Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1247 | 1248 | (Page 1249) | 1250 | 1251 | .... | 3348 | newer

  0 0

  MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) yaadhimisha siku ya mazingira duniani kutokana na kutambua umuhimu wake kwa kuwa na mitambo mbalimbali ambayo inazalisha hewa ambayo inaweza kuharibu mazingira.

  Hayo ameyasema Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mazingira wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Thobias Mwasobwa amesema kuwa shughuli za bandari zianaenda na mitambo hivyo suala mazingira hawawezi wakaliacha likiharibu mazingira.

  Amesema kuwa tangu kuanza kwa maadhimisho hayo wametoa elimu kwa watu 60 ambao watakuwa mabalozi katika utunzaji wa mazingira katika sehemu zao kazi kutokana na shughuli nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zikaharibu mazingira. Aidha amesema wataendelea kutoa elimu zaidi juu mazingira na mabadiliko ya nchi kama mamlaka inalitambua na wanadhibiti jinsi ya kuweza kuhifadhi mazingira 
   
  Baadhi ya wafanyakazi wa mamraka ya Bandari TPA wakifanya usafia katika eneo la Chuo Cha Bandari Dar es Salaam jana kwa ajili ya maadhimisho ya Usafi wa mazingira duniani.

  0 0

  Na. Hadija Maulid - Chuo Kikuu Ardhi. 

  Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.

  Wito huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.

  Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).

  Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.

  Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.
  Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha.
  Wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Maximilian walipotemblea Maabara ya Sayansi ya Mazingira na Tekinolojia ya Chuo Kikuu Ardhi. Maabara hiyo hutumika kwa ajili ya shughuli za Ufundishaji, Utafiti na Uhauri wa kitaalamu katika fani ya Sayansi ya Mazingira.
  Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
  Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.
   

  0 0

  Baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es salaam, wakiwa katika soko la Buguruni wakijipatia mahitaji yao kufuatia kuanza kwa Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kwa mujibu wa wananunuzi hao,wameiambia Globu ya jamii kwa nyakati tofauti kuwa bei ya bidhaa hizo aghalabu zina unafuu,mahitaji hayo ni ya kuridhisha japo baadhi yao wamelalamikia kupanda kwa bei ya baadhi ya vyakula ikilinganishwa na siku za kawaida.
  Kwa upande wa matunda bei zake ni kama ionekanavyo hapo.
  Mihogo, Viazi na Magimbi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya China, Bi. Zhang Shuo alipofika Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao Bi. Zhang alieleza nia ya Benki yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 07 Juni, 2016.
  Sehemu ya ujumbe ulioongozana na Bi. Zhang wakifuatilia mazungumzo. 

  Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) pamoja na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Bi. Zhang (hawapo pichani). Kulia ni Bw. Ali Kondo na Bw. Humphrey Shangarai (katikati). 


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Jamal Athuman (kulia) akishirika katika kufanya usafi wa mazingira eneo la makao makuu ya TCAA Banana, Ukonga jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira uliyofanyika mwishoni mwa wiki.Kushoto ni afisa wa Mamlaka hiyo Adnan Mvungi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Jamal Athuman (kushoto) akishirika pamoja na wafanyakazi wenzake katika kufanya usafi wa mazingira eneo la makao makuu ya TCAA Banana, Ukonga jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira iliofanyika mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Grace Kiunsi(kushoto)na Mwanaidi Kaku wakishirika katika kufanya usafi wa mazingira eneo la makao makuu ya TCAA Banana, Ukonga jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira uliofanyika mwishoni mwa wiki.
  Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa (TUGHE) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Samwel Pastory akifafanua jambo kwa wafanyakazi wenzake wakati walipokuwa wakifanya usafi wa mazingira mazingira eneo la makao makuu ya TCAA Banana, Ukonga jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira uliofanyika mwishoni mwa wiki.

  0 0

  MAMA ni miaka tisa (9) bila wewe katika maisha yetu ya kila siku, tunakukumbuka daima. UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku mama hatuna la kusema, umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi. 


  Ushauri wako tutaendelea kuufuatilia na mema uliyotufundisha. Daima tutaendelea kukumbuka hekima na busara zako huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe pamoja na Maria (IA). 

  DAIMA huachwi kukumbukwa na Mumeo George Mapango, wanao Mariam, Eva (Hawa), Jackson, Rose, Patrick (Said) na Richard, Wadogo zako, Kaka zako, Wakwe zako, Marafiki, Wafanyakazi Wenzako pamoja na Wajukuu zako. 

  INNA LILLAH WAYNA ILAYH RAJ’IUN .

  0 0  0 0

   Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akiwaongoza Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo kumpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu hao wa Idara walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam.
   
   Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jenita Ndone akimpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam
  Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edwin Makene (kulia) akimpa pole Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira kwa kufiwa na mdogo wake, Fredina Mbasha. Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo walienda kumfariji kiongozi huyo nyumbani kwa marehemu, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi (kulia) wakati Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo walipoenda kumfariji kiongozi huyo, baada ya kufiwa na mdogo wake, Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nonela Sisamo, Shemeji wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  SERIKALI imesema kisiwa cha shungimbili kilichopo Wilayani Mafia mkoani Pwani hakijauzwa kwa kampuni ya Zululand ya Afrika Kusini na badala yake kimeingizwa katika uwekezaji kupitia kampuni ya Thanda Tanzania Ltd inayojenga hoteli ya kitalii.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mwanakwerekwe (CCM), Ali Said Khamis, leo Bungeni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema Alisema uwekezaji huo umepitia taratibu zote za Serikali na pindi utakapokamilika mwekezaji atatekeleza wajibu wake ikiwemo kulipia tozo zote kwa mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria.

  Makani alisema alisema kisiwa cha shungimbili ni miongoni mwa visiwa 15 ambayo ni maeneo tengefu yanayosimamiwa na Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini (MPRU).

  Mhandisi Makani alisema MPRU iliianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge na.29 ya mwaka 1994 ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia maeneo yote yaliyotangazwa kuwa hifadhi za Bahari na maeneo tengefu ya bahari.

  Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ndiyo yenye dhamana ya kuingia mikataba  yote ya kimataifa yenye maslahi kwa Taifa.

  Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida, Martha Mlatta, Makani alisema Serikali inaendelea kuvijengea uwezo vyuo vya utalii vilivyopo nchini ili kuhakikisha kuwa wahitimu wake wanakuwa mahiri katika soko la ajira nchini.

  “Mfanyabiashara akitafuta mwajiriwa ni lazima ahakikishe kuwa anaye mwajiri anakuwa na sifa zote za kumletea faida, hivyo na sisi pia tunataka wahitimu wetu katika vyuo vya utalii wanakuwa wanapata umahiri wa kutosha ili waweze kuajiriwa katika nafasi za juu kabisa katika kampuni yoyote”   alisema Makani.

  Mbunge Mlatta alitaka swali lake la nyongeza alitaka kufahamu Serikali ina mikakati ipi katika kuhakikisha kuwa wahitimu wa Tanzania wanapewa nafasi za juu za kazi katika hoteli za kimataifa.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

  Dkt Kayandabila ameyasema hayo leo hii jijini Dare s Salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds Fm.

  “Sisi kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji na tuko mbioni kumaliza tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji wa kodi hizi za nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa wananchi na hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.

  Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye makubaliano ya pande zote mbili kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na kushauri kama watashindwa kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.

  Awali ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika kwa Sera ya nyumba ambayo iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote na kwa kiasi kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba kwa ujumla.

  Mwaka huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali kutungwa kwa sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

  0 0


   Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles  mkumbo akiwa anaongea na viongozi wa dini zote wa mkoa wa Arusha hii  ikiwa ni mkutano wa kwanza wa kufanya na viongozi hao tangu kuwasili mkoani hapa
   Picha ya juu na chini ikionyesha baadhi ya mashehe ,askofu,wachungaji ,madiwani pamoja na askari waliohudhuria katika mkutano ulioandaliwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongea na viongozi wa dini juu ya namna gani ya kuendelea kudumisha amani ya nchi na mkoa kwa ujumla mkutano uliofanyika katika ukumbi wa polisi mesi uliopo jijini hapa

   Habari picha na 
  Woinde Shizza, Arusha
  Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Charles  mkumbo amewataka
  viongozi wa dini mkoani Arusha kuakikisha wanaubiri amani katika
  nyumba zao za ibada ili kuweza kuweka hali ya usalama na amani katika
  mkoa wa Arusha.

  Aliyasema hayo juzi katika   kongamano la siku moja la viongozi wa
  dini mkoani Arusha katika kongamano la viongozi wa dini mkoa Arusha
  lilondaliwa na kamanda mkumbo  na kuwashirikisha madiwani wa jiji la
  Arusha pamoja na viongozi wa kisiasa.

  Aidha kwa upande wake meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiwa kama
  mmojawapo wa washiriki wa kongamano hilo na kueleza kuwa ujio
  kongamano hilo liloandaliwa na kamanda Mkumbo ni kuonyesha mwelekeo
  mzuri wa kulinda amani ya Arusha.

  Aidha pia meya wa jiji la arusha alitumia muda huo kuwaasa
  wafanyabiashara hususa ni wauzaji wa chakula pamoja na vinywaji vikali
  kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa kufuata sheria ambapo alisema
  kuwa airuhusiwi sehemu ambayo inauza chakula kuuza vinjwaji vikali
  ikiwemo bia pamoja na pombe

  "unaja sasa ivi tunataka tufanya mji wetu safa hairusiwi mtu anaeuza
  pombe kuuza chakula na chakula kuuza pombe pia  kumekuwa na tatizo la
  sehemu nyingi apa mjini kufungua mziki kama wanavyotaka sasa sasa hivi
  airuhusiwi mtu yeyote kufungua mziki mkubwa iwe kwenye bar au grosary
  pasipo kuwa na kibali rasmi kutoka sehemu husika hii pia inawahusu
  hawa vijana ambao unakuta wanaingiza nyimbo kwenye cd yaani unakuta
  kafungua mziki hadi kero  inakuwa usumbufu sasa kuanzia sasa hivi
  airusiwi mtu kufungua mziki mkubwa pasipo kibali"alisema Kalist

  Aidha alisema anaimani swala hili litafanikiwa kwakuwa polisi
  wameshaamua  kushirikiana nao na watafanya kazi kwa umoja hadi
  waakikishe mji wao unakuwa tulivu na msafiki.

  Wakati huo huo mchungaji wa kanisa la Angilkana mchungaji  Kenoni
  Kajembe alisema kuwa wao  kama  viongozi wa dini mkoani hapa wana
  jukumu kubwa la kuakisha kwamba dhima ya amani inajulikana kwa waumini
  wao wanaowaongoza.

  Kongamano kama hilo linatarajiwa kufanyika mfululizo katika wilaya
  sita zilizobakia za mkoa wa Arusha na wiki  hii na na pia  kamanda
  Mkumbo anatarajiwa kufanya kongamano la amani kama hili na viongozi wa
  serekali za mitaa ndani ya jiji la Arusha.
   Mashehe kutoka katika misikiti mbalimbali ya mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na  kamanda wa polisi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha akiwemo meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
   Wachungaji kutoka katika madhehebu mbalimbali wakiwa  katika picha ya pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha pamoja na meya wa jiji 

  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha pia aliwataka baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo kupiga na viongozi hao picha ya pamoja

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Umoja wa Mafundi Gereji Wilaya ya Kinondoni,Umemkabidhi madawati 100 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikiwa ni sehemu ya kuunga kampeni ya mkuu wa mkoa huyo ya kuchangia madawati.

  Akizungumza na Mafundi hao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa umoja huo umekuwa na watu wenye kujitoa katika juhudi za serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kusomea.

  Makonda amesema kuwa kwa unyonge wao, wameamua kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Pombe Magufuli katika suala zima la upatikanaji wa madawati kwa shule mbalimbali,hivyo Makonda amebainisha kuwa hilo ni jambo jema katika suala zima la kuunga mkono Serikali na kwamba hata Rais pia atafurahi kusikia na kuona hata watu kadhaa kwa unyonge wao wanatoa sehemu ya mkate wao.

  Wakati huo huo Umoja wa Mafundi wa Gereji wa Wilaya Kinondoni wametengeneza magari ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa zaidi ya Sh.Milioni 42 ikiwa ni sehemu kusaidia ofisi hiyo wafanyakazi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutoa huduma kwa wananchi.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema bila ya madereva hao kutokea kuna baadhi ya watumishi walikuwa tayari wanajiandaa kununua magari hayo.Makonda amesema kuwa kutengeneza magari hayo kuna baadhi ya watu walikuwa wanaombea suala hilo lishindikane lakini mafundi wameonyesha uwezo wao kwa kutengeneza bure ikiwa ni sehemu kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Pombe Magufuli.

  Amesema wapo watu wanauwezo lakini wameshindwa kusaidia isipokuwa mafundi wamedhubutu kutengeneza magari ya serikali kwa gharama yao wenyewe.Makonda amesema kuwa mafundi gereji kwa mara ya kwanza watakuwa wameandika historia ya dunia kujitoa kwa kutengeneza magari serikali bure watumishi wasiweze kutengeneza mazingira ya kukaa ofisini kutokana na kukosa usafiri.

  Mkuu wa Mkoa kwa awamu ya kwanza amekabidhiwa magari manne yaliyongenezwa na mafundi gereji yaliyo gharimu zaidi ya sh.milioni 17 na magari mengine yatagharimu za zaidi ya sh.milioni 25 .

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na viongozi wa umoja wa mafundi gereji ambao walikuwa wanamkabidhi magari manne  waliyotengeneza bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam. 
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hayupo pichani leo jijini Dar Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI 

  Ndugu zangu waandishi wa habari,

  Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).

  Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.

  Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa. 
  Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. 

  Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili. Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.

  Asanteni sana kwa kunisikiliza .

  Imetolewa na:-
  Nsato M. Mssanzya – CP
  Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0


  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako baada ya mapumziko ya wachazaji yanayoishia Juni 10, 2016 ambapo Juni 15 - 30 itakuwa ni uhamisho wa wachezaji na kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15 hadi Juni 30, mwaka huu.

  Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wachezaji.

  Usajili wa wachezaji utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.

  Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili, ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.

  TFF YATANGAZA KOZI ZA UKOCHA.


  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Idara ya Ufundi, imetangaza kozi nne (4) za Leseni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinazotarajiwa kuanza Juni 20, 2016 katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam. Kwa Mkoa wa Mwanza, TFF itaendesha kozi ya leseni Daraja C. kozi hiyo inatarajiwa kuanza Juni 20, 2016 hadi Julai 4, mwaka huu ambako baadhi ya washiriki 29 wamekwisha kujiandikisha ingawa bado kuna nafasi 11 ili kutimiza darasa la wanafunzi 40.

  Sifa za watakaochukua kozi hiyo ni kuwa kuwa na cheti ngazi ya kati (intermediate) na umahiri (activeness). Hii ni kozi ya CAF itakayoendeshwa na TFF na kwamba watu wenye ndoto za kuwa makocha wa mpira wa miguu wanaruhusiwa kuomba na kwa Jiji la Mwanza na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, kozi hiyo inaratibiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Vedastus Rufano na Mwalimu atakuwa Wilfred Kidao ambaye ni Mkufunzi wa ukocha anayetambuliwa na CAF.

  Kozi nyingine ni ya leseni Daraja B ambayo itafanyika kuanzia Julai 1, hadi Julai 16, mwaka huu mkoani Morogoro na utaratibu wa kujiunga unaratibiwa na Ofisi ya Idara ya Ufundi ya TFF iliyoko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam na kwa upande wa Dar es salaam ambayo kuanzia Julai 1, hadi Julai 16, mwaka huu ambapo washiriki wa kozi hiyo ni ya TFF makocha ambao tayari walifanya kozi ya FIFA-IOC iliyofanyika Oktoba, 2014 hivyo kwa sasa wanatakiwa kuthibitisha kushiriki kabla ya Juni 15, 2016 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.

  Kadhalika kozi nyingine ji ya Leseni Daraja A ambayo itafanyika kuanzia Julai 17, 2016 hadi Julai 31, mwaka huu kwa hatua ya kwanza yaani Module 1 wakati Module 2 itafanyika Novemba, mwaka huu. Wakufunzi wa kozi hiyo ya juu ni Makocha Salum Madadi na Sunday Kayuni, kabla ya CAF kumleta mtoa tathimini ya matokeo ya makocha hao kabla ya kutoa leseni ya daraja husika.

  Washiriki wa kozi hiyo wanatarajiwa kuwa makocha wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwani msimu wa mwisho wa makocha wa Leseni Daraja B na C ni msimu wa 2016/2017.

  0 0

  Mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee amesema yuko tayari kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kuvitangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani nab nje ya nchi.
  Mdee ametoa ahadi hiyo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na uongozi wa Bodi hiyo kuhusu namna TTB inavyoweza kushirikiana nae katika kutangaza na utalii wa Tanzania.
  Ujio huo wa mwanamziki huyo ambaye pia ni nguli wa miondoko ya R&B, Hip Hop, na Afro Pop ulifuatia mwaliko wa uongozi wa TTB kuomba kukutana na kuzungumza na mwanamuziki huyo katika azma na mkakati wa TTB kuwatumia wasanii na watu wengine maarufu nchini katika kutangaza Utalii wa Tanzania.
  Katika mazungumzo hayo Vanessa Mdee amesema yuko tayari kufanya kazi na TTB kwa lengo la kutangaza vivutio vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa balozi wa hiari wa Utalii 
  “ Tutaendelea kujadiliana kuona ni namna gani nzuri tunaweza kushirikiana, na mimi niko tayari kuifanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa hiari wa Utalii” alisema Mdee.
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi alielezea kufurahishwa kweke na utayari wa Vanessa Mdee katika kuunga mkono juhudi za TTB katika kuutangaza na kuundeleza Utalii wa ndani sambamba na ule wa Kimataifa, na kuahidi kukamilisha haraka mchakato mazungumzo hayo na hatimaye kusainiwa kwa makubaliano baina ya pande hizo mbili.
  Katika kutekeleza jukumu lake la kuitangaza vivutio vya Utalii Tanzania ndani na nje ya nchi Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikibuni na kutekeleza mbinu na mikakati mbalimbali kama vile kuweka matangazo katika televisheni za kimataifa, kutumia mitandao ya kijamii viwanja vya mipira ya miguu, kuandaa safari za waandishi wa habari, kutumia watu maarufu na njia nyinginezo nyingi.

   Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi (kulia) akijadliana jambo na Vanessa Mdee  leo walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania.
  Vanessa Mdee Mdee (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB (kushoto), Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Meneja Masoko wa TTB  Bw. Geofrey Meena.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.Dkt Kayandabila ameyasema hayo leo hii jijini Dare s Salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds Fm.

  “Sisi kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji na tuko mbioni kumaliza tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji wa kodi hizi za nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa wananchi na hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.

  Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye makubaliano ya pande zote mbili kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na kushauri kama watashindwa kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.

  Awali ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika kwa Sera ya nyumba ambayo iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote na kwa kiasi kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba kwa ujumla.

  Mwaka huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali kutungwa kwa sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na viongozi wa umoja wa mafundi gereji ambao walikuwa wanamkabidhi magari manne  waliyotengeneza bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na viongozi wa umoja wa mafundi gereji ambao walikuwa wanamkabidhi magari manne  waliyotengeneza bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
   Magari yaliyotengenezwa bure na mafundi hao
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiendesha moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wamiliki wa magari makubwa (Maboza) ya kusambaza huduma ya Majisafi katika maeneo ambayo bado haijafikiwa na huduma hiyo jijini Dar es salaam, wametakiwa kutumia magari hayo kusambaza Majisafi na salama ili kuepukana na adha ya kuugua magonjwa ya mlipuko yakiwamo magonjwa ya kipindupindu kwa watumiaji wa Maji hayo.

  Hayo yamezungumzwa na Afisa mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja katika kikao cha pamoja na wamiliki hao wa magari ya kusambaza huduma ya Maji kwa wananchi waishio jijini Dar es salaam na mkoa wa Pwani.

  Mhandisi Luhemeja, amewataka wamiliki hao kujali afya ya wateja wao ambao ndio watumiaji wakuu wa Maji hayo kwa kusambaza huduma ya Majisafi na salama ili kuepuka adha ya kuugua magonjwa ya mlipuko yakiwamo magonjwa ya kipindupindu, kwani Dawasco imewaamini na kuwapa kibali cha kusambaza Maji kwa wananchi.

  “Tumieni Magari yenu kusambaza Majisafi na salama, tumewaamini tumewapa kibali cha kutoa huduma ya Majisafi na salama kwa wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma hii, kuweni wawakilishi wazuri ili kwa pamoja tujenge nchi yetu” alisema Luhemeja.

  Aidha, Mhandisi Luhemeja ameahidi kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hiyo, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazokwamisha utoaji wa huduma hiyo, ili wamiliki hao waweze kutoa huduma bora kwa wateja pamoja na wananchi wote.

  Naye, mwenyekiti wa umoja huu wa wamiliki wa magari ya kusambaza huduma ya Maji Bw. Fredrick Mayunga amepongeza juhudi zinazofanywa na Dawasco pamoja na ushirikiano mzuri uliopo baina yao na shirika, kwani unawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kufanya kazi na kuwa wawakilishi wazuri kwa jamii wanayoihudumia.

  “Tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu, namna ambavyo mnatambua umuhimu na mchango wetu katika kutoa huduma ya Maji kwa wananchi, tunaahidi kutoa huduma bora kwa jamii kwa kusambaza Majisafi na salama kama Afisa Mtendaji mkuu alivyoagiza” alisema Mayunga.

  Dawasco iliamua kushirikiana na wamiliki wa maboza kwa kuanzisha vizimba vya Maji kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo ambayo hayana miundombinu ya Majisafi.
  Mmoja wa wamiliki wa magari yakusambaza huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo ya Maji Steven Peter akichangia kwenye kikao cha pamoja cha wamiliki wa maboza na Dawasco kilichofanyika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es salaam. 

  0 0

  Jaji Kiongozi mpya Mhe. Ferdinand Leons KatipwaWambali

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021 unalenga kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha Sekta zinazoajiri watu wengi na walio masikini zinakuwa kwa kasi. 
   Akizindua Mpango huo leo (Jumanne, Juni 7, 2016) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itahakikisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Uvuvi na Mifugo zinakua kwa kasi ya kuridhisha ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini. Amesema utekelezaji wa Mpango huo ambao umefungamanisha maendeleo ya viwanda na maendeleo ya watu na unatazamiwa kujibu changamoto ya umasikini Tanzania. 
   Waziri Mkuu amesema katika Mpango huo kuna maeneo mbalimbali ya vipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango huo ni miradi mikubwa kama ya chuma cha Liganga, kufufua shirika la Ndege, Makaa ya Mawe Mchuchuma, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha standard Gauge ambayo matokeo yake yanatarajiwa kuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mingine. 
   “Tunatarajia ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga nchi ambayo ina maisha bora, yenye amani, umoja na utawala bora, jamii inayojifunza na iliyoelimika, yenye uwezo wa kuzalisha na kuwa na ukuaji wa uchumi endelevu na wenye ushindani,” amesema. 
   Waziri Mkuu Majaliwa amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ukuaji huo wa uchumi unakuwa shirikishi zaidi katika utekelezaji wa Mpango huu na kwamba uendelezaji wa viwanda ndio utakaoleta mafanikio makubwa karika mwelekeo huo. 
   Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema jumla ya viwanda 39 kati ya 106 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambavyo vilikuwa vya vinazalisha bidhaa za chuma, ngozi, korosho zana za kilimo, sabuni na mafuta ya kupikia wamevifunga na kutoviendeleza. 
   Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kwa Msajili wa Hazina itaendelea na zoezi la kuvirejesha viwanda hivyo Serikalini ili waangalie utaratibu mwingine ulio bora wa kuviendeleza kwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo. 
   Amesema Mpango huo ambao utajikita zaidi katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na vile vilivyobinafsishwa ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi wengi. 
   Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambao utahitimishwa Juni 30, 2016 Serikali ilifanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara za lami na madaraja ya Kigamboni, Maligisu Nagoo, Mbutu na Ruhekei. Pia ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542), ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika maeneo ya Madimba na Songosongo, ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi vya Somanga-Fungu na Kinyerezi.

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati akizindua  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua  rasmi Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016 .  Wengine kutoka kushoto ni  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lugimbana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wananchi waliohudhuria katika  uzinduzi wa  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016
    Wabunge, Viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016
   Baadhi ya Mawaziri, Wabunge, Viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016
  Baadhi ya Mawaziri, Wabunge, Viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka  Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

older | 1 | .... | 1247 | 1248 | (Page 1249) | 1250 | 1251 | .... | 3348 | newer