Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 121 | 122 | (Page 123) | 124 | 125 | .... | 3282 | newer

  0 0


   Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau akizungumza wakati wa Mkutano wa 39 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika katika Hotel ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Mzee Mfaume.
   Meneja Kiongozi, Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Eunice Chiume (kuli), akifuatilia mada wakati wa mkutano huo.
  Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, wakati wa Mkutano wa 39 wa Baraza Kuu la wafanyakazi uliofanyika mjini Bagamoya juzi. Kulia ni Mkurugenzi Rasilimari Watu wa NSSF, Chiku Matesa.

  0 0

  Rais Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe. Andry Rajoelina aliyewasili jioni ya leo Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini,katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU


  0 0

  Leo ni hepi besdei ya kuzaliwa Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Shyrose Bhanji. Anamshukuru Mola kwa kumfikisha umri huo na hapo alipo. Anaishukuru pia familia yake, ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa naye katika shida na raha. Anasema anawapenda wote

  0 0

  Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kupitia Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA-ISP) imekabidhi vitabu vinavyohusiana na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini.
  Vitabu hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira katika kujenga uwezo kwa wadau kuweza kuelewa na kutunza mazingira. Ofisi kwa kupitia programu hii itaendelea kushiriana na wadau mbalimbali kuelimisha umma dhana zima ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.
   Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu hivyo kwa Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Misitu na Uhifadhi ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Prof. Yonika M. Nganga.

   Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Idrisa Kikula (katikati), kulia ni Prof. Kinabo akishuhudia.

   Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kulia) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Naibu Mrajisi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijini cha Dodoma, Prof. Innocent J.E Zilihona.


  Hapa akikabidhi baadhi ya vitabu hivyo kwa  Kaimu Makamu Mkuu wa Mafunzo, ndugu Edwin Lyanda wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa. Aidha vitabu vingine vilikabidhiwa kwa Vyuo Vikuu vya St. John’s, Dodoma, Chuo Kikuu cha Kiislamu, Morogoro na Chuo Kikuu cha St. Augustine Tawi la Morogoro (Jordan University)

  0 0
 • 05/03/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Waasisi wa Hip Hop Bongo Kwanza Unite a.k.a KU wanakupa 'Mimi Msafiri'

  0 0

  Ankal akiwa na Dkt Licky Abdallah na mtangazaji Chacha Maginga wa TVT (siku hizi TBC1) wakati wa uchambuzi wa mechi za Kombe la Ulaya (UEFA Championship) kwenye stesheni hiyo mwaka 2004 zilizofanyika Ureno (Portugal).
  Euro 2004, kama ilivyojulikana, ilikuwa michuano ya 12 kwa timu za Taifa za soka za wanaume za Ulaya zilishindana, na kwa mara ya kwanza ilifanyika Ureno toka Juni 12 hadi Julai 4 katika miji minane tofauti ya Aveiro, Braga, Coimbra, Guimarães, Faro/Loulé, Leiria, Lisbon na Porto.

  Jumla ya timu 16 ilishiriki katika michuano hiyo iliyoshuhudia Ujerumani, Spain na Italy wakiondolewa katika hatua za makundi, ambapo bingwa mtetezi, Ufaransa, aliondolewa na Ugiriki katika robo fainali,na wenyeji Ureno wakazinduka baada ya kufungwa kwenye mchezo wa ufunguzi na kufika fainali, kwa kuwafunga Uingereza na Netherlands.

  Mwaka huo kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa fainali ikizikutanisha timu zilizofungua dimba (wenyeji Ureno na Ugiriki), ambapo Uguriki walishinda na kushangaza wengi kwani waliwahi kufuzu mara mbili tu katika michuano mikubwa – Euro 1980 na kombe la dunia mwaka 1994. Na ushindi wao katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ureno ulikuwa wa kwanza katika michezo yote ya fainali waliyowahi kucheza.


  0 0


  Mzee Alfred Tandau Enzi ya uhai wake

  Uwezo Tandau na Andrew (K.P)Tandau waishio DMV wanawakaribisha kwenye misa ya mpendwa baba yao, marehemu Mzee Alfred Tandau itakayofanyika kesho Jumapili May 5, 2013 kuanzia saa 7 mchana  address ni 
  6513 Queens Chapel Rd, 
  Hyattsville, MD 20782 
  Baada ya misa kutakuwa na chakula cha pamoja na kuwapa pole wafiwa. Nyumbani kwa wafiwa hapa Maryland kwa address hii:
  17 Gas Light Court, 
  Gaitherburg, Md 20879.
  Kwa maelezo zaidi pia unaweza kupiga simu kupitia number hizi,
  Andrew Tandau 
  # 240 421 8392. 
  Uwezo Tandau
   #240 476 0094. 
  Jacqueline Korassa
   # 240 706 6831.
  Tafadhali zingatia muda na upatapo taarifa hii usiache kumtaarifu mwenzio.
  Bwana alitoa, Bwana ametwaa na juna lake lihimidiwe, Amin

  0 0


  First-ever event celebrating local and locally inspired fashion design in Zanzibar set to premiere.

  The  all-new Fashion Week Zanzibar will take over Zanzibar in a celebration of local fashion and unique East African design. The new initiative is dedicated to showcasing fashion created in or inspired by the beautiful island of Zanzibar, Tanzania. 

  The island’s homegrown fashion industry has been developing in exciting new ways in recent years. One-of-a-kind designs pulling from the varied influences of Zanzibari culture and island life, mixed with the brightly coloured patterns of kanga and kitenge, create a strong sense of place and culture in the local fashion industry.  

  The event is founded and organized by photographer and filmmaker Javed Jafferji, internationally renowned designer Farouque Abdela, and budding photographer Adnan Abbas. “We decided to celebrate Zanzibar’s up-and-coming fashion and create a festival dedicated to our one-of-a-kind fashion flavor,” says Jafferji. “The decision was made on the spur of the moment and the whirlwind hasn’t stopped since.” 

   “We hope to encourage the local fashion industry and empower young designers,” says Abdela. As a part of the community, organizers say the event will continue to grow and shape the potential of this promising industry in Zanzibar’s future. 
  For up-to-the-minute information and updates, please visit www.fashionweekzanzibar.com or on Face book see the following link 


  0 0

  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na baraza lake la kwanza la mawaziri baada ya kuliapisha 

  0 0


  0 0

  Dun and Bradstreet Credit Bureau, Ofisi ya kwanza yenye kibali cha kutunza kumbukumbu za Mikopo Tanzania, Dar es Salaam imepanga kukutana na kushauriana na watendaji wakuu wa Benki zote Tanzania katika semina iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt-Kilimanjaro siku ya tarehe 3/05/2013.

  Uwepo wa Dun and Bradstreet Credit Bureau nchini Tanzania unategemewa kwa kiwango kikubwa kuimarisha na kujenga daraja kati ya Benki ya Tanzania na Sekta za Benki.

  Warsha hii inaambatana na utambulisho na ufunguzi wa ofisi ya Dun&Bradstreet Credit Bureau nchini Tanzania, semina hii inalenga kukuza mahusiano kati ya ofisi hii, mabenki na taasisi zote za kifedha ambazo zimeleta mchango muhimu katika kuhakikisha kwamba wanapata ofisi ya kudhibiti kumbukumbu za mikopo yenye viwango vya kimataifa.

  Kwa mujibu wa Bwn. Miguel Llenas – Mkurugenzi Mkuu wa Dun & Bradstreet Credit  “Lengo kuu ni kujenga taasisi itakayoweza kusimamia jukumu la kuinua uchumi wa Tanzania na utimamu katika taasisi za fedha na Benki. Kwa maana hii, semina hii itaeleza kwa kina jinsi ya kusaidia benki na taasisi za fedha nchini Tanzania juu ya kutathimini na kuboresha maombi ya mikopo/mkopo kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanakuwa na habari na utambuzi juu ya waombaji wa mikopo katika mabenki na taasisi zao.”

  Pia, katika semina hii, meneja mkuu wa Dun & Bradstreet Credit Bureau  - Adebowale Atobatele amesema “Tumeangazia mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania kuwa washirika wetu. Fursa pekee ya kukutana, kusikilizana na kushauriana na washirika wetu katika hili semina. Tunahitaji kuwatumikia wao na ni muhimu kuelewa changamoto husika wanazokumbana nazo katika biashara hii ya ukopeshaji. Tunaamini ufumbuzi wa kuendeleza maslahi bora ya mabenki, sekta za fedha na uchumi watanzania, na watanzania kiujumla ni kwa kupata michango mbalimbali kutoka katika benki na taasisi za fedha ambazo zitakutanisha taarifa za mikopo zitakazotambuliwa katika kiwango cha kimataifa”.

  Kwa muda mrefu, mabenki na taasisi za fedha nchini Tanzania zimekuwa zikiweka kumbukumbu juu ya uwiano wa mikopo isiyofanya vizuri katika vitabu vyao kiasi inafikia kiwango cha kusamehe madeni hayo na kurekodi faida ndogo. Uanzilishi wa taasisi ya kutunza kumbukumbu za mikopo katika mifumo ya kibenki, taasisi za kifedha na wateja, itasaidia kuleta mwangaza katika siku zijazo.

  Semina iliyoandaliwa na Dun & Bradstreet Credit Bureau inafuatiwa na mafanikio ya shughuli zake katika ofisi zilizopo Ghana ambapo soko lake limekuwa kubwa kwa uwepo wa D&B nchini Ghana.

  Soma zaidi kuhusu D&B hapa www.dnbcb.com

  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Brandstreet Credit Bureau Adebowale Atobatele akiongea wakati wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha uliofanyika Dar es Salaam May 3 2013. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Miguel Llenas.

   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Miguel Llenas akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam 03 May 2013 wakati wa semina ya wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha. Kushoto ni kuhusu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Adebowale Atobatele.

  0 0


  0 0

  Jakaya+Kikwete+Doug+Pitt+Named+Goodwill+Ambassador+VYq30mnJnaol
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza wanahabari ,wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini kwa kuadhimisha Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani (World Press Freedom Day) leo, Ijumaa, Mei 3, akiwahakikishia kuwa Serikali yake itaendelea kukuza, kulea, kulinda na kutetea Uhuru wa Habari ulioshamiri kwa kiwango cha juu kabisa nchini kwa sasa.

  Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake na yeye binafsi, kama mdau wa habari, wataendeleza kuelekeza nguvu kubwa katika kupanua Uhuru wa Habari kwa sababu uhuru huo ni kigezo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania na katika kujenga na kupanua demokrasia nchini.

  Katika salamu zake kwa wanahabari, wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini ambayo inasherehekea Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunia kitaifa mjini Arusha leo katika shughuli zilizoandaliwa na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania, Rais Kikwete amesema:


  0 0

   Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho,ni miongozi mwa viongozi waliohudhuria katika sherehe ya kuwaapisha wajumbe wa Tume ya
  Uchaguzi pamoja na Mwenyekiti wake Ikulu Mjini Zanzibar leo.
   Waziri wa Nchoo Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,pia walihudhuria katika sherehe ya kuwaapisha wajumbe wa Tume ya Uchaguzi pamoja na Mwenyekiti wake Ikulu Mjini Zanzibar leo
    Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,akisalimiana na Viongozi waliohudhuria katika sherehe ya kuwaapisha wajumbe wa Tume ya Uchaguzi pamoja na Mwenyekiti wake Ikulu Mjini Zanzibar leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Jecha Salim Jecha,kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi. 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Balozi Omar Ramadhan Mapuri, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Nassor Khamis Mohamed, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Salmin Senga Salmin, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Dkt.Idris Muslim Hija, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Ayoub Bakari Hamad, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Jaji Abdulhakim Ameir Issa, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Haji Ramadhan Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na viongozi wenginge wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wakuu,pia wakiwemo Mwenyekiti wa  Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,(wa pili kushoto)na wajumbe wa tume hiyo,akiwemo  Mkuu wa Mkoa kusini,(waliosimama kulia)baada ya hafla ya kiapo Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha zote na Ramadhani Othman Abdallah wa Ikulu, Zanzibar

  0 0

  Na Grace Michael 
  WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amesema ni wakati muafaka sasa kwa kuwa na chombo kimoja kitakachokabidhiwa jukumu la kusimamia bima ya afya kwa Watanzania badala ya kushughulikiwa na taasisi nyingi kama ilivyo hivi sasa. 
   Dk. Mwinyi ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua bodi mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo ameitaka bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kuanzisha mjadala wa kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia huduma za bima ya afya ili kuwafikia watanzania wote katika utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua.
   “Hadi sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeonesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia huduma za afya hali inayonishawishi kuwa na chombo kimoja,” alisema Dk. Mwinyi. Alisema kuwa Serikali inatambua wingi wa mifumo na taasisi zinazojihusisha na huduma za bima ya afya na lengo lililopo ni kuhuishwa ili kuimarisha mfumo wa uchangiaji wa huduma za afya ambapo kwa sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekasimiwa mamlaka ya kuendesha Mfuko wa Afya ya Jamii utakaoangalia namna nzuri ya kupanua wigo. 
   Akizungumzia mchango wa NHIF katika uboreshaji wa huduma za matibabu vituoni, alisema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Mfuko huo angependa kuona Mfuko ukijikita katika uwekezaji unaolenga uboreshaji wa huduma za afya na si vinginevyo, hivyo akaiagiza bodi mpya kuhakikisha inaagalia na kuurejea upya utaratibu wa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ili watoa huduma wachangamkie zaidi fursa hiyo. 
   Dk. Mwinyi pia hakusita kuzungumzia mahusiano mazuri ya kazi baina ya bodi, menejimenti na watumishi wa Mfuko ambapo alisema kuwa Mfuko mpaka sasa umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kujenga misingi bora ya uhusiano mwema wa kazi miongoni mwa watendaji wake ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa na taasisi zingine hivyo akasisitiza hali hiyo kuendelezwa ili kuongeza zaidi ufanisi wa utoaji huduma. 
   Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya, Regina Kikuli aliiambia bodi hiyo kuwa jukumu walilokabidhiwa ni kubwa kwa kuwa linagusa moja kwa moja afya za wanachama na watanzania kwa ujumla hivyo ni vyema bodi ikaliona hilo na kuhakikisha inakuja na mbinu mpya za kuhakikisha inaimarisha na kuboresha Mfuko huo ili uweze kufikisha malengo yake ya kuwahudumia watanzania wote. 
   Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo aliahidi kuwa kazi aliyokabidhiwa kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wataifanya kwa uaminifu mkubwa na kwa kutumia uwezo wao wote ili kuhakikisha Mfuko huo unawasaidia watanzania wote. 
   Akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba alisema kuwa moja ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Mfuko kwa sasa ni watanzania wengi kutambua umuhimu wa bima ya afya hivyo Mfuko unafanya kila jitihada ya kuhakikisha inafikia watanzania wengi zaidi na kukabiliana na changamoto zote zilizopo ili lengo la afya bora kwa wote liweze kufikiwa. 
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdoe alipowasili kuindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa NHIF, leo kwenye Hoteli ya Courty Yard, Sea View, Dar es Salaam. Wengine ni Mwenyekiti mpya wabodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina Kikoli.
   Wakurugenzi wa NHIF, wakipiga makofi wakati Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mwinyi alipokuwa akiingia kuzindua bodi hiyo.
  Dk. Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mchumo.
   Baadhi ya mameneja wa Mikoa wa NHIF, na maofisa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo.
   Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Mchumo (kushoto) akimshukuru Waziri, Dk. Mwinyi kwa kuzindua bodi hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Humba.
   Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa maelezo kuhusu utendaji wa mfuko huo,  Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli
   Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo akuhutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (wa nne kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya NHIF. Kutoka kushoto ni Mwanaidi Mtanda,Donnan Mmbando, Mwenyekiti Balozi Ali Mchumo, Mohammed  Hashim, Charles Kajege, Dk. Ali Mohammed na Naibu Katibu Mkuu wa wa wizara hiyo, Regina Kikoli.Waliosimama ni Mkurugenzi Mkuu, Emmanuel Humba (kulia na Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdoe.
   Waziri Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa NHIF.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
   Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
  Add caption

  Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
  Dk.Mwinyi akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (kushoto) pamoja na Mjumbe wa bodi hiyo, Mohammed Hashim.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli 9kulia) akiagana na Balozi Ali Mchumo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.

  0 0

  Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge akizungumza na waalikwa kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa habari Duniani iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi utakao kuwa ukisaidia waandishi wa habari pindi wapatapo matatizo wakiwa kazini. Kushoto ni Mzee Kassim Mapili wa Mjomba waliosherehesha usiku huo kwa buradani ya aina yake.(Picha na Dewji Blog).
  Baadhi ya Wanahabari walioshiriki kwenye Gala Dinner ya siku ya Uhuru wa Habari iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi kusaidia waandishi wa habari ambao wamepata matatizo wakiwa kazini.
  Blogger Pamela Mollel (katikati) wa Jamii Blog ya jijini Arusha akibadilishana wanahabari wenzake Tonia Kasoni( kushoto) wa Radio 5 pamoja na Mhariri wa Sibuka TV wakati wa hafla hiyo.
  Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi na mtoto wa mwisho wa marehemu wakati wa uzinduzi wa Mwangosi Fund utakaokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi wa Tuzo hizo atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
  Mzee Kassim Mapili wa Mjomba Band akikung'uta gitaa wakati akipiga wimbo wa Mbaraka Mwishe" Njoo mjionee Morogoro"....wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za mfuko wa Daudi Mwangosi zilizoenda sambamba na uzinduzi wa mfuko huo katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
  Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiimba nyimbo za zamani pamoja na Mjomba Band inayoongozwa na Mzee Kassim Mapili na Mrisho Mpoto.
  Bi. Leila Sheikh akisakata Rhumba la enzi hizo sambamba na Mzee Makwaiya Wakuhenga wakati Gala Dinner katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani kwenye Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan.
  Wanahabari kutoka Zanzibar nao walijumika na wenzao wa Bara kutoka nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Gala Dinner.
  Wakongwe katika tasnia ya habari hapa nchini akiwemo Mzee Salim Salim na Mzee Hamza Kasongo na wenzao wakibadilishana mawazo.
  Mgeni rasmi kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani ulioenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu kilichoandaliwa na Media Council Tanzania (MCT) pamoja na Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa salamu za Rais Kikwete za Pongezi kwa wanahabari Tanzania kwa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambapo Serikali imeahidi kushirikiana na wanahabari bega kwa bega kwa mustakabali wa kuboresha tasnia hiyo.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizindua Ripoti ya Habari hapa nchini ya mwaka 2012 iliyoandaliwa na Media Council of Tanzania (MCT) aliyeshika kitabu hicho ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Taasisi ya Media Council of Tanzania (MCT) Bi. Alakok Mayombo na Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa na MC wa Gala Dinner hiyo Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji.
  Sasa imezinduliwa rasmi.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene, Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera na mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland kwa pamoja wakizuindua Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika kilichoandaliwa na MISA katika Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akionyesha kitabu "SO THIS IS DEMOCRACY" mara baada ya kukizindua rasmi.
  Usia Nkhoma wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na mwanahabari mwenzake wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.
  Mzee Hamza Kasongo akiendesha Harambee kwa wanahabari na wahariri kwa ajili ya kuchangisha mfuko wa Mwangosi utakaokuwa ukisaidia wanahabari pindi wapatapo matatizo kazini.
  Stella Vuzo wa UNIC akitangaza ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kutoa Dola 300 kuchangia Mfuko wa Mwangosi.
  Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera akitoa ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kuchangia Laki moja huku Misa-Tan imetoa ahadi ya Shilingi Milioni moja kuchangia mfuko wa Mwangosi uliozinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
  Mwakilishi kutoka BBC ambao nao pia waliguswa na kuchangia mfuko wa Mwangosi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.
  Mwendeshaji wa Harambee hiyo Mzee Hamza Kasongo akitangaza kiasi cha fedha zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni 19 wakati wa Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akikabidhi fedha taslim shilingi laki 5 zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo kwa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dun & Brandstreet Credit Bureau Limited Adebowale Atobatele akiongea wakati wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha uliofanyika Dar es Salaam May 3 2013. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited Miguel Llenas.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia warsha hiyo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited Miguel Llenas akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam Aprili 3 2013 wakati wa semina ya wa semina ya maofisa wa benki na taasis za fedha. Kushoto ni kuhusu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Adebowale Atobatele.

  0 0

   Salaam Ankal,

  Leo nimeudhiwa sana na Dereva wa Lori hili,aliekuwa ameegesha vibaya kwani alikuwa ameziba njia tena kwa makusudi kabisa,njia ambayo inaunganisha mitaa.halafu nilipomfata na kumuomba aegeshe vyema lori lake hilo ili sisi wengine tupite kwa kua njia yenyewe ni hiyo hiyo tu,alinijibu jeuri na kunitaka nifanye lolote lakini yeye hatoi gari hapo kwani ndivyo alivyoamua kupaki.kiukweli alinikera sana na kauli zake hizo,kwani alikuwa amefanya kosa kuziba njia halafu anajibu jeuri kana kwamba hii njia ni ya kwake peke yake au familia yao.

  Mdau wa Globu ya Jamii.
   Hebu angalieni jamaa alivyoweka gari.


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Waziri wa Zamani wa Kazi ,Marehemu Balozi Alfred Tandau wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Alfred Tandau ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini alifariki tarehe 30 Mwezi Aprili wiki iliyopita.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Mau katika kaburi la Marehemu Balozi Afred Tandau wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.Picha na Ikulu)

  0 0

  Mihayo Wilmore, the CEO of UhuruOne with Steve Gannon, CEO of Serengeti Breweries Ltd, at the launch of the UK Alumni in Tanzania Network's Leadership series at the British Council.

  Around 40 British and Tanzanian alumni from UK universities met at the British Council in Dar-esSalaam on 30 April for the launch of a series of Leadership events. 

  The presentations, being organised by the UK Alumni in Tanzania (UKAT) Network, aim to inspire and inform the members about effective leadership. Steven Gannon, CEO of Serengeti Breweries, together with Mihayo Wilmore, CEO of UhuruOne, shared their unique insights in response to the question ‘What is it really like to be a CEO?’ 

  The speakers provided fascinating responses which reflected on how their family background, educational achievements and professional development had influenced their leadership journeys. They also discussed how they mobilise and inspire others to achieve success in their role as a CEO. 

  The presentations were followed by a networking reception sponsored by Serengeti Breweries where members had the chance to meet and mingle with the guest speakers. Leeds University graduate Evarist Mganga, a UKAT management team member, commented, “These CEOs are great role models to young professionals in our network who wish to assume leadership roles in a wide variety of sectors.” 

   UKAT was founded in 2012 for UK alumni across Tanzania to foster support and mutual success through a range of activities. The organisation promotes UKAT’s events on Twitter @UKATz and the tzukalmni.co.tz website. The network warmly welcomes new members to join and be involved in the exciting calendar of upcoming events.

older | 1 | .... | 121 | 122 | (Page 123) | 124 | 125 | .... | 3282 | newer