Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1250 | 1251 | (Page 1252) | 1253 | 1254 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KATIBU mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohammed Kiganja amewataka walimu wa shule za msingi nchini, wanaoandaa timu kwa ajili ya mashindano ya Umitashumta kuepuka kuwatumia wachezaji mamluki katika mashindano hayo ambayo yanaendelea nchi nzima katika ngazi mbalimbali.

  Kiganja amesema hayo juzi alipoitembelea kambi ya mazoezi ya timu ya Umitashumta ya Manispaa ya Kinondoni katika shule ya Sekondari ya Lord Baden iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani na kwa kuwatumia mamluki katika mashindano hayo ni kuyaondolea hadhi na kuwanyima haki walengwa hali ambayo alisema ni makosa kisheria na kwamba, yeyote atakaethubutu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

  "Mashindano haya ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi, naomba washirikishwe hao tu, kamwe msijaribu wala kuthubutu kuwatumia mamluki katika mashindano hayo, sioni mantiki ya kufanya hivyo, waandaeni wanafunzi wenu kwa ushindani itakuwa vizuri kuliko kutumia mamluki ili kupata ushindi wa hila, akibainika mwalimu ametumia mamluki katika timu yake, ngazi husika za maamzi zimchukulie hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na timu yake kufutwa na kuondolewa mashindano" amesema Kiganja.

  Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Kiduma Mageni mbali na kumshukuru Kiganja alimhakikishia kuwa, timu yake haitakuwa na mchezaji mamluki hata mmoja, haijawahi na haitatokea na kuunga mkono kuchukua hatua dhidi ya watakaobainika kuwatumia wachezaji mamluki.

  Naye mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Umitashumta Manispaa ya Kinondoni, Masau Bwire amesema katika mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam yanayoanza Ijumaa hii Juni 10, 2016  katika viwanja vya Chuo Kikuu, Mlimani yakishirikisha timu za Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke hawatarajii kuwepo kwa vitendo vya kihuni kwa timu kuchezesha wachezaji mamluki na ikitokea, walimu waliohusika ni majipu tayari, lazima watumbuliwe!

  0 0

  Serikali imekubaliana na mifuko ya hifadhi ya jamii kuanza utekelezaji wa ujenzi wa viwanda nchini ili kuhakikisha kuwa adhma ya Tanzania ya kufikia uchumi wa viwanda inafanikiwa ifikapo mwaka 2020.

  Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli aliyeitaka mifuko hiyo kuwekeza katika ujenzi wa viwanda nchini.

  Akizungumza mara baada ya kikao cha pamoja baina ya Serikali na mifuko hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Ulemavu, Jenister Mhagama alisema Serikali imekusudia kuhakikisha uanzishwaji wa viwanda unaanza haraka na kuongeza fursa za ajira nchini.

  Mhagama alisema kuwa mali ghafi na nguvu kazi ya kutosha zipo hapa nchini hivyo hakuna sababu ya kuchelewa kuanza, ambapo Serikali imepanga hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, utekelezaji wa adhma hiyo inaanza kuonekana machoni mwa Watanzania.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA)alisema, Irene Isaka alisema ni agizo hilo limekuja katika wakati mwafaka kwa kuzingatia kuwa kwa mifuko ya Hifadhi ya jamii imekusudia kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali ya awamu ya tano inayosisitiza kuijenga Tanzania kupitia uchumi wa viwanda.

  Kwa mujibu wa Isaka alisema kuwa kanuni na mifumo ya mifuko hiyo inaruhusu suala la uwekezaji katika viwanda ama kwa njia ya ubia au ya hati fungani au kutoa mikopo kwa wanotaka kuwekeza katika viwanda.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt, Adelhelm Meru alisema uwekezaji katika viwanda ni suala ambalo linawashirikisha wadau wengi zikiwemo wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya malighafi za viwandani, Elimu kwa ajili ya ujuzi wa watu wa kufanya kazi viwandani na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda.

  “Kwa kuangalia raslimali tulizo nazo tumewaomba wadau waanze na viwanda ambavyo vilikuwepo lakini kwa sasa havifanyi kazi kama vile Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC), General Tyre, NARCO na Kiwanda cha Viwadudu cha Kibaha, alisema Dr. Meru na kuongeza kuwa malighafi za viwanda hivi zinapatikana hapa nchini.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha mashauriano ya pamoja baina ya Serikali na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhusu adhma ya ujenzi wa viwanda nchini wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichoitishwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu). Kikao hicho kilifanyika leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Bw. Adam Mayingu na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Bw. William Urio wakifuatilia kikao cha pamoja baina ya mifuko ya hifadhi ya jamii na Serikali kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu), Mhe. Jenister Mhagama akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara (katikati) akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.

  0 0

  Na: Lilian Lundo,MAELEZO

  Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini  (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.

  “Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo  huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.

  Temba aliendelea kuainisha kwamba  siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.

  Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akizungumza na waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAS Dar es Salaam, Gabriel Aluga, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba na Mratibu kutoka asasi ya kiraia ya BADEF.
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Good Hope Star na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Albino duniani Al Shamaymaa Kwegyir akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kuliani Mwenyektiwa TAS Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba (kushoto) na Mwenyekiti wa TAS Taifa Nemes Temba.

  0 0


  0 0


  0 0

  Magari yazuiliwa kupita na lori  la Mizigo kupata hitilafu katikati ya Barabara  likiwa likiingia Barabarani Eneo la Mahenje Njiapanda ya Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.
  Magari yakitafuta pa  kupita ili kuendelea na Safari
  Upenyo ukiendelea kutafutwa na baadhi ya Magari yaliyo wekewa Uzio na lori la  Mbele yao. PICHA NA MR.PENGO MMG

  0 0

   DAKTARI MSHAURI MWANDAMIZI MAGONJWA YA MOYO  HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO NA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU FRANCIS, DKT HARUN NYAGORI AMEALIKWA KUIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WATAALAMU WA MAGONJWA YA MOYO DUNIANI UNAOFANYIKA NCHINI MEXICO.
  TUKIONGEA NAYE KWA MAWASILIANO YA TEKNOLOJIA DKT NYAGORI ALIKUWA MTANZANIA WA KWANZA MWAKA JANA KUPATA TUZO YA KIMATAIFA NCHINI UINGEREZA NA KUTAMBULIWA NA SHIRIKISHO LA MADAKTARI BINGWA WA MARADHI YA MOYO BARANI ULAYA.

  AMESEMA MADA YA MKUTANO HUO UNAOFANYIKA NCHINI MEXICO NI KUPUNGUZA KASI YA VIFO VYA WAGONJWA WANAOKUFA KWA MARADHI YA MOYO HASA KUSINI MWA NCHI ZA KUSINI MWA AFRICA KAMA TANZANIA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA NA NAMNA YA KUWAFIKIA HAO WAGONJWA.  WADAU MBALIMBALI WAMEMPONGEZA DR HARUN NYAGORI KWA KUPATA NAFASI HIYO AMBAYO TANZANIA IMEPIGA HATUA SASA YA KUFANYA UPASUAJI WA WAGONJWA WA MOYO WENYE MATATIZO MAKUBWA YALIYOHITAJI  KUTIBIWA NJE YA NCHI SASA HUDUMA HIZO ZINAPATIKANA TANZANIA.
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
  Baadhi ya Waandishi wa habari wa Taasisi za Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Mwandishi mwandamizi wa Shirika la Habari la Utangazji ZBC Tv Khamis Fakih akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar leo Hapsa Golo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu,Zanzibar.]

  0 0

  Kumekuwa na matatizo mengi ambayo wamekuwa wakiyapata Watanzani wengi wanaokwenda nchi za nje kufanya kazi kwa minajiri ya kujipatia kipato, wengi wa watanzania hao ni Wasichana hasa wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushilikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kisiga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Bi Mindi Kisiga aliendelea kusema kuwa kwa miezi ya hivi karibuni hususani kati ya mwezi Machi-Mei 2016, Barozi za Tanzania nchini Malaysia na India zimepokea maombi ya kusaidia kuwarejesha nyumbani Watanzania ambao walipelekwa nchini India na Thiland kwa ahadi za kupatiwa ajira. Aliongeza kuwa ahadi hizo za ajira zimekuwa zikitolewa na watu wasio waaminifu ambao wanashukiwa kujihusisha na mtandao wa biashara ya kusafirisha binadamu 'human trafficking', mtandao ambao unahusisha raia wa Tanzaniana waliopo ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na raia wa kigeni waliopo kwenye nchi hizo.

  Nchini India pekee kuna Watanzania wapatao 500 waliolipotiwa kuwa huko wakiwa 350 New Delh, 45 Bangalore, Mumbai 20 na wengine wanaelekea Goa. Watanzania hao hulazimishwa kuingia katika biashara ya ukahaba,hunyang'anywa pasi za kusafiria na kulazimishwa kufanya shughuli zingine tofauti na zile walizoahidiwa kabla ya kwenda huko.

  Kufuatia hali hiyo alitoa wito kwa Watanzania wote wawe makini na kjiridhisha na mikataba ya ajira inayotambuliwa na Mamlaka za nchi unayotaka kwenda, kwa hapa nyumbani mamlaka zinazoweza kukusaidia ni pamoja na Ofisi za Ubarozi za nchi husika,Wakala wa Ajira Tanzania(TESA) kwa Tanzania Bara au Kamisheni ya Kazi - Zanzibar.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ambapo alizungumzia juu ya biashara haramu ya binadamu ambayo imekuwa ikiendendeshwa na mtandao wa watu wasiowaaminifu kwa kuwalaghai mabinti wa Kitanzania kwa kuwaahidi kuwapa ajira nje ya nchi.kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
  Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mkutano na waandishi wa habari.
  Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza na kunukuu yaliyokuwa yanazungumzwa na Mkuu wa kitengo Bi. Mindi Kasiga (hayupo pichani).
  Mkutano na waandishi wa Habari ukiendelea.

  0 0

  Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

  Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri.
  Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6.
   Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija.

  Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake.
  “Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na kwamba imeamuru jalada lirudishwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufani ya upande wa Jamhuri kuhusu kuondolewa kwa shtaka hilo” alisema Msajili na kuongeza.
  “Kwa kuondolewa shtaka hilo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hakuwa na namna ya kurudi Mahakama ya Kisutu kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa sababu kila shtaka linajitegemea na kwamba shtaka la kutakatisha fedha lilishaondolewa na kumalizika katika hati hiyo ya mashtaka dhidi ya washtakiwa” alisema Msajili Maruma wakati akisoma hukumu hiyo.
  Akifafanua zaidi alisema Mahakama ya Rufani imebatilisha uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu na kuamuru kusikilizwa rufani ya DPP kama ilivokuwa imekatwa.
  Mapema Mei 31, mwaka huu upande wa Jamhuri ukiongozwa na DPP, Biswalo Mganga, Naibu DPP, Osward Tibabyekomya, Mawakili wa Serikali Waandamizi, Shadrack Kimaro na Awamu Mbagwa uliomba mahakama hiyo kuangalia uhalali wa kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na uamuzi wa Jaji Mzuna kutupilia mbali rufani yao.
   “Watukufu Majaji ni rai yetu upande wa Jamhuri, tunaomba  mahakama hii iangalie upya na kuiamuru Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha …”alidai DPP Mganga.
  Akiwasilisha hoja za rufaa hiyo mahakamani hapo, Tibabyekomya alidai kuwa malalamiko yao ni kwamba Jaji Mfawidhi, Mosses Mzuna alikosea kukataa kusikiliza rufaa ya kuondolewa kwa shtaka hilo na mahakama ya chini.
  Alidai kuwa kinachashtakiwa katika shtaka ni kosa ambalo limekamilika na kwamba linasisimama kwa kujitegemea.
  “Watukufu majaji kitendo cha kufuta kabisa shtaka la nane la kutakatisha fedha dhidi ya washtakiwa kulihitimisha shtaka hilo kama lilivyokua limeshtakiwa  kwa kuwa lilikuwa linajitegema”alidai na kuongeza kuwa.

  “Jaji Mzuna alikataa kwamba mahakama yake haina uwezo wa kuruhusu kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka na kwamba uamuzi huo ulionyesha haiwezekani kufanyika mabadiliko amri ambayo inahitimisha shtaka la nane” alidai msaidizi huyo wa DPP.
  Mawakili wa utetezi wakijibu hoja za Jamhuri kwa nyakati tofauti;
  Wakili Majura Magafu alidai kuwa rufaa hiyo haina mashiko ya kisheria na kwamba ilifunguliwa mapema kinyume cha sheria mahakama hiyo itupilie mbali.
  “Hakimu Mchauru hakukosea kama inavyodaiwa na Jamhuri kwa sababu alitoa nafasi kwamba wakati utakapofika kisheria wataruhusiwa kufanya mabadiliko… “alidai Magafu.
  Dk. Ringo Tenga alidai kuwa baada ya kuondolewa shtaka hilo, upande wa Jamhuri haukuwasilisha maombi ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka.
  Alex Mgongolwa alidai kuwa hoja zao za utetezi kwamba rufaa hiyo haina sababu za kutosholeza kisheria imefunguliwa kinyume cha sheria mahakama ifutilie mbali.
  Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Solomon.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
   Mwandishi mwandamizi wa Shirika la Habari la Utangazji Zanzibar (ZBC) Redio Hassan Vuai  akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifafanua jambo kwa  Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
   MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Utangazji Zanzibar (ZBC) Hassan Mitawi alipokuwa akitoa mchango wake  wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Mwandishi wa Shirika la Habari la Utangazji Zanzibar (ZBC)Tv Maulid Kipevu  akitoa mchango wake wakati wa mkutano uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. Picha na IKULU, Zanzibar

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09, 2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi ya Mpira kutoka kwa Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu NBA Marekani Hashim Thabit, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini. (PIcha na OMR).

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

  Lengo kuu la kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake na ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii.

  Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.

  Nae Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

  Aidha aliwataka wafanyabishara wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa njia za panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.

  Kwa upande wake mwakilishi wa makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred Kadilana ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali.

  Wateja wa simu za mkononi watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel uku kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL.

  Katika maonyesho hayo Taasisi mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA-CCC) na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.
  TELEGRAMS:   POLISI,                                                    OFISI YA
  TELEPHONE: 2500712                                           KAMANDA WA POLISI,
  Fax: 2502310                                           MKOA WA MWANZA,
  E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                    S.L.P.120,
             rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                  MWANZA.


  MWANAMKE MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA WILAYANI MAGU.

  MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI WILAYANI NYAMAGANA.

  KWAMBA MNAMO TAREHE 08.06.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA MAKALE KIJIJI CHA KAYENZE B KATA YA NKUNGURU TARAFA YA NDAGULA WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA , MARIAM NHABAGULA MIAKA 33 MKAZI WA KAYENZE B ALIKUTWA AKIWA AMEJINYONGA  HADI KUFARIKI PAPO HAPO KWENYE MTI KWA KUTUMIA KAMBA YA KATANI.
  INADAIWA KUWA MAREHEMU KABLA YA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUJINYONGA ALIKWENDA KUPIMA AFYA YAKE NDIPO ALIPOKEA MAJIBU KUWA NIMUATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI, HALI ILIYOPELEKEA  KUAMUA KUJINYONGA HADI KUFARIKI DUNIA.
  MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI JUU YA TUKIO HILO ILI KUWEZA KUJIRIDHISHA JUU YA MADAI YA KIFO HICHO.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMEWATAKA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA KUISHI KWA UPENDO NA USHIRIKIANO PAMOJA NA KUFARIJIANA KATIKA KILA HALI, ILI KUWEZA KUZUIA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA KATIKA JAMII ZETU.
  KATIKA TUKIO LA PILI
  KWAMBA TAREHE 09.06.2016 MAJIRA YA SAA 14:00HRS KATIKA MTAA WA LIBERTY KATA YA PAMBA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO NA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA MATONDO JAMES MIAKA 39 MKAZI WA IGOMA AKIWA NA PAKITI MOJA [01] YA MADINI YAZANIWAYO KUWA NI BANDIA WAKIYATUMIA KUTAPELI WATU KATIKA MITAA BARABARANI NA KWENYE MABENKI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
  AIDHA MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, NA TAYARI WATU WENGINE WATATU AMBAO MAJINA YAO YAMEHIFADHIWA WAMEKAMATWA HIVI PUNDE NA JESHI LA POLISI WAKIHUSIANISHWA KUSHIRIKIANA NA MTUHUMIWA KATIKA KUFANYA UHALIFU HUO KATIKA JIJI LA MWANZA.
  INADAIWA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA KAZI YA KUWATAPELI WAPITA NJIA NA WATEJE WA MABENKI KUWA WANAUZA MADINI, HIVYO HUWAAMBIA WANAUZA MADINI YA AINA YA ZAHABU NA MARA NYINGINE HUWAANBIA WANAUZA ALMASI LAKINI KIPINDI HICHO WANAKUWA WAMEYAFUNGA MADINI HAYO BANDIA KWENYE PAKITI NA HUMSHAWISHI MNUNUAJIA AKAIFUNGUE PAKITI HIYO YENYE MADINI SEHEMU WANAPO NUNUA MADINI, PINDI MPITA NJIA AKIKUBALI KUUZIWA MADINI HAYO ANAKUWA TAYARI WAMEMTAPELI NA MATAPELI HAO HUTOROKA MUDA HUO MAHALI WALIPOFANYA UHALIFU.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUWEZA KUWAKAMATA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTAPELI WA AINA KAMA HIYO NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, LAKINI PIA AKIWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA MTU AU WATU WANAOZANIWA KUWA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

  IMESAINIWA NA:
  SACP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Saalam. Katika kikao hicho NIDA iliwasilisha mpango usajili kufikia 31 Desemba 2016 ambapo usajili utakamilika nchini nzima na wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu Alphonce Malibiche
  Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, akifafanua namna mwananchi anaweza kutumia tovuti salama kujua taarifa zake wakati wa kikao na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi Rose Mdami.

  Serikali imekusudia kukamilisha Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote kufikia Desemba 31 mwaka huu.
  Akuzungumza na vyombo vya habari leo, msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya Utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA.

  Akifafanua, Bi Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana Nambari ya Utambulisho, kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili.

  “kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32 vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha taarifa za umri, uraia na makazi” alisisitiza.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya  jamii

  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia, Mwananke mmoja alietambulika kwa jina la Rosemary Khiwili (23) mkazi wa Kimara  kwa kosa la kutupa mtoto katika shimo la choo.

  Rosemary ambaye ni mfanyakazi wa Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam anadaiwa kumtupa mtoto mchanga katika choo cha shimo cha nyumba anayoishi na mtoto huyo amegundulika na mama mwenye nyumba, Upendo Mboma baada ya kuingia kwa ajili ya kumwaga maji machafu na ndipo aliposikia mtoto analia kutokea kwenye choo.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 8 mwaka huu huko maeneo ya Kimara Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Kamishina, Sirro amesema mtoto huyo aliokolewa na akiwa hai na kikosi cha Zimamoto na uokoaji  cha jiji kwa kushirikiana na askari polisi , na mtoto huyo amehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uangalizi maalum huku upelelezi ukiendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

  Wakati huo huo jeshi la polisi limeokota silaha mbili zilizotengenezwa kienyeji  pamoja risasi sita  zikiwa kwenye begi katika shamba la matuta ya viazi baada kutelekezwa na watu wasiojulikana na jitihada zinaendelea kuwabaini watu hao.

  Kamanda, Sirro amesema katika operesheni ambayo wanaifanya kwa wiki hii wameweza kuwakamata watu 711  kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kukutwa bhangi na Gongo , mitambo ya kutengeneza gongo, kucheza kamari pamoja na biashara ya kuuza mwili.

  Amesema  Kawe pamoja na Mabibo zinaongoza kwa utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu ya Gongo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  MABINGWA wa ligi kuu Vodacom 2015/2016 Yanga wanatarajia kuondoka siku ya jumapili Juni 12 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejala utakaopigwa Juni 19 nchini Algeria.

  Yanga itaweka kambi nchini Uturuki na itakaa kwa siku chache kabla ya  kuunganisha moja kwa moja nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza na Mo bejan ya Algeria kati ya tarehe 17,18,19 mwezi huu.

  Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa kikosi kitaondoka mapema na kuweka kambi Uturuki ikiwa ni moja ya mikakati ya mwalimu Hans Van De Pluijm katika kujiandaa na mchezo huo wa kwanza na pia kuwajenga kisaikolojia wachezaji hususani kutokana na mechi za ugenini kuwa ngumu sana na fitina pia.

  "Timu itaondoka jumapili kuelekea Uturuki na lengo kuu sana ni  kuweza kukiandaa kikosi vizuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mo bejala na tunafahamu utakuwa ni moja ga mechi ngumu sana kwanj tunafahamu tutakuwa ugenini na watatumia mbinu mbalimbali za kututoa mchezoni lakini tunajua jinsi ya kupambana nazo kwahiyo wachezaji watajengwa kisaikolojia na kuweza kutoka na ushindi,"amesema Jerry.

  Yanga itaondoka na wachezaji 20 huku Juma Abdul akisalia nchini kutokana na kuwa majeruhi akiumia kifundo cha mguu na nafasi yake kuchukuliwa na Hassan Kessy.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Zambia,  jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan magogo katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Gladynes Mkamba na Kaimu Mtendaji Mkuu TFS, Richard Kamwenda (kushoto). Waliosimama kulia ni Mwanasheria wa TFS, David Mung’ong’o na Mwanasheria wa Wizara ya Maliasili, Stephen Mwamasenjele. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda akisaini  makubaliano hayo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakibadilishana hati ya makubaliano waliyosaini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiangalia sehemu ya magogo yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo. 


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Katika miaka ya hivi karibuni ufugaji wa kuku umekua kwa kiasi kikubwa na kuwa mtaji mkuu wa wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kujiingizia kipato.

  Mkurugenzi wa Kuku Project Mary David
  Hata hivyo ufugaji wa kuku nao umekuwa ukienda kwa wakati kutokana na ukuaji wa teknolojia. Moja ya teknolojia hizo ni mashine za kutotoleshea vifaranga kitaalamu; ‘incubator’.

  Mary David maarufu kama ‘Mama Kuku’ ni Mkurugenzi wa Kuku Project Tanzania, ambaye pia ni msambazaji wa mashine za kisasa za Incubator, yeye anasema kuwa mashine hizo zimekuwa mkombozi kwa wafugaji wa kuku nchini kwa kuwa huuzwa kwa bei rahisi inayoendana na mahitaji ya mfugaji mwenyewe.“Incubator zetu ni za bei tofauti kuanzia shilingi laki nne na nusu ambazo zina uwezo wa kubeba mayai arobaini na nane na kubwa kabisa ambayo hubeba mayai elfu kumi na tisa mia saba kumi na mbili ambayo huuzwa kwa shilingi milioni ishirini,” anasema Bi. Mary.

  Mbali na hayo, Bi. Mary anasema kuwa incubator hizo huwa na uwezo wa kutumia umeme, nishati ya jua na pia kuhifadhi umeme kwa masaa sita baada ya umeme  kukatika ambapo pia mtumiaji atapata fursa ya kuelekezwa jinsi ya utumiaji wake huku mashine hizo zikiwa na waranti ya mwaka mzima.


  Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kununua Incubator fika DAR ES SALAAM,MAGOMENI MWEMBE CHAI,NYUMA YA KANISA LA  WASABATO. SIMU : +255 653 691 138+255 715 908 307,+255 678 226 988


  Kujua zaidi Like Page yao kwa kubofya hapa :  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza hivi karibuni alitembelea Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia mjini Riyadh na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mwanamfalme Bandar bin Muhammad Al-Saud. Aidha, alitembelea Kamisheni ya Utalii ya nchi hiyo na kukutana na Kiongozi mkuu wa Kamisheni hiyo Mwanamfalme Sultan bin Salman bin Abdul-Aziz.

  Mazungumzo ya Mhe. Balozi Mgaza na viongozi hao wawili yalilenga kuanzisha utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano hususan katika sekta ya Maliasili na Utalii kwa mujibu wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia ambao ulisainiwa tarehe 23 Machi, 2016 mjini Dar es Salaam.
  Balozi Hemedi Iddi Mgaza akiwa Ofisini kwa Kiongozi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii ya Saudi Arabia, Mwanamfalme HRH Sultan bin Salman bin Abdulazizi kwenye mazungumzo ya ushirikiano.
  Mhe. Balozi Hemedi Iddi Mgaza akipokea zawadi maalum ya kumbukumbu ya Utalii kutoka kwa Mwanamfalme HRH Sultan bin Salman bin Abdulazizi, Kiongozi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii ya Saudi Arabia.

older | 1 | .... | 1250 | 1251 | (Page 1252) | 1253 | 1254 | .... | 3272 | newer