Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1241 | 1242 | (Page 1243) | 1244 | 1245 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Imam Qasim Ibn Khan kutoka nchini Marekani akiongea na jumuiya ya vijana wa kiislam vyuo vikuu  mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam katika kongamano maalum la kukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Imam Qasim Ibn Khan kutoka nchini Marekani akisisitiza jambo kwa vijana waliopo katika umoja wa wanafunzi wa kiislam wa vyuo vikuu (hawapo pichani) wakati wa kongamano la vijana la kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
    Vijana wa TAMSYA mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini mafundisho kutoka kwa mtoa mada mkuu wa kongamano la vijana Imam Qasim Ibn Khan(hayupo pichani) wakati wa kongamano hilo lililofanyika jana
    Vijana wa TAMSYA mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini mafundisho kutoka kwa mtoa mada mkuu wa kongamano la vijana Imam Qasim Ibn Khan(hayupo pichani) wakati wa kongamano hilo lililofanyika jana
   Imam Qasim Ibn Khan kutoka nchini Marekani akitoa mada kwa vijana waliopo katika umoja wa wanafunzi wa kiislam wa vyuo vikuu (hawapo pichani) wakati wa kongamano la vijana la kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 
    Vijana wa TAMSYA mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Imam Qasim Ibn Khan alipokuwa akitoa mafundisho mbalimbali kuhusiana na dini ya kiislam katika kongamano la vijana lililofanyika jana

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu amefanya mkutano wa kifungua kinywa (breakfast meeting) na wafanyabiashara wa Sweden uoliandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika Mashariki(SWEACC). Mhe. Balozi Dora Msechu amewahamasisha Wafanyabiashara wa Sweden kuwekeza Tanzania kwa kuweleza kwa kina fursa zilizopo pamoja na juhudi mahsusi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na mikakati kabambe ya kuimarisha sekta ya viwanda na kuboresha miundombinu.  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto) akipokea sehemu ya madawati 70  kutoka kwa  Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya  yaliyotolewa ba benki hiyo kusaidia  Shule ya Sekondari Handeni kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto), akikabidhi madawati hay kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wilayani humo hivi karibuni. 
   Meneja Masoko  wa Benki ya B arclays Tanzania  (BBT) Nasikiwa Berya (watatu kushoto), akikabidhi sehemu ya  msaada wa madawati 70 kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari handeni, Amani Mmbaga, yaliyotolewa na benki kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga .  


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu kushoto), nyumba ya kwanza katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa kuwa majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa pole katika familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika Kata ya Mzizima, mkoani Tanga.


  0 0


  0 0

  Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, 
  Mhandisi Norbert Kahyoza.
  Na Rhoda James

  Imeelezwa kuwa uelewa juu ya upatikanaji wa ardhi, Ushiriki wa wananchi na ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa ili kupisha mradi wa bomba la mafuta litakalo jengwa kutoka kabaale nchini Uganda hadi Tanga Tanzania vitachangia katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa ardhi na kukamilisha shughuli za kimazingira kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo.

  Hayo yameelezwa hivi karibuni mjini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza wakati wa Warsha iliyolenga kujadili upatikanaji wa ardhi na kutathimini athari za Mazingira (EIA) ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta kwa serikali ya Tanzania na Uganda.

  “Serikali kutoka pande zote mbili lazima tuwe makini kuhusu upatikanaji wa ardhi, lazima wananchi wapate uelewa mzuri na waone uwepo wa umuhimu wa bomba hili la mafuta na faidi zake kwani mradi huu ni muhimu.” alisema mhandisi Kahyoza.

  Aidha, Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson alieleza kuwa warsha hiyo ya upatikanaji wa ardhi pamoja na masuala ya mazingira ni ishara nzuri ya mwanzo katika utekelezaji wa mradi huo wa bomba la mafuta.

  Vile vile mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda, Francis Elungat alisema kuwa Waganda wamekuwa wakijiuliza ni lini watafaidika na mafuta yao, hivyo amefurahishwa kuona kuwa mradi huo uko mbioni kuanza hivyo wananchi wa Uganda kufaidika na mafuta yao.
  Ujumbe kutoka Uganda wakifuatilia Mada zilizowasilishwa katika kikao cha wadau wa mafuta, kutoka kulia ni afisa Mwandamizi wa Mazingira, Jane Byaruhanga, wa pili ni afisa Mwandamizi wa Ardhi, Francis Elungat na afisa mwandamizi wa Ardhi Denis Karamagi.

  Mchakato wa upatikanaji wa ardhi na kushugulikia masuala ya mazingira ni hatua za awali za safari ya wananchi wa Uganda kupata faida za mali asilia inchini mwao.

  Aliongeza kuwa ujenzi wa bomba la mafuta na kiwanda cha kuchakata mafuta hayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki hivyo ni vema pande zote mbili zikubaliana katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.

  Naye Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Total Uganda, Jean Luc Bruggeman, alisema kuwa ni lazima kuwepo na maelewano ya pamoja kwa pande zote mbili juu ya nini kinahitajika na taratibu za upatikanaji wa cheti cha mazingira (EIA) ili kuwezesha kuanza shughuli za ujenzi wa mradi mapema, na kinachotarajiwa kufanyika kulingana na makubaliano ya nchi hizo mbili na kuelewana nani atafanya nini katika mradi huo.
  Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao cha wadau wa Bomba la mafuta kilichofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.

  Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Uganda, Kampuni ya Total E&P Uganda, wajumbe kutoka Halmashauri ya Tanga, Bandari ya Tanga na Dar es Salaam, Shirika la Reli Tanzania, Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Chuo cha Ardhi, Tanroads, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.

  0 0

  Kupitia mradi wa Airtel fursa ambao umekuwa ukitoa msaada mbalimbali kwa vijana nchini kwa kuwawezesha kufanikisha ndoto zao mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na mradi huo Bi Theresia Maliatabu leo amemtembelea mkurugenzi mkuu wa Airtel na kumkabidhi picha yake aliyoichora mara tu airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika miezi miwili iliyopita na kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwaajili ya kuboresha ubunifu wao.

  Akikabidhi zawadi hiyo Theresia alisema” vifaa hivyo vinanisaidia kubuni baadhi ya michoro ambayo ni ya kisasa zaidi, lakini hasa inanisaidia mazoezi katika kuchora na vile vile inanisaida kama sehemu ya kutangaza biashara yangu kupitia social media”.

  “Napenda kuwaambia vijana wenzangu kwamba wajiamini na vipaji walivyokuwa nazo wasikate tamaa kwani kila kitu kinawezekana na wasiache kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza, aliongeza Theresia

  Mpaka sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia vijana wapatao 4000. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA utaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi. Vijana wanahamasishwa wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani elimu inayotolewa ni bure kabisa bila gharama yoyote.
  Kijana mjasiriamali Theresia Maliatabu (Kulia) akimkabidhi picha aliyoichora kwa ubunifu wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso (Kushoto) kama shukrani yake kwa Airtel baada ya kuwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA "Tunakuwezesha" kwa kupatiwa vifaa vya kuboresha biashara yake, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (katikati). Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya mkutano wa mwezi wa wafanyakazi Airtel uliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao makuu morocco jijini Dar es salaam.
  Kijana Theresia Maliatabu mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiongea na wafanyakazi wa Airtel (hawapo pichani ) alipofika kwenye ofisi za Airtel makao makuu kukabidhi picha yake aliyoichora baada ya airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika miezi miwili iliyopita na kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwa ajili ya kuboresha kazi zao.

  0 0

  Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

  Kama inavyofahamika kuwa kila mashindano huwa na kanuni zinazosimamia mashindano husika, sasa basi kuelekea mashindano haya ya Copa Amerika waandaaji wamefanya marekebisho ya kanuni mbili ambazo zimetumika na kuzoeleka katika mashindano mbali mbali ikiwemo haya ya Copa Amerika. Kanuni zilizofanyiwa marekebisho ni kanuni ya 'MUDA WA NYONGEZA' na ile ya 'KADI YA NJANO'.

  Kanuni ya muda wa nyongeza (EXTRA TIME) ambayo katika mashindano haya kwa miaka yote imekuwa ikitumika kuanzia ngazi ya mtoano, robo fainali, nusu fainali na fainali iwapo timu zinatoka sare katika muda wa kawaida wa dakika 90, basi huongezwa dakika 30 na mshindi asipopatikana hupigwa mikwaju ya penati tano tano na mshindi kupatikana, kwenye michuano hii sheria hii itatumika katika mchezo wa FAINALI pekee. Kwenye hatua nyingine haitatumika bali timu zikienda sare basi moja kwa moja zitapigiana penati.

  Sababu zilizotolewa na waandaaji wa mashindano zinasema kuwa kwa hivi sasa nchini Marekani hali ya hewa ni joto kali sana. hivyo wachezaji wakicheza kwa dakika 120 yaani dakika 90 za kawaida na dakika 30 za nyongeza basi watakuwa wamechoka sana hali inayopelekea kushindwa kupiga penati kwa uzuri zaidi.

  Nayo kanuni ya kadi ya njano (YELLOW CARD) ambayo hutumika kwa mchezaji yoyote anayepata kadi tatu za njano basi hukosa mechi mbili zinazofuatia, katika mashindano haya ni kuwa mchezaji akipata kadi mbili za njano basi atakosa mchezo mmoja unaofuata.

  Lakini rekebisho lingine hapo hapo kwenye kadi ya njano ni kuwa mchezaji iwapo atapata kadi mbili kabla ya mchezo wa FAINALI yaani kwenye mchezo wa robo na nusu fainali, kadi hizo zitafutwa na ataweza kushiriki kwenye kipute hicho cha FAINALI, isipokuwa mchezaji yoyote akipata kadi nyekundu (RED CARD) kwenye mchezo wa nusu fainali hii haitafutwa hivyo ataukosa mtanange huo wa FAINALI.

  Hizo ni kanuni mbili zilizofanyiwa marekebisho tunazopaswa kuzifahamu, hebu sasa tuangalie kwa ufupi wasifu wa timu japo mbili zitakazoshiriki kwenye michuano hii.
  JAMAIKA

  Timu hii ya Jamaica almaarufu kama 'REGGAE BOYS' inatokea kwenye CONCACAF ikishiriki kama waalikwa. Kikosi hiki chenye nyota kama golikipa Andre Blake anayedakia klabu ya Philadephia Union ya Marekani, mlinzi Wes Morgan anayekipiga kwa mabingwa wa EPL Leicester City na Giles Barnes kiungo mahili wa klabu ya Houston Dynamo ya Marekani, chini ya kocha W. Schafer watategemewa kuleta upinzani mkubwa wakitumia mfumo wao wa 4-3-3, wakiwa na nguvu huku wakishambulia kwa kasi.
  MAREKANI

  Waandaaji wa mashindano haya maalum, pia wana uzoefu na michuano hii kwani wamekuwa wakialikwa mara kwa mara kushiriki kwenye michuani hii. Timu hii itaingia ikiwakosa nyota kadhaa akiwemo Jozy Altidore. Marekani haikuwa na kiwango kizuri msimu uliopita hali inayomfanya kocha Juergen Krinsman kutaka kuirudisha timu kwenye mstari angalau hata wafikie katika nusu fainali ya michuano hii. Marekani ina timu yenye mchanganyiko wa wachezaji wenye umri mkubwa takribani miaka 30 wapatao 8 watachanganyika na vijana wadogo waliochini ya miaka 24 ambao ni hatari sana. Timu hii itawategemea zaidi wachezaji kama Christian Pulsic kinda wa miaka 17 anayekipiga Borussia Dortmund, Kyle Berkerman wa Real Salt Lake ya Marekani, Jermaine Jones wa Colorado Rapids ya Marekani, mlinzi Geoff Cameron wa Stoke City na mshambuliaji Clint Dempsey wa Seattle Sounders FC ya Marekan.

  ENDELEA KUTEMBELEA LIBENEKE LA GLOBU YA JAMII KWA TAARIFA ZAIDI ZA MICHUANO HII.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Felix Lyniva wakifuatilia mada katika mafunzoa ambapo Halmashauri za Wilaya zao za Butiama na Rorya mkoani Mara ndio zimechaguliwa kuwa za kwanza kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za umma(PS3) katika sekta za afya, elimu na kilimo.

  HALAMSAHAURI Za Wilaya ya Rorya na Butiama mkoani Mara zimechaguliwa kuwa za kuanza utekelezaji wa mradi Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

  Tayari watendaji kutoka halamshauri husika wanapatiwa mafunzo ya siku moja leo na wiki ijayo madiwani wao nao watapatiwa mafunzo maalum ya namna ya kushiriki utekelezaji wa mradi huo. Mafunzo hayo ya wiki moja yatafanyika mjini Bunda. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


  0 0

  `Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.

  Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

  “Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.

  Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .Hata hivyo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.

  Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.

  Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha katika kila Halmashauri ambapo kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo.   Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Bendeyeko akifungua kikao kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama KinderuKatibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
   

  0 0

  Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.
  Vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo vikiwa kwenye toroli maalumu la kuhifadhia katika hospitali hiyo.
  Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.


  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo akikabidhi kombe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kahama,Anderson Msumba aliyeongozana na nahodha wa timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama. 
   Wachezaji wa timu ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kombe ilipoichapa timu ya Mgodi wa Buzwagi mabao 2 kwa 1. 
   Wachezaji wa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakisalimiana na viongozi mara baada ya kumalizika kwa mcheoz wa kirafiki ambapo timu ya Hospitali wilaya ya Kahama iliibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 . 
   Baadhii ya wananchi wakifuatilia zoezi la utoaji kombe kwa washindi hao.Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz  amezindua rasmi Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’  na kuwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku msanii Rich Mavoko akisaini mkataba wa kufanya kazi na Lebo hiyo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. 

  WCB inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Tanzania kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamuziki, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.

  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WCB, Diamond Platinumz alisema lengo la kuanzishwa lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sanaa ya muziki izalishe pato la taifa.

  Msanii Diamond ameomba serikali kuwaunga mkono ili waweze kusonga mbele maana kwa sasa amekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakimtegemea katika kufanya sanaa ya muziki.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz (wa pili kushoto) akiwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo ya ‘WCB Record Label’ ambayo ameizindua leo ndani ya hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na mameneja wake Hamis Tale na Mkubwa Fela. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Msanii Queen Darleen, Raymond na Hamonize. 
  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akisaini mkataba wa kufanya kazi na msanii Rich Mavoko huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo. Nyuma ni uongozi wa WCB na msanii Diamond.
  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akibadilishana mkataba na Rich Mavoko mara baada ya kusaini huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.

  0 0

  Kamera Yetu ilipata kuangazia baadhi ya Taswira kutoka katika Mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya kama ambavyo Taswira hapo juu ikionyesha moja ya Majengo yaliyopo katikati ya Mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
  Ankal Michuzi Akivizia miwa kwenye moja ya shamba la miwa lililopo Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
  Kijani Kibichi chenye Kumeremeta kikiwa kimezunguka baadhi ya Nyumba zilizopo Bondeni karibu na Soko Kuu la Tukuyu.
  Baadhi ya Magari yakikatiza katika Barabara Kuu ya kuelekea Kasumulu, Itungi mpaka Malawi.
  Machinjio ya Ng'ombe Tukuyu Mjini..
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa kufanya usafi katika fukwe za bahari ya Salender jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni na kulia ni Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda.
  Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53 zilizotolewa na Burhan Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini Dar es Salaam.
  Mkaazi wa mtaa wa Sea-View mzee Peter Kabelwa almaarufu kama Mzee Mzungu akishiriki zoezi la kuondoa uchafu uliozunguka katika fukwa za bahari ya Salender Bridge.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Umoja wa Ulaya wamezindua kitabu cha nishati jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kuwezesha Tanzania kuwa na nishati ya ukuwaji wa uchumi endelevu.
   Balozi, Roeland Van De Geer akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha (Empowerin Tanzania Energy for Growth and Sustainable Development) jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Nishati ya Umeme hapa nchini lazima iwe kwa maendeleo endelev kwa kuwa Tanzania inatakiwa kuwa ni nchi ya viwanda inahitaji kuwa na umeme wa uhakika.
    Balozi, Roeland Van De Geer akikata utepe kuzindua kitabu cha Nishati.
  Baadhi ya wadau wakiwa  wameshika vitabu vya nishati.

  0 0  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Prof James Mdoe, akielezea historia ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa ( wa tatu kutoka kushoto waliokaa mbele) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini  Prof James Mdoe ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele)  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi  huo.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico) limetakiwa kushirikiria uchumi wa nchi kutokana na  ubia uliopo kati ya Wabia na Serikali.

  Hayo ameyasema  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa,  Justin Ntalikwa wakati wa uzinduzi bodi mpya ya Stamico , amesema kuwa mashirika mengi ya serikali yanayosimamia madini ndiyo yamekuwa yakishikiria uchumi wa nchi.

  Amesema bodi inawajibu kuhakikisha stamico inabadilika  kutokana na  miradi iliyo chini yake inaendelezwa  na kusimamiwa ipasavyo  ili kuipatia serikali manufaa mbalimbali ikiwemo gawio  katika migodi ya ubia.

  Profesa Ntalikwa amesema kuwa bodi katika kufanya kazi zake moja ni kufanya usaili wa wafanyakazi kutokana nafasi nyingi ikiwemo ya mkurugenzi mtendaji  kukaimiwa  na zingine.

  Aidha amesema kuwa ina wajibu wa kuboresha mikataba iliyopo kwa kukaa na wabia ili pande zote ziweze kunufaika na manufaa yatokanayo na miradi ya uwekezaji katika sekta ya madini.

  Bodi hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni na  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo  inaundwa na wajumbe watano ambao ni pamoja na Abdalah  Mussa, Dkt. Coretha Komba, Felix  Maagi, Dkt. Lightness Mnzava, John  Seka chini ya Mwenyekiti wake  Balozi  Alexander Muganda.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing katikati ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa Wananchi,Meja Jenerali Venance Mabeyo wakati hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijeshi wa serikali ya China na Tanzania  katika hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa Wananchi, Meja Jenerali Venance Mabeyo akizungumza juu ya ushirikiano wa Tanzania na China katika kubadilishana uzoefu wa  kijeshi hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  KUTOKANA na kuwepo kwa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali  katika bahari ya hindi  kumesababisha serikali kukosa mapato yatokanayo na kodi ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba msaada wa boti kwa serikali ya China kwa ajili ya kufanya doria  katika  fukwe za bahari za jiji la Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa katika hafla ya ziara ya Meli za Kivita ya China iliyozuru jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kuwa  boti zikiwepo zitasaidia kufanya doria katika bahari ya hindi na kuweza kuua mtandao wa usafirishaji biashara zinazosafirishwa kwa boti kushushwa katika fukwe na kuingia mtaani.
  Amesema licha kuwepo kwa usafirishaji wa bidhaa katika bahari ya hindi kuwepo usafirishaji bidhaa lakini kuna matukio ya  uhalifu yanafanyika hivyo boti za doria zitafanya kazi na kuweza kukomesha uhalifu huo.

  Makonda amesema ujio boti huo utaendana na kuja kwa askari 300 wa China ambao watatoa mafunzo kwa askari wa Tanzania kuweza kutumia boti hizo pamoja na mbinu za kufanya doria za kuweza kuweakamata wahalifu wote katika fukwe zote.
  Aidha amesema kuwa doria hizo zitakwenda sambasamba na ndege ndogo pamoja na gari maalumu za kufanya doria hiyo kwa wale wanaokamatwa kuwekwa katika gari hizo.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe. Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akichangia jambo wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.


older | 1 | .... | 1241 | 1242 | (Page 1243) | 1244 | 1245 | .... | 3272 | newer