Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1245 | 1246 | (Page 1247) | 1248 | 1249 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amewataka wananchi wa kisiwa Panza katika Mkoa wa Kusini Pemba, kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutunza mazingira hasa kwa kupanda miti ya mikoko kwa wingi,ili kunusuru kisiwa hicho kumezwa kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari.

  Mhe. Mpina ameyasema hay leo kisiwani Pemba alipozingua kampeni maalum ya kupanda miti ya mikoko ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupanda miti.

  Awali Mhe. Mpina alisemakuwa, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kupata kiasi cha fedha shilingi milioni 165 maalum kwa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kujenga kuta za fukwe za Ocean Road jijini Dar es Salaam,Pangani Mjini Tanga, Kilimani mjini unguja na kisiwa Panza kisiwani Pemba.

  Naibu wa Waziri wa Wizara ya Nishati, Maji na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Juma Makungu Juma (Kushoto), akimueleza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina (katikati) walipokuwa wakielea kupanda miti ya mikoko kisiwa panza kusini Pemba. Kulia ni Muwakilishiwa mkuu wa Wilaya.

  Aliongeza kuwa, kiasi hicho cha fedha pia kimeanza kutumika katika kampeni hiyo ya kitaifa ya kupanda miti kwa kupanda miti ya mikoko katika eneo la kisiwa Panza na ambapo miti zaidi ya milioni Moja inatarajiwa kupandwa katika eneo la hekta 238, kisiwani pemba, pamoja na zoezi hilo kuzinduliwa leo kisiwani pemba, miti hiyo aina ya mikoko pia inatarajiwa kupandwa katika maeneo ya kilimani mjini unguja,bwawani,tovuni, micheweni na Rufiji.

  Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa suala la mazingira si suala la Muungano lakini serikali hizi mbili zimeona umuhimu wa kushirikiana katika eneo hili ili kuweza kukabiliana kikamilifu na madhara na hasara zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kunusuru visiwa hivi kumezwa na bahari.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipanda mbegu za miti ya mikoko katika eneo la kisiwa cha Panza ikiwa ni siku ya uzinduzi wa upandaji miti hiyo kisiwani Pemba, kushoto ni Afisa Mazingira mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Cretus Shengena.

  Akitolea mfano wa shule ya msigi na sekondari kisiwapanza ambazo zipo hatarini kumezwa, mhe Mpina aliongeza kuwa wataalam wa masuala ya mazingira watafanya tathmini kikamilifu na kuona namna gani serikali inaweza kuongeza mbinu zaidi za kushughulikia maeneo haya hatarishi, ili maji ya bahari yasiweze kuingia katika maeneo ya makazi.

  Naibu Waziri Mpina aliwasisitizia wananchi wa kisiwa panza kutunza mazingira kwa kutokukata miti ovyo na kuchoma misitu na watunze na kuilinda miti ya mikoko iliyopandwa ili kuweza kufikia dhamira ya kukinusuru kisiwa icho kumezwa.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mazingira kutoka katika wizara ya Ardhi,Maji,Nishati,na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Juma makungu Juma amesema maeneo mengi ya Zanzibar yaliyopo pembezoni mwa bahari yameharibiwa na shughuli za binadamu, hivyo upandaji wa miti ya mikoko katika maeneo hayo utazuia adhari za mabadiliko ya tabia nchi kwa makazi ya watu na mashamba ambayo yamepelekea watu kuanza kuhama katika makazi yao na haya yote ni matokea ya vitendo vya wananchi.

  Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira na Idara ya Mazingira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa nadani ya boti kuelekea kiwapanza kisiwani, mkoa wa kusini  Pemba kushiriki zoezi la uzinduzi wa kupanda miti ya mikoko.(Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi).

  Zoezi hilo la kupanda miti ya mikoko lililofanyika kisiwani pemba limeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo hufanyika tarehe tano Juni kila mwaka.

  0 0

  Mgeni rasmi Injinia Mtende Hassan,akikata utepe kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TCRA Zanzibar,kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mlandege mjini humo mwishoni mwa wiki,Katika jengo la Muzamil Center.Wengine katika picha Afisa Mkuu wa Usambazaji wa kampuni hiyo,Hassan Saleh,Ahmed Hassan na Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo,Mohamed Mansour.
  Afisa Mkuu wa Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh (kushoto) na Ofisa wa Mamlaka ya mawasiliano TCRA,Ahmed Hassan (kulia) wakimshuhudia Mgeni rasmi Injinia Mtende Hassan, akikata keki kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TCRA Zanzibar, kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mlandege mjini humo mwishoni mwa wiki, Katika jengo la Muzamil Center.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Injinia Mtende Hassan (sita kushoto) mara baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TCRA Zanzibar, Duka hilo lipo Mlandege mjini Zanzibar, Katika jengo la Muzamil Center.

  0 0

  Mabalozi wa nchi za Afrika waliopo Kenya, jana waliadhimisha sherehe za Siku ya Afrika (AU Day), ambazo ziliahirishwa mwezi uliopita kupisha Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira kuhusu Afrika, uliofanyika Nairobi. Siku ya Afrika huadhimishwa Mei 25 kila mwaka.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Kenya, Balozi Amina Mohamed, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zilizofanyika viwanja vya Ubalozi wa Malawi jijini Nairobi. Katika hotuba yake, Waziri huyo alisema nchi za Afrika simepiga hatua katika kujenga amani na utengamano chini ya Agenda 2063, inayolenga kuliinua bara hili kiuchumi.

  Chini ya mpango huo, Afrika imekusudia kumaliza kabisa mizozo ya kivita na mifarakano mingine kati ya nchi wanachama ifikapo mwaka 2020. Malengo mengine makubwa ni kupunguza utegemezi nje wa bajeti ya mipango ya maendeleo ya Afrika, na kuondoa vikwazo vya miingiliano ya watu, bidhaa na huduma baina ya nchi za bara hilo.

  Waziri Mohamed alisema Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na mawaziri wa Mambo ya Nje watapatiwa pasi za kusafiria za Afrika mwezi Oktoba mwaka huu chini wa mpango wa kuondoa vikwazo vya usafiri barani Afrika. Sherehe hizo ziliandaliwa na Mabalozi wa Kundi la Afrika (African Diplomatic Community) nchini Kenya, akiwemo Balozi wa Tanzania, Mhe. John Haule.

   Balozi wa Uganda nchini Kenya, Mhe. Angelina Wapakhabulo (kushoto) akionja mvinyo aina ya Presidential unaotengenezwa Dodoma alipotembelea  banda la Tanzania. Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania, Mhe. Haule
   Na sasa ni wakati wa kuserebuka! Balozi Haule (wa tatu kulia), Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Fastjet, Bw. Jimmy Kibati (wa pili kulia) na mshereheshaji, wanajimwaga uwanjani baada ya Balozi kukabidhi washindi wawili (kushoto) tiketi za kwenda Dar es Salaam na kurudi kwa ndege ya Fastjet.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Kenya, Balozi Amina Mohamed (wa pili kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, alipotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya kusherehekea Siku ya Afrika. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Nje, Balozi Monica Juma na kushoto ni mke wa Balozi Haule, Bibi Maria.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Monica Juma, akitizama bidhaa za kutoka Tanzania kwenye maonyesho hayo.
  Wageni kwenye banda la Tanzania.

  0 0

  Government leaders and Ambassadors from across East and Southern Africa joined forces in Tanzania today to launch a new initiative called Vuna, which links smallholder farmers, governments and private companies in the first major ‘climate smart agriculture’ initiative for the region.

  As a result of the increasing temperatures and droughts, farmers across the country and region are facing reduced yields, less food and reduced incomes. Processing companies face raw material shortages and this makes it harder to their businesses to stay viable. Countries across the region are working to strengthen the agricultural sector in the face of this climate change. 
  The initiative launched today in Dar es Salaam will increase efforts to help smallholder farmers, by finding and supporting use of practice and technologies which reduces climate risks.

  Attendees at the launch recognised the need to look at all the relevant dimensions of farming, and to forge partnerships between multiple stakeholders which focus on increasing market viability and adapting to climate change. Governments and scientists recognise that helping farmers adapt to the changing climate requires regional level collaboration and lesson learning, to identify and then rapidly scale up best practice, which really works for farmers, to combat current and future climate impacts.
  Executive Director for Tanzania Nationa Business Council (TNBC), Mr. Raymond Mbilinyi with John Cantrill, Vuna Programme Team Leader.

  “Our efforts cannot be on just national levels; we need a regional effort to address the recurring droughts which threaten our agriculture sectors, as well as the other climate change impacts such as increasing temperature. Government welcomes this new support to the region and is already working with Vuna, so that we can help our farmers face these challenges.” Mr. Raymond Mbilinyi – Executive Director for Tanzania Nationa Business Council (TNBC)

  The joining of forces – of farmers, government, private sector companies and development partners - at this meeting signifies a major step towards finding the best approach to helping farmers to build their resilience, in a region which is the most vulnerable to climate change, affected by climate impacts such as flooding, erosion and variable rainfall.

  The event was co-hosted by the Vice President’s office of Tanzania and Vuna and attended from over 100 representatives from across research, NGOs, the private sector and government. A series of events will follow across East and Southern Africa, sharing best practice and lessons across the whole region.
  Sam Kareithi, Senior Advisor Vuna Program 

  “This new initiative represents an exciting and innovative opportunity to work more on the potential for agriculture to thrive as a business, based on all parties working together to address the challenges created by the changing climate, in partnerships which raise income levels and improve the overall health of the agriculture sector. We are delighted to be working alongside the governments of Tanzania to achieve our shared objectives and we welcome their support.” John Cantrill – Vuna Programme Team Leader
  John Cantrill, Vuna Programme Team Leader.

  Vuna, a programme funded by the UK’s Department for International Development (DFID) and implemented by a consortium of partners led by Adam Smith International, works with partners to achieve shared objectives in: increasing; research evidence about climate smart agriculture; create and strengthen sustainable incentive structures in agricultural value chains, to change how smallholder farmers and private companies respond to climate risks.

  0 0


  Mlimbwende Maria Frances (katikati) ametwaa taji la MISS ILEMELA 2016. Shindano la kumsaka mlimbwende huyo lilifanyika usiku wa jana June 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza.Katika shindano hilo, nafasi ya pili imenyakuliwa na Mwanaisha Hija (kulia) huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Happness Contantine (kushoto).

  Washiriki wa Miss Ilemela waliobahatika kuingia nafasi tano bora. Kulikuwa na washiriki 22
  Washiriki wa Miss Ilemela 2016 wakipita jukwaani kwa madaha kabisa
  Msanii Nay Wa Mitego akitoa burudani katika shindano la Miss Ilemela 2016.


  0 0
  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa soka nchini, kulia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi, Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini FAT Said El Maamry, upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa zamani wa TFF Muhidini Ndolanga na  Rais wa zamani wa TFF Ndugu Leodgar Tenga muda mfupi kabla ya kuanza ka mechi ya Taifa Stars na Misri. 
   Viongozi na wapenzi wa soka wakiimba kwa pamoja wimbo wa Taifa kabala ya mechi kuanza.
   Viongozi na wadau wa michezo wakitoa heshima kwa kusimama wakati wa wimbo wa Taifa.
   Mbunge wa Jimbo la Chalinze akizungumza na Khamis Mgeja kabla ya mechi haijaanza.
   Timu ya Taifa Stars ikipeleka mashambulizi kwenye goli la timu ya Misri hata hivyo mpaka mchezo umeisha Misri waliibuka na ushindi wa 2-0.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitazama mechi ya Taifa Stars, wengine pichani ni Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Frederick Sumaye.
  0 0

  Usiku wa kuamkia leo, mitanange mitatu ilikanyagwa katika viwanja 3 tofauti.

  Mchezo wa kwanza uliwa shuhudia Peru wakiwafunga Haiti goli 1-0. Kipindi cha kwanza hakikuwa na goli ingawa Peru walimiliki zaidi mpira hasa katikati ya uwanja wakitumia mfumo wa 4-4-2 na kuwabana Haiti ambao wao walitumia mfumo wa 4-3-3.

  Iliwachukuwa Peru mpaka dakika ya 66 kujipatia bao lao lililowekwa kimiani na mshambulizi hatari Paolo Guerrero kwa kichwa cha kuchumpa kufuatia krosi mujarabu iliyotumwa na Edson Flores na kumshinda golikipa Johny Plaside wa Haiti. Haikushangaza Guerrero kufunga bao hili kwani ikumbukwe kuwa huyu ndiye mfungaji bora wa mashindano haya kwa misimu miwili iliyopita.
  COSTA RICA vs PARAGUAY

  Wengi walitarajia kuwa mpambano huu utakuwa wa mbinu za kutafuta mabao pamoja na ufundi mkubwa, lakini tofauti yake ikawa ni mtanange wa nguvu zaidi na kukamiana, kitu kilichopelekea mwanuzi kugawa kadi kama njugu, kwani alitoa kadi za njano kwa wachezaji 5 kadi nyekundu kwa mchezaji wa Costa Rica Kendall Waston mnamo dakika ya 94.

  BRAZIL vs EQUADOR

  Katika kipute hiki matokeo yalikuwa ni kutofungana (0-0), lakini ukweli ni kuwa huu ulikuwa ni mchezo uliokuwa wa kuburudisha (very entertaining) kuliko michezo mingine yote iliyokwisha kuchezwa hadi sasa. Kwa upande wa Brazil waliotumia mfumo wa 4-2-1-2-1 na kuwatumia zaidi Willian Coutinho kuchezesha timu, walipeleka sana mashambulizi langoni mwa Equador lakini kipa wa Equador aliweza kuokoa hatari zote.

  Mnamo dakika ya 66 ya mchezo, mchezaji hatari wa Equador Miller Balanos alimpita golikipa wa brazil pembeni ya lango na kuuweka mpira kimiani, lakini mwamuzi alilikataa bao hilo kwa madai mpira ule ulikuwa umetoka kabla mfungaji hajaitia kambani. Hivyo mpaka mwisho matokeo ni 0-0.

  Leo usiku kuamkia kesho

  JAMAICA vs VENEZUELA (Soldier Field)
  MEXICO vs URUGUAY (Phoenix Stadium)

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(kushoto)akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Terrat Mlimani,Kata ya Murirt,jiji la Arusha Mbuzi ukiwa ni mpango wa serikali ikishirikiana na wadau wa maendeleo kunusuru kaya masikini .
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda(kushoto)akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Terrat Mlimani,Kata ya Murirt,jiji la Arusha Mbuzi ukiwa ni mpango wa serikali ikishirikiana na wadau wa maendeleo kunusuru kaya masikini . 
  Wakazi wa Kata ya Muriet jiji la Arusha wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda. 

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Wilson Nkambaku aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Msingi Kiranyi.Ameagiza wananchi wote walijenga kwenye eneo lilitengwa kwaajili ya chanzo cha maji wabomoe wenyewe. 

  Mtendaji Mkuu wa Mamkala ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni, Sophia Shoko akizungumza jambo katika maadhimisho hayo. 


  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.

  Kituo Cha kusaidia Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Sober House kilichopo Bagamoyo kimekanusha kuwepo kwa taarifa juu ya msanii wa miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro maarufu kama Child Benz kutoroka kituoni hapo.

  Akikanusha tuhuma hizo za kutoroka kwa Msanii huyo, Mkuu wa Kituo hicho, Al-Kareem Bhanji ameeleza kuwa Chid Benzi aliondoka kituoni hapo baada ya kufuata taratibu zote za uongozi pale alipoonekana yuko sawa.

  "Ukweli ni kwamba Chid hakutoroka kituoni hapo bali alifuata taratibu na baraka zote za uongozi zilizotolewa baada ya kuonekana yuko sawa"amesema Bhanji

  Pia amekanusha kuwepo kwa taarifa ya kuwa Babu Tale alimtelekeza Chid kituoni hapo.

  "Babu Tale alitoa ushirikiano wa hali ya juu katika kusaidiana kama mnavyojua ukweli mpaka kumleta Chid kituoni. Tulikuwa muda wote tunashirikiana naye" ameendelea kueleza Bhanji

  Chid Benzi alikaa kituoni hapo kwa takriban Mwezi Mmoja na Nusu na kuruhusiwa na uongozi wa kituo hicho baada ya hali yake kuona inaridhisha.
  Mkuu wa kituo cha "Life and Sobber House Bagamoyo" Al-Karim Bhanj akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) juu ya uvumi ulioenezwa kuwa Msanii Rashid Makwito al maarufu kwa jina la 'CHIDI BENZ' alitoroka kwenye kituo hicho cha kutibu waathirika wa Dawa za kulevya. 

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha polisi cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, mradi unaohusisha pia majengo mbalimbali ya Mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia nae Mkataba.

  Katibu Mkuu amesema mradi huo ni mkubwa sana na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha Mkataba huo ambao utekelezaji wake unaendelea ili aweze kuufahamu vizuri mkataba huo unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania limited.

  Jenerali Rwegasira ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo na kwamba ujenzi wake bado unaendelea. Jenerali Rwegasira ametembelea pia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Oysterbay ili kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya jeshi.

  Aidha mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Mara World Tanzania limited katika eneo la Polisi Oysterbay atajenga kituo cha polisi cha kisasa, ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.

  Kwa upande mwingine, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha jumla ya Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa (59) kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake walikokuwa wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali nchini.

  Akizungumzia uhamisho huo, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji, ambapo amesisitiza kuwa zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara ya Uhamiaji linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kiutendaji.

  Jenerali Rwegasira ameeleza kuwa watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio mbalimbali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi.

  0 0


  0 0

  Na Dac Popos, Globu ya Jamii. 
  Michuano ya Copa Amerika imeingia katika siku yake ya tatu kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti huko nchini Marekani. 

  Mtanange uliotolewa macho na masikio na wengi ulikuwa kati Uruguay ya Luis Suarez na Mexico ya Javier Hernandez 'chicharito'. Twaweza sema kuwa Uruguay walifungwa kabla ya mpira kuanza, kwa sababu mbili, ya kwanza ni kukosekana kwa mshambuliaji wa hatari Luis Suarez aliye majeruhi na pili kutopigiwa wimbo wao wa taifa na badala yake wakapigiwa wimbo wa taifa wa Peru.

  Mchezo ulianza kwa kasi na dakika ya nne tu mlinzi wa Uruguay Max Perreira alijifunga mwenyewe kwa kichwa katika harakati za kuokoa, hadi mapumziko Mexico 1 Uruguay 0. Kipindi cha pili Uruguay walijitahidi kubadili mchezo na kunako dakika ya 74 Diego Godin akaisawazishia timu yake bao. Mexico wakaja juu tena na kijipatia mabao mawili ndani ya dakika tano, kwani dakika ya 85 R.Marquez alifunga goli la pili na dakika ya 90 Hector Herrera akagongelea msumali wa mwisho.
  Mtanange mwingine uliwakutanisha 'Reggae Booys' Jamaica waliokipiga na Venezuela, ambapo Venezuela walifanikiwa kuondoka na pointi zote tatu kwa kuifunga Jamaica goli 1-0. Goli hilo liliwekwa kimiani na mshambulizi Josef Martinez, huku mchezaji Rodoph Austin wa Jamaica akilambwa kadi nyekundu. Pia kocha wa timu hiyo Juan Carlos Osorio alitolewa uwanjani na kwenda kukaa jukwaani kutokana na kumtolea maneno makali mwamuzi.

  Hadi kipyenga cha mwisho kuashiria mchezo umemalizika, Venezuela1 Jamaica 0.

  Leo tunahitimisha mechi za mzunguko wa kwanza ambapo ni kati ya
  BOLIVIA vs PANAMA
  ARGENTINA vs CHILE

  Pia hapo baadaye usikose kupitia ukurasa huu kwa sababu rasmi tunaanza kukuletea dondoo mbali mbali za kuelekea UFARANSA kwenye patashika ya EURO 2016.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel imetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha inaokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wadogo nchini Tanzania. Airtel imechangia katika kuendesha kampeni ya wazazi Nipendeni (Afya ya wajawazito na Watoto) kwa kutoa elimu kupitia ujumbe mfupi toka mwaka 2012.  Mpaka sasa Airtel imeweza kutuma ujumbe mfupi wa taarifa muhimu za afya zaidi ya milioni 22 kwa wateja zaidi ya 350,000 wenye thamani ya shilingi 1,518, 000,000

  Airtel kwa kushirikiana na mHealth Tanzania PPP waendeshaji wa huduma hii inayomilikiwa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inawezesha wateja wake kote nchini kupokea taarifa muhimu za afya ya mama wajawazito na kuwakumbusha kuhudhuria kliniki na kupata chanjo. “Taarifa zinazotolewa kupitia ujumbe mfupi zinahakikisha mtoto ambaye hajazaliwa na mama mjazito wako katika usalama wakati wote” alisema Mratibu na mshauri wa mradi Muttah Saulo kutoka mhealth Tanzania PPP

  Aliongeza kwa kusema” akina mama pia wanashauriwa jinsi ya kuwatunza watoto wao kwa usalama baada ya kujifungua, waliojiunga na huduma hii watapata ujumbe mfupi wa idadi isiyopungua nne kwa wiki”

  Akiongea kuhusu ushirikiano huo , Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu wa wazazi nipendeni kupitia huduma yetu ya ujumbe mfupi.  Mpango huu unaonyesha uwezo wa teknologia katika jamii na kwamba teknologia ya simu za mkononi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama. Maelfu ya wajawazito, wazazi na wasaidizi wamenufaika na huduma hii.  Kwa kutoa huduma hii bure mpaka sasa tumeweza kuwekeza kiasi cha shilingi 1,518, 000,000 na tunaendelea kushirikiana na mhealth Tanzania PP katika kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu na kuwanufaisha watanzania wengi. Airtel tumejipanga kuendelea kuhamasisha usalama katika maisha ya watanzania na kuwawezesha jamii kufatilia na kutia mkazo katika afya zao kwa kuwapatia elimu juu ya afya bure bila gharama zozote.”

  Mmoja kati ya watumiaji wa huduma hii , Bi Francis ambaye sasa ni mama mwenye mtoto wa miezi mitatu  alisema”  Tunafurahia huu mpango  kwani unatupatia elimu juu ya afya zetu na watoto na kutusaidia kufatilia siku za kuhudhuria kliniki pamoja na  kuwapeleka watoto kliniki.  Mimi na mume wangu tunafurahi huduma hii ya bure kutoka Airtel inayotuwezesha kuendelea kumlea mtoto wetu katika afya.”

  Takwimu kutoka katika ripoti ya mHealth Tanzania PPP Mei 2016 zinaonyesha kila mwezi wateja wa Airtel takribani 7300 wamejiunga na huduma ya bure ya sms ya wazazi nipendeni. Kati yao 43% ni wa kina mama wajawazito na 15% ni wa kina mama wenye watoto wadogo na 44%  ni wasaidizi wa wakinamama wakiwemo waume , ndugu na  wale wanaotafuta taarifa za afya  ya uzazi kwa ujumla.
  Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende”. mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto.
  Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapatia taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akifatiwa Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans.
  Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayo wapatia taarifa mbalimbali za afya ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania na washirika wengine chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Kulia ni Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC)Tanzania, Dr Maestro Evans.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI


                                                                                                                       
  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Dk. Steve Mdachi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.

  Kufuatia uteuzi huo, amewateua pia wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PBPA kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.
  1.  Dkt. Daniel Sabai
  2.  Dkt. Henry  Chalu
  3.  Dkt. Siasa Mzenzi
  4.  Mr. Salum Mnuna

   Imetolewa na;
  KATIBU MKUU
  6 Juni, 2016


  0 0

  Waziri wa Maliasili na utalii Mh.Jumanne Maghembe akifungua mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Kebwe Steven Kebwe. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro leo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
  Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakimsikiliza waziri wa Maliasili na utalii,Jumanne Magembe Mjini Morogoro leo.
  Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakimsikiliza waziri wa Maliasili na utalii,Jumanne Magembe Mjini Morogoro leo,alipokuwa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
  Baadhi ya Wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakijadiliana jambo kabla ya mkutano huo kuanza,mjini morogoro leo

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BAADA ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuvurunda kwenye mchezo wao wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Misri kwa kukubali kichapo cha goli 2-0, wadau wa mpira wa miguu wamemshushia zigo la lawama kocha mkuu wa timu hiyo kwa kuonyesha udhaifu katika kuteua kikosi cha timu hiyo na kuishilia kuwalaumu wachezaji kwa kiwango kibovu wanachokionesha uwanjani.

  Moja ya wadau wa mpira, Musa Adinani amesema kuwa Mkwasa hakutaka kuangalia na mechi inayotukabili ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwetu na hata ukiangali kikosi alichokipanga kilikuwa na mapungufu makubwa sana hasa safu ya kiungo kwa kuchezesha viungo wenye aina moja ya mpira na kushindwa kutengeneza nafasi kwa washambuliaji. 

  "Hatuelewi kwanini  aliwaanzisha wachezaji Himid Mao na Mwinyi Kazimoto ambao wote wana aina moja ya mpira, hata ukiangalia washambuliaji wameshindwa  kupata  mipira mingi ya kulishwa kutoka safu ya kiungo na muda mwingi sana Mbwana Samatta alikuwa anazunguka na mpira akitafuta kwa kupiga,"amesema Adinani. 

  Misri waliweza kumiliki pale kati na hata ukiangali kuanza kwa washambuliaji wawili ambao wote ni wapiganaji lilikuwa ni kosa sana. Samatta na Elius Maguli ni wachezaji wa aina moja huwezi kuwaanzisha katika mechi yenye umuhimu kama hiyo tena ukiweka viungo wawili tu kati.

  Wadau wengine wameonekana sana kuchukizwa na kitendo cha Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga kuwazomea wachezaji wa timu pinzani pale anapofanya makosa na hilo limeonekana ni kama hali isiyo nzuri hasa ukizingatia ni timu ya Taifa ndiyo inacheza na ni muhimu kuungana ili kuwapa hari na hamasa wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

  0 0

  Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji nchini, Abas Irovya akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari - Maelezo jijini Dar es salaam, juu ya Idara hiyo kuanzisha utaratibu wa kuwatoza faini wahamiaji haramu pindi watakapokamatwa. Wengine pichani ni toka kushoto ni Mrakibu Msaidizi Uhamiaji, Rosemary Mkandala,Afisa wa Divisheni, Usimamizi na Udhibiti Mipaka, Wilson Bambaganya pamoja na Mkaguzi wa Uhamiaji, LesileJames Mbotta.

  0 0

   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Boniface Jacob akiwaonesha waandishi wa habari ramani  inayoonyesha eneo la makaburi lililovamiwa na taasisi ya Mkapa Foundation ambalo limegaiwa na manispaa kinyume na taratibu. Kwa maelezo ya nyaraka za manispaa  zinavyoonyesha, eneo hilo limetolewa wakati baraza la madiwani likiwa limemaliza muda wake. Cha kushangaza eneo hilo, manispaa haijaambulia hata shilingi. Na mwisho kabisa mstahiki meya, ameaagiza kusimamishwa shughuli zozote katika eneo hilo.
  Meya wa manispaa ya kinondoni Mhe. Boniface Jacob amepiga marufuku watendaji wa manispaa hiyo kuacha tabia ya kubadirisha hati za viwanja vilivyotengwa kwa ajili ya kuzikia kwenda kwenye ujenzi wa huduma za watu. Mhe. Jacob ameyasema hayo leo jijini wakati alipofanya ziara maeneo ya kawe ambapo kulikuwa na mgogoro juu kubadirishwa eneo la kuzikiwa na kwenda kuwa makazi ya watu.


older | 1 | .... | 1245 | 1246 | (Page 1247) | 1248 | 1249 | .... | 3348 | newer