Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1251 | 1252 | (Page 1253) | 1254 | 1255 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundation wamekabidhi mifuko 600 ya saruji kwa Shule ya Msingi Mbande iliyopo kata ya Chamazi ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu kwa kukabiliana na changamoto za Uwepo wa madarasa uliokuwa unaikabiri shule hiyo kwa muda mrefu.

  Licha ya kukabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji Mkuu wa wilaya Mjema ameahidi kufanya jitihada za kutafuta madawati 400 kukabiliana na changamoto za wanafunzi. kukaa chini huku akiongeza kuwa atalishughulikia ipasavyo suala là Uhaba wa walimu kwa shule hiyo kwa kuongeza walimu 40.

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Dauden Mwakyambiku amesema msaada huo unatija kwao kwani tangu kuanza kwa sera ya elimu bure kumekuwa na changamoto ya ongezeko la wanafunzi ambalo linahitaji madarasa, ambapo shule hiyo inawanafunzi 5,815 huku vyumba vya madarasa vikiwa 16 na serikali imeagiza kila chumba kukaa wanafunzi 45.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wanne kulia) na Meneja Mkuu wa GSM Foundation Shannon Kiwamba (katikati) pamoja na wadau wengine, wakikabidhi mifuko hiyo 600 ya Saruji kwa uongozi wa Shule ya Msingi Mbande leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema akiwa pamoja na uongozi wa Taasisi ya GSM Foundation wakiwa kwenye stoo ilipohifadhiwa saruji hiyo.
  Sehemu ya wazazi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema.

  0 0

   ISO 9001:2008 CERTIFIED

  Walipakodi wote wanakumbushwa kuzingatia mwisho wa kulipa kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) PASIPO ADHABU

  1.OULIPAJI WA KODI YA MAPATO – MAKADIRIO YA AWALI

  walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/06/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya nne ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
  walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/09/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya tatu ya makadirio ya awali ya mwaka 2016
  walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 30/12/2016, wanapaswa kulipa sehemu ya pili
  walipakodi wote ambao hesabu zao za mizania zinaishia tarehe 31/03/2017, wanapaswa kulipa sehemu ya kwanza ya makadirio ya awali ya mwaka 2017
  Tarehe za malipo kwa ufupi:
  Tarehe ya mwisho wa mwaka wa MahesabuAwamu za MalipoTarehe ya Mwisho wa Malipo bila Adhabu
  30/06/2016Awamu ya nne ya mwaka wa Mapato 201630/06/2016
  30/09/2016Awamu ya tatu ya mwaka wa Mapato 201630/06/2016
  31/12/2016Awamu ya piliya mwaka wa Mapato 201630/06/2016
  31/03/2017Awamu ya kwanza ya mwaka wa Mapato 201730/06/2016

  2.0UWASILISHAJI WA RITANI ZA MAPATO KWA MWAKA 2016
  Walipakodi wote ambao mwaka wao wa mapato uliisha tarehe 31/12/2015, wanatakiwa kuwasilisha ritani zao pamoja na hesabu zilizokaguliwa na kulipa kodi yote inayotakiwa mnamo au kabla ya tarehe 30/06/2016

  3.0UWASILISHAJI WA RITANI ZA VAT ZA MWEZI MEI 2016
  Walipakodi wote ambao wamesajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanatakiwa kuwasilisha ritani za mwezi mei 2016 na kulipa kodi inayotakiwa kabla ya tarehe 30/06/2016. Pia wale wote ambao hawakufanya biashara wanatakiwa kuwasilisha ritani zao zisizokuwa na malipo (NIL RETURN)

  4.0UTOAJI WA RISITI ZA KODI ZA KIELEKITRONIKI/ ANKARA YA KODI 
  Walipakodi wote waliosajiliwa na wasiosajiliwa kwenye kodi ya Ongezeko la Thamani wanakumbushwa Kutoa risiti za kodi za kielekitroniki/Ankara ya kodi kwa mauzo yote wanayofanya kulingana na fedha zilizopokelewa. Ni kinyume cha sheria kupokea malipo kwa kuuza Bidhaa au huduma bila Kutoa risiti ya kodi ya kielekitroniki/Ankara ya kodi

  5.0KUMBUKA
  Riba na Adhabu itatozwa/itatolewa kwa Pointi ya Sarafu (Currency Points) kwa mlipakodi yeyote ambaye hatalipa kodi kwa muda unaotakiwa au atakayeshindwa kuwasilisha ritani kwa muda unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

  Ili kuepuka  msongamano na usumbufu mwingine walipakodi wanashauriwa kutosubiri siku ya Mwisho. Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri.

  “Pamoja Tunajenga taifa letu”

  Imetolewa na:
  Idara ya Huduma na Elimu kwa mlipakodi
  TRA Makao Makuu
  S.L.P 11491
  Dar es Salaam.
      Barua pepe: huduma@tra.go.tz
  Kituo cha Huduma
  Simu bila Malipo
  0800 780078
  0800 750075  0 0

  Na Jonas Kamaleki, MAELEZO, Dodoma
  10/6/2016
  KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni  imemuunga mkono Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo katika miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli.
  Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya  maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17.
  “Tunamuunga mkono Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuondoa posho za vikao (Sitting Allowances) na tunamwomba aondoe posho hizo kwa wabunge nao watumie mishahara yao ili kuwe na usawa,” alisema Silinde.
  Silinde alisema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inaunga mkono juhudi za Mhe Rais Magufuli za kukusanya kodi ambayo inabidi ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.
  “Tunaungana na Serikali kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais apanue wigo wa kodi hiyo hadi kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya,” alisema Silinde.
  Kwa upande wake, mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR-Mageuzi), Mhe. James Mbatia amesema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inamuomba Mhe. Rais Magufuli kufuta posho za vikao kwa wabunge haraka ili kuleta usawa kwa watanzania wote.

   Mbunge wa Momba (CHADEMA), Mhe. David Silinde akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Katikati ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali.
  Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi),  Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Kushoto ni Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Mhe. Riziki Mngwali. PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
  Mkutano wa nganzi ya juu  kuhusu  ukimwi jana  ( alhamis) uliingia katika  siku yake ya pili ambapo viongozi mbalimbali wakiwamo  Mawaziri na  Naibu waziri  wanaohusika na masuala ya afya wameendelea kuelezea nini ambacho  nchi zao zinatekeleza  katika kukabili na kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vinavyo sababisha ukimwi  pamoja na  huduma   wanazopatiwa  watu ambao wamekwisha kuathirika na kuugua.
   Mmoja ya  nchi ambayo iliwasilisha   mafanikio,  changamoto na mwelekeo  wa baadaye katika kukabiliana na  janga  la ugonjwa wa ukimwi,  ugonjwa ambao  jumuiya ya kimataifa umejiweka lengo la  kuutokomeza ifikapo mwaka 2030 ili  kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Juhudi za Tanzania dhidi ya Ukimwi,   zilielezwa  na    Naibu Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto Mhe. Dr. Hamis A Kigwangalla (Mb). Ambaye  katika  maelelezo yake, amesema,  Tanzania inaamini   kuwa   inawezekana  kufikia hali ya  kutokuwa na  maambukizi mapya, kumaliza  ubaguzi na  unyanyapaa, na kuwa na kiwago sifuri   cha vifo   vinavyohusiana na  ukimwi fikapo mwaka 2030.
  Hata hivyo anasema,  ili kufikia  hatua  hiyo au mafanikio hayo,  mambo   kadhaa yanapashwa kufanyika,  yakiwamo ya  uimarishwaji wa elimu ya kinga,  vijana na   jumuiya kwa ujumla kufundishwa mbinu  za kuepukana na tabia hatarishi ambazo zinachangia ongozeko la  waathirika na kuhakikisha  upatikanaji  kirahisi wa za dawa  na ambazo zitakuwa  za gharama nafuu.
  Kwa mujibu wa  Naibu  Waziri ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika  mkutano  huu, amekwenda mbali  zaidi   kwa  kusema  pia patahitajika kupunguza vifo vitokanavyo na   ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watu wanaoishi na  virusi vya ukimwi,  kujadili   masuala ya jinsia  pamoja na  mila na tamaduni,  kutenga raslimali za kutosha kwaajili ya   watu wenye mahitaji wakiwamo vijana, kuwa na   viwanda  vitakavyoweza kuzalisha dawa.
  Akizungumza baadhi ya mafanikio ambayo Tanzania imekwisha kuyafikia katika kukabili tatizo la   ukimwi, Naibu Waziri  ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni   pamoja  na  kupunguza maambukizi mapya kutoka  140,000 mwaka 1990 hadi kufikia 63,000 mwaka 2014. Vile vile vifo vitokanavyo au vinavyosaabishwa na ukimwi pia  vimepungua kwa asilimi 40 katika kipindi hicho.
  Akaeleza pia kwamba hata  watu wanaopatiwa huduma ya  matibabu nayo imeongezeka kufikia asilimia 60 huku  ongezeko likiwa kwa watoto  na hasa baada ya  kupitisha mpango   unaotambulika kama Option B+  miaka sita iliyopita.
  Kuhusu kupungua kwa  raslimali fedha hususani kutoka kwa  wafadhili, Dr. Kingwangalla, amesema  katika  kukabiliana na changamoto hiyo, na  kwa kuzingatia wito wa jumuiya ya kimataifa kupanua wigo wa mapato ya ndani,  serikali ya Tanzania ilianzisha  Mfuko wa ukimwi,  (AIDS Trust Fund) mfuko anaosema hadi sasa  serikali ndiyo imekuwa mchangiaji mkuu, ingawa pia  kwamba sekta binafsi nayo inatazamiwa  kuchangia.
   Akasema sehemu  au nusu ya fedha hizo (55%) itakwenda kusaidia upatikanaji wa huduma na kuongeza kuwa juhudi hizo za serikali pia zimesaidiwa na  ushirikiano  baina ya Tanzania na  nchi nyingine  rafiki pamoja na mashirika ya kimataifa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wale  wote ambao wanachangia juhudi za serikali.
   Kuhusu  mipango  mingine ambayo  serikali  inaendelea nayo ,  Naibu waziri alikuwa na haya ya kueleza “ baada ya  kuwa tumeanza utaratibu wa kupima na kutibu kwa baadhi ya wilaya chache nchini, tunakusudia  kuisambaza huduma hiyo lakini   itakuwa  ni kwa hatua ili  kutoa nafasi ya kuwajengea uwezo watoaji wa huduma  ya afya, kuhuisha  mifumo ya usambazaji wa  vifaa  ikiwa ni  pamoja ushiriki wa  jamii   ili  iweze kupokea na kuukubali mfumo huu mpya wa utoaji wa huduma” ameeleza Naibu Waziri.
  Akasisitiza zaidi kwa kusema ingawa  ugonjwa wa ukimwi  umeendelea kuwa  changamoto kubwa kwa maendeleo ya nchi  ambapo  inakadiriwa watu 1.5 milioni wameathirika, huku mzingo mkubwa ukiwaelemea wanawake na vijana hasa  watoto wa kike,  serikali ya  tanzania  itaendelea na jitihada zake za kuhakikisha inafikia lengo  la kutokuwa na maambukizi mapya,  kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi, na vifo vinatokanavyo na ukimwi.
  Katika hatua nyingine amesema ili kutorudisha nyuma mafanikio ambayo  Tanzania imeyafikia hadi sasa pamoja na  nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara  Jumuiya ya  Kimataifa inaombwa kusaidia jitihada zinazofanywa na serikali  za nchi hizo  za kuwa na  mapato yake yenyewe ya kugharamia   huduma za afya kwa wagonjwa wa ukimwi  na  pamoja na huduma nyinginezo badala ya kuziachia  kabisa jukumu hilo.

   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na  Watoto,  Mhe. Dr. Hamisi Kigwangalla ( Mb) akizungumza   kwa niaba ya serikali kuhusu  mafanikio na changamoto ambazo  serikali imekuwa ikikabiliana nazo  dhidi ya  ugonjwa wa ukimwi ni katika mkutano wa ngazi ya juu  wa Baraza Kuu la  Umoja wa  Mataifa kuhusu ukimwi unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa, Naibu Waziri anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Dr.Hamis Kigwangalla ( Mb)  akiwa na   baadhi ya wajumbe wa Tanzania Dr. Hamis Mwinyimvua, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Policy &Coordination)  na Mhe. Constantine Kanyasu (  Mbunge wa Geita na Makamu  Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Ukimwi,  katika  siku ya kwanza ya  ufunguzi wa  Mkutano wa ngani ya juu  kuhusu Ukimwi ambao umeandaliwa na  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mkutano huyu umefunguliwa na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon   
  Naibu Waziri  Mhe. Dr. Hamisi Kingwangalla akiwa  katika picha ya pamoja mbele ya bendera ya Tanzania na  sehemu ya ujumbe wa Tanzania  unaoshiriki mkutano wa   ngazi ya  juu  kuhusu  ukimwi,  mara tu baada ya kusoma hotuba yake katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo mkutano huu  wa siku unafanyika.

  0 0

  Does your Business Struggle To Attract Enough Customers?

  Get a Copy of "The 3 Biggest Lead Generation Mistakes Small Businesses Make...And How To Overcome Them All" eBook For FREE.
  When You Sign For Your eBook, You will also get a series of videos and articles that teach You How To Out Think...Out Market...Out Sell...Your Competition. You Will Love Them.
  Subcribe-Ebooks


  0 0

   Gulio la simu Expo litakalofanyika katika viwanja vya posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na Jumapili wiki hii litawawezesha wateja wa Vodacom Tanzania na wananchi kwa ujumla kujipatia simu za uhakika zenye gharama nafuu ikiwemo simu za bure kwa wateja watakaonunua vifurushi vya aina mbalimbali vya muda wa maongezi na intanenti.
  Akiongea juu ya gulio hilo,Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia alisema kuwa lengo la gulio hili ni kuwawezesha wateja wa kampuni kuweza kupata maelezo kuhusu huduma za kampuni ikiwemo kuweza kununua simu halisi zenye viwango vinavyotakiwa kwa gharama nafuu kuanzia simu za shilingi elfu 18/- na kuna ofa ya wateja kujipatia simu za bure kabisa.
  “Gulio hili la Vodacom Simu Expo limekuja katika wakati mwaafaka ambapo tarehe ya mwisho ya kuzima simu zisizo na viwango inakaribia hivyo tunawakaribisha wateja wetu wote watembelee gulio hilo na kuweza kujipatia simu zenye viwango vinavyostahili kwa gharama nafuu ambapo pia watapata fursa ya kupata maelezo ya huduma zetu mbalimbali”.Alisema.
  Alisema katika gulio hilo pia kutakuwepo na watoa huduma mbalimbali ambao watashughulikia matatizo ya simu za mkononi pamoja na huduma zinginezo kwa wateja watakafika kwenye gulio hilo.
  Mworia alisema katika Simu Expo pia yanakaribishwa makampuni yanayouza simu nchini kushiriki na kuhakikisha yanatoa punguzo maalum kwa wateja  kwa ajili ya kuwanufaisha wateja hususani katika kipindi hiki cha mwisho ambacho Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) inakaribia kuzima simu zisizokidhi viwango,hatua ambayo itawaathiri baadhi ya watumiaji wa simu kwa kuachwa nje ya mtandao.
  Kuhusiana na ofa ya kujipatia simu ya bure alisema kuwa mteja atakayenunua kifurushi cha muda wa maongezi wa dakika 330 za kupiga mitandao yote chenye jumbe fupi za maneno 2000 na MB 500 za intanent ambacho kinadumu kwa mwezi mmoja atajipatia simu yenye thamani ya shilingi 18,000/-,wakati atakayenunua  kifurushi cha dakika 550 cha kutumia mitandao yote chenye jumbe fupi za maneno na MB 500 atajipatia simu  yenye thamani ya shilingi 25,000/-.
  Pia alisema kuwa wateja watakaonunua kifurushi cha dakika 1000 cha kupiga mitandao yote chenye jumbe fupi za maneno 10,000 na MB 500 za internet kinachodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja atajipatia simu ya bure yenye thamani ya shilingi 50,000/-
  Alisema ofa ya simu za bure inawahusu wateja wanaotumia simu za Smart phone wanaoishi jijini Dar e Salaam ambao tayari wamefahamishwa kuhusu ofa hii kupitia jumbe fupi za maneno na pindi watakaponunua vifurushi kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa wataweza kujipatia simu bure za aina ya Smart Phone ITEL 1406.
  “…Tunawaomba wateja wetu na wananchi wote wafike katika viwanja vya Kijitonyama ili waweze kujipatia simu nzuri na za kisasa wazipendazo kwa punguzo la bei hadi asilimia 50 kwa baadhi ya simu na kupata ofa ya simu za bure kwa kununua vifurushi,” alisema


  0 0


  KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LILILOPO SASABASA ILELEMA JIJINI MWANZA CHINI YA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA, LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UITWAO “OPEN YOUR EYES AND SEE” KWA KIFUPI “OYES CONFERENCE” UKIWA NA MAANA “FUNGUA MACHO NA UONE” AMBAO HUFANYIKA MARA MOJA TU KWA MWAKA.


  MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA KUANZIA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 12 MWEZI WA 6 HADI TAREHE 19 MWEZI WA 6 MWAKA HUU, KUANZIA SAA 8 KAMILI MCHANA HADI SAA 12 ZA JIONI.


  KATIKA MKUTANO HUO, MHUBIRI WA KIMATAIFA KUTOKA OTTAWA NCHINI CANADA ALIEKUFA NA KUFUFUKA BAADA YA SIKU NNE, MAMA DOMITILA NABIBONE, PAMOJA NA MCHUNGAJI JARED MLOGECHA KUTOKA BOSTON MASACHUSSETS NCHINI MAREKANI, WATAKUWEPO.


  WAIMBAJI MBALIMBALI AKIWEMO MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM, CHAMWENYEWE JEMBE KUTOKA MOROGORO, NA KUTOKA MWANZA HAVILLA KWAYA, HOT SPEARS KWAYA, AGNES AKRAMA,THEO DAV, HAPPY SHAMAWELE, JOSEPH RWIZA, MITAGATO, SARAH GAGALA PAMOJA NA CHACHA WATAHUDUMU KATIKA MKUTANO HUO.


  ILI KUFIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA, PANDA MAGARI YA AIRPORT AU ILEMELA, SHUKA KITUO CHA SABASABA KONA YA KISEKE, TEMBEA HATUA CHACHE HADI SOKO JIPYA LA SABASABA, ULIZA KANISA LA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA UTAELEKEZWA.


  USIKOSE KUFUATILIA MAHUBIRI YA MKUTANO HUO KATIKA RUNINGA YAKO PENDWA YA STAR TV KUPITIA KING’AMUZI JABARI LA VING’AMUZI CHA CONTINENTAL PAMOJA NA 96.8 AFYA RADIO.


  WALETE WAGONJWA NA WENYE MAHITAJI MBALIMBALI ILI WAFUNGULIWE KWA JINA LA YESU. KWA USHAURI NA MSAADA WA KIROHO, WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU, MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA, KWA NAMBARI ZA SIMU 0767 74 90 40 AU 0784 74 90 40
  Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Play Hapo Chini.

  0 0
  0 0  Katika miaka ya hivi karibuni ufugaji wa kuku umekua kwa kiasi kikubwa na kuwa mtaji mkuu wa wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kujiingizia kipato.

  Mkurugenzi wa Kuku Project Mary David
  Hata hivyo ufugaji wa kuku nao umekuwa ukienda kwa wakati kutokana na ukuaji wa teknolojia. Moja ya teknolojia hizo ni mashine za kutotoleshea vifaranga kitaalamu; ‘incubator’.

  Mary David maarufu kama ‘Mama Kuku’ ni Mkurugenzi wa Kuku Project Tanzania, ambaye pia ni msambazaji wa mashine za kisasa za Incubator, yeye anasema kuwa mashine hizo zimekuwa mkombozi kwa wafugaji wa kuku nchini kwa kuwa huuzwa kwa bei rahisi inayoendana na mahitaji ya mfugaji mwenyewe.

  Kwa maelezo zaidi

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, maadhimisho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na kufanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake alitoa wito kwa mataifa yote kuweka mbele suala la amani ili kuepuka kupoteza maisha ya wananchi wasio na hatia ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika kujiletea maendeleo.
  Balozi wa wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura akiongea na wageni katika mkutano huo, ambapo aliwasihi jumuiya za wanyarwanda popote ulimwenguni kuzidi kuwafariji wahanga wa mauaji hayo na kuzidi kudumumisha amani. 
  Kutoka kulia Waziri Mahiga pamoja na Mhe. Balozi Kayihura, Mhe. Alvaro Rogrigues Mwakilishi mkazi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Bw. Jean Pierre Nkuranga (Mhanga wa Mauaji hayo ya Kimbari), wakiwa wameshika mishumaa iliyowashwa ikiwa ni alama ya matumaini ya maisha ya baadae kwa Wanyarwanda. 
  Sehemu ya wageni walioshiriki maadhimisho wakiwemo mabalozi wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha mataifa yao nchini, wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha nchini Tanzania na wageni wengine walikwa wakiwa wameshika mishumaa katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bw. Gishuli Charles (wa nne kushoto), wakati alipoanza ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu katika Mkoa wa Singida. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu, na wa tatu kushoto ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo.
   Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa uharibifu wa barabara unaotokana na ajali za barabarani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilometa 89.3 mkoani Singida.
   Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo (wa tano kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto) kuhusu mradi wa ujenzi wa mzani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambao ujenzi utakamilika hivi karibuni.
   Muonekano wa ujenzi wa kituo cha Mzani Itigi, kinachojengwa katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, mkoani Singida.
   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akionesha moja ya picha ya uharibifu wa alama za barabarani uliofanywa na wananchi katika ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  --------------------------------------------------------------------------------------
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewaagiza viongozi wa Serikali kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi mkoani Singida kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaohujumu miundombinu ya barabara na kuisababishia hasara Serikali.
  Profesa Mbarara ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 kwa kiwango cha lami na kubaini kuwa baaadhi ya wananchi wameanza kuhujumu barabara hiyo.
  “Tumepanga kujenga barabara ya Mkiwa-Itigi-Makongolosi kwa kiwango cha lami, sasa kitendo cha kuanza kuhujumu barabara iliyokwisha kamilika ni kitendo kisichokubalika na hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaobainika”, amesema Prof. Mbarawa.
  Prof. Mbarawa amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi wa Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuilinda miundombinu ya barabara, reli na mawasiliano ambayo inajengwa kwa fedha nyingi ili idumu kwa muda mrefu.
  “Tutaimarisha stesheni ya Itigi na kuimarisha mawasiliano ya simu ili kuwezesha eneo hili kuwa na mawasiliano ya uhakika na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Singida”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
  Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa mzani wa kupima magari katika eneo la Bumbuwa katika ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya na kumtaka Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo kuhakikisha ujenzi wa mzani huo unakamilika kwa wakati na magari yote yanayostahili yanapimwa.
  Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa kilomita 89.3 umekamilika kwa asilimia 98 na umehusisha makalvati makubwa 48 madogo 118.

  Zaidi ya shilingi bilioni 109.6 zimetumika katika ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya iliyojengwa katika mfumo wa usanifu na ujenzi ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Manyoni-Itigi-Chaya-Nyahua hadi Tabora.  0 0

  Taifa stars wakijiandaa kukwea pipa kuelekea nje ya nchi kucheza mechi ya kimataifa. Mwenye kumbukumbu ya haya msaada tutani tafadhali.

  0 0


  0 0  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Picha na IKULU.  0 0

  WANAFUNZI wa chuo cha kodi (TRA) waaswa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya kodi kwa vijana wenzao ili kujifunza na kukuza uelewa wa kulipa kodi kwa hiyari.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa vijana wapewe elimu ya kulipa kodi kwa hiyari mapema ili kipindi watakapoanza kupata mapato waweze kulipa kodi bila kushurtishwa.

  Amesema kuwa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni iliyofunguliwa leo iwe taa kwa jamii nzima na wanachama wa jumuiya hiyo waweze kutoa elimu ya kodi watakayoipata kwa wenzao ndani na nje ya mazingira ya chuo.


  Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.
  Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru (Aliyesimamama) akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo, Pia amemshukuru mgeni rasmi kwa kufika katika chuo chao na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo hicho kujifunza zaidi katika kuhamasisha jamii kulipa kodi kwa hiyari. Kaliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa huduma za wanafunzi  wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza.
   Wanafunzi wa chuo cha kodi(TRA) wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  MAADHIMISHO ya wiki ya utumishi wa umma mwaka huu kufanyika kivingine ikitofautiana na miaka mingine yote ikiwa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma hufanyika Juni 16-Juni 23 kila mwaka.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa watendaji wakuu katika wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisis za Serikali watatakiwa kutenga siku moja ya kukutana na watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi kwaajili ya kusikiliza kero za watumishi wa umma kwa madhumuni ya kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kutenga siku moja kwa watendaji wakuu kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na huduma zinazotolewa na taasisi zao na kuzitafutia ufumbuzi.

  Pia amewaagiza makatibu wakuu, Katiu Tawala na mikoa na wakuu wa Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa wafanye Tathmini ya uwepo wa watumishi hewa na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa changamoto hiyo.
  Amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma ni " Uongozi wa umma kwa ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka."

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kuhusiana na namna maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yatakavyofanyika kwa mwaka huu.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamchukua hatua kiongozi yeyote atakayedonoa fedha za michango ya madawati inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

  Pia amewaagiza watendaji wote wa Serikali, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa

  Wilaya na Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha michango hiyo inayotolewa inawafikia walengwa.

  Aidha, amezitaka wilaya zote nchini zianzishe mpango endelevu wa kuhakikisha kwamba upungufu wa madawati unasahaulika kabisa katika maeneo yao na kwamba utendaji wa viongozi wa elimu na Serikali katika ngazi mbalimbali utapimwa kutokana na jinsi ambavyo wametekeleza maagizo hayo.

  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati wa matembezi ya hisani ya kukusanya fedha za kununulia madawati kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

  Katika maadhimisho hayo yaliyoanzia BOT hadi viwanjja vya Mnazi Mmoja, Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndulu alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya shilingi milioni 263 zilizochangwa na benki hiyo pamoja na watumishi wake kama mchango wao kwa ajili ya ununuzi wa madawati.

  Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa BOT kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto hiyo ambapo alitoa wito kwa taasisi zote katika sekta ya umma na binafsi pamoja na watu binafsi kuchangia uboreshaji wa elimu nchini kama sehemu ya “Majukumu ya Taasisi kwa Jamii” (Corporate Social Responsibility).

  Amesema kuwa na elimu bora, siyo tu faida kwa Taifa, bali kwa waajiri pia, kwani itahakikisha kwamba taasisi za umma na binafsi zinapata wafanyakazi ambao wameiva na wenye weledi wa kutekeleza majukumu mbalimbali ya uzalishaji katika taasisi hizo. 

  “Nitoe wito pia kwa wanafunzi wote ambao watafaidika na kuboreshwa kwa mazingira ya kusomea, ikiwemo kupewa madawati na mahitaji mengine, kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa faida yao na Taifa kwa ujumla na kwa kufanya hivyo, wanafunzi watakuwa wanaenzi jitihada za Serikali, taasisi za umma, taasisi binafsi na watu binafsi katika kuboresha elimu nchini,” amesema.

  Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kupambana na changamoto za sekta ya elimu na kwamba tangu Uhuru, Serikali za Awamu zote zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha elimu kwa wananchi wake.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU.

older | 1 | .... | 1251 | 1252 | (Page 1253) | 1254 | 1255 | .... | 3270 | newer