Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA AITEMBELEA TIMU YA TAIFA MAZOEZINI

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Kipa wa timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, Deogratius Munishi maarufu kwa jina la Dida, akifanya mazoezi ya kuzuia penalti kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Mshambuliaji Elius Maguri na Kiungo Hassan Kabunda wakipumzika katika mazoezi hayo.
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

SERIKALI YAAHIDI KUVIPATIA MAJI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA BOMBA KUU LA MAJI LA ZIWA VICTORIA NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA TANZANIA.

$
0
0
Serikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itatekeleza mradi wa maji katika vijiji 100 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu la maji linalotoka ziwa Victoria hadi Kahama na Shinyanga ili kuwawezesha wanachi wanaoishi katika vijiji hivyo kupata huduma ya maji safi na salama.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa mradi wa kuvipatia maji vijiji hivyo utakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma ya maji kwenye vijiji 40 vilivyotambulika katika Halmashauri za Misungwi, Kwimba, Shinyanga na Msalala.

Amesema kazi ya kupima na kufanya usanifu wa miradi katika katika vijiji hivyo vya Halmashauri ya Msalala na Shinyanga imeanza na gharama yake imekadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.59 huku akiongeza kuwa hadi machi, 2016 ujenzi wa miradi ya maji umekamilika katika vijiji 11 vya Halmashauri hiyo.

Mhe.Lwenge amesema katika mwaka wa bajeti 2016/2017 Wizara yake itakamilisha ujenzi a miradi ya maji katika Halmashauri za wilaya za msalala na Shinyanga na kuanza Usanifu wa miradi hiyo kwenye Halmashauri za Kwimba na Misungwi ambapo kiasi cha shilingi milioni 760.67 kimetengwa kwa kazi hiyo.

Amevitaja baadhi ya vijiji ambavyo sasa wananchi wake wanapata maji safi na salama kufuatia kukamilika kwa miradi hiyo kuwa ni Nyashimbi, Magobeko, Kakulu, Butegwa, Ngihomango, Jimodoli, Kadoto,Lyabusalu ,Mwajiji Ichongo na Bukamna.

Katika hatua nyingine Mhe.Lwenge amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji itatekeleza mradi mkubwa wa maji utakakaowawezesha wananchi Laki mbili (200,000) wa Halmashauri zote za mkoa wa Kigoma kupata maji safi na salama.

Amesema mradi huo unatarajia kugharamia kiasi cha Euro milioni 8.8 ambapo kati ya fedha hizo Euro milioni 8 zitatolewa na Serikali ya Ubelgiji na fedha iliyobaki itatolewa na Serikali ya Tanzania.

Ameongeza kuwa vijiji 26 vya kipaumbele vya mkoa wa Kigoma vimeainishwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa wizara yake tayari imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni 5.28 zote zikiwa ni fedha za nje kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Pia amesema Serikali katika mwaka wa 2016/2017 wa fedha imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kufanyia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya maji ili kuzipatia maji kata saba za wilaya ya Masasi zenye idadi ya watu 84,082.

Aidha, amesema katika mwaka huo wa fedha serikali itatekeleza mradi wa kutoa maji mto Ruvuma kuyapeleka Mtwara –Mikindani pamoja na vijiji 26 vitakavyopatikana kilometa 12 kutoka eneo la bomba kuu.

Mradi huo utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya China kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 189.9 ambapo kazi ya ujenzi wa chanzo kutoka mto Ruvuma , Chujio la kutibu maji , nyumba ya kusukuma maji , matanki 26, tanki kuu la ujazo wa lita milioni 30 litakalojengwa eneo la maghamba.

Aidha, vituo vya kuchotea maji 234 na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali kilometa 63 yatajengwa ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 9 hadi lita milioni 120 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya watu na viwanda mbalimbali vinavyojengwa vikiwemo vya Saruji na Gesi.

Angalia Kipindi Chote Cha ' Football Family' Kilichorushwa TBC1

SERIKALI YATANGAZA KUISAFISHA SEKTA YA ELIMU NA WATUMISHI WA UMMA WENYE VYETI BANDIA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Na Aaron Msigwa - DODOMA.
 Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa katika  sekta hiyo  wakitumia vyeti bandia.

Aidha, imewataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na mabadiliko makubwa ya kusafisha sekta ya elimu na utumishi wa umma yanayokuja nchini. 

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu nchini ili kuhakikisha kuwa Elimu inayotolewa katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali inazalisha wahitimu wenye sifa na ubora kwa maslahi ya Taifa.

Amesema katika kulitimiza hilo Serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria watendaji wote walioshiriki na wale wanaoendelea kushiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha maendeleo ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na wale waliohusika katika udahili wa wanafunzi wasio na sifa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Songea.

"Serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kabisa kuboresha kiwango cha elimu yetu kwa kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu, naomba niwahakikishie kwamba pale panapohitajika kufanyika mabadiliko tutayafanya bila woga" Amesisitiza.

Amesema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za elimu hapa nchini, serikali imejipanga kubadilisha mfumo wa elimu ambao umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba mabadiliko hayo yatafanyika kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta hiyo.



" Tunapotaka kufanya mabadiliko kwenye mfumo wetu wa elimu tumekubali tumekubali kwamba tuna changamoto,  katika changamoto hizi lazima tuwe na mahali pa kuanzia hivyo tunapochukua hatua tunaomba Watanzania mtuunge mkono" Amesisitiza Prof.Ndalichako.

Prof.Ndalichako Amesema lengo la Serikali kupitia Wizara yake ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa hapa nchini kwa kuendelea kutoa wahitimu bora wanaokidhi vigezo na viwango katika soko la ajira.

Amesisitiza kuwa mkakati wa Serikali ni kuanza kuwafuatilia wahitimu wote wasio na viwango ambao wako katika maeneo mbalimbali ya ajira huku akisisitiza kwamba elimu ya Tanzania ni sawa na kiwanda kinahitaji malighafi nzuri ili kitoe bidhaa bora.

Ameeleza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuvikagua vyuo vyote vinavyotoa elimu ya juu kuona kama vinakidhi sifa na vigezo vya kiutendaji ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote wanaowadanganya wananchi  na kuwapotezea muda vijana wanaowadahili bila kuzingatia sifa.

"Wizara yangu tunaendelea kufanya mawasiliano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili tuchukue hatua kwa wote walioichezea sekta hii muhimu, tulichofanya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kinaendelea kwa vyuo vingine"



Akizungumzia suala la Ada elekezi amefafanua kuwa suala hilo linaendelea kutazamwa kwa umakini mkubwa kwa kuwashirikisha wadau husika wa sekta hiyo kwa kulifanyia utafiti kwa kuzingatia changamoto zinazojitokeza.



Ili kukidhi matarajio ya wananchi kuhusu suala la ada elekezi amesema serikali inaendelea kuchukua hatua kwa kulifanyia utafiti kuliangalia na madaraja ya shule binafsi na kuongeza kuwa serikali itaendelea kutumia taratibu zilizowekwa na Ofisi ya Kamishna wa Elimu nchini.



Amesema Serikali kupitia Ofisi ya Kamishna wa Elimu inaendelea kulifuatilia kwa karibu suala la ada na michango mingine kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuona kama michango na ada zinazotozwa zinazingatia maslahi ya Taifa.

Prof. Ndalichako amebainisha kuwa ukaguzi utakaofanywa katika shule hizo utajielekeza katika kuangalia uhalali wa michango inayotozwa kwa wanafunzi ikiwemo michango ya kila muhula ya majengo, ulinzi na mingineyo ambayo imekuwa kero kwa wananchi.

" Kama Serikali hatuwezi kukubali wananchi kuendelea kutozwa michango ya majengo wakati kigezo kimojawapo cha mtu kuruhusiwa kutoa elimu ni kuwa na majengo, hili halikubaliki na hatutalifumbia macho"  Amesisitiza Prof.Ndalichako.

Amewataka wananchi kuelewa kwamba serikali kutotoa ada elekezi haina maana kwamba imejitoa kabisa katika kufuatilia masuala ya elimu hapa nchini bali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya kuwawezesha watanzania kupata elimu bora kwa gharama nafuu.

Kuhusu ujenzi wa maabara amesema kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwa shule zote 1536 ambazo zimekamilisha ujenzi wa majengo ya maabara kote nchini.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itafanya ukaguzi wa vyuo vyote vya Maendeleo ya Jamii kote nchini ili majengo ya vyuo hivyo yaweze  kutumika kuanzishia vyuo vya Ufundi Stadi VETA katika wilaya na mikoa ili kuwapatia stadi za kazi vijana waweze kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wao baadhi ya Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia wakati wa Kupitisha Bajeti ya wizara hiyo wameiomba Serikali kuweka mkazo katika usimamizi wa Sekta ya Elimu nchini ili shule, Taasisi na vyuo vya Tanzania vitoe wahitimu wenye ubora kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, wameiomba Serikali kupitia Bajeti hiyo itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa shule, kuboresha maslahi na kulipa madai ya walimu pamoja na kuziimarisha Mamlaka za Udhibiti wa Elimu ili ziweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.




Serikali yanunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Serikali kupitia wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .
Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu waTBA  Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa  miradi mbalimbali  ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.
“Lengo la kununua vifaa hivi ni kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale inapodi” alisisitiza Mwakalinga.Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo Mwakalinga amesema kuwa  hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.
Aidha vifaa hivyo vitawezesha Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.Vifaa hivi ni kama Rebund hammer inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.
Akitaja vifaa vingine Mwakalinga amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Milki  Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.
Mhandisi  Ujenzi kitengo cha Upimaji  na Ukaguzi Majengo  toka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wakwanza kulia Bi Khadija Salum  akionesha kwa waandishi wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
( Picha   na Habari na Frank Mvungi ).

NEWS ALERT: Godawn la Kampuni ya Simba Mtoto laponea chupu chupu kuteketea kwa Moto

$
0
0
 Godawn la Kampuni ya Simba Mtoto lilolopo eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es salaam, limenusurika kuteketea kwa moto usiku huu, baada ya vijana wawili waliokuwa wakiishi katika eneo lilolopo jirani na hapo, kuchoma matairi mabovu yaliyokuwepo ndani ya eneo lao hilo. Walipoulizwa sababu za wao kufanya hivyo, vijana hao waliofahamika kwa majina ya Peter na Amdan, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi, walisema kuwa walifanya hivyo kwa lengo la kupunguza wingi wa majani yaliyolizunguka eneo hilo na hawakuwaza kama moto huo ungeshika kwenye matairi hayo ambayo ni chakavu ya magari yaliyokuwamo ndani ya eneo hilo. Taharuki ilitanda eneo lote la Tabata pale moshi mwingi na mzito ulipotanda angani na kuwafanya hata wale waliokuwa kwenye mapumziko ya mwisho wa wiki kushindwa kufanya hivyo huku wengine wakifanya mawasiliano na baadhi ya ndugu zao waliowaacha majumbani. Hadi Ripota wetu anaingia mitamboni hakukuwa na madhara yeyote yaliyotokea na jitihada za kukitafuta kikosi cha Zimamoto na Uokoaji zilikuwa zikiendelea. Na vijana hao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi. 
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka.
vijana hao ambao walifahamika kwa jina Moja Moja, Peter na Amdan wakipakizwa kwenye gari ya Polisi.
Vijana hao wakiwa chini ya Ulinzi. 

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam, awatoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji mafuta ya ndege.

$
0
0

  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta  wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali imewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.
Hayo yamesememwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

“Mafuta ya ndege yapo na ndege zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.

Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya petroli.

Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

Imeonekana si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia hatua hiyo na hali ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza kwa wiki mbili kuanzia sasa.

Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika kwa matumizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam, Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi yanayoingia nchini.


Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com, TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies. 


AFRICA DAY ANNUAL GALA DINNER JW MARIOTT HOTEL, WASHINGTON, DC

$
0
0

Kutoka kushoto ni Balozi wa Lesotho nchini Marekani Mhe. Prof. Eliachim Molapi Sebatane, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi, Balozi wa Rwanda nchini Marekani Mhe. Prof. Mathilde Mukantabana na Mke wa Balozi wa Ethiopia nchini Marekani Mama Biru wakiongea mawili matatu walipokua kwenye mchapalo kabla ya Gala dinner kuanza.


Nyimbo za Taifa ya Marekani na Umoja wa Afrika.

Washereheshaji wa siku ya Afrika kutoka kushoto Vicent Makori, mtangazaji Voice of America na Mareen Uheh mtangazaji kituo cha luninga cha FOX NEWS.


Baadhi ya mabalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BWANA EDWIN MASHAYO NA BI. MARY MOLLEL WAUAGA UKAPELA

$
0
0
Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam leo May 28, 2016. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog -(Kajunason Studio).
Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam. Pembeni ni wasimamizi wao.
KWA PICHA ZIDI BOFYA HAPA.

SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA LAMSHUKURU RAIS WA TFF KWA MCHANGO WA TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA OLYIMPIC

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AWATAKA VIJANA KUWA MFANO KATIKA NCHI ZAO

$
0
0
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa kuhusu Vijana kutoka nchi nane Afrika uliofungwa jana kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mratibu wa Kongamano hilo Marx Chocha akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Vijana wakisikiliza kwa makini mada mijadala iliyokua inatolewa.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Tarehe kama ya leo miaka saba iliyopita (29/05/2009). Mama yetu mpendwa Mary Donata Watondoha alifariki Dunia, Kifo chake kimeacha nafasi kubwa ya wazi isiyoweza zibika kamwe katika familia yake na kwa upande wa ukoo wa Kalembo na Watondoha (Mbwette).

Kwa watoto wako na wajukuu zako kifo chako bado kinaleta majozi na uchungu unakumbukwa kila siku kwa ukarimu, msaada, busara na mawazo ya faraja kwa kila mmoja.

Tunashukuru kwa wanandugu wote, marafiki wa karibu na wa mbali kwa kuwa nasi katika kuadhimisha siku yako uliyotangulia.

Ama kwa hakika tutakuja kukutana tena.

May her soul and the souls of all the faithful departed, through the mercy of God, rest in peace. Amen.

NCHI ZILIZONYUMA KIMAENDELEO BADO ZINA SAFARI NDEFU

$
0
0
Na Mwandishi Maalum

Mkutano unaotathimini mafanikio ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Miaka 10 kuhusu Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo, ( Istanbul Program of Action for LDCs) unaendelea huko Antalya, Uturuki, ambapo imeelezwa kwamba nchi hizo 48 zilizomo katika kundi hilo bado zina safari ndefu.

Baadhi ya mambo yanayochelewesha mataifa hayo ku-graduate ambayo 38 ni kutoka Bara la Afrika, 13 kutoka Bara la Asia na moja kutoka Amerika ya Latini,ni pamoja na, umaskini uliokidhiri ambapo asilimia 51 ya idadi ya watu katika nchi hizo ni maskini, idadi kubwa ya watoto ( milioni 18) wenye umri wa kwenda shule hawaendi shule , rushwa, na ukuaji wa uchumi.

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na Serikali ya Uturuki na unafanyika nchini Uturuki ambapo ndipo chimbuko la mpango kazi huo uliopitishwa mwaka 2011. Tanzania ambayo ni kati ya nchi 38 kutoka Afrika ambazo zimokwenye orodha ya umoja wa Mataifa kama nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) inashiriki kikamilifu mkutano huo.

Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Bw. Songelael Shilla akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Tanzania, pamoja na mambo mengine ameelezea jitihada mbalimbali zinazotekelezwa na serikali ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuhakikisha kwamba inafunzu na kuondoka katika kundi la nchi zilizonyuma kimaendeleo.

Miongoni mwa juhudi na mikakati inayofanywa na serikali ni pamoja na kuhakikisha inapunguza idadi ya wananchi wake wanaoishi katika umaskini uliopindukia, uboreshaji wa huduma muhimu za kijamii, ambazo ni afya sambamba na upunguzaji wa vifo vya watoto wachanga na wanawake wajawazito,, elimu, ujenzi wa makazi bora, usambazaji wa huduma za maji safi na salama na ujenzi wa miundo mbinu ikiwamo ya mawasiliano.

Katika taarifa yake Tanzania pia imeanisha mafanikio kadhaa katika ukuaji wa uchumi wake huku ikisisitiza haja na umuhimu wa mataifa yaliyoendelea kutimiza ahadi zake katika eneo la misaada ya kimaendeleo hatua mbayo itasaidia kuharakisha nchi maskini kupiga hatua na kuondoka hapo zilipo.

Pamoja na kusisitiza ubia na ushirikiano kutoka mataifa yaliyoendelea, Tanzania imesema bado inaamini kwamba wajibu wa kwanza wa kuondoka katika kundi la nchi maskini au zilizonyuma kimaendelo unapashwa kuwa wa nchi zenyewe zilizonyuma kimaendeleo.

Tanzania pia imewasilisha Taarifa yake ( National Mid –Term Review Report) kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa IPoA.
Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa unaofanya tathimini ya utekelezaji wa Mpango Kazi kuhusu Nchi ambazo zimo nyuma kimaendeleo ( LDCs) Mkutano huu wa siku tatu unafanyika Antalya nchini Uturuki.

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

JWTZ Mtwara wawabana waendesha bodaboda na madereva kushiriki katika zoezi la usafi mkoani humo


SERIKALI YATAKIWA KUFUNGUA OFISI ZA UTALII KATIKA NCHI AMBAZO ZINALETA WATALII WENGI HAPANCHINI

$
0
0
Serikali imetakiwa kufungua ofisi za utalii katika kila nchi ambazo zinaleta watalii hapa nchini pamoja na kupunguza viingilio vya wageni wanaotembelea hifadhi zetu za taifa ili kuweza kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini .

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari alipotembelea katika maonyesho ya utalii ya Karibu fair yanayofanyika ndani ya viwanja ya magereza, jijini Arusha .
wananchi wakiendelea kupata maelezo ya utalii ndani ya banda la Ngorongoro Conservation lililopondani ya maonyesho hayo.

Alisema kuwa serekali inapaswa kufungua ofisi katika kila nchi ambayo inajua inaletawageni hapa nchini ili kuweza kutangaza utalii wetu vizuri,na ili kuweza kupata wageni wengi zaidi ambapo wakiingia kwa wingi watasaidia kuongeza pato la taifa na kupunguza tatizo la ajira kwani vijana wengi wanaweza kujiajiri kupitia utalii pamoja na biashara za utalii .

Alibainisha kuwa ni jambo la ajabu nchi kama Tanzania ambayo inavivutio vingi vya utalii huku ikiwa ni nchi mojawapo ambayo iko katika nchi kumi bora ambazo zinaongoza kwa kuwa na vivutio vya utalii lakini ni nchi ambayo inangiza watalii wachache sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo.

“nchi kama Tanzania pamoja na vivutio vyote lakini kwa mwaka tunaingiza watalii milioni moja wakati nchi kama Malaysia kwa mwaka wanaingiza watalii miolini 15 ni jambo la kushangaza alafu ukiwaangalia viongozi wetu badala ya kukaa na kuangalia jinsi ya kufanya ili wataliii waingie na wawe wengi lakini wao wanakaa wanachekelea na wanafanyakazi ya kuongeza ada ya kuingia katika hifadhi zetu kila mara, sasa hii kweli si itakimbiza wageni badala ya kufanya wageni waongezeke kila siku”alisema Olemeiseyeki.
Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi Gibson Olemeiseyeki akipata maelekezo ya huduma zinazotolewa na kampuni ya utalii OSUPUKO nature Paradise iliopo mkoani Arusha.

NAPE AENDELEA KUKUTANA NA WANANCHI WA VIJIJI VILIVYOPO NDANI YA JIMBO LAKE AAHIDI KUMALIZA AHADI ZAKE MAPEMA MNO

$
0
0


Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongozana na wakazi wa kijiji cha Kilimanjaro kilichopo kata ya Mtumbya kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya wanakijiji cha Kilimanjaro kilichopo jimbo la Mtama , wilaya ya Lindi Vijijini.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasomea wakazi wa kijiji cha Mtumbya vijiji vitakavyopata umeme wa mradi wa umeme vijijini ( REA) awamu ya tatu katika jimbo la Mtama.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wakijiji cha Mpenda, Mtama .
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Mpenda ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa barabara ya kutoka Mtama, kupitia Mpenda , Mtumbya kwenda Kilimanjaro mkandarasi ameshapatikana na ataanza kazi hiyo mara moja na kuwahakikishia kuwa pamoja na kuwepo miradi mikubwa ya maji lakini Mpenda na Kilimanjaro watapata visima mapema.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA NIDA, ATOA HABARI NJEMA KWA WATUMISHI 597 WALIOSITISHIWA MIKATABA YAO

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.

Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.

Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.

“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.

Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.

Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba.

Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji kukamilika.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Vodacom Foundation kuendelea kukabiliana na changamoto za hedhi kwa wasichana

$
0
0
Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania itaendelea kusaidia wasichana nchini kuondokana na vikwazo vinavyosaabisha wabaki nyuma pia kutojiamini kupitia mradi wake wa ‘Hakuna Wasichoweza’ ambao imeanza kuutekeleza mkoani Mtwara.

Mradi huo ambao inautekeleza kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC Tanzania na wadau wengine umelenga kuwapatia wasichana waliopo mashuleni elimu ya afya ya uzazi ikiwemo kuwapatia vifaa vya kuwaweka salama wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza,alisema wataendelea na kampeni ya kukabiliana na changamoto za hedhi na alishauri kuwa  jukumu hili sio la serikali pekee bali linahusu taasisi zote na watu binafsi wa kuwa linachangia watoto wa kike hasa wanaotoka kwenye familia zenye vipato vya chini kubaki nyuma na kukosa kujiamini.

“Vodacom Foundation siku hii  ya hedhi duniani ni muhimu kwetu kwa kuwa tayari kupitia mradi wetu wa ‘Hakuna wasichoweza’  tumeanza kusaidia wasichana kukabiliana na changamoto wanazozipata wanapokuwa kwenye hedhi mojawapo ikiwa ni kutohudhuria masomo katika vipindi hivyo kutokana na kutokuwa na  vifaa vya kuwaweka salama na miundo mbinu isiyo rafiki kwenye shule wanazosomea,na mafanikio makubwa yameanza kupatikana na tunatamani miradi kama hii itekelezwe nchi nzima”.Alisema Rwehikiza.

Alisema ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwa watoto wa kike mashuleni ya kuwaweka salama wanapokuwa kwenye hedhi nchini ni tatizo kubwa ambalo sio la kufumbia macho bali linahitaji mikakati maalumu ya kulimaliza kwa kuwa linarudisha nyuma maendeleo ya wasichana  kielimu ambapo ipo idadi kubwa ya wasichana hawahudhurii masomo kwenye vipindi vya hedhi.

Meneja Mradi huo kutoka  taasisi ya T-MARC Tanzania inayotekeleza mradi chini ya  ufadhili wa USAID na Vodacom Foundation,Lilian Semanyesa, amesema kuwa mradi umeonyesha kuwa na mafanikio ambapo hadi kufikia sasa idadi kubwa ya wasichana wamepata mafunzo ya afya ya uzazi  na pedi za bure  kuwafikia wasichana  waliopo mashuleni na wasiokuwa mashuleni mkoani Mtwara.

“Lengo la Mradi wa Hakuna Wasichoweza  ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia Pedi watoto wa kike zaidi ya wasichana 10,000 waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mtwara na Lindi.Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume”.Alisema
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi, akisalimiana na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation, Sandra Osward, wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama iliyofanyika katik viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa Hakuna wasichoweza wa T-Marc, Lilian Semanyesa na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation, Sandra Osward, (wapili kulia) wakitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Dareda Mission iliyopo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, walipotembelea banda la Vodacom Foundation na T-Marc Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi Salama iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana, Mifuko hiyo ni wadau wakubwa wa kutoa elimu mashuleni kwa wasichana ya jinsi kujisitiri.
Baadhi ya wanafunzi washule za sekondari wakipatiwa elimu juu ya matumizi ya pedi na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation ,Sandra Osward, wakati walipotembelea banda la T-Marc Tanzania na Vodacom Foundation wakati wa maadhimisho ya siku ya Hedhi salama iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,Mifuko hii ni wadau wakubwa wa kutoa elimu mashuleni kwa wasichana ya jinsi kujisitiri kupitia mradi wao wa "Hakuna wasichoweza".

WABUNGE WAPIMWA AFYA DODOMA

$
0
0
 Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza katika Zahanati ya Bunge, Dodoma Mei 28, 2016.
 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma
 Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Sokombi akipimwa afaya na Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Asha Shao. Katikati ni muuguzi mwingine Christina Chamwela.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images