Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1249 | 1250 | (Page 1251) | 1252 | 1253 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Uendeshaji wa magari wa aina hii unaleta kero na adha kubwa kwa madereva wengine barabarani,Uendeshaji huu wa kutofuata sheria za usalama barabarani,Jeshi la Polisi liongeze kasi kupambana na kuwadhibiti vilivyo madereva wa aina hii,ambao kwa makusudi mazima huamua kukiuka sheria hizo na kupelekea usumbufu mkubwa kwa madereva wengine wenye kutii sheria.

  Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga ameeleza leo kuwa ongezeko la makosa ya watumiaji wa barabara limechangia jeshi hilo kuagiza askari wake kukamata watumiaji kumi kila siku wanaovunja sheria za barabarani.

  Kamanda Mpinga alibainisha Makosa yanayofanywa na madereva wengi ni pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking),(tazama picha juu na chini), kupita taa nyekundu, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha wakiwa wamelewa, madereva bodaboda kutovaa kofia ngumu, kubeba mishikaki, kutokuwa na leseni na pikipiki kutokuwa na Bima.

  Na sisi Globu ya Jamii katika kuliunga mkono Jeshi la Polisi,Kikosi cha usalama barabarani,liendelee kukaza uzi kukamata makosa kumi kila siku ya madereva wazembe barabarani mpaka tunyooke. 


  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bi.  Zamaradi Kawawa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 8, 2016. 
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Mhe. Shally Raymound (kulia) na Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Juni 8, 2016.
  Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishina  Valentino Mlowola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa tawi la hospitali hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho leo kwenye ukumbi wa CPL, Muhimbili.
   Wajumbe wa TUGHE wakiimba nyimbo za mshikamano leo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya.

   Mmoja wa wajumbe wa TUGHE, Helmut Ngalawa akipiga kura leo kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.
   Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya wajumbe kupiga kura leo kwenye ukumbi wa CPL-Muhimbili.
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa TUGHE katika Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege (kulia) na katibu wake, Faustine Kaitaba wakipongezana leo baada ya kuchaguliwa tena katika nafasi hizo kuongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano.
   Picha na JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  0 0

   Mtandao wa kuuza magari mtandaoni wa Cheki.co.tz umezindua huduma mpya ya uunganishwaji wa uigizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji magari bandarini (clearing and forwarding), huduma ambayo itawarahisishia wananchi ambao wanaagiza magari nje ya nchi kuwa na uhakika wa usalama wa magari wanayoagiza mpaka yanakapowafikia.
   Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus, alisema kampuni yake imeanzisha huduma hiyo ili kuwarahisishia Watanzania wanaoanzisha magari nje ya nchi kutokana na kubaini kuwa wamekuwa wakisumbuka kukamilisha uagizwaji wa magari na kuyatoa bandarini.
  “Tayari tumewapa wateja wetu chaguo kubwa la magari kutoka kwa wauzaji wa kuaminika kutoka nje ya huduma hii ya utoaji wa mizigo itarahisisha utoaji wa magari kutoka bandarini na hivyo wateja kupunguza gharama na muda wa kusubiri,” alisema Bencus.
  Nae Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo, alisema kuwa kampuni hiyo haihusiki na uuzaji wa magari ila inachofanya ni kumuunganisha mnunuzi wa gari na muuzaji ili waweze kufanya biashara kwa haraka na urahisi zaidi.
  Ujio wa huduma hiyo imekuwa mwendelezo wa uboreshwaji wa huduma za ununuzi wa magari kwa kupitia mtandaoni ambazo zinafanywa na mtandao wa Cheki.co.tz ambao unafanya kazi na wauzaji wa magari wa kimataifa wa  nje ya nchi na wauzaji wa magari wa hapa nchini.
   Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo akionyesha jinsi watumiaji wa mtandao wa Cheki.co.tz jinsi wanavyoweza kutumia huduma ya clearing and forwarding.
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus akielezea kuhusu huduma ya uunganishwaji wa uagizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji wa magari bandarini (clearing and forwarding), huduma ambayo kampuni yake imeanza kuitoa kwa Watanzania wanaoagiza magari.

  0 0


  Kanisa la Gilgal Christian Ministries International, lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza chini ya Askofu Eliab Sentozi, linawakaribisha wana wa Mungu katika Uzinduzi wa albamu Mpya ya “Nayajua Mawazo” iliyoimbwa na Kwaya ya kanisa hilo ijulikanayo kama “Gilgal Choir”.


  Uzinduzi huo wa Kihistoria unatarajiwa kufanyika jumapili ijayo tarehe 12.06.2016 kuanzia saa nane mchana, katika viwanja vya kanisa hilo, ambapo hakuna kiingilio, yaani watu wote watashuhudia uzinduzi huo BURE kabisa.
  Waimbaji mbalimbali kama vile Emmanuel Mwakisepe, Sarah Joel, HHC Ilemela Choir, Rivival Mission Band, EAGT Mlima wa Utukufu Choir, AIC Nyakato, EAGT Lumala Mpya, EAGT Msumbiji, Happnes Mwakyusa Band, Uinjilisti Choir Gilgal, EAGT Imani Pasiansi, Betty  Lucas, Christian Calvin na wengine wengi watakuwepo ili kunogesha uzinduzi huo.


  Kwa ushauri zaidi, Wasiliana na Gilgal Choir kwa nambari za simu 0757 16 85 85 au 0753 89 37 55 na Mwenyezi Mungu Atakubariki zaidi.
  Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Play Hapo Chini

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango akiwasilisha bungeni  Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka  wa Fedha  2015/2016 na Mwelekeo  wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.


  Kusoma hotuba hiyo kwa Kiingereza BOFYA HAPA

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akionyesha mkoba wenye bajeti ya serikali kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma leo Juni 8, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Na Zuena Msuya, Bagamoyo Pwani

  Wizara ya Nishati na Madini imesema itaendelea kuimarisha miundombuni ya upatikanaji wa huduma ya umeme wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wateja.

  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Leornard Masanja alisema hayo wilayani Bagamoyo baada ya kufanya ziara katika Ofisi ya shirika la umeme nchini (Tanesco) hivi karibuni.

  Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Masanja alielezwa kuwa transfoma 56 ziliibwa mafuta na kusababisha wananchi wengi kulalamikia Tanesco kwa kuchelewa kuwapatia huduma ya umeme licha ya kukamilisha hatua zote za kuunganishwa na huduma hiyo na umeme kukatika mara kwa mara.
  Baadhi ya transfoma zilizoibwa mafuta zikiwa katika ofisi ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

  Pia alielezwa kuwa, Tanesco imekuwa ikichelewa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo pindi inapotokea hitilafu ya umeme au kukatika kwa huduma ya umeme katika eneo fulani la Wilaya na Mkoa huo.

  Baada ya kupokea malalamiko hayo, Mhandisi Masanja aliwataka Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya ya Tanesco wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi kutoa ufafanizi wa namna ya kukabiliana na changamoto hizo pamoja na kutatua malalamiko hayo kutoka kwa Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi.

  Kwa upande wake Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu, alisema kuwa malalamiko hayo yanatokana na uchache wa miundombinu hasa kwa wale wanaohitaji kuunganishiwa huduma ya umeme.
  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja( wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo ( kushoto).

  Aidha alifafanua kuwa watumishi wachache waliofukuzwa wamekuwa wakidaiwa kuhujumu shughuli nzima za kuunganisha huduma za umeme kwa wananchi kwa kudai rushwa kwanza jambo lililokuwa likiwakatisha tamaa wananchi.

  Hata hivyo alielezwa kuwa, tayari wafanyakazi wanane wamefukuzwa kazi wilayani bagamoyo kwa makosa mbalimbali ikiwemo rushwa,matumizi mabaya ya ofisi na kuchelewesha huduma kwa wananchi.

  Naye Meneja wa Tanesco wilayani Pwani Mhandisi Julias Doyi alisema kuwa tatizo la kuchelewa kuwahudumia wananchi hasa wale wanaopata tatizo la kukatika huduma ya umeme linatokana na miundombinu mibovu ya kuwafikia wananchi hao na kuwa na Gari moja la kutoa huduma kwa wilaya nzima.

  Aliongeza kuwa Tanesco wamekuwa wakichelewa kupata taarifa kutoka kwa wananchi kutokana na wengi wao kutoa taarifa hizo kupitia Viongozi wa Serikali za mitaa na kusababisha taarifa hizo kuchelewa kuwafikia Tanesco.
  Kaimu Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja( mbele) akiwa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu( nyuma kulia) na Meneja wa Tanesco Wilaya ya Bagamoyo( nyuma kushoto) wakitoka katika ofisi ya serikali ya mtaa kupata maoni ya viongozi wa mtaa juu ya huduma ya umeme wilayani humo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Weston Zambi akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) Ofisini kwake jana.
  Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi wakiwa katika kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akimkabidhi Ipad Afisa Habari wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Elibariki Mafole (kulia) jana.
  Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Tawala Mkoa, Wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa na Waandishi wa Habari.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  BEKI wa kulia aliyetia wino Yanga, Hassan Kessy pamoja na winga wa Coastal Union, Juma Mahadhi wameanza vizuri mazoezi yao baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu huku kila mmoja akifunga goli katika mechi ya mazoezi waliyocheza kwenye uwanja wa Taifa,Jijini Dar es salaam.

  Kessy ameanza mazoezi rasmi na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na wekundu wa Msimbazi na kujiunga nao huku wachezaji wa timu hiyo wakimpa sapoti kwa asilimia zote. 

  Uwezo ambao kessy ameuonesha kwenye mazoezi hayo ni wa hali ya juu huku kwa mara kadhaa akimvisha kanzu Geofrey Mwashiuya aliyekuwa anakabana nae.

  Naye Mahadhi ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali ingawa mazingira halisi hakuwa ameyazoea ila ameweza kufunga goli moja kwa ustadi mkubwa sana na kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm akisifia kiwango cha wachezaji wake hao wapya. 

  Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa kumi jioni yakiongozwa na mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana na Juma Mwambusi yameshuhudiwa na mashabiki wa timu hiyo huku wakionekana kupiga makofi pale Kessy na Mahadhi wanapofanya vizuri uwanjani.

  Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo mashabiki wameonekana kuwazonga Kessy na Mahadhi na kupiga nao picha wakiwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  SERIKALI  imetakiwa kushirikisha sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ili kuifanya sekta hiyo iweze kutanuka na kuongeza ajira nchini.

  Akizungumza na  wadau wa biashara leo  katika hoteli ya Double Tree  wakati wa kujadili bajeti iliyowasilishwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Bungeni Mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Kampuni ya EY Tanzania,  Joseph Sheffu, amesema kuwa  kuweza sekta binafsi kuweza kutanuka serikali  inawajibu kushirikiana kwa baadhi ya miradi ikiwemo ujenzi wa barabara.

  Amesema kuwa bajeti ni  nzuri kutokana na serikali kusimamia ulipaji wa kodi ambayo nchi zote zimeweza kusonga mbele kwa kuweka mbele kiumbele cha kodi.

  Sheffu amesema kuwa, katika bajeti hii inahitaji kuwa na bajeti ya wafadhili ambayo inatakiwa kuwa na masharti nafuu , kuacha tusihitaji inaweza  kusababisha baadhi ya miradi kukwama.

  Aidha  amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuja bajeti yenye unafuu kutokana na serikali imeingia ikiwa haina kitu lakini katika ukusanyaji wa mapato imejitahidi sana.

  Sheffu amesema kuwa sasa serikali iweke kipaumbele cha kilimo kwani kumekuwepo na mkazo lakini matokeo katika sekta ya kilimo hayaonekani.
  Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa jana Bunge na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango. Mkutano huo uliondaliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernest Young (EY), umefanyika leo Juni 9, 2016 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree, Jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.

  Mmoja wa wachumi Nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Prof. Sufiani Bukurura akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika Mkutano wa kujadili bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa jana Bunge na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango. Mkutano huo uliondaliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernest Young (EY), umefanyika leo Juni 9, 2016 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree, Jijini Dar es salaam.

  Sehemu ya Wadau wakifatilia mbada mbali mbali kwenye Mkutano huo.


  0 0

  Kufuatia kudaiwa deni la zaidi ya sh. mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki wa jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumza leo  mke wa mmiliki  wa jingo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 

  Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
  Hili ni eneo la Kanisa Hilo
  Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje
   Vyombo vya Muziki vikiwa nje.


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni hiyo,Saurabh Jaiswal na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
  Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh Jaiswal(kushoto)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,wakimsikiliza Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.


  0 0
  0 0

  SIMU.TV: Madiwani 24 wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha wamefikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la kuharibu uzio wa wenye thamani ya Sh. Mil 7; https://youtu.be/uLgUkTFtCoU
   SIMU.TV:  Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani amesema jumla ya madereva 54 wamekamatwa jijini kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kugonga mabasi ya mwendokasi;https://youtu.be/jHUIc1zrWz0
   SIMU.TV: Lori la mizigo ya mawe limeporomoka bila dereva na kuparamia duka na kugonga wapiti njia hatua iliyosababisha taharuki katika mji wa Songea; https://youtu.be/n5W8fiPp_7g
   SIMU.TV: Shirikisho la ngumi za ridhaa duniani yatoa nafasi ya mwisho kwa Tanzania kushiriki katika mashindano ya Olympic; https://youtu.be/BcoqUTewlPA
   SIMU.TV: Shirikisho la tennis duniani lamfungia mchezaji Maria Sharapova kutoshiriki katika mchezo huo kwa kipindi cha miaka miwili; https://youtu.be/EdQwpN_5ZdI
   SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Limeanza kutoa fomu za leseni  kwa vilabu vya soka ligi kuu na ligi daraja la kwanza; https://youtu.be/z9M9Szm2p0M
  SIMU.TV: Fahamu mambo mengi kutoka katika mamlaka ya chakula na dawa TFDA  wakikufahamisha kuhusu  bidhaa feki: https://youtu.be/P5tfYTH3sjY 
  SIMU.TV: Yajue mambo mbalimbali kutoka katika mada motomoto inayojadili kiundani kuhusu  bajeti  iliyopelekwa katika sekta ya kilimo: https://youtu.be/kE5bn4FDhB0
  SIMU.TV: Fahamu mambo mengi  kutoka kwa mfatiliaji  wa masuala ya serikali  na  uchumi akikujuza kuhusu bajeti ya kwanza kwa serikali ya awamu ya tano: https://youtu.be/tdbsfpqjsrc

  0 0

  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.


  TAASISI ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.


  Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
  Ibrahim Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.


  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  KOCHA mkuu wa timu ya walemavu ya Tenisi, Riziki Salum amesema kuwa timu yake ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya kuelekea michuano ya wazi nchini Kenya na kujihakikishia kuwa watarejea na ubingwa huo kwa mara nyingine tena kwani watahakikisha wanatetea taji hilo.

  Tunachokiamini kuwa wachezaji saba wachanga tuliokuwa nao tukijumuisha na wakongwe kama Novatus Temba tunaahidi kurudi kifua mbele.

  Amesema, kwa rekodi waliyoiweka toka 2013, walipochukua timu bora ya mwaka kwenye kombe la Dunia nchini Uturuki na waliposhiriki kwenye michuano ya mataifa nane Afrika Kusini 2014 na kuchukua nafasi ya pili yanawapa nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya vizuri zaidi wao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya wazi ya Kenya.

  "Tuna wachezaji wazuri ukichukua chipukizi na mkongwe Novatus Temba na wamenihakikishia kufanya vizuri zaidi ukiangalia rekodi yetu ni nzuri, 2013 tumekuwa timu bora Duniani katika kombe la Dunia, 2014 tumeshiriki mashindano yaliyohusisha mataifa nane nchini Afrika ya Kusini na tukashika nafasi ya pili na ukizingatia tunaenda tukiwa mabingwa watetezi ,"amesema Salum.

  Ametoa wito kwa wazazi kuwapa fursa watoto wao zaidi kwani kuwa mlemavu sio chanzo cha kushindwa kujumuika na wenzake kwenye michezo mingine na hata hivyo amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuja kusaidia mchezo huo hususani kwa walemavu kwani timu hiyo imeweza kufanya vizuri lakini hakuna wanaoangalia zaidi ya Mpira wa miguu.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria, Balozi Daniel Ole Njolaay akimkabidhi hundi ya dola 2000 za Kimarekani sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nne, Mh. Dk Angelina Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha shule za msingi zinakuwa na madawati ya kutosha hapa nchini, Hafla hiyo ilifanyika kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Abuja nchini Nigeria mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Maendeleo ya Makazi jijini humo.
  Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaziakizungumza katika hafla hiyo huku Balozi Daniel Ole Njolaay akimsikiliza.
  Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazipamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Balozi Daniel Ole Njolaay wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ubalizi huo na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
  Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Balozi Daniel Ole Njolaay pamoja na maofisa waubalozi huo na Shirika la Nyumba Tanzania NHC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

  0 0

  Na Atley Kuni- RS Mwanza.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza katika siku za karibuni katika mkoa huo.

  Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa mkaanza kutumia visiwa vyetu,

  “Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na maliasili”

  Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini.

  Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko la kozi za askari kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi, mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia ardhi.

  Mkuu huyo wa chuo amesema mbali yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika chuo hicho.
  Mkuu wa mkoa wa akipanda, mti katika taasisi hiyo, ikiwa ni sehemu ya ukumbusho wa miaka hamsini toka kuanza kwa chuo hicho.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akisalimiana na mmoja wa wakufunzi katika chuo cha taasisi ya mafunzo ya wanyamapori Pasiansi jiji Mwanza, alipofika kwenye uzinduzi wa maonesho ya miaka 50.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akihutubia, wakufunzi, wakurufunzi na jamii inayozunguka chuo hicho, hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa maonesho ya miaka 50 ya chuo hicho.
  Hapa picha ya pamoja ni muhimu kwaajili ya kalenda ijayo ya Mwaka, hii nikatika miaka 50 ya chuo cha wanyamapori Pasiansi.

  0 0

  Katika kutengeneza Msingi mzuri kwa wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya inafanya Maonyesho Makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku ya tarehe 11 June 2015.
  Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira wamealikwa kutoa mada na kuonyesha uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walioalikwa kwenye Tamasha Hilo ni; Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba amba ye ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wakujitegemea na mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – MenejawaTawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo ni Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.LuhagaMpina.
  Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.

older | 1 | .... | 1249 | 1250 | (Page 1251) | 1252 | 1253 | .... | 3284 | newer