Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR ATEMBELEA MAGHALA YA KUHIFADHIA VYAKULA KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.

$
0
0

Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar .
          
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza bidhaa zilizopitwa na wakati. 

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi  Amina Salum Ali, amesema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi juu ya tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuwauzia vitu vilivyopitwa na wakati.

Amefahamisha kuwa, udanganyifu huo unaofanywa na wafanyabiashara huwasababishia wananchi kupata maradhi mbalimbali ikiwemo saratani.Akiwa katika ziara ya kukagua maghala mbalimbali ya chakula kisiwani Unguja kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani, Balozi Amina amesema serikali imechoka kuona wananchi wanauziwa vyakula visivyokuwa na kiwango kutokana na kumalizika muda wao wa matumizi.

Waziri huyo amekemea vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara kuuza vyakula vilivyokaa maghalani kwa muda mrefu hata kupindukia  miaka mitano, hali aliyosema ni kuwaathiri na  kuwadhulumu wananchi.“Wazanzibari tumechoka kulishwa michele mibovu. Tunasema sasa imetosha na hatutawafumbia macho wafanyabiashara watakaoendeleza vitendo hivyo,” alisema Waziri Amina.

Amesema serikali inakusudia kuweka bei elekezi kwa wafanyabiashara wote ili kuzuia  upandaji bei kiholela hali inayowapa usumbufu wananchi hasa wa kipato cha chini.Aidha Balozi Amina amesema kila mwaka ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani, serikali  imekuwa ikipunguza kodi za bidhaa muhimu kwa wafanyabiashara ili kutoa punguzo kwa wananchi.

Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni unga wa ngano, sukari na mchele.
Hata hivyo, ameeleza kusikitishwa kwake kwamba bei za bidhaa hizo zimebakia palepale au kuongezeka zaidi licha ya nia nzuri ya serikali.Ili kuandaa mazingira ya kuwapa unafuu wananchi, amesema serikali inakusudia kukaa na wafanyabiashara wote ili kujadili na kupanga mipango mizuri kwa itakayowaletea maendeleo wafanyabiashara hao na taifa kwa jumla.

Kwa upande wao, wafanyabiashara waliotembelewa na Waziri huyo,  wamemuhakikishia kuwa chakula kipo cha kutosha katika kipindi hiki cha kuelelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.Aidha wamesema chakula hicho kimeagizwa miezi mitatu kabla ya mwezi huo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mfanyabiashara Abdulghafar Ismail Mohammed wa kampuni ya Evergreen Ltd, ameiomba serikali kukaa pamoja nao pale inapotaka kufanya maamuzi yoyote yanayowahusu ili kuweka uwiano kwa upande wao, serikali na wananchi.

Ziara ya Balozi Amina ilihusisha maghala ya kampuni za Yassir Provision, Akhtar Enterprises Malindi, Evergreen Ltd Saateni, Sub Sahara Maruhubi, Azam Mtoni, Vigor Turkey Group  na Bopar Enterprises zote za Mombasa mjini Unguja.

Pamoja na kujua akiba ya chakula iliyopo nchini kupitia ziara hiyo, Waziri Amina pia alitaka  kujua hali ya mfumko wa bei kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saaeteni mjini Zanzibar.
WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.
 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari azindua matukio ya Siku ya Msanii 2016 Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wasanii wakati wa uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
Mwanamziki mkongwe wa miondoko ya rhumba Stara Thomas akizungumza na wasanii wenzake (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
Picha mbalilmbali za viongozi wa serikali na wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam. Picha na WHUSM

MKUTANO WA 5 WA MWAKA WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE WAFANYIKA JIJINI ARUSHA.

$
0
0
 Prof. Magimba (Kulia) akifungua mkutano wa 5 wa mapitio wa Mpango wa Taifa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambao unapitia na kupanga mikakati ya utekelezaji wa kutoa elimu,kukinga na kutibu magonjwa hayo nchini ambayo ni usubi,vikope(trakoma), kichocho, minyoo ya tumbo pamoja na matende na mabusha.Mkutano ambao unaendelea kufanyika mjini Arusha ili kwaajili ya kupambana na magonjwa hayo.
 Baadhi ya mdau wa mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele toka nchi mbalimbali akichangia mada kwenye mkutano huo.
Prof.Magimba mwenye tai nyekundu(aliyekaa katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja wadau wa maendeleo toka mashirika mbalimbali toka Tanzania na nje ya nchi.

HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO 2016/2017 MJINI DODOMA LEO

Vodacom yazindua huduma ya kutoa habari za ‘Papo Hapo’ za wasanii

$
0
0
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Global Publishers imezindua huduma itakayowawezesha wateja wake kupata habari kuhusu wasanii mbalimbali kila siku kwa njia ya SMS.

Kwa shillingi 100 tu kwa siku, mteja atakayejiunga na huduma hii ataweza kupata habari mbalimbali kuhusu msanii atakaemchagua. Ili kujiunga na huduma hii, mteja anatakiwa kutuma neno ambalo ni jina la msanii wake pendwa, mfano Lady Jaydee au Ali Kiba kwenda namba 15542.

“Huduma hii inaleng kuwaunganisha wateja wetu na wasanii wao pendwa, tunataka kuwaweka karibu. Na hii ni moja ya jitihada zetu kabambe za kutumia teknolojia kurahisisha na kufanya maisha kuwa murua kwa wateja wetu na hivyo kuwapa uwezo wa kupata habari zinazohusu wasanii wao kupitia simu zao za mkononi,” alisema Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.

Aliongeza kuwa ingawa huduma hii imeunganishwa moja kwa moja, mteja bado anao uwezo wa kujiondoa wakati wowote. Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema wanatarajia kutumia nafasi hii kutoka Vodacom Tanzania kuwapa wasomaji wao habari zinazowahusu wasanii wao pendwa kwa njia ya simu.

Mpaka sasa huduma hii ina wasanii nane ambao ni Alikiba, Lady Jaydee, Kajala, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Shilole and Rose Ndauka. Vodacom Tanzania na Global Publishers imeahidi kuongeza wasanii wengi zaidi kwenye huduma hii.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa huduma  ya kutoa habari za ‘Papo Hapo’ za wasanii mbalimbali  kila siku kwa njia ya SMS kwa kushirikiana na Global Publishers. Ili kujiunga na huduma hii mteja  wa mtandao huo anatakiwa kutuma neno ambalo ni jina la msanii wake pendwa, mfano Lady Jaydee au Ali Kiba kwenda namba 15542. Na kukatwa shillingi 100 tu  kwa siku,Kutoka kushoto ni Msanii wa Bongo movie,Kajala Masanja,Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho na Shilole”Shishi Baby”.
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa huduma  ya kutoa habari za ‘Papo Hapo’ za wasanii mbalimbali  kila siku kwa njia ya SMS kwa kushirikiana na Global Publishers. Ili kujiunga na huduma hii mteja  wa mtandao huo  anatakiwa kutuma neno ambalo ni jina la msanii wake pendwa,  kwenda namba 15542. Na kukatwa shillingi 100 tu  kwa siku.Kutoka kushoto Msanii wa Bongo Movies Auntie Ezekiel,Kajala Masanja na Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho. 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole”Shishi baby”akiofafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa huduma  ya kutoa habari za ‘Papo Hapo’ za wasanii mbalimbali  kila siku kwa njia ya SMS kupitia mtandao wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Global Publishers. Ili kujiunga na huduma hii mteja  wa mtandao huo  anatakiwa kutuma neno ambalo ni jina la msanii wake pendwa,  kwenda namba 15542. Na kukatwa shillingi 100 tu  kwa siku.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akifurahia jambo na Msanii wa bongo movies Auntie Ezekiel na wasanii wengine Kajala Masanja, Shilole”Shishi Baby” na Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho wakati wa Uzinduzi wa huduma  ya kutoa habari za ‘Papo Hapo’ za wasanii mbalimbali  kila siku kwa njia ya SMS kwa kushirikiana na Global Publishers. Ili kujiunga na huduma hii mteja  wa mtandao huo anatakiwa kutuma neno ambalo ni jina la msanii wake pendwa, mfano Lady Jaydee au Ali Kiba kwenda namba 15542 na kukatwa shillingi 100 tu  kwa siku.
 

DKT SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA MJINI LEO, ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama, wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwashukuru kuwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza na kuwashukuru wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi wa marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani 
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
 

TAASISI YA BENJAMINI MKAPA NA THET WASAINI MKATABA KWAJILI YA KUTOA MAFUNZO YA AFYA YA JAMII.

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maendeleo ya Mradi wa miaka mitatu ambao utashirikisha vyou vya afya ya jamii pamoja na hospitali za rufaa za kanda ya ziwa pamoja na kusaini mkataba ya makubaliano ya kuendesha mradi wa wataalamu wa afya ya jamii pamoja na watu wa kada ya afya wa mikoa ya kanda ya ziwa. 

Amesema kuwa mradi huo unashirikisha Taasisi ya Benjamini Mkapa, Tropical Health Education Trust(THET) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwaajili ya kuwapa mafunzo wafanyakazi pamoja na wafunzi wa vyuo vya kada ya afya ili kuimarisha afya ya jamii hapa nchini.


Ellen amesema kuwa Mradi wa kada ya afya umeshaanza tangu Machi huu na utagharimu kiasi cha shilingi bilion 3.3 kwaajili ya kuimarisha uwezo wa Wataalam wa Afya ya Jamii hapa nchini ambao unalenga katika kuimarisha vyuo vya Afya  kumi na kutoa Mafunzo katika hospitali za kanda ya ziwa.


Vyuo hivyo vilivyopo mikoa ya kanda ya ziwa vya kada ya afya ni Bukumbi school of Nursing, Ngudu School of Invironmental Health, Tandabui Institute of HST, Geita Nursing & Midwifery School, Bishop Kisula College of HS, Rubya Health Training Institute, Karagwe Institute of Allied Health Sciencies, Murugwanza School of Nursing, Kahama SON, Kolandoto of Nursing na Hospitali za Rufaa za kanda ya ziwa zitakazo fikiwa na mradi huoni Sekou Toure Geita Regional Referral Hospital, Kagera na Shinyanga.
Kuanalia uhaba wa watumishi wa afya.
Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusaini Mkataba wa kushirikiana katika kutoa mafunzo ya afya ya jamii ili kupunguza uhaba wa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini.
amesema kuwa kupitia mradi huo wataalam wa afya ya jamii wataongezewa ujuzi pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kanda ya ziwa watapata ujuzi ambao utakua unastahili. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakisaini mkataba kati Taasisi ya Mkapa na Tropical Health Education Trust(THET) kwaajili ya kutoa mafunzo kwa wananchi wa kada ya Afya ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa kada ya afya waliopo katika huspitali zilizopo hospitali za rufaa za kanda ya ziwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakibadilishana mikataba jijini Dar es Salaam leo, Kwaajili ya mradi ambao umaeshirikisha Taasisi pamoja na serikali kwaajili ya kusaidi wataalam pamoja na wanafunzi wa kada ya afya hapa nchini.

Tatizo la hewa ya Ukaa kupungua hapa nchini.

$
0
0


Frank Mvungi-Maelezo 

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umeanza kufanya utafiti utakaosadia kupunguza kiwango cha Hewa ya Ukaa (green house gases) kinachozalishwa kutokana na shughuli za ujenzi ili kupunguza uharibifu wa mazingira. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Heri Hatibu kutoka wakala huo amesema utafiti utasaidia kupunguza gharama za Ujenzi hapa nchini. Akizungumzia Malengo ya Utafiti huo Hatibu amesema kuwa, utasaidia kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza hewa hivyo kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine. 

“Sekta ya Ujenzi inachangia asilimia 40 ya hewa ya ukaa hivyo lengo la utafiti huu ni kusaidia kuondoa tatizo hili mara baada ya utafiti wetu kukamilika.” Alisisitiza Mhandisi Hatibu. Aidha Hatibu amesema kuwa, utafiti huo utawezesha kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo kwenye hatua ya ujenzi na hata wakati wa matumizi ya majengo husika. Pia utachochea matumizi ya vifaa vya Ujenzi vinavyopatikana katika maeneo ya karibu na shughuli za ujenzi. 

Pia utafiti huo utasaidi kutoa elimu kwa wadau wa ujenzi kuhusu nishati mbadala katika kutekeleza shughuli za ujenzi, ikiwemo kuacha kukata miti. Vile vile wananchi wataelimishwa kuhusu njia bora za uchomaji wa matofali ili waweze kutumia vifaa vingine badala ya kukata miti kwa ajili ya uchomaji matofali. 

Matokeo ya utafiti huo unaotarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu yatasaidia wadau wa sekta hii kupanga mipango ya ujenzi itakayosaidia kupunguza athari katika mazingira zinazosababishwa na matumizi makubwa katika uzalishaji vifaa vya ujenzi na hata katika ujenzi.Utafiti huo unafanyika katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga.

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEI LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific  ACP, mkutano  uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
 Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya  kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandaaji wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific  ACP baada ya kuhutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
(Picha na OMR).

Hifadhi ya Selous yapoteza asilimia 90 ya Tembo wake.

$
0
0


Na Daudi Manongi

Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya Tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.

Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na ujangili basi watatoweka kabisa.

Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40 iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.

Aidha ripoti hiyo inaonyesha hathari kubwa kiuchumi itakayotokea kutokana na kwamba Tanzania kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.

Pamoja na Hayo Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.

Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.

Rais Wa Chirikisho La Ngumi Afungiwa

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAMKO KUKEMEA WIMBI LA VITENDO VYA MAUAJI VILIVYOANZA KUSHAMIRI NCHINI.

$
0
0
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini, hususani kanda ya Ziwa, Mkoa wa Pwani, na Dar es Salaam.

Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake. 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote nchini. 

Baadhi ya matukio hayo kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tume yametokea usiku wa Mei 11, 2016 katika kitongoji cha Nyigumba, Kijiji cha Sima Wilayani Sengerema, Mwanza, ambako watu watano (5) wa familia moja waliuwawa kwa kukatwa mapanga; Mei 18 watu watatu (3) pia waliuwawa kwa kukatwa mapanga wakiwa katika nyumba ya ibada, Msikiti wa Rahman, eneo la Ibanda relini, mtaa wa Utemini, Kata ya Mkolani,Wilaya ya Nyamagana, Mwanza; Usiku wa Mei 25, mwanamume mmoja na mkewe waliuwawa kwa kukatwa mapanga kijijini Manzavi, Wilayani Butiama, Mara.

Aidha, mnamo Mei 22, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa, Mwanza, Bwana Alphonce Musanyenzi aliuawa. Mauaji mengine yametokea Mei 18, Mkoani Pwani, Askari Polisi, Sajenti Ally Salum Kinyogoli alipouwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika. Mei 23, jijini Dar es Salaam, eneo la Kiwalani, watu wanne (4) waliuawa kwa kuchomwa moto wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao; Mei 26, Bi. Anathe Msuya aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Matukio haya ya ukatili yanakiuka haki ya kuishi iliyoainishwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria za nchi, matamko na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ya kikanda na kimataifa.

Kufuatia wimbi hili la mauaji linaloonekana kuendelea nchini, Tume inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya kikatili.

Mbali ya ukiukaji mkubwa wa haki ya msingi ya kuishi, mauaji haya na matukio haya pia ni kinyume na mafundisho ya imani zetu mbalimbali, hivyo yasifumbiwe macho na kuachwa yaendelee, kwani yanaweza kuleta mazoea mabaya ya kuona suala la kuuwa ni jambo la kawaida na hivyo kuhatarisha amani, maisha ya watu na jamii. 

Hivyo, Tume inashauri yafuatayo:
1.Serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali. Jeshi la Polisi lihakikishe watu wote waliohusika kutekeleza mauaji haya wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake.

2.Tume inawataka pia wananchi wahakikishe wanashirikiana na vyombo vya dola kufichua maovu na kubaini uvunjifu wowote wa sheria na haki za binadamu ndani ya jamii, na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuzuia matukio kama haya kujirudia, au kusaidia upelelezi wa mauaji haya na matendo mengineyo ya uvunjifu wa sheria.

3.Jamii ijenge utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.
4.Mamlaka za Serikali za mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
5.Tume inatoa rambirambi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya na pole kwa majeruhi.
Jukumu la ulinzi na utetezi wa haki za binadamu ni letu sote!

 Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Mei 31, 2016.

MBEYA CITY KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI NCHINI MALAWI.

$
0
0
TIMU ya Mbeya City imeanza mikakati yake ya kujiandaa kwa msimu mpya huku uongozi wa timu hiyo ukiamua kuingia msituni na kuamua kwenda nchini Malawi kucheza michezo mitatu ya kirafiki.

Kwenye ratiba hiyo, City  imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka ‘dimbani’ Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18  kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo.

Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano  kwenye kikosi cha City, Dismas amesema kuwa mchezo wa pili  nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni  21 na kumalizia na Mzuni Juni 25.

“Baada ya mchezo huo  wa pili jijini Lilongwe,tutarudi kwenye mji  ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 huu utakuwa mchezo wa mwisho kwenye ziara hii ya michezo ya kirafiki, baada ya hapo tutarudi nyumba tayari kwa michezo mingine ambayo  imepangwa ukiwemo  dhidi ya Simba tutakaocheza Morogoro,"amesema Ten. 

Kama mambo yatakwenda sawa, ratiba hii inaweza kuwa na ongezeko la  michezo miwili ya kirafiki katikati ya mwezi julai kabla ya mchezo wa mwisho wa mwezi huo dhidi ya Simba na mwingine  mwanzoni mwa mwezi wa nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.

ZIJUE TIMU ZITAKAZOSHIRIKI COPA AMERICA CENTENARIO-USA 2016

$
0
0
Na David Mwaipopo, Globu ya Jamii.

Zikiwa zimebaki siku mbili tu ambapo kwa wale wa ughaibuni wanasema 'Two days to go' ili kuanza kwa Mashindano yenye mvuto wa aina yake na utamu wa kabumbu lenye ufundi na vipaji vya hali ya juu toka Bara la Amerika ya kusini. Leo katika mfululizo wa kuelekea michuano hii tunaangazia timu shiriki,makundi yao na wasifu wa baadhi ya timu.

Timu zitakazo shiriki michuano hii maalumu ya kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni timu 16, ambapo timu 10 ni wanachama wa shirikisho la kabumbu la Amerika ya Kusini (CONEMBOL) na timu 6 ni waalikwa ambazo zote zinatoka shirikisho la kabumbu la Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF). Nchi hizo 16 ni Argentina, Brazil, Bolivia, Chile, Colombia, Equador, Paraguay, Peru, Uruguay na Venezuela (CONEMBOL). Costa Rica, Haiti, Jamaica, Mexico, Marekani na Panama (CONCACAF).

Timu hizi zimegawanywa katika makundi manne yenye timu nne kila kundi, ambapo michezo hiyo itachezwa kwenye viwanja vya mji kumi tofauti nchin Marekani. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
CHILE

Hawa ndiyo wanaolitetea taji lao walilolitwa mwaka jana 2015, Chile wanajivunia wachezaji kama mshambuliaji Alexis Sanchez, mshambuliaji mwenye nguvu na kasi anayefanya vizuri kwenye EPL akiwa na klabu ya Asernal. Pia watamtegemea sana kiungo wao mtukutu lakini makini sana awapo uwanjani, huyu ni Artulo Vidal, huyu ndiyo muhimili wa timu kwani huwa na jukumu kubwa la kuunganisha timu. Tegemeo lao jingine ni kwa golikipa wao Claudio Bravo anayekipiga kwenye klabu ya Barcelona ya nchini Hispania. Swali ni je watalitetea taji lao hasa baada ya kuachana na kocha aliyewapa mafanikio makubwa pamoja na taji hilo JORGE SAMPAOLI?

URUGUAY

Hawa ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hii kwani wao wameweza kuchukuwa taji hilo mara nyingi kuliko timu yoyote ya ukanda huo. Chini ya kocha OSCAR TABAREZ, Uruguay watamtegemea sana mshambulizi anayesukuma ndinga katika timu ya PSG nchini Ufaransa Edson Cavani kufuatia kuumia kwa mshambuliaji nguli kabisa aliyechukuwa kiatu cha ufungaji bora kwenye Laliga Luis Suarez. Katika idara ya ulinzi watamtegemea zaidi Diego Godini, mlinzi mwenye roho ya paka anayepambana mpaka dakika ya mwisho.Mchezaji mwingine wa kuangaliwa katika kiosi hiki ni Max Perreira.

BRAZIL

Brazil wanaonekana kutoipa umuhimu mkubwa sana michuano hii bali wataelekeza nguvu kwenye michuano ya Olimpiki itakayo fanyika nchi humo baadaye mwaka huu, hii inatokana na kuwaacha nyota wake wengi kama Oscar, Thiago Silva,David Luiz na mshambuliaji matata Neymar wakisema wazi kuwa hao wote watashiriki kwenye michezo ya olimpiki. Sasa kazi kubwa kwa kocha Carlos Dunga ni namna atakavyo watumia wachezaji machachali kama F.Coutinho wa Liverpool, mlinzi Dani Alves, mkongwe Ricardo Kaka mshambuliaji mwenye nguvu Hulk na wengineo chipukizi.

ARGENTINA

Sijui mfumo gani atakaoutumia kocha GERARD MARTINO katika mashindano haya hasa kutokana na hazina kubwa ya wachezaji alionao kikosini, ingawa tunategemea kuona wachezaji wa Argentina watacheza wakimzunguka gwiji wa wakati huu mchezaji bora wa dunia mara tano Lionel Messi. Katika ushambuliaji Messi ataanza na nani kati ya Gonzalo Higuaini au Sergio Aguero na nyuma yao kutokea pembeni wakiunganishwa na A.Di Maria na ukutwa utakaoongozwa na Nicolas Otamendi.

Tutaendelea kuwaletea taarifa na dondoo mbali mbali kuhusu michuano hii kadri siku zinazoendelea.

U.S. GOVERNMENT CALLS ON GOVERNMENT OF TANZANIA TO EXPAND INVESTMENTS IN HEALTH COMMODITIES

$
0
0
June 1, 2016 - Speaking today at an end-of- project event in Dar es Salaam for the Supply Chain Management System (SCMS) and USAID | DELIVER PROJECT, U.S. Agency for International Development (USAID) Health Office Director Janean Davis emphasized the need for the Government of Tanzania to prioritize health commodities and the national public health supply chain. The event marked 10 years of supply chain strengthening in Tanzania and showcased the projects’ most successful interventions that will be key to building momentum around supply chain management.

“On behalf of USAID, I am pleased that the Government of Tanzania allocated funds toward health commodities, and urge the various ministries represented here to ensure that funds from your respective health budgets are disbursed toward that goal,” Davis said. “Consistent, transparent supplies and distribution networks for medicine and equipment are one of the keys to unlocking a healthier, more prosperous future for Tanzania.”

SCMS and USAID | DELIVER — working in concert with Tanzania’s Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children, the Ministry of Health in Zanzibar, and other health commodity supply chain stakeholders — have been procuring health commodities and providing technical assistance in supply chain management for the past decade, helping to make health commodity supply chains in Tanzania more effective and efficient.

This technical assistance was made possible through USAID under the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and the U.S. President’s Malaria Initiative.

Collectively, as of March 2016, the two projects had invested more than $466 million to strengthen Tanzania’s health commodity supply chain, including the procurement of more than $375 million worth of medicine and equipment to fight HIV/AIDS, malaria, and other diseases. This amount also included $67 million in reproductive and maternal health commodities.

The projects’ interventions have had visible impact at all levels, from program management at the national level to end users at the approximately 5,000 service delivery points in Tanzania. Among the results highlighted on Wednesday were strengthening data usage for timely policy decision making; ensuring the efficacy of medicines by improving storage facilities and commodity management practices; and improving organizational capacity to sustainably manage the health commodity supply chain in Tanzania.

Systems strengthening at the local government level and country ownership were two key themes at the end-of- project event, with stakeholders presenting lessons learned on what works to sustainably strengthen health systems in service of consistent, accountable supply chains. An interactive marketplace exhibition prior to the event gave participants a forum to discuss best practices for capacity building.

"These projects have worked hand in hand with the Ministry to strengthen Tanzania's health system in providing innovative and sustainable supply chain solutions," said Dr. Mpoki Ulisubisya, Permanent Secretary for the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children. "Today we join hands in reflecting on a decade of partnership that has led to the strengthening of pharmaceutical supply chains, saving lives both here in mainland Tanzania and Zanzibar.

" To request more information about this event, please email Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Senior Information Specialist at U.S. Embassy Dar es Salaam.
A health care worker conducts physical inventory in a health facility in Kinondoni District. U.S. Government support in Tanzania has strengthened the health commodity supply chain and resulted in the procurement of over $300 million worth of medicine and equipment to fight HIV/AIDS, malaria, and other deadly diseases.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATUA MKOANI TANGA, AZUNGUMZA NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI, ATEMBELEA MSITU WA MAPANGOPORI YA AMBONI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.

YANGA YAIGEUKA TFF, SASA KUFANYA UCHAGUZI JUNI 11.

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii.
UONGOZI wa Yanga umesema hawawezi kupangiwa tarehe ya Uchaguzi na Shirikisho la Mpira  wa miguu (TFF) na tayari wameshapanga tarehe ambapo kwa sasa utafanyika Juni 11 badala ya ile ya awali Juni 25.Uamuzi huo umekuja baada ya kukutana kwa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo pamoja na bodi ya wadhamini. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo ilipewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Yanga na Baraza la Michezo la Taifa(BMT). 

TFF ilishaanza mchakato wa utoaji fomu kwa wanachama wa klabu hiyo na hadi juzi wagombea tisa wameshajitokeza kuchukua na kurudisha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali. Akizungumza juu ya mabadiliko ya uchaguzi ya klabu hiyo Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesema kuwa wao kama klabu wameamua kupanga tarehe wanayohisi itawafaa. Uongozi wa Yanga ulishtushwa na agizo la TFF kusimamia uchaguzi wao bali suala hilo lilizua pia maswali mengi kutoka kwa wanachama wa klanbu hiyo.

Amesema wanachama hao walishangazwa na kitendo cha Serikali kuitaka TFF kusimamia uchaguzi huo wakati wao kama klabu wana kamati ya uchaguzi. Baraka amesema kuwa kitu cha ajabu zaidi ni TFF kutoa fomu hizo bila kuwasiliana nao ili kujua kma wanaochukua fomu hizo ni wanachama halali na kama wana Yanga wameamua kuja na msimamo wao na kupanga tarehe za mchakato mzima wa uchukuaji fomu hadi kutangaza matokeo.

Klabu imepanga ratiba yake ambapo June 2 na 3 itakuwa siku ya kuchukua fomu na kurejesha huku June 4 ikiwa ni siku ya mchujo wa awali na kubandika orodha ya wale waliopita, June 5 itakuwa ni siku ya mapingamizi huku June 6 na 7 ikiwa ni siku ya kupitia mapingamizi, kufanya usaili wa awali na kupeleka majina ya waliopita TFF. June 7 hadi 10 itakuwa ni siku ya wagombea kufanya kampeni kuelekea siku ya uchaguzi ambayo ni June 11 huku matokeo yakitangazwa siku Juni 12. Alisema uchaguzi huo utatumia katiba yao ya mwaka 2010 huku wanachama wakiruhusiwa kutumia kadi walizonazo zikiwemo zile za Posta Bank pamoja na CRDB.

"Tunapenda wanachama wetu kufahamu kuwa kadi zote zitatumika kupiga kura hivyo wasiwe na wasiwasi kikubwa wawe wamelipia kadi zao za uanachama licha ya kutumia katiba ya 2010", amesema Baraka. Akitolea ufafanuzi juu ya fomu za awali zinazotolewa na TFF, baraka amesema kuwa watafanya utaratibu kwa kushirikiana na TFF kwani hawana hakika kama kweli ni wanachama au laa. Baraka amesema, pia wanashangazwa na kauli za viongozi wa TFF kusema kuwa hawautambua uongozi uliopo madarakani wakati majina ya viongozi wa klabu hiyo yapo. "Kama ni kweli hawatambui uongozi wetu mbona barua zao zinapitia kwa mwenyekiti na katika makombe yetu tuliyoshinda pongezi zilienda kwa mwenyekiti, iweje leo waseme hawatambui uongozi uliopo?", amesma Baraka.

Wakati huo huo.
YANGA YAWASHUTUMU VIGOGO WA SERIKALI NA TFF KUHUJUMU UCHAGUZI WAO.
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema umebaini mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya watu ili kutaka kuvuruga uchaguzi wao na lawama hizo zimetupwa moja kwa moja kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo, viongozi wa Serikali pamoja na watendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF). Yanga si wa kwanza kutupa lawama kwa TFF kwani ni juzi tu kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) alielekeza lawama zake kwa mmoja wa watendaji wa TFF. 

Kinacholalamikiwa zaidi kwa mtendaji huyo ni kuchelewesha kwa makusudi zoezi zima la uchukuaji fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali. Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Afisa habari wa Yanga, Jerry Muro alisema kuwa wanashangazwa na kitendo cha baadhi wa watendaji hao kutaka kuwahujumu ila kwa bahati mbaya hujuma hizo zimegonga mwamba kwani uchaguzi wao utafanyika na tayari wana ushahidi wa kutosha juu ya watu hao. 

Jerry amesema kuwa tayari wana ushahidi wa sauti na video unaoonesha mipango ya kuharibu uchaguzi wa klabu yao. "Tunawajua watu wanaotaka kuvuruga klabu yetu na tuna ushahidi wa sauti na video unaoonesha vile vyote walivyokuwa wanavipanga", amesema Muro. Kinachosubiriwa sasa ni kuukamilisha ushahidi huo na kuuweka hadharani ili watu wabaini hujuma wanazofanyiwa. 

Muro amewataka watu hao wasithubutu kuendelea kuingia uchaguzi wao na endapo wataendelea na vitendo hivyo wataonja joto ya jiwe.

MATUKIO BUNGENI WAKATI WA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO MJINI DODOMA LEO.

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, Bungeni Mjini Dodoma leo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (Kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss Nyimbo, mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mjini Dodoma leo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo ambapo kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kushoto kwake ni naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma mara baara ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo.

TAARIFA KWA WANAJUMUIYA WA TANZANIA HOUSTON COMMUNITY (THC) NA UMMA KWA UJUMLA

$
0
0
Uongozi wa Tanzania Houston Community (THC) unapenda kukanusha taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa mitandaoni ya kwamba ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Mh. Balozi Wilson Masilingi haukufanya lolote wakati jumuiya yetu ilipopatwa na misiba miwili ya Bw.Henry Kiherile na Bw.Andrew Nicky Sanga iliyotokea kwa nyakati tofauti mapema mwezi April mwaka huu.
Uongozi wa THC unapenda umma utambue kwamba tulipata na tunathamini sana ushirikiano ulioonyeshwa na kutolewa na ubalozi pamoja na balozi mwenyewe Mh. Masilingi wakati wa misiba hiyo miwili na hata baada ya shughuli hizo za misiba kumalizika.
Marehemu Andrew Sanga ( kushoto ) na Marehemu Henry Kiherile ( kulia ) enzi za uhai wao

Baadhi ya mambo yaliyofanywa na balozi ni kuwatafuta viongozi wa jumuiya THC na kuzungumza nao mapema baada ya misiba hiyo kutokea (balozi alitutafuta viongozi na si vinginevyo) ambapo alizungumza na Rais wa jumuiya Bw. Daudi Mayocha kwa simu na Katibu mkuu wa jumuiya Bw. Michael Ndejembi na kuwapa pole kwa niaba ya familia na jumuia nzima.
Uongozi unafahamu kwamba sababu za balozi kushindwa kufika Houston wakati wa misiba hiyo ni yeye kumuwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli kwenye kongamano la DICOTA lililokuwa likifanyika jijini Dallas, Texas. Tunatambua pia kwamba nia ya balozi kuja Houston bado iko pale pale.
Aidha Balozi Masilingi alimtuma afisa ubalozi Bw. Dismas Assenga kumuwakilisha katika shughuli za Misa na Kuaga mwili wa marehemu Andrew Nicky Sanga, ambapo afisa huyo pamoja na mambo mengine alitoa salamu za rambirambi toka kwa balozi na alikabidhi rambirambi ya $500 kwa kila familia pamoja na kuzungumza na wafiwa hao kwa nyakati tofauti.
Kwa taratibu za kiupelelezi Uongozi wa THC hauwezi kutoa taarifa zaidi ya namna suala hili linavyoshughulikiwa kati ya vyombo vya usalama nikimaanisha HPD Homicide Department na Ubalozi wa Tanzania lakini tunatambua kwamba ubalozi unafuatilia kesi zote mbili kwa ukaribu sana.
Uongozi wa THC unasisitiza kuwa hauhusiki kwa aina yoyote na Waraka (Petition) unaosambazwa kwenye mitandao kumchafua Balozi Masilingi na ubalozi wetu wa Washington D.C kwa ujumla.

Daudi Mayocha,
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Houston (THC)
thc.leaders@gmail.com

SHEAR ILLUSIONS AFRICA YAADHIMISHA MWAKA MMOJA TANGU UZINDUZI WA KIPODOZI CHA LUV TOUCH MANJANO

$
0
0
Kampuni ya Shear Illusions imehadhimsha mwaka mmoja tangu uzinduzi wa Kipodozi Pendwa cha LuvTouch Manjano. Kipodozi cha LuvTouch kilizinduliwa mnamo tarehe 31 May mwaka 2015 jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi aliyekuwa mke wa Waziri Mkuu wa zamani Mh. Mama Tunu Pinda katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika maadhimisho hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions mama Shekha Nasser amewashukuru wanawake na Watanzania kwa ujumla kwa kufanikisha kutambulika kwa bidhaa za LuvTouch Manjano. 

LuvTouch ni Brand ya Kipodozi cha kwanza nchini inayomilikiwa na mwanamke mzalendo wa Kitanzania. Kupitia bidhaa hiyo pia imeanzisha Taasisi ijulikanayo kama 'Manjano Foundation' yenye lengo kuu ya kuwasaidia wanawake kiuchumi. Katika mwaka mmoja tangu uzinduzi wa bidhaa za LuvTouch Manjano, Taasisi hiyo imefanikiwa kuwaelimisha zaidi ya wanawake 195 katika mikoa mitano nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Arusha na Dodoma. 
Pia katika kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuwakopesha wanawake mitaji ya vipodozi vya LuvTouch Manjano yenye thamani ya shilingi milioni 45 (TSh.45,000,000). Akieleza zaidi mama Shekha Nassr amesema ataendelea kuwashika mkono wanawake wenzake kadiri ya uwezo wake unavyoruhusu kwa lengo la kumkomboa mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa Ajira.Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wanawake walio washiriki wa mradi wa Manjano Dream-Makers na wadau (Mentors), washauri na watu waliojitolea kuwasaidia washiriki hao.

Wanawake na washauri waliohudhuria hafla hiyo walimpongeza mama Shekha Nasser kwa moyo wake wa kujitolea na kuwabeba wanawake vijana. Mmoja wa wazungumzaji na mdau wa mradi, mwanasaikolojia maarufu aunt Sadaka Gandi alisema, ameishi na wanawake wengi nchini lakini hajawahi kuona Mwanamke mwenye moyo wa kujitolea kama wa Shekha. Amewaasa wanawake walionufaika na mradi huo kufanya kazi kwa bidii kupitia Mradi huo kwa kuwa wao wanabahati sana kunufaika kwa kuwa wapo wanawake wengi nchini wasiokua na kazi na wangetamani kunufaika lakini wamekosa nafasi hiyo
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images