Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1226 | 1227 | (Page 1228) | 1229 | 1230 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Tiganya Vincent, Dodoma.

  Wakala wa Vipimo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakusudia kuanzisha  vituo maalum vya ununuzi wa mazao ya wakulima (buying centres) katika vitongoji nchi nzima ili kuondoa unyonyaji na ukandamizaji unaofanwa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni lini Serikali itasimamia sheria kuondoa unyonyaji unaofanywa na wachuuzi wakati wa kununua mazao ya wakulima.

  Alisema kuwa katika kutekeza hayo hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kusafirisha mazao ambayo yamefungashwa kinyume kinyume cha Sheria ya vipimo na kuongeza kuwa katika kusimamia jambo hilo vitaanzishwa vituo maalum vya ukaguzi bila kusabaisha usumbufu katika ufanyaji biashara.

  Mhe. Mwijage amewaagiza Maafisa Ugani walioko vijijini watumike kusimamia matumizi ya vipimo rasmi katika vituo hivyo na kutoa taarifa zote muhimu kwa Wakala wa Vipimo.

  Aidha ,alisema kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio Sheria ya Vipimo sura 340 ili kuondokana na unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.

  Alisema kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio ya Sheria hiyo ili kuweka mazingira mazuri kwa lengo la kumlinda muuzaji kwa kuwadhibiti manunuzi wanaotumia njia za udandanyifu wakati wanaponunua mazao ya wakulima.Mhe. Mwijage alisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho Serikali itawalisha mabadiliko hayo bungeni ili ifanyiwe marekebisho yanayostahili.

  Aidha , Waziri huyo alisema kuwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vipimo yanatarajia kufanywa , Wakala wa Vipimo imewasilisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ndogo(by laws)  ili ziweze kuwaongoza wakulima na wafanyabiashara kufungasha mazao.

  0 0  EAST AFRICAN COMMUNITY

  OFFICE OF THE FACILITATOR OF THE BURUNDI DIALOGUE
   
  Former President of the United Republic of Tanzania H.E. Benjamin William Mkapa who was appointed on March 2, 2016 by the Summit of the East African Community in Arusha, Tanzania has confirmed that the Burundi Dialogue will take place from 21 – 24 May 2016 in Arusha at the Arusha International Conference Centre.

  Preparations  for  the dialogue  are all  in their  different  advanced stages of  their completion. Invitations to the Government of Burundi, Former Presidents of Burundi, Political  Parties,  Civil Society  Organization,  Religious  Groups and some selected important political actors have all gone. So far the Office of the Facilitator has received confirmations for participations from over 63 entities.

  Delegates are expected to start arriving by today, and the majority will arrive tomorrow ready for the opening ceremony scheduled for Saturday, May 21st from 10am – 12 Noon. The opening ceremony will be attended by the Executive Secretary of the ICGLR, Special Envoys from the USA, Belgium, UK, EU, AU and the UN; and some Ambassadors and High  Commissioners  accredited to Tanzania. The Dialogue  is expected to conclude on Wednesday, 25th May, 2016 with the decision being reached on the agenda, venue and participation to the next dialogue.

  0 0

  Na Zainab Nyamka

  MASHINDANO ya Afrika kanda ya tano ya mpira wa Kikapu yamesogezwa mbele hadi Julai 19 kutokana na kukosa fedha za kuandaa mashindano hayo kwa sasa hadi pale bajeti ya serikali itakapopitisha mwaka mpya wa kifedha.

  Mwenyekiti wa mashindano na katibu mkuu msaidizi Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (BFT) Mwenze Kabinda amesema wamepokea taarifa hizo ila awali timu zimeshaanza kujiandaa kwa ajili ya michuano hiyo ya kanda ya tano Afrika.


  "Tumepokea barua kutoka kwa katibu mkuu wa Kanda ya tano Afrika kutoka nchini Misri ikisena kuwa michuano hiyo itasogea mbele hadi julai 19 na kumalizika Julai 24,"amesema Kabinda.

  Mashindano hayo yanakuwa ni kwa nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Somalia Rwanda, Sudani na Sudan kusini.

  0 0

  Na Tiganya Vincent, Dodoma

  Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa  iko tayari kutoa mafunzo maalum ya elimu ya fedha kwa wananchi wote wakiwemo wakinamama kuhusu ili kuleta uelewa mpana wa upatikanaji wa huduma za fedha na taratibu zinazohusu mikopo.

  Kauli hiyo imetolewa leo mijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kachwamba Kajaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Lupembe aliyetaka kujua mipango ya Serikali ya kupeleka huduma za kibenki vijijini ili wanawake waweze kupata mikopo.

  Aidha, alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imehakikisha kuwa huduma za kibenki zinawafikia wananchi wengi ili kurahisisha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi katika maeneo ya mjini na vijiji.Alisema kuwa baadhi ya Benki zimeanzisha huduma za Kibenki kupitia mawakala, na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi ambazo zimewasaidia wananchi kwenye sehemu ambako hakuna matawi ya Benki.

  Mhe. Dkt.Kajaji aliongeza kuwa  Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Benki Kuu inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kusaidia nguvu za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha.

  Alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuzishawishi Benki kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao.Mhe. Dkt.Kajaji alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kushawishi Benki nchini kupanua shughuli zao ili ziwafikie wananchi wengi hasa wale wa vijijini wakiwemo akina mama.

  Aidha, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na BOT iko tayari kutoa mafunzo maalum ya elimu ya fedha kwa wananchi wote wakiwemo wakinamama kuhusu utumiaji wa huduma za kifedha ili kuleta uelewa mpana wa upatikanaji wa huduma za fedha na mikopo.

  0 0

  Wadau wa Mawasiliano Kanda ya Ziwa, wakiwa katika picha ya pamoja katika Semina juu ya utoaji wa elimu juu ya simu bandia (fake) na halali (orginal) ulioandaliwa na TCRA, kabla ya kusitisha matumizi ya simu bandia mwezi ujao.

  Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imeendelea kuwakumbusha watumiaji wa simu za mkononi kuhakiki simu zao kabla mamlaka hiyo haijazima simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu.

  Soma Zaidi HAPA

  0 0

  Na FATMA SALUM -MAELEZO

  Jumla ya wadaiwa wapya 21,721 wa mikopo ya elimu ya juu wamejitokeza ili kuanza kulipa madeni yao kufuatia agizo la siku 60 lililotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mnamo Machi 14 mwaka huu.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tathmini ya agizo lililotolewa na bodi hiyo kwa wanufaika wa mikopo na waajiri ili kutimiza wajibu wao kisheria.

  Bw. Kibona alifafanua kuwa jumla ya Shilingi bilioni 151.5 zinatarajiwa kurejeshwa na wadaiwa hao ambao walikopeshwa ili kuwawezesha kupata elimu yao ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 1994.“Lengo la agizo lilikuwa ni kuhahakisha madeni yote yaliyoiva yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi na agizo hili limeisha Mei 13 mwaka huu.” alisema Bw. Kibona

  Kwa mujibu wa Bw. Kibona, kati ya wadaiwa waliopatikana, wadaiwa 19,528 walipatikana baada ya Bodi kuchambua taarifa za waajiriwa zilizowasilishwa na waajiiri na wadaiwa wengine wapatao 2,007 walijitokeza kwa hiari.“Waajiri wana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao, baadhi yao walifanya hivyo katika siku hizo sitini na tukawabaini wadaiwa hao, tunawapongeza waajiri kwa ushirikiano walioutoa na wanufaika wote waliojitokeza kwa hiari” alisema Bw. Kibona.

  Aidha Bw. Kibona aliongeza kuwa Bodi imeongeza siku 30 za ziada kuanzia Mei 20, 2016 kwa wadaiwa waliobaki kujitokeza na uamuzi huo umetokana na tathmini iliyoonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya waajiri na wanufaika wanaoendelea kujitokeza. Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo Bw. Cosmas Mwaisobwa alisema kuwa kiwango cha ukusanyaji wa madeni kwa mwezi kinatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.7 zinazokusanywa hivi sasa na kufikia shilingi bilioni 8 ifikapo mwezi Juni 2016.

  Katika kipindi cha mwaka 1994/1995 hadi sasa, kiasi cha shilingi trilioni 2.44 kimetolewa kwa wanufaika 378,504 wakiwemo wanafunzi wanaoendelea na masomo yao hivi sasa ambao kwa sasa hawana wajibu wa kulipa hadi pale watakapomaliza au kusitisha masomo yao. 

  Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la siku 60 kwa wadaiwa wa Bodi hiyo na waajiri, ambapo takribani asilimia 72 ya wadaiwa wote wameshawasilisha taarifa zao. Kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo
  Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo kwa wadaiwa ambao mikopo yao imeshaiva. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona.PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO 

  0 0

  KAMPUNI YA MOSAN LIMITED INAKUTANGAZIA NAFASI ZA KAZI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:
  1.       MAAFISA MASOKO NA MAUZO (SALES AND MARKETING OFFICERS)
  2.       MAAFISA MAUZO (SALES OFFICERS)

  SIFA
  I.                    UWEZO WA KUENDESHA PIKIPIKI NA GARI
  II.                  UWEZO WA KUUZA NA KUTAFUTA MASOKO, PIA KUONGEZA THAMANI KWENYE BIASHARA
  III.                MAARIFA YA MASOKO
  TUMA MAELEZO BINAFSI (CV) KWENYE EMAIL HII: employment.mosan@gmail.com.

  AU PIGA SIMU HII KWA MAELEZO ZAIDI: +255 717 49 87 73.
  Mwisho wa kutuma maombi ni Mei, 27, 2016.

  0 0

   


  0 0

  DAR ES SALAM, Tanzania – The tiny country of Israel has an abundance of world-class doctors and surgeons. But they're not keeping their medical expertise to themselves.Pediatric cardiac specialists from Save a Child's Heart recently traveled to East Africa to provide life-saving heart surgeries to desperately ill children in Tanzania, as well as to help develop that specialty there. 
  Dar Es Salam is Tanzania's largest city. Home to more than 50 million people, this East African country has only one hospital for heart patients. Last year, the Jakaya Kikwete Cardiac Institute at the Muhimbili hospital saw 25,000 patients and performed 270 surgeries. That's not nearly enough. 
   Help is needed and the Israeli organization, Save a Child's Heart, is answering the call. At the Wolfson Medical Center in Holon, Israel, doctors give their time to Save a Child's Heart (SACH). Over the years they've saved the lives of more than 4,000 babies and children from Africa, South America, Asia and the Middle East. 

  0 0
 • 05/20/16--12:00: GADO
 • Trump joins the Club!

  0 0

   Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm 
  akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga.

  Na Zainab Nyamka,
   Globu ya Jamii.
  MABINGWA wa soka Ligi Kuu ya Bara wamewasili jijni wakitokea Angola katika mechi ya narudiano dhdi ya Espirance Sagdrada ya Angola.
  Yanga ambayo imefuzu hatua makundi wamewasili mida ya saa nane na dakika 45 na mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa kocha wa timu hiyo Hans Van Pluijim amesema timu imefanya vizuri pamoja na figisu figisu ambazo wamefanyiwa.
  Amesema anawapongeza viongozi wa Yanga kwa kupambana na hujuma lakini wamefanikiwa kuingia hatua ya makundi na wamejifunza mengi Angola ambapo watayafanyiwa kazi huku akiwapongeza wachezaji wake kwa juhudi walizoonyesha uwanjani kuhakikisha wanafuzu.
  "Wachezaji wamefanya vizuri na wamejituma na kuhahakikisha wanavuka hatua hiyo na wamejituma sana nawapongeza na tumejifunza mengi sana Angola,"amesema Pluijm.
  Amesema  kikosi kwa sasa hakina cha kupoteza kitaendeea na kambi kuhakikisha wanasonga mbele katika mashindano hayo lengo lao ni kuona wanafika hatua ya fainali.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya Toleo la nane 8 kuhusu hali ya Uchumi Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/5/2016 katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. 
  Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Makamu wa Rais picha hayupo wakati wa uznduzi wa ripoti ya toleo la nane 8 kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/05/2016 .kwenye hotel ya Hyatt Begency jijini Dar es salaam.[Picha na OMR]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Madame Bella Bird baada ya uzinduzi wa ripoti yatoleo la nane 8kuhusu hali ya uchumi Tanzania.
  Serikali imesisitiza azma yake ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kikamilifu katila maendeleo ya Taifa.Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo kwenye uzinduzi wa ripoti ya toleo la nane la hali ya uchumi Tanzania uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam.
  Hali ya uchumi Tanzania ni ripoti inayochapishwa na Benki ya Dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kukuza mjadala wa sera unaojengeka baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye masuala muhimu ya uchumi nchini.Makamu wa Rais alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuendeleza nchi lakini katika baadhi ya miradi na hasa ile mikubwa mambo hayakuwa yanaenda vizuri kutokana na ukosefu wa fedha.
  "Dunia ilivyo sasa, tutapata fedha, tena nyingi kutoka sekta binafsi. Sasa kuna haja ya kurekebisha sheria zetu, sera na matamko mbalimbali ili kuiingiza sekta binafsi," alisema Mheshimiwa Samia.Alisema Serikali imeona kushirikiana na sekta binafsi kupitia mpango wa ubia baina ya sekta za umma na binafsi (PPPs) ndiyo njia pekee ya kuiwezesha Tanzania kupiga hatua ya maendeleo.
  Alibainisha kwamba katika uzinduzi huo wajumbe wametafakari pia umuhimu wa kuwaingiza wazalishaji na hasa wakulima wadogo na wakubwa kama sehemu ya ubia wa maendeleo ya Tanzania.
  Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za serikali katika kukusanya kodi, kupunguza rushwa na kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na kusema hatua hizo zimezaa matunda huku makusanyo ya mapato ya kodi kwa kila mwezi yakivuka lengo tangu Disemba, mwaka jana.
  Mapema, akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird alisifia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka 2014 na 2015 ukilinganisha na wa Afrika kwa ujumla ambao umeshuka toka asilimia 4.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.2 mwaka 2015.
  Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kwa kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ambao umeiongezea heshima serikali ndani na nje ya nchi.Bella alisema wakati Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa kati serikali inapaswa kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi (PPPs) kwa ajili ya uwekezaji.
   
  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es salaam
  20/5/2016

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ameshiriki kwenye Mkutano mkubwa wa Kimataifa, Women Deliver uliofanyika Copenhagen, Denmark tarehe 16-19 Mei, 2016. Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe wanaokaribia 5800 kutoka nchi 169. 
   Akiwa kwenye mkutano huo, Mhe. Waziri Ummy Mwalimu alipata pia fursa ya kutembelea maonyesho yaliyokuwa yakifanyika sambamba na mkutano huo. Mhe. Waziri Ummy Mwalimu alipata pia fursa ya kufanya Kikao na washiriki wote kutoka Tanzania. 
  Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kupanga Mikakati ya kuyafanyia kazi kwa pamoja mambo yote muhimu yaliyojitokeza kwenye Women Deliver Conference. 
   Tanzania ilikuwa na washiriki zaidi ya 40 kutoka taasisi mbalimbali zinazohusiana na masuala ya wanawake wakiwemo wabunge, wanafunzi,NGOs na wadau wengine wa sekta zinazojihusisha na masuala ya wanawake.

  Mbunge wa Babati, Mhe Pauline Gekal, Dkt. Neema Rusibamayila, Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dora Msechu, Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na Baltic katika mjadala
   Mhe. Waziri alihudhuria pia East African Regional Caucus

  Ni wakati wa maswali na majibu
   Mhe. Waziri alipiga picha ya pamoja na nyingine na washiriki kutoka Tanzania
   Mhe. Waziri alipiga picha ya pamoja na nyingine na washiriki kutoka Tanzania
  Mhe. Waziri alitembelea pia banda la Tanzania.

  0 0

  SAGCOT Kongai ya ihemi imefanya Mkutano wake wa tathmini wa yale walio kubaliana katika kukuza uhusiano kati ya sekta binafsi na seriakali katika kuendelaza uwekezaji. Mkutano huo wa siku 2 ulimalizika Njombe Mei 20, 2016. 

  Uliudhuriwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza na wakuu wa wilaya za Ludewa, Wanging'ombe, Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini uliandaliwa na kituo cha SAGCOT chini ya Mkurugenzi Mtedaji Geofrey Kilenga.

  Kongai (CLUSTER) ya Ihemi walijadili masuala ya uzalishaji, usafirishaji, Usindikaji pamoja na utafiti katika kukuza uwekezaji na kipato cha wananchi. Sekta binafsi ilihudhuriwa na makampuni makubwa yanayo jihudisha na kilimo pamoja na ufugaji kama ASAS, Darsh INDUSTRIES (RED GOLD), muungano wa wafugaji Ngombe Njombe. Pia Bi Neema Mwingu kutoka World Bank alitoa mada yenye kuonyesha kuwa Benki ya Dunia imetenga kiasi cha dola za kimarekani Milion 70 kukuza sekta binafsi inayokua (SME) ili waweze kushirikiana na wewekezaji wakubwa katika mnyororo wa thamani.

  Mapema Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatoly Chonya alisema Mikoa ya Njombe na Iringa ndio mikoa ambayo ikifanya vizuri katika kilimo na ufugaji basi tanzania itakuwa imeongeza pato la taifa maradufu, aliwaomba SAGCOT kuhakikisha wanazidisha juhudi za kukuza kilimo katika mikoa hiyo.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisistiza suala la sekta binafsi kuhemshimu makubaliano ya awali hasa ya kunufaisha wanannchi walio wakuta, pia alichukizwa na mtindo wa makampuni hayo kuhamisha ulipaji wa kodi ya mapato kwenda Dar es salaam jambo ambalo linapunguza pato la mkoa kwa kiwango kikubwa.

  Naye Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jolwika Kasunga akichangia alisema " wawekezaji wana kuwa karibu sana na serikali mwanzoni wakati wa kuhangaikia vibali wanapo fanikiwa wanapotea mpaka wapate shida ingine" .

  Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisisitiza suala la masoko na wawekezaji kupata social licence kutoka katika jamii kabla ya kuanza uwekezaji hili litapunguza sana migogoro isiyo kuwa ya lazima.

  Katika mkutano huo pia Mkurugenzi wa Sagcot Catalyst Fund alisema lazima sasa wakulima wadogo wawe matajiri la msingi ni kuhakikisha fedha zote hizi zinawanyanyua na kuwafanya matajiri.
  Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akichangia mada katika Mkutano wa tathmini wa yale walio kubaliana katika kukuza uhusiano kati ya sekta binafsi na seriakali katika kuendelaza uwekezaji (SAGCOT Kongai ya ihemi) uliofanyika Mkoani Njombe.
  Sehemu ya viongozi kutoka katika mikoa ya Njombe na Iringa wakisikiliza mada. Katikati ni Spika wa Bunge Mstaafu, Mama Anna Makinga.


  0 0


  Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said) 

  NA K-VIS MEDIA

  MKOA wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.

  Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. “Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga.
  Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
  Bandari ya Kigoma.
  Mwalo wa Kibirizi.
  Manispaa ya Kigoma- Ujiji
  Uwanja wa Lake Tanganyika

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) akifungua Semina ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhusu Kuanzishwa kwa TADB na Utekelezaji wa Majukumu yake. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba.
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Aliyesimama) akizungumza wakati wa Semina ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhusu Kuanzishwa kwa TADB na Utekelezaji wa Majukumu yake. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu.
  Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi akiwasilisha Mada kuhusu Kuhusu Kuanzishwa kwa TADB na Utekelezaji wa Majukumu yake mbele ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  0 0
 • 05/21/16--01:49: SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0

  Miaka miwili iliyopita, katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzama Meli ya Mv.Bukoba, kwa msaada wa mtandao, niliandaa makala haya hivyo nimehariri kidogo ili kuendana na wakati, japo uhalisia wake uko pale pale.
  Na George Binagi

  Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea Mkoani Kagera.
  Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba abiria 430).
  Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21 Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
  Wakati leo tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
  Lakini wakati tunatafakari suala hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe bila kusubiri kusukumwa na mtu hususani wale wenye mamlaka ya kuleta matokeo chanya katika kuboresha hali ya usafiri majini Ikiwemo Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA  kwamba tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?
  Na Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu? Je, tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu?.


  Lakini pia wapo waliohoji na bado wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado wanaendelea kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo? Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya Watanzania ikiwemo ile ya mv Spice Ireland iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika Mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja Zanzibar.
  Lakini yote Tisa, Kumi ni stofahamu iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa nchini.Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Wakaguzi wa na Waangalizi kwa maana ya Mamlaka husika, Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na Timu yake na wapo waliosema chombo kilikuwa kibovu.
  Wapo waliodai chombo hicho kilikuwa kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe walisababisha ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda Melini ilihali chombo kilikuwa kimejaa huku mlolongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali hiyo na Imani za Kishirikina.
  Mimi nasema sina nia ya kuandika hayo yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo yote ili kila mmoja kwa namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna ya kufanya ili kuepukana na ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine husema tusiangalie tulipoanguka bali tuangalie tulipojikwaa.


  Wapo wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao na mmoja wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha yake ni Mwanamitindo maarufu hapa nchini ambae pia anafanya shughuli zake barani Ulaya Flavian Matata ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi pamoja na binamu yake.
  Pamoja na watu wengine, Matata amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa kufika Mkoani Mwanza katika eneo la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.Hakina inauma sana.

  Yapo mengi ya kuzungumza na kuandika lakini swali la kujiuliza ni moja tu, miaka 21 mwaka huu 2016 tangu kuzama meli ya Mv.Bukoba Mei 21 mwaka 1996, Je usafiri wa majini ni salama hapa nchini ama tunasafiri kwa kudra za Mwenyezi Mungu? Mimi nihitimishe kwa kusema ni jukumu la kila mmoja wetu kwa kushirikiana na Mamlaka husika ikiwemo SUMATRA kuhakikisha kuwa usafiri wa Majini Unakuwa usafiri salama hapa nchini.

  0 0


  Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Azzan Mussa Zungu akiongoza Bunge mjini Dodoma leo 21 Mei, 2016.


  Mbunge wa CCM, Mhe. Ally Mohamed Keissy (kulia) akijadiliana na Wabunge wenzie ndani ya Bunge mjini Dodoma leo 21 Mei, 2016.


  Naibu Waziri, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Eng. Ramo Matala Makani (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Selemani Saidi Jafo Bungeni mjini Dodoma 21 Mei, 2016.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Jenista Joackim Mhagama (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles John Mwijage (katikati) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Alphonce Kolimba wakiteta jambo leo Bungeni Mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
  Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Mhe. Edwin Amandus Ngonyani (kulia) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe wakijadiliana jambo leo Bungeni Mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
  (Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma)
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1226 | 1227 | (Page 1228) | 1229 | 1230 | .... | 3285 | newer