Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 123 | 124 | (Page 125) | 126 | 127 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo (kushoto) akiwania mpira na beki wa Ruvu Shooting,  Shaban Suzan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Simba ilishinda 3-1. (Picha na Habari Mseto Blog)
  Mshambuliaji wa Simba, Amri kihemba akimtoka beki wa Ruvu Shooting
  Kocha Mkuu wa Simba akiteta jambo na beki wa timu hiyo, Shomari Kapombe.

  0 0

  Waumini wakiwa katika taharuki kufuatia mlipuko huo wa bomu jijini Arusha leo. Chini makachero wa polisi wakifanya uchunguzi eneo la tukio. Picha na Woinde Shizza
  Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Kanisa Katoliki Arusha, Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Mwakilishi wa Papa, Nuncio, Francisco Montecillo Padilla kabla ya mlipuko huo. Viongozi hawa wa dini walinusurika na waliondolewa haraka eneo la tukio na wasaidizi wao wakiwa salama

  Taharuki mara baada ya mlipuko huo wa bomu

  Na Ahmed Mahmoud
  MTU mmoja amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu lililorushwa kwa waumini wa Kanisa Katoliki jana ambapo watu 66 wamejeruhiwa wakiwamo wanawake 41 na wanaume 25, huku majeruhi wawili hali zao zikiwa mbaya zaidi.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Magesa Mulongo alimweleza Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema,Naibu waziri wa mambo ya ndani Mhe Pereira Silima,na Naibu Waziri wa Nishati na Madini  Mhe Stephen Masele wakati walipowatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mount Meru jana jioni.
  Alisema kati ya majeruhi hao, wawili hali zao ni mbaya, huku mmoja akiwa akiwa amepelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
  Makamu wa Rais alitarajiwa kuondoka na majeruhi mwingine mtoto ambaye anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
  RC Mulongo alithibitisha kwamba aliyefariki katika tukio hilo ni mama mmoja wa kwanya ya Kimasai ambayo ilikuwa ikiimba kwenye shughuli za uzinduzi wa kanisa hilo.
  Akitoa pole kwa wagonjwa waliolazwa pia kwa wale ambao jamaa zao wamepata maradhara kwa tukio hilo, kwa waumini wa Kanisa Katoliki, kwa wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla, Dk Bilal alisema tukio hilo ni la aibu na baya sana.
  “Tukio hili ni la aibu sana, baya, limeshtusha kutokea hapa nchini, serikali inalaani na itafanya kila linalowezekana kuwatia mbaroni wahusika na tayari imekwishaanza kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
  “Vyombo vya usalama vimeagizwa kufanya kazi hii usiku na mchana kuhakikisha kwamba wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua,” alisema.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwema akitokea Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge ambako leo Wizara ya Mambo ya Ndani inawasilisha bajeti yake, alielezea tukio hilo kuwa ni la kushutua sana.
  “Ni tukio la kushtua, kusikitisha, tumefika eneo la tukio na mpaka sasa mtu mmoja amekamatwa na anaonyesha ushirikiano mzuri wa kutoa taarifa.
  “Tukio kama hili sio la mtu mmoja, wapo waliohusika katika kupanga, kuratibu, kushauri, kuchangia gharama na wale waliofanikisha. Hata huyu mmoja aliyekamatwa ni mchango wa ushirikiano wenu, naombeni muendelee kushirikiana na polisi katika kufanikisha uchunguzi huu.
  Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, ambaye aliambatana na Makamu wa Rais kutokea mkoani Shinyanga, alisema amesikitishwa sana na tukio hilo.
  Alisema tukio hilo sio la kawaida na limewashtua watu wengi wanaopenda amani lakini amewaomba waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linapoendelea kufanyiwa uchunguzi.
  “Wakristo tuendelee kuhubiri amani, kuombea amani kwa sababu Mungu wetu ni wa amani,” alisema.

  Majina ya waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospitali za  mount Meru, na hospitali teule ya jiji la Arusha ya St Elizabeth wametambulika kuwa ni:- John Thadei, Regina Fredirick, Joram Kisera, Novelt John, Rose  Pius, John  James, Anna Kessy, Joan Temba, Neema Kihisu, Gloria Tesha, Innocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, Simon Andrew, Anna Edward, Lioba Oswald, Rose Pius, Philemon Gereza,Kisesa Mbaga na Beata Cornell. 
  Majeruhi wengine na umri wao katika mabano, ni Consensia Mbaga (53), Christopher Raymond (10), Deborah Joachim (24), Elizabeth Isidori (24), Anna Didas (52), Bertha Cosinery (49), Edda Ndowo (77), Derick Cyprian (8), Faustine Andrea (35), Mary Okech, Mesoit Siriri (33), Clenes pius (22), Joyce yohana (15), Restituta Alex (50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James Gabriel (16), Regina James (17),Elizabeth Masawe(15), Elizabeth Sauli (18), Njau (35), Yasinta Msafiri (16) Doreen Pancras (28), Alex Arnold, Agripina Alex (9), James Gabriel (16), Loveness Nelson (17), Amalone Pius (25), Frank Donatus (10), Alphonce Nyalandu (26), Athanasia Reginald (14), Phillemon Ceressa (49), Neema Daud (13), Sophia Kanda (72), Theofrida Innocent (21) na Regina Darnes(17).
  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.  Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.  

  Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake. 


  Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.  Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.  
  "Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma.  Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu.  
  "Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake" amesema Rais ambaye anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.

   Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

  Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  IKULU,

  DAR ES SALAAM

   5 Mei, 2013


  0 0
 • 05/05/13--13:32: KAMERA IPO SOKONI
 • Sale sale ofa nzuri kwa wateja mzigo umeingia mjini pata zipo kamera za 160000 na 170000 unapata pia memorycard yenye ukubwa Wa 8 GB bureeeeee sambamba na kamera ulionunua wahi zinapatikana dar er salaam na zinatoka nchin sweden wasiliana nasi kwa email hii camera.sweden@gmail. Com au kwa sm no 0686276061

  0 0
 • 05/05/13--13:59: DKT. SHEIN AWASILI PEMBA LEO
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Wakuu wa vikosi vya Ulinzi Pemba alipowasili uwanja wa Ndege wa Karume,leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali na wananchi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba ,leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali na wananchi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba ,leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi aliyekaa katikati akitoa maelekezo kwa Watendaji Wakuu wakiwemo Wakuu wa Idara na Maafisa Bajeti wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Kikao cha ndani cha maandalizi kabla ya mawasilisho ya Bajeti ya Wizara hiyo inayotarajiwa kusomwa kesho mjini Dodoma, kilichofanyika katika ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma.

  Sehemu ya Watendaji Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishiriki katika mapitio ya nyaraka za bajeti ya wizara hiyo katika kikao cha ndani cha Maandalizi kabla ya Mawasilisho ya Bajeti ya Wizara hiyo inayotarajiwa kusomwa kesho mjini Dodoma.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi aliyevaa shati jeupe akimuelekeza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak AbdulWakil wa pili kutoka kulia akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mwamini Malemi katika Kikao cha ndani cha maandalizi kabla ya mawasilisho ya Bajeti ya Wizara hiyo inayotarajiwa kusomwa kesho mjini Dodoma.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali itachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika na tukio la mlipuko wa bomu lililosababisha mauaji ya mtu mmoja na kujeruhi wengine 59 wakiwemo watano waliojeruhiwa vibaya katika tukio lililotokea leo katika kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti mjini Arusha.

  Waziri Nchimbi amewataka watanzania kuwa watulivu wakati huu na kuviachia vyombo vya dola kufanya kazi yake na kwamba watanzania wanapaswa kuchukua tahadhari juu ya watu waovu wanaotaka kuwavuruga na kuwafarakanisha kwa misingi ya dini.

  Akihojiwa na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake leo mjini Dodoma Waziri Nchimbi amesema tukio hilo limetokea Mjini Arusha leo majira ya saa tano ya asubuhi wakati waumini wa Parokia hiyo walipokuwa wakiendelea na ibada ya misa kanisani hapo iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Arusha Josephat Lebulu pamoja na Balozi wa Vatican hapa nchini Fransis Padila .

  Waziri Nchimbi amesema tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu sita kwa ajili ya mahojiano juu ya tukio hilo na kwamba tayari Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Amme Silima na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IJP) Said Mwema wako mjini Arusha kusimamia hali ya usalama mjini humo.

  Amesema kwa sasa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la polisi inashirikiana na Wizara ya Ulinzi limeanza uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo ikiwemo chanzo cha tukio hilo pia.

  Aidha ametoa pole kwa wote waliofiwa na ndugu yao, waliojeruhiwa, Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha Josephat Lebulu pamoja na Balozi wa Vatican Nchini Tanzania Askofu Mkuu Fransis Padila” amesema Waziri Nchimbi.

  0 0

  Salasala Vision Group (SVG), ni kikundi cha wakazi wa salasala Kilimahewa wapenda maendeleo kichoanzishwa mwaka 2012. SVG ilianzishwa ikiwa na malengo ya kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na ulinzi kwa maeneo ya Salasala Kilimahewa. 

  Tangu SVG ilipoanzishwa mwaka jana, kundi hili limeweza kutekeleza mambo mengi katika mwaka mmoja; Kuanzisha ulinzi shirikishi katika maeneo ya Salasala kilimahewa, Kutengeneza uwanja wa michezo, kuchangia mavazi rasmi ya waendesha bodaboda, Kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wa SVG, Kuendeleza mahusiano na makundi mengine yenye malengo yanayoshabihiana na SVG.

   Katika kuazimisha mwaka mmoja, wanachama wa SVG wamepanda miti zaidi ya 1,500 katika maeneo yanayozunguka salasala kilimahewa. Zoezi hili endelevu linatarajiwa kuendelea mwezi wote wa Mei na kufikia zaidi ya miti 2,000 kupandwa.
  Wana SVG wakijiandaa na zoezi la upandaji miti 1,500.
  Wakazi wa kilimahewa wakichangamkia zoezi la kupanda miti.
  Zoezi la upandaji miti liliendeshwa mitaa mbalimbali ya kilimahewa.
  Watoto pia walishiriki kwenye zoezi la upandaji miti.

  0 0

  Mshindi wa shindano la mrembo wa Redds Miss Hai 2013 Winnie Shayo( katikati) mshindi wa pili Mary Chemponda (kulia kwake) na mshindi wa tatu Catherine Leonard wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi.
  Mwakilishi wa TBL wilaya za Siha na Hai ,Edimund Rutaraka akikabidhi pesa taslimu kwa mshiriki wa shindano la kumtafuta Redds Miss Hai 2013 aliyeshika nafasi ya tano.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Hai.

  0 0
 • 05/05/13--15:12: BAD GYAL MUSIC VIDEO PROMO

 • 0 0


  KAMATI ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo kwa kila mchezo.


  Majina ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa kupata majina.

  Pia vyama viwili vya michezo ya  paralimpiki na baiskeli bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu pia kimeshindwa kuwasilisha majina.

  Hatua ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.


  0 0

  Wachezaji wa Timu ya KMKM wakiwa pamoja na kocha wao Ally Bushiri wakishangilia ubingwa wa soka wa ligi kuu ya soka ya Grandmalt huko Zanzibar walioupata hivi karibuni.
  Wachezaji wa Timu ya KMKM,Uongozi wa ZFA pamoja na Viongozi wa Grand Malt wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kombe hilo la Ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar inayodhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt.
  Nahodha wa timu ya KMKM,Maulid Ibrahim akipokea kombe na mfano wa hundi ya Shilingi milioni kumi toka kwa mgeni Rasmi Waziri Asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Machano Othman mara baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya soka ya GrandMalt.

  0 0


   Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo lililofungwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
   Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Profesa Fredy Mhalu akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
   Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Washiriki Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kongamano hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 


  =======  ======  ========

  MUHAS yaaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti 


  CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili (MUHAS) kimeaswa kuzidi kujenga uwezo wa ufanyaji tafiti mbali mbali zinazohusiana na masuala ya afya ili kuimarisha huduma ya afya nchini.

  Akizungumza wakati wa sherehe za kufunga kongamano la Kwanza la Sayansi lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mganga Mkuu, Dk Donan Mmbando, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alisema kuwa ili kuboresha huduma za afya nchini kuna haja ya watafiti na wataalamu kuendelea kutafuta njia za kuimarisha huduma hiyo licha ya changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta hiyo.

  "Utaalamu katika kutafuta njia za kuboresha huduma za afya ni muhimu kwa watanzania wote. Nawasihi kuendelea kufanya tafiti lakini pia kuyatumia matokeo haya ya kitafiti kikamilifu ili kusaidia serikali kuboresha huduma ya afya kwa wananchi, "alisema Dk Mmbando.

  Alibainisha kuwa ili kuboresha ,masuala ya afya wafanyakazi katika sekta hiyo wanahitaji kupewa mwanga zaidi kuhusiana na masuala ya afya na kupitia makongamano watapata elimu zaidi juu ya jinsi gani wanaweza boresha utoaji wa huduma za afya na kuleta ufanisi katika kazi yao.

  "Tunahitaji kuendelea kukuza maarifa kwa kuendelea kuandaa makongamano ya aina hii zaidi hususani ya tafiti za masuala ya kisayansi na afya kwa kuwa yanatoa fursa za kubadilishana uzoefu na kutafuta mbinu mbali mbali za kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya afya.

  "Makongamano ya kisayansi kama hili tunalofunga leo hii utoa fursa nzuri katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto nyingi za afya hususani jinsi gani ya kukabiliana na magonjwa kama malaria na vvu/ukimwi," aliongeza

  Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo hicho, Profesa Efata Kaaya aliipongeza serikali kwa kukiunga mkono chuo hicho hususani katika utoaji wa fedha ili kusaidia kufanikisha tafiti mbali mbali za kisayansi na kiafya zinazofanywa na chuo hicho nchini.

  “Naishukuru serikali kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kipindi kirefu katika tafiti zetu hususani katika utoaji wa fedha ili kufanikisha tafiti hizi. Naimani kutokana na mchango huo, wataalam wetu wataendelea kutafuta mbinu jinsi ya kuboresha huduma za afya nchini,” alisema Profesa Kaaya.  

  0 0


   Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa  ikiwa ni msaada ulitolewa kuchangia elimu  toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila, anaeshuhudia wakwanza kulia ni  Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga

  Kulia ni Afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikimkabidhi kati ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Mwishoni mwa wiki Airtel ilitoa vitabu kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu,  Kwendimu na Magila,. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga.

  ==========  ========   =======
  Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Tanga.

  •       Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu Tanga ni shule ya sekondari
  ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila
  •       Airtel yaahidi kuingia katika awamu mpya ya ugawaji wa vitabu kwa
  sekondari kila mkoa nchini.


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vitabu
  vya hesabu,chemistry na baologia vyenye thamani ya shilingi milioni 12
  kwa shule nne za mkoa wa Tanga. Msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel 
  wa kusaidia ukuaji wa sekta ya limu kupitia kampeni yake ya shule 
  yetu.

  Akipokea vitabu hvyo kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu
  wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa alisema, “ Tunawashukuru
  Airtel kwa msaada huu wa vitabu kwani utasaidia kupunguza tatizo la
  uhaba wa  vitabu kwa shule zilizopatiwa msaada huo na kuongeza kiasi
  cha ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi zisihishie hapa
  ziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine ya
  Tanzania ili kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu
  bora kwani hawa ndio taifa la kesho.


  Kwa upande wake meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro
  Bw. Edmund Lasway amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni
  yake wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu
  wa Shule yetu tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.

  Akiongea kwa niaba za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa
  shule ya secondari ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema”  Tunatoa
  shukurani kwa Airtel kwa msaada wa vitabu katika shule zetu za
  sekondari, kwa hatua hii itasaidia kupunguza tatizo la vitabu
  linalozikabili na kuongeza ufanisi katika masomo ya sayansi.
  Tunawaomba wanafunzi wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani
  ni nyenzo muhimu katika elimu ya sekondari.

  Vilevile Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni
  alidokeza kuwa Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya
  ugawaji wa vitabu kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni
  program yake ya mwaka huu ya kurudisha kwa jamii kupitia elimu
  “tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa vitabu kwa shule ngingi
  zaidi  kila mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule
  za sekondari zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi
  zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa
  kusaidia jamii wa Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.
  Airtel toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita
  tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania
  kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika
  kila kona ya Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye
  maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango
  cha elimu kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.

  Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja
  na shule ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.
  mkakati ni kuendelea kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini ambapo
  droo ya shule za sekondari zitakazo faidika na vitabu kwa mwaka huu wa
  2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni  na kutoa nafasi kwa shule nyingine
  nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa Airtel shule yetu.

  0 0

  Mwenyekiti aliemaliza muda wake wa Umoja Veteran Bwana Nuhu akimkabidhi nguvu ya kuendeleza klabu Mwenyekiti mpya Ndugu Mallisa. Wakiangalia kwa makini ni Elia (Mweka Hazina) na Shaban michezo (Msemaji wa Klabu).

  0 0


   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana jioni kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, kama Mgeni rasmi sambamba ya kuzindua Shule ya Taasisi hiyo inayofundisha masuala ya urembo.
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akishiriki kukata Keki na Maza Sinare, ambaye ni mmiliki wa Saluni ya Maznat, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, jana Mei 5, 2013, sambamba na sherehe hizo pia Mama Asha, alizindua rasmi shule ya masuala ya Urembo inayosimamiwa na Taasisi hiyo. Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, jana, sambamba na sherehe hizo pia Mama Asha, alizindua rasmi shule ya masuala ya Urembo inayosimamiwa na Taasisi hiyo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mohamed Shein,akizindua mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa kwa kuuwasha huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,(kulia) Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Tanzania Bara,Dk.Fenelle Mukangara,na Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Zainab Omar Mohamed,(kushoto).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mohamed Shein,akizindua mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa baada ya kuuwasha huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mohamed Shein,akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Juma Ali Sima,(kushoto) kutoka Mkoa wa Kusini Unguja,baada kuzindua rasmi mbio hizo Kitaifa huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

  0 0


  New Picture (9)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.

  Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.

  Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.


  0 0

  The Italian Ambassador Hon. Pierluigi Velard (Third right) Adressing the media, Earlier today during the press confernce.
  The Egypt Air country Managing Director Mr. Hany Osman, insisting something to the media, earlier today.
  Mr. Gabrielle Maneo from ST.Gaspar Hospital Singida, adressing the press (not on the picture), Earlier today during the press conference held at the Golden Tulip Hotel.

  The Embassy of Italy is organazing a Charity Concert on 7th May 2013 at the Golden Tulip Hotel with a group called " TWO HOT DALTONICS" from Italy. The funds raised shall be donated to the St. Gaspar Refferal Hospital of Itigi, Singida region..

  The two artistes Vito Mannarini and Giuseppe Pascucci from Italy will perform during the concert. “we are very happy to be In Tanzania for the first time and be part of this noble project” said Vito Mannarini

  The Hospital urgently needs a new Operating Table for the Operation Theater as the old one is broken. The new Operating table which costs to the tunes of Usd 15,000 will serve about 600 patients annually who receive major operation and 900 patients annually who receive minor operation at the Hospital.

  “We look forward to the Support from the public to attend this concert and get to know the sights and sound of Italy which at the end will benefit the people in Singida region” stated the ambassador Mr. Perluigi Velardi. The tickets for the charity Concert is pegged at Tzs 70,000 and is available from the Embassy of Italy and Golden Tulip Hotel.

  The event is sponsored by Golden Tulip Hotel, Egypt Air, Advertising Dar, Dar Life, Cetawico, Dar Guide, Eventlites and 361 Degrees

  ABOUT TWO HOT DALTONICS

  Was Born during the warm winter of 2010 and is an experience joined by Vito Mannarini (guitar) and Giuseppe Pascucci (guitar), two artists who come from different musical backgrounds. Vito Mannarini graduated in classic guitar in 2008 with merit at the “N. Piccinini” Conservatory in Bari. Giuseppe Pascucci started playing the guitar at 14 and has a different background. He is a self taught instrumentalist, he studied briefly with Marco Mannarino, through which he found the passion for improvisation and jazz.

  At the end of 2009 Vito Mannarini discovered the art of improvisation that pushed him to form with fellow guitar player Giuseppe Pascucci the project TWO HOT DALTONICS, with which he explored the jazz sounds of the beginning of the 20th century. It is through this interest that they studied in depth that period of time when jazz music was just starting and artists such as “Fats” Waller, “Jelly Roll” Morton up to the music of T. Monk.

  Thanks to the variety of their repertoire, they played in different venues, music festivals, radio programs and book readings. “To play music” is the best expression to understand the way they approach music, making each song different and new every time, while enjoying every single note for our and all the audience’s pleasure.

  ABOUT BENEFICIARY - ST GASPAR REFFERAL HOSPITAL.Itigi – Singida Region

  St. Gaspar Referral Hospital is now 23 years old with an approved capacity of 320 beds. It is run by the Society of the Precious Blood Catholic missionaries and is situated at Itigi town in central Tanzania.

  The hospital provides residential consultancy services in paediatrics, general surgery, obstetrics and gynaecology. The AMREF, based in Nairobi continues to provide outreach consultancy services in orthopaedics, ENT and urology twice per year for each discipline. The Bambino Gesu hospital in Rome maintains its voluntary consultancy visits for plastic surgery and cardiology.

  0 0

  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Deric Siprian Kessy (8) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto kwa Makamu ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo na (kulia) kwa Makamu wa Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa mahututi, aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa Kanisa hilo.
  Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha. Picha na OMR

  0 0

  Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Bara),Ndugu Philip Mangula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sudani nchini Tanzania, Dr. Yassir M. Ali aliemtembelea leo kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.Picha na Adam Mzee.
  Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Bara),Ndugu Philip Mangula akiagana na Balozi wa Sudani nchini Tanzania, Dr. Yassir M. Ali mara baada ya mazungumzo yao leo.Picha na Adam Mzee.

older | 1 | .... | 123 | 124 | (Page 125) | 126 | 127 | .... | 3272 | newer