Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 122 | 123 | (Page 124) | 125 | 126 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm akitoa mada kuhusu haki za binadamu jinsia na mitazamo ya Mataifa Mbalimbali ulimwenguni kuhusu Uhuru wa Habari na Haki za Binadamu siku ya mwisho ya Kongamano la maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa maoni yake katika kuchangia Azimio la Arusha la kupaza sauti za waandishi wa habari kudai uhuru wa habari kwenye siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jijini Arusha.
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakati wa kufunga kongamano la Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jioni jijini Arusha.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Shinyanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili leo Mei 04-2013. Picha na OMR.

  0 0


  KAMISHNA Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akikagua Guard ya heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Ziwa leo tarehe 4 Mei, 2013 katika viwanja vya Gereza Shinyanga.
  Kamishna Jenerali wa Magereza akimvalisha Nishani ya Utumishi wa muda Mrefu na Tabia njema Mkuu wa Magereza Mkoa Shinyanga, ACP Abdul Kasim Mgwanda. Jumla ya Maafisa na Askari 42 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamevalishwa Nishani mbalimbali Leo tarehe 4 Mei, 2013.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Ally Nasoro Lufunga( wa kwanza Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anna Rose Nyamubi( wa pili kutoka kulia) Mara Baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Leo tarehe 4 Mei, 2013.
  Guard Maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja hayupo kwenye picha kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza lililofanyika katika viwanja vya Gereza Shinyanga Leo tarehe 4 Mei, 2013.

  0 0

   Children from New Life Home in Dar es Salaam enjoy a ride on a toy train during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.
    Tatu Issa from New Life Home orphanage center in Dar es Salaam get a ‘face lift’ during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.

  One of the children from New Life Home orphanage center in Dar es Salaam engages in jumping castle during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.
   Women Footprints Initiative ( WOFI) Neema Msuya, address the media at charity family bonanza that provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.

   ============  ============  ==========  Watoto yatima washiriki tamasha la hisani la WoFI.


  Dar es Salaam Mei 4, 2013: Shirika la Women Footprints Initiative (WoFI), leo limefanya tamasha la hisani la familia lijulikanalo kama Cheza Time na kushirikisha watoto kutoka vituo vya kulelea watoto yatima ambao wamecheza michezo mbalimbali na kupata fursa ya kujumuika na ndugu zao. Tukio hilo la aina yake limefanyika katika viwanja vya Leaders Club.  

  Meneja miradi wa WoFI Neema N. Msuya amesema kuwa pamoja na kutoa burudani za michezo, tamasha hilo pia limetumika kupata fedha za kusaidia vituo hivyo vya watoto yatima na kuendeleza miradi ya wanawake inayoendeshwa na shirika hilo kwa lengo la kusaidia watoto na kuwawezesha kina mama kiuchumi..  

  Alisema kuwa kusudi kubwa ya shirika la WoFI ni kuwawezesha watoto hao kupata mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu na kuyataka makampuni, mashirika na watu binafsi kujitokeza kusaidia ili kuwajengea watoto hao msingi imara wa maisha yao ya baadaye.


  “Tamasha  la hisani la familia tunalofanya hapa leo linakusudiwa kuwa tukio la kila mwaka ambalo, mbali ya kuhamasisha wahisani kuchangia mfuko wa shirika, litatumika kama chombo cha kuwaunganisha watoto na ndugu na jamaa zao huku wakiburudika na vinywaji baridi, michezo mbalimbali pamoja na kucheza muziki”, alisema.


  Tamasha la leo lililovuta hisia za watu mbalimbali lilishuhudia watoto wachangamfu wakishiriki michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuruka, kuogolea na kukimbia ndani ya gunia. Watoto hao pia walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao vya kuimba na kucheza muziki.


  Shirika la WoFI ambalo siyo la kibiashara vile vile huendesha kampeni ya kuwaelimisha wasichana walioacha shule kwa sababu mbalimbali kuachana na tabia hatarishi na kujishughulisha na biashara halali ili kujipatia kipato cha kuwasaidia katika maisha yao. Kampeni hii inafahamika kama Binti Amka.


  Kampeni nyingine inayoendeshwa na shirika hili inajulikana kama Jitambue uwezo wako Sasa ambayo inawahamasisha wasichana wa shule za sekondari kusoma kwa bidii na kushinda vishawishi vilivyo mbele yao na hatimaye kutimiza ndoto za kuwa na maisha bora hapo baadaye. 


  0 0

  BENDI ya Mashujaa imetangazwa kutoa burudani katika shindano la Redds Miss Kibaha 2013 shindano lililopangwa kufanyika Mei 17 katika ukumbi wa Container Mailimoja Kibaha.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) Khadija Kalili ilisema kwamba tayari wamemalizana na uongozi wa bendi ya Mashujaa hivyo ndiyo burudani itakayorindima na kuwasindikiza wanyange wa Redds Miss Kibaha.

  “Uteuzi wa bendi ya mashujaa umekuja baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya burudani ambayo itakidhi kiu kwa wakaazi wa Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa ujumla hivyo kura nyingi likwenda kwa bendi ya Mashujaa naamini siku hiyo mabo yatakuwa bambam” alisema Kalili.
  Baadhi ya Warembo wa Miss Kibaha 2013
  Kalili aliendelea kwa kusema kuwa naifahamu vema bendi ya Mashujaa ambayo inaongozwa na mwanamuziki nyota nchini Charles Mbwana ‘ Charlz Baba , Kingunge’ , pia wamo waimbaji wenye sauti tamu kama Jado FFU, Marapa machacharikama 33, Fagurson na wengineo wengi.

  Akizungumzia kwa upande wa maandalizi Kalili alisema kuwa yanaendelea vizuri huku LIMSO wakijipanga kuingia kambini na warembo ambako watakaa kwa siku chache kabla ya shindano.

  Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chache cha Redds Premium Cold, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV,Clouds FM , Times FM Michuzi Media Group (MMG),Mikopo Finance,Santorine ,PR.Promotion, Chicago General Company, Image Pub na wadhamini kutoka Kibaha ni Mama Koka , Amazon Night Club, Panandipanandi Pub na Santorine Holiday Resort iliyopo Kiluvya.

  0 0

  Mama Ye! leo, Mei 5, inatoa wito kwa Mh. Dk Hussein Mwinyi (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kushughulikia kwa haraka upungufu wa idadi ya wakunga wanaohitajika ili kuwasaidia akina mama wa Tanzania kujifungua salama.

   Wakunga wana jukumu kubwa la kuwahudumia wanawake katika kipindi chote cha ujauzito na pia ni wataalamu wenye ujuzi wa kushughulikia matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua. 

   Wakunga wengi wanatembea umbali mrefu na kufanya kazi masaa mengi ili watoe huduma bora kwa wanawake katika jamii zao. Wataalamu wa masuala ya afya ya wajawazito na watoto wachanga wamekadiria kuwa, iwapo wanawake wote wa Tanzania wangepata huduma za wakunga wenye ujuzi, basi maisha ya akinamama wapatao 5,000 na vichanga 32,000 yangeweza kuokolewa ifikapo 2015. 

  Akiongea kwa niaba ya kampeni ya Mama Ye! Craig Ferla amesema: “Ni vyema kabisa kuwaenzi wakunga wetu katika Siku ya Wakunga Duniani. Tunapongeza ahadi za serikali kuitilia mkazo sera ya huduma za afya ya uzazi kuwa bure, lakini mengi bado yanahitaji kufanyika ili kuongeza idadi ya wahudumu wa afya.”

   Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives) zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma. 

  Craig Ferla ameongeza kuwa: “Tunawaalika na kuwahimiza Watanzania kutoa shukrani kwa wakunga – na kusaidia kuwapa moyo vijana nao waamue kuwa wakunga siku za baadae. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia ‘Twitter’ ukiwaambia asante kwa kujituma kazini, pia waweza kuweka picha kwenye ukurasa wetu wa ‘Facebook’ zinzazowaunga mkono wakunga wetu wa Tanzania pamoja na mathalan kutambua juhudi kubwa za mkunga unayemthamini kwa kazi zake kubwa katika jamii yako.”

   Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya wakunga nchini Tanzania, tembelea tovuti ya www.mamaye.or.tz/sw ambapo utapata ushahidi uliowekwa kwa namna rahisi kuelewa, habari kuhusu mashujaa katika uzazi salama, ahadi zilizowekwa na serikali na hatua mbali mbali unazoweza kuchukua web: www.mamaye.or.tztwitter: @MamaYeTZfacebook: facebook.com/MamaYeTZ 

  MamaYe! 164C Msasani Beach, Kinondoni, P.O. Box 13731, Dar es Salaam, Tanzania Phone: +255 (0) 754 588 233 ili kufanikisha kampeni hii muhimu. Ipaze sauti yako isikike na toa madai ya msingi zaidi, jiunge na kampeni ya Mama Ye!

  0 0
 • 05/05/13--02:44: katambuga sokoni
 •  Viatu vinavyoundwa kutokana na Mabaki ya Magurudumu ya Magari maarufu kwa jina la Kata Mbuga,vikiwa sokoni kusubiria wateja.


  0 0
 • 05/05/13--02:52: Mambo ya Mazoezi

 • 0 0  Mungu uwe upande wetu
  Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
  eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu  kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....


  Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha
  MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja yu  mahututi na wengine zaidi ya 49  wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa  4 asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.


  Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

  Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za  maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina  Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

  Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim 

  Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ,  ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

  Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
  Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
  Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
   Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
  Picha kwa hisani kubwa ya 


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi.Juliet Kairuki akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo na Rais Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi.Juliet Kairuki akiwa ameshilia maua aliyokabidhiwa na wafanyakazi wa kituo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo na Rais Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi.Juliet Kairuki akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Bi. Beatrice Chonjo (kulia) akimpa maelezo mafupi ya kituo kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alipowasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo na Rais Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni.Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma, Bi. Senzie Nakuala, Mkurugenzi wa Mifumo ya Habari na Mawasiliano, Dkt. John Kyaruzi na Meneja wa PPP, Bwana Said amiri.

  0 0

  Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka (katikati) akisisitiza jamboa baada ya kumkabithi kitabu cha Majukumu na Mafanikio ya Wizara hiyo toka kuanzishwa kwake mpaka mwaka 2011, Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt. Diwani Mruttu(wa pili kulia).Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimali watu Bi Mazoea Mwera kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ulifanyika mwishoni wa wiki jijini Dare s Salaam.
  Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Techinojia Dkt. Forens Turuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo mwishoni mwa wiki. Mwenyekiti wa Taifa wa Tughe Dkt. Diwani Mruttu ( wapili kulia), Watatu kulia kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Utumishi , Bi. Mazoea Mwera.


  0 0

  CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezipongeza timu zake tatu zilizofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa, baada ya kumalizika kwa Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora Aprili 27 mwaka huu.

  Timu hizo ni Red Coast, Abajalo na Friends Rangers, zitakazoungana na timu za mikoa mingine kucheza Ligi ya Mabingwa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya Usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, alisema ligi hiyo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuzitaka timu zilizofuzu hatua hiyo kujipanga vizuri ili kuuwakilisha vyema mkoa na hatimaye kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

  “Kwa niaba ya DRFA napenda kuchukua nafasi hii kuzipongeza timu hizo kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Dar es Salaam katika kutafuta kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2013/2014.

  “Tunaamini watajiandaa vyema na kutuwakilisha vizuri katika ligi hiyo, kufanya kwao vizuri ndio itakuwa fahari yetu DRFA na wadau wa mpira wa miguu mkoa wa Dar es Salaam, tunawatakia kila la kheri na tupo pamoja katika kushirikiana nao.

  Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora mkoa wa Dar es Salaam ilianza Aprili 15 mwaka huu ambapo ameziomba timu za Sharif Stars, Day Break na Boom FC zilizoshiriki ligi hiyo kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano yajayo.

  0 0

  Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman Bwana li Omar Al-Sheikh akizunguza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman uliofika ofisini kwake mapema asubuhi.
  Balozi Seif akiiomba Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman kupitia Mwakilishi wake Bwana Ali Omar Al-Sheikh kutumia fursa zilizopo za rasilmali Zanzibar kuwekeza vitega uchumi vyao Nchini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Kibiashara ya Shanfar & Patners ya Mjini Salala Nchini Oman baada ya mazungumzo yao yaliyohusu suala la uwekezaji hapa Nchini. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini,Jescar Msambatavangu (wapili kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya Chuo Kikuu cha Ruaha, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Iringa.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja wa Kampuni ya Bia wa kanda za juu Kusini ,Raymond Degera.

  CHUO kikuu cha Ruaha (Rucco), kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani ya 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013' baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 13-10 dhidi ya chuo kikuu cha Mkwawa katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.

  Mashindano hayo yaliyoshirikisha vyuo vikuu vitatu vya mkoani hapa yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) yalifanyikia kwenye ukumbi wa Twisters.

  Chuo kikuu cha Ruaha kwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo kwa wanafunzi wa elimu juu mkoani hapa mbali ya kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia kilikata tiketi ya kuuwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Chuo kikuu cha Mkwawa kilichoshika nafasi ya pili kilizawadiwa Sh.300,000 na chuo cha Tumaini ambacho kilishika nafasi ya tatu kiliondoka na Sh.200,000.

  Mbali ya vyuo hivyo kupata fedha hizo taslim lakini pia kila chuo kilipata mbuzi mmoja mmoja waliotolewa na diwani wa kata ya Kitanzini katika manispaa ya Iringa mjini, Jesca Msambatavangu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo.

  Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Said Mohamed wa chuo cha Ruaha alifanikiwa kutetea ubingwa wake baada ya kumfunga Hamphrey Tengie wa chuo cha Tumaini magoli 3-0.

  Mohamed kwa kutwaa ubingwa huo alizawadiwa Sh.150,000 na pia kukata tiketi ya kuuwakilisha mkoa huo katika mashindano hayo ngazi ya fainali wakati, Tengie alliyeshika nafasi ya pili alizawadiwa Sh.100,000.

  Na kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Hellen Kitali wa chuo cha Tumaini alitwaa ubingwa huo baada ya kumfunga Beatrice Nadafu wa chuo cha Ruaha magoli 4-3 na kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya kuuwakilisha mkoa huu katika fainali za taifa, wakati Beatrice aliyeshika nafasi ya pili aliondoka na Sh.50,000.

  Zawadi zote kwa washindi zilikabidhiwa na diwani wa kata ya Kitanzini, Jesca Msambatavangu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

  Baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi, diwani huyo licha ya kuwapongeza mabingwa wa mashindano hayo pia aliwataka wachezaji wa vyuo vingine ambao hawakuchukuwa ubingwa kuongeza bidii ya mazoezi ili mwakani waweze kufanya vizuri.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizundua bohari ya madawa ya MSD mjini Dodoma Mei 5,2013.Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif RashidWatatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe wakati alipozindua bohari ya kuhidi madwa ya MSD, eneol la Kizota mjini Dodoma Mei 5,2013.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani (wapili kulia) wakati alipozinduaghala la kuhifadhia madawa katika Kanda ya Kati la MSD mjini Dodoma Mei 5, 2013. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madawa yaliyohifadhiwa kwenye boahari ya MSD ya Kanda ya Kati eneo la Kizot mjini Dodoma baada ya kuzindua bohari hiyo Mei 5,2013. Wapili Kulia ni Naibu Waziei wa Afya, Dkt.Seif Rashid , Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0
 • 05/05/13--10:12: KUMBUKUMBU

 • MAREHEMU MWALIMU NOVATI SIMEON RUTAGERUKA

  TAREHE 5 - MEI – 2013, UMETIMIZA MIAKA MITATU TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.

  UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FROLIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

  IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 5 - MEI - 2013, KATIKA KANISA LA BIKIRA MARIA MAMA WA HURUMA, MBEZI BEACH, TANKI BOVU, DAR-ES-SALAAM, SAA 2.30 ASUBUHI.

  BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. 

  AMINA

  0 0

  Wanafunzi kutoka nchi 5 za Afrika Mashariki tunaosoma nchini Algeria tupo katika mchakato wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wanafunzi wote wa EAC wanaosoma katika nchi hii.Changamoto ya kuanzishwa kwa hii Jumuiya imetokana na idadi kubwa ya wanafunzi wa EAC wanaokuja kusoma kila mwaka nchini Algeria,Pia changamoto ilitokana na jitihada zinazo endelea sasa hivi nyumbani za ushirikiano wa nchi 5 za EAC.

  Tukaona sisi kama Vijana kutoka EAC hili linatuhusu zaidi kwani sie ndo Taifa la kesho, na hivyo tukaona tuanzishe Jumuiya yetu hapa ili kuongeza ukaribu kati ya Vijana kutoka nchi 5 za EAC tukiwa hapa Algeria na baadae baada ya kumaliza masomo yetu.Pia hakuna nchi hata moja ya EAC yenye Ubalozi wake nchini Algeria na hivyo tunahitaji chombo cha kushughurikia matatizo yetu sisi sote kwa pamoja badala ya kuacha kila nchi kuwa kivyake na huku Serikali zetu zikitaka kuwa na Ushirikiano wa pamoja.

  Kikao cha kwanza cha kujadili hili swala kilifanyika tarehe 03 mwezi Mei katika mji Mkuu wa Algeria, Algiers.Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi kutoka kila chama cha wanafunzi cha Nchi ya Afrika Mashariki ambazo ni Rwanda, Burundi,Kenya,Tanzania, na Uganda.Na wote tulikubaliana kuanzishwa kwa Jumuiya hii itakayo simama kwajina la EAC-Students in Algeria (EACSA).Changamoto tuliyonayo sasa nikupata baraka za Serikali zetu zote 5, pamoja na kusajili chama hapa Algeria.

  Tunakuomba sana Kaka Michuzi kutumia blog yako ambayo hutembelewa sana na watanzania wengi waishio nje ya nchi kupata habari, kutangaza habari hii ili watu wote walioko hapa Algeria na sehemu zote wajue nini kinaendelea.

  Na hiyo picha hapo ni picha ambayo tungepende iende sambamba na habari hii ni picha ya Viongozi wa Jumuiya za wanafunzi wa nchi za EAC, pamoja wadau wengine waliokutana kujadili swala hili.

  Samahani sana kwa Usumbufu mkuu.

  Wako katika kujenga Taifa,

  Kikwembo D. Mlekwa,
  Vice President EACSA.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Kuwait City mchana wa leo, Jumapili, Mei 5, 2013, kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika Taifa la Kuwait kwa mwaliko wa Mfalme wa Kuwait, Amir Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al Sabah. 
  Ndege ya Rais Kikwete ambaye anaandamana na Mama Salma Kikwete imewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Amiri, Kuwait City saa saba na nusu za mchana ambako Rais amepokewa na Mfalme – His Highness Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah na viongozi wa juu wa Dola la Kuwait. 
  Rais amekagua gwaride la heshima la Jeshi la Kuwait kabla ya msafara kuanza safari ya kwenda kwenye Kasri ya Bayan ambako Rais na ujumbe wake umefikia. 
   Katika ziara hiyo, Rais ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Zanzibar Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais. Fedha, Uchumi na Mipango wa Serikali ya Zanzibar Mheshimiwa Omar Yussuf Mzee. 
  Miongoni mwa shughuli kubwa za Rais Kikwete kwenye siku ya leo ya kwanza ya ziara hiyo ya kwanza kufanywa na kiongozi mkuu wa Tanzania katika Kuwait katika historia ni kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na ujumbe wa Taifa la Kuwait ukiongozwa na Mfalme Sheikh Sabah Al Ahmad Al Jaber Al Sabah Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Kuwait Mheshimiwa Ali Fahad Al Rashed na Waziri Mkuu Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah. Mazungumzo hayo yatafanyika kwenye Hoteli ya Jahra 3 katika Kasri ya Bayan ambako Rais na ujumbe wake umefikia.
   Baadaye leo usiku, Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa kwa heshima yake na Mfalme. 
  Katika siku ya pili ya ziara yake kesho, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine atatembelea Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Kuwait katika eneo la Al Ahmadi. Kuwait ni nchi ya sita duniani kwa kuzalisha mafuta mengi ikiwa inatoa asilimia saba ya mafuta yote duniani na ikiwa na kiasi cha utajiri wa mafuta unaokadiriwa kufikia mapipa bilioni 104 katika eneo lake na lile la bahari kuu ambako inagawanya utajiri huo na nchi jirani ya Saudi Arabia.
   Rais Kikwete pia atakutana na kuzungumza na Bwana Ghanim Sulaiman Al-Ghaniman, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait ambao umegharimia miradi mingi na yenye thamani ya mabilioni ya fedha na hasa ile ya barabara katika Tanzania. 
  Rais pia atakutana na kufanya mazungumzo na Bwana Mohamed Thunyan Al Ghanim, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda katika Kuwait. Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Bwana Bader Mohamed Al-Saad wa Mamlaka ya Uwekezaji katika Kuwait na baadaye ataandaliwa chakula cha jioni na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
   Imetolewa na: 
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
  IKULU, DAR ES SALAAM 
   5 Mei, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipokea mashada ya mauwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakiingia sehemu ya mapokezi na kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.


  0 0
 • 05/05/13--10:39: MSAADA TUTANI

 • Hii picha imenifanya nijiulize maswali mengi... wewe je? (ongeza kwenye comment)

  1. Hayo maandishi yaliyoandikwa nyuma ya gari hilo ni wangapi wameweza kusoma? (OANGEZ, DANGEZ...)

  2. Tanzania tunatumia lugha ya kiswahili zaidi, na kwenye gari hilo la mafuta hakuna neno lolote la kiswahili kumjulisha mtanzania kuwa hilo gari limebeba nini? na usalama wake ni nini?

  3. Hapo inaonyesha hilo gari inamwaga mafuta kwenye tanki la chini la kituo cha mafuta katikati ya jiji la Dar es Salaam, na hakuna mhudumu yoyote aliyopo jirani nayo. je ikitokea bahati mbaya nani wa kulaumu?

  4. Ndoo moja imelala chali jirani na kisima hicho... ilikuwa na nini? Maji/Mafuta/Mchanga...

  5. Usalama wa gari na mali uko wapi?

  6. Nijuavyo mimi, kila gari la mafuta inapewa sticker fulani ya kujulisha kuwa hilo gari limebeba mafuta ya aina gani, na kwenye ajali litazimwa na aina gani ya zima moto? kwenye gari hilo iko wapi?

  7. Hiyo alama iliyoandikwa kulia la gari hilo (juu ya reflector) lina maana gani?

  8. OSHA / EWURA / FAYA / N.K. ... mpo?

older | 1 | .... | 122 | 123 | (Page 124) | 125 | 126 | .... | 3272 | newer