Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WALIOGHUSHI NYARAKA ZA NHIF WATUPWA JELA MIAKA 27

$
0
0
Mkaguzi wa NHIF, Charles Mjema akizunguza na waandishi wetu  juu ya hukumu ya iliyotolewa leo katika mahakama ya Ilala kwa watu wawili waliohukumiwa kwenda jela miaka 27 kwa makosa ya kugushi nyaraka za NHIF za kujipatia dawa katika madauka ya dawa yaliyosajiliwa na NHIF leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WATU wawili wamehukumiwa kwenda jela kwa makosa ya kugushi nyaraka za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  za kuweza kujipatia dawa katika maduka ya dawa yaliyosajiliwa na mfuko huo.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Mhe. Juma Hassan ambaye alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa wote  wawili watatumikia jela kutokana na makosa yao tisa ambapo mtuhuhumiwa wa kwanza Bakari Ramadhan amehukumiwa miaka 27 jela kwa makosa yote tisa na Ahmed Mohamed amehukumiwa miaka 12 kwenda jela kwa makosa manne.
Washitakiwa hao walikamatwa Desemba 14 , 2014 katika Duka JD Pharmance lilopo Posta wakiwa wanataka kuchukua dawa na kabla ya kukamatwa.
Akizungumzia hukumu hiyo Mkaguzi wa NHIF, Charles Mjema amesema kuwa wananchi watumie mfumo uliowekwa na NHIF na sio kughushi kutokana na mifumo iliyopo inabaini watu walio halali wa kuchukua dawa.
Amesema kuwa NHIF imeweka utaratibu wa mtu kuweza kupata matibabu na kupata dawa katika mfumo ulio bora kughushi hakuwezi kuwasaidia na akifanikiwa kufanya hivyo jela ina mwita.

TANZIA: Ras BUPE BAKWERESA KARUDI AFARIKI DUNIA

$
0
0
Na Sultani Kipingo

Habari za uhakika na kusikitisha zimetufikia kuwa mwanaharakati Ras Bupe Bakweresa Karudi, maarufu pia  kama kaka Bupe Mkushi (pichani kushoto), amefariki dunia katika hosptali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari.

Ras Bupe ameacha mke na watoto. Mke na mtoto wake wa kiume wameshawasili nchini kutokea Uingereza. Msiba hupo Karakata jijini Dar-es-salaam. Marehemu Ras Bupe Bakweresa Karudi alikuja nchini Tanzania katikati mwa miaka ya 70 akifuatana na mkewe na watoto wawili Kiyenda(msichana) na Nyamiche mvulana. Ras Bupe Karudi alikuja kumuomba marehemu baba wa taifa mwalimu Nyerere hili atoe idhini kwa watu weusi wa visiwa vya Karibian vya Jamaica warudi Afrika (Tanzania) kama nyumbani kwani ndio asili yao.
Baada ya kukubaliwa maombi yake, Marehemu Bupe akaungana na wanaharakati wenziwe hapa nchini wakiwemo marehem Prof. Joshua Mkhululi aka Prof. Keneth Edward, Marehem Ras Kwetenge Zanaki Sokoni (Wa Jamaica) pamoja na  wengine ambao wapo hai Imani Mani wakaungana na wenyeji wao Said Jazbo Vuai, Isza Suleiman na Ebrahim Makunja au Kamanda Ras Makunja kiongozi ambapo wakasajili chama cha ushirika chenye jina la UHURU, UMOJA NA MAENDELEO chenye makao kule Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakiwa wanajishughulisha na mipango ya kilimo na kumiliki maroli ya usafirishaji. 
Marehem Kaka Ras Bupe atakumbukwa sana kwa harakati zake zake za kuupigania uafrika na kuwahamasisha raia wenye asili ya kiafrika kurudi Tanzania.
Mungu mlaze pema peponi marehemu 
Bupe Bwakweresa Karudi 
Amen

Kijipu upele makutano ya mitaa ya zanaki na kisutu jijini Dar es salaam

$
0
0
Wasamaria wema wameweka tairi katika moja ya mitaro mingi ya maji taka ambayo mifuniko yake imeibwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wadau wa vyuma chakavu ambao baada ya kukwapua mifuniko hiyo huacha shimo lenye kuhatarisha maisha ya wapita njia.

JOTO LA ASUBUHI MEI 24, 2016 LA 93.7 EFM Kuanzia saa 12 Asubuhi - usikose!

Bank M unveils the Rotary Dar Marathon 2016

$
0
0
Rotary Dar Marathon turns eight this year and Bank M Tanzania for eight year in a row has once again joined hands to become the main partner of the Rotary Dar Marathon 2016 which will be held Monday 14th of October 2016 -Nyerere day. The iconic Marathon is organized by seven Rotary Clubs in Dar es Salaam in partnership with Bank M.
The famous Marathon in the city of Dar es Salaam will be graced by His Excellency former President Ali Hassan Mwinyi.
The Marathon theme stands to be “Healing Lives, Transforming Communities” whereby the marathon proceeds will be towards construction of a Rotary teaching hospital in Dar es salaam.
Speaking to the press in Dar es Salaam yesterday on the preparations for the Marathon, the organizing committee chair Ms. Agnes Batengas said the committee is well prepared and all arrangements are going well and they are expecting to make it a memorable sporting and family event. She added that RDM is aimed at collecting funds to overcome several community challenges, as in this year we are proceeding with the last year’s project which is building of a teaching hospital. The hospital will be built at the University of Dar es salaam, Mlimani area. About TZS 1bil was raised during last year’s Marathon and this year more collections are expected.
Ms. Batengas said this year’s event is expected to attract over 15,000 participants and as usual it will include the 5km family walk, 9km walk and a 21.1km which is the Marathon itself as well as cycling. All the races will start and end at the Green, Oysterbay.
Commenting on the Bank M’s participation in the Marathon as the main partner, the bank’s CEO (Designate) Ms. Jacqueline Woiso said that the bank is always dedicated to supporting the sustainable community based projects and it has been working together with Rotary in this noble cause since inception of the Marathon in 2009.
She added, “It is our policy to work together with other reputed organizations in making a difference to the needy communities of this land.  We sincerely believe that together we will make this a great success by building state of the art healthcare facility in Dar es salaam. This means a lot to us – seeing that our community health is taken care of” avowed Woiso.
For the past 8 years, the Rotary Dar Marathon in partnership with Bank M has conducted several projects including planting of trees, providing water and sanitation facilities to schools and the project was setting up a state of the art Children Cancer ward at the Muhimbili National Hospital. The ward, which is one of the best Pediatric Oncology facility in the African continent, also the newly refurbished and well equipped Rotary Entrepreneurship Centre at the University of Dar es Salaam.
“Bank M’s CEO-Designate Ms. Jacqueline Woiso and the Rotary Dar Marathon Committee chair Ms. Agnes Batengas exchanging the copies after signing the MOU in the press conference held in DSM yesterday. Bank M and the Rotary clubs will build a teaching hospital at the University of DSM Mlimani area through Rotary Dar Marathon which will be held in October this year. Looking on is the Rotary protocol chair Mr. Hamza Kasongo (Left), Rotary Dar Marathon Board chair Ms. Sharmila Bhatt (Right)”.
Rotary protocol chair Mr. Hamza Kasongo explains to  reporters about the Rotary International. With him from left is the Rotary Dar Marathon Vice chair Ms. CatherineRose Barreto, Bank M CEO-Designate Ms. Jacqueline Woiso, Rotary Dar Marathon Committee chair Ms. Agnes Batengas, Rotary Dar Marathon Board chair Ms. Sharmila Bhatt, Nirmal Sheth represented the Rotary club of Dsm president, Mahmood Panju represented the Rotary club of Bahari president and Leana Lemomo from the Rotary club of Mikocheni.

KIBOKO ALIYETISHIA MAISHA YA WATU AULIWA KIJIJI CHA MAGUNGA, IRINGA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wananchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi hao wa kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. 

Kiboko huyo alijificha kwenye eneo ambapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipatikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake. 

Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi​
Mmoja wa Maafisa Wanyaka pori akitoa maelezo kwa wananchi kabla ya kwenda kufanyika kwa zoezi la kumdhibiti Kigoko huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa ameambatana na baadhi ya wananchi na Maafisa Wanyama Pori kuelekea aliko Kiboko huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa maelekezo wakati wa kumtoa Kiboko huyo baada ya kuuliwa.


DC KIHATO: NI AIBU MWANAMKE KUTOKA ALFAJIRI KUTAFUTA KUNI, MUME AMELALA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, akipanda mti katika Ofisi ya Kijiji cha Magoza kama sehemu ya utunzaji wa mazingira pamoja na uzinduzi wa mradi wa Majiko Banifu uliofadhiliwa na Green Voices. 

“NI aibu mwanamke anatoka alfajiri kwenda kutafuta kuni wakati mume amelala, tena ni mateso makubwa kwa wanawake,” ndivyo anavyoanza kueleza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magoza.

DC Kihato alisema hayo hivi karibuni alipokuwa anazindua mradi wa Majiko Banifu wa kikundi cha ‘Moto Moto’ unaotekelezwa na wanawake wa kijiji hicho kupitia mradi wa Green Voices.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba, kitendo cha mwanamke kuamka alfajiri kwenda vichakani kutafuta kuni kinaitia doa hata ndoa yenyewe kwa maana kinaongeza mateso kwa upande mmoja hasa mama anapokosa usingizi wa alfajiri.

Alisema mradi huo wa majiko banifu ni wa msingi hasa katika kipindi hiki ambapo mazingira yameharibiwa kutokana na ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya mkaa na kuni, hali ambayo inawawia vigumu hata wanawake kupata kuni za kupikia.

Majiko hayo banifu yanajengwa kwa kutumia udongo wa kawaida wa kwenye vichuguu na gharama pekee ni sukari na vibao vya kufyatulia matofali.

“Misitu yote imekatwa, tena wanaume ndio wanaoongoza kwa ukataji wa miti huku wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa.

“Kila siku ukisimama barabarani utaona malori na baiskeli zimebeba mkaa na kuni kupeleka mjini (Dar es Salaam), wanaume wanaona fahari kukata kuni na mkaa kwenda kuuza lakini hawako tayari kutafuta kuni za kupikia nyumbani, ni aibu kubwa,” alisema DC Kihato.

Aidha, alisema kuni bora zinapelekwa kuuzwa mjini Dar es Salaam wakati wanawake wanabaki kuokoteza kuni ndogo ndogo ambazo zinakwisha baada ya muda mfupi, hivyo kulazimika tena kurudi vichakani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, akiwasili katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda kuzindua mradi wa Majiko Banifu uliofadhiliwa na Green Voices ambao unalenga wanawake kupaza sauti zao katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO


HAFLA YA MAAMUZI YA FOMU ZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2016

$
0
0
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano limeingia katika hatua ya pili ya kupokea fomu na kuwachuja wakina mama waliotuma maombi ya ushiriki wao baada ya hatua ya mwanzo ya kugawa fomu hizo kufanyika katika uzinduzi wa shindano hilo mkoani Mtwara mapema mwaka huu.

Fomu hizo zimepokelewa leo katika kituo cha mazoezi cha Azura jijini Dar ambapo timu ya majaji kumi kutoka taasisi mbalimbali walizipitia fomu hizo katika zoezi litakalochukua takribani wiki nzima hadi kukamilika kwake.

Kwa mujibu wa Afisa Miradi kutoka shirika la kimataifa la Oxfam, Kefah John, alisema kuwa takribani washiriki 3,000 wametuma maombi yao kupitia fomu hizo ambapo katika hatua ya kwanza watapatikana washiriki 28 ambao watachujwa na kubakia washiriki 18 watakaopiga kambi mkoani Monduli, Arusha na hatimaye kumpata mshindi mmoja.

Wakizungumza na waandishi wa habari, msanii Jacob Stephen JB na mtangazaji wa EFM, Dina Marios ambao ni mabalozi wa shindano hilo, waliwahamasisha wakina mama watumie shindano hilo litakalorushwa laivu kupitia kituo cha televisheni ya ITV ili kujifunza njia mbalimbali za kuboresha uzalishaji wao ili kukuza kipato cha familia.

Meneja Utetezi wa Shirika la kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona akizungumza neno la utangulizi wakati wa hafla ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016.
Afisa Miradi kutoka Shirika la kimataifa la OXFAM Kefah Mbogela akizungumzia juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Umiliki wa Ardhi na Changamoto za ardhi na mitaji ili kujiendeleza.
Katikati ni aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula 2014, Ester Kulwa akiwahamasisha wakina mama kushiriki katika Shindano la Mama Shujaa linaloendeshwa na Shirika la Mataifa la OXFAM.

UZINDUZI WA KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FUND JIJINI DAR ES SALAAM WAFANA

$
0
0
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kariakoo family Development Foundation Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi polisi mstaafu Jamal Rwambow akiogea machache na  amekitaka  chama hicho kujali maendeleo ya jamii ya cha hicho kinachowajumuisha wzawa na waliowahi kuishi na wanaoishi eneo lote la Kariakoo jijini Dar es salaam kwa lengo la kushirikiana mambo mbalimbali ya limaendeleo na kijamii.
Mwenyekiti wa kariakoo family development fund mh.mohamed bhinda akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa City Lounge jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kariakoo Family  Development Foundation, Mohamed Bhinda akiwa na Jamal Rwambow (mwenye suti nyeusi) wakikata keki mara baada ya kuzindua  umoja huo.
Wakongwe wa Kariakoo Senpai Yusuf Kivuli (kushoto) na Senpai Waheed  wakiwa katika shoo  ya Goju Ryu Karate  katika uzinduzi wa Kariakoo Family Development Foundation.
 Mkurugenzi wa MMG, Ankal Muhidin Issa Michuzi akilishwa keki katika uzinduzi wa Kariakoo Family Development  Foundation 
Picha ya Pamoja ya Wanakariakoo na Mgeni Rasmi.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU NA JAJI MKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU.

TaESA KUTOA FURSA YA MAFUNZO KATIKA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA AJIRA NCHINI

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa CHADEMA Jimbo la Iringa Mjini, Mhe. Mchungaji Peter Simon Msigwa wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo leo 24 Mei, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Mhe. Joseph Leonard Haule akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Mwijarubi Muhongo akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew John Chenge (kulia) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.

INTRODUCING K SHINER - VYA BURE VINAUA

VIJANA WATAKIWA KUACHANA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0

Na Woinde Shizza,Arusha

Timu ya Intersport club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana mara baada ya kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.

Tamsha hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi kikubwa

Akizungumza wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na kuwapa elimu ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo

"nia alisi ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira"Alisema Neema Mollel

Aidha aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na jamii.Akikabidhi kombe kwa washindi ambao ni Interspot club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.

Sambamba ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na Tsh 100,000 ,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black Eagle Tsh 50,000. 

Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.

PSPF INTER-COLLEGE BONANZA ARUSHA LAFANA

$
0
0
Bonanza maalum kwa ajili ya wanavyuo wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki (Mei 21, 2016) Jijini Arusha lilifana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakijiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.

Viongozi wa vyuo mbalimbali mkoani wakiwa katika picha ya pamoja Afisa Mfawidhi wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina (wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma)  baada kikao cha maandalii kilicho fanyika katika ofisi za PSPF mkoa wa Arusha.

Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini Arusha, lilijumuisha vyuo vya Makumira, Mt. Meru, SAUT, MAN U (Chuo Kikuu cha Arusha), Chuo cha Ufundi Arusha na IAA.
Wanachuo wa IAA, wakishangilia baada ya timu yao kuibuka mshindi katika mpira wa miguu.

Michezo iliyoshindaniwa ni pamoja na Football, Netball, Basketball na Volleyball, hata hivyo mchezo uliovuta hisia za washiriki wengi ni mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya Chuo cha Uhasibu Arusha kilibuka mshindi
Wanachuo wakifatilia Burudani kutoka kwa Mjomba Band
Akifungua mashindano hayo, Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Bw. Daniel Machunda aliwataka wanavyuo hao kutumia michezo hiyo kama sehemu ya kujenga uhusiano Mwema na ushirikianao kati ya vyuo na kati ya yao wenyewe.

Pia aliishukuru PSPF kwa kuandaa Bonanza hilo ambalo msingi wake mkubwa ulikuwa ni kuwaelimisha wanavyuo juu ya huduma za PSPF. “Hili jambo mnalofanya PSPF ni jambo zuri sana kwa wanafunzi wa vyuo vya Arusha pamoja kutoa burudani lakini pia mnawapatia ufahamu juu ya Mfuko wenu (PSPF), hili ni jambo zuri sana na ninawaomba wana vyuo kuazingatia elimu mtakayopatiwa na wakati ukifika mfanye maamuzi sahihi,” alisema Bw. Machunda.
Ukaguzi wa timu kabla ya mchezo, wa tatu kulia ni Afisa Mfawidhi wa PSPF Arusha Bw. Philbert Leina.

Twanga Pepeta kuzindua Albamu ya 13 jijini Mwanza, kuchangia madawati

$
0
0
Bendi ya muziki ya African Stars “Twanga Pepeta” itazindua albamu yake ya 13 ijulikanayo kwa jina la Usiyaogope Maisha mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa Villa Park Jumamosi.

Akuzungumza jijini jana, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekwisha kamilika na wanamuziki wake wapo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya uzinduzi huo.

Mbali ya wimbo wa Husiyaogope  Maisha uliotungwa na Ali Choki, nyimbo nyingine zinazounda albamu hiyo ni Ndoa (Luizer Mbutu), Uso Chini, (Choki), Michepuko (Msafiri Diouf), Mapenzi Yanaumiza (Haji Ramadhani) na Ganda la Mua uliotungwa na Saleh Kupaza ambaye kwa sasa hayupo kwenye bendi hiyo.

Asha alisema kuwa wamekwisha rekodi nyimbo zote na mauzo ya CD 1000 ya kwanza, yatatumika kuchangia ununuzi wa madawati mkoani humo. Alisema kila CD itauzwa Sh3, 000 na Sh 1,000 watatumia kununua madawati.

 “Hii ni heshima kwa wapenzi wa muziki wa Mwanza, bendi inafanya uzinduzi wa albamu hii kwa mara ya kwanza mkoani, albamu zote 12 zilizinduliwa  hapa Dar es Salaam, hii ni mara ya kwanza katika historia ya bendi yetu,”

“Tunataka tuwe tofauti, mpango wa kununua madawati pia utafanyika katika uzinduzi wa albamu hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam katika siku itakayopangwa, tumepiga hesabu na kujua dawati moja ni Sh50,000 (kama utatengeneza mwenyewe), “ alisema Asha.

Alisema kuwa albamu hii ni ya aina yake kwani wanamuziki wake wametunga nyimbo ambazo mbali ya kuburudisha, pia zinatoa mafundisho mbalimbali.

Albamu za nyuma ya bendi hiyo ni  Kisa Cha Mpemba, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binfasi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa,  Safari 2005, Password, Mtaa wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam, Dunia Daraja na Nyumbani ni Nyumbani.

AZAM YAZINDUA DUKA LAKE LA VIFAA VYA MICHEZO JIJINI DAR

$
0
0
Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Azam leo imezindua rasmi duka lake la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya uzinduzi wa duka hilo,Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo,Saad Kawemba amesema duka hilo linauza vifaa mbalimbali vya michezo vya timu hiyo na kuuzwa kwa watu mbalimbali.Pia amesema wanatoa nafasi kwa Wanachama wa Klabu hiyo kuwa vifaa hivyo vinapatikana dukani hapo pamoja na kuzingatia familia za Wanachama hao ikiwemo kupatikana Mabegi ya shule kwa watoto wao.

Ameeleza kuwa kwa wale walio nje ya mkoa wa Dar es Salaam watawasiliana na Tovuti(Website) ya Azam pamoja na Mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Facebook’.Kawemba amewaomba Wanachama wa Klabu hiyo kujitokeza kununua vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mechi ya kesho baina ya Azam FC dhidi ya Dar es Salaam Young Africans,mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kuhusu maandalizi ya Mchezo wa Kesho wa Fainali baina yao na Yanga,Kawemba amesema wamejiandaa vyakutosha na watahakikisha wananyakua ubingwa wa Kombe hilo ambalo linadhaminiwa na wenyewe Azam.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akkata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa moja ya mashine ya kisasa iliyomo dukani hapo kwa ajili ya kubandika namba pamoja majina kwenye jezi za washabiki ama wapenzi wa timu hiyo iwapo watapenda kufanya hivyo kwa gharama iliyo nafuu kabisa.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo la uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.PICHA NA MICHUZI JR

Moja ya jezi "uzi" ukioneshwa mbele ya wana habari hawapo pichani

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa baadhi ya jezi mbalimbali za timu hiyo zinazopatikana dukani humo maalum kwa mashabiki na wapenzi wa soka.

DC MONDULI AENDESHA ZOEZI LA UKAMATAJI WATOTO MINADANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Francis Miti.


Na Woinde Shizza,Monduli

Imeelezwa kuwa Asilimia 10 ya watoto wilayani Monduli wanatajwa kutokwenda shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro,pamoja na kufanya biashara katika baadhi ya minada wilayani humo jambo ambalo limeamsha hisia za viongozi wa wilaya na kuamua kufanya operesheni ya kuwakamata na kuwapeleka shule kwa lazima Zaidi ya watoto 21.

Hayo yameelezwa leo naAfisa elimu msingi Theresia Kyala kutoka wilaya ya Monduli mara baada ya ya zoezi la ukamataji wa watoto watoro amnao wanafanya biashara eneo la minada ambapo zoezi hilo lilifanyika mnada wa katika eneo la losirwa iliyoko kata ya mto wa mbu iko ambapo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa wilaya ya Monduli bw,Francis Miti ambapo eneo hilo lina wakazi laki tatu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 huku Zaidi wakiwa ni wakazi wa jamii ya kifugaji.

Ambapo zoezi hilo limeendeshwa chininya usisamizi wa mkuu huyo na uongozi wa idara ya elimu imetembelea eneo la mnada wa Kigongoni na kuona watoto namna ambavyo wanaendelea kufanya biashara ndani ya mnada huo wakati wenzao wakiwa madarasani ambapo nikazungumza na baadhi ya watoto hao ambao wanaelezea baadhi ya sababu zilizowapelekea kutokwenda shule ikiwemo ugumu wa maisha huku wengine wakishindwa kujielezea.

Theresia Kyara ni afisa elimu msingi wilayani Monduli alisema kuwazoezi la operesheni hiyo wameianza rasmi katika soko la Alhamisi la eneo la monduli mjini na kufanikiwa kukamata watoto 16 na leo hii wamekamata watoto 21 hii kati ya hao watoto sita wamepelekwa bweni shule ya Manyara inaongeza idadi ya watoto ambao hawajaenda shule katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo ya Monduli Francis Miti amesema kuwa ameamua kutoa agizo hilo na kutekelezwa kwa lengo la kuwawezesha kwa kila mtoto mwenye sifa ya kwenda shule aweze kupata elimu hiyo ya kuanzaia msingi bure kwa lengo la kumuunga mkono mh,Rais katika utoaji wa elimu bure ili kuweza kuweza kushinda katika sekta ya elimu.

Pia amewataka wazazi wote wenye watoto kuhakikisha wanapeleka shule watoto wao na kuwaandikisha na endapo mzazi ama mlezi atakae mhusisha na kumkataza mtoto wake hatua za kisheria zitachukuliwa.Mkuu wa wilaya ya Monduli ameongeza kuwa zoezi hili la ukamatwaji wa watoto hao ambao kati yao wapo waliotoka kwaajili ya kuchunga katika minada huku wengine wakiwa hawajasoma kabisaa.

Nae mmoja wa mzazi bi,Moses ole laizer amesema kuwa zoezi hilo la kukamata watoto hao litaleta tija katika jamii kutokana na kuwa hakuna sababu inayofanya watoto hao wasiende shule kutokana na elimu kuwa bure na wazazi kuwaachia baadhi yao kuenda kufanya biashara minadani.Aliongeza kuwa baadhi ya Jamii za kifugaji hususani wamasai wamekuwa na muamko mdogo wa kupeleka watoto wao kupata elimu jambo ambalo linawanyima haki ya msingi kwa kila mtoto mwenye sifa kwenda shule

CBE yatoa ufafanuzi tuhuma za upostoshaji.

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na Baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini kuhusu chuo hicho.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema amesema tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa kutisha si za kweli na zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho.

“Chuo kinafanyiwa ukaguzi wa Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali na kwa kipindi cha miaka minne tumepata hati safi (clean audit report) kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 .” alisisitiza Prof. Mjema.Katika ukaguzi huo ripoti hiyo ilionyesha kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikizingatia sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma hali iliyopelekea kupata hati safi kwa kipindi chote.

Pia Chuo hicho kilifanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Udhibiti wa manunuzi Serikalini (PPRA) kwa mwaka unaoishia 2014/2015 na Chuo hicho kupata alama 95.8 hivyo kuwa moja ya Taasisi za Umma zinazofanya vizuri katika kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi ya umma.

Prof. Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika.

Mafanikio mengine ni kujenga hema kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya vipimo na mizani chuoni hapo.
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari.
 Mkuu wa Chuo cha Elimu Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ya Mwaka huu inayoonesha chuo hicho ni moja kati ya Taasisi 14 zilizofanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 95.8 katika kufuatilia sheria ya manunuzi ya umma na kuutaka umma kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa wanakiuka sheria hizo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images