Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1252 | 1253 | (Page 1254) | 1255 | 1256 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairukiakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo hufanyika Juni 16 -23 kila mwaka.

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa kuondoa watumishi hewa katika mfumo malipo ya mishahara ya serikali.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki  jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana  mara baada ya kuanza kwa kutafuta watumishi hewa wa serikali.

  Amesema kuwa watumishi ambao wameshaondolewa tangu Machi, 1 hadi Mai 30 ni watumishi 12,246 ameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya Serikali kwa sababu mbalimbali ikimo kutimiza umri wa Kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kuhitimishwa kwa mikataba.

  Aidha amesema kuwa wasingeondolewa kwenye mfumo wa mishara kwa wafanyakazi wa serikali zaidi ya shilini Bilioni 25 zingepotea.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Hainan International Limited anayejenga Daraja la mto Sibiti ambalo linaunganisha mkoa wa Singida na Simiyu kuendelea na ujenzi  wake.
  Amesema hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi  wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa daraja hilo litakamilika katika kipindi cha hivi karibuni baada ya Serikali kuanza kumlipa mkandarasi huyo.
  "Tumeanza kumlipa mkandarasi fedha hivyo tunawahakikishia kwamba katika kipindi kifupi kijacho litakamilika ili kufungua shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Wilaya ya Mkalama na Meatu" , amesema Prof. Mbarawa.
  Aidha  Waziri huyo wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kutoza ushuru katika mto huo na kusisitiza kwamba tabia hiyo iachwe mara moja na atakayefanya hivyo anakiuka sheria na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
  "Wananchi wanatakiwa kupita hapa bila ya kulipa gharama yoyote katika mto huu, nimemuagiza Mkuu wa Wilaya na Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida waboreshe eneo la kuvukia ili wakati ujenzi unaendelea huduma za kuvuka ziendelee kama kawaida", amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo amemhakikishia waziri kuwa ujenzi wa Daraja la mto sibiti pia utahusisha barabara ya maingilio yenye urefu wa kilomita 25 inayounganisha wilaya ya Mkalama na Meatu.
  "Ujenzi wa barabara za maingilio unahusisha makalvati makubwa 10 na madogo 55 ili kuruhusu maji kupita kwa kasi na hivyo kudhibiti mafuriko", amefafanua Eng. Kapongo.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw. Christopher Ngubiagai amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa jitihada zake za kutaka kuunganisha wilaya yake na Meatu kwani kukamilika kwa daraja hilo kutaimarisha fursa za usafirishaji wa mazao na huduma za usafiri katika Wilaya hizo.
  Zaidi ya shilingi bilioni 18.2 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Daraja la mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 na upana wa mita 10.5 ambapo tayari Serikali imeshalipa zaidi ya shilingi bilioni 4 mpaka sasa.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa kwanza kushoto) kuhusu usimamizi wa ujenzi wa Daraja la mto Sibiti.
   Muonekano wa juu wa Daraja la Msingi lenye urefu wa mita 75 linalounganisha Wilaya ya Mkalama na Iramba, lililopo mkoani Singida.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw. Christopher Ngubiagai (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) alipokagua ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akikagua jengo la nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) mkoani Singida.
  Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa nyumba za viongozi wa Wilaya ya Mkalama na jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwataka makandarasi wanaoendelea na  ujenzi wa miradi hiyo kuongeza kasi na  kutumia fedha wanazopata kujenga jengo moja moja kwa awamu ili kupunguza changamoto ya  makazi na ofisi Wilayani humo badala ya utaratibu wa sasa wa kujenga majengo yote kwa pamoja.
  ."Msisubiri  mpate fedha zote  kwa nyumba zote, kamilisheni ujenzi wa nyumba moja moja kadri mnavyopata fedha ili kupunguza changamoto za makazi na ofisi", amesisitiza Prof. Mbarawa.
  Prof. Mbarawa yuko katika siku ya pili ya ziara yake ya siku nne mkoani Singida ya kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, nyumba na  Mawasiliano.
  Muonekano wa moja ya nguzo inayoshikilia Daraja la Mto Sibiti linalounganisha Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na Meatu mkoani Simiyu.Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Na Geofrey Tengeneza
  Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TTB iliyoteuliwa hivi karibuni imekutana leo katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam katika mkutano wake wa kwanza toka iingie madarakani.
  Mkutano huo ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya wajumbe wa Bodi hiyo kufahamu zaidi kazi na majukumu ya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) ulifanyika chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na kuhudhuriwa pia na Menejimenti ya TTB.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi alitumia pia mkutano huo kuwatambulisha wajumbe wa Menejimenti ya TTB kwa Mwenyekiti na Wakurugenzi hao wa Bodi. Bodi ya wakurugenzi iliyoteuliwa mwezi Mei mwaka huu ina wajumbe sita ambao ni Bw. Ibrahimu Mussa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA; Balozi Joseiph Sokoine , Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda; Bw. Mark Leveri, Mtaalamu wa filamu na matangazo.
  Wengine ni  Bw. Richard Rugimbana, Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bibi Zubein Muhaji Mhita, Bibi Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi  Msataafu na Bw. Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya fedha na Mipango. Mjumbe mwingine ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
  Mwenyekiti na Wajumbe hao wa Bodi ya Wakurungenzi wa TTB  watakuwa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019 .

   Bodi ya Wakurugenzi wa TTB. Kutoka kushoto ni Bw. Agustine Kungu H. Olal, Bw. Mark Leveri, Bibi Zubein Mahita, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Mwenyekiti), Bi Devota Mdachi (Katibu), Bw. Ibrahimu Mussa na Balozi Josiph Sokine 
   Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TTB.
  Mkuu wa Kitengo cha IT cha TTB bw. Rossan Mduma (wa kwanza kulia) akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi namna tovuti maalumu ya TTB (Portal) inavyofanyakazi na inavyoweza kutumiwa na wadau mbalimbali wa Utalii.
   Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB katika kikao na Menejimenti ya TTB.


  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo.
   wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa.
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  0 0

  Na Geofrey Chambua
  #1.TEMBO unayemjua wewe kwa wastani ana uzito wa kilogramu elfu kumi kwenda mbele (Hapa namuongelea tembo mkubwa)  Tembo pamoja na ukubwa wake akitembea hana kishindo kabisa miguu yake kwa chini ni kama ina sponge hivi.

  #2. Wakati mwanamke anabeba ujauzito kwa kipindi cha miezi tisa, TEMBO mkubwa wa kike anabeba ujauzito kwa jumla ya miaka miwili yaani miezi ishirini na minne kabla hajazaa.
  #3. Ukimwondoa mwanadamu ambaye ana KIDEVU, Tembo ndiye mnyama mwinginbe  ambaye pia anacho kidevu…..
  #4. Tembo anao uwezo wa kumsikia Tembo mwenzake akilia kutoka umbali wa kilometa tano….Tembo hana uwezo mkubwa wa kutambua vitu kwa kuona. hutegemea zaidi pua na masikio kuweza kufanikisha shughuli zake. kutokana na hali hiyo, mara nyingi ukiwa porini unashauriwa kumpiga picha tembo BILA ya kutumia flash. hii inatoka na kwamba, endapo utatumia flash wakati unampiga picha, tembo atajenga hisia ya kutoelewa nini kimetokea. kwa kifupi hataweza kutofautisha kama ni kitu cha kawaida au ni hatari. katika mazingira haya, huanza ku-charge kuelekea upande ule ambao mwanga
   #5. Ni Tembo wa Afrika pekee mwenye uwezo wa kutofautisha kabila, jinsia na umri wa mwanadamu. Ikiwa jana alijeruhiwa na mtu anayezungumza kiingereza, akisikia kiingereza anakumbuka upesi…
  #6. Takribani Tembo mia moja huuwawa kila siku kwa sababu ya pembe zao….
  #7. Kila mnyama kuna kitu anakiogopa sana, lakini ni ajabu sana kwa Tembo ambaye anamuogopa nyuki kuliko kitu chochote.
  #8. Tembo mkubwa na mzito kupita wote anapatikana Afrika…
  #9. Ikiwa mwanadamu hulala walau masaa nane kwa siku, kwa Tembo ni tofauti… Tembo hulala masaa mawili hadi matatu kwa siku!!
  #10. Kuhusiana na mambo ya kula na kunywa… Tembo mkubwa huitaji walau kilo mia tatu za chakula na maji lita 160 kwa siku!!! Kama unahitaji kumfuga ujiandae……
  11. Tembo anategemea sana uwezo wake wa kunusa ili kuweza kutambua mazingira aliyopo na vitu vinavyomzunguka. Sambamba na harufu, tembo pia ana uwezo mkubwa wa kusikia kupitia masikio yake makubwa (by the way, tembo porini huitwa Masikio).
  12 Tembo ana fanya mapenzi kwa masaa 12; masaa 6 ya mwanzo anamuandaa mwenzi wake na 6yanayobaki ndio shughuli yenyewe na hiyo ni ile raundi ya kwanza.
  13 Tembo dume huwa na wanawake wawili mpaka wanne
  14. Akipiga bao tembo dume manii zake ni ujazo wa lita tano

  0 0

  Kikosi cha timu ya Yanga.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KUNDI la kwanza la wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kuondoka usiku wa leo kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalumu ya kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo bejala ya Nchini Algeria utakaopigwa kati ya Juni 17,18,19. Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Yanga kukosa ndege ya pamoja na kuamua kiwasafirisha wachezaji wake kwa makundi mawili huku wengine wakitarajiwa kuondoka kesho sa 10 jioni.

  Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Jerry Muro amesema kuwa wachezaji watakaosafiri jumla ni 21 ikijumuishwa na benchi la ufundi saba pia wataongozana na mjumbe wa kamati ya utendaji mmoja kwani timu inakwenda kwa ajili ya kujiandaa na hawatataka wapate usumbufu wa aina yoyote ndiyo maana wameonelea benchi la ufundi lifanye kazi yake kwa ufasaha. Uamuzi huo umekuja zaidi kwa ajili ya kubana matumizi ila viongozi wengine wataondoka Juni 15 kuanzia hapa kuelekea nchink Algeria kwa ajili ya kuungana na wachezaji.

  "Wachezaji wataondoka kwa awamu mbili, leo saa nane usiku na wengine kesho saa kumi jioni ila wataongozana na kiongozi mmoja wa kamati ya utendaji pamoja na saba kutoka benchi la ufundi, "amesema Muro. Hata hivyo kikosi kitakaa kwa muda hadi Juni 15, ambapo wataanza safari ya kwenda nchini Algeria ila mpaka leo bado hawajajua mechi itakuwa lini kati ya tarehe zilizokuwa zimepangwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF ila hata kama ikiwa Juni 17, kikosi kitakuwa kamili kuvaana nao.

  Yanga itawakosa Juma Abdul ambaye ni majeruhi na Nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' anayetumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wao wa hatua ya 16 bora dhidi ya Segrada Esperanca ya nchini Angola ambayo itamuweka nje kwa mchezo mmoja.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kwenye vitabu ambavyo ni muongozo wa kazi kwa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.Katika hotuba yake, Waziri Ummy ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwekeza katika viwanda vya dawa hasa kwa zile dawa za msingi, kwani utaboresha sana upatikanaji wa huduma, utapunguza malalamiko kwa wanachama wake, utaongeza ajira na pia kupunguza matumizi ya fedha chache za kigeni kwa ajili ya kununulia dawa hizo nje ya nchi.
   
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda, akitoa shukrani zake baada ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, wakiwa tayari kwa kazi hiyo ya uchaguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
   Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji akiandikishwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
  Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kupigia kura, katika unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
   Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga, Hans van Pluijm nae ni Mmoja wa Wanachama wa Yanga wanaopiga kura leo kuchagua uongozi mpya wa Klabu hiyo.
  Wanachama wakipiga kura.

  0 0

   
    Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Shambwe akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Daudi Ntibenda wakipiga makofi kuashiria furaha ya ukaribisho wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Safaricity Matevez Arusha leo.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Misonge Shambwe akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Daudi Ntibenda na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa #SafariCity
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kushoto Ndugu David Shambwe akizungumza na wananchi pamoja na wafanya Biashara wa Jiji la Arusha wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa #SafariCity Mh Felix Daudi Ntibenda akipanda mti pamoja na Mstahiku Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa mji wa #SafariCity.

  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Pinda akimsikiliza Kelvin Agustino mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke alipokuwa akisoma kitabu cha Kiingereza wakati alipoitembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
    Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Pinda akiongea na wanafunzi  wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipoitembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
   Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Pinda akiwauliza maswali wanafunzi wa shule ya awali wa shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipotembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
   Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Pinda akimsikiliza Glorius Nkinda ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza  katika shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati akijibu swali la Hesabu alilomuuliza. Mhe. Pinda alitembelea shule hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kuwasalimia  wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Pinda akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa darasa la tatu wakati alipoitembelea  shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Katavi iliyopo Mikwambe, Kigamboni Wilayani Temeke wakati alipotembelea shule hiyo hivi karibuni ili kuwasalimia wanafunzi na kujionea maendeleo ya shule hiyo.  0 0

   Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa (kushoto) akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema  katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake jijini Dares salaam Juni 10, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi (kushoto) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Siro katika futari  aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamanda  wa Kanda Maalum  ya  Dar es salaam , Simon Siro  katika futari aliyoiandaa kwenye Makazi yake  jijini  Dar es salaam Juni 10, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Wazazi Tanzania , Abdallah Buelembo katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake  jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  MAJALIWA: UHABA WA SUKARI KUMALIZIKA NCHINI.  
                         WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia  Watanzania kwamba  Serikali inaendelea na jitihada za kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambapo jumla ya tani 20,000 zilisambazwa jana katika maeneo mbalimbali nchini.
  Amesema shehena nyingine ya tani 35,000  inatarajiwa kusambazwa hivi karibuni katika kanda zote nchini hivyo amewataka wafanyabiashara watakapoipokea kuiuza kwa wananchi bila ya kuificha na bei isizidi shilingi 2,200.
  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana jioni ( Ijumaa, Juni 10, 2016) wakati akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Dar es Salaam alipowaalika katika futari aliyoiandaa nyumbani kwake.
  Amesema tayari viwanda vimeanza kufunguliwa na tani 300 zilizotoka katika kiwanda cha Sukari cha Kagera  zitasambazwa katika wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu, Uvinza na Kigoma ili kutosheleza maeneo hayo.

  Hata hivyo amewataka Maofisa Biashara katika Halmashauri zote nchini kuendelea kufanya ufuatiliaji katika maduka ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana na hakuna mfanyabiashara atakayeificha.
  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara kote nchini  kutopandisha bei za vyakula katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
  Akizungumza kuhusu tabia za baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa hasa vyakula katika kipindi hiki cha mfungo amewataka kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa sababu kitendo hicho kinawapa wafungaji wakati mgumu.
   “Kufunga Ramadhani si jambo la anasa, si matashi binafsi bali ni jambo  la kiimani hivyo tusipandishe bei ya bidhaa kwa lengo la kuwaadhibu Waislam kwa sababu tu wamefunga.
   “Katika Quran surat  Baqarah aya ya 183 inasema kwamba enyi mlioamin imefaradhishwa kwenu kufunga kama walivyoamrishwa kufunga kwa waliopita kabla  yenu ili muwe wachamungu, hivyo hatuna budi kufunga” alisisitiza.
  Alisema tabia hiyo si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo kwa wafanyabiashara kuamua kupandisha bei hivyo aliwataka waiache kwani Serikali haitawavumilia na atakayethubutu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

  0 0

  Ni mwaka mmoja bila wewe katika maisha yetu ya kila siku ,tunakukumbuka daima.
  UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku,hatuna la kusema,umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako.
  Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU kwa muda wote uliokuwa nasi.
  Daima tutaendelea kukukumbuka hekima na busara zako huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe.
  Daima unakumbukwa na Mumeo Julius,mwanao John,Mama yako,wifi zako,shemeji zako,Dada na kaka zako,Maraafiki,majirani wa Bahari Beach na Ubungo Kibangu na watu wote waliokufahamu ktk uhai wako.
  Misa ya kumuombea Marehemu itafnyika ktk kanisa la Mt. Andrea liliopo Bahari Bech – DSM tarehe                                                                                        12/06/2016.
                                                                         Wote mnakaribishwa.

  0 0
  0 0

  Bendi ya Poli ikiongoza matembezi  ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Zaidi ya shilingi263 milioni zilichangwa.
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu ha viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Zaidi ya shilingi milioni 262 zilichangwa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuongoza  matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016. Zaidi ya shilingi milioni 263 zilichangwa. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wasanii wa Benki Kuu baada ya kuongoza matembezi  kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.  Zaidi ya shilingi milioni263 zilichangwa.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Hussein Makame-MAELEZO
  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na wafanyakazi wake wa matawi yote nchini kwa kushirikana na baadhi ya Taasisi za kifedha na kampuni za simu nchini, imetoa Shilingi Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki hiyo.
  Fedha hizo zilikabidhiwa leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya matembezi ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati, yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora wa elimu kupitia upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.
  “Tunatambua kwamba changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini mchango wetu utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi ya watoto wetu ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema Gavana Prof. Ndulu
  Akifafanua mchango huo, Gavana Prof. Ndulu alisema kati ya fedha hizo, BOT imetoa Shilingi Milioni 167, Wafanyakazi Milioni 29.8, Taasisi za Kifedha Milioni 22 na kampuni za simu Milioni 54.3 na kwamba madawati hayo yatasambazwa kwenye shule zenye upungufu au ukosefu wa madawati za Dar es Salaam na zilizoko mikoa ambayo Benki hiyo ina matawi yake.
  Alitaja mikoa hiyo na fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya mikoa hiyo kuwa ni Makao Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24), Chuo cha Benki Mwanza (680,000) Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186), Mtwara (850,000) na Dodoma (Milioni 1.18).
  Alisema taasisi zilizochangia fedha hizo ni Benki ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib (Milioni 5), Benki ya Exim (Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni 2), Tanzania Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2) na NIC Bank aliyotoa Milioni 1.
  Kwa upande wa kampuni za simu zilizotoa fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani 10,000, kampuni ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa Dola za Kimarekani 5,000.
  Akizungumza baada ya kupokea hundi ya mfano, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike kama zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo achukuliwe hatua mara moja.
  Katika kuthamini sekta ya elimu nchini, Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili kwa wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu hapa nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu na TEHAMA.
  “Lengo kubwa la mfuko huu ni kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati yakiwemo masomo kuhusu gesi na mafuta.Katika idadi hiyo, 16 ni wanafunzi wa kike na waliobaki 8 ni wanaume” alisema Gavana Prof. Ndulu.
  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilianza kutoa huduma kwa wananchi mnamo tarehe 14 Juni mwaka 1966 na Juni 14 mwaka huu inatimiza Miaka 50 na katika kuadhimisha miaka hiyo wafanyakaz wa matawi yote nchini wanafanya matembezi hayo ili kutoa mchango kwa jamii.

  0 0
  0 0


  0 0

  Matokeo ya Awali ya ya Uchaguzi Mkuu wa Yanga, Mpaka sasa kwa nafasi ya wa Yanga 

  Kura za
   NDIO :   1468 
  HAPANA:   0 
  HARIBIKA:  2

  Matokeo ya Awali ya makamu mwenyekiti
  Sanga kura za NDIO 1428
  Ossoro  kura kura NDIO 80

  Matokeo Rasmi ya uchaguzi Wote yatatangazwa kesho

  0 0


   Dkt. Charles Tizeba
  Mhe. Mwigulu Nchemba.

  0 0older | 1 | .... | 1252 | 1253 | (Page 1254) | 1255 | 1256 | .... | 3286 | newer