Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1248 | 1249 | (Page 1250) | 1251 | 1252 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Timu nzima MMG chini yake Ankal Issa Michuzi, inawatakia mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndugu wote katika Imaan ya Dini ya Kiislam, Duniani kote. Hiki ni kipindi muhimu sana kwa waislam wote katika Ibada ya Toba, hivyo tujitahidi kuhimizana kufanya ibada na kumcha Allah Sub Hannahu Wataala. Amin
  Ramadhan Kareem.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Bilioni 12 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey ikiwa ni bakaa (salio) ya tume hiyo zilizopangwa kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015. Hafla hiyo fupi imefanyika Ikulu, Dar es salaam leo Juni 7, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea mfano wa hundi ya Bilioni 12 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey ikiwa ni bakaa ya tume hiyo zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015. Hafla hiyo fupi imefanyika Ikulu, Dar es salaam leo Juni 7, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakimsiliza Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima Kobwey wakati akitoa taarifa ya namna Tume ya Uchaguzi ilivyookoa kiasi cha shilingi Bilioni 12 zilizopangwa kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015. Hafla hiyo fupi imefanyika Ikulu, Dar es salaam leo Juni 7, 2016. PICHA NA IKULU
  0 0

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amezitaka Halmashauri zote nchini kutoa vitambulisho kwa wazee waliopo katika Halmashauri zao. Haya ameyasema leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee, uliofanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Maktaba Kuu ya Mkoa.
  Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania.
  Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wazee walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania

  Akihutubia katika uzinduzi wa Mkutano huo Mheshimiwa Waziri Ummy alizitaka Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kutoa vitambulisho kwa wazee ili kuwezesha utambuzi wa wazee waliopo katika Halmashauri zao hususan katika utoaji huduma na mahitaji mbalimbali.

  Mfano wa kitambulisho kinachotolewa kwa wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasuru.

  Waziri Ummy alisisitiza kuwa Halmashauri zinatakiwa kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Mzee Kwanza” hususan katika utoaji wa huduma za afya ambapo kila kituo cha Afya cha Umma kinatakiwa kiwe na chumba na watumishi maalum wa kuhudumia wazee. Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanakuwa na regista ya Wazee kwa kuainisha pia ujuzi wa wazee hao.

  Mheshimiwa Waziri Ummy alieleza kuwa Serikali inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria ya Wazee Bungeni Mwezi Septemba mwaka huu. Pia, aliwahakikishia wazee kuwa tatizo la upatikanaji wa dawa kwa wazee litapatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa kuanzia mwezi Julai 2016.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Blog ya Jamii

  MSHAMBULIAJI wa timu ya Mtibwa Shiza Kichuya amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja kwahiyo watakaomuhutaji wafuate uongozi na wakae mezani kwani yeye hana mamlaka ya kuongea na timu yoyote kwa sasa zaidi kama watakaomtaka wakifikiana makubaliàno hatakuwa na budi kwenda.

  Kichuya amesema, kwa sasa haangalii ni timu gani inamuhitaji ila anachokiwaza ni kuweza kujiandaa vyema kuelekea msimu ujao na zaidi anachokifanya kwa sasa ni kufanya mazoezi na toka Jumatatu baada ya kurejea toka kwenye majukumu ya Timu ya Taifa.

  "Kama kuna timu inayotaka huduma yangu mimi siwezi kuongea nao kwani bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa na zaidi kwa atakayenihitaji aje kuongea na kiongozi wangu na mimi sitakataa kama wao wakiamua,"amesema Kichuya. Kwa kweli sina mipango ni kuja kufanya mara mbili zaidi ya msimu uliopita kwani nachokijua mimi ni mchezaji na mpira ndiyo kazi yangu kwahiyo najipanga kwa kujikita muda wote kwenye mazoezi.

  Kichuya amekuwa moja ya chipukizi wanaofanya vizuri kwenye kandanda na zaidi ameweza kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa na amecheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya na kuweza kufanya vizuri.

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imewaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mazingira na maliasili na kuzitaka mamlaka za usimamizi wa mazingira na maliasili kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali imewaamini na kuwapa jukumu hilo.

  Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mufindi katika maadhimisho ya siku ya mazingira iliyofanyika katika kijiji cha Lugoda Lutali wilayani Mufindi mkoani Iringa Afisa Mawasiliano wa LEAT Miriam Mshana ,alisema kuwa uharibifu wa mazingira umechangiwa kwa sehemu kubwa na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na ukataji miti ovyo bila kupata vibali na uvunaji haramu wa wanyamapori, usio rafiki kiuchumi na kimazingira.

  Mshana alisema, uvunaji wa kasi hasa wa misitu umeathiri na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, kuiweka nchi katika hatari ya kuwa jangwa. Uvunaji haramu wa wanyamapori hususan tembo umeipa hasara taifa.Kwa mujibu wa ripoti ya Mtaalam Mashuhuri wa tafiti za tembo duniani, Ian Douglas Hamilton, kwa mara ya kwanza mwaka 1976 alifanya utafiti wa angani, Tanzania kwa ujumla ilikuwa na tembo 316,000, ambayo ilikuwa idadi kubwa sana ikilinganishwa na maeneo mengine duniani’’’’’alisema mshana .Kwakufanya hivyo tutakuwa tunaitikia wito wa kaulimbiu ya mwaka 2016 ya siku ya mazingira duniani-‘Shiriki kufanya dunia mahali pazuri’. 

  Jowika Ksunga ni mkuu wa wilaya ya Mufindi nae alisema, Mwaka 1976, mbuga ya Selou pamoja na maeneo jirani ilikuwa na idadi ya tembo109,000,Utafiti uliofanywa mwaka 2013, ulibaini kuwa mbuga ya Selou ilikuwa na tembo 13,084 pekee.Kasunga alisema takwimu hizo zinaashiria hatari ya kutoweka kabisa kwa tembo katika nchi yetu na itaathiri biashara ya utalii ambayo ilikuwa ikitoa mchango mkubwa katika pato la taifa.

  "Maeneo mengi ya mijini yamechafuliwa kwa utupaji taka ovyo, hivyo kuharibu mandhari ya miji yetu na kuchangia katika magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu, alisema Kasuga.Alisema, utupaji taka ngumu na zenye sumu karibu na makazi ya watu au vyanzo vya maji, umeleta athari kubwa kiafya kwakuwa kemikali hizo hupenya ardhini na kudhuru ardhi na vyanzo vya maji, hasa kwa wananchi wanoishi karibu na viwanda na sehemu za uchimbaji madini.

  “Inasikitisha kuwa wamiliki wa viwanda vingi na machimbo ya madini wanakiuka sheria ya mazingira lakini pia wameshindwa kuwajibika kwa jamii zinazo wazunguka ambazo ndio wadau wakubwa wa biashara zao, kwa kaidi kuchukua hatua za kuzuia uharibifu wa mazingira hata baada ya athari kutokea”, alisema Jowika

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Asumpta Mshama alisema kuwa shirika la LEAT limekuwa mstari wa mbele kwa zaidi ya miaka 20, katika kusimamia mazingira nchini katika sekta ya madini, viwanda, machinjio na mazingira kwa ujumla.Asumpta alisema taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa mwezi Aprili, 2016 inaonesha takribani watu milioni 2 hufa kila mwaka duniani na zaidi ya watu bilioni moja hupatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchafuzi wa mazingira.

  "Iwapo serikali, wananchi na wamiliki wa viwanda na machimbo ya madini, kila mmoja akitimiza wajibu wa kutunza mazingira tutakuwa natekeleza haki ya kuishi, haki ya afya bora na ustawi, kama ambavyo serikali ilivyo ridhia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo mkataba wa Stockholm nchini Sweden na Rio De janeiro nchini Brazil"alisema Asumpta.
  Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Asumpta Mshama akihutubia wananchi wakati wa sherehe za siku ya mazingira duniani, katika kijiji cha Lugodalutali, wilaya ya Mufindi.
  kikundi cha sanaa kutoka kijiji cha mapogoro kikihamasisha utunzaji wa mazingira na maliasili ktk sherehe za siku ya mazingira zilizo fanyika tarehe 3 June 2016 kijijini Lugodalutali. Kikundi hiki kinalelewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT).
  LEAT yagawa vitabu na vipeperushi vinavyotoa elimu ya mazingira na maliasili.


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johari(kushoto), akikabidhi msaada wa Kompyuta kwa wanafunzi wenye mahitaji maluum wenye ulemavu wa akili wa shule ya Msingi Mtambani, iliyopo Boko jijiniI Dar es salaam. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule hiyo Mariana Saso na Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Wanafunzi wenye Ulemavu wa akili wa shule hiyo Asaph Maerere.Hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCAA Ukonga, Banana.
  Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Wanafunzi wenye Ulemavu wa akili wa shule ya msingi Mtambani iliyopo Boko jijini Dar es Salaam, Asaph Maerere. akiwa na wanafunzi wake wakiwa wamebeba kompyuta mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johar(hayupo pichani) .
  Wanafunzi wenye mahitaji maluum ya ulemavu wa akili wa shule ya Msingi Mtambani, iliyopo Boko jijini Dar es salaam,wakifurahia komputa mara baada ya kukabidhiwa msaada na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johar(hayupo pichani)hafla hiyo Hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCAA Ukonga, Banana.

  0 0  Jeshi la Polisi limesema kuwa ongezeko la makosa ya watumiaji wa barabara limechangia jeshi hilo kuagiza askari wake kukamata watumiaji kumi kila siku wanaovunja sheria za barabarani.

  Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed R. Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Mpinga amesema kuwa kumekuwa na ongezekezo kubwa la uvunjifu wa sheria za barabarani kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu ambapo katika kipindi hicho makosa 290,161 zaidi yaliyokamatwa tofauti na mwaka jana.

  Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Mei 2015 jumla ya makosa 484,034 yalikamatwa nchi nzima wakati kwa kipindi cha Januari mpaka Mei 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa Tanzania bara.

  “Kwa mfano kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka 2015 jumla ya makosa ya usalama barabarani 484,034 yalikamatwa katika mikoa yote Tanzania Bara na kwa kipindi kama hicho cha Januari hadi Mei mwaka 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa pia katika mikoa yote Tanzania Bara” alisema Kamanda Mpinga.

  Akizungumzai hoja ya kuweka kiwango cha ukamataji wa makosa kwa askari wa jeshi hilo, Kamanda Mpinga alisema kuwa Polisi haiwezi kuweka idadi ya makosa ya kukamata wakati madereva wanaendelea kufanya makosa barabarani na ajali zinaendelea kutokea.

  “Askari wameelekezwa wakamate makosa mengi iwezekanavyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba madereva wengi Barabarani hawazingatii sheria za Usalama Barabarani hivyo kusababisha ajali,” alisema Kamanda Mpinga.Aidha Kamanda Mpinga amewatahadharisha madereva wote kuacha kufanya makosa Barabarani kwani Jeshi la Polisi halitawavumilia, litawakamata na kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.

  Makosa yanayofanywa na madereva wengi ni pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking), kupita taa nyekundu, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha wakiwa wamelewa, madereva bodaboda kutovaa kofia ngumu, kubeba mishikaki, kutokuwa na leseni na pikipiki kutokuwa na Bima.

  0 0

  Na Jonas Kamaleki 

  Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango wakati akitoa hotuba kuhusu taarifa ya hali ya uchumi nchini na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17.

  Waziri Mpango amesema kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ya serikali na kuongeza kuwa fedha za ndani ni shilingi bilioni 8,702.697 ambazo ni sawa na asiliia 74 ya bajeti ya maendeleo na fedha za nje ni shilingi bilioni 3,117.805 sawa na aslimia 26 ya maendeleo.

  Aidha, Mpango amesema kuwa sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuanzisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango huo.

  “ Kwa ujumla fedha za maendeleo zimeelekezwa zaidi katika miradi inayolenga kuendeleza viwanda kama vile uchukuzi,ujenzi, nishati, kilimo, maji, elimu na afya,”amesema Waziri Mpango.
  Ameongeza kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 umeainisha miradi mikubwa ya kielelezo ambayo itapewa msisitizo katika utekelezaji wake.

  Waziri Mpango ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma, mradi wa chuma Liganga, ujenzi wa reli mpya kati ya Dar – Kigoma na Tabora- Mwanza na matawi yake Isaka- Kigali/Keza- Msongati na Kaliua- Mpanda kwa kiwango cha standard gauge.

  Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 utategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango akiwasilisha bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwelekeo wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Shally Raymound (kulia) na Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishina Valentino Mlowola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Zamaradi Kawawa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 8, 2016.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  Wabunge wa Viti Maalum (CCM) wakiongozwa na Mhe. Margaret Sitta wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi cha bunge hilo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16),  Aeesha Kamara, kitabu maalum kinachoelezea sifa kem kem za Tanzania, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia Watanzania mbalimbali waishio ndani na nje ya nchi. Mbali na Mrembo huyo, Bodi ya Utalii, ilikutana pia na Mchezaji wa mpira wa Miguu wa kimataifa, Mbwana Samatta pamoja na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, Vanessa Mdee.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), Devota Mdachi (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa, Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16),  Aeesha Kamara, mara baada ya kuzungumza nae leo.

  Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16),  Aeesha Kamara akifafanua jambo, wakati alipokutana na Bodi ya Taifa ya Utalii, jijini Dar es salaam leo.
  Mrembo wa Tanzania nchini Marekani (Miss Tanzania USA Pageant 2015/16), Aeesha Kamara (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB), mara baada ya kufika na kuzungumza na Bodi hiyo, leo Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mama mzazi wa Mrembo huyo, 

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.

  Mkongwe wa Soka nchini Nigeria ambaye aliwahi kuwa Nahodha wa Kikosi hicho cha Super Eagles na kuwahi kunyakua taji la AFCON akiwa kama Kocha na Mchezaji, Steven Keshi amefariki Dunia ghafla.

  Kifo cha Keshi imeelezwa kuwa alikua akisumbuliwa na matatizo ya Moyo kwa muda mrefu.

  Keshi aliwahi kunyakua taji la AFCON mwaka 1994 kabla ya kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Dunia katika hatua ya Robo Fainali mwaka huohuo wa 1994.

  Ameinoa Super Eagles katika kipindi cha awamu tatu,akiiongoza kunyakua taji la AFCON mwaka 2013 nchini Afrika ya Kusini na kuifikisha timu hiyo hatua ya 16 Bora katika Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.

  Keshi hakusaini mkataba wa kuinoa Nigeria baada ya kumalizika Michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil licha ya timu hiyo kushindwa kufuzu AFCON mwaka 2015.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimpa zawadi ya kanga Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo mjini Dodoma. Picha na Anna Nkinda
  Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimwonyesha Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad picha za mazao ya mbogamboga ambayo yamelimwa katika kilimo kinachowezesha mazao mchanganyiko kustawi katika mazingira yenye hali ya hewa iliyodhibitiwa mkoani Mtwara.
  Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad akivaa kanga aliyopewa zawadi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura aliyekutana naye leo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Wambura akimwangalia.
  Mhe. Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad (kushoto) akimweleza Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Norway hapa nchini ukiwemo mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia VICOBA.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango akiwasilisha bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwelekeo wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akikagua stoo ya sukari katika kiwanda cha kagera sugar kuona akiba ya sukari iliyobakia sambamba na kujionea hali halisi ya uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.
   Mkuu wa mkoa wa kagera  Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akisikiliza taarifa ya kiwanda cha kagera sugar kutoka kwa meneja mkuu wa kiwanda hicho(hayupo pichani)katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuona akiba ya sukari iliyobakia sambamba na kujionea hali halisi ya uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.Picha na Editha Karlo,Globu ya Jamii-Kigoma
   Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (mwenye suti)akiwa na viongozi wa kiwanda cha kagera sugar wakati alipofanya ziara yake kiwandani hapo
   Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali staafu Salum Kijuu na ujumbe wake wakiangalia sehemu ya maji yaliyojaa kwenye shamba la miwa la kiwanda cha kagera sugar,hali hiyo ilipelekea kiwanda kusimamisha uzalishaji
   Baadhi ya mifuko ya sukari iliyohifadhiwa katika stoo ya kiwanda cha kagera sugar.

  0 0

  Wafanyabiashara na wateja wa soko kuu la kariakoo wataanza kunufaika na huduma mbalimbali za mawasiliano na za kifedha kwa urahisi zaidi, Kwani kampuni ya Vodacom Tanzania katika kutekeleza mkakati wake wa kusambaza huduma zake karibu zaidi na wateja wake popote walipo leo imezindua duka jipya la kisasa sokoni hapo.

  Duka hili ni mwendelezo wa kusambaza huduma ambapo kwa mwaka huu kampuni itafungua maduka sehemu mbalimbali ikiwemo vituo vidogo vya kutoa huduma vipatavyo 500 nchini kote.

  Kufunguliwa kwa duka hili kutawarahisishia wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo na wananchi wanaofika  eneo hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za Vodacom kwa urahisi.

  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua maduka na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kampuni yao umebuniwa ili kuwapunguzia wateja wao adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma.

  “Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka mengine na mawakala eneo hili la Kariakoo sehemu  bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
  Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya maduka na  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi ya 1000 watanufaika na mpango huu na  ni utekelezaji wa  moja ya malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa kuwanufaisha watanzania.

  Akizindua duka hilo,Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka hilo zaidi ya kuipongeza kampuni hiyo kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja,aliwataka wafanyabiashara wa soko la Kariakoo na wananchi kwa ujumla  kutumia huduma za mawasiliano za kampuni hiyo kwa ajili ya kurahisisha maisha yao na kutokupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta sehemu za kupata huduma hizo kwani wameletewa huduma hizo karibu zaidi.

  Mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo Abdallah Rajabu akiongea kwa niaba ya wakazi wenzake alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutawapunguzia kero wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo  kutembea na kuzunguka katika maeneo mbalimbali kufuata huduma za Vodacom“Tunaishukuru Vodacom kwa kutukumbuka wafanyabiashara wa sokoni hili la Kariakoo kwa kweli tutanufaika sana na huduma zao kama vile M-pesa na zinginezo nyingi”alisema
  Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(katikati)akikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.Wengine kushoto Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama.
  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama,akimuonesha Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni moja ya simu aina ya”smart phone”zinazopatika kwa bei nafuu katika duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko hilo mara baada ya kulizindua rasmi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha wateja rejareja wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama,wakimshuhudia Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(kushoto)akikata keki kuashiria uzindua wa duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
  Kaimu Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo,Mrero Mgheni(kushoto)akimlisha keki Maria Shabani,ambaye ni mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo langoni mwa soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo,Wengine katika picha Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,Dominician Mkama(wapili kushoto)na Mkuu wa kitengo cha wateja rejareja wa kampuni hiyo,Brigita Stephen.

  0 0

  Na KhadijaKhamis –Maelezo Zanzibar 8/06/2016.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amelizindua rasmi Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira lenye wajumbe nane kutoka sekta za Serikali na sekta binafsi .

  Akizindua Baraza hilo katika Wizara ya Afya Mnazimmoja, alisema lengo la kuundwa Baraza hilo ni kudhibiti hali ya afya na mazingira ili kuisaidia jamii kujiepusha na maradhi ya mripuko na maradhi ya kuambukiza.

  Alisema Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Muhammed Shein alimteuwa Mwenyekiuti wa Baraza hilo mwaka 2013 lakini kutoakana na kutokuwepo wajumbe ambao huteuliwa na Waziri anaehusika na Afya lilishindwa kufanyakazi kwa muda wote.

  Aliwataka wajumbe hao kuwa wabunifu katika kutafuta fedha za kusaidia kuendesha kazi bila kutegemea Bajeti ya Wizara kwani fedha wanazopata ni kidogo na haziwezi kuendesha Baraza kwa ufanisi.Ameeleza matumaini yake kwa wajumbe hao, kutokana na umahiri wao wa masuala ya Afya na Mazingira, watafanyakazi kwa mashirikiano na kuleta ufanisi mkubwa kwa jamii ambayo imetuzunguka .

  Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Omar Juma Khatib alimshukuru Waziri wa Afya kwa kuona umuhimu wa kuwepo Baraza hilo na kuharakisha kuteuwa wajumbe kuanza kazi rasmi.Ameahidi kuwa atashirikiana na wajumbe kuhakikisha kuwa wanapunguza vifo vinavyotokana na mazingira machafu na kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa .

  “Wajumbe kazi iliyopo mbele yetu ni muhimu sana kwani inagusa maisha ya watu wetu, hivyo tunapaswa kutoa michango na mapendekezo yetu katika kufanikisha kazi hii, ”alisisitiza Mwenyekiti.Wajumbe wa Baraza hilo wamemshukuru Waziri kutokana na muda mfupi tokea achukue nafasi hiyo kuona kunaumuhimu wa kuundwa rasmi Baraza kwa kufanya uteuzi wa wajumbe.

  Wameahidi kuwa watatoa ushirikiano wa karibu kwa Mwenyekiti wao ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuundwa Baraza la Ushauri wa Afya na Mazingira yanafikiwa .IDARAYA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisoma baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira kabla ya kulizindua Baraza hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi sheria Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib mara baada ya kulizindua.
  Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo wakati wa uzinduzi, kushoto yake Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
   

  0 0  0 0

  Na Allan Ntana, Kaliua

  MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora Hamis Seleman na Mkuu wa wilaya ya Kaliua Hadija Nyembo kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mauaji vinavyozidi kushamiri wilayani humo.

  Agizo hilo amelitoa jana katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Milenia mjini Kaliua.

  Alisema vitendo vya mauaji kwa raia wasio na hatia katika mkoa huo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku vikichochewa na imani za kishirikina, wivu wa mapenzi na ugomvi wa mali huku matukio mengi yakiripotiwa kutoka katika wilaya hiyo.

  Alibainisha kuwa takwimu zinaonesha mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye matukio mengi ya mauaji jambo ambalo hawezi kuliacha liendelee pasipo kuchukua hatua za makusudi za kukomeshwa kwa vitendo hivyo.

  ‘Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC), OCD Kaliua na Mkuu wa wilaya hakikisheni mtu yeyote atakayeua mwenzake akamatwe mara moja na afikishwe katika vyombo vya sheria’, aliagiza.

  Aidha aliwaagiza madiwani, watendaji wote wa vijiji na kata kwa kushirikiana na Kamati nzima ya ulinzi na usalama ya wilaya kusimamia ipasavyo agizo hilo ili kuhakikisha matukio ya namna hiyo yote yanakomeshwa na wananchi wanaishi kwa amani.

  ‘Ndugu zangu hatuwezi kukubali watu wandelee kuuana kama kuku, watendaji wa vijiji na kata toeni ushirikiano katika hili, leteni taarifa za wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa diwani au ofisi ya Mkuu wa wilaya ili kukomesha mauaji hayo,’ aliongeza.

  Aidha RC aliwataka madiwani wa halmashari hiyo kuhamasisha wazazi wote kupeleka watoto wao shule ili wapate elimu kwa kuwa msingi mzuri wa maisha ni elimu huku akiwaagiza kuchukua hatua kwa wote watakaokaidi.

  Agizo la Mwanri kukomesha mauaji katika wilaya hiyo liliungwa mkono na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Haruna Kasele, Mbunge wa jimbo la Ulyankulu John Kadutu, Mbunge wa jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya na Mkuu wa wilaya hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wa tatu toka kulia) akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya ya Kaliua jana,anayeongea katika kipaza sauti ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Haruna Kasele. (Picha na Allan Ntana)

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akifungua semina  kwa Wanaharakati pamoja na viongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa waliofika katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Geofrey Adroph)
  Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akitoa elimu kwa wanaharakati kuhusu utendakazi wao wa kila siku wakati wa semini iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao.
   Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Kibuko, Bw. Valentino Lukoo akitoa ufafanuiz kuhusu maendelea yaliyofikia katika kata yao baada ya kuonekana kwa changamoto nyingi katika kata hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Baada ya kukabidhi magari mawili na pikipiki kumi kwa wasikilizaji wake kupitia shindano la shikandinga , EFM redio inakuja na donge nono kupitia mchezo wa sakasaka ambao huchezeshwa kila mwaka toka kituo kianzishwe.

  Saka saka ni shindano ambalo efm redio huficha kitu katika eneo ambalo hata hivyo msikilizaji hupewa maelekezo yake ambapo atatakiwa kwenda katika eneo hilo na kukitafuta hicho kitu kulingana na shindano.

  Mwaka huu mchezo wa sakasaka utaanza tarehe 12/06/2016, utachezeshwa katika wilaya tano (5) ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga, na Kisarawe ambapo jumla ya kiasi cha milioni tatu (3) kushindaniwa katika kila wilaya.

  Ili kuweza kushiriki katika mchezo huu jamii inapaswa kusikiliza kwa makini vipindi vya redio ambapo atapata dondoo za jinsi mchezo utavyokua ukichezwa
  Lengo madhubuti la mchezo huu ni kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine kwani pesa ambazo watajishindia zitawasaidia katika maisha yao kiujumla kama biashara, familia, elimu, n.k

  “Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wanachangamoto nyingi za maisha hivyo kama redio tunawawezesha kwa kupitia vitu tofauti tofauti ambavyo vitawasaidia kujikwamua kimaisha”


  0 0

  Na Zaynab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Leseni za Klabu (Club Licensing) za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.

  Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya Juni 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatuamia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema.

  Tayari TFF imeteua Kamati ya Leseni ya Klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.

  Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.

  Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.

  Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.

  Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.

older | 1 | .... | 1248 | 1249 | (Page 1250) | 1251 | 1252 | .... | 3285 | newer