Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO


Melisa John Aibuka Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania

$
0
0
Mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya taifa  yamefikia mwisho ambapo Melisa John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam.

Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki wakimarekani Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2.

Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2.

Kufatia ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.

Mshindi wa  Airtel Trace Music Afrika atapata nafasi ya kupata mafunzo ya muziki  na kurekodi video na mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo Keri Hilson , Atlanta nchini Marekani.

“Nimefurahi sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi ndoto zangu. Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini Nigeria.”

Katika fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon 
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa  mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo. Melisa amejishindia shilingi milion50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika.
 mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John akipongezwa na mama yake baada ya kuibuka mshindi nakupata kitita cha shilingi milioni 50.
 Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi Gabriel Kaisi (kulia) akimkabithi Nandi Charles mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, katika shindano hilo Melisa John aliibuka kuwa mshindi wa kwanza.
wanavyoimba ili kupata mshindi wa shindano hilo kwa Tanzania
 Mshindi wa tatu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Salim Mlindila akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Tabasamu, Lucy Ngongoseke.
 mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi na  kukabithiwa mfano wa hundi ya shilingi miliioni 50. Kulia ni mama yake Melisa John,na kushoto nao MC wa fainali hizo.

PSPF Yatoa Elimu kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar Kujiunga na Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji kwa Hiari wa PSPF

$
0
0

Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF Ndg Mohammed Salum akitowa maelezo ya manufaa ya Kujiunga na Uchangiaji wa Hiyari kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano na faida zake kupitia Mfuko huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliodhaminiwa na PSPF.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar Ndg Khamis Rashid, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira kuufungua mkutano huo Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Jengo Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira akitowa nasaha zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la Sanaa Rahaleo Zanzibar
 
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Ramadhani Nzori, akizungumza kabla ya kumkaribisha Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF kuzungumzia umuhimu wa kujichangia kwa hiari katika Mfuko huo kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 

LOWASSA KUANZA MIKUTANO YA KUIMARISHA CHAMA NCHI NZIMA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeneo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa tiketi ya chama hicho na kuungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa akisalimiana na viongozi wa walemavu wilayani Monduli kwenye Mkutano wa kwanza wa kuimarisha chama nchi nzima.

NHIF TANGA YAWAPIGA MSASA WARATIBU WA CHIF MKOA WA TANGA.

$
0
0
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akisisitiza jambo wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo.
Mratibu wa GIZ Mkoa wa Tanga,Apolinary Primus Rutakuburwa ambao wanasapoti huduma za afya na matibabu kulia akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akifuatilia kwa umakini.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga,Miraji Msile akiwaelekeza jambo waratibu wa CHF wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo.

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Akabidhi Msaada wa Madawa na Maji kwa Ajili ya Kambi za Kipundupindu Zanzibar

$
0
0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar, kulia Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Halima Maulid na kushoto kwa Balozi Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed na Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar. Dk Mohammed Dahoma. 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akikabidhi msaada wa Dawa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said, wakishuhudia kulia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Halima Maulid na kushoto Daktari Dhamana Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Halima Maulid akimkabidhi Madawa Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed, baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania.

WAZEE YANGA WAMUUNGA MKONO MANJI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
Na  Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BARAZA la wazee wa Yanga wamesema wanamuunga mkono Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Yusuph Manji kuelekea uchaguzi mkuu wao unaotarajiwa kufanyika Juni 25 mwaka huu kufuatia kukaa miaka miwili nje ya katiba bila kuwa na kiongozi wa juu.

Akizungumza huku wakionesha msimamo wao kama baraza la wazee la Yanga wakiwa kwa pamoja na wenyeviti wa matawi wa mkoa wa Dar es salaam,  Katibu wa baraza hilo Ibrahim Akilimali amesema kuwa wanamuunga mkono Manji kwa asilimia zote kwani ameweza kuisaidia timu hiyo toka akiwa mdhamini mpaka kufikia kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.

"Kwa upande wa baraza la wazee tunamuunga mkono Manji kwani toka Yanga imekuwa chini yake kumekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuweza kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho na kama kuna masuala mengine ikiwemo ya uwanja uongozi mpya utakapoingia tutakaa nao kuweza kujua tunafikia wapi malengo yetu ya kujenga kwani tumeshafikia kwenye hatua bado kibali tu,"amesema Akilimali.

Amesema, watu wasitake kuangalia suala la Uwanja kwa Manji tu mbona kuna viongozi wengine wamepita na hawajajenga cha msingi ni kuangalia wapi tunaelekea na nini kinachotakiwa kufanyika kwenye klabu kwa ajili ya maendeleo.

Wazee hao wamesema kwa pamoja kuwa mbali na hilo pia wanawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 26 pamoja na kuingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirishiko ikiwa ni moja mafanikio wanayojivunia chini ya Manji.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.tv: Maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini yamezidi kuongezeka zaidi kwa vijana huku vijana wa kike wakiwa hatarini zaidi kuliko wale wakiume;https://youtu.be/6TeIhJ5v4Z0

SIMU.tv: Baraza la madiwani halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi wametoa dira ya bei ya zao la ufuta kwa wakulima huku bei ya mwanzo ikiwa ni shilingi 2000;https://youtu.be/S7WedHZTtdQ

SIMU.tv: Manispaa ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imetakiwa kujitathimini baada ya kutoa taarifa ya uongo juu ya uwepo wa bidhaa feki katika manispaa hiyo;https://youtu.be/NiG1cCZQp5w

SIMU.tv: Wananchi wa kijijini cha Kiru wilayani Babati wameahidi kutomaliza migogoro ya ardhi nawawekezaji wilayani humo endapo serikali haitokwenda kupima maeneo yao;https://youtu.be/yWSqh24dldI

SIMU.tv: Ligi kuu ya Tanzania bara inamalizika hii kwa michezo mbalimbali kupigwa katika katika viwanja tofauti nchini huku mabingwa wa ligi hiyo Yanga wakiwa songea kukipiga na Majimaji na Simba watakuwa uwanja wa taifa jijini Dar; https://youtu.be/TXnPwMlro4c

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata watumishi wawili wa halmashauri ya Bunda kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 2; https://youtu.be/GPdz2MUsEQo

SIMU.tv: Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella ameingilia kati mgogoro wa muda mrefu wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Msalala Kahama;https://youtu.be/ZHXnsRu73ec

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametangaza msako wa wanafunzi wote watoro mkoani humo na kuwarudisha darasani mapema wiki ijayo;https://youtu.be/cgHmO0UWJVI

SIMU.tv: Wanafunzi wa kidato cha pili katika sekondari ya Madimba mkoani Mtwara wanalazimika kusomea katika maabara baada ya kukosekana kwa vyumba vya kutosha vya madarasa pamoja na nyumba za walimu na matundu ya vyoo;https://youtu.be/F75vQ7GtSE4

SIMU.tv: Timu ya taifa ya vijana Serengeti boys imekosa nafasi ya kucheza fainali katika mashindano maluumu yanayoendelea nchini India baada ya hapo jana kutoka sare ya 2-2 na Malaysia; https://youtu.be/SokSl2EjctQ

SIMU.tv: Ligi kuu ya Tanzania bara inamalizika hii kwa michezo mbalimbali kupigwa katika katika viwanja tofauti nchini huku mabingwa wa ligi hiyo Yanga wakiwa songea kukipiga na Majimaji na Simba watakuwa uwanja wa taifa jijini Dar; https://youtu.be/dZ3jeZJT0qA

SIMU.tv: Timu ya soka ya Azam imesema kwa sasa iko katika mazungumzo na klabu ya Deportivo Terenife ya nchini Hispania  kuhusu mauzo ya mchezaji wake Farid Mussa baada ya kufuzu majaribio yake ya soka la kulipwa; https://youtu.be/tXPRMDNosbA

RAIS FIFA GIANNI INFANTINO AIPONGEZA YOUNG AFRICANS

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.

Young Africans imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.

Katika salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa wa Young Africans kwamba umetokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.

“Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa. Taji la Young Africans ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Young Africans.

Amesema pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Young Africans.

“Kwa niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Young Africans na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.
Tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya fedha Sh 81,345,723.

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAKUNWA NA TAMASHA LA JEMBEKA

$
0
0
Msanii kutoka nchini Marekani Neyo akishambulia jukwaa na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Mwanza .
Neyo akiwa pamoja na Diamond Platnumz jukwaani wakiambulisha wimbo wao mpya mbele ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ruby akiimba kwenye tamasha la Jembe Festival kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Rapa Stamina akiupagawisha umma na mistari iliyo simama kwenye tamasha la Jembe mjini Mwanza.
Mr. Blu akirap nyimbo zake zilizompa umaarufu kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Diamond Platnumz na vijana wake wakishambulia jukwaa kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye viwanja vya CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mgeni rasmi wa tamasha la muziki la Jembe , Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk. Sebastian Ndege kwenye chumba maalum nyuma ya jukwaa ,CCM Kirumba .

DKT. SHEIN AFUNGUA MASHINDANO YA TAMASHA LA MICHEZO YA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMI YA JUU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo wa vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyuo hivyo yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo Kizimbani wakiwa katika maandamano wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika Ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.

TAARIFA KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU WILSON KABWE KUFUATIA UPOTOSHWAJI WA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Familia ya Marehemu Wilson Kabwe  imesikitishwa sana na taarifa zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu kauli na msimamo wa familia katika shughuli za maazishi ya mpendwa wao Wilson Kabwe.

Familia inapenda kuchukua nafasi hii kutamka bayana kwamba, Dk. Zawadi Machuve si msemaji wa familia. Kauli yake iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba:-

" Sisi hapa hatukaribishi viongozi, huu ni msimamo wa familia kama wao watafanya utaratibu wao sawa, lakini hatuko kwa ajili ya viongozi"

Kauli hiyo ambayo ililenga kutoishirikisha Serikali katika msiba wa mtumishi wake tunaomba ipuuzwe na siyo kauli ya familia.

Familia inatambua na inathamini sana mchango mkubwa wa Serikali katika kugharamia matibabu na  huduma  zote za mazishi.

Familia inachukua fursa hii kuwakaribisha viongozi wote wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki wanaopenda kushiriki katika shughuli za mazishi ya mpendwa wetu.
Imetolewa na:

PHILIP MKENGA KABWE
MSEMAJI WA FAMILIA.

MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV NDANI YA ENEO LA CUSTOM, BAGAMOYO MKOANI PWANI

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AWAHIMIZA WATANZANIA KUUPENDA UTAMADUNI WAO

$
0
0
 Wadau wa utamaduni wakicheza bao
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kushoto akipokea picha ya Rais John Pombe Magufuli kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Bi. Lilly Beleko iliyochorwa na msanii wa Kitanzania Bw.Furaha Mwakitalu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana
Baadhi Ya wasanii wakionyesha umahiri wao wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea na wadau mbalimbali wa Sanaa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Picha na Benjamin Sawe

HOSPITALI YA SEKOUTOURE YANUFAIKA NA MSAADA WA MASHINE ZA KUSAIDIA WATOTO NJITI TOKA VODACOM FOUNDATION TANZANIA

$
0
0
 Mwanzilishi wa Doris Mollel Foundation,Doris Mollel(kushoto)Mkurugenzii wa Jembe Media pamoja na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Tanzania,Renatus Rwehikiza(katikati)wakimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela kwa niaba ya hospitali ya Sekoutoure(wapili kushoto)mashine ya kutoa uchafu(Manual Suction Machine)kwa watoto waliozaliwa Njiti zilizotolewa msaada hospitalini hapo na Vodacom Foundation Tanzania kupitia Doris Mollel Foundation leo,Msaada huo umegharimu shilingi Milioni 30.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela(wapili kushoto)akipatiwa maelekezo na Afisa muuguzi msaidizi wa wodi ya wazazi wa hospitali ya Sekoutoure mkoani humo,Rukia Setembo jinsi ya matumizi ya mashine ya kusaidia watoto Njiti kupumua(Oxygen Concentrator)zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation Tanzania kupitia Doris Mollel Foundation leo,Wengine katika picha kushoto,Doris Mollel,Renatus Rwehikiza na Sebasian Ndege,Msaada huo umegharimu shilingi Milioni 30.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela(wapili kushoto)pamoja na Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania,Renatus Rwehikiza(kushoto)wakimkabidhi mkazi wa mwanza zawadi ya kanga,Rehema Kamugisha,katika hospitali ya Sekoutoure mkoani humo mara baada ya kupokea msaada wa mashine za kusaidia watoto Njiti kupumulia wenye thamani ya shilingi milioni 30,Uliotolewa na na Vodacom Foundation Tanzania kupitia Doris Mollel Foundation leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela(kushoto)Doris Mollel,Sebasitian Ndege,wakimshuhudia Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kulia)akimkabidhi zawadi ya kanga,Rose Mwenda alielazwa katika hospitali ya Sekoutoure mkoani humo, mara baada ya kutoa msaada wa mashine za kusaidia watoto Njiti kupumulia wenye thamani ya shilingi milioni 30,Uliotolewa na na Vodacom Foundation Tanzania kupitia Doris Mollel Foundation leo.

WAZIRI NAPE ATOA NENO UZINDUZI WA WEMA SEPETU MOBILE APLICATION JIJINI DAR LEO.

$
0
0

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpa mkono wa pongezi msanii wa filamu hapa nchini,Wema Sepetu kwa kubuni huduma ya kisasa kabisa WEMA MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar 
 Mwanadada Wema Sepetu akifafanua jambo kwa  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar. 
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar
 Msanii mahiri wa filamu hapa nchini Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),jioni  ya leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali  yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Wema Sepetu amesema kuwa huu ni mwanzo mzuri na anaahidi kutumia huduma hiyo kutoa elimu kunufaisha jamii,kutangaza sanaa na utamaduni wetu,kuwa karibu na wapenzi ama mashabiki wake wote watakaokuwa wanahitaji kupata habari zake za kweli na uhakika.

Mfumo huo wa kipekee kabisa kwa mwanadada huyo,umezinduliwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye,mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote."Mfumo wangu huu ni wa kipekee na wa kwanza katika Afrika Mashariki kwa msanii wa tasnia ya Filamu,mfumo huu utaleta fursa nyingi sana zikiwemo ajira kwa vijana na wasanii wenzangu na kutambulika kirahisi"alisema Wema Sepetu.

Kujua mafanikio na Umuhimu wa kazi za Usanii Tanzania,huduma ya Wema Sepetu Mobile ni rahisi na ya uhakika,unatuma neno WEMA kwenda 15404,tayari unakuwa umeishajiunga na utaanza kupokea taarifa na habari za Wema sepetu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno,picha na video kutegemeana na aina ya simu yako unayotumia.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpongeza mwanadada Wema Sepetu kwa kubuni mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote na pia utamsaidia kumuingizia kipato na kuweza kuisaidia jamii inayomzunguka kwa namna moja ama nyingine.


Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile,Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION
 Meneja wa Biashara  wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo
 Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali kwa Wema Sepetu namna huduma hiyo inavyoweza kufanya kazi.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

TIBA ASILIA YA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME

$
0
0
Je wewe ni mwanaume unayesumbuliwa na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguivu za kiume lililo sababishwa na athari za kujichua kwa muda mrefu?

Unahitaji tiba ya uhakika ya tatizo lako ? Kama jibu ni NDIO basi hii ni HABARI NJEMA SANA KWAKO.

NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC ni duka linalo uza dawa mbalimbali za asili.

Tunayo dawa asilia iitwayo JIKO ambayo inatibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume ndani ya siku thelathini.

Dawa hii ni ya asilia kabisa (Pure Herbal ) ambayo haijachanganywa na kemikali yoyote ya viwandani na IMETHIBITISHWA NA MKEMIA MKUU WA  SERIKALI.

Dawa hii inapatikana kwa gharama ya SHILINGI ELFU THEMANINI ( Tshs.80,000/=) TU ZA KITANZANIA.

Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA.

Kwa wateja waliopo jijini Dar Es Salaam, wasio weza kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ), kwa  wateja wa mikoani na nchi jirani watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi, kwa wateja waliopo Zanzibar watatumiwa dawa kwa njia ya boti na kwa wateja waliopo ughaibuni watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.
Kwa mahitaji ya dawa ya JIKO, wasiliana nasi kwa simu namba 0766 53 83 84. Kufahamu jinsi suala la kujichua linavyo sababisha tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume na jinsi dawa ya Jiko inavyo fanya kazi ya kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, tembelea; http://www.neemaherbalist.com/2015/07/ijue-sayansi-ya-mfumo-wa-nguvu-za-kiume.html

RC KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA ZIARA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Nsere .
Chanzo cha Maji cha Nsere ambacho kiwango cha maji kinatajwa kushuka kutoka lita za ujazo Milioni 12 hadi Milioni 9.5.
Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadick akitembelea maeneo ya chanzo hicho.
Mkuu wa Mkoa Said Mecky Sadick na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri .

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 23

BENKI YA CRDB YAFANYA MKUTANO MKUU WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

$
0
0

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akihutubia mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICC Arusha. 
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akijibu maswali ya wanahisa.

Wanahisa wakiwa katika mkuano.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images