Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1246 | 1247 | (Page 1248) | 1249 | 1250 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0

  Waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akifurahia zawadi ya maboga aliyepewa na wananchi wa kijiji cha KilaMpanda jimbo la Iramba mkoa wa Singida wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kumchagua bila kufanya kampeni mwaka jana kuendelea kuwa mbunge wao kwa kipindi cha pili sasa.

  Wananchi wa jimbo la Iramba kata ya Kilampanda wakimpokea mbunge wao Bw Mwigulu Nchemba kwa zawadi za maboga wakati wa ziara yake jimboni humu jana Juni 5.
  Mbunge Mwigulu akitembea kwa miguu na wananchi wake katika moja kata ya bonde ambalo ni hesemu ya barabara inayolalamikiwa na uwananchi kutokana na ubovu eneo hilo halina daraja.


  0 0

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  MKOA wa Morogoro upo mbioni kukuza uchumi wake kutokana na kuanza kuchimba madini ya Graphite kwakuwa yampepatikana katika mkoa huo katika kijiji cha Epanko Wilayani Ulanga mkoani humo.
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa andamizi wa vyombo mbalimbali vya habari katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa mikotano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.

  Madini hayo yalipatikana katika matokeo ya tafiti mbalimbali na utafutaji wa madini ambapo madini mengine ya aina mbalimbali yakiwemo ya rubby, spinal, dhahahu, mawe meusi na graphite (kinywe-Pichani Kushoto) yamepatikana katika  mkoa huo.

  Upatikanaji wa madini hayo utaongeza uwekezaji katika sekta ya madini katika wilaya ya Ulanga utasaidia kukuza uchumi wa ndani na nje utakaotokana na mauzo ya vito kwa kutumia fedha za ndani na za kigeni.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro leo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha na  Mwenyekiti wa  Kamati ya Ushauri wa Wizara ya Maliasili na Uatalii na Profesa wa masoko na utalii chuo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Wineaster Anderson wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
  Baadhi ya  wahariri na waandishi wa habari wandamizi wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Mkutano unaofanyika mkoani Morogoro leo. 
   Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi Irene Isaka ameipongeza Bodi ya Wadhamini na Mkuurgenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kuweza kuwafikia wadau wake muhimu kwanza kabla ya kuanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi. 

  Bi Isaka aliyasema hayo leo Juni 6, 2016 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari 124 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenye ukumbi wa jengo la PPF Plaza jijini Mwanza.Aidha, amesema kuwa sasa hivi wafanyakazi wasifanye kazi kwa wasiwasi kwani kuna chombo maalumu ambacho ndiyo kinga na msaada wao endapo watapatwa na majanga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Pia Bi. Isaka ametoa wito kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na madaktari kote nchini kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wote kutoka sekta Binafsi na Umma.

  Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ni taasisi ya Serikali iliyoko Ofisi ya Waziri Mkuu, na ulianzishwa kwa sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008. Lengo la kuanzishwa kwake ni kuhakikisha Mfanyakazi anapata fidia stahiki kutokana na kuumia kazini au magonjwa yatokanayo na kazi na kwa wanafamilia kupokea fidia kwa niaba ya mwenza wao aliyefariki akiwa kazini.

  Mafao yatolewayo na Mfuko huo ambayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba ni pamoja na Fao la matibabu, fidia ya ulemavu wa muda, fidia ya ulemavu wa kudumu, Fidia ya huduma ya marekebisho (Rehabilitation services), Fedha za uangalizi wa mara zote, (Constant attendance care grant), Fedha za mazishi, na fidia kwa wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki akiwa kazini au kutokana na maradhi yaliyosababishwa na kazi aliyokuwa akifanya. “Mfuko utaanza kutoa mafao ya kwanza kabisa tangu uanzishwe kuanzia mwaka wa fedha unaoanza Julai, 2016/2017.” Alisema Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba.Mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano wa WCF na Shirika la Kazi Duniani, ILO. 
  NA K-VIS MEDIA, MWANZA
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku tano kwa madaktari wanaotoka mikoa ya kanda ya ziwa kuhusu ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Jijini Mwanza. Bi. Isaka alisisitiza umuhimu wa WCF na madaktari kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wote kutoka sekta Binafsi na Umma. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Mkoa wa Mwanza, Bw. Salvatory KyaKyarwenda, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo, Bw. Emmanuel Humba.
  Mwenyeketi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake.
  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo.
  Baadhi ya Madaktari, wakufunzi kutoka ILO wakifuatilia maelezo ya utangulizi.
   

  0 0

  MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe.

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo.

  Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka katika ukusanyaji wa mapato.

  “TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha, ambapo kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo hususani katika pwani ya bahari ya Hindi na mipaka yote, kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za kodi za keielektroniki , kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema Kamishna Mkuu.

  Bw. Kidata ameendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.Katika kutekeleza agizo la Mh. Rais na kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD Mamlaka imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wadogo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

  TRA imeanza ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wapatao 5,703 wenye mauzo ghafi kati ya Shilingi milioni 14 na milioni ishirini (20) kwa mwaka, wafanyabiashara hao wanatakiwa wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato za Mikoa wanayolipia kodi ya Ilala, Kinondoni na Temeke ili waweze kuhakiki usajili wao wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na kupewa kibali cha kupewa Mashine ya EFD zoezi lililoanza Juni Mosi alisisitiza Kamishana Mkuu.

  Aidha, Bw. Kidata alifafanua kuwa zoezi hili litaendelea katika Mikoa yote Tanzania kwa awamu kwa utaratibu utakaotangazwa mara kwa mara na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wenye mauzo tajwa wote nchini kutoa ushirikiano pindi inapofika zamu yao katika Mikoa yao.

  Zoezi hili litasaidia kuongezaka kwa Mapato ya nchi endapo wafanyabiashara na wananchi watakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha wanatumia mashine hizo na kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu wafanyabiashara wote watakao kiuka kutumia mashine hizo za EFD.

  Kwa upande wa wananchi, kamshna mkuu amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia sambamba na risiti walizopewa .


  “Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

  Imetolewa na:

  Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (katikati) na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba (kushoto) wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia anayepiga makofi ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye.
  Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari tisa kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini. Wa pili kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshiba akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Thobias Andengenye. Wa pili kulia ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatus Kipali na Kamishna Msaidizi, Fikiri Salla. Tukio hilo lilifanyika nje ya Jengo la Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya magari tisa yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshiba kwa niaba ya Serikali yake yakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Magari hayo yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, jijini Dar es Salaam leo. 


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba , bungeni mjini Dodoma Juni 6, 2016.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiteta na Naibu wake, Dkt. Medard Kalemani, bungeni mjini Dodoma Juni 6, 2016.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kushoto) akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi , Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, bungeni mjini Dodoma Juni 6, 2016.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akisoma Azimio la Bunge kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Udhibiti wa Matumizi ya Dawa na Mbinu za kuongeza Nguvu Michezoni, bungeni mjini Dodoma Juni 6, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.

  Prof Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya Wanawake Tanzania.

  Aidha amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi yetu.“Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake waanzE kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure.”Alisema Prof Mkenda.

  Pia alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi siku na kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka wafanye biashara kwa faida kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuongeza uzalishaji.

  Katika upande mwingine aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kujiinua kiuchumi kwani Serikali ya awamu ya tano iko makini na inaweka mazingira mazuri kwa wanawake kama kuondoa tozo zisizokuwa za lazima ili kuvutia wawekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

  Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alizindua jukwaa hilo na akaunti ya mikopo ya wanawake ya MALAIKA kupitia benki ya wanawake ambayo akaunti hiyo itakuwa na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 5 kwa muda wa miezi sita,mafunzo yanatolewa bure,hamna haja ya kuleta mchanganuo wa mahesabu na hakuna hitaji la dhamana yenye lengo la kuwakwamua wanawake kiuchumi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameyaomba mashirika ya Kimataifa na Nchi zilizoendelea zishirikiane na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia wakimbizi.

  “Kwa sasa tunashirikiana na UN (Umoja wa Mataifa) kuwahudumia wakimbizi, hivyo tunaomba mataifa mengine nayo yatusupport katika jambo hili,” amesema.Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Juni 6, 2016) alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Mhe. Dibr Reynders ofisini kwake Bungeni, Dodoma.

  Amesema Tanzania inahifadhi jumla ya wakimbizi 165,000 kati ya 230,000 walioko katika nchi za Maziwa Makuu, ambapo bajeti ya Serikali haitoshelezi kuwapa huduma wanazostahili.Waziri Mkuu Majaliwa amesema wakimbizi hao wanaishi kwenye kambi mbalimbali nchini zikiwemo za Nyarugusu na Nduta zilizoko wilayani Kasulu na Kibondo ambazo alizitembelea Desemba mwaka jana.

  Amesema wakimbizi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uhaba wa maji safi, ufinyu wa huduma za afya na elimu na uharibifu wa mazingira .Amesema wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Burundi, Kongo na Rwanda, pia amemuomba Mhe. Reynders atakapofika Burundi akahamasishe amani.

  Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema Tanzania inakkaribisha wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na mataifa mengine kuja kuwekeza katika Sekta za Viwanda, Nishati na Miundombinu.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema hali ya siasa visiwani Zanzibar ni ya utulivu na Rais Dk. Ali Mohamed Shein anafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na vyama vya upinzani.

  Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mhe. Reynders aliyetaka kujua hali ya kisiasa inavyoendelea visiwani huko.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  06 Juni, 2016 .

  0 0

  0 0
 • 06/06/16--08:43: CCM YAVUNJA UKIMYA

 • 0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
  Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan leo hii amezindua jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti maalum ya mikopo ya MALAIKA inayolenga kuwawezesha wanawake wa hali ya chini kiuchumi kupitia Benki ya wanawake katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Akiongea katika uzinduzi huo Mheshimiwa Samia Suluhu amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni kuwapa uwezo wanawake waweze kutoka katika sekta isiyo rasmi na kuingia katika sekta rasmi na hivyo kuwainua kiuchumi kwani mchango wa mwanamke mpaka sasa bado haujaongezeka thamani.

  Aidha Bi Samia ameagiza kuwa kuanzia sasa asilimia 35% ya tenda za serikali za mitaa ziende kwa wanawake na vijana ili kuwawezesha kiuchumi na kuwataka wanawake kubadilika kifikra na hata wanapopata mikopo hii wawe na nidhamu katika matumizi yake.

  Hata hivyo Mhe. Suluhu ametoa rai kwa mabenki kufikisha huduma zao vijijini ili huduma ya mikopo iwafikie wanawake wachangie uchumi wa dunia na sio tu kwa familia huku akiwahimiza wanawake kupendana,kushirikiana na kusaidiana.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Dkt.Hamisi Kigwangala amesema kuwa serikali imeendelea kusaidia wanawake katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kuweka usawa wa jinsia kwa wanawake kiuchumi ,kutoa vikwazo katika masoko na kuondoa mila kandamizi.

  Aidha Dkt Kigwangala ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa wanawake kwa kufanya mafunzo ya ujasiliamali na kuweka sera nzuri ambayo yote haya yameainishwa katika ilani ya chama cha mapinduzi ya 2015-2020 uku akieleza mafanikio makubwa ya benki ya wanawake ambayo mpaka sasa imetoa mikopo yenye thamani ya bilioni 86.

  Uzinduzi wa Jukwaa hilo na akaunti ya MALAIKA ya mikopo uliendana na mada mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali kama Crdb,Benki ya wanawake,Nssf ,Wizara ya Viwanda na Biashara na Tcra.
   

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza Laptop kuzindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu wakati uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06,2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya CD yenye vipindi mbalimbali kutoka kwa watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu kwenye uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06,2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
   


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa pole kwa Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya kidemokrasia ya Saharawi nchini Mhe. Brahim Buseif alipokwenda ubalozini hapo kutoa pole na kusaini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Rais wa Saharawi Mhe. Mohamed Abdelaziz Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam leo.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi na Waislamu wote nchini katika Risala hiyo amewataka Wananchi kuwa Amani na Utulivu na kuwaombea kwa Mola wetu kuwajaalia Rehma na baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Pia amewataka kufanya ibada kwa wingi katika kipindi chote cha mwezi huu. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo.  0 0


  TAARIFA KWA UMMA

   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.  Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).  Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.  Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz).

  IMETOLEWA NA:

  KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,

  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,

  JUMANNE, JUNI 7, 2016

  Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)

  0 0


  atibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akimkabidhi kipolo chenye Mchele, unga, sukari na mafuta ya kula kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramazan mmoja wa wazee wa Tumbatu Jongoe.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin wakatikati na mwenziwe Huseyin Kursun (kushoto) wakiwapa nguo watoto wa Tumbatu Jongoe ikiwa ni miongoni mwatarati iliyojiwekea Jumuiya hiyo.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akiagana na watoto wa kisiwa cha Tumbatu Jongoe, mara baada ya kumaliza kutoa sadaka ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya milioni kumi na nane. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
   

  0 0

  Baadhi ya Tax bubu za kusafirisha Abiria kutoka Stendi Kuu kwenda sehemu nyingine yakiwa yameegeshwa katika Sehemu yao yaliyo pangiwa katika Stendi hiyo ya Mkoa wa Mbeya iliyopo Jijini Mbeya.
  Baadhi ya Wafanya Biashara waliopo ndani ya Stendi hiyo wakinadi Bidhaa zao kwa baadhi ya Abiria wanao fanya Safari katika Stendi hiyo..
  Dereva wa Tax akimfuata Abiria...
  Moja kati ya wapiga Debe wa Stendi kuu ya Mkoa wa Mbeya akining'inia kwenye Basi lililo kuwa  likitoka katika stendi hiyo...
  Baadhi ya wafanya Biashara ndogondogo ndani ya Stendi hiyo ya Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Sehemu yao...
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

older | 1 | .... | 1246 | 1247 | (Page 1248) | 1249 | 1250 | .... | 3348 | newer