Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1229 | 1230 | (Page 1231) | 1232 | 1233 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Hapa ni katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo leo Jumapili Mei 22,2016 Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga(Ahmadiyya Muslim Jamaat Shinyanga) imefanya mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga ukiwa na kauli mbiu ya " Love For All Hatred For None (Mapenzi Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote".

  Mgeni rasmi alikuwa katibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji aliyemwakilisha kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella huku waumini wa dini hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano huo.

  Mkutano huo uliolenga kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu hali itakayosaidia kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na albino, umehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (pichani juu).

  Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya watu watu msikitini na kuongeza kuwa dini ya kiislam hairuhusu vitendo kama hivyo huku akiviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho haramu.

  Kupitia mkutano huo jamii imeelimishwa juu ya dhana potofu dhidi ya uislamu ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha dini hiyo pamoja na vikundi vya kigaidi mfano wa Boko haram, Isis, Al-shabaab na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikidhuru binadamu.

  Mada mbalimbali zimetolewa na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwemo nafasi ya dini katika maisha ya binadamu,malezi ya watoto na majukumu ya wazazi sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu,umuhimu wa kuwa kiongozi (Khalifa) wa kiroho na barakaza ukhalifa pamoja na masharti ya kujiunga na jumuiya hiyo(masharti 10 ya Baiat na wajibu wa waumini.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa mkutano huo,ametusogezea picha 55 kilichojiri.
  Mgeni rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ambapo alisema suala amani katika jamii ni watu wote hivyo kuwataka watanzania kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kutenda uhalifu .
  Aliyesimama ni Afisa wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai mkoa wa Shinyanga Issa Ramadhan akitoa neno ambapo alisema jamii yenye malezi mema haiwezi kuwa na vitendo vya kihalifu na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua watu wote wanaofanya vitendo vya uhalifu

  Wanawake wa Kiislam wakiwa katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa mwaka,ambapo kwa mara ya pili sasa mkutano kama huo unafanyika mkoani Shinyanga,mkutano mwingine ulifanyika mwaka 2014

  Waumini wakifutilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano huo. 


  0 0


  0 0

   Independence Former First Ladies expected to grace Special Sitting on May 31, 2016.


  East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: May 21, 2016: The East African Legislative Assembly (EALA) holds its sitting in Arusha, Tanzania, next week. The Sixth Meeting of the Fourth Session of the Third Assembly takes place from Monday, May 23, 2016 to Friday, June 3, 2016.

  The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two week period is the EAC Budget Speech which is expected to be delivered on Thursday, May 26th, 2016, by the Chair of the Council of Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.  The Assembly is then expected to debate and approve the Budget as part of its mandate.

  The Budget Speech is a key activity of the EAC calendar. Last year, EALA debated and approved EAC Budget estimates for the Financial Year 2015/2016 totaling to USD 110, 660,098.

  The 2015/2016 Budget prioritized on the operationalization of the Single Customs Territory, enhanced implementation of the EAC Common Market Protocol with particular focus on implementation of the new generation EAC internationalised e-Passports and development of the EAC trading, payments and settlements systems.

  Also top on the agenda during the two week period is a Special Sitting to be addressed by the Partner States’ Independence former First Ladies, Their Excellences, Mama Ngina Kenyatta (Kenya), Mama Miria Obote (Uganda) and Mama Maria Nyerere (United Republic of Tanzania).

  The Special Sitting on May 31st, 2016, presents a unique opportunity for the Members to interact and to share experiences with the distinguished former first ladies’ given that EAC as is constituted today, borrows a number of best practices from the first bloc.

  Debate on the recent State of EAC Address, is also on the menu.  On March 8th, 2016, The Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Rt Hon Kassim Majaliwa delivered the State of EAC Address to EALA at the 5th Meeting of the 4th Session in Dar Es Salaam, Tanzania.

  The Prime Minister informed the House that progress had been realised following the entry of the Single Customs Territory. He remarked that finalization of key operational instruments, revision of business manuals, development of M&E tool framework, deployment of staff and revision of an enforcement framework had opened the path for the operationalisation of the SCT in the Partner States.

  Two key Bills on the cards at the EALA meeting are the EAC Persons with Disabilities (PWD) Bill, 2015 and the EAC Supplementary Appropriation Bill, 2016.

  The object of PWD Bill, 2015 is to provide a comprehensive legal framework for the protection of the rights of persons with disability in the Community. The Bill is premised under the provisions of Article 120 (c) of the EAC Treaty under which, Partner States closely co-operate amongst themselves in the field of social welfare with respect to the development and adoption of a common approach towards disadvantaged and marginalized groups.  Such groups include children, the youth, the elderly and persons with disability through rehabilitation and provision of among others, foster homes, healthcare, education and training.

  The House is also expected to receive and to debate on a number of Committee reports.  On the other side, its Committees shall hold consultative meetings with the EAC Council of Ministers.   The Communications, Trade and Investments Committee has a date with the EAC Council of Ministers to review the EAC Sectional Properties Bill, 2016 and the EA Customs Management (Amendment Act) 2016. 

  On its part, the General Purpose Committee will consult with the Council on the Supplementary Budget Bill and the PWD Bill respectively, prior to tabling of both Bills in the House.

  0 0

   Seminar in session with members from 24 towns, villages and hamlets of Bagamoyo District research areas.
  A group picture of Members of the Community Advisory Board of TB Research work of new TB drugs to go on  trial soon. Seated centre is CAB Chairman Sayed Abdul Hai and second right in stripped T-shirt is coordinator Dr. Omar Juma. standing on left in blue shirt is Secretary Micky Dhamir.

  0 0

  • Wawezeshwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni tano.

  Airtel Tanzania inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kuwashika mkono vijana hapa nchini  ambapo mwishoni mwa wiki hii kupitia mpango wake wa kutoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha, uliweza kuchagua vijana wawili walioweza kuelezea na kuwakilisha changamoto wanazozipata katika biashara wanazozifanya mbele ya jopo la washauri ambao leo hii wamekabidhiwa  vitendea kazi vyenye dhamani ya shilling milioni 5  ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

  Akizungumza wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel huduma kwa Jamii Hawa Bayumi alisema "baada ya kufanya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali wiki chache zilizopita na kuweza kufikia vijana zaidi ya 300 jijini Dar Es Salaam  waliojitokeza na kuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira na na uwezo wa kujenga fursa nyingine. Leo hii tupo hapa kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

  “Na siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja kwani vijana waliweza kujifunza mambo mengi sana na mwisho wa siku waliweza kuelezea na kuwasilisha biashara zao mbele ya jopo la washauri na ulikuwa uamuzi mgumu sana lakini mwisho wa siku tuliweza kupata vijana wawili bora walioweza kushinda nyoyo za jopo la washauri hao, ambao leo  hii tupo hapa kwajili ya kuwakabidhi vifaa vyao ili waweze kwenda  kukabiliana na changamoto walizonazo katika biashara zao. "

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
   Stephen Gimase (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiangalia vifaa alivyokabidhiwa na Airtel FURSA kwa ajili ya kuboresha biashara yake ya kutengeneza mashine za kutengenezea vifaranga vya kuku, Kushoto ni Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi 
  Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (2 Kushoto) akimkabidhi Theresia Maliatabu (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” vifaa vyakuboresha biashara yake ya uchoraji ikiwemo meza ya kuchorea na kompyuta ya kisasa. Kijana huyu Aliyechaguliwa kutoka kwenye mafunzo ya biashara ya ujasiriamali  ya Airtel FURSA yaliyofanyika Dar es Salaam wiki chache zilizopita. Akishuhudiwa na mama yake mzazi Judith Benedicto (Katikati) na mama mkubwa Salome Benedicto (Kulia) pamoja na Afisa mauzo wa Airtel katika hafla iliyofanyika Mbagala kuu, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  makongoro
  Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
  Makongoro (2)
  Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni (Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika.Makongoro (1)
  Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.Makongoro (3)
  Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.

  0 0


  0 0

  Kampuni ya simu inayoongoza visiwani Zanzibar, Zantel, imewekeza jumla ya dola milioni 10 za kimarekani ili kuimarisha huduma zake za mawasiliano nchini.Mpango huo unajumuisha kubadilisha mfumo mzima wa mawasiliano kwa kubadilisha vifaa vilivyokuwepo na kuweka mitambo mipya kwa madhumuni ya kuimarisha mawasiliano ya simu na kuongeza kasi ya mtandao.

  Akizungumza na waandishi wa habari visiwani humu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Benoit Janin alisema kuimarisha huko katika huduma za simu na mtandao kwa upande wa Zanzibar ndio kilikuwa kipaumbele cha kwanza cha kampuni ya Zantel.‘Kampuni ya Zantel imeanza safari mpya kabisa yenye lengo la kuimarisha na kurudisha nafasi ya mtandao wa Zantel katika ubunifu na kutoa huduma bora visiwani hapa’ alisema bwana Janin.Bwana Janin pia alisema uboreshaji wa huduma za Zantel ni mpango endelevu na katika kipindi kifupi kijacho, Zantel itaendelea kufunga vifaa vipya hali ambayo itawafanya wateja waweze kuwasiliana kwa bei nafuu na bila ya bughudha.

  ‘Maboresho haya yamelenga kuhakikisha tunakuza na kuimarisha teknolojia ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kipekee na kutekeleza ahadi yetu ya kuendelea kuongoza katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu’ alisema Bwana Benoit.Janin pia alielezea mpango wa kampuni ya Zantel kuboresha huduma ya EzyPesa kwa kurekebisha mfumo mzima ili uweze kuhimili mawakala wengi na kuongeza huduma za ndani ya mfumo huo. Katika kipindi kifupi pia kampuni ya Zantel pia imefanikiwa kuondoa mtandao wa 2G na kuweka mtandao wa 3G, sambamba na kuzindua rasmi mtandao wa kasi wa intaneti wa 4G mjini Unguja. 

  ‘Nina furaha kubwa jinsi utekelezaji wa mikakati yetu unavyoendelea wa kuboresha huduma zetu ambao utawapa wateja wetu nafasi ya kufurahia huduma zetu na pia kuwapunguzia gharama za mawasliano huku tukukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa wakati huu na siku zijazo’ alisema Janin. Bwana Janin pia alisema tayari matatizo ya mawasiliano ya huduma za 3G yameshatatuliwa kwa kutumia mkonga wa fiber katika ya maeneo ya Unguja na Pemba.

  ‘Tumefanikiwa kuyatatua matatizo madogo madogo katika mji mkongwe kwa kuweka vifaa ambavyo vimesaidia sana kuondoa msongamano wa mawasiliano majumbani na katika sehemu za wazi’ alisema Janin. Kampuni ya Zantel ambayo ilizindua huduma ya mtandao wa 4G katika mji wa Unguja mwezi uliopita pia imefanikiwa kufikisha mawasiliano kwa asilimia 80% ya watanzania kutoka asilimia 40% waliyokua wanawafikia awali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel upande wa Zanzibar, Ibrahim Attas.

  0 0  0 0

  HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

  KUSHIKILIWA NA KIKOSI KAZI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHIFADHI MWANDAMIZI GENES SHAYO.

  Mhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Genes Shayo (60) anashikiliwa na Kikosi Kazi Maalum cha kupambana na ujangili nchini kufuatia taarifa za kuhusishwa kwake na upatikanaji wa jino la tembo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

  Shirika la Hifadhi za Taifa kupitia taratibu za utendaji kazi lilipokea taarifa za kintelijensia tarehe 14.05.2016 zikimhusisha mwananchi mmoja mkazi wa Ngarenanyuki, Arumeru Emmanuel Nassari (46) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa TAG kumiliki jino la tembo na kuwa alihitaji kupata mtu wa kufanya naye biashara. Baaada ya kupata taarifa hizi shirika liliwasiliana na Kikosi Kazi Maalum cha Kitaifa kinachohusika na masuala ya ujangili ili kushirikiana kwa ajili ya ufuatiliaji.

  Kikosi Kazi hiki mara baada ya kupata taarifa hizi kiliendelea na taratibu zake za kiuchunguzi na baada ya ufuatiliaji walifanikiwa kumkamata Emmanuel Nassari tarehe 15.05.2016 akiwa na jino moja la tembo ambapo katika mahojiano yaliyofanyika alimhusisha Mhifadhi Mwandamizi wa TANAPA Genes Shayo kuwa anazo taarifa za yeye kuwa na jino hilo na hivyo kukamatwa tarehe 16.05.2016 kwa ajili ya mahojiano zaidi. 

  Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea kutoa wito kwa raia wema wa nchi hii kuendelea kutoa taarifa za kufichua vitendo vya ujangili na kwamba halitasita kuchukua hatua stahiki kwa yeyote anayehusika na vitendo hivi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake watakaobainika kisheria kuhusika na vitendo hivi.

  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
  Hifadhi za Taifa Tanzania
  S.L.P 3134
  ARUSHA
  Simu: +255 027 254 4082
  Baruapepe: dg@tanzaniapaks.go.tz
  Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz

  0 0

  Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Masuala ya Afya wa Mawaziri unaoandaliwa na Chuo Kikuu cha Harvard ujulikanao kama Harvard Health Leaders' Ministerial Roundtable uliofanyika Geneva leo. 
  Mkutano huo wenye lengo la kujenga uwezo wa Mawaziri wa Afya na Wataalam kwa njia ya kubadilishana uzoefu umehudhuriwa na mawaziri wa Afya kutoka nchi zaidi ya 40 wakiwemo Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo. 
  Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu alialikwa kushiriki na kuelezea uzoefu wake katika mjadala kuhusu 'Mafanikio ya Kukumbukwa kwa Kuwezesha Utekelezaji wenye Matokeo' (Achieving a Legacy in Goverment by Getting Things Done). Katika mjadala huo, 
  Rais Mstaafu Kikwete alielezea uzoefu wake kuhusu changamoto za utekelezaji wa programu na miradi ya Serikali na chimbuko la kuanzishwa kwa 'Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa' (BRN) ikiwemo mafanikio na changamoto zake. Katika jopo hilo, walishiriki pia Mhe. Baroness Tessa Jowel, Waziri wa Zamani wa Uingereza wa Masuala ya Olimpiki na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Habari, na Mheshimiwa Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia anayeshughulikia Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Matokeo Malaysia ujulikanao kama PEMANDU.
  Mheshimiwa Rais Mstaafu ameelezea changamoto aliyoipata kabla ya kuansishwa kwa BRN ambapo ilikuwa vigumu kujua na kufuatilia kwa uhakika hatua inayopigwa katika utekelezaji wa miradi na shughuli za Serikali. Kiu yake ilipata jawabu alipofanya ziara nchini Malaysia na kujifunza namna Mpango wao wa PEMANDU ulivyokuwa ukifanya kazi. 
  Aliamua kujifunza kuwaalika wataalamu wa PEMANDU kuja kusaidia wataalam wa Tanzania kubuni mpango wa BRN. Ameusifia mpango wa BRN kuwa umewezesha ufanisi kwa kuwezesha kupata 'matokeo makubwa kwa rasilimali zile zile'. 
  Aidha mpango umewaleta pamoja wadau wote wa ndani na nje ya Serikali kushirikiana pamoja na kuainisha changamoto, kukubaliana vipaumbele, ufumbuzi, kugawana majukumu na kuhimizana katika kutimiza wajibu wa kila mdau. Aidha imewezesha kuwepo kwa takwimu na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uwajibikaji wa Serikali katika kutekeleza ahadi zake. Pamoja na uzuri wa mpango huo na mafanikio yaliyopatikana, changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa rasilimali katika kutekeleza miradi hiyo kwa wakati. 
   Katika mjadala huo, Mawaziri wa nchi za Afrika wamevutiwa na uzoefu wa Tanzania na Mpango wa BRN na wameonyesha shauku ya kutaka kujifunza zaidi juu ya mpango wa BRN. Wamempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuonyesha uongozi kwa kuwezesha ubunifu katika utekelezaji wa programu za Serikali ambao umekuwa na matokeo mazuri yenye kupimika.
  Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo  katika Mkutano wa Masuala ya Afya wa Mawaziri unaoandaliwa na Chuo Kikuu cha Harvard ujulikanao kama Harvard Health Leaders' Ministerial Roundtable uliofanyika Geneva leo. Wengine ni Mhe. Baroness Tessa Jowel, Waziri wa Zamani wa Uingereza wa Masuala ya Olimpiki na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Habari, na Mheshimiwa Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia anayeshughulikia Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Matokeo Malaysia ujulikanao kama PEMANDU.
  Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni  Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo. 
  Balozi Modest Melo akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo mkutanoni
  Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo. 


  0 0  0 0

  UN Women Executive Director Phumzile Mlambo-Ngcuka and Deputy Executive Director Yannick Glemarec will join other world leaders at the first World Humanitarian Summit (WHS) held today and tomorrow in Istanbul, Turkey.

  The first gathering of its kind, the Summit aims to place humanity—people’s safety, dignity and the right to thrive—at the heart of global decision-making and initiate a set of concrete actions and commitments to enable countries and communities to better prepare for and respond to crises. With more than 5,000 expected participants, the programme will include seven high-level leaders' roundtables on priority action areas.

  At the Summit, UN Women will advocate for greater investment for gender equality and for women’s rights and women’s empowerment to become standard principles of humanitarian planning and action. UN Women and UNFPA Executive Directors will be UN co-chairs for tomorrow’s Roundtable Four, entitled “High-Level Leaders’ Roundtable on Women and Girls: Catalyzing Action to Achieve Gender Equality”, where Member States, UN and multilateral actors will come together to endorse core commitments to improve humanitarian action for women and girls worldwide.  

  Member State co-chairs for Roundtable four will include: President Kolinda Grabar-Kitarović (Croatia); President Michael D. Higgins (Ireland); Deputy Prime Minister Fiame Naomi Mata’afa (Samoa) and Deputy Prime Minister and Minister for Foreign Affairs Margot Wallström (Sweden). The Roundtable will be attended by more than 25 Member States and civil society representatives.

  READ MORE HERE

  0 0
 • 05/23/16--02:00: Kumbukumbu • 0 0

   The construction of the main terminal building – facilitating 6 million annual passengers – including parking lots, access roads, platforms and taxiway.

  Phase 1 of the scope of work comprises the construction of the main terminal building - facilitating 3.5 million annual passengers - including parking lots, access roads, platforms, and a taxiway. 
  The design of the roof is inspired on the traditional sailing boats that can be found at the Dar es Salaam Coast. The new terminal 3 is designed (together with NACO, Netherlands Airport Consultants) for the anticipated growth of international air traffic, leaving the existing international Terminal 2 to cater for domestic flights. The second phase will then provide further capacity to facilitate 6 million annual passengers.
   Terminal II view from the new terminal
   The new Terminal III taking shape
   Front under construction
   Part of  terminal III under construction
  Engineers, consultants  and contractors busy at work. 

  0 0
 • 05/23/16--02:19: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Manispaa ya Kinondoni imeahidi kusimamia sekta ya michezo kikamilifu ili kuinua vipaji vya vijana katika Manispaa ya Kinondoni.

  Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob wakati kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo Sekondari Tanzania (UMISETA) kwa Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika shule ya Sekondari Makongo Jumapili 22/5/2016,ikiwa zimeshirikishwa shule kutoka Majimbo matano ya Dar es salaam.

  Akiongea Mstahiki Meya amesema Halmashauri inapambana kurudisha maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na matajiri ili vitumike kwa ajili michezo katika kukuza vipaji vya vijana katika Manispaa ya Kinondoni.Amemtaka Afisa elimu Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni kuangali viwanja ambavyo vimeharibika achukue greda la Manispaa lipo viwanja vichimbwe ili vijana wacheze kwenye viwanja vyenye hali nzuri.

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob akikabidhi kikombe kwa Nahodha wa moja ya Timu zilizoshiriki Mashindani ya UMISETA.  "Tulikuwa na mazungumzo na waziri viwanja virudishwe kwa wananchi mfano uwanja wa KIFA na UFI, vijana wapate maeneo ya kucheza, tukianza leo kuweka msisitizo katika michezo usishangae 2030 kuwaona vijana wetu wanashiriki kombe la dunia au vipi wanamichezo?" Amesema Mstahiki Meya.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  KAMPUNI YA MOSAN LIMITED INAKUTANGAZIA NAFASI ZA KAZI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:
  1.       MAAFISA MASOKO NA MAUZO (SALES AND MARKETING OFFICERS)
  2.       MAAFISA MAUZO (SALES OFFICERS)

  SIFA
  I.                    UWEZO WA KUENDESHA PIKIPIKI NA GARI
  II.                  UWEZO WA KUUZA NA KUTAFUTA MASOKO, PIA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIASHARA
  III.                MAARIFA YA MASOKO
  TUMA MAELEZO BINAFSI (CV) KWENYE EMAIL HII: employment.mosan@gmail.com.

  AU PIGA SIMU HII KWA MAELEZO ZAIDI: +255 717 49 87 73.
  Mwisho wa kutuma maombi ni Mei, 27, 2016.

  0 0

  Na Bashir Yakub. 

   Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. Kama ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka. 

   Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sura ya 29 ya Sheria ya ndoa na si katika imani ya dini yoyote. 

   1.TALAKA NININI. 

   Talaka ni amri /tamko maalum la mahakama linalotamka kuhusu kuvunjika kwa ndoa. Hii ndio maana ya talaka lakini kwa mujibu wa sheria. Katika maana hiyo twapata kujua kuwa talaka ni lazima itolewe na mahakama. 

  Mahakama ndicho chombo chenye dhamana kuu katika kubatilisha ndoa kwa namna ya talaka. 

   2. JE UNAWEZA KUOMBA TALAKA MUDA GANI BAADA YA KUFUNGA NDOA. 

   Ili uweze kuomba talaka ni lazima ndoa itimize miaka iwili . Huwezi kufunga ndoa mwezi huu halafu mwezi ujao ukakimbilia mahakamani ukitaka talaka. Ndoa ikifikisha miaka miwili basi haki ya talaka inafunguka. 

   3. TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA. 

   Sio kila kuachana ni talaka. Aina nyingine za kuachana zina sifa za kutengana na sio talaka. Kutengana ni hatua ambapo wanandoa wanaacha kuishi chini ya paa au dari moja. Wanaweza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.Halikadhalika wanaweza kuishi nyumba tofauti na hata pakawa mbali ya nchi kwa nchi, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya,kijiji kwa kijiji n.k. 

   Tofauti kubwa kati ya talaka na kutengana ni kuwa katika talaka kunakuwa na tamko maalum kutoka mamlaka maalum linalositisha mahusiano ya ndoa, wakati katika kutengana hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka linalotangaza kuisha au kusitishwa kwa mahusiano ya ndoa. Kutengana kupo kwa aina mbili. 

   Kwanza ni kutengana kwa hiari ambapo wanandoa kwa hiari yao wanatengana, na pili ni kutengana kwa kuiomba mahakama kuwatenganisha. Yapo mazingira ambapo kumtenga mwenza kunaweza kuwa kugumu kutokana na mazingira kadha wa kadha na hapo ndipo unapoweza kuiomba mahakama iwatenganishe.


  0 0

older | 1 | .... | 1229 | 1230 | (Page 1231) | 1232 | 1233 | .... | 3270 | newer