara baada ya kumaliza mbio zake katika mji wa Mbinga, jana.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, George Mbijima (kulia) akikabidhi Chandarua chenye dawa kwa mkazi wa kijiji cha Mbuji kata ya Mbuji wilayani Mbinga, Sailice Komba ikiwa ni mpango wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa wananchi wake. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga vijijini, Venance Mwamengo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, George Mbijima akiangalia ubora wa meza na madawati katika kijiji cha Mbuji wilayani Mbinga kabla ya kusambazwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani humo.
Mratibu wa Elimu katika kata ya Litura Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini mkoani Ruvuma, Nicodem Hyera akijaribu kuwasha moja kati ya pikipii zilizotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuwawezesha waratibu elimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ziweze kuwasaidia kufuatilia maendeleo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari wilayani Mbinga. Picha zote na Muhidin Amri

NSSF YAWAFIKIA MADEREVA WA BODABODA MKOANI DODOMA

0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya semina na kuzindua mpango wa kuwaandikisha maadereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma, Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA , Trafiki Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.

Pamoja na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama aliwapatia Vifaa vya Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo ni Kofia ya Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua mfumo wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea na Madereva wa Bodaboda (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa rasmi wa Kampeni ya Kuandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu kwa Madereva wa Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa kampeni rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.

VIONGOZI WA MFUKO WA MAENDELEO YA PAMBA WAUMBULIWA GEITA

0
0
MKUU wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Ibrahimu Marwa amesema viongozi wa Mfuko wa Wakfu wa maendeleo ya zao la pamba uliwapelekea wakulima pembejeo feki na kuwasababishia hasara.

Amesema hatua hiyo inatokana wafanyabiashara na viongozi wa mfuko huo kuwa na maslahi binafsi katika zao la pamba hivyo kushindwa kuwasaidia wakulima ipasavyo.

Marwa aliyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga alipokuwa akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa alipowasili Mkoani hapo.

Alisema mara baada ya wakulima kupelekewa pembejeo hizo na kubaini kuwa na kasoro walizipeleka katika Kiituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukirigulu kilichoko mkoani Mwanza ambacho nacho kilithibitisha kuwepo kwa kasoro.

Kwa upande wake Waziri Mkuu amewataka Maofisa Kilimo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuwasaidia wakulima wa pamba ili waweze kupata tija.

Ametaka Maofisa Kilimo na viongozi wa maeneo yanayolima pamba kujipanga upya baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka kwa kuanza mikakati ya kufanya utafiti wa mbegu bora za pamba na kuziandaa za kutosheleza wakulima wote.

Alisema hakuna sababu ya kuendelea kuwa na Maofisa Kilimo ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao kwa sababu mashamba ya wakulima yanashindwa kuendelea kwa kuwa hakuna mtu anayewafuatilia.

“Mwakani muanze kufanya utafiti kuanzia hatua za awali na kituo cha Ukirigulu kipewe kazi ya kusimamia zao hili na kiwe na shamba darasa kwa ajili ya kufundishia wakulima. Lengo ni kuhakikisha zao hili linakuwa na tija,” alisema.

Hata hivyo Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri za Wilaya zinazolima pamba zifanye utafiti ili kujua sababu zilizosababisha wakulima kupunguza ari ya kulima zao hilo.  

Pia amewataka waachane na mfumo wa kilimo cha mkataba kwa sababu hauna tija kwa mkulima kwani hautengenezi ushindani na badala yake wajifunze mfumo unaotumika katika uuzaji wa zao la korosho.

MAREKANI YAICHAPA PARAGUAY 1-0 NA KUONGOZA KUNDI LAO, COLOMBIA YALALA 3-2 KWA COSTA RICA

0
0
Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Marekani imefanikiwa kuongoza kundi A mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Ikicheza mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wake kwenye uwanja wa Lincoin Financial Field jijini Philadelphia, Marekani ilionyesha kiwango kizuri cha uchezaji na kunako dakika ya 27 Clint Dempsey aliifungia Marekani bao hilo pekee katika mtanange huo.

Ingawa Marekani walicheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa muda mrefu wa mchezo, kwani dakika ya 36 beki wa kulia wa Marekani Yedlin alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, bado Marekani waliweza kulilinda lango lao na kushambulia kwa kushitukiza. Hadi mwisho Marekani 1, Paraguay 0.

Kwa kuongoza kundi kuna uwezekano mkubwa kuwa Marekani akawa amekwepa kukutana na Brazil katika hatua ya mtoano.
Kwenye mchezo kati ya Colombia na Costa Rica, kocha Jose Pekerman wa Colombia aliwapanga nyota wake kama wachezaji wa akiba kitu ambacho alikijutia baadaye, baada ya timu yake kupata kichapo cha mabao 3-2 toka kwa Cost Rica. 

Kituko au kivutio kwenye mchezo huu ilikuwa kwa mchezaji wa Colombia Frank Fabra, yeye alifunga mabao mawili, moja kwa kila timu yaani aliifungia timu yake dakika ya 7 na akaifungia timu pinzani (Costa Rica) dakika ya 34.

Mabao mengine ya Costa Rica yalifungwa na Johan Venegas dakika ya 2 na Celso Borges dakika ya 58. Na lingine la Colombia lilifungwa na Marlos Moreno.

Leo tutawashuhudia
HAITI vs EQUADOR
BRAZIL vs PERU

MSHIKE MSHIKE KOMBE LA ULAYA 2016: SWITZERLAND YAICHAPA 1-0 ALBANIA, SLOVAKIA YALALA 2-1 KWA WALES NA ENGLAND YABANWA MBAVU NA RUSSIA

0
0
Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Michuano ya Euro 2016 imeendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa katika miji tofauti.

Kwenye dimba la Stade Bollaert-Delelis jijini Lens, Albania ikicheza na wachezaji kumi kwa muda mrefu wa mchezo ilichapwa bao 1-0 na Switzerland. Bao hilo pekee na la ushindi lilifungwa na Fabian Schar dakika ya 5 tu, kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Xherdan Shaqiri, ambapo kipa wa Albania Etrit Berisha akipiga ngumi hewa kutaka kupangua mpira huo.

Kunako dakika ya 36 mwamuzi wa mechi hiyo Carlos Velasco Carballo wa Hispania alimwonesha kadi nyekundu nahodha wa Albania Lorik Cana baada ya kumpa kadi mbili za njano kwa kosa la kuushika mpira makusudi akimzuia Haris Seferovic asiende kufunga.
Katika dimba la Stade de Bordeaux, Gareth Bale mchezaji anayesukuma kandanda katika klabu ya Real Madrid aliiongoza Wales kuishinda timu ya Slovakia kwa mabao 2-1. Wales ambayo inacheza mashindano makubwa kwa mara ya kwanza tangia mwaka 1958 kwenye mashindano ya kombe la dunia, imerejea sasa na kucheza kabumbu safi.

Gareth Bale katika dakika ya 10 alipiga kwa ufundi mpira wa adhabu ndogo ambao ulikwenda moja kwa moja kimiani na kuiandikia Wales goli la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kunako dakika ya 61 kipindi hiki cha pili Slovakia walirejesha goli hilo kupitia kwa mchezaji Odren Duda.Lakini dakika ya 81 Wales walijihakikishia pointi tatu muhimu kwa kujipatia goli la pili lililofungwa na Hal Robson-Kanu.Hadi mwamuzi Sevein Oddvar Moen wa Norway anapuliza kipenga cha mwisho Wales 2,Slovakia 1.

Mchezo wa mwisho kwa usiku huo ambao ulikuwa unasubiriwa na wengi ni kati ya Uingereza na Urusi uliopigwa kwenye uwanja wa Stade Velodrome jijini Marseille.Kutokana na watu wengi kuifuatilia ligi kuu ya Uingereza basi wana hamu ya kuiona timu hiyo taifa inafanya nini kwenye michuano hii.

Mtanange huo ulikuwa mkali na wa kuvutia ni Uingereza ndiyo walifanikiwa kufika mara nyingi langoni mwa Urusi lakini washambuliaji wao wakiongozwa na nahodha Wayne Rooney, Adam Lallana, Harry Kane na wengineo hakuwa makini na kukosa nafasi nyingi za kujipatia mabao. Hivyo hadi mapumziko timu zote zikawa suluhu 0-0.

Kipindi cha pili kkunako dakika ya 56 'free kick' nzuri iliyopigwa na Eric Dier inazama nyavuni mwa Urusi na kuipatia Uingereza bao la utangulizi. Urusi nao hawakukata tamaa na juhudi zao zilizaa matunda kunako dakika ya 90 pale mabeki wa Uingereza Gary Cahill na Chris Smalling waliposhindwa kumzuia V.Berezutski kupiga kichwa mpira ulioenda moja kwa moja wavuni.

Leo ni vita kati ya
UTURUKI vs CROATIA......Uwanja: Parc de Prince
POLANDI vs IRELAND KASKAZINI....Stade de Nice
GERMANY vs UKRAINE......Stade Pierre Mauroy

YANGA WAAMUA, MANJI NA CLEMENT SANGA WACHUKUA NAFASI ZAO KWA KISHINDO KIKUU

0
0

Na Sultani Kipingo
Mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu Dar es salaam Young Africans Football Club maarufu kama  Yanga  ulifanyika kwa utulivu na amani na kumalizika salama jana Jumamosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam na matokeo kamili ni  kama ifuatavyo:
Mwenyekiti Yusuph Manji (pichani juu) alitangazwa mshindi rasmi wa kiti hicho kwa mara ingine tena baada  kuzoa kura zote za ndio isipokuwa mbili tu. Yaani alipata  kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika. Hakukuwa na kura ya hapana. Manji hakuwa na mpizani kwenye nafasi hiyo.
Makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye naye pia alikuwa akigombea  nafasi hiyo kwa mara ingine kwa kupambana  na Titus Osoro, aliibuka mshindi  kwa  kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa. Mpinzani wake aliambulia kura 80 tu.
Nafasi za 20 za ujumbe ambazo wagombea waliibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni:
1. Siza Augustino Lymo (1027)
2. Omary Said Amir (1069)
3. Tobias Lingalangala (889)
4. Salim Mkemi (894)
5. Ayoub Nyenzi (889)
6. Samuel Lucumay (818)
7. Hashim Abdallah (727)
8. Hussein Nyika (770)
Idadi ya wajumbe 12 ambao walishindwa kuibuka na ushindi baada ya kura kutotosha ni: 
1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima "Jembe Ulaya" (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)
12. Silvester Haule (197)


VOA:Mchango wa Muhamed Ali katika uislamu

Tukio la shambulizi katika klabu Orlando

SIMU TV: habari kutoka televisheni

0
0

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Ahamad Masauni amelitaka jeshi la polisi nchini kuongeza bidii katika kutokomeza uhalifu; https://youtu.be/8aLYyB9IPoM

Walimu wa shule za sekondari nchini wametakiwa kuwa na desturi ya kuongeza kiwango cha ufaulu mashuleni kwa kuweka mikakati imara katika mbinu za ufundishaji;https://youtu.be/y1URcnViN4g

Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais anayeshughulikia mazingira Ruhaga Mpina amewataka wahitimu wa elimu ya juu kujikita katika fursa za kilimo cha miti;https://youtu.be/NWK56UssGig

Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi na mawasiliano Eng. Joseph Nyamhanga amewataka makandarasi wanaojenga barabara mikoani kukamilisha kwa haraka miradi hiyo;https://youtu.be/mrds0EOPFz4

Mazungumzo maalumu juu ya umuhimu wa teknolojia katika kurahisisha mambo hususani katika sekta ya elimu kwa wanafunzi; https://youtu.be/hL-nCmdbA3k

VODACOM WAVUTIA MAMIA YA WANANCHI KATIKA GULIO LA SIMU KIJITONYAMA, JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Afisa wa Vodacom huduma kwa wateja, Jesca Mnosi, akitoa maelezo ya simu halisi na zisizo halisi kwa wananchi waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonyesho ya simu yaliyoanza jana Juni 11, 2016 kwenye viwa nja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa simu wa Vodacom,Gabriel Mvamba, (kulia), akimpatia maelezo ya kitaalamu ya kutofautisha simu halisi na simu isiyo halisi, mteja wa kampuni hiyo alipotembelea banda la Vodacom kwenye maonyesho ya simu orijino kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2016.
Wananchi wakipatiwa maelezo juu ya tofauti ya simu halisi (Original) na simu zisizo halisi (Fake), kutoka kwa maafisa wa kampuni ya simu ya Vodacom wakati wa maonyesho ya simu kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Juni 11, 2016. Maonyesho hayo yanakuja huku zikiwa zimebaki siku 5 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuzifungia simu zote zosizo halisi.

NEWZ ALERT:OLE MEDEYE ATIMKA CHADEMA NA KUHAMIA UDP LEO

0
0
Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.

Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.
 Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt.Goodluck Ole Medeye, akionesha kadi yake ya uanachama mbele ya Waandishir wa habari (hawapo pichani),kuashiria kuwa sasa ni mwanachama halali wa chama hicho cha United Democratic Party UDP,shoto ni Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
  Dkt.Goodluck Ole Medeye, akikabidhiwa kadi ya uanachama mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) na Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United Democratic Party UDP.

Bw. Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John Momose Cheyo.

Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.

Kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao wamelaani uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya Bunge, na kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao kurejea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili utaratibu wa kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live




Latest Images