Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1227 | 1228 | (Page 1229) | 1230 | 1231 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakati alipowasili kuzungumza na wafanyabiashara wa nyama katika Machinjio ya Vingunguti kabla ya kuifungua rasmi jana. Katikati ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti.

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akielekeza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi.
  Taswira ya choo cha kisasa kilichojengwa kwenye machinjio hiyo.
  Wafanyabiashara katika machinjio hiyo wakimsikiliza Makonda (hayupo pichani)
  Mwonekano wa machinjio hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati.

  0 0

   Mh. Charles Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  Yamoto Band wakishirikiana na Wadogo zao Salamu TMK wameandaa wimbo huu wa kuhamasisha usafi katika jiji la Dar es Salaam kufatia kauli ya Rais John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda.

  0 0

  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


  Simu ya Upepo   : “N G O M E”                Makao Makuu ya Jeshi,

  Simu ya Mdomo : DSM  22150463            Sanduku la Posta 9203,

  Telex                     : 41051                           DAR ESSALAAM,21  Mei, 2016

  Tele Fax                : 2153426

  Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

  Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz


  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya ufunguzi wa mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF CUP) ambayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 24 Mei 2016 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye.

   Mashindano haya yalianzishwa mwaka 2014, awali JWTZ lilikuwa likiteua wanamichezo wa kushiriki michezo ya kimataifa kupitia timu teule za Jeshi hali iliyopelekea kutovumbuliwa kwa vipaji vipya katika michezo, ikaonekana upo umuhimu wa kubadili mfumo wa uteuzi. Hivyo kuanzisha mashindano ya Kombe la  Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) ambayo huanzia ngazi za vikosi hadi kufikia ngazi za brigedi.

  lengo la mashindano haya ni kudumisha mshikamano, kuvumbua na kukuza vipaji, pia mashindano hayo yatatumika katika kuteua kombaini ya timu ya JWTZ itakayoliwakilisha Jeshi na Taifa kwa ujumla katika mashindano ya michezo ya majeshi na utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi wa nane mwaka huu.

  Kauli Mbiu ya mashindano haya ni “Michezo ni Ulinzi na Umoja Daima”

  Timu zinazoshiriki mashindano haya ni Ngome (Makao Makuu JWTZ), Kamandi ya Jeshi la nchi kavu ikiwakilishwa na timu za Tembo, Faru, Nyuki, Mbuni na Chui, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).

  Mashindano haya yatahusisha michezo ifuatayo, Mpira wa miguu kwa wanaume, Mpira wa kikapu kwa  wanaume, Mpira wa mikono kwa wanaume, Mpira wa pete kwa wanawake na Mbio za nyika kwa wanaume na wanawake.Michezo hii itafanyika katika viwanja vya Twalipo vilivyopo Mgulani pamoja na uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. 
  Mashindano haya yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 06 Juni 2016. Mgeni rasmi katika ufungwaji wa mashindano haya anatarajiwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange.


  Wananchi wote wanakaribishwa. Hakuna kiingilio.

    
  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


  Kwa Mawasiliano zaidi: 0756716085/ 0713506757


  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu 
  ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .
  Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.
  Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.
  Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.
  Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.
  Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
  Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Mussa akizungumza wakati wa kuiaga timu ya Kitaysce.
  Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
  Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimorial. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Watumishi wa Serikali 210 wameidhinishiwa mikopo nyumba yenye thamani shilingi bilioni 2.3 baada ya kukidhi vigezo vya Bodi ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba za Watumishi wa Serikali.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (pichani) wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

  Alisema kuwa Serikli imekamilisha uhakiki wa maombi mapya 191  ya watumishi wa umma waliomba mkopo wa nyumba katika maeneo mbali.
  Mhe. Lukuwi aliongeza kuwa kati ya maombi hayo watumishi 181 yamekidhi vigezo vya mfuko huo na yanatarajiwa kuidhimishwa mwishoni mwa mwezi huu.
  Aidha , alisema kuwa Serikali kupitia Watumishi Housing Company (WHC) imeanza kujenga nyumba za kuuza kwa watumishi wa umma katika mikoa ya  Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga  na Mwanza
  Mhe. Lukuvi alisema kuwa watumishi wa umma wanaotaka kununua nyumba hizo wanawaweza kupata mikopo yenye mashrti nafuu kupitia Benki za Azania , CRDB, NMB, BoA na Exim zilizoingia makubaliano na Watumishi Housing Company wanaojenga nyumba kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini.


  0 0

  Kampuni ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo ambayo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100. Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kushiriki bahati nasibu inayoendeshwa kitaalamu na inayowezesha washindi kujishindia donge nono na kubadilisha maisha yao.  
  “Zawadi ya milioni 100 sio ndogo itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi na kushiriki katika mchezo huu. Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.
   “Tiketi za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi wengi kushinda”Alisema. 
   Alisema mbali na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 1,000.
   Mwenyekiti wa kampuni ya  Gidani  ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Profesa Bongani Aug Khumalo,akitoa maelekezo ya mchezo huo kwa waandfishi wa habari na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi (kulia ) ni Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba na Katikati ni Meneja mradi wa Kampuni hiyo,Brett Smith.
   Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akionyesha mashine za bahati nasibu zinavyofanya kazi
   Meneja mradi wa  Kampuni ya Gidani Brett Smith akionyesha tiketi zinavyokatwa kwa mashine
   Baadhi ya wafanyakazi ya Gidani wakiwa ofisini
  Mkurugenzi Mkuu wa  bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akipozi na badhi ya wadau baada ya hafla hiyo

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
  Tanzania (TFF) Jamal Malinzi
  PAZIA LIGI KUU YA VODACOM KUFUNGWA KESHO
  Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16 kutinga katika viwanja vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16.
   Michezo itakayopigwa kesho ni pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini

  AIRTEL TANZANIA YAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO SOKA LA VIJANA
  Kampuni ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
   Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. “Naamini ya kwamba kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa kupata matokeo mazuri.”
  Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini

  0 0

  Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea kituo hicho Mei 19, 2016.
  Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji (kulia)  akikikabidhi taarifa hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima, mara baada ya kuisoma.
  Mmoja wa Vijana waliokuwa wameathiriwa na Madawa ya Kulevya ambaye sasa amerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kupatiwa tiba aliefahamika kwa jina la Abdullatif, akisoma ngonjera aliyoiandaa mwenyewe yenye ujumbe wa kuwataka vijana wengine kuachana kabisa na matumizi ya madawa ya kulevya, kwani yanaathari kubwa kwao.
  Abdullatif akimtabithi Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima ngonjera yake hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  SIMU.TV:  Zanzibar yatuma salamu za rambirambi nchini Oman kufuatia kifo cha balozi Alli Abdallah Rashid aliyekuwa balozi wa Oman nchini; https://youtu.be/EkPxMtEvaXM 
  SIMU.TV:  Serikali ya Zanzibar imeeleza kuwa ina matarajio makubwa na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP kwatokana na kuwa ofisi hiyo inawagusa wananchi moja kwa moja; https://youtu.be/n_DVLTXeiJk
   SIMU.TV:  Serikali yaweka wazi mkakati wake wa kuongeza wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali ili kuweza kuwainua kiuchumi wafugaji na wakulima;https://youtu.be/Ij2E9SdPoDo
   SIMU.TV:  Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar yapokea msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine ya kusaidia kupumua kwa wodi ya wazazi;https://youtu.be/kOBVklfFAFg
   SIMU.TV:  Mamlaka ya mapato Zanzibar ZRB yaanzisha utaratibu wa kodi ya zuio ili kubaini viwango vya mauzo ya wafanyabiashara; https://youtu.be/TIktShGqt4w
   SIMU.TV:  Tatizo la msongamano mkubwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Rorya  mkoani Mara lapatiwa usingizi baada ya kupata msaada; https://youtu.be/Isd_TEsuxTs
   SIMU.TV:  Watanzania waungana na kufanya ibada kwaajili ya kumbukumbu ya wahanga wa ajali ya meli ya Mv Bukoba. https://youtu.be/PsvQE3y5PDw
   SIMU.TV:  Bodi  ya ligi kuu na TFF kufanya marekebisho ya mapungufu katika viwanja vya soka nchini baada ya ligi kuu kumalizika; https://youtu.be/jXWceOuvKlY 
   SIMU.TV:  Jeshi la kujenga taifa JKT mgulani limepokea msaada wa ulingo wa ngumi wenye thamani ya Sh.Mil.22  ili kuendeleza mchezo huo nchini; https://youtu.be/hxOZ4JYlbRg  


  0 0

  Mwanafunzi Benadetha Msigwa amepata upofu akiwa chuo, hivyo anapmba msaada pesa ili akatibiwe macho na kuweza kurudi katika hali yake, inahitaji kama milion 30 kwa yeyote atakaeguswa anaweza tuma chochote kupitia namba hizo hapo kwenye hicho kipeperushi.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  KIKOSI cha Mbeya City Fc  kesho jumapili kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo wa kufungia msimu  wa 2015/16 wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara dhidi ya wageni wao Ndanda Fc 'wana kuchele' kutoka mkoani Mtwara.

  Meneja  wa kikosi cha City, Geoffrey Katepa  amesema kuwa  nyota wote 18 wametayarishwa kwa ajili ya kuwakilisha  timu yao na wako kwenye hali nzuri na tayari kabisa kusaka ushindi.
  “Kama unavyoona  tumemaliza mazoezi  muda huu, yalikuwa ni mazoezi mepesi kuelekea  mchezo wa kesho kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwetu ni kushinda mchezo huo ili tumalize ligi kwa heshima, hatuna wasiwasi wowote tuko salama kwenye msimamo wa ligi, kumaliza kwa ushindi kutatuweka kwenye mapumziko mazuri  kwa matayarisho ya msimu mpya”, amesema Katepa.

  Kuhusu  majeruhi Katepa  alisema kuwa City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili aliye majeruhi kufuatia maumivu ya nyama za paja  yanayomkabili, pia  Temi Felix na Deo Julius  hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo.

  “Mkuu wa kitengo  chetu cha utabibu Dr Joshua kaseko, amenieleza asubuhi kuwa  tutawakosa wachezaji hao kutokana na majereha waliyonayo hii ina maana kuwa wataonekana uwanjani  wakati wa matayarisho ya msimu mpya, mwalimu tayari kashafanya utaratibu wa wale wataochukua nafasi zao hivyo tuna uhakika wa kuingia uwanjani na kikosi kilicho bora licha ya kuwakosa hao tutahakikisha ushindi unapatikana.

  0 0

  Na Zainab Nyamka

  AFISA ushirika wa manispaa ya Temeke, Martin Mwela amezindua mfuko wa akiba na mikopo unaotambulika kama KIUMA wenye lengo la kuinua wanachama katika kuwapatia mikopo ya riba nafuu huku akiwataka wanachama kuwa waaminifu kwenye urejeshaji wa mikopo.

  Akizindua ushirika huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bi Sophia Mjema, Mwela amesema kuwa ushirika huo unatikiwa kujiendeleza na kuwa na mshikamano kwani siku zote adui wa ushirika wowote ni mwanachama mwenyewe pale anaposhindwa kufanya marejesho kwa wakati na kufanya mfuko kukosa fedha za kujiendesha ikiwemo kuwapatia mikopo wanachama wengine.

  "Wanachama ndio mchawi mkubwa wa kufa kwa vyama kadhaa vya ushirika kutokana na kutokupeleka marejesho kwa wakati pamoja na kukifanya kushindwa kujiendesha ukiwemo wanachama wengine kutokupata mikopo kwa wakati,"amesema Mwela. Huku akiwataka kutokujiingiza kwenye mikopo ya Mifuko ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF, LAPF na PPF kwani inakuwa na riba kubwa sana ambapo watakuwa watumwa.

  Naye Mwenyekiti wa Mfuko huo wa Ushirika, Ally Pilimo amesema kuwa malengo yao ni kuja kufikia benki kwani wameanzia kikundi cha watu 10 na kwa sasa wapo zaidi ya 30 na tayari wameshatoa mikopo kwa robo ya wanachama wa kikundi hicho.

  "Ushirika wetu umekua kutoka kikundi cha watu 10 na kwa sasa tupo zaidi ya 30 na tumeshaweza kutoa mikopo kwa robo ya wanachama na wameweza kujiendeleza kiuchumi ikiwemo kufanya biashara mbalimbali,"amesema Pilimo.

  Baada ya uzinduzi huo Wanachama wa chama cha ushirika KIUMA wamekabidhiwa vitabu vyao ambavyo watavitumia kwa ajili ya kuweka akiba zao.
  Afisa ushirika Manispaa ya Temeke, Martin Mwela akitoa nasaha kwa wanachama wa Ushirika wa KIUMA wakati wa uzinduzi huo katika viwanja vya Mwembe Yanga leo.
  Afisa Ushirika Manispaa ya Temeke, Martin Mwela akikabidhi katiba na Cheti kwa katibu mkuu wa Ushirika wa KIUMA,Peter Daud wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirika huo.
  Wanachama ya ushirika wa KIUMA wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Ushirika Manispaa ya Temeke Martin Mwela katika uzinduzi wa Ushirika huo leo.

  0 0


  SHEKHE Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir pamoja amelaani vikali tukio la kinyama lililotokea Mei 17 mwaka huu katika Msikiti wa Ibanda Mkolani, Masjid Rahmaan mkoani Mwanza. 

  Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa  kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na hakivumiliki.

  Tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu na kusababisha mauaji ya waumini watatu wa Msikiti wa Ibanda Mkolani waliokuwa katika Ibada  miongoni mwao akiwa ni Imam wa Msikiti huo ikiwa na wengine kujeruhiwa.

  "Kwaniaba ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania(Bakwata) tunalaani vikali tukio hili pamoja na kuwataka Waislam wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Shekhe Zuberi.

  Amewaomba Waislam na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano wa hali na mali vyombo vya usalam ili hatimae kuwapata waharifu hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria.  Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, na kulaani kitendo cha mauaji ya watu wasio na hatia katika Msikiti huko Mkoani Mwanza. Kulia ni Msaidizi katika ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe, Ally Khamisi Ngeruko. na Kushoto ni Shekhe, Abuubakari Kharid.
   Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir (Mwenye kofia Nyeupe katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya waamini wa dini ya Kiislamu pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kulia) akimkabidhi moja ya dawati Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Salum Upunda ikiwa ni miongoni mwa msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kulia) akimkabidhi moja ya dawati Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Salum Upunda (kushoto) ikiwa ni miongoni mwa msaada wa madawati 50 kwa Shule ya Msingi Majimatitu yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala.Kikundi cha kwaya cha Shule ya Msingi Majimatitu kikiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule hiyo. Kikundi cha kwaya cha Shule ya Msingi Majimatitu kikiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule hiyo.Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu wakisoma risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu wakisoma risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto), Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto) akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia) akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
  Picha ya Pamoja.


  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) akioneshwa maeneo mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe, Mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kikazi leo Mei 21, 2016 Gerezani hapo(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Songwe, ACP. Laizack Mwaseba.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia moja ya shamba la alizeti katika Gereza la Kilimo Songwe.Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira(kushoto) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja kwa pamoja wakiangalia mazao ya mahindi katika Mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe walipotembelea Gereza hilo leo Mei 21, 2016.Mazao ya Mahindi yakiwa tayari yamevunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya kabla ya kupukuchuliwa kwenye mashine maalum.
   

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipiga mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipiga mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Chuo cha Habari Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.

  0 0


older | 1 | .... | 1227 | 1228 | (Page 1229) | 1230 | 1231 | .... | 3283 | newer